Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 119562 articles
Browse latest View live

WATUMISHI OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI WAPEWA SOMO KUHUSU VIRUSI VYA CORONA

$
0
0


Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu na Utawala Bw. James Kibamba akizungumza na sehemu ya watumishi waliohudhulia mafunzo kuhusu namna sahihi ya kujinga na virusi vya ugonjwa wa Corona wakati akimkaribisha muwezeshaki Dkt. Peter Kibacha ambaye ni mtalaam bingwa wa afya na mtoto kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili. zoezi la kutoa elimu hiyo limefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali uliopo Jijini Dar es Salaam.
Bw. Yusuph Varisanga kutoka kitengo cha Uhasibu akiuliza sawali kuhusu ugonjwa wa Corona wakati zoezi la utoaji wa elimu kuhusu jinsi ya kujikinga na ugonjwa huo kiliendelea.
Sehemu ya Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu Wa Serikali wakipata elimu kuhusu ugonjwa wa Virusi vya Corona, elimu hiyo imetolewa na mtaalam bingwa wa magonjwa ya afya na mtoto kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Peter Kibacha.

……………………………………………………………………………………………

Na. Dennis Buyekwa.

Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa hatari wa virusi vya Corona (COVID – 19). Muda wote wanapokuwa ndani na nje ya kituo cha kazi.

Wito huo umetolewa mapema leo ofisini hapo na Daktari bingwa wa magonjwa ya Afya na mtoto Dkt. Peter Kibacha kutoka Hosipitali ya Taifa Muhimbili wakati akitoa elimu juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa huo.

Kisa cha kwanza cha ugonjwa wa Corona kiliibuka kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka jana katika mji wa Wuhan jimbo la Hubei nchini China, mpaka sasa umesambaa katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo nchi za Afrika Mashariki na hivyo kupelekea Shirika la Afya duniani (WHO) kuutangaza ugonjwa huo kuwa ni janga la dunia.

Dkt. Kibacha amesema ugonjwa wa Corona unaweza kumpata mtu yoyote hivyo amesisitiza kuwa ni vyema kuchukua tahadhari kila wakati hatua itakayosaidia watumishi hao kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa huo wao pamoja na familia zao.

Akizungumizia kuhusu dalili za ugonjwa huo Dkt. Kibacha amezitaja dalili hizo kuwa ni pamoja na mtu kupata homa kali, kukohoa kikohozi kikavu, uchovu wa mwili, kuharisha na kutapika, kupumua kwa shida sambamba na kukosa hamu ya chakula.

Akielezea kuhusu tiba ya ugonjwa huo Dkt. Kibacha amesema kuwa kwa sasa ugonjwa huo hauna chanjo wala tiba lakini kinachoweza kufanyika ni kufuata kanuni za afya ambazo zinaweza kuwasaidia watu kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Akiainisha njia za kujikinga na ugonjwa huo mtalaamu huyo amesema kuwa ni muhimu kwa kila mtu kujenga tabia ya kunawa mikono yake mara kwa mara pamoja na kujiepusha kugusana na mtu mwingine hasa pale watakapohitaji kusalimiana.

Amezitaja njia nyingine za kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo kuwa ni kuepuka kugusa macho, mdomo na pua kabla ya kunawa mikono, kuvaa barakoa wakati wote (Mask) pamoja kufunika kinywa kwa kitambaa kisafi wakati wote mtu anapokohoa au kupiga chafya.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali Watu na Utawala Bw. James Kibamba amemshukuru mtaalamu huyo kwa kukubali wito wa kuja kutoa elimu hiyo kwa watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali huku akiwahimiza watumishi hao kutumia vyema elimu hiyo ili iweze kuwasaidia kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

Nao watumishi waliopata mafunzo hayo wameushukuru uongozi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa kuandaa mpango wa mafunzo kuhusu ugonjwa huo kwa kuwa umewawezesha kupata elimu itakayowasaidia kujua njia bora za namna ya kujikinga na ugonjwa huo hatari unaosambaa kwa kasi duniani.

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA YAIPONGEZA WAKALA WA VIPIMO (WMA)

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Dkt. Ludovick Manege (aliyenyoosha mkono)  akiwaongoza wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira waliofika kutembelea katika kituo cha Misugusugu Kibaha - Pwani kujionea shughuli zinazofanywa ikiwemo kujifunza mambo mbali mbali.
Mjumbe wa kamati ya bunge viwanda, biashara na mazingira akiuliza swali mara baada ya  mara baada ya katika kituo Wakala wa Vipimo kilichopo Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira mheshimiwa Suleman Saddiq mbunge wa Mvomero (aliyenyoosha mikono) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Vipimo Kituo cha Misugusugu Kibaha - Pwani, Alban Kihuld (wa tatu toka kushoto).
Wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira akitembelea katika kituo cha Wakala wa Vipimo kilichopo Misugusugu Kibaha- Pwani.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira mheshimiwa Suleman Saddiq mbunge wa Mvomero akieleza jambo kwa vyombo vya habari mara baada ya kupata maelezo juu ya utendaji kazi na majukumu ya Wakala wa Vipimo mara baada ya katika kituo cha Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Dkt. Ludovick Manege akiongea na wanahabari juu ya huduma zinazotolewa na wakala wa vipimo mara baada ya kutembelewa na wabunge kamati ya bunge viwanda, biashara na mazingira katika kituo chao cha Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani. 

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

 Kamati ya Bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira imewapongeza Wakala wa Vipimo (WMA)kwa kufanya kazi kisasa ili kuendana na sera ya Serikali kuelekea Uchumi wa Viwanda. Akizungumza na wanahabari mara baada ya ziara ya kutembelea kituo hicho Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Ahmed Saddiq amewataka kuendelea kujituma kwa kufata sheria na taratibu za upimaji.

 “Kiukweli nimefurahi kufika mahali hapa na kujionea mambo mengi yanayofanywa kisasa na wakala wa Vipimo katika kituo cha Misugusugu Kibaha - Pwani hivyo niwaombe waendelee kuchapa kazi kwa bidii," amesema Mhe. Saddiq. 

Ameongeza kuwa Wakala wa Vipimo wamekuwa msaada mkubwa katika kutatua changamoto hasa katika upimaji magari na upimaji wa mita za maji na kuziomba mamlaka za maji ikiwemo DAWASA,DUWASA, MURUWASA lazima zote zipitie hapa WMA na kuhakikiwa kisha kupewa kibari tayari kutumika kwenye jamii. Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Vipimo (WMA), Ludovick Manege, amesema mafanikio ya kituo hicho yametokana na kujituma na kupata ushirikiano mkubwa kutoka Serikalini kwa kutatua baadhi ya changamoto. 

Amesema mpaka sasa kituo hicho kimepata mafanikio makubwa kwa kuendelea kusimamia misingi na kanuni bora katika upimaji wa matenki ya mafuta na dira za maji. "Tumepewa dhamana ya kuhakikisha matenki ya mafuta yana hakikiwa hapa, yanapoenda kujazwa mafuta, na Dira za Maji zinazoletwa nchini zote lazima zipimwe ili kuhakikisha mamlaka za maji zinatumia mita sahihi” amesema Ludovick.

KAMATI YA BUNGE YAVUTIWA UTEKELEZAJI MRADI WA VIWANJA ILEMELA

$
0
0

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi akifafanua jambo wakati akijibu hoja za baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji mradi wa viwanja katika halmashauri ya manispaa ya ilemela mkoani Mwanza jana. Kushoto kwa Waziri ni Mwenyekiti wa Kamati Kemilembe Lwota.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo akijibu hoja kutoka kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji mradi wa viwanja katika halmashauri ya manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza jana
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii Kemilembe Lwota (wa pili kushoto) akifuatilia uwasilishaji taarifa ya utekelezaji mradi wa viwanja katika halamsahauri ya manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza jana. Kushoto ni Waziri wa Ardhi William Lukuvi na kulia ni Naibu wake Dkt Angeline Mabula
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakifuatilia uwasilishwaji taarifa ya utekelezaji mradi wa viwanja katika halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jana mkoani Mwanza. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo.

Wajumbe wa Kamti ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii wakifuatilia uwasilishwaji taarifa ya utekelezaji mradi wa viwanja katika halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jana mkoani Mwanza. (PICHA ZOTE NA HASSAN MABUYE WIZARA YA ARDHI).

*********************************

Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imevutiwa na utekelezaji mradi wa kupanga na kupima viwanja eneo la East Buswelu katika kata ya Buswelu na Nyamhongo halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoa wa Mwanza.

Katika utekelezaji mradi huo, halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ilipewa mkopo usio na riba wa shilingi Bilioni 1,550,000,000 na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kupanga na kupima viwanja 500 na kufanikiwa kuurejesha mkopo huo kwa wakati na kupata faida ya milioni 195,374,000.

Karibu wajumbe wote wa Kamati hiyo waliochangia utekelezaji mradi wa viwanja katika halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jana wakati wa kupokea taarifa ya mradi huo walionesha kuridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa na watendaji wa halmashauri hiyo chini ya Mkurugenzi wake John Wanga kwa kuitumia vizuri fedha waliyokopeshwa na kuzalisha faida.

Hata hivyo, Mbunge wa Jimbo la Korogwe Timotheo Mzava alishauri faida inayopatikana kutokana na mkopo usio na riba kwa halmashauri nchini itumike katika kazi za ardhi hasa upangaji na upimaji badala ya kutumika katika shughuli nyingine na kutaka kuongezwa kipengele ndani ya mkataba wa mkopo kinachoelekeza suala hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii Kemilembe Lwota aliipongeza halmashauri ya Manispaa ya Ilemela pamoja na Mbunge wake ambaye ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi Dkt Angeline Mabula kwa kazi nzuri ya kuhakikisha kiasi cha fedha ilichokopeshwa kinatumika vizuri na kuleta matokeo chanya katika halmashauri hiyo.

Kwa mujibu wa Kemilembe, kamati yake inaunga mkono jitihada zilizofanywa na wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuzikopesha halmashauri ili kuongeza kasi ya upimaji ardhi na kubainisha kuwa asilimia kubwa ya ardhi nchini hajapimwa na hivyo kuchangia migogoro ya ardhi.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alisema utaratibu ulioanzishwa na wizara yake wa kuzikopesha halmashauri unalenga kuongeza kasi ya upimaji katika halmashauri mbalimbali na hivyo kuzalisha walipa kodi ya pango la ardhi.

Amezitaka halmashauri kutengeneza miradi ya kimkakati na kuandika maandiko yatakayosaidia kupata fedha za mkopo usio na riba na hivyo kuzisaidia katika shughuli zao upangaji, upimaji na umilikishaji ardhi na kuzalisha walipa kodi .

Aidha, Lukuvi alibainisha kuwa, katika kuhakikisha sekta ya ardhi inafanya vizuri zaidi Wizara yake imeanza zoezi la kuwapanga upya wataalamu wa sekta ya hiyo nchi nzima kulingana na uhitaji sambamba na kuanzisha ofisi za mikoa ili kuondoa changomoto za upangaji, upimaji na umilikishaji ardhi nchini.

‘’Kuna baadhi ya halmashauri zina wataalamu wengi wa sekta ya ardhi huku nyingine zikiwa na wataalamu wachache hali hiyo inasababisha shughuli za ardhi katika halmashauri kutofanyika vizuri’’ alisema Lukuvi.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula alisema halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imekuwa ikifanya vizuri katika zoezi la upangaji, upimaji na umilikishaji ardhi na katika kipindi cha miaka miwili imefanikiwa kupunguza migogoro ya ardhi kwa kiasi kikubwa na kutoa hati 22,185.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi Mary Makondo alisema wizara yake imejipanga kuhakikisha inakabiliana na changamoto ya watumishi kwa kuwapanga katika mikoa yote ishirini na sita ya Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa Mary, katika kipindi hiki ambacho idadi ya wataalamu wa sekta ya ardhi hawatoshelezi halmashauri zenye miradi zinaweza kutumia wataalamu kutoka halmashauri nyingine ili kuharakakisha kazi na hivyo kuongeza kasi ya upangaji na upimaji katika maeneo mbalimbali.

Waziri wa Ulinzi wa Marekani na naibu wake wawekwa karantini baada ya maafisa 37 wa Pentagon kupatwa na corona

$
0
0
Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Thomas Esper na Naibu wake wamewekwa karantini tangu Jumatatu ya jana baada ya kuthibitika kuwa, maafisa 37 wa wizara hiyo wameambukizwa virisi vya corona.

Taarifa ilitotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) imesema kuwa, miongoni mwa maafisa wa wizara hiyo walioathirika na virusi vya corona wamo askari 18, suala ambalo limezidisha wasiwasi wa kusambaa zaidi virusi hivyo katika jeshi la Marekani.

Habari hii ya kuwekwa karantini Waziri wa Ulinzi wa Marekani na naibu wake kwa hofu ya corona imetangazwa huku duru mbalimbali nchini humo zikiendelea kuikosoa serikali ya Rais Donald Trump kwamba, haikuchukua hatua zinazofaa za kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo.

Kwa upande wake Donald Trump amewataka Wamarekani kuwa watulivu na kuacha manunuzi ya pupa akidai kuwa maafisa wa serikali wanafanya kazi vizuri.
 

KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA YAIPONGEZA WAKALA WA VIPIMO (WMA)

$
0
0
Na Cathbert Kajuna, Globu ya Jamii. 

Kamati ya Bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira imewapongeza Wakala wa Vipimo (WMA)kwa kufanya kazi kisasa ili kuendana na sera ya Serikali kuelekea Uchumi wa Viwanda. 

Akizungumza na wanahabari mara baada ya ziara ya kutembelea kituo hicho Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Ahmed Saddiq amewataka kuendelea kujituma kwa kufata sheria na taratibu za upimaji. 

“Kiukweli nimefurahi kufika mahali hapa na kujionea mambo mengi yanayofanywa kisasa na wakala wa Vipimo katika kituo cha Misugusugu Kibaha - Pwani hivyo niwaombe waendelee kuchapa kazi kwa bidii," amesema Mhe. Saddiq. 

Ameongeza kuwa Wakala wa Vipimo wamekuwa msaada mkubwa katika kutatua changamoto hasa katika upimaji magari na upimaji wa mita za maji na kuziomba mamlaka za maji ikiwemo DAWASA,DUWASA, MURUWASA lazima zote zipitie hapa WMA na kuhakikiwa kisha kupewa kibari tayari kutumika kwenye jamii. 

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Vipimo (WMA), Ludovick Manege, amesema mafanikio ya kituo hicho yametokana na kujituma na kupata ushirikiano mkubwa kutoka Serikalini kwa kutatua baadhi ya changamoto. 

 Amesema mpaka sasa kituo hicho kimepata mafanikio makubwa kwa kuendelea kusimamia misingi na kanuni bora katika upimaji wa matenki ya mafuta na dira za maji. "Tumepewa dhamana ya kuhakikisha matenki ya mafuta yana hakikiwa hapa, yanapoenda kujazwa mafuta, na Dira za Maji zinazoletwa nchini zote lazima zipimwe ili kuhakikisha mamlaka za maji zinatumia mita sahihi” amesema Ludovick.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Dkt. Ludovick Manege (aliyenyoosha mkono)  akiwaongoza wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira waliofika kutembelea katika kituo cha Misugusugu Kibaha - Pwani kujionea shughuli zinazofanywa ikiwemo kujifunza mambo mbali mbali.
Mjumbe wa kamati ya bunge viwanda, biashara na mazingira akiuliza swali mara baada ya  mara baada ya katika kituo Wakala wa Vipimo kilichopo Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira mheshimiwa Suleman Saddiq mbunge wa Mvomero (aliyenyoosha mikono) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Vipimo Kituo cha Misugusugu Kibaha - Pwani, Alban Kihuld (wa tatu toka kushoto).
Wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira akitembelea katika kituo cha Wakala wa Vipimo kilichopo Misugusugu Kibaha- Pwani.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira mheshimiwa Suleman Saddiq mbunge wa Mvomero akieleza jambo kwa vyombo vya habari mara baada ya kupata maelezo juu ya utendaji kazi na majukumu ya Wakala wa Vipimo mara baada ya katika kituo cha Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Dkt. Ludovick Manege akiongea na wanahabari juu ya huduma zinazotolewa na wakala wa vipimo mara baada ya kutembelewa na wabunge kamati ya bunge viwanda, biashara na mazingira katika kituo chao cha Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani.

MDAHALO WA KIMATAIFA WA KUPAMBANA NA UGONJWA WA CORONA WAENDESHWA NA TAGLA KWA NJIA YA VIDEO

$
0
0
MDAHALO wa kimataifa umeendeshwa na Wakala ya Mafunzo kwa nia ya Mtandao (TaGLA) ikishirikisha nchi za Korea ya Kusini, Sri Lanka, Thailand, Japan na Shirika la Afya Duniani. Wawasilisha mada walisisitiza muhimu wa kuwatafuta, kuwatenga, kufanyia uchambuzi wa haraka na kutibu kila mgonjwa atakaepatikana. Juhudi hizo zimguse kila mtu, kila familia, jamii na kitaifa ili kuleta ufanisi kutokomeza janga hili la ugonjwa wa corona. Washiriki kutoka Tanzania walikuwa madaktari, wasomi, viongozi, watunga sera na wataalamu katika nyanja mbalimbali.
Meneja Mafunzo kutoka Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Dickson Mwanyika akizungumza na Michuzi Tv baada ya kumalizika mkutano kwa Njia ya Mtandao uliohusisha nchi  mbalimbali kuhusu Virusi vya Corona leo jijini Dar es Salaam .ambapo amempongeza  Rais Magufuli  kwa kusitisha mbio za Mwenge mwaka huu mpaka pale hali ya tatizo la Virusi vya Corona litakapopatiwa ufumbuzi huku bajeti ya Mwenge akiagiza iende Wizara ya Afya kununua Vifaa na dawa za Corona.
  Dkt.Kija Luhuti (kushoto)  akizungumza na Michuzi Tv baada ya kumalizika mkutano kwa Njia ya Mtandao uliohusisha nchimbalimbali kuhusu Virusi vya Corona leo jijini Dar es Salaam. ambapo amesema wananchi wazingatie 
 usafi ili kujikinga na Virusi vya Corona kulia ni Meneja Mafunzo toka Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), Dickson Mwanyika

 Watumishi Wakala wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) pamoja na  wadau mbalimbali  wawakimsikiliza mtoa mada kwa njia ya video (Tele Conference) leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao Tanzania TaGLA, Fredrick Massawe akiwashukuru wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano kwa Njia ya Mtandao uliohusisha nchi mbalimbali kuhusu Virusi vya Corona leo jijini Dar es Salaam.


KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA YAIPONGEZA WAKALA WA VIPIMO (WMA)

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Dkt. Ludovick Manege (aliyenyoosha mkono)  akiwaongoza wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira waliofika kutembelea katika kituo cha Misugusugu Kibaha - Pwani kujionea shughuli zinazofanywa ikiwemo kujifunza mambo mbali mbali.
Mjumbe wa kamati ya bunge viwanda, biashara na mazingira akiuliza swali mara baada ya  mara baada ya katika kituo Wakala wa Vipimo kilichopo Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira mheshimiwa Suleman Saddiq mbunge wa Mvomero (aliyenyoosha mikono) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Vipimo Kituo cha Misugusugu Kibaha - Pwani, Alban Kihuld (wa tatu toka kushoto).
Wabunge wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira akitembelea katika kituo cha Wakala wa Vipimo kilichopo Misugusugu Kibaha- Pwani.
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira mheshimiwa Suleman Saddiq mbunge wa Mvomero akieleza jambo kwa vyombo vya habari mara baada ya kupata maelezo juu ya utendaji kazi na majukumu ya Wakala wa Vipimo mara baada ya katika kituo cha Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Dkt. Ludovick Manege akiongea na wanahabari juu ya huduma zinazotolewa na wakala wa vipimo mara baada ya kutembelewa na wabunge kamati ya bunge viwanda, biashara na mazingira katika kituo chao cha Misugusugu kilichoko mkoani Kibaha - Pwani. 

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
KAMATI ya Bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira imewapongeza Wakala wa Vipimo (WMA)kwa kufanya kazi kisasa ili kuendana na sera ya Serikali kuelekea Uchumi wa Viwanda.

Akizungumza na wanahabari mara baada ya ziara ya kutembelea kituo hicho Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Suleiman Ahmed Saddiq amewataka kuendelea kujituma kwa kufata sheria na taratibu za upimaji.

“Kiukweli nimefurahi kufika mahali hapa na kujionea mambo mengi yanayofanywa kisasa na wakala wa Vipimo katika kituo cha Misugusugu Kibaha - Pwani hivyo niwaombe waendelee kuchapa kazi kwa bidii," amesema Mhe. Saddiq.

Ameongeza kuwa Wakala wa Vipimo wamekuwa msaada mkubwa katika kutatua changamoto hasa katika upimaji magari na upimaji wa mita za maji na kuziomba mamlaka za maji ikiwemo DAWASA,DUWASA, MURUWASA lazima zote zipitie hapa WMA na kuhakikiwa kisha kupewa kibari tayari kutumika kwenye jamii.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Vipimo (WMA), Ludovick Manege, amesema mafanikio ya kituo hicho yametokana na kujituma na kupata ushirikiano mkubwa kutoka Serikalini kwa kutatua baadhi ya changamoto.

Amesema mpaka sasa kituo hicho kimepata mafanikio makubwa kwa kuendelea kusimamia misingi na kanuni bora katika upimaji wa matenki ya mafuta na dira za maji.

"Tumepewa dhamana ya kuhakikisha matenki ya mafuta  yana hakikiwa hapa, yanapoenda kujazwa mafuta,  na Dira za Maji zinazoletwa nchini  zote lazima zipimwe  ili kuhakikisha mamlaka za maji zinatumia mita sahihi” amesema Ludovick.

DC KASESELA: MARUFUKU SHEREHE ZA HARUSI BILA KIBALI CHA DMO

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya iringa Richard Kasesela akitoa maagizo kwa wadau wa sekta ya afya juu ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya Corona
Mkurugenzi wa  kiwanda cha uzalishaji wa maziwa kampuni ya Asas mkoani Iringa Ahmed Asas na wadau wengine wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitoa maagizo juu ya virusi vya Corona.

Na Frendy Mgunda Iringa
SERIKALI ya wilaya ya Iringa imepiga marufuku sherehe zote harusi ambazo hazina kibali maalumu kutoka kwa Mganga mkuu wa wilaya (DMO) kutokana na kuwepo kwa tishio la maambukizi ya virusi vya Corona nchini.

Akizungumza kwenye kikao cha wadau wa sekta ya afya,mkuu wa wilaya ya iringa Richard kasesela alisema kuwa sherehe zote za harusi haziruhusiwi kufanyika bila kupata kibari maalumu kwa lengo la kulinda afya za wananchi wanaokuwa wanasherekea harusi kutokana na kuwepo kwa tishio la maambukizi ya virusi vya corona.

Ni lazima kila sherehe katika wilaya ya Iringa kuwepo mfumo wa kusafishia mikono kwa lengo la kukwepa  maambukizi ya virusi vya corona ambavyo vimekuwa tishio hapa nchini na duniani kwa ujumla.

Kasesela alisema kuwa kwenye harusi huwa kuna kuwa na mkusanyiko wa watu wengi hivyo ni lazima kuweka king a mapema ili yasitokee maambukizi makubwa kama ambayo yametokea nchi nyingine.

Aisha kasesela aliwataka wananchi wa wilaya ya Iringa kuwa makini na mikusanyiko ya watu ili kuepuka kupata maambukizi ya virusi vya corona ambavyo vimekuwa vinatishia uhai wa wananchi.

"Misiba,kusalimia,vituo vya usafiri,makanisani na misikitini ni lazima kuondokana na Mira na tamaduni zetu ambazo tumekuwa tumezizoea ili kuepukana na maambukizi ya virusi vya corona" alisema kasesela

Kasesela alitaka halmashauri zote za wilaya ya Iringa kuhakikisha kwenye vituo vya afya,vituo vya mabasi,maduka makubwa,kampuni mbalimbali zote lazima kuwe na sehemu za kunawia mikono ili kuepuka na maambukizi ya virusi vya corona.

"Iringa hakuna hata mgonjwa mmoja wa maambukizi ya virusi vya corona na taarifa zinazoenea sio za kweli wananchi wa iringa wanatakiwa kuzipuuza na mwenye jukumu la kutangaza uwepo virusi hivyo ni waziri husika au viongozi wa ngazi za juu"alisema kasesela

Kwa upande wake mdau wa sekta ya afya mkoani Iringa Ahmed Asas alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya corona kwa waandishi wa habari,wafanyakazi wa kampuni ya Asas na taasisi binafsi kwa lengo la kuepuka kuambukizwa virusi vya corona.

Ahmed alisema kuwa kwenye kampuni ya Asas wamefanikiwa na kuwa na chumba maalumu kwa ajiri ya wafanyakazi watao kuwa na dalili za maambukizi ya virusi vya corona na wameganikiwa kutoa elimu kwa baadhi ya wafanyakazi kwa lengo la kuwa msaada kwa wafanyakazi wengine.


"Sisi tupo tayari kutoa elimu juu ya maambukizi ya virusi vya corona sehemu yeyeyo ile kwa kushirikiana na serikali ya wilaya ya Iringa kama ambavyo yumeanza na mkuu wa mkoa wa Iringa Richard kasesela" alisema Ahmed

Naye mganga mkuu wa wilaya ya Iringa Dr Samwel Marwa alisema kuwa wamejipanga kila idara kuhakisha wanatoa elimu na kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

DKT. NDUMBARO AKUTANA NA BALOZI WA UBELGIJI, SWEDEN

$
0
0
Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker pamoja na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Anders Sjoberg leo jijini Dar es Salaam. 

Mazungumzo ya Mhe. Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro pamoja na Balozi wa Ubelgiji yalijikita katika masuala mbalimbali ikiwemo masuala ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji hasa kwenye sekta za Kilimo na Madini.

Balozi wa Ubelgiji, Mhe. Acker amesema kuwa Ubelgiji itaendelea kuwekeza katika kilimo cha maharage mkoani Kigoma, na kilimo cha Tumbako katika mikoa ya Tabora, Ruvuma, Katavi na Rukwa.

"kupitia uwekezaji wa kilimo nchi zetu mbili (Tanzania na Ubelgiji) zimekuwa zikinufaika sawa hivyo ni rai yangu kuona uwekezaji huu unaendelea kutoa fursa za ajira kwa mataifa haya mawili," Amesema Balozi Acker.

Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema kuwa Tanzania itaendelea kuhakikisha inazidi kuimarisha Uhusiano wake na Ubelgiji katika sekta ya Kilimo, Uwekezaji na Biashara ili kuendelea kutoa fursa za ajira na kukuza uwekezaji nchini.

Katika nyingine, Naibu Waziri Dkt. Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Anders Sjoberg, ambapo mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia.  

Pamoja na mambo mengine, Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Sjoberg amemuahidi Naibu Waziri kuwa Sweeden itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha kuwa nchi hizi mbili zinapiga hatua katika maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Kwa upande wake Mhe. Naibu Waziri amemhakikishia Balozi Sjoberg kwamba Tanzania itaendelea kukuza na kuimarisha Ushirikiano na Uhusiano wake na Sweden kwani uhusiano huo wa muda mrefu umekuwa na manufaa kwa nchi zote mbili.


Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akisalimiana na Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker kabla ya kuanza kwa mazungumzo yao jijini Dar es Salaam



Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam



Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimfafanulia jambo Balozi wa Ubelgiji nchini, Mhe. Peter Van Acker wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam



Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Anders Sjoberg wakisalimiana bila kushikana mikono kabla ya kuanza kwa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam


Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Anders Sjoberg akiongea na Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam


Naibu Waziri, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akimueleza jambo Balozi wa Sweeden nchini Mhe. Anders Sjoberg wakati wa mazungumzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

JKT Tanzania yavunja kambi rasmi

$
0
0
Klabu ya JKT Tanzania Leo tarehe 18/03/2020 rasmi imevunja kambi yake kutokana na maelekezo yaliyotolewa Jana na Serikali kupitia Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kuhusu zuio la kuwepo kwa mikusanyiko mbalimbali kutokana na kuwepo ugonjwa wa Corona hapa nchini.

Hivyo klabu yetu ya JKT Tanzania Leo imewaruhusu Wachezaji kwenda kwenye familia zao lakini wametakiwa kuendelea kujikinga na kufuata maelekezo yanayotolewa na serikali sambamba na wataalam wa afya.

Kampuni za mawasiliano ya simu zinavyosaidia kuinua wanawake nchini Tanzania

$
0
0

Wiki iliyopita wanawake barani Afrika walisherehekea Siku ya Kimataifa ya Mwanamke. Siku hii muhimu husherehekea mafanikio ya mwanamke kijamii, kiuchumi, kiutamani na kisiasa na kuchagiza mjadala wa usawa wa kijinsia.

Nchini Tanzania usawa wa kijinsia umeongezeka katika miaka ya karibuni kutokana na nguvu za serikali, taasisi na watu binafsi kuweka mazingira ya upatikanaji wa elimu kwa mtoto wa kike na haki ya mwanamke kumiliki na kutumia ardhi.Licha ya maendeleo hayo, yapo mengi ambayo inabidi kufanywa kuendelea kumpa nafasi zaidi mtoto wa kike.

Eneo mojawapo ambalo kuna mengi ya kufanya ni katika teknolojia na mawasiliano. Takwimu na hivi karibuni zinaonyesha katika suala la umiliki wa simu za mkononi Tanzania kuna pengo la asimili 9 kati ya wanawake na wanaume, wanaume wakiwa juu. Takwimu zinaonyesha pia kwamba hata katika upatikanaji wa mtandao wa intaneti, wanaume wako juu zaidi kwani kuna pengo la asilimia 13 kati ya wanaume wenye uwezo wa kupata na kutumia intaneti ukilinganisha na idadi ya kundi hilo upande wa wanawake. Sote tunafahamu kwamba mtandao wa intaneti ni moja ya njia bora za kuinua aina ya maisha ambayo mtu anaishi. Mfano, intaneti inatoa nafasi ya kupata huduma za fedha, bima za afya na hata nafasi za kazi. Hii leo, mtandao wa intaneti na kuunganishwa kidijitali kunawapa nafasi wanawake ambao zamani hawakuwa na fursa nyingi, fursa mpya ya kufaidi hayo yote.

Bahati nzuri, hapa Tanzania sekta ya mawasiliano ya simu imeleta namna mpya na za kibunifu kupata faida za kuuganisha kidijitali kwa wanawake. Kampuni kama Tigo imeunda apps zinazosaidia wanawake kuendesha na kusimamia mipango yao ya fedha. Mfano Tigo Pesa App inawapa wanawake nafasi kuweka fedha, kufanya malipo na hata kupata mikopo. Mbali na hiyo, Tigo pia inasaidia kuhakikisha kwamba wanawake wanapata ujuzi ili kufurahia fursa hizi. Katika hili, Tigo Tanzania wamezindua programu kama “Apps and Girls” ambapo wanawafunzi wa kike wanafundishwa mbinu za kuvuna fursa katika dunia ya kidijitali.

Katika haya yote, lazima kukumbuka kuwa programu kama hizi za kampuni za simu zimewezekana kutokana na miaka mingi ya uwekezaji wa kampuni hizi. Uwekezaji huo umejenga msingi wa mipango kama hii ambayo inawapa nguvu na kuwainua wanawake pamoja na jamii kwa ujumla. Ili kuhakikisha kwamba kampuni hizi zinaendelea na mipango ya namna lazima taifa letu liendee kuunga mkono ukuaji wa sekta hiyo kwa kuipa mazingira bora ya uwekezaji na sheria bora za kiuendeshaji.

Tuendelee kufanya kazi pamoja kuunga mkono mipango kuwainua watoto wa kike na wanawake kwa ujumla.


TTCL YAWEZESHA MKUTANO WA SADC KUFANYIKA KWA 'VIDEO CONFERECE'

$
0
0
Pichani ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwasalimia wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC (hawapo pichani) alipokuwa akifungua mkutano huo leo jijini Dar es Salaam uliofanyika kwa njia ya mtandao (Video Conference) kufuatia mlipuko wa ugonjwa hatari wa Corona unaoendelea kuzikumba nchi nyingi duniani. Huduma ya 'Video Conference' imewezeshwa na Shirika la Masiliano Tanzania, TTCL. 
Pichani ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwapungia mkono wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC (hawapo pichani) alipokuwa akifungua mkutano huo leo jijini Dar es Salaam uliofanyika kwa njia ya mtandao (Video Conference) kufuatia mlipuko wa ugonjwa hatari wa Corona unaoendelea kuzikumba nchi nyingi duniani. Huduma ya 'Video Conference' imewezeshwa na Shirika la Masiliano Tanzania, TTCL. 
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC na wageni waalikwa upande wa Tanzania wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa akifungua mkutano huo leo jijini Dar es Salaam uliofanyika kwa njia ya mtandao (Video Conference) kufuatia mlipuko wa ugonjwa hatari wa Corona unaoendelea kuzikumba nchi nyingi duniani. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Masiliano Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuelezea namna shirika hilo lilivyofanikisha kufanyika kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao (Video Conference) kufuatia mlipuko wa ugonjwa hatari wa Corona unaoendelea kuzikumba nchi nyingi duniani. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Masiliano Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuelezea namna shirika hilo lilivyofanikisha kufanyika kwa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika kwa njia ya mtandao (Video Conference) kufuatia mlipuko wa ugonjwa hatari wa Corona unaoendelea kuzikumba nchi nyingi duniani. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bi. Puyo Nzalayaimisi. 

Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA la Masiliano Tanzania, TTCL limefanikisha Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC) kufanyika kwa njia ya mtandao (Video Conference) kufuatia mlipuko wa ugonjwa hatari wa Corona unaoendelea kuzikumba nchi nyingi Duniania.


Mkutano huo umeanza Machi 16 mwaka huu kwa maofisa waandamizi kutoka nchi 16 wanachama kushiriki vikao wakiwa katika nchi zao, kabla ya kufunguliwa rasmi jana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam huku akiwahutubia mawaziri wote wakiwa katika nchi zao.

Mkutano huu wa mawaziri wa SADC pamoja na mambo mengine unajadili hatua zaidi za utekelezaji wa Kauli mbiu ya mwaka huu ya Jumuiya ya SADC inayosema 'Mazingira wezeshi kwa ajili ya Maendeleo Endelevu na Jumuishi ya Viwanda, Kukuza Biashara na Ajira ndani ya SADC'.

Akizungumza na Wandishi wa Habari mara tu baada ya Mhe. Waziri Mkuu kufungua mkutano huo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amesema kufanikisha mkutano huo kufanyika kwa mfumo wa 'video conference' ni jambo la kujivunia kama nchi kwani limewezesha kukidhi matakwa ya Shirika la Afya Duniani la watu kujihepusha na misongamano ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Amesema TTCL imeandika historia mpya ya kuwezesha mkutano huo kufanyika kisasa zaidi kwani hii ni mara ya kwanza kwa nchi wanachama wa SADC kufanikisha mkutano huo kwa mfumo wa 'video conference'. "Tanzania imewekwa kwenye kumbukumbu kwani imeweza kufanya mkutano huo kwa njia ya 'video conference' hii ikiwa ni mara ya kwanza," alisema Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Kindamba.

Amesema hatua hii imefanikiwa ikiwa ni kutii maagizo ya Mwenyekiti wa SADC Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli baada ya Mawaziri wa Afya wa SADC kukutana kwa kikao cha dharura jijini Dar es Salaam na kushauri vikao vyote vya jumuiya hiyo vifanyike kwa njia ya mtandao mpaka hapo ugonjwa wa Corona utakapodhibitiwa.

“Tumewezesha na tumelifanikisha kwa vitendo suala hili hivyo niwapongeze sana wahandisi wa TTCL na Wizara husika pamoja na wadau wote kwakuhakikisha jambo hili linawezekana bila mkwamo wowote,” Alisema Kindamba.

Aidha aliongeza kuwa TTCL imeweza kuunga mkono juhudi za serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kutoa mchango wake wa huduma hiyo ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona, ambapo ushauri wa wizara hiyo ilikuwa kupunguza mkusanyiko wa wananchi kujiepusha na maambukizi ya corona.

Hata hivyo, Waziri Kindamba amewatoa wasiwasi taasisi, mashirika ya umma na binafsi kuwa TTCL inatoa huduma hii kuwezesha mikutano, semina, warsha na elimu mtandao kwa watakaohitaji huduma hiyo ili kufanikisha majukumu hayo hasa katika kipindi hiki ambacho Dunia iko kwenye mapambano ya ugonjwa wa corona na kuzuia msongamano.

Kindamba amebainisha kuwa mpaka sasa zipo taasisi zaidi ya sita amabazo zimeomba huduma hii ili kuwa sehemu ya mapambano ya corona. TTCL kwa kushirikiana na Wizara ya Afya imeweka namba maalum kwa ajili ya mtu kupiga simu bure kutoa taarifa za mgojwa wa Corona au kujipatia taarifa mbalimbali kuhusu ugonjwa huu.

"…sisi na Wizara ya Afya tumeweka timu moja kwa ajili ya kituo cha miito (call center) ili kuwahudumia wananchi saa ishirini na nne waweze kutoa taarifa za mtu mwenye dalili za ugonjwa wa corona au kujipatia taarifa mbalimbali kuhusu ugonjwa huu,” alisema Kindamba.

WAZIRI KAMWELWE AITAKA LATRA KUCHUKUA HATUA KUKABILIANA NA CORONA KWENYE VITUO VYA MABASI

$
0
0
Charles James, Globu ya Jamii
SERIKALI imeziagiza Halmashauri za Majiji na Miji kukaa na Mamlaka za Udhibiti Usafiri wa Ardhini (LATRA) ili kuweka utaratibu maalum ambao utadhibiti mrundikano na wingi wa watu kwenye vituo vikuu vya mabasi.

LATRA na Halmashauri hizo zimepewa siku tatu kuhakikisha zinaratibu agizo hilo ikiwa ni hatua za serikali katika kujikinga na maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma leo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema wadau wote wa usafiri kwa kushirikiana na wataalamu wa afya na Shirika la ViwangoTanzania (TBS) wakae pamoja ili kuangalia njia gani watakazotumia katika kudhibiti wingi wa abiria vituoni.

Mhandisi Kamwelwe pia amewataka madereva na makondakta wa mabasi ya mijini kutekeleza kwa vitendo maelekezo watakayopewa juu ya idadi ya abiria wa kusimama kama itakavyoshauriwa na wataalam.

" Mamlaka hizo pia zinatakiwa kutenga vyumba maalumu kwa ajili ya abiria watakao bainika kuwa na dalili hizo ili vyumba hivyo viweze kutoa huduma ya kwanza huku taratibu nyingine za kuwafikisha sehemu ya tiba zikifanyika", Ameagiza Waziri Kamwele

Kuhusu usafiri wa Treni, Mhandisi Kamwelwe ameliagiza Shirika la Reli Nchini (TRC), lile la Tanzania na Zambia (TAZARA) Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) kuweka vitakasa mikono kwenye vyombo vyao vyote vya usafiri ikiwa ni agizo la Waziri wa Afya katika kukabiliana na mamabukizi hayo.

Mhe Kamwelwe pia ametoa wito kwa mamlaka hizo kushirikiana na wataalam wa afya katika kutoa elimu kwenye vituo vya mabasi, bandari, kwenye vivuko, uwanja wa ndege na kwenye stesheni ili kuwasaidia wananchi ambao ndio wasafiri kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa huo.

Hospitali ya wilaya ya Njombe “piga ua” lazima itoe huduma mwezi julai

$
0
0
Na Amiri kilagalila,Njombe
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe mkoani humo Ally Juma Ally ameihakikishia kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa LAAC kuwa halmashauri hiyo inategemea kuanza kutoa huduma za afya katika hospitali mpya ya wilaya mapema itakapofika mwezi wa saba mwaka huu.

Bwana Ally Juma ameieleza kamati kuwa majengo ya hospitali ya halmashauri ya wilaya yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 98,hivyo hakuna jambo lolote litakalo kwamisha kuanza kutoa huduma kwa kuwa shughuli ndogo zilizobakia zinaendelea kushughulikiwa.

“Kama mnavyoona majengo haya yamekamilika kazi iliyobaki ni kazi ya kuweka mifumo,kuchimbo mashimo ya taka,lakini tumeshafunga milango,vioo vipo tayari na tumeshavuta umeme kutoka barabarani kwa hiyo hatua tulizofikia ni kama asilimia 98 au 99 na tumebakiwa na shughuli ndogo ndogo ambazo piga ua lazima julai tuanze kutoa huduma hapa”alisema Ally Juma Ally

Aidha Mkurugenzi amesema mradi wa ujenzi wa hospitali  ya wilaya ya Njombe,mpaka sasa umetumia bilioni 1.5 iliyotolewa na Rais Magufuli lakini halmashauri hiyo ilitenga milioni 100 kwa ajili ya kuchangia mradi huo na mpaka sasa imekwishatoa milioni 65.

Hata hivyo bwana Ally Juma ametaja sababu za kuchelewa kukamilika kwa mradi huo ni pamoja na mvua kubwa zinazonyesha katika wilaya ya Njombe.

“Huu mradi tungemaliza mapema sana lakini changamoto kubwa iliyotusibu ni mvua,kwa hiyo masika ilibidi tusimamishe ujenzi,lakini changamoto nyingine ya pili tulikuwa tunasafirisha material umbali mrefu sana,lakini tunajito kupambana ili majengo haya yaweze kukamilika”alisema tena Ally Juma

Edward Mwalongo ni mbunge wa jimbo la Njombe mjini na Ezekiel Maige ni mbunge wa jimbo la Msalala ambao ni miongoni mwa wajumbe wa kamati ya LAAC walihoji vigezo vilivyotumika kujenga hospitali hiyo ya wilaya katika kata ya Matebwe ambayo ipo takribani kata za mwisho za wilaya,ambapo mkurugenzi amekiri kujengwa katika maeneo hayo kutokana na sababu mbali mbali

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati LAAC Abdalah Chikota amepongeza kasi ya ujenzi wa hospitali ya wilaya hiyo na kuomba sasa huduma inaanza kutolewa katika majengo hayo.

“Mkurugenzi na DMO sasa hakikisheni tunakwenda kwenye matumizi ya hii hospitali na sisi lengo tuone huduma imeanza kutolewa,kwa majengo mmejitahidi kusimamia na hali inaonekana sasa nguvu kubwa tuelekeze kwenye matumizi ya haya majengo”alisema Chikota.

Hospitali ya wilaya ya Njombe ni miongoni mwa hospitali 67 zinazojengwa hapa nchini kwa ghalama ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na Rais kwa wilaya tofauti tofauti huku ikitakiwa kujengwa majengo 7 kwa kutumia mafundi wa ndani.

Aidha kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa ikiwa wilayani Njombe,wabunge wamefanikiwa kukagua mradi huo wa ujenzi wa hospitali inayojengwa kata ya Matembwe,Mradi wa maji wa Kidegembye pamoja na mradi wa umwagiliaji wa kikundi cha Twilumba uliopo kijiji cha Itipinga kata ya Igongolo na kuridhishwa na miradi hiyo.
Mkurugenzi wa halmashauri ya  wilaya ya Njombe bwn Ally Juma Ally akiieleza kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za serikali ulipofikia mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Njombe


Baadhi ya majengo ya hospitali ya wilaya ya Njombe wakati yakikaguliwa na kamati ya bunge ya kuduma ya hesabu za serikali za mitaa.
 Makamu mwenyekiti wa kamati ya LAAC akizungumza mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Njombe
 Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akinawa mikono kutokana na tahadhari ya korona mara baada ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Njombe.
Kamati ya bunge ya kudumu ya hesabu za serikali za mitaa wakizungumza katika mradi wa umwagiliaji uliopo Kijiji cha Itipingi.

LIGI TANZANIA KUCHEZWA BILA WATAZAMAJI

$
0
0
KIKAO cha Kamati ya Uongozi cha TFF kimeazimia kuwa, baada ya siku 30 serikali itakaporuhusu michezo kuendelea, mechi za ligi kuu, ligi daraja la kwanza, ligi daraja la pili na ligi ya mabingwa wa mikoa (RCL) zitachezwa bila watazamaji, ili kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Corona.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almas Kasongo mara baada ya kikao hicho ambacho kimehudhuriwa pia na Rais wa TFF, Wallace Karia.

Kasongo amesema pia kuwa wachezaji wote watafanyiwa vipimo maalum kuchunguzwa endapo wameathirika na virusi vya Corona au la kabla ya ligi hizo kurejea.

PSPTB YASIMAMISHA UTOAJI WA MAFUNZO ILI KUEPUKANA NA CORONA

$
0
0

BODI ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB)  imesitisha utoaji wa mafunzo yaliyopanga kufanyika kuanzia Machi 18 mwaka huu na kuwataka wadau kusubiri hadi pale itakavyopangwa tena.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bi Shamim Mdee, Afisa mwandamizi masoko na uhusiano kwa umma wa Bodi hiyo imeelezwa kuwa kusitishwa kwa mafunzo hayo kumetokana na tamko rasmi la Serikali kupitia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzuia uwepo wa mikusanyiko ya watu katika maeneo mbalimbali nchini na hiyo ni mara baada ya kuthibitishwa kuwepo kwa maambukizi ya virusi ya Corona (Covid 19) ambapo hadi sasa visa vitatu vimeripotiwa nchini.

Bodi hiyo imewataka wadau na wananchi kwa ujumla kufuata taratibu zilizowekwa katika harakati za kupambana na maambukizi na hiyo ni pamoja na miongozo ya afya iliyotolewa na Wizara husika ikiwemo kunawa mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka na kuepuka kushikana  mikono kwa kipindi hiki ambacho maambukizi ya virusi vya Corona (Covid 19)  yanashika kasi kote duniani.

AHADI YA RAIS MAGUFULI KWA MAAFISA TARAFA YATIMIA, WAPATIWA PIKIPIKI NCHI NZIMA

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Kapteni George Mkuchika na Wakuu wa Mikoa wa Dodoma na Singida pamoja na Makatibu Tawala wao wa Mikoa baada ya kukabidhiwa pikipiki za maafisa tarafa kwa niaba ya Wakuu wa mikoa wenzao wa mikoa 24.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi wakuu wa mikoa pikipiki kwa ajili ya maafisa tarafa wao leo jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Kapteni George Mkuchika akizungumza katika hafla ya utoaji pikipiki kwa maafisa tarafa wa mikoa 24 ya Tanzania bara leo jijini Dodoma.
 Baadhi ya pikipiki ambazo zimetolewa na serikali ikiwa ni ahadi ya Rais Dk John Magufuli kwa maafisa tarafa wote nchini. Pikipiki hizi zimegaiwa leo jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Mhe Jafo kwa wakuu wa mikoa 24 ya Tanzania bara.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk Rehema Nchimbi akionesha moja ya funguo za pikipiki ambazo amekabidhiwa kwa ajili ya maafisa tarafa wake wote. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora, Kapteni George Mkuchika.

Charles James, Globu ya Jamii
SERIKALI katika kuthamini kazi inayofanywa na Maafisa Tarafa wake nchini leo imekabidhi jumla ya Pikipiki 448 kwa maafisa tarafa wa Mikoa 24 nchini zenye thamani ya Sh Bilioni Moja.

Hafla ya kukabidhi pikipiki hizo imefanyika leo katika mji wa kiserikali wa Mtumba jijini Dodoma ambapo Wakuu wa Mikoa ya Dodoma na Singida wamepokea kwa niaba ya wakuu wenzao wa mikoa.

Akizungumza kabla ya kukabidhi pikipiki hizo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo amesema pikipiki hizo zimenunuliwa na serikali ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Mhe Rais Dk John Magufuli aliyoitoa katika kikao chake na maafisa tarafa hao Juni 4, 2019.

Mhe Jafo amesema serikali ya awamu ya tano inatambua changamoto ya vitendea kazi kwa watumishi wake nchini na kwamba itaendelea kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo kadri mapato yatakavyoimarika.

" Ninyi ni mashahidi kuwa katika mwaka huu wwa fedha serikali imezipatia ofisi zenu magari kwa ajili ya viongozi wa Mikoa, Wilaya na Mamlaka za serikali za mitaa  na kuajiri maafisa tarafa na watendaji wa kata, walimu na watumishi wa sekta ya afya kwa wingi. Kama serikali tumedhamiria kwa vitendo kuboresha ofisi za umma.

Niwatake kuhakikisha pikipiki hizi zinawafikia walengwa ambao ni maafisa tarafa kwa kuzingatia mgawanyo wa tarafa mlizoziwasilisha, lakini pia Wakuu wa Mikoa hakikisheni zinatumika kwa shughuli za serikali katika maeneo yenu na si vinginevyo," Amesema Jafo.

Amewataka Wakuu wa Mikoa wote nchini kuwa wasimamizi wa Vyombo hivyo ili viweze kudumu kwa muda mrefu na kutoa huduma kwa wananchi na kuhakikisha pia vinafanyiwa matengenezo kwa wakati.

" Pikipiki hizi 448 ni kwa mikoa 24 ambayo ilikua haijapata kwa sababu tayari mikoa ya Songwe na Pwani ilishapatiwa. Kwa hesabu ya leo maana yake Serikali tumetoa pikipiki kwa maafisa tarafa wetu wote nchi nzima," Amesema Jafo.

Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa wenzake, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk Rehema Nchimbi ameahidi kusimamia vyombo hivyo ili vitumike kwa ajili ya wananchi na siyo matumizi binafsi.

" Nikuahidi Mhe Waziri kwamba pikipiki hizi zitaenda kwa walengwa hasa wale wenye leseni, lakini pia zitatumika kama ambavyo tumeelekezwa na siyo kuzigeuza kuwa vitega uchumi vyao.

Zaidi ya yote tunamshukuru sana Mhe Rais Dk Magufuli kwa kufanikisha upatikanaji wa Vyombo hivi ambavyo sasa vinaenda kuwa mwarobaini wa changamoto ya usafiri kwa watumishi wetu hawa hii inaonesha jinsi Mhe Rais ni mtendaji wa ahadi wa ahadi zake, " Amesema Dk Nchimbi.

UTUMISHI YAPOKEA VITENDEA KAZI TOKA UNDP KUBORESHA UTENDAJI

$
0
0
James Mwanamyoto - Dodoma
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, katika kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi, imepokea vitendea kazi vya kielektroniki toka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Vitendea kazi vilivyopokelewa ni Kompyuta saba (7), “printer” 10 na kompyuta mpakato tatu (3) vyenye thamani ya shilingi 45,919,500/=.

Akipokea vitenda kazi hivyo leo toka kwa Bw. James Bwana, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amemshukuru kwa jitihada zake za kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi hivyo toka UNDP. Awali, James Bwana alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Rais, Utumishi.

“Nakupatia kompyuta mpakato moja itakayokuwezesha kutekeleza majukumu yako ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wako katika upatikanaji wa vitendea kazi hivyo.” Dkt. Ndumbaro amesisitiza.

Aidha, Dkt. Ndumbaro ameishukuru UNDP kwa kutoa vitendea kazi hivyo vitakavyosaidia kuongeza ufanisi wa kiutendaji kwa watumishi wa ofisi yake.

Kwa upande wake, Bw. Bwana, amemshukuru Dkt. Ndumbaro kwa kumpatia ridhaa ya kufanya mchakato wa upatikanaji wa vifaa hivyo toka UNDP kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia) akimpongeza Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana kwa kuwezesha kupatikana kwa vitendea kazi vya kielektroniki toka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Umoja wa Mataifa (UNDP) mara baada ya Katibu Tawala huyo kukabidhi vitendea kazi hivyo leo katika ukumbi wa Ofisi ya Rais, Utumishi, Mtumba jijini Dodoma.
 Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana akitoa maelezo ya vitendea kazi vilivyotolewa na UNDP kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia) katika ukumbi wa Ofisi ya Rais, Utumishi, Mtumba jijini Dodoma leo.
 Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana, akionyesha nyaraka zenye orodha ya vitendea kazi vilivyotolewa na UNDP kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia).
 Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Utumishi, Bw. Victor Ngole, akipokea nyaraka leo toka kwa Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana zinazoonyesha orodha ya vitendea kazi vilivyotolewa na UNDP. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro.

Vitendea kazi vya kielektroniki vilivyotolewa na UNDP kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi vikishushwa leo kwa ajili ya makabidhiano rasmi katika ofisi hiyo, Mtumba jijini Dodoma.

NAIBU WAZIRI MGALU ASEMA BOMBA LA GESI KUVINUFAISHA VIWANDA VIPYA 50 PWANI,DAR NA MTWARA

$
0
0
VICTOR MASANGU, MKURANGA
 Naibu Waziri wa nsihati Subira Mgalu alisema kwamba katika kutimiza azma ya Tanzania kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 serikali imedhamilia kusambaza na kuwaunganishia  nishati ya umeme wa gesi asilia  katika viwanda vipya vipatavyo 50  ambavyo vimepitiwa na bomba la gesi ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam Pwani pamoja na Mtwarana kuongeza gharama za umeme zitashuka pindi mradi wa bwawa la umeme mwalimu nyerere utakapomalika Juni 2022 na kuzalisha mega wati 2115.

Mgalu  aliyasema hayo wakati wa ziara ya kikazi ya  kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na Madini ambayo yameifanya  kwa lengo la kutembelea baadhi ya viwanda vilivyopo Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani  ambavyo vinajiendesha kwa kutumia nishati ya umeme ikiwa pamoja na kuzungumza na wawekezaji ili kubaini changamoto wanazokabiliana nao na kuzitafutia ufumbuzi.

Naibu Waziri huyo alibainisha kwamba kwa sasa serikali ya awamu ya tanoi mpango wake mkubwa ni kuhakikisha inasambaza na kuviunganishia viwanda mbali mbali nishati ya umeme ili viweze kutimiza malengo ya azma y serikali ya kuwa na uchumi wa kati pamoja na kutoa fursa  mbali mbali za ajira kwa vijana  ambao ni wazalendo  lengo ikiwa waweze kujikwamua na wimbi la umasikini.

“Mpango wetu wa serikali licha ya kuwa bado kuna baadhi ya maeneo ya viwanda hayajafikiwa na nishati ya umeme lakini kwa sasa kupitia nishati ya gesi asilia tuna mpango wa kuviunganishia viwanda vipya vipatavyo 50 ambavyo vipo katika Mikio ya Dar es Salaam, Mtwara pamoja na Mkoa wa Pwani hivyo juhudi za makusudi bado zinaendelea kwa hiyo viwanda ambavyo vinapitiwa na bomba kubwa la gesi vitaweza kunufaika.

Aidha Naibu Waziri huyo alifafanya kwamba pindi mradi wa umeme wa bwawa la Malimu Nyerere uliopo Wilayani Rufiji utakapokamilika utaweza kuwa ni mombozi mkubwa kwa wawekezaji wa viwanda vidogo, vya kati na vile vikubwa kutoka maenne mbali mbali sambamba na kuwaunganishia wananchi wengine pamoja na taasisi za serikali na sizozo  za serikali.

Katika hatua nyingine Mgalu ameipongeza kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini kwa kuweza kwenda kutembelea katika kiwanda cha kuzalisha chuma pamoja na mabomba ya maji ili kuweza kubainichangamoto mbali mbali ambazo zinawakabili wawekezaji na hatimaye kuweza kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambao utasaidia kutimiza azma ya serikali ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda hivyo.

Kwa upande wake  Kaimu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na Madini Vedastus Matayo alibainisha kwamba ujenzi wa kiwanda hicho utaweza  kuipunguzia serikali gharama kubwa ambazo zimekuwa zikitumia kwa ajili ya kuagiza baadhi ya Nondo kutoka nje ya nchi hivyo amempongeza mwekezaji huyo kwa  kuwekeza katika  Wilaya ya Mkuranga kwani kumesaidia vijana zaidi ya 1 300 kupata fursa ya ajira.

“Sisi kama kamati kwa kweli tunapenda kumpongeza mwekezaji huyo kwa kuweza kuwekeza katika Wilaya ya Mkuranga ambayo ipo katika Taifa letu ya Tanzania hii ni hatua nzuri ambayo ameifanya na kwa sasa anazalisha bidhaa mbali mbali kwa kutumia nishati ya umeme wa gesi asilia hivyo kutaweza kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi wenyewe pamoja na wale wawekezaji wa ndani na nje ya nchi,”alibainisha  Matayo

Aidha Matayo katika hatua nyingine alibainisha kuwa Kamati ya bunge ya nishati ya kudumu ya nishati na  madini  ilibaini kuwepo kwa urasimu na ucheleweshaji wa vibali kutoka kwa baaadhi ya mamlaka zinazohusika kwa wawekezaji wa sekta ya viwanda pamoja na gharama ya nishati ya umeme kuwa ni kubwa hivyo hivyo watayachukua mapendekezo hayo kwa ajili ya kuyawasilisha bungeni ili serikali iweze kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu.

Pia alisema kuwa mapendekezo pamoja na changamoto mbali mbali ambazo wamekutana nazo katika kiwanda hicho ikiwemo na maeneo mengine ambayo tayari wameshayapitia watayawasilisha serikalini ili yaweze kufanyiwa kazi ikiwemo na kutilia mkazo katika suala la usumbufu mkubwa wanaoupata wawekezaji pindi wanapohitaji kuagiza matilio mbali mbali kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zao.

Awali  akitoa taarifa mbele ya Kamati ya nishati na madini Mkurugenzi mtendajiwa wa kiwanda hicho cha kuzalisha chuma Haluni Lodhia amebainisha kwamba hapo awali walikuwa wanakabilia na changamoto kubwa ya ukosefu wa nishati ya umeme wa uhakika pamoja na miundombinu ya barabara,ambapo ameipongeza serikali ya awamu ya tano kupitia Shirika la maendeleo ya  Petroli Tanzania (TPDC) kwa litafutia ufumbuzi suala hilo na hatimaye kuanza utekelezaji wa kuzalisha bidhaa mbali mbali, ikiwemo Nondo, mabomba ya maji na bodi za jasi.
Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu akizungumza jambo kuhusiana na mikakati ya serikali ya awamu ya tano ya kuweka mipango ya kuunganisha nishati ya umeme wa gesi asilia katika viwanda vipya 50 wakati wa ziara ya Kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na madini ambayo ilifanya ziara yake ya kikazi ya kutembelea baadhi ya viwanda vilivyopo katika Wilaya ya Mkuaranga.
Badhi ya wabunge wanaounda kamati ya nishati na madini wakati wanaingia katika kiwanda cha kuzalishia chuma cha Lodhia ikiwa ni moja ya ziara yao ya kikazi kwa ajili ya kuijionea shughuli mbali mbali zinazofanywa na wawekezaji pamoja na kubaini changamoto zao, wa kati kati ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa.
Kaimu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya nishati na Madini Vedastus Matayo akipokea maelekezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa kiwanda cha kuzalishia chuma cha Lodhia kilichopo kata ya Kisemvule wakati wa ziara ya kamati hiyo ilipokwenda kwa ajili ya kujionea shughuli mbali mbali za uzalishaji kiwandani hapo
Mmoja wa wakurugenzi wa kiwanda cha Lodhia ambacho kinajishighulisha na uzalishaji wa bidhaa mbali mbali ikiwemo chuma, akiwaonyesha wajumbe wa kamati ya bunge ya nishati na madini jinsi ya kiwanda hicho kinavyofanya kazi pamoja na kuwaelezea changamoto mbali mbali zinazowakabili ili kuziwasilisha kwa serikali zifanyiwe kazi.
Mwonekano wa mtambo maalumu wa kuzalishia nishati ya umeme wa gesi asilia ambao umefunngwa na  shirika la TPDC katika kiwanda hicho cha kuzalishia chuma pamoja na kutengenezea  mabomba ya maj wakati wa ziara hiyo ya kamati ya bunge ya nishati na madini.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya bunge ya nishati na madini wakiwa na viongozi mbali mbali wa kiwanda hicho wakitembezwa katika maeneo mbali mbali ili kuweza kujionea mwenendo mzima wa vyuma chakavu vinavyoyayushwa na kutengenezwa Nondo mpya kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ikiwemo ile ya serikali.
Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Lodhia  Haruni Lodhia ambacho kinajihusisha na uzalishaji wa kutengeneza Nondo pamoja bidhaa zingine mbali mbali akizungumza mbele ya wajumbe  kamati ya bunge ya nishati na madini  hawapo pichani ilipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea kiwanda hicho.(Picha na Victor Masangu)

JIJI LA DODOMA LAKABIDHI MAGARI YENYE THAMANI YA SH MILIONI 345 KWA WATAALAMU WAKE WA MIPANGO MIJI

$
0
0
Charles James, Globu ya Jamii

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma limekabidhi magari matatu kwa Idara ya Mipango Miji kwa ajili ya kurahisisha shughuli za wataalamu wake katika kudhibiti ujenzi holela kwenye jiji hilo.

Hayo yamefanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Mhe Kassim Majaliwa la kusimamia utekelezaji wa mpango kabambe wa Jiji la Dodoma.

Akizungumza wakati wa kukabidhi magari hayo, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi amesema magari hayo yamegharimu kiasi cha Sh Milioni 345 kwa idara ya mipango miji ambapo yatatumiwa na ofisi ya udhibiti ujenzi holela, mkuu wa upimaji na mkuu wa idara ya mipango miji.

Kunambi amesema halmashauri ya jiji inaamini ili kutekeleza agizo la MWaziri Mkuu ni lazima wawe na vitendea kazi ambavyo vitarahisisha ufanyaji kazi wa watalaamu wao.

" Mhe Mkuu wa Mkoa tunakushukuru kwa kuja kwenye tukio letu hili, haya ni mafanikio makubwa kwetu katika kuondoa changamoto ya vitendea kazi kwa wataalamu wetu ambao wanakua field muda wote kuhakikisha wanaondoa tatizo la ujenzi holela kwenye jiji letu.


Fedha hizi Milioni 345 ni fedha zetu za mapato ya ndani, Jiji la Dodoma hatuombi fedha serikali kuu kama halmashauri zingine. Sasa tunaamini hakuna nyumba yoyote ambayo itawekea X kwa sababu kabla hata ya kujenga wataalamu wetu watakua wameshatoa elimu kwa wananchi juu ya maeneo gani ya kujenga na ya yapi hayafai kujenga," Amesema Kunambi.

Ameongeza kuwa Jiji la Dodoma linapiga hatua kutokana na ushirikiano uliopo baina ya Ofisi yake, Mkuu wa Wilaya pamoja na Baraza la Madiwani linaloongozwa na Mstahiki Meya, Prof Davis Mwamfupe.

" Mhe RC hakuna Jiji lingine ambalo limepangwa vizuri kwa asilimia 100 zaidi ya Jiji letu la Dodoma, lakini pia Jiji letu limepimwa kwa asilimia 60 hatutaki kabisa kuharibu madhari ya Jiji letu na tunakuhakikishia mpango kabambe tuliokabidhiwa na Mhe Waziri Mkuu tutautekeleza kwa asilimia 100," Amesema Kunambi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amelipongeza jiji hilo kwa kupiga hatua ya kuwanunulia watalaamu wake magari ambayo pia yatakua msaada kwa wananchi waliokua wanasafiri umbali mrefu kufika ofisi za Jiji.

" Sitegemei kuwaona watalaamu ofisini, hizi gari tunazowakabidhi leo zitumieni vizuri kwa kwenda field walipo wananchi, muwape elimu nzuri ili kuepusha changamoto za baadae za ujenzi holela.

Hatutaki tena kuona ujenzi holela, wala kuona alama za X maana zikiendelea kuwepo zinatoa picha kwamba nyie watalaamu wetu hamfanyi kazi ipasavyo licha ya kukabidhiwa magari mazuri yanayorahisisha utendaji kazi wenu," Amesema Dk Mahenge.


RC Mahenge amelitaka Jiji la Dodoma kuhakikisha linaondoa pia changamoto ya wananchi kujenga kwenye maeneo ya wazi, milima pamoja na maeneo ya hifadhi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge akizungumza na wandishi wa habari baada ya kutoka kukabidhi magari matatu kwa idara ya mipango miji ya Jiji la Dodoma ili kusaidia kuongeza ufanisi wao wa kazi. Kulia ni Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge akimkabidhi ufunguo wa gari Mkuu wa Idara ya Mipango Miji ya Jiji la Dodoma, Pius Mafuru katika hafla iliyofanyika leo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi akizungumza na wandishi wa habari baada ya halmashauri ya Jiji lake kukabidhi magari kwa watalaamu wake wa mipango miji ili yaweze kusaidia katika kazi zao za kudhibiti ujenzi holela.
Mojawapo ya gari tatu ambazo Halmashauri ya Jiji la Dodoma imezikabidhi kwa Idara yake ya Mipango Miji leo ili kusaidia kuboresha ufanisi kazi wao katika kudhibiti ujenzi holela wa Jiji hilo.
Viewing all 119562 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>