Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 990 | 991 | (Page 992) | 993 | 994 | .... | 3285 | newer

  0 0


  Wafanyakazi wa Kissa Pharmacy Ltd  Pharmaceuticals Whole Sale And Retali Mbeya Tz wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika eneo la mapango ya Amboni (AMBANI CAVES ) kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ya kihistoria ndani ya Mapango hayo sanjali na kuhamasisha utalii wa ndani.Picha na Emanuel Madafa Baba JJ

  Wafanyakazi Kissa Pharmacy wakisikiliza kwa makini maelezo ya mmoja wa watoa huduma katika mapango hayo Ndugu Allan Yohana kabla ya kuanza rasmi shughuli ya kutembelea mapango hayo.(JAMIIMOJABLOG)

  The Amboni Caves are the most extensive limestone caves in East Africa. They are located 8 km north of Tanga City in Tanzania off the Tanga-Mombasa road. The caves were formed about 150 million years ago during the Jurassic age. It covers an area of 234 km². According to researchers the area was under water some 20 million years ago. There are altogether ten caves but only one is used for guided tours.

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Devotha Mdachi (kulia) akizungumza jana Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya onesho la Swahili International Expo linalotarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba Mosi hadi 3, mwaka huu katika ukumbi wa mlimani City Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa kampuni ya fastjet Jimmy Kibati kama mmoja wa wadhamini.
  Mratibu wa onesho la Swahili International Expo Philip Chitaunga (kulia) akizungumza Dar es Salaam jana kuhusu onesho hilo linalotarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba Mosi hadi 3, mwaka huu katika ukumbi wa mlimani City Dar es Salaam.Wenginekutoka kushoto ni Meneja wa kampuni ya fastjet kama mmoja wa wadhamini, Kaimu Mkurugenzi TTB Devotha Mdachi na Milat Mekennon kutoka shirika la ndege la Ethiopia.
   

  ONESHO la Swahili International Expo linatarajiwa kufanyika wiki hii, kuanzia tarehe 1-3 Oktoba,2015 katika ukumbi wa Mlimani City ambapo Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
  Hii ni mara ya pili kwa Onesho hili kufanyika,Mwaka jana ilikuwa mara ya kwanza October 1- -4,2014

  Onesho la mwaka jana liliweza kuwavutia Waoneshaji 40,Mawakala wa Utalii walioalikwa kutoka nje ya nchi 19 (hosted Buyers),Waaandishi wa Habari kutoka nje ya nchi 4 (media),Wageni waliotembelea onesho hilo 1,200,Wadhamini  40 na Mdhamini mkuu alikuwa Ethiopian Airlines
  Mwaka huu Waoneshaji ni 100,Mawakala wa utalii na waandishi wa habari walioalikwa 43, Wageni wanaotegemewa kutembelea onesho 2,000,Wadhamini 41 na Wadhamini wakuu wamegawanyika katika makundi.

  Kuna Platinum Category ambao ni Ethiopian Airlines – Mdhamini Mkuu (usafiri kwa ajili ya mawakala wa nje walioalikwa)
  Pia kuna Gold Categoryambao ni Fast Jet Airline Limited, An’gata camps Ltd, FB cars Ltd, Gibbs Farm,Ramada Resort Dar es ssalaam, SAA North America, Seacliff Hotel, Sopa Lodges and Spicenet Tanzania .

  Kwa upande mwingine kuna Silver category ambao ni Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Antelope Tours and Safaris, Azam Marine, Congema Tours and safaris Ltd, Fernandes Tours & safaris, Melau Tours & Safaris Ltd, Precision Air Services, Shirika la ndege la Qatar, Rwandair, Shirika la ndege la Afrika Kusini , Shidolya Tours & Safaris Ltd, Sun Tours &travel Lts and Shirika la ndege la Uturuki.

  Wengine ni BougainvillaSafari Lodge, Ledgar Plaza Hotel, Cenizaro Hotels & Resorts, Emerald Collection Zanzibar, Essque zalu Zanzibar, Holiday Inn Dar es salaam, Kudu Lodge, Kunduchi bBeach Hotel, Manyara Wildlife safari Camp, Maru Maru Hotel, Mberesero Lodges & Tented Camps, Melia Zanzibar, Neptunes Hotels, New Africa Hotel, Ocean Paradise Resort & Spa, PlanHotel Hospitality Group, Protea Hotel Courtyard, Seacliff Court Hotel & Luxury Apartments, Seacliff Resort & Spa Zanzibar, Serena Hotel, Southern Sun Dar es salaam,  White Sands Hotel.

  Black tomato, Boogle Woogle, Cultural Art Center,Chuo Kikuu cha Tumaini  Makumira.
  Kwa upande mwingine kutakuwa na kitengo cha Hosted Buyers Programme ambapo Programme Maalum ya kuwatembeza mawakala wa Utalii katika maeneo Wageni hao watatembelea Zanzibar , Lake Manyara na Ngorogoro.Lengo ni kuona, kujifunza kuhusu utalii wa Tanzania, na kuonja (kuexperience ) ukarimu wetu.
   
  Pia kutakuwa na kitengo cha Cultural Village ambalo ni Eneo lililotengwa kwa ajili ya maonesho ambapo wajasirimali wadogo wataweza kuonesha bidhaa na huduma zao.

  Baadhi ya bidhaa hizo ni kama Tinga Tinga, Wachongaji vinyago, watengenezaji wa Sanaa mbalimbali, wanamitindo, vikundi vya burudani  muziki wa bendi na burudani (Utalii Band) na Kikundi cha utamaduni kutoka Chuo cha Tumaini , Arusha .Pia kutakuwa na Nyama Choma (wageni wataweza kupata vyakula vya kitanzania )
   
  Kwa ujumla TTB inawataka watanzania watembelee onesho hilo kutokana na ukweli kwamba onesho la S!TE ni fursa ya kuhamasisha utalii wa ndani,Watoa huduma mbalimbali za kitalii watakuwepo, wataweza kutumia fursa hiyo kutoa maelezo kuhusu huduma zao na kuwahamasisha watanzania kutembelea maeneo ya kitalii (vikundi mbalimbali vitawea kuhamasika –wanafunzi, wafanyakazi nk)

  0 0

  Dk. Magufuli asema iwapo atapata ridhaa yakuiongoza nchi atahakikisha anatoa mikopo kwa wasomi wanao maliza elimu ya juu nchini. https://youtu.be/bjV9jNZsh9Q

  Tanzania yapata mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 240 kutoka serikali ya Poland kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha matrekta. https://youtu.be/W70x_FxENZo

  Kampuni ya bima ya insuarance TANRI yasema huduma za bima ni muhimu kwa mtanzania sababu zinatoa kinga dhidi ya majanga mbalimbali. https://youtu.be/NAm0yAbsdJE

  Timu ya Azam Fc yasema swala la kuzalilishwa kwa mshambuliaji wa John Bocco na mlinzi wa Mbeya city Juma Nyoso wanaliacha mikononi mwa TFF. https://youtu.be/JsHwxJOMS3M

  Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu yatoa tahadhari kuhusu uwezekano mkubwa wa kutokea mlipuko wa homa ya bonde la ufa. https://youtu.be/3JxqAVSOb5o

  Mwili wa marehemu mama Celine Kombani waagwa leo huku makamu wa rais akiongoza maombolezo hayo katika viwanja vya karimjee. https://youtu.be/zHGeLbZA6Jo

  Mkutano wa mgombea urais Edward Lowassa wavunjika mkoani Tanga baada ya umati mkubwa wa watu kujitokeza na kuzimia kwa wingi. https://youtu.be/7tdAhq_BxY0

  Dk John Pombe Magufuli ahaidi mfumo wa utoaji huduma za afya kwa watanzania ikiwemo kuboresha upatikanaji wa dawa. https://youtu.be/IhsjD9GeFHE

  Bodi ya utalii Tanzania yatangaza kua maonesho ya kimataifa ya sekta ya utalii yatafanyika kuanzia oktoba 1-3 mlimani city. https://youtu.be/r0i-XZgYY5w

  Jumla ya wachezaji 24 wanaounda kikosi cha timu ya taifa stars kitakachocheza dhidi ya Malawi chatangazwa rasmi.https://youtu.be/ryM00jNJhZA

  Kundi la mashabiki wanaosadikiwa kua klabu ya Nice ya ligi kuu Ufaransa walishambulia gari la rais wa PSG kwa mawe.https://youtu.be/D3I_lBsseaA

  Mgombea uraisi wa CCM Dr.Magufuli amtaka mwekezaji wa mashine za kusagia mahindi Iringa kuhakikisha zinafanya kazi la sivyo atazirudisha. https://youtu.be/33w2SRw5_NA

  Ugonjwa wa Kipindu pindu waendelea kutishia maisha katika maeneo mbali mbali hapa nchini baada wakazi 11 kulazwa mkoani Singida. https://youtu.be/EEla58ZIofQ

  Uhalifu dhidi ya makanisa mkoani Kagera waendelea kushika kasi baada ya makanisa matatu kuvunjwa na thamani zake kuchomwa moto. https://youtu.be/9sKnCWfDYJs

  Umoja wa katiba ya wananchi mkoani Tabora walitaka jeshi la polisi nchini kutofungamana na chama chochote ili kutunza amani kuelekea uchaguzi mkuu. https://youtu.be/i2MyvoicC_w

  Mlipuko wa Kipindu pindu wazua tharuki na kutishia maisha ya wakazi wa musoma baada ya mtu mmoja kufariki huku wengine 60 wakilazwa. https://youtu.be/wktGWSoJ1Tk

  0 0


  0 0

  President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete meets the United Nations Secretary General’s Special Advocate for Inclusive Finance for Development (or as it's more simply known, UNSGSA) Netherlands Queen Maxima at the UN Headquarters in New York this afternoon  (photo by Freddy Maro)

  0 0

  Mwigulu Nchemba mmoja ya wajumbe 32 wa timu ya Ushindi ya Chama cha Mapinduzi akisalimiana na Wananchi wa Karatu Mjini jioni ya leo alipofika kwaajili ya Kuomba kura kwaajili ya Rais,Mbunge na Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi.
  Sehemu ya Wananchi wa Karatu Mjini waliofika Uwanjawa Mazingira Bora kusikiliza Mkutano wa hadhara wa Mwigulu Nchemba.Mwigulu Nchemba akitoa darasa kwa Wananchi wa karatu kuhusu biashara ya Kumuacha Dr.slaa na kumpatia Edward Lowassa aliyehamia kutoka CCM.Dr.slaa aliyetumia Jasho na Damu kuuimarisha Upinzani wenye meno,Hii leo ameondolewa kwakuwa DILI imewekwa mezani ili Mtu mwenye kashafa mbalimbali chafu aweze kuwania Urais.Kwaaina ya Mgombea waliosimamisha UKAWA,Mwigulu amesema itakuwa rahisi sana kwa Magufuli kushinda kwa asilimia kubwa sana ya Kura.Wananchi wa Mbulu Vijijini wakisikiliza Mkutano wa Mwigulu Nchemba wakati akinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


  Telephone: 255-22-2114512, 2116898

  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,

        STATE HOUSE,

                1 BARACK OBAMA ROAD,  

  11400 DAR ES SALAAM.

  Tanzania.

   
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Tanzania yatangaza hatua tano za kuendeleza haki za wanawake na usawa wa kijinsia

  ·        Yaahidi kufanya mabadiliko makubwa ya kisera na kisheria

  ·        Miongoni mwa Sheria zitakazohusika ni Sheria ya Ndoa na Sheria ya Urithi

  ·        Ni katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu  - SDG’s

  Tanzania imeahidi kuchukua hatua tano muhimu za kutetetea na kuendelea haki za wanawake kati ya sasa na mwaka 2030, ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko makubwa ya kufuta sheria zinazokandamiza wanawake na kutunga sheria za kuleta usawa wa kijinsia, yote katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG) mapya kwa manufaa ya wanawake wa Tanzania.


  Miongoni mwa hatua hizo itakuwa ni pamoja na kufuta ama kufanya mabadiliko ambayo yanaendeleza vitendo vya kiutamaduni ambavyo kwavyo vinaendeleza ubaguzi wa wanawake kama vile Sheria ya Ndoa, Sheria ya Urithi na kutunga Sheria ya Kukomesha Ukatili dhidi ya wanawake.


  Msimamo huo wa Tanzania umeelezwa Jumapili, Septemba 27, 2015 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipozungumza katika Mkutano wa Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Akinamama: Dhamira ya Kuchukua Hatua uliohudhuriwa na wakuu wa nchi mbali mbali duniani kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York, Marekani.


  Rais Kikwete ameuambia mkutano huo ulioitishwa  kwa pamoja na Jamhuri ya Watu wa China, Denmark, Mexico na Kenya kuwa hatua ya pili ambayo Tanzania inakusudia kuchukua ni kuridhia makubaliano yote ya kimataifa kuhusu haki za akinamama hasa Makubaliano ya Kimataifa Juu ya Kukomesha Aina Zote za Ubaguzi Dhidi ya Wanawake – Convention on the Elimination of All Forms of Discrimination Against Women (CEDAW).

  Hatua nyingine ambazo Rais Kikwete amesema kuwa Tanzania itachukua katika miaka 15 ijayo ili kuhakikisha usawa wa kijinsia nchini ni zifuatazo:

  ·        Kuendeleza na kuunga mkono upatikanaji wa raslimali fedha zinazolenga kuongeza usawa wa kijinsia kwa mujibu wa Ajenda ya Kugharimia Maendeleo ya Addis Ababa, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha zinatolewa pesa za kutekeleza mipango ya kitaifa na ya Serikali za mitaa za kukomesha ukatili dhidi ya wanawake.


  ·        Kuhakikisha utekelezaji wa uwakilishi wa uongozi wa asilimia 50-50 kati ya wanawake na wanaume katika nafasi zote za maamuzi kwenye ngazi zote.

  ·        Kupatikana na kutumiwa kwa data na habari za ukweli katika utunzi wa sera na utoaji maamuzi ya kukomesha ubaguzi wa kijinsia.

  ·        Kutunga na utekelezaji mfumo wa uwajibikaji na ufuatiliaji wa haki za kijinsia na haki za akinamama zilizokubaliwa kitaifa na kwenye ngazi ya Serikali za mitaa.


  Rais Kikwete pia amewaambia wajumbe wa mkutano huo kuhusu hatua za kisera na kisheria ambazo zimechukuliwa na Tanzania katika miaka ya karibuni kujenga usawa wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999 na marekebisho yake ya mwaka 2004 ambayo yanawapa akinamama nafasi na haki ya kupata, kushikilia, kutumia na kumiliki ardhi.


  Hatua nyingine ni kuwapa wanawake nafasi za maamuzi na uongozi katika nyanja za kisiasa na maisha ya umma. Katika kutekeleza hilo, idadi ya wabunge wanawake imeongezeka kutoka asilimia 21.5 ya wabunge wote mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 34.5 mwaka huu, mawaziri wanawake wameongezeka kutoka sita mwaka 2005 hadi kufikia 26 mwaka huu na idadi ya majaji wanawake imeongezeka kutoka wanane mwaka 2005 hadi kufikia 41 mwaka huu.


  Rais Kikwete amesema kuwa hatua nyingine zilizochukuliwa na Serikali ni kupunguza vifo vya wanawake wakati uzazi, kutunga Sheria dhidi ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya wanawake na watoto; kuanzishwa kwa uandaaji wa Bajeti inayotilia maanani mahitaji ya wanawake na kuongeza uwezekaji wa kiuchumi wa akinamama kupitia kuanzishwa kwa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) yenye kulenga kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa akinamama wafanyao biashara ndogo ndogo na za kati.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.

  28 Septemba, 2015
  0 0

  Na: Hassan Hamad, OMKR
  Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ametembelea kisima kinachosadikiwa kuwa na mafuta katika eneo la Tundauwa, na kusema kuwa mafuta ya Zanzibar yatachimbwa  katika kipindi kifupi kijacho.

  Amesema  kwa miaka mingi Zanzibar imeshindwa kuchimba mafuta yake kutokana na kutokuwepo mikakati imara, na kuahidi kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar atahakikisha kuwa suala hilo linawekewa mikakati imara ya uchimbaji, ili wananchi waweze kunufaika na rasilimali hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.

  Kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopatikana katika eneo hilo, kisima hicho chenye urefu wa zaidi ya futi 12 elfu na mia saba, kilijengwa miaka 53 iliyopita na kuonesha dalili za kuwepo mafuta.

  Wakati huo huo Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ametembelea Jumuiya ya maendeleo ya wanawake Tundauwa, na kutoa wito kwa wananchi wa kijiji hicho kujiunga na jumuiya hiyo ili kupata mafanikio zaidi.

  Amesema jumuiya hiyo inayojihusisha na masuala mbali mbali yakiwemo uhifadhi wa mazingira na kilimo, imekuwa mfano mzuri wa kuigwa kutokana na mafanikio inayoyapata tokea kuanzishwa kwake.

  “Jumuiya hii inafanya kazi nzuri ya kupigiwa mfano, hivyo natoa wito kwa wananchi wa vijiji hivi kujiunga kwa wingi ili kuleta mafanikio zaidi” amesema Maalim Seif.

  Mapema akisoma risala ya Jumuiya hiyo, bibi Raya Abdallah Rashid amesema lengo la kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ni kupambana na umaskini, maradhi pamoja na uhifadhi wa mazingira.

  Amesema Jumuiya hiyo pia imekuwa ikiielimisha jamii juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi na dawa za kulevya.

  Amesema Jumuiya hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 imepata mafanikio makubwa yakiwemo kutambuliwa kama jumuiya rasmi, kupanda mikoko ekari mbili kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira, ufugaji wa nyuki na kilimo cha mboga mboga.

  Hata hivyo bi Raya amesema bado wanakabiliwa na changamoto ikiwa ni pamoja na ukosefu wa jengo la ofisi, na kulazimika kuanzisha ujenzi ambapo zaidi ya shilingi milioni saba na nusu tayari zimetumika kwa ajili ya ujenzi huo, na kuomba kupatiwa misaada zaidi ili wamewe ukamilisha ujenzi wao.

  Katika hatua nyengine Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF, amefungua tawi jipya la CUF Tandani shehiya ya Kilindi lililokuwa chini ya Chama cha ADC.

  Amesema Tawi hilo limebadilishwa kutoka ADC na kuwa tawi la CUF baada ya wanachama  25 wa ADC kuamua kujiunga na CUF na kuongeza idadi ya wanachama wa tawi hilo kufikia 103.

  Tawi jengine la ADC la eneo la meli tisa Wingwi, pia lilibadilishwa kuwa tawi la CUF baada ya wanachama wake kukihama chama hicho.

   Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwasalimia watoto Othman na Zainab waliokaa kwenye kisiwa kinachosadikiwa kuwa na mafuta katika eneo la Tundauwa.
   Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipandisha bendera katika tawi la CUF Tandani shehiya ya Kilindi lililokuwa chini ya Chama cha ADC, kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi hilo.
  Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na wanachama wa wanachama wa Jumuiya ya maendeleo ya wanawake Tundauwa. (Hawapo pichani). 
  Picha na Salmin Said, OMKR

  0 0

  Baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakiwa wamenyanyua juu mikono yao kwa pamoja ni Ushindi sambamba na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto),kuonesha kuwa wasanii hao wanamuunga mkono Dkt Magufuli katika mbio zake za kuusaka Urais kwa kutembea nchi nzima kutumia Bajaji zao tano,ambapo Bajaj mojawapo itakuwa na kazi ya kukusanya kadi za wale wanaomua kurudi/kujiunga na chama cha CCM.


   Magufulika staili kama kawa,hata baadhi ya wasanii nyota wa Bongo Movie hapa nchini wakiongozwa na Nnape Nnauye (pili shoto) walikumbwa na zoezi hilo jioni ya leo mbele ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake waliokuwa wamefurika kwenye mkutano wa kampeni ndani ya uwanja wa Samora,zoezi hilo kwa sasa limeanza kujizolea umaarufu mkubwa hapa nchini,la kupiga push up kama ionekanavyo pichani.


   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wananchi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo septemba 28 ndani ya uwanja wa Samora mkoani Iringa.


    Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwaeleza wananchi sababu zilizosababisha CCM kutomteua Lowasa kuwa mgombea urais kupitia CCM hasa kutokana na hasa kile kilichoelezwa kuwa na kadhia ya ufisadi ya rushwa,mbapo pia Nape amewaomba Wananchi kumuombea afya Mgombea huyo wa Urais kupitia Chadema, ili aje ashuhudie CCM ikishinda  nafasi ya Urais.
    Wananchi wa Iringa na vitongoji vyake wakishangilia wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba wampigie kura ya ndio itakapofika Oktoba 25,mwaka huu (ambapo uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika )ili aweze kuibuka mshindi na kuchaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano
   Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mgombea ubunge Jimbo la Iringa mjini, Ndugu Frederick Mwakalebela wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja samora mjini Iringa.


   Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kilolo Ndugu Venance Mwamoto,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Ilula,mkoani Iringa.
   Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini kwenye mkutano wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,jioni ya leo kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.

  PICHA NA MICHUZI JR-IRINGA

  PICHA ZAIDI INGIA HAPA

  0 0

    
  1.         Mwezi Machi, 2015, Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

  Lilipitisha  Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni Nchini Na.1 ya Mwaka 2015 (The Non - Citizens (Employment Regulation) Act). Sheria hii ilisainiwa na Mheshimiwa Rais mwezi Mei, 2015 na imetangazwa kuanza kutumika rasmi tangu tarehe 15/09/2015 kupitia Gazeti la Serikali Na. 406 la mwaka 2015.


  2.          Sheria hii inaanzisha Mamlaka moja ya utoaji wa vibali vya ajira kwa wageni

   na Mamlaka hiyo ni Kamishna wa Kazi. 
  3.            Kwa kuzingatia matakwa ya Sheria hii, Wawekezaji au Waajiri wanaokusudia kuajiri wageni nchini wanapaswa kuwasilisha maombi kwa Kamishna wa Kazi  na  hati maalum ya kibali  cha Ajira itatolewa kwa mgeni husika.

  4.            Mgeni atakayepatiwa kibali cha ajira atatakiwa kuwa na kibali  cha Ukaazi ambacho kinatolewa na Idara ya Uhamiaji.
  5.                      Ada ya Vibali vya Ajira italipwa kwa kuzingati aina ya daraja la kibali husika kama ifuatavyo;

                                                       i.        Daraja  A kwa Wawekezaji na waliojiajiri wenyewe-USD 1,000

                                                     ii.        Daraja B kwa Taaluma maalum zilizoainishwa chini ya Sheria-USD 500

                                                   iii.        Daraja C kwa Taaluma nyinginezo-USD 1,000

                                                   iv.        Daraja D kwa walioajiriwa na Mashirika ya Dini na ya hisani-USD 500

                                                     v.        Daraja E kwa ajili ya Wakimbizi- Bure.

  Malipo au Ada  ya huduma hii italipwa  kupitia Akaunti inayotajwa hapa chini;


  Name:        Permanent Secretary, Ministry of Labour and Employment

  A/C No:      0250211745400

  Bank:        CRDB

      Aidha ,Mfumo huu mpya wa utoaji wa vibali vya Ajira kwa wageni utaanza rasmi tarehe 1/10/2015 na maombi yawasilishwe  Ofisi ya Kamishna wa Kazi,makao Makuu ya Wizara ya Kazi na Ajira,jengo la NSSF-Mwl.Nyerere Tower,Na 42,iliyopo Barabara ya   Bibi Titi      Dar-es-salaam.


  6.      Wizara inapenda kutoa Rai kwa wadau wote kutoa ushirikiano ili kutekeleza matakwa ya Sheria kwa ufanisi wa maendeleo ya nchi yetu.


  Imetolewa
  Ridhiwani M. wema

  Msemaji.

  Wizara ya Kazi na Ajira.
  28/09/2015


  0 0

  SIKU YA MOYO, WANANCHI KUPIMWA SHINIKIZO LA DAMU BURE. 

   KATIKA kuazimisha  siku ya afya ya Moyo Duniani Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- leo itatoa huduma ya upimaji wa shinikizo la damu bure pamoja na kuwashauri wale watakaopatikana na tatizo hilo.

  Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu siku ya afya ya moyo Duniani ambayo huazimishwa Septemba 29 kila mwaka , Daktari Bingwa wa magonjwa ya Moyo  Tulizo Shemu kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kitwete amesema magonjwa ya moyo yanachangia asilimia 31 ya vifo vyote vinavyosababisha takribani watu MIlioni 17. 3 kufa kila mwaka .


            Inasadikika itakapofika mwaka 2030 zaidi ya watu Milioni 25 watakuwa wanapoteza maisha kutokana na maradhi hayo hasa katika nchi zilizo na uchumi wa  chini na kati.


            Siku ya afya ya moyo Duniani hutoa fursa kwa watu wote Duniani kuazimisha kwa vitendo katika kujilinda na janga la magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ambayo yanachangia vifo vingi .


            Dokta  Shem  ametaja baadhi ya visababishi vinavyochangia magonjwa ya moyo kuwa ni matumizi ya tumbaku, chumvi , pombe, vyakula vyenye mafuta, kutofanya mazoezi , unene uliokithiri , kutotibu ugonjwa wa kisukari na kuwa na mafuta mengi kwenye damu.  Kauli mbiu ya mwaka huu ni kuweka mazingira mazuri ya afya bora ya moyo katika sehemu zetu tunazofanyia kazi kwa kuhakikisha kila mtu anatoa mchango katika kujenga afya bora ya moyo ili kupunguza visababishi vinavyochochea magonjwa hayo.
   Daktari Bingwa wa magonwa ya moyo, Dk Tulizo Shemu (kulia) wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza na waandishi wa habari katika taasisi hiyo kuhusu siku ya afya ya moyo duniani ambayo inafanyika Septemba 29, kila mwaka.
   Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo nchini, Dk Tatizo Wane (kulia) wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza na waandishi wa habari katika taasisi hiyo kuhusu siku ya afya ya moyo duniani ambayo inafanyika Septemba 29, kila mwaka.  Kesho watu watapimwa bure shinikizo la damu na watakaopatikana na tatizo hilo watapewa ushauri wa bure. Pia siku ya kesho (Septemba 29, 2015) Taasisi hiyo itagawa vepeperushi, majarida na CD zinazozungumzia magonjwa ya moyo.
  Baadhi ya waandishi wa habari.


  0 0

                   KUSOMA  ZAIDI  links  goes  to  sheriayakub.blogspot.com
  Na  Bashir  Yakub.

  Tulipoandika namna  bora  na  taratibu  maalum  za  kufuata unapotaka  kununua  ardhi  tulisema  pia   kuwa   taratibu  za  ununuzi  wa  ardhi  huwa  zinatofautiana  kutegemea  na   mazingira  ya  kila  ardhi. 

  Tukasema  unaponunua  ardhi  kwa  msimamizi  wa  mirathi  ni  tofauti  na  unaponunua  kwa  mmiliki  mwenyewe. Unaponunua  ardhi  ya  familia  ni  tofauti  na  unaponunua  isiyo  ya  familia. 

  Vilevile  unaponunua  ardhi  ya  kijiji  ni  tofauti  na  unaponunua ardhi  isiyo  ya  kijiji.  Taratibu  hutofautiana  na  hasa  tofauti  ipo  katika  nyaraka  ambazo  zinatakiwa  kuambatanishwa  ikiwa  kama  ithibati  ya  ununuzi. Hata  uandishi  wa   mkataba  wa  manunuzi  pia  nao huwa na tofauti  katika  hili.


  1.ARDHI  YA  KIJIJI  KWA  UWEKEZAJI.

  Wako  watu  wamekuwa   wakinunua  ardhi  hasa  huko  vijijini  lakini  baadae  wamekuwa  wakijikuta  katika  migogoro  mikubwa  na  wenyeji. Mwamko  wa  kununua  maeneo  kama  bagamoyo, kisarawe, huko  chanika  dondwe na  maeneo  mengine  umekuwa  mkubwa  sana.

   Hata  hivyo  mwamko  unavyoongezeka  ndivyo  na  migogoro  inavyoongezeka. Kubwa  katika  migogoro  hii  ni  hatua  ya  wanunuzi  kutokufuata  utaratibu  wa  ununuzi aidha  kwa  kujua, kutokujua  au  kupotoshwa.


   Wakati  mwingine  ni  uelewa mdogo  miongoni  mwa  wenyeji  lakini  zaidi  ni  hili  la  kutofuata utaratibu. Mara  zote  huwa  tunasema  ni  bora  zaidi  mgogoro  unapotokea  halafu  ukukute  ulifuata  taratibu  wakati  wa  manunuzi. Bila  shaka hautakuwa  na  athari  kubwa  kwako  lakini  ni  mbaya   zaidi  ukitokea  halafu  ukukute kuna  taratibu  hukufuata kwa  bahati  mbaya  au  bila  kujua. Unakuwa  katika  hatari  ya  kupoteza. Unapokwenda  kununua  ardhi  ya  kijiji  kwasababu  yoyote  ile  hasa uwekezaji  upo  utaratibu maalum wa kufuata  nitakaoeleza.


  2.  ARDHI  YA  KIJIJI  NI  NINI.

  Ardhi  ya  kijiji  ni  ile  ardhi  iliyopo  katika  mipaka  ya  kijiji  fulani  ilyoainishwa  na  mamlaka  za  wilaya  husika  huku  ikiwa  na  hati ya  usajili  wa  kijiji. Ardhi  hii  hulindwa  kwa  taratibu  za  kimila  za  eneo  husika  ikiwa  ni  pamoja  na sheria  namba  4 ya  1999.


  3.    UTARATIBU  WA  KUNUNUA  ARDHI  YA  KIJIJI  KISHERIA.

  ( 1 ) Maombi  maalum huandaliwa  na  kuwasilishwa  kwa  mtendaji  wa  kijiji  ambaye  hupatikana  katika  kila  kijiji.

  ( 2 ) Maombi  huandaliwa  katika  fomu  maalum  ambazo  hupatikana  katika  kila  ofisi  za  kijiji. Si  maombi  ambayo  huandaliwa  kama  barua  za  kawaida za maombi.

  ( 3 ) Ikiwa  mwombaji  ni  mtu  mmoja   basi   atasaini  sehemu  maalum  na ikiwa  ni  maombi  kwa  niaba  ya  famliia  basi  watu  wawili  kutoka  ile  familia  watasaini  na  ikiwa  ni  ardhi  kwa  ajili  ya  kikundi  pia  wawakilishi  wasiopungua wawili  kutoka  kile  kikundi  watasaini  kwa  niaba  ya  wengine.

  ( 4 ) Kama  mwombaji  ni  chama  cha  ushirika  au  kampuni  basi  inatakiwa  kuwepo  wadhamini  wawili   kwa  ajili  ya  shirika  au  kampuni  hiyo. Wanaweza  kuwa  zaidi  ya  wawili  lakini  wasipungue.

  ( 5 ) Kama  anayeomba  ardhi  si  mwenyeji  wa  eneo  husika  basi  atatakiwa  kuwa  na  wadhamini  wasiopungua  watano  ambao  ni  wenyeji  wa  eneo  hilo. Sharti  ni  kuwa  kati ya  hao  wadhamini  wasiwepo  ndugu  wa  mwombaji.

  ( 6 ) Mwombaji  atatakiwa  kuambatanisha katika  maombi  yake  tamko  linaloonesha  ardhi  nyingine  anayoimiliki  Tanzania  nje  na  hiyo  anayoomba.

  ( 7 )  Ikiwa  ardhi  inaombwa  kwa  ajili  ya  makazi  basi  mwombaji  atatakiwa  kuambatanisha  tamko  linaloonesha  kuwa  ataanza  ujenzi wa  makazi hayo ndani  ya  miezi  mitatu  tangu  siku  ya  kuidhinishiwa  ardhi.

  ( 8 ) Ikiwa  mauzo  ni heka 50 au  kuendelea  ni lazima  yaidhinishwe  na  mkutano  mkuu  wa  kijiji.

  ( 9 ) Baada  ya  kukamilisha  taratibu  hizo  halmashauri  ya  kijiji  itakaa  vikao  na  ndani  ya  siku  tisini itatakiwa  kutoa  majibu.

  Kamwe  usikubali  kuuziwa  ardhi  ya  kijiji  na  viongozi   wa  kijiji  bila  kufuata  utaratibu  huu. Hii  hasa  ni kwa  wawekezaji  wanaochukua  maeneo  makubwa  kwa  shughuli  za  kiuchumi.

  MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com
  0 0

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Taarifa zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki na kujeruhiwa huko Saudi Arabia.  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kupitia Ubalozi wake mjini Riyadh, Saudi Arabia imepokea taarifa kuwa hadi kufikia tarehe 27 Septemba, 2015 watu waliopoteza maisha kufuatia tukio la mkanyagano (stampede) wa Mahujaji waliokuwa wakielekea Jamarat kutupa vijiwe huko Mina nje kidogo ya mji wa Makkah, lililotokea siku ya Alhamisi tarehe 24 Septemba, 2015 wameongezeka na kufikia 769 na majeruhi 934.


  Aidha, Wizara kupitia Ubalozi huo inaendelea kufuatilia hatma ya Mahujaji wa Tanzania waliopotea katika tukio hilo la ajali ambapo hadi sasa Mahujaji wa Tanzania wapatao 50 bado hawajaonekana. Vikundi wanavyotoka Mahujaji hao na idadi yao ni kama ifuatavyo:-

  1.  Ahlu Daawa-Mahujaji  30;

  2.  Khidma Islamiya-Mahujaji 16; na

  3.  TCDO-Mahujaji 4

  Vile vile juhudi za Ubalozi kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission na viongozi wa vikundi vilivyopoteza Mahujaji wao zimefanikiwa kuutambua mwili wa hujaji mmoja aliyefariki dunia anayejulikana kwa jina la Shafi Khamis Ali kutoka kikundi cha Ahlu Daawa. Kutambuliwa kwa mwili wa hujaji huyo kunafanya idadi ya Mahujaji wa Tanzania waliofariki dunia katika ajali hiyo kufikia watano (5).


  Pia, Wizara kupitia Ubalozi wake imepokea taarifa ya kupatikana kwa hujaji mwingine anayeitwa Nasra Abdullah akiwa hai naye kutoka kikundi hicho cha Ahlu Daawa.


  Kuhusu majeruhi, taarifa kutoka Ubalozini zinaeleza kuwa, hujaji mmoja aliyejulikana kwa jina la Mahjabin Taslim Khan alipata majeraha yaliyopelekea kukatwa mguu na kwa sasa anaendelea kupata matibabu huku hali yake ikiendelea vizuri.


  Ubalozi unaendelea na juhudi za kuwatafuta Mahujaji wengine wa Tanzania ambao bado hawajaonekana kwa ajili ya kubaini wale waliofariki au majeruhi wanaoendelea kupatiwa matibabu.


  Mahujaji wengine wa Tanzania wapo salama ambapo tarehe 26 Septemba, 2015 walimaliza ibada ya hija na tarehe 28 Septemba, 2015 wameanza safari ya kurejea nyumbani.


  Wizara inaendelea kuwaomba Wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati Serikali ikiendelea kufuatilia.

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

  Dar es Salaam


  28 Septemba, 2015


  0 0

   Mratibu wa Kampeni upande wa Vijana CCM kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Vyuo Vikuu Bw. Daniel Zenda akizungumza na Zaidi ya Vijana 500 kutoka Jimbo la Mbagala wakati wa uzinduzi wa MAGUFULI Club jijini Dar es Salaam jana. MAGUFULI Club imeanzishwa kama jukwaa la kuwakutanisha vijana nchini kote wanaomuunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli.
   Mratibu wa MAGUFULI Club wilaya ya Temeke Bw. Peter Dafi akizungumza na vijana kutoka Jimbo la Mbagala wakati wa uzinduzi wa MAGUFULI Club jijini Dar es Salaam jana. MAGUFULI Club imeanzishwa kama jukwaa la kuwakutanisha vijana nchini kote wanaomuunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli.
   Baadhi wa vijana wakifuatilia uzinduzi wa MAGUFULI Club katika Jimbo la Mbagala jana jijinI Dar es Salaam.
   Wanachama wa MAGUFULI Club wakifurahia wakati uzinduzi wa Club hiyo katika Jimbo la Mbagala jana jijini Dar es Salaam.
  Picha na:  Frank Shija
  0 0
 • 09/28/15--21:09: MUZIKI MNENE KIBAHA

 • 93.7 EFM yajinyakulia ushindi baada ya kuwafunga kibaha veterans mabao mawili kwa moja, katika mchezo  uliochezwa mwishoni mwa wiki  katika uwanja wa Tamco kibaha, Mechi hiyo ni baadhi ya mechi zinazoendelea baina ya EFM na timu mbalimbali za wasikilizaji wake, Kupitia kampeni ya Muziki mnene bar kwa bar .
  Burudani haikuishia hapo,  baada ya mechi hiyo shangwe ziliendelea ndani ya kibaha kontena. Ilikuwa ni bandika bandua ya ngoma kali kutoka kwa Rdj’s wa 93.7 EFM na  shamra shamra kutoka  kwa timu nzima ya EFM na wakazi wa kibaha.

  0 0

  NA JAMIIMOJABLOG)
  WATU wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba
  JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI????!!
  ~Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na Inje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe.

  ~ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles
  ~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50
  AINA ZA BAWASIRI
  ~Kuna Aina mbili za bawasiri
  (A) BAWASIRI YA NDANI
  ~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili
  ~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa
  ~Aina hii imegawanyika katika madaraja manne
  (1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pale panapohusika
  (2)DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyewe ndani baada ya kujisaidia.
  (3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe.
  (4)DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi
  (B)BAWASIRI YA NNJE
  ~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS
  CHANZO CHA TATIZO
  ~chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni ÷
  👉KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
  👉KUHARISHA KWA MUDA MREFU
  👉TATIZO LA KUTOPATA CHOO
  👉MATATIZO YA UMRI
  👉KUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU
  👉UZITO KUPITA KIASI
  👉MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU
  DALILI ZA BAWASIRI
  👉Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  👉kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
  👉kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  👉kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
  👉kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana
  MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI
  ~matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa na anion chip kubandika mahali penye tatizo na kuondoa tatizo Hilo
  ~Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia
  👉KULA MBOGAMBOGA ZA MAJANI, MATUNDA, NA NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
  👉KUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GRASS 6/12 Kwa siku
  👉EPUKA KUKAA CHOONI KWA MUDA MREFU
  MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI
  👉kupata upungufu wa damu (anemia)
  👉Kupata tatizo la kutokuweza kuhimil choo
  👉hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake
  👉kuathirika kisaikolojia
  👉kukosa moral ya kufanya Kazi kutokana na maumivu makali
  WASILIANA KWA 0717035770 AU 0753692612.

  0 0

   Bi Harusi mtarajiwa Ester Diana Nana (kushoto) akigonisha glasi na msimamizi wake, Hellen, wakati wa sherehe ya kuagwa (Send off) iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
  Bi harusi mtarajiwa akiwa na mumewe mtarajiwa wakielekea kupata chakula cha usiku ukumbini hapo. Watarajiwa hao wanatarajia kufunga ndoa jumamosi ya wiki hii.
  Wakati wa mlo wa usiku


  0 0
 • 09/28/15--23:10: JIFUNZE LUGHA YA ALAMA


 • 0 0

  Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
  Hiki ni kipindi kilichosikika Septemba 28, 2015
  Kutoka Tanzania tuliungana na Liberatus Mwang'ombe. Mgombea ubunge jimbo la Mbarali kwa tiketi ya CHADEMA
  Studioni alikuwepo Dj Luke Joe, na kwa njia ya simu tukaungana na wasikilizaji wengi ndani na nje ya Marekani
  KARIBU


  0 0
 • 09/29/15--01:07: MECHI ZA UEFA USIKU HU
 • Hii ni ratiba ya mechi za Jumanne ya September 29Mechi hizi zote zitachezwa saa 21:45 kwa saa za Afrika Mashariki
  Hii ni ratiba ya mechi za Jumatano ya September 30

older | 1 | .... | 990 | 991 | (Page 992) | 993 | 994 | .... | 3285 | newer