Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 119398 articles
Browse latest View live

IGP SIRRO AFANYA ZIARA YA UKAGUZI MKOA WA KIPOLISI ILALA

$
0
0



Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati) akizungumza na Maofisa wa Jeshi hilo leo jijini Dar es salaam, wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika mkoa wa Kipolisi Ilala kwa lengo la kuona utayari wao na namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kazi za Kipolisi. Picha na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, akizungumza na askari wa Jeshi hilo leo jijini Dar es salaam, wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika mkoa wa Kipolisi Ilala kwa lengo la kuona utayari wao na namna wanavyotekeleza majukumu yao ya kazi za Kipolisi. Picha na Jeshi la Polisi.

MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ZAHARIBU MAZAO WILAYANI LUDEWA MKOANI NJOMBE

$
0
0
Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo wilaya ya Ludewa iliyopo mkoani Njombe imepelekea kufanya uharibifu wa mazao mbalimbali ikiwemo mahindi na kushusha kiwango cha uzalishaji kutoka tani laki moja na elfu kumi na moja kwa mwaka jana mpaka kufikia tani isiyozidi laki moja kwa mwaka huu 

Akizungumzia suala hilo mkuu wa wilaya ya Ludewa Adrea Tsere amesema wilaya yake inaongoza kwa uzalishaji mkubwa wa zao la mahindi katika mkoa wa Njombe ambapo kwa mwaka jana ilivuna tani laki moja na elfu kumi na moja ambapo tani elfu sitini kwaajili ya matumizi ya chakula na tani 51 kwaajili ya biashara na mpaka sasa wamebakiwa na mahindi ya biashara tani 615.

Alisema wilaya hiyo ina jumla ya tarafa tano ambapo tarafa tatu amzazo ni Mlangali, Mawengi pamoja na Liganga huzalisha mahindi kwa wingi huku tarafa ya Masasi na Mwambao huzalisha mihogo na ufuta kidogo.

Alisema mvua hizi zimeleta athari katika baadhi ya maeneo ya tarafa ya mwambao ukanda wa ziwani ambao zao lao kuu ni mihogo mvua hizi zimeleta mafuriko katika mto Luhuhu na kupelekea baadhi ya mashamba ya mihogo kwenda na maji.

“Tarafa hii ya mwambao imeathirika kwa kiwango kikubwa na kusababisha upungufu wa chakuala kwakuwa watu wa ukanda huu hutegemea zaidi zao hilo kwaajili ya kupata unga n.k”, Alisema Tsere.

Aidha kwa upande wa mmoja wa wakulima hao Aliyefahamika kwa jina la Agatha Haule alisema kuwa mvua za mwaka huu zimekuwa nyingi zaidi tofauti na miaka mingine na zimekuwa na athari katika mazao yao ya mahindi pamoja na maharage.

Alisema maharage yameungua na mengine kuanza kuota kabla hayajavunwa kitu ambacho kimewaleta shida katika kutafuta masoko kwakuwa wateja wengi wanayaona hayana ubora kwakuwa yameungua.
Mkuu wa wilaya ya Ludewa, Andrea Tsere

Waganga wa kienyeji Tunisia wavuna kwa kuuza 'dawa ya Corona'

$
0
0
Katika hali ambayo hakuna dawa mjarabu ya kutibu ugonjwa wa Corona iliyotangazwa rasmi au kuidhinishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), lakini waganga wa kienyeji nchini Tunisia wameendelea kupata faida kubwa kutokana na mauzo ya mitishamba na dawa za kiasili wanazodai kuwa zinatibu Corona.

Katika mji mkuu Tunis, wananchi wameendelea kumiminika katika soka la jadi la Souk el-Blat lenye waganga wa kienyeji kutafuta kinga au tiba ya Corona.

Mbali na kwenda kwa waganga wa kienyeji, baadhi ya Watunisia wanatumia vitunguu saumu kujikinga dhidi ya Corona, jambo ambalo limefanya bei ya bidhaa hiyo iongozeke, na hivi sasa inauzwa dinari 25 (yuro 8) kwa kilo.

Dakta Hedi Oueslati, Mkurugenzi wa Afya ya Umma wa Tunisia amewatahadharisha wananchi dhidi ya kwenda kwa waganga hao wa kienyeji kutafuta tiba ya Corona au kutumia mimea inayodaiwa kutibu Corona.

Dakta Oueslati ambaye pia ni mwanafamasia amefafanua kwa kusema, "nafahamu hofu ya watu iliyowafanya warejee katika tiba asilia, lakini hivi sasa hakuna dawa wala mmea wa muujiza unaotibu Corona."
 

KATIBU MKUU KADIO AWAONGOZA WATENDAJI WAKUU MAGEREZA KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA, WAJUMBE WAKAGUA UJENZI KIWANDA CHA USEREMALA, MSALATO DODOMA

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kabla ya Kamati hiyo kupokea taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Useremala cha Magereza, Msalato Mkoani Dodoma, leo. Wajumbe hayo walitoa ushauri wa kuboresha ujenzi wa Kiwanda hicho ambao tayari umenza. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.   
 Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Salim Mwinyi Rehani, akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo kilichojadili Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Useremala cha Magereza, Msalato Mkoani Dodoma, leo. Wapili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio. Kushoto ni Katibu wa Kamati hiyo, Ramadhani Abdalla, na kulia ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Suleiman Mzee.
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kulia), akisalimana na Katibu wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Ramadhani Abdalla, wakati alipokuwa anawasili na Wajumbe wa Kamati hiyo kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Useremala cha Magereza, Msalato Mkoani Dodoma, leo.

Mhandisi wa Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Useremala cha Magereza, Bonaza Malata (kulia), akiwaonyesha Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Ujenzi wa Kiwanda hicho kilichopo Msalato Mkoani Dodoma, leo. Kamati hiyo ilipokea taarifa ya Mradi huo ambao tayari umeanza na kutoa ushauri wa kitaalamu wa ujenzi wa Kiwanda hicho. Wapili kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Salum Mwinyi Rehani, na watatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio.

Mhandisi wa Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Useremala cha Magereza, Bonaza Malata (kulia), akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kuhusu Ujenzi wa Kiwanda hicho kilichopo Msalato Mkoani Dodoma. Kamati hiyo ilipokea taarifa ya Mradi huo ambao tayari umeanza na pia kutoa ushauri wa kitaalamu wa ujenzi wa Kiwanda hicho. Watatu kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Salim Mwinyi Rehani, na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio.

VODACOM YATAMBULISHA PEPPER ROBOT KWENYE MAONESHO YA UBUNIFU DODOMA

$
0
0

Mratibu wa mradi wa Instant Schools ulio chini ya Vodacom Tanzania Foundation,Christine Lucas (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ,Dk Avemaria Semakafu wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya mashindano ya Sayansi na Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania , Jacquiline Materu (kulia) akiwapa maelezo baadhi ya wananchi kuhusu kazi anazofanya roboti ajulikanaye kwa jina la Pepper ,walipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya mashindano ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknilojia kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania ,Jacquiline Materu (kushoto) akimpa maelezo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia ,Dk.Avemaria Semakafu (kulia) na msafara wake kuhusu kazi anazofanya roboti ajulikanaye kwa jina la Pepper ndani ya banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yaliyoandaliwa na Wizara hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo.

BREAKING NEWZZZZZZZ:SERIKALI YAZIFUNGA SHULE ZOTE KUANZIA LEO SABABU YA CORONA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa



SERIKALI imesema shule zote za awali, msingi na sekondari zitafungwa kwa siku 30 kuanzia leo Machi 17, 2020.



Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo (Jumanne, Machi 17, 2020) wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salam.



Amesema wanafuzi wa kidato cha sita walipaswa kuanza mitihani Mei 4, 2020 lakini nao pia watapaswa kusibiri Wizara ifanye utaratibu mwingine kulingana na matokeo ya hali ya maambukizi.



Amesema mikusanyiko yote mikubwa ya ndani na nje isiyo ya lazima imesitishwa kuanzia sasa ikiwemo shughuli za michezo, matamasha ya muziki, mikutano mbalimbali ikiwemo ya shughuli za kisiasa, mahafali na shughuli nyingine za kijamii.



Amezitaka wizara na taasisi zizitishe semina, warsha, makongamano na mikutano yote hapa nchini ambayo inahusisha washiriki toka nchi zenye maambukizi makubwa. “Watanzania wenye safari zisizo za lazima kwenye nchi zenye maambukizi makubwa, wanashauriwa wasitishe safari hizo,” amesisitiza.



Akielezea hatua nyingine zinazochukuliwa na Serikali ili kudhibiti ugonjwa huo, Waziri Mkuu amesema: “Serikali imesitisha michezo yote inayokusanya makundi ya watu ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL), Ligi Daraja la Pili (SDL) na aina nyngine. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iziandikie taasisi zake.”



Pia amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya wahakikishe maeneo yote yaliyobainishwa na kutengwa (vituo vya huduma na ufuatiliaji) kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa endapo watajitokeza katika maeneo yao yanakuwa na mahitaji yote muhimu na yanahudumiwa ipasavyo.



Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali tayari imetoa shilingi milioni 500 kati ya sh. bilioni moja zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizokuwa zianze Aprili 2, mwaka huu.



“Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizokuwa zianze Aprili 2, mwaka huu na kuagiza shilingi bilioni moja zilizokuwa zimeandaliwa kwa ajili ya shughuli hiyo, zipelekwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya maandalizi ya kujiweka tayari kudhubiti maambukizi ya CORONA. Serikali tayari imetoa shilingi milioni 500.”



Akielezea hatua zilizochukuliwa baada ya mgonjwa wa kwanza kubainika kuwepo nchini Tanzania, Waziri Mkuu amesema Serikali imechukua hatua kwa kumchukua mgonjwa huyo na kumhifadhi kwenye eneo maalum kwa ajili ya kumpatia huduma (isolation).



“Pia, Serikali imefanya ufuatiliaji wa watu waliokutana na mgonjwa huyu tangu aingie nchini na kuwaweka kwenye karantini ya siku 14, na pia kuchukua sampuli kwa lengo la kubaini kama wameambukizwa virusi hivi,” amesema.



Ugonjwa huu umeingia nchini baada ya Mtanzania mwenye miaka 46 aliyesafiri kwenda nchi za Ubeligiji, Sweden na Denmark hivi karibuni, kupimwa na kuthibitika kuwa na virusi vya Corona (COVID-19).



Akielezea hatua zaidi zinazochukuliwa, Waziri Mkuu amesema licha ya hatua ambazo zimechukuliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Serikali itaimarisha ukaguzi na ufuatiliaji wa wasafiri wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege, bandari na mipaka ya nchi kavu ili kuwabaini wasafiri wenye dalili za ugonjwa na viashiria vyenye hatari.



“Tutaimarisha uwezo wa kupima sampuli kwa watu wanaohisiwa kuwa na viashiria au dalili za ugonjwa huu ambapo maabara yetu ya Taifa kwa sasa inao uwezo wa kutoa majibu kwa haraka.”



Amesema Serikali inaendelea kuwajengea uwezo (mafunzo) watumishi wa sekta ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko ikiwemo jinsi ya kutoa tiba, kuchukua sampuli, uelimishaji na kuzingatia kanuni za afya.



“Serikali imetenga hospitali maalum za Mloganzila (DSM), Kituo cha Buswelu (Mwanza) na Hospitali ya Mawenzi (Kilimanjaro), Mnazi Mmoja (Zanzibar) na ChakeChake (Pemba) kwa ajili ya kutoa huduma kwa waathirika.”



Ameiagiza Wizara ya Afya ihakikishe vifaa vya kinga ikiwemo vimiminika vya kudhibiti maambukizi (hand sanitizer) vinapatikana katika maduka yote husika na kwa bei ya kawaida na kuongeza kwamba Serikali itachukua hatua kwa wafanyabiashara watakaobainika kufanya ulanguzi wa vifaa hivyo.



Amewataka Watanzania wazingatie ushauri unaotolewa na Serikali na kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii. “Watanzania tuache mzaha wa kutumia mitandao ya kijamii kufanya upotoshaji wa tahadhari katika jambo hili,” ameonya.



Amewaomba viongozi wa dini waendelee kushirikiana na Serikali katika kuwaelimisha waumini wao wote kuzingatia tahadhari za ugonjwa huu. Pia amevitaka vyombo vyote vya habari vishirikiane na Serikali katika utoaji wa elimu kwa umma kuhusu kujikinga na Corona bila kufanya upotoshaji wala kuipa jamii hofu.



Amewataka wananchi watoe taarifa kuhusu uwepo wa mgonjwa au kupata ufafanuzi kuhusu ugonjwa huu kupitia namba za bure za 0800110124, 0800110125 na 0800110037.

BENKI YA CRDB YAZINDUA MPANGO MAALUM WA KUTOA MAONI KWA NJIA YA "QR CODE"

$
0
0
Benki ya CRDB imezindua mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code. Akizindua mpango huo Mkurugenzi wa Mawasiliano wa benki hiyo, Tully Esther Mwambapa alisema, Njia hiyo itamwezesha mteja kutoa maoni kwa Benki bila usumbufu wowote na kwa muda mfupi sana. 

"Anachotakiwa kufanya mteja ni kuscan kwenye QR Code kwa kutumia simu yake ya smart ambayo imeunganishwa na internet, Mteja atafungua camera ya simu yake na kuscan kwenye QR Code ambazo zinapatikana kwenye matawi yote ya Benki halafu itampeleka moja kwa mojo kwenye website ya CRDB Bank, huko atakutana na maswali ambayo yatamwongoza kwenye kutoa maoni; ikiwa, kuona listi ya Matawi yote ya Banki ambayo atatakiwa kuchagua tawi ambalo anahitaji kulitolea maoni na baada ya hapo atatuma amoni yake, Maoni hayo yatakwenda moja kwa moja kwenye kitengo husika cha Benki ya CRDB na kufanyiwa kazi".

 Aidha Mkurugenzi wa Mawasiliano amewataka wateja kutumia huduma hii kuwasilisha maoni yao amboyo kwanamna moja yatasaidia kuboresha huduma za kibenki na kuendelea kuwahudumia wateja wake kwa weledi mkubwa zaidi bila wasiwasi.

Uzinduzi wa mpango huo wa kutoa maoni, umeanza kutimiwa na Matawi matano ya jijini la Dar es salaam na baadaye huduma hiyo itapatikana kwenye matawi na mawakala wote wa Benki hiyo nchi nzima.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (katikati) akinguzumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB, Mlimani City jijini Dar es salaam, leo Machi 17, 2020. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urio na kushoto ni Meneja Biashara wa Benki ya CRDB Kanda ya Pwani, George Yatera.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kushoto) akionyesha namna ya kutumia mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB, Mlimani City jijini Dar es salaam, leo Machi 17, 2020. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urio na kushuhudiwa na wafanyakazi wengine wa Benki hiyo. Huduma hiyo imezinduliwa kwa kuanza na Matawi matano ya jijini la Dar es salaam na baadaye huduma hiyo itapatikana kwenye matawi na mawakala wote wa Benki hiyo nchi nzima.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (wa pili kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urio (kulia) wakimuelekeza mmoja wa wateja wa Benki ya CRDB, namna ya kutumia mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB, Mlimani City jijini Dar es salaam, leo Machi 17, 2020. Huduma hiyo imezinduliwa kwa kuanza na Matawi matano ya jijini la Dar es salaam na baadaye huduma hiyo itapatikana kwenye matawi na mawakala wote wa Benki hiyo nchi nzima. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Matawi wa Benki ya CRDB, Bonventura Paul
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urio (kulia) wakimuelekeza mmoja wa wateja wa Benki ya CRDB, Beatrice Bariki namna ya kutumia mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika kwenye Tawi la Benki ya CRDB, Mlimani City jijini Dar es salaam, leo Machi 17, 2020. Huduma hiyo imezinduliwa kwa kuanza na Matawi matano ya jijini la Dar es salaam na baadaye huduma hiyo itapatikana kwenye matawi na mawakala wote wa Benki hiyo nchi nzima.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Mlimani City jijini Dar es salaam wakionyesha namna ya kutumia mpango maalumu wa kuwasilisha maoni ya mteja kwa njia ya QR Code, wakati wa uzinduzi wa mpango huo
Picha ya pamoja.







KAMATI YAWAHAKIKISHIA AJIRA WAKAZI WA MBAGALA

$
0
0



Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Hawa Mchafu akipimwa na kifaa maalum kama ana viashiria vya virusi vya Corona kabla ya kuingia kwenye kambi ya mradi wa ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (BRT), kwa awamu ya pili uliopo Mbagala, wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi huo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, akimuonesha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso na Mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Miraji Mtaturu (Kushoto) moja ya nondo katika miundombinu iliyoanza kujengwa ya mabasi ya yaendayo haraka (BRT), wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi huo, jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso, akizungumza na wananchi wa maeneo ya Mbagala, mara baada ya kupokea maombi yao ya kupewa kipaumbele katika mradi wa ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (BRT), ya awamu ya pili, mara baada ya kamati hiyo kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo, jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya moja ya vituo vya mabasi yaendayo haraka (BRT) awamu ya pili, eneo la DUCE jijini Dar es Salaam. Awamu hiyo itahusisha ujenzi wa vituo vya mabasi 29, vituo vikuu vya mabasi (Terminals) 2 na vituo mlisho viwili (2), daraja moja la waenda kwa miguu, ujenzi wa karakana (Depot) 1, barabara yenye urefu wa kilometa 20.3 na Flyovers mbili (2).Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imewahikikishia ajira wananchi wa maeneo ya Mbagala katika mradi wa ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (BRT) kwa awamu ya pili unaoendelea kutekelezwa jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Selemani Kakoso, wakati aliposimamishwa na wananchi wa maeneo hayo wakati kamati hiyo ilipokuwa ikikagua ujenzi wa mradi huo unaotekelezwa na mkandarasi Synohydro Corporation kutoka china kwa muda wa miezi 36.

Kufuatia maelezo ya wananchi hao, Mwenyekiti huyo ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha wanasikiliza kero za wananchi hao ili kuwe na usawa kwenye ajira ambazo zinatolewa kwa wazawa.

"Kilio chenu tumekipokea na sisi kama Kamati tunatoa agizo kwa msimamizi wa mradi kulisimamia hili kwa haki na usawa kwani huu mradi ni wa kitaifa na ndo umeanza", amesisitiza Kakoso.

Ametoa wito kwa wananchi waliopo maeneo jirani na miradi yote inayoendelea kutekelezwa nchini kulinda na kuthamini miradi hiyo kwa kutojihusisha na vitendo vya uhujumu wa miunbombinu kwa kuiba mafuta na vifaa vya ujenzi.

"Watanzania mkipewa kazi kwenye miradi itunzeni iyo heshima mliyopewa kwa kutoshiriki katika matukio ya wizi wa mafuta, saruji na vitu vingine visivyopendeza", amesema Kakoso.

Kuhusu suala la utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa awamu ya pili ya miundombinu ya BRT, Kamati imeipongeza Serikali kwa hatua iliyofikiwa na wataalamu wa ujenzi wa miundombinu hiyo yenye lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

Ameitaka TANROADS kumsimamia mkandarasi vizuri ili aweze kukamilisha miundombinu hiyo kwa muda uliopangwa. "Tunajua kuwa kila siku idadi ya watu inaongezeka hivyo tunahitaji miundombinu imara ambayo iko salama ili itufikishe kwenye uchumi wa kati", amesema Mwenyekiti huyo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hawa Mchafu, ameishauri TANROADS kutoelekeza mifereji ya maji katika makazi ya watu ili kunusuru uhabirifu wa mazingira na mali zao.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo, Zuberi Kuchaukwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Liwale, amewataka wataalamu wa usanifu wa miradi ya barabara nchini kutumia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa ili kupanga vizuri namna ya kuboresha miundombinu hiyo kwa kuwa na madaraja makubwa na makalvati sehemu husika.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, ameihakikishia kamati hiyo kutekeleza maelekezo yote yaliyoelekezwa kwa Wizara na TANROADS na kuusimamia mradi wa BRT kwa viwango na ubora.

Naye, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mhandisi Crispianus Ako, ameieleza kamati hiyo kuwa ujenzi wa mradi huo unahusisha barabara yenye urefu wa kilometa 20.3, Flyovers mbili (2), vituo vya mabasi 29, daraja moja la waenda kwa miguu, ujenzi wa karakana (Depot) 1, vituo vikuu vya mabasi (Terminals) 2 na vituo mlisho viwili (2).

Ujenzi wa Miundombinu ya usafiri wa haraka wa mabasi (BRT), awamu ya pili unahusisha barabara ya Kilwa (Kamata hadi Mbagala), barabara ya Chang'ombe/Kawawa (Magomeni hadi Mgulani) na barabara ya Sokoine (Gerezani - City Hall).


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

CHUO KIKUU MZUMBE CHAPONGEZWA KWA UMAHIRI KATIKA UFUNDISHAJI MASOMO YA SHERIA

$
0
0

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi. Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Mkuu wa Kitivo cha Sheria Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. John Ubena mara baada ya kuwasili chuoni hapo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka akitoa taarifa kwa Waziri kuhusu maendeleo ya Chuo 
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Balozi.Dkt.Augustine Mahiga akizungumza na wanataaluma wa Kitivo cha Sheria wa Chuo Kikuu Mzumbe
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akitoa maelezo ya awali ya lengo la ziara 

Wataalamu wa kitivo cha Sheria wakimsikiliza Waziri
Waziri akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wahadhiri wa Sheria Chuo kikuu Mzumbe.

======  =======  =======  ==========
Chuo Kikuu Mzumbe kimepongezwa kwa umahiri wake katika ufundishaji masomo ya sheria, na kuwa Chuo bora chenye wahitimu mahiri na wajuzi kwenye fani ya Sheria nchini. 

Pongezi hizo zimetolewa leo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga alipotembelea Chuo hicho kwa mara ya kwanza, tangu ameteuliwa kushika nafasi hiyo; akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Prof. Sifuni Mchome, Naibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju na baadhi ya watendaji kutoka taasisi na Idara za Sheria zilizopo chini ya Wizara hiyo. 

Pamoja na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe, amewataka kuongeza ubunifu zaidi katika kutoa wanafunzi bora, kwa kuzingatia miiko ya kazi ili kuwaandaa vijana wenye nidhamu na weledi. 

Chuo Kikuu Mzumbe ni Chuo cha Umma kinachotoa kozi mbalimbali za Sheria kuanzia ngazi ya Astashahada (Certificate), Stashahada (Diploma), Shahada ya Awali (Degree) na Shahada za Umahiri (Masters) katika Sheria. 

Vyombo vitatu vya habari vyapigwa faini ya sh.milioni 11

$
0
0

*SAM misago tv yachapisha mwanamke kunyanyua kiuno


Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) kupitia Kamati ya

Maudhui mtandaoni, imevitoza faini ya sh.milioni 11 vyombo vya habari vitatu kwa kukiuka kanuni za mawasiliano ya kielektoniki na posta.

Vyombo hivyo ni Radio Classic FM, Luninga mtandaoni ya Sami Misago na Rock Media Group.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui, Joseph Mapunda amesema lengo la kamati kufanya hivyo ni kuimarisha tasnia ya habari nchini kwani inatakiwa kuwa na ubunifu usiovuka mipaka kutokana sheria za leseni walizopewa.

"Suala la utangazaji linahitaji watangazaji wabunifu na walio na elimu ili kutumia lugha zisizoleta athari kwa jamii, hivyo nashauri uongozi kuweka usimamizi mzuri kwa wafanyakazi wao ikiwa kuwaongezea kiwango cha elimu na kutambua miiko ya waandishi katika utoaji wa taarifa ,"amesema Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui

Mapunda amesema Redio Classic kupitia kipindi cha Pepeta waliwadhalilisha waislamu kwa kutumia lugha ya kiarabu na kukiuka kanuni za mawasiliano ya kielektoniki na posta kutokana na masuala ya imani yanatofautiana uvumilivu.

Amesema baada ya kutokea hivyo kamati iliwaita wahusika kwa ajili ya kuwahoji na wao kuweza kutoa utetezi kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria ambapo waliahidi kusimamia misingi ya utangazaji na kutaka kuomba radhi siku saba kuanzia Machi 18.

Makamu mwenyekiti huyo alisema tathmini ya kamati baada ya kuwahoji ilibaini redio hiyo imefanya kosa la kutokuwa waangalifu kwa kutangaza maneno yenye ukakasi kwa jamii.

Kamati hiyo iliamua kuwatoza faini ya sh. 1,000,000 na kuwapa onyo kali na haki ya kukata rufaa kwenye Baraza la Haki ya Kibiashara iko wazi ndani ya siku 21 kuanzia sasa.

Kwa upande mwingine TCRA imewatoza faini ya sh.milioni tano luninga mtandaoni ya Sami Sago kwa kuchapisha maudhui ya matusi.Sami Sago nao wamepewa onyo kali kwa kutakiwa kutorudia tena na kuwaomba radhi watazamaji wao kwa siku saba mfululizo na rufaa ipo wazi ndani ya siku 21 kutokana na kuchapisha picha ya mwanamke kunyanyua kiuno juu na kufanya kushabikia vitendo.

Kamati hiyo ya maudhui ya TCRA imetoza faini ya sh.milioni tano luninga mtandaoni ya Rock Media Group, kwa kutangaza taarifa bila ulinganifu na kuwadhalilisha wananchi wa Bagamoyo.

Hata hivyo wametakiwa kuomba radhi ndani ya siku saba mfululizo na kupewa onyo kali.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Joseph Mapunda akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maamuzi kamati kwa vyombo vya tatu vya habari vilivyokiuka maudhui ya utangazaji katika vyombo vyao jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi na wamiliki wakisikiliza maamuzi ya kamati ya maudhui jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Joseph Mapunda akitoa maamuzi ya kamati ya Maudhui.

BRELA YAPATIWA MAFUNZO YA KUJIKINGA NA VIRUSI VYA CORONA NA HOMA YA INI

$
0
0
Watumishi kutoka Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamepewa mafunzo ya kujikinga dhidi ya virusi vya Corona (COVID-19) pia namna ya kuepuka ugonjwa wa homa ya Ini. Mafunzo hayo yametolewa na Madaktari bingwa wa magonjwa ya mlipuko kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. John C. Rwegasha na Dkt. Lilian Tina Minja katika ukumbi wa mikutano wa BRELA leo tarehe 17/03/2020 jijini Dar es salaam.

Katika mafunzo hayo Dkt. Minja amesisitiza kunawa vizuri mikono kila wakati kwa kutumia sabuni na dawa ya kuua vijidudu kwa angalau sekunde sitini (60), kukaa umbali wa angalau hatua mbili (2) kutoka kwa mtu anaepiga chafya au kukohoa, kuepuka kushika macho, pua na mdomo kwa mikono isiyo safi kwa sababu mikono hushika sehemu nyingi na ni rahisi kubeba vimelea vya maradhi hayo, kuhakikisha kila mmoja na walio karibu yako wanazingatia ustaarabu wa kuzuia pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya, kubaki nyumbani ikiwa hujisikii vizuri pia kuwasiliana na wataalamu wa afya kupitia namba 0800110124, 0800110125 ili kuongea nao na kukupa maelekezo kwa msaada, vilevile kuepuka sehemu za misongamano  pamoja na kutumia Sanitazer ili kuuwa vijidudu kwenye mikono. 

Aidha Dkt. Rwegasha amewataka wafanyakazi wa BRELA kuwa na utaratibu wa kupima afya ikiwa ni pamoja na homa ya Ini ili kujua afya zao.
Aidha Mtendaji Mkuu wa BRELA amewashukuru Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Rwegasha na Dkt. Lilian kwa kufika na kutoa elimu ya kujikinga na virusi vya Corona pia kutoa elimu ya homa ya Ini kwa wafanyakazi wa BRELA. Virusi vya Corona (COVID-19) vimedhibishwa kuwepo nchini Tanzania mnamo tarehe 16/03/2020.
 Dr. John. C. Rwegasha akitoa elimu ya kujikinga na homa ya Ini.
 Wafanyakazi wa BRELA wakifatilia kwa umakini mafunzo ya kujikinga na virusi vya Corona COVID-19.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa akifuatilia mafunzo ya kujikinga na virusi vya Corona COVID-19 na homa ya Ini.
 Dkt. Lilian Minja akitoa mafunzo ya Kujikinga na Corona COVID-19  leo 17/03/2020 katika ukumbi wa mikutano BRELA .






MASAUNI-POLISI ZINGATIENI MISINGI YA SHERIA KUDHIBITI UHALIFU

$
0
0



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na wajumbe(hawapo pichani),  wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Kumi na Mbili cha Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi ambapo amelitaka jeshi hilo kuzingatia misingi ya sheria katika kudhibiti viashiria au matendo ya uhalifu katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.Ufunguzi wa kikao hicho umefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambae pia ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Kumi na Mbili cha Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi ambapo ameahidi kupanga bajeti itakayosaidia kupambana na changamoto mbalimbali kuelekea kipindi cha Uchaguzi Mkuu  unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.Ufunguzi wa kikao hicho umefanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es Salaam.Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni.
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambae pia ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro akitoa taarifa ya ulinzi na usalama kwa nchi nzima mbele ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kulia),muda mfupi kabla ya naibu waziri kufungua Kikao cha Kumi na Mbili cha Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi,kilichofanyika Ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi,Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akiweka saini katika daftari la wageni baada ya kuwasili Bwalo la Maafisa wa Polisi,Oysterbay kufungua Kikao cha Kumi na Mbili cha Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

………………………………………………………………..

Na Mwandishi Wetu

Serikali imelitaka Jeshi la Polisi kuzingatia misingi ya sheria katika kudhibiti viashiria au matendo ya uhalifu katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Hayo yamesemwa leo Machi 16,2020 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni wakati akifungua Kikao cha Kumi na Mbili cha Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi kilichofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

“Napenda kuwapongeza Jeshi la Polisi chini yako(IGP Sirro),kwa kufanikiwa kudhibiti matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo dawa za kulevya,ajali za barabarani na uhalifu mwingine ambao hapo nyuma wote tulishuhudia ukiwa umeoata mizizi ila napenda kutoa angalizo kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu mdhibiti viashiria vya uhalifu au matendo ya uhalifu kwa kufuata misingi ya sheria ili tuweze kupita kwa amani na salama katika kipindi hicho” alisema Masauni

Akizungumza katika kikao hicho cha baraza Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ambae pia ni Inspekta Jenerali wa Polisi,Simon Sirro alisema wao kama jeshi wanaishukuru serikali na wamejipanga kibajeti kuhakikisha wanakabiliana na changamoto zozote zitakazotokea katika kipindi cha uchaguzi

“Kwa kiasi tumefanikiwa kutengeneza bajeti itakayochochea usalama wa raia na mali zao,bajeti iliyoandaliwa itasaidia kutatua changamoto na kwa kuwa kila uchaguzi una changamoto zake sisi tumejipanga na tunazichukua chgangamoto kama fursa” alisema IGP Sirro

Watumishi hao wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara ya Jeshi la Polisi wanakutana katika kikao hicho lengo ni kujadili masuala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2019/2020 na Rasimu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2020/2021.

SIMIYU YAFUNGA KAMBI YA KITAALUMA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA

$
0
0

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mkoani humo, kabla ya kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao   ambayo ilikuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Sita wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(hayupo pichani) akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mkoani humo, kabla ya kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao  ambayo ilikuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
Afisa Afya wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Reuben Malimi akitoa elimu ya tahadhari dhidi ya Homa ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Korona kwa wanafunzi wa kidato cha Sita mkoani humo waliokuwa katika kambi ya Kitaaluma shule ya Sekondari ya Wasichana ya Maswa, kabla ya kambi hiyo kufungwa ili kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Sita wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(hayupo pichani) akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mkoani humo, kabla ya kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao ambayo ilikuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya hali ya kambi ya kitaaluma kwa waanfunzi wa kidato cha sita mkoani humo, kabla ya kumkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini kuzungumza na wanafunzi hao, kabla ya kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao ,  ambayo ilikuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
……………………………………………………………………………………….

Na Stella Kalinga, Simiyu RS

Uongozi wa Mkoa wa Simiyu umefunga kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha Sita mwaka 2020 iliyokuwa ikifanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa , ikiwa ni sehemu ya tahadhari dhidi ya Homa kali ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona.

Akifunga kambi hiyo, Machi 16, 2020  Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema uongozi wa mkoa umefikia hatua hiyo kuchukua tahadhari kama ilivyoelekezwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa juu ya kuzuia mikusanyiko ya watu wengi isiyo ya lazima katika kipindi hiki ambacho kumeripotiwa idadi ya watu kadhaa kubainika kuwa na virusi vya Corona katika nchi mbalimbali.

“Kutokana na Maelekezo ya Serikali Mkoa umeona kambi hii ifungwe kwa ajili ya tahadhari dhidi ya Corona,  Mhe. Rais amesitisha mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2020, Mhe. Waziri Jafo amesitisha UMISETA na UMITASHUMTA na tahadhari mbalimbali zimeendelea kutolewa na Serikali ikiwemo ya kuzuia mikusanyiko; sisi hapa tuna wanafunzi  takribani 1000 kutoka shule 10 hivyo tumekubaliana kwa pamoja tuifunge kambi hii,” alisema Sagini.

Aidha, Sagini amesema pamoja na kambi za kitaaluma kufungwa Mkoa utaendelea kusimamia utekelezaji wa mkakati wa taaluma wa mkoa ili walimu, wanafunzi na wadau wengine wa elimu waweze kutimiza wajibu wao kuhakikisha Mkoa unatimiza adhma yake ya kuwa miongoni mwa mikoa itakayofanya vizuri katika mitihani yote ya Kitaifa.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema wanafunzi hao walitakiwa kukaa kambini muda wa wiki sita kwa ajili ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa unaotarajiwa kufanyika mwezi Mei 2020, hivyo pamoja na kusitisha kambi hiyo walimu wamehimizwa kutimiza wajibu wao katika ufundishaji na wanafunzi wametakiwa kwenda kusoma kwa bidii ili kufikia lengo la Mkoa.

Awali akitoa elimu ya ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona kwa wanafunzi na walimu kabla ya kambi kufungwa, Afisa Afya wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Reuben Malimi amesema ugonjwa huo hauna tiba matibabu yanayofanyika yanazingatia dalili zinazoonekana kwa mgonjwa, hivyo ni vema kila mmoja  akachukua tahadhari kwa kuzingatia maelekezo na elimu inayotolewa na wataalamu wa afya katika maeneo mbalimbali.

Nao wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Mkoa wa Simiyu wameshukuru uongozi wa Mkoa kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona kwa kutoa elimu kuhusu Corona  kabla ya kufunga kambi, huku wakieleza namna ambavyo kufungwa kwa kambi kunaweza kuathiri malengo yao waliyojiwekea.

“Tunashukuru uongozi wa Mkoa kutoa elimu  na kuchukua tahadhari ya Corona kwa kufunga kambi ni hatua ya kutuhakikishia usalama, lakini kambi ilitusaidia kujua namna ya kujibu maswali ya mtihani wa Taifa na kujifunza mada ngumu tulizoshindwa shuleni kupitia kwa walimu mahiri, tutatumia muda huu kujisomea kwa bidii ili tufaulu vizuri mtihani wa Taifa,” alisema Isack Ndassa kutoka Shule ya Sekondari Kanadi Itilima.

Zoezi la Uhakiki Vyama vya Siasa Laanza kwa Mafanikio

$
0
0
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Bw. Sisty Nyahoza akifafanua jambo mbele ya viongozi wa Kitaifa wa Chama cha United Democratic Party (UDP) wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa walipotembela Makao Makuu ya chama hicho leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa UDP Taifa, John Momose Cheyo.
Mkuu wa Idara ya Gharama za Uchaguzi na Ruzuku toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Bi. Hollo Kazi akielezea jambo mbele ya viongozi wa Kitaifa waChama cha Wakulima Tanzania (AAFP) wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa walipotembela Makao Makuu ya chama hicho leo jijini Dar es Salaam. Kushotoni Afisa Mipango wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP), Bw. EmmanuelMsengi.
Afisa Mipango wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP), Bw. Emmanuel Msengi akifafanua jambo mbele ya viongozi wa Kitaifa wa Chama cha Wakulima Tanzania (AAFP) wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa walipotembela Makao Makuu ya chama hicho leo jijini Dar es Salaam. Zoezi la uhakiki limeanza leo ambapo jumla ya vyama sita vimehakikiwa ambavyo ni AAFP, ADC, UMD, UDP, NLD na NRA.
Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima (AAFP), Bw. Rashid Rai akijibu hoja wakati wa zoezi la uhakiki wa vyama vya siasa walipotembelewa na Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) leo jijini Dar es Salaam. Zoezi la uhakiki limeanza leo ambapo jumla ya vyama sita vimehakikiwa ambavyo ni AAFP, ADC, UMD, UDP, NLD na NRA. Viongozi wa chama cha AAFP wamevaa maski ikiwa ni tahadhari ya kuambukizwa ugonjwa wa Corona Virus.
Mhazini wa Chama cha Wakulima (AAFP), Bw. Ndonge Said Ndonge akitoa maelezo kuhusu namna wanavyo tunza taarifa zao za mapato namatumizi mbele ya Maafisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (ORPP) walipofika katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho kwa ajili ya zoezi la uhakiki lililoanza leo jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa nje wa Ofisi za Vyama vya siasa vya AAFP na UDP (Na: Mpiga picha wetu)

DAWASA WATEKELEZA AGIZO LA SERIKALI KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA COVID_19

$
0
0
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Sslaam na Pwani (DAWASA) imeendelea kutekeleza agizo la Serikali la kuhimiza unawaji mikono kwa sabuni. 

Ofisi zote za Mamlaka zimeandaa masinki katika milango mikuu ya kuingia katika Majengo yake ili kuwezesha Watumishi  na wageni wote kupata  huduma kunawa mikono kwa majisafi  na sabuni kabla ya kuingia.


TIMUZA DHARURA ZA KUKABILI MAGONJWA AMBUKIZI YA MLIPUKO ZATAKIWA KUTUMIA DHANA YAAFYA MOJA

$
0
0

Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akisisitiza umuhimu wa kutumia Dhana ya Afya moja ambayo hujikita katika kujumuisha sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu wakati wa mafunzo kwa timu za dharura za kukabili magonjwa ambukizi ya mlipuko leo, Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.
Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya kutoka kwa timu za dharura za kukabili magonjwa ya mlipuko kutoka ngazi ya mkoa na wilaya zilizo mipakani, wakifuatilia mafunzo ya kukabili magonjwa ya ambukizi ya mlipuko kwa kutumia Dhana ya Afya moja, wakati wa mafunzo hayo, leo Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.
Mratibu wa Mradi wa ECTAD Tanzania kutoka FAO, Fasina Folorunso akisisitiza umuhimu wa kuimarisha Afya ya Binadamu kwa sekta za Afya kutumia Dhana ya Afya Moja, wakati wa mafunzo kwa timu za dharura za kukabili magonjwa ya ambukizi ya mlipuko leo, Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.
Mkuu wa Ndaki ya Mifugo, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine-SUA, Profesa, Amandus Muhairwa akisisitiza sekta ya Afya ya mifungo na Afya ya Binadamu, kushirikiana katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu wakati wa mafunzo kwa timu za dharura za kukabili magonjwa ambukizi ya mlipuko kwa kutumia Dhana ya Afya moja  leo, Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.
Baadhi ya Wakufunzi na wataalamu wa sekta za Afya kutoka kwa timu za dharura za kukabili magonjwa ya mlipuko kutoka ngazi ya mkoa na wilaya zilizo mipakani, wakifuatilia mafunzo ya kukabili magonjwa ya ambukizi ya mlipuko kwa kutumia Dhana ya Afya moja, wakati wa mafunzo hayo, leo Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa sekta za Afya kutoka kwa timu za dharura za kukabili magonjwa ambukizi ya mlipuko kutoka ngazi ya mkoa na wilaya zilizo mipakani, kwa kutumia Dhana ya Afya moja, wakati wa mafunzo hayo, leo Jijini Dodoma, tarehe 17 Machi, 2020.
********************************
Dhana ya Afya moja ambayo hujikita katika kujumuisha sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu imeendelea kufundishwa kwa Wataalamu wa sekta hizo za Afya, ikiwa ni Sekta ya Afya  ya Binadamu, Wanyamapori, Mifugo, Kilimo na Mazingira, ili wataalamu hao watumie dhana hiyo kuimarisha udhibiti wa magonjwa ambukizi kati ya Binadamu na wanyama  ambayo hutokea mara kwa mara katika maeneo ya mipakani kutokana na kuwepo kwa  muingiliano mkubwa kati ya  watu na wanyama katika mazingira yao.
Katika kuimarisha Afya ya binadamu, Shirika la Chakula na Kilimo  la Umoja wa Mataifa (FAO), pamoja  na watalaamu kutoka Wizara ya Mifugo na  Uvuvi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine wamewapa mafunzo wataalamu wa sekta za Afya wanao toka katika Halmashauri za Mkoa wa Kagera, Rukwa, Katavi,  Rukwa na Songwe zilizo mipakani juu ya namna ya kujiandaa na kukabili magonjwa ambukizi ya mlipuko kama  vile Ugonjwa wa Corona na Ebola kwa kutumia Dhana ya Afya  moja.
Akiongea wakati wa kufungua mafunzo hayo leo tarehe 17 Februari, 2020, Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa  Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, amebainisha kuwa ushirikiano wa wataalam na sekta za Afya  kwa kutumia dhana ya Afya Moja hivi sasa ni agenda ya dunia nzima. Aidha, ameeleza kuwa Dhana hiyo imekusudiwa kutumika maeneo ya mipakani   ambapo mwingiliano huo huchochewa na wasafiri kutoka eneo moja kwenda jingine, ongezeko la watu duniani, mabadiliko ya tabia nchi, utandawazi, ongezeko la mahitaji ya maji na chakula.
“Mafunzo haya  ni  muhimu sana nchini kwa kujenga uwezo wa nchi katika utayari wa kukabiliana na magonjwa yanayosambazwa na wanyama na kuathiri wanyama na binadamu.Tanzania tumeabiwa yupo mgonjwa wa Corona19, ambapo Tumeambiwa mgonjwa anaendelea vizuri na matibabu, na serikali inaendelea kuchukua hatua za madhubuti za kuhakikisha ugonjwa huu unadhibitiwa ili usisambae nchini”.
Awali akiongea katika mafunzo hayo, Mkuu wa Ndaki ya Mifugo, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine-SUA, Profesa, Amandus Muhairwa amebainisha kuwa  sekta za Afya zikishirikiana katika Kudhibiti magojwa zitasaidia kuimarisha Afya ya Binadamu kwa kuwa kila sekta itakuwa inachukuwa tahadhari kwa wakati.
Aidha, Mratibu kutoka FAO wa Mradi wa  ECTAD Tanzania, Fasina Folorunso amabainisha kuwa FAO inaendelea kushirikiana na serikali mya Tanzania kupitia Dawati la  Afya moja katika kujenga uwezo wa kukabiliana na magonjwa ambukizi ya mlipuko kwenye ngazi ya mkoa na wilaya hususani maeneo ya mipakani.

Katika kuhakikisha watalaam hao kutoka sekta za Afya wanaweza kutumia Dhana  hiyo katika kudhibiti magonjwa katika maeneo ya mipakani wameweza kujengewa uwezo wa namna ya kutoa taarifa za milipuko ya magonjwa ambukizi kama vile ugonjwa wa Corona 19 na Ebola  yanapotokea maeneo ya mipakani, namna ya kuunda vikosi vya kufuatilia na kukabili Ugonjwa, Mawasiliano wakati wa kufuatilia na kukabili magonjwa hayo kwa kutumia Dhana ya Afya moja,  pamoja na masuala ya kutumia vifaa Kinga Binafsi vya Kitaalamu.
Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za Afya moja nchini. Kwa kutambua umuhimu huo Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja  kwa kushirikiana Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) wakishirikiana na USAID, OIE, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine – SUA wakishirikiana na Chuo Kikuu cha Kansas cha nchini Marekani waliandaa na kuratibu mafuzo hayo.

MATUKIO KATIKA PICHA KAMATI YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA

$
0
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni George Mkuchika akiwasilisha mbele ya Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa Taarifa ya Mapato na Matumizi ya Mafungu ya ofisi yake kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021, kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dkt. Mary Mwanjelwa. Kikao hicho cha Kamati kimefanyika katika Ofisi za Bunge, Jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakiwa katika kikao cha Kamati ambapo wamepokea na kujadili Taarifa ya Mapato na Matumizi ya Mafungu ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021. Kikao hicho cha Kamati kimefanyika katika Ofisi za Bunge, Jijini Dodoma.
Katibu wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Ndugu Chacha Nyakega akitoa ufafanuzi wa jambo katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge, Jijini Dodoma, kulia ni Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Jason Rweikiza.

Bluefins yatwaa ubingwa kuogelea ya Mwanza

$
0
0









Waogeleaji wa klabu ya Bluefins wakishangilia baada ya kushinda mashindano ya kuogelea ya Mwanza yaliyofanyika kwenye bwawa la kuogelea la Isamilo.

**************************

Dar es Salaam. Klabu ya Bluefins ya Dar es Salaam imefanikiwa kunyakua ubingwa wa mashindano ya kuogelea ya mkoa wa Mwanza yajulikanayo kwa jina la Isamilo swimming championships.
Kwa ushindi huo, Bluefins inakuwa klabu pekee Tanzania kufanikiwa kutwaa ubingwa mara mbili katika mashindano matatu yaliyokwisha fanyika mpaka sasa kwa mujibu wa kalenda ya mashindano ya mwaka huu iliyotolewa na Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA). 

Bluefins awali ili nyakua ubingwa wa mashindano ya Morogoro (Mis Piranhas) na baadaye kumaliza katika nafasi ya pili katika mashindano ya Taliss-IST yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha zaidi ya waogeleaji 200 kutoka klabu 10, Bluefins ilikusanya jumla ya pointi 3,031.5 na kufuatiwa na wenyeji, Mwanza waliojikusanyia pointi 2,932.5.

Kwa upande wa wavulana, Bluefins ilinyakua nafasi ya kwanza kwa kupata pointi 1,500 na kufuatiwa na Mwanza iliyopata pointi 1,209. Mwanza ilishika nafasi ya kwanza kwa upande wa wanawake baada kwa kupata pointi 1,493.5 na kufuatiwa na Bluefins kwa kukusanya pointi 1,341.5.

Klabu ya Bluefins ilifanikiwa kushinda jumla ya medali 93 ambapo kati ya hizo, 28 ni dhahabu, 31 za fedha na 34 za shaba. Kocha Mkuu na Muasisi wa klabu hiyo, Rahim Alidina aliwapongeza wachezaji wake kwa bidii waliyoifanya na kufanikiwa kutwaa ubingwa huo.

“Tumefarijika sana na matokeo ya Mwanza ambayo yameendelea kuipa sifa klabu katika mchezo wa kuogelea. Mara ya kwanza tulitwaa ubingwa mwaka 2016 na kufanikiwa kurejesha ubingwa wetu,” alisema Alidina. Alisema kuwa bado tunaendelea kuwanoa waogeleaji wetu ili kuendelea kufanya vyema katika mashindano ya ndani nan je ya nchi.

Mbali ya Bluefins na Mwanza, klabu nyingine zilizoshiriki katika mashindano hayo ni Braeburn, Dar Swim Club, FK Blue Marlins, Geita Gold Mine International, Lake, Taliss-IST, Tanzania Latham Swim Club na UWCEA ya Moshi.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA (NUU) YAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MRADI WA UJENZI WA KIWANDA CHA USEREMALA GEREZA MSALATO

$
0
0


Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi ndugu Christopher D. Kadio (wa nne toka kushoto ) akimkaribisha Mkuu wa Msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,ambaye ni Mbunge wa Zanzibar Jimbo la Uzini ndugu Salum Rehani(wa nne toka kulia) walipowasili eneo la Mradi, Msalato. Wa tatu toka kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza Selemani Mzee.
Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi ndugu Christopher D. Kadio akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Msafara kuzungumza na viongozi wa Jeshi la Magereza pamoja na wajenzi wa mradi
Mkadiriaji Mkuu wa Ujenzi Makao Makuu ya Magereza Kamishna Msaidizi Aaron Lunyungu akitoa maelezo ya ramani ya mradi kwa Mkuu wa Msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,ambaye ni Mbunge wa Zanzibar Jimbo la Uzini ndugu Salum Rehani.
4.Msimamizi Mkuu wa Mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Useremala Gereza Msalato Mrakibu Bonanza Malata akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.Picha zote na Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Dodoma

CCM Z’BAR YATOA TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA

$
0
0
NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewataka wananchi visiwani hapa kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga dhidi ya ugonjwa hatari wa virusi vya Corona ambao ulianzia nchi za nje na hivi sasa tayari umeripotiwa kuingia Tanzania.

Mbali na hilo, CCM imezitaka Ofisi zote za chama,Jumuiya,matawi na maskani za chama kutoa elimu na ufafanuzi wa kina kwa wanachama wao juu ya maelekezo yaliyotolewa na chama ngazi ya taifa dhidi ya kujikinga na ugonjwa huo.

Kauli hiyo ameitoa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla “Mabodi”, Ofisini kwake Kisiwandui mjini Unguja ambapo alisema ugonjwa huo ni janga la kiafya dunia nzima.

Alisema kuwa Zanzibar ni miongoni mwa nchi zinazopokea raia wengi wa kigeni kupitia sekta ya utalii, hivyo ni lazima mamlaka husika kufanya kazi ya ziada ya kuhakikisha maeneo yote yanayotumika kama njia za kuingia visiwani humu wanakuwepo wataalamu wa afya kwa ajili ya kufanya vipimo vya ugonjwa huo.

Alisema ni wajibu wa kila mwananchi bila kujali tofauti za kisiasa, kidini, kikabila na rangi kuanza kuchukua hatua stahiki za kujikinga dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona.

Dk.Mabodi, alisema kuwa maamuzi yote yaliyofikiwa na Chama kwa ngazi ya Taifa ya kusitisha shughuli mbalimbali za kichama zinazotengeneza mkusanyiko wa watu unaoweza kusababisha maambukizi ya ugonjwa huo.

Pia, Dk. Mabodi alisema kuwa anazipongeza hatua zilizochukuliwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ), chini ya Rais Dk.John Pombe Magufuli na Rais Dk.Ali Mohamed Shein kwa kusitisha baadhi ya shughuli za kitaifa kwa lengo la kudhibiti ugonjwa huo.

Katika maelezo yake,Naibu Katibu Mkuu huyo aliitaka Serikali kuendelea na juhudi za kuchukua hatua mbalimbali za kujikinga na ugonjwa huo, ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi na kuandaa vifaa tiba vya dharura vitakavyosaidia kuwa kinga wananchi dhidi ya Corona.

Naibu Katibu Mkuu huyo aliwataka wananchi kutoa taarifa pindi watakapobaini uwepo wa watu wenye dalili za ugonjwa huo ili mamlaka husika ziweze kuchukua hatua za haraka kwa mujibu wa taratibu za kiafya.

Pamoja na hayo Naibu Katibu Mkuu huyo aliwasihi wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla, kuepuka mikusanyiko mbalimbali kutokana na kuwa ugonjwa huo unasamba kwa njia ya hewa na hata kugusana baina ya mtu na mtu.

Alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kudhibiti bandari bubu na njia mbalimbali zisizo rasmi za kuingia katika visiwa vya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ili kuzuia baadhi wa watu wanaotumia njia hizo kuingia nchini wasilete ugonjwa huo.

Naibu Katibu Mkuu huyo Dk.Mabodi, aliongeza kwa kutoa wito kwa waumini wa dini mbalimbali nchini, kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya pindi wanapokusanyika kwa ajili ya ibada ikiwemo Makanisani na Miskitini.

Pamoja na hayo alivitaka vyombo vya habari nchini kutoa taarifa na elimu sahihi kwa umma, huku serikali ikiendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na janga hilo.

Alisema elimu ya Afya ya jamii juu ya kinga ya Corona itolewe kwa kasi kubwa hasa Vijijini kwa njia ya vipeperushi, upatu, Matangazo ya mabomba na Maskulini.

“Maradhi haya ni hatari sana kila Mwananchi achukue tahadhari, na Mihadhara yote ya kidini na kijamii ihusishe taaluma ya Elimu ya kinga ya Maradhi ya Corona”, alisema Dk.Mabodi.

Dk.Mabodi, alishauri wataalamu wote wa tasnia ya Afya waliostaafu na walio makazini pamoja na sekta nyingine waungane na kutengeneza timu moja, itakayosaidia katika mapambano dhidi ya maradhi haya ya Corona.

Aidha, amewataka viongozi,wanachama na makada wa ngazi mbalimbali wa CCM kuendelea kuiamini Serikali yao kuwa itachukua hatua madhubuti za kuhakikisha wananchi wote wanabaki salama dhidi ya ugonjwa huo.
Viewing all 119398 articles
Browse latest View live