Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109570 articles
Browse latest View live

BENKI YA DUNIA: TANZANIA YAONGOZA DUNIANI KUTOA HUDUMA ZA PESA KWA SIMUTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

TANZANIA ni nchi ya kwanza duniani kutoa huduma za pesa, kutoa mikopo na kutoa riba kwa kutumia mawasiliano ya simu, Benki ya Dunia imesema na kuongeza kuwa Tanzania ni moja ya masoko makubwa zaidi duniani ya kutoa huduma ya fedha kwa njia ya simu.


Benki hiyo ya Dunia pia imesema kuwa Serikali ya Tanzania imewekeza kwa kiwango cha juu katika mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) ikilinganishwa na nchi nyingine duniani na kulingana na uwezo wake.


Benki hiyo pia imesema kuwa nchi jirani ya Kenya inaongoza kwa kutuma pesa kupitia mfumo wa M-Pesa katika eneo ambalo miaka michache iliyopita lilikuwa eneo la kujidai la nchi tajiri tu duniani.


“Huu ni mfano kutoka Afrika ambao unaweza kuigwa na nchi zote duniani,”amesema Profesa Kaushik Basu, Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia (WB) wakati akiwasilisha kwa ufupi tu yaliyomo katika Ripoti ya Benki hiyo ya World Development Report ambayo itatolewa hivi karibuni.


Profesa Basu alikuwa anazungumza jana, Jumatatu, Septemba 28, 2015 kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi uliozungumzia Hali ya Enzi za Digitali (Digital Age) uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), ikiwa ni sehemu ya majadiliano kuhusu Malengo ya Maendeleo Mapya (SDG’s) ambayo yanachukua nafasi ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG’s) ambayo muda wake wa utekekezaji wa miaka 15 umefikia mwisho mwaka huu.


Akizungumza katika mkutano huo uliohudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Estonia Mheshimiwa Toomas Hendrik Ilves na Rais wa Benki ya Dunia (WB) Dkt. Jim Kim, Profesa Kaushik alisema:


“Tuko katikati ya mapinduzi makubwa ya teknolojia, ambayo athari zake bado ni ngumu sana hata kubashiri. Na hizi ni shughuli ambazo miaka michache iliyopita zilikuwa hata hazina jina, lakini sasa inteneti na teknolojia ya digitali inabadilisha maisha ya kijamii na kisiasa ya binadamu,” alisema Profesa Basu.


Aliongeza: “Chukulia takwimu hizi – kuna kiasi cha utafuta habari kwenye google kiasi cha bilioni 4.2 kwa siku moja, kila sekunde watu wanatuma tweet 6,000 na rekodi ilikuwa Agosti mwaka 2013 wakati zilipotumwa tweet 143,199 kwa sekunde wakati ilikuwa inaonyeshwa filamu moja ya sanaa.”

Aliongeza: “Mfumo wa uwekaji na utumaji pesa wa M-Pesa katika Kenya sasa unashindana na mifumo ya siku nyingi ya nchi matajiri duniani. Kila watu wazima 1,000 kuna akaunti 700 katika Kenya ikiwa ni ongezeko 103 kutoka mwaka 2013.”


“Jirani na Kenya kuna mfano mwingine wa mafanikio makubwa zaidi duniani katika nchi jirani ya Tanzania. Tanzania imewekeza sana katika ICT na katika mfumo wa kuhamisha na kusambaza fedha. Sasa Tanzania ni soko kubwa zaidi duniani la kutuma fedha kwa njia ya simu,” alisema Profesa Kaushik.


Aliongeza: “Tanzania sasa ni nchi ya kwanza duniani kutoa huduma ya pesa, kutoa mikopo na kutoa riba kwa njia ya simu. Hii ni mifano ambayo nchi zote duniani zinaweza kuiga kutoka Afrika.”


Wakati huo huo, Rais Kikwete leo, Jumanne, Septemba 28, 2015, amekutana na kufanya mazungumzo na Malkia wa Uholanzi, Malkia Maxima wa Uholanzi, Mke wa Mfalme Willem-Alexander kuhusu jinsi gani ya kuzidi kuisaidia Tanzania kuongeza kasi yake katika kuboresha huduma za pesa kupitia ICT.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

29 Septemba, 2015

MAWAKALA ZAIDI YA 300 MWANZA WAWEZESHWA KUPATA MIKOPO

0
0
 Afisa Masoko wa Airtel kanda ya ziwa akiongea na mawakali mara baada

ya kuendesha seminar inayowapatia fulsa Mawakala wa Airtel Money
nchini nzima kupata mikopo kupitia simu zao za mkononi

Wakala wa Airtel Money katika maeneo ya Metro Mwanza, Bwn John Hainga

akichangia mada wakati wa semina ya mawakala inayowapatia  fulsa ya
kupata mikopo isiyo na dhamana ijulikanayo kama Timiza Mikopo kwa
Mawakala

 KAMPUNI ya simu za mkononi nchini Tanzania Airtel imeendelea
kuboresha huduma zake  kwa wateja hususani wajasiliamali
wanaojihusisha na shughuli mbalimbali za kibiashara, ikiwa ni pamoja
na utoaji wa huduma za Airtel Money , kwa kuwawawezesha mawakala
kupata mikopo inayoitwa " Timiza mikopo kwa Mawakal " Kupitia simu zao
za mikononi.

Airtel imewakutanisha  mawakala wa Airtel Money kutoka sehemu
mbalimbali za jiji la Mwanza ili kuwapatia mafunzo ya uboreshaji na
ukuzaji vipato katika biashara zao.

"Ukosefu wa  elimu ya uendeshaji biashara kwa wajasiliamali walio
wengi hapa nchini umeendelea kuwa ni tatizo linaloshusha kiwango cha
mapato kwa wajasiliamali kupitia shughuli zao hivyo kuzorotesha uchumi
wa taifa .

 Kwa kutambua tatizo hili Airtel imeona ipo haja kuwapatia mafunzo ya
uendeshaji biashara yatakayomwezesha mjasiliamali kutambua njia bora
ya uendeshaji biashara, Ikiwa ni pamoja na utoaji mikopo isiyo na
dhamana  kwa zaidi ya mawakala 20,000  kote nchini Ili kusaidia kukuza
biashara za mawakala , kuongeza faida zaidi katika shughuli zao na pia
upatilkanaji wa huduma ya za fedha katika jami". alisema meneja kanda
ya ziwa wa Airtel, Bwana Raphael Daudi.

Kwa upande wake mmoja ya wakala aliyehudhuria semina hiyo  bwana John
Paschal alisema" tunayofuraha kuwezesha kupata mikopo kupitia huduma
hii ya Timiza mikopo kwa mawakala. Na hii itaturahisishia kuboresha
biashara zetu kwani sasa tuna uhakika wa mitaji.  Lakini pia mafunzo
haya yatatusaidia sana katika kutunza mahesabu na kuendesha biashara
zetu kwa ufanisi zaidi."

Airtel katika kukabiliana na changamoto za kijamii na kiuchumi kwa
wateja wake imefanikiwa kuzindua huduma hii ya timiza mikopo kwa
mawakala, huduma itakayowawezesha mawakala  wa airtel money kote
nchini kupata mikopo isiyo na dhamana ya kuanzia sh. 50,000/- hadi
500,000/-

Mpiganaji Sunday Simba Shomari aadhimisha miaka mitatu ya ndoa

0
0
Leo ni mwaka wa tatu tangu niingie kwenye klabu hii ya wajanja na kuaga ukapela kwanza namshukuru Mungu kwa kunipa mke bora na familia njema , pia naomba aendelee kutoa Baraka zake kwa familia yetu daima na tusonge mbele na safari Empress wangu pendo la moyo wangu.Mungu ndiye kiongozi wetu. Amina - Sunday Simba Shomari

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA KATIKA JESHI LA MAGEREZA KWENYE BAADHI YA MITANDAO YA KIJAMII

0
0

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na tangazo kuhusu nafasi za ajira katika Jeshi la Magereza linalodaiwa kuwa limetolewa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza na kusambazwa kwenye baadhi ya Mitandao ya kijamii. Umma unajulishwa kuwa taarifa hizo siyo za kweli.

Jeshi la Magereza linapenda kuufahamisha umma kuwa ajira hutolewa na kutangazwa kupitia Vyombo vya Habari pamoja na tovuti ya Jeshi la Magereza ya www.magereza.go.tz 

Hivyo, Jeshi la Magereza linawatahadharisha Wananchi wote kuwa macho na mitandao ya kitapeli inayotoa taarifa za kupotosha na kuleta usumbufu mkubwa kwani mfumo wa ajira ndani ya Jeshi la Magereza ni wa wazi na unafuata Kanuni na Taratibu za ajira za Utumishi wa Umma.

Imetolewa na kusainiwa na,
John C. Minja
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA
29 Septemba, 2015

na si vinginevyo.

NEC: HAKUNA WIZI NA UDANGANYIFU WA KURA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 25

0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC), Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Chama cha Kitaifa cha Watu Wasioona Zanzibar (ZANAB), Adili Mohamed wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC), Jaji Damian Lubuva akisalimiana na Mwakilishi wa Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Mkoa wa Dar es Salamm Mohamed Chazi  wakati wa mkutano baina ya taasisi za watu wenye ulemavu nchini na NEC iliyofanyika leo Jumanne Septemba 29, 2015 Jijini Dar es Salaam.

Na Ismail Ngayonga MAELEZO
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)  imevitoa wasiwasi  vyama vya siasa  kuwa hakutakuwepo na wizi na udanganyifu wa kura katika matokeo ya uchagauzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajia kufanyika nchini tarehe 25 Oktoba, mwaka huu.

AIdha NEC imesema ipo tayari kushirikiana na wataalamu wa vyama hivyo katika kubaini vyanzo vya wizi wa kura iwapo tatizo hilo litajitokeza na hivyo kuhakikisha haki inatendeka kwa vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huo.


Hayo yamebainishwa leo Jumanne (Septemba 29, 2015) Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Damian Lubuva wakati wa mkutano wake na wawakilishi wa vyama vya watu wenye ulemavu aliokutana nao kwa ajili ya kupata ushauri na maoni ya taasisi hizo kuelekea uchaguzi mkuu mwezi oktoba mwaka huu.

TAARIFA ZA KUPATIKANA KWA MAJINA 18 YA MAHUJAJI KUTOKA TANZANIA WALIOPOTEA HUKO SAUDI ARABIA

0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

 


Simu: 255-22-2114615, 211906-12

Barua pepe: nje@nje.go.tz

Barua pepe: gcu@nje.go.tz

Nukushi: 255-22-2116600

              

 


                20 KIVUKONI FRONT,

                           P.O. BOX 9000,

                  11466 DAR ES SALAAM, 

                                    Tanzania.


 


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Taarifa za kupatikana kwa majina 18 ya Mahujaji kutoka Tanzania waliopotea huko Saudi Arabia


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imepokea majina 18 ya Mahujaji kutoka Tanzania ambao hadi sasa hawaonekani kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015 na kusababisha vifo vya watu 769 na wengine 934 kujeruhiwa.


Itakumbukwa kuwa tarehe 28 Septemba, 2015 Wizara ilitoa taarifa kuwa Mahujaji wa Tanzania wapatao 50 bado hawajaonekana huku wengine watano wakiwa wamefariki dunia.


Majina ya baadhi ya Mahujaji wa Tanzania ambao mpaka sasa bado hawajaonekana ni kama ifuatavyo:-


1. Abdul Iddi Hussein

2. Awadh Saleh Magram

3. Burhani Nzori Matata

4. Yussuf Ismail Yusuf

5. Saleh Mussa Said

6. Adam Abdul Adam

7. Archelaus Antory Rutayulungwa

8. Farida Khatun Abdulghani

9. Rashida Adam Abdul

10. Hamida Ilyas Ibrahim

11. Rehema Ausi Rubaga

12. Faiza Ahmed Omar

13. Khadija Abdulkhalik Said

14. Shabinabanu Ismail Dinmohamed

15. Salama Rajabu Mwamba

16. Johari Mkesafiri Mwijage

17. Alwiya Sharrif Salehe Abdallah

18. Hafsa Sharrif Saleh Abdallah


Mbali na taarifa za kupatikana kwa majina hayo, Wizara imepokea taarifa ya kutambuliwa kwa mwili wa hujaji mmoja wa Tanzania anayeitwa Hadija Shekali Mohammed wa kikundi cha Ahlu Daawa.


Aidha, Serikali ya Saudi Arabia imetoa picha za maiti za Mahujaji waliokufa Makkah ambao wamehifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti kwa ajili ya utambuzi. Hivyo, Ubalozi wa Tanzania nchini humo kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission pamoja na vikundi vya Mahujaji unaendelea na zoezi la kuzihakiki picha hizo ili kubaini kama zinalingana na sura za Mahujaji wetu waliopotea.


Vilevile, Mamlaka ya Serikali ya Saudi Arabia imesema kuwa imechukua alama za vidole za Mahujaji waliokufa ili wazilinganishe na zile walizozichukua Uwanja wa Ndege wakati Mahujaji hao wakiingia nchini humo. Wizara inaamini kuwa taarifa za alama za vidole zitakapotolewa zitasaidia sana kuwatambua Mahujaji wetu.


Pamoja na jitihada zote hizo, Ubalozi pia unaendelea na juhudi za kuwatambua Mahujaji wengine wa Tanzania ambao hawajaonekana kwa kutembelea katika hospitali zilizohifadhi maiti na kulaza majeruhi wa ajali hiyo.



Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

Dar es Salaam


29 Septemba, 2015

WASIMAMIZI NA WARATIBU WA UCHAGUZI MIKOA YA IRINGA MBEYA WATAKIWA KUJIEPUSHA NA UPENDELEO KWA WAGOMBEA

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (PICHA MAKTABA)
Na Kahema Emanuel,Mbeya

WITO umetolewa kwa Waratibu  wa uchaguzi wa mikoa ,wasimamizi  wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi wa halmashauri mikoa ya kanda za juu kusini  kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa waledi na kwa uadilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa ua mgombea.


Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro wakati akifungua mafunzo ya wasimamizi wa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi pamoja na maafisa uchaguzi halmashauri ambao ni wakurugenzi wa halmashauri na maafisa uchaguzi katika mikoa  ya Iringa na Mbeya.


Amesema ili zoezi hilo la uchaguzi liende vizuri na lisighubikwe na vurugu nivema wasimamizi hao wakatumia waledi wao na udilifu bila kuwa na upendeleo wa chama chochote cha siasa au mgombea yoyote ili kuepuka hali hiyo. 


Amesema mara baada ya kupatiwa mafunzo hayo nivema wakaendelea kutumia muda wao wa ziada kusoma na kupitia  vitabu vya maelekezo waliyopatiwa kwa kutumia kanuni na maadili ya uchaguzi ili kuimarisha uelewa zaidi kuhusu wajibu na majukumu yao katika zoezi hili la uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.


Amesema pamoja na majukumu mengine waliyonayo pia wametakiwa kutoa kipaumbele katika kutekeleza zoezi hili la kitaifa kwa ufanisi zaidi na kwa muda uliopangwa kwani uchaguzi huu utafanyika kwa siku moja tu kwa kila baada ya miaka mitano.


Aidha amesema kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetekeleza jukumu lake katika hatua ya mafunzo na maandalizi ya vifaa na rasilimali nyingine hivyo wao kama wasimamizi wanatakiwa kutekeleza wajibu wao katika ngazi zote kwa mujibu wa taratibu zilizopangwa na Tume.


Katika semina hiyo wasimamizi hao watajifunza wajibu wa wasimamizi wa vituo vya kupigia kura  ,uwendeshaji wa zoezi la upigaji kura vituoni  sanjali na uendeshaji wa zoezi la kuhesabu kura,kujumlisha kura na kutanganza matokeo ya uchaguzi.
Baadhi ya wakurugenzi na Maafisa uchaguzi kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa wakiwa katika mafunzo ya waratibu wa uchaguzi mikoa ,wasimamizi wa uchaguzi ,wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na maafisa uchaguzi wa halmashauri yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Septemba 29 ,2015.

NYOSO AFUNGIWA MIAKA MIWILI

0
0
Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu iliyokutana leo kupitia ripoti mbalimbali za michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso wa timu ya Mbeya City kucheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC John Bocco.
Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.
Klabu ya Young Africans imepigwa faini ya shiligi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake watano kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Simba SC. Kwa mujibu wa kanunu namba 42 (11) timu ambayo wachezaji wake watapata kadi zaidi ya tabo katika mchezo mmoja itapigwa faini ya shilingi laki tano.
Wachezaji waliopata kadi za njano wa Young Africans katika mchezo huo ni ni Salum Telela, Mbuyu Twite, Malimi Busungu, Ali Mustafa na Mbuyu Twite.
Aidha klabu ya Yanga imepigwa faini nyingine ya shilingi laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake kwenda kushangilia upande wa Simba SC mara baada ya mchezo kumalizika.
Mchezo utatazamwa tena ili kuangalia malalamiko ya Simba SC dhidi ya mwamuzi.
Simba pia inapigwa faini baada ya wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuwashambulia waamuzi baada ya mchezo ambapo waliwarushia chupa za maji ambazo nyingine ziliwakosa waamuzi na kumpata kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.
Mchezo namba 26 wa VPL kati ya Coastal Union na Mwadui uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Chumba cha Coastal Union kilikuwa na harufu kali sana. Baadhi ya mashabiki wa Coastal Union waliokuwa nyuma ya goli la upande wa kaskazini walitoa  lugha ya matusi kwa waamuzi na kutishia kuwapiga na pia walimrushia mawe mwamuzi msaidizi wa pili Shafii Mohamed na jiwe moja lilimpiga mgongoni na kumjeruhi kidogo mwamuzi na aliomba msaada wa jeshi la polisi kutuliza ghasia, mchezo ulisimama kwa dakika 3.
Kwa mujibu wa kanuni namba 42 (1) ya udhibiti wa wachezaji Coastal Union itatozwa faini ya Tsh 500,000/=
Mchezo namba 22 wa VPL kati ya Mtibwa Sugar na Ndanda uliofanyika kwenye uwanja wa Manungu, Turiani. Ndanda hawakuleta watu wa kutosha kwenye pre match meeting hivyo wanapigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000/=)
Mchezo namba 23 wa VPL kati ya Simba SC na Kagera Sugar uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Dar es salaam. Simba walikuwa na wajumbe watatu na Kagera Sugar walikuwa na mtu mmoja tu tena hakuja na vifaa. Timu zote zimepigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000).
Mchezo namba 17 wa VPL kati ya Stand united na African Sports kocha wa Stand United alitolewa nje ya eneo la ufundi kwa kutoheshimu taratibu za eneo hilo na pia alikataa kuongea na vyombo vya habari kwa hiyo kwa mujibu wa kanuni namba 40 (11) anafungiwa kukaa kwenye benchi la ufundi kwa mechi mbili na faini ya sh 500,000/= kwa kila kosa jumla 1,000,000/=.
Friends Rangers na KMC Mechi Na 8 Kundi A iliyofanyika uwanja wa Karume 27.9.2015. Timu ya KMC ya kinondoni ilifanya mabadiliko kwa kuingiza wachezaji 4 ambao ni kinyume cha kanuni. Kwa mujibu wa taarifa ya mwamuzi wachezaji waliofanyiwa mabadiliko ni
i. Frank Mashoto badala ya Kudra Omari
ii. Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon
iii. Mfanyeje Musa badala ya Kabange Mgunda na
iv. Sultani Kasiras badala ya Adam Said
Kwa mujibu wa kanuni namba 14 (25) KMC imepoteza mechi na kupigwa faini ya Tsh 200,000/=. Mwamuzi wa akiba anafutwa kuchezesha ligi msimu huu na mwamuzi wa kati anapewa onyo.


MAENDELEO ENDELEVU 17 YA DUNIA YAZINDULIWA TANZANIA

0
0
IMG_3349
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins-Falk (katikati) wakipata picha ya kumbukumbu sambamba na mmoja wa wadau wa maendeleo. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Mwandishi wetu
UMOJA wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wamezindua rasmi malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).

Malengo hayo ambayo pia yanajulikana kama malengo ya dunia yamezinduliwa jana Septemba 29 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

Uzinduzi huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, na Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame kwa niaba ya serikali, Bi. Fionnuala Gilsenan, Balozi wa Ireland na Bi. Liz Lloyd, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa niaba ya wadau wa mradi wa Project Everyone Partners.

SDGs ni wito wa dunia wa kuchukuliwa kwa hatua za kuufuta umaskini, kuihami dunia dhidi ya uharibifu wa mazingira na kuhakikisha kwamba kila mwanadamu anaishi maisha stahiki katika amani na ustawi.
Katika malengo hayo 17 yapo makusudio 169 yanayotoa ramani ya utengenezaji wa sera za maendeleo na namna ya kutekeleza kwa miaka 15 ijayo.
Malengo hayo yakijengwa juu ya mafanikio ya malengo ya milenia (MDGs), yameingiza vitu vipya kama mapambano dhidi ya tofauti za kiuchumi, ubunifu, mabadiliko ya tabia nchi, lishe, amani na haki. SDGs ni mpango wa dunia unaojikita kwa ustawi wa wanancni na dunia.
IMG_3303
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (kushoto) na Kiongozi wa mabalozi wa nchi za nje hapa nchini Mheshimiwa Juma Mpango, ambaye ni balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiwa wameshikilia lengo namba 16 na 17 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ambayo yamezinduliwa rasmi nchini Tanzania jana 29, Septemba 2015.

UPENDELEO WA KISHERIA KWA NYUMBA YA MAKAZI KABLA YA KUNADISHWA.

0
0
KUSOMA  ZAIDI  links  goes  to  sheriayakub.blogspot.com
Na  Bashir  Yakub.

KISHERIA  haizuiwi  kuweka  rehani  nyumba  ya  makazi  kwa  ajili  ya  kupata  mkopo  kutoka  taasisi  yoyote  ya  fedha. Jambo la msingi  sana  ni  kuwa  watoa  mkopo   wajiridhishe   na  umiliki  wa  nyumba  hiyo  hasa  kwa  kuangalia ikiwa  ni  mali  ya  familia  au  hapana ili wachukue  hadhari  za  kisheria.


Nyumba  ya  makazi  ni  ipi.  Nyumba  ya  makazi  ni  ile  nyumba  ambayo  inatumiwa  na  binadamu  kuishi  lakini  zaidi  wanaoishi  mle  ndani  iwe  ni  familia  ya  mchukua  mkopo.  Yawezekana  nyumba  ikawa  ni  ya makazi kwa  watu  wengine  lakini  ni  ya  biashara  kwa  mchukua  mkopo. Kwa  mfano  nyumba  za  kupanga  ambapo  mwenye  nayo  anaishi  kwingine   na nyumba  iko  kwingine ikiwa  na  watu  wengine.

 Nyumba  ya  namna  hii  haitaingia  kwenye  nyumba  ya  makazi  kwa  tafsiri  hii.  Hata  hivyo  haitarajiwi  mchukua  mkopo  kuhamia  kwenye  nyumba  ambayo  sio  ya  makazi  kwa  makusudi  na kuifanya  ya  makazi  akilenga   kuhadaa  ili  kupata  upendeleo  wa  mahakama.  Akifanya  hili  atakuwa  amedanganya  na  ni  kosa  kama  tutakavyoona.


1.MAKOSA  YA  KISHERIA  KWA  MKOPAJI.

( a ) Sheria  ya  masuala  ya  rehani  ya  2008  inamtaka  mkopaji  kutofanya  udanganyifu  wa  aina  yoyote  kwa  taasisi inayotarajia  kumpa mkopo. Moja  ya  udanganyifu  ni  kama  ilivyoelezwa  hapo  juu  lakini  pia  upo  udanganyifu  mwingine  mwingi  ambao hufanywa  na  wakopaji. Kwa  mfano  kuweka  rehani  nyumba  moja  kwa  taasisi  tofauti,  kudanganya  nyumba  sio  ya  familia  wakati  ni  ya  familia  na  udanganyifu  mwingine  mwingi  ambao  hulenga  kumnufaisha  mkopaji.  


IT BRIDGE YAWAFIKIA WANAFUNZI 60,000

0
0
IMG_3000
Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Na mwandishi wetu
JUMLA ya wanafunzi 60,000 katika shule 150 nchini wamepitiwa na mafunzo ya programu ya Bridge IT yenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kidijiti (digital technology) katika ufundishaji na ujifunzaji wa Hisabati,Sayansi na Stadi za Maisha.
Hayo yamsemwa na Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome kuzindua maonesho ya Tehama.

Alisema kutokana na mafanikio yaliyotokea sasa wanatanua wigo baada ya kuwezeshwa kifedha na Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya elimu (Global Partnership For Education) kwa ajili ya kuendeleza teknolojia hiyo katika kujifunza na kufundisha katika shule za msingi na hasa darasa la awali la kwanza hadi la nne.

Aidha maonesho hayo yanayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere yana lengo la kuonesha ubunifu ambao upo tayari kutumika kufanikisha mafunzo hayo.

Pia maonesho hayo yanatarajia kujadili na kuangalia mbinu za kielektroniki zitakazoweza kuendana na mazingira ya Tanzania katika ufundishaji na kujifunza kwa gharama nafuu.

Pia wanatarajia kuangalia utayari wa walimu na namna ya kuwabadilisha mtazamo ili waweze kufundisha na kufundishika.
“Lengo la serikali kupitia Wizara ya Elimu ni kupanua wigo wa elimu hasa elimu ya awali kwa kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano ambayo itabadilisha ufundishaji kutoka kutumia vitabu vilivyopo katika mfumo wa ‘hard copy’ na kuwa katika mfumo wa sauti na picha au ‘soft copy’,” alisema Profesa Bhalalusesa.
IMG_3089
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifuatilia kwa makini risala Kamishina wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Eusella Bhalalusesa (hayupo pichani).

NAMELOK SOKOINE AZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE MONDULI AHIDI KUENDELEZA ALIPOISHIA LOWASSA

0
0
 Namelok Moringe Sokoine akiwasili katika uwanja huo wa Nanja tayari kwa uzinduzi wa kampeni.
 
Wazee wa Kimila wa Jamii ya Kimaasai wa Monduli wakiongoza dua maalim ya kumuombea Binti yao Namelok.
 Mwalimu Lorinyu Nkoosi, mmoja wa waliochuana na Namelok Sokoine katika mchakato wa uteuzi ndani ya CCM akiongea. 
 Wananchi wa Monduli wakiwa katika mkutano huo.
Wajane wa Waziri Mkuu wa Zamani wa Tanzania, Edward Moringe Sokoine ambao ni mama za Namelok Sokine wakitambulishwa mkutanoni hapo na Mwenyekiti wa kamati ya kampeni za CCM jimbo la Monduli, Paul Kiteleki.
 Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro (kulia) akimkabidhi ilani ya Chama cha Mapinduzi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Monduli Mkoani Arusha kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Namelok Sokoine wakati wa uzinduzi wa jkampebni zake uliofanyika Monduli jana.
 Dk Asha-Rose Migiro akisalimiana na wamama wa kimaasai alipowasili mkutanoni hapo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MAGUFULI AENDELEA NA KAMPENI ZAKE, LEO KUUNGURUMA LIVE UWANJA WA JAMHURI MKOANI DODOMA

0
0
 Pichani kati ni Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli akiwa sambamba na Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde kwa pamoja wakiwapungia wananchi wa Mtera (hawapo pichani),ndani ya mji wa Mvumi wilayani Chamwino mkoani Dodoma
 Wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kuomba kura za Urais jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dododma.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia  Wakazi wa jimbo la Mtera huku akiwamwagia sera zake za kuomba kura za kuwania nafasi ya Urais katika awamu ya kipindi cha tano,mapema jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dododma.
 Mgombea Ubunge wa jimbo la Kibakwe,Wilayani Mpwapwa,Ndugu Dkt.Simba Chawene akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa kijiji cha  Chipogolo (hawapo pichani),wakati akitokea Iringa vijijini akielekea mkoani Dododma kuanza kampeni zake mkoani humo,kulia kwake ni Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwatazama wananchi waliokuwa wakimuuunga mkono kuwa watampa kura za ndio 
 Dkt Magufuli akiwapungia Wananchi wa kijiji cha Chipogolo Wilayani Mpwapwa,mara baada ya kuwahutubia mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni,shoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma,Alhaji Adam Kimbisa.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Kada mkongwe wa chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.John Samuel Malecela akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kwa wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni.
Wakazi wa jimbo la Mtera,mjini Mvumi,Wilayani Chamwino wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kuomba kura za Urais jioni ya leo,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dododma.
 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani Ndugu William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo mapema leo asubuhi mkoani Iringa wakati wa kumnadi Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli
  wakazi wa Kijiji cha Idodi na Pawaga wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mapema leo asubuhi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.


BBC DIRA YA DUNIA JUMANNE 29.09.2015

Article 12


SUZA 2nd Round admission for 2015-2016 academic year

Taarifa za kupatikana kwa majina 18 ya Mahujaji kutoka Tanzania waliopotea huko Saudi Arabia

0
0
 Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imepokea majina 18 ya Mahujaji kutoka Tanzania ambao hadi sasa hawaonekani kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015 na kusababisha vifo vya watu 769 na wengine 934 kujeruhiwa.

Itakumbukwa kuwa tarehe 28 Septemba, 2015 Wizara ilitoa taarifa kuwa Mahujaji wa Tanzania wapatao 50 bado hawajaonekana huku wengine watano wakiwa wamefariki dunia.

Majina ya baadhi ya Mahujaji wa Tanzania ambao mpaka sasa bado hawajaonekana ni kama ifuatavyo:-

1. Abdul Iddi Hussein
2. Awadh Saleh Magram
3. Burhani Nzori Matata
4. Yussuf Ismail Yusuf
5. Saleh Mussa Said
6. Adam Abdul Adam
7. Archelaus Antory Rutayulungwa
8. Farida Khatun Abdulghani
9. Rashida Adam Abdul
10. Hamida Ilyas Ibrahim
11. Rehema Ausi Rubaga
12. Faiza Ahmed Omar
13. Khadija Abdulkhalik Said
14. Shabinabanu Ismail Dinmohamed
15. Salama Rajabu Mwamba
16. Johari Mkesafiri Mwijage
17. Alwiya Sharrif Salehe Abdallah
18. Hafsa Sharrif Saleh Abdallah

Mbali na taarifa za kupatikana kwa majina hayo, Wizara imepokea taarifa ya kutambuliwa kwa mwili wa hujaji mmoja wa Tanzania anayeitwa Hadija Shekali Mohammed wa kikundi cha Ahlu Daawa.

Aidha, Serikali ya Saudi Arabia imetoa picha za maiti za Mahujaji waliokufa Makkah ambao wamehifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti kwa ajili ya utambuzi. Hivyo, Ubalozi wa Tanzania nchini humo kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission pamoja na vikundi vya Mahujaji unaendelea na zoezi la kuzihakiki picha hizo ili kubaini kama zinalingana na sura za Mahujaji wetu waliopotea.

Vilevile, Mamlaka ya Serikali ya Saudi Arabia imesema kuwa imechukua alama za vidole za Mahujaji waliokufa ili wazilinganishe na zile walizozichukua Uwanja wa Ndege wakati Mahujaji hao wakiingia nchini humo. Wizara inaamini kuwa taarifa za alama za vidole zitakapotolewa zitasaidia sana kuwatambua Mahujaji wetu.

Pamoja na jitihada zote hizo, Ubalozi pia unaendelea na juhudi za kuwatambua Mahujaji wengine wa Tanzania ambao hawajaonekana kwa kutembelea katika hospitali zilizohifadhi maiti na kulaza majeruhi wa ajali hiyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
29 Septemba, 2015

Deaths of Wildebeest in Mara River a natural phenomenon

0
0
Africa Geographic website ran a story with a caption “hundreds of wildebeest found dead in Tanzania”. The website posted a number of pictures taken along Mara river displaying dead wildebeest and went further stating that “…the authorities have been contacted and the exact cause of death has yet to be confirmed”. 
Tanzania National Parks would like to clarify on the story which has also been quoted by other social media as follows: 
Serengeti Wildebeest Migration is an annual natural phenomenon which takes place between Serengeti National Park in Tanzania and Maasai Mara Game Reserve in Kenya where a number of  up to two millions animals mostly wildebeest and zebra move in a clockwise rotational route determined by the availability of grazing and water. 
During the migration a number of catastrophes occur, including disease, predation and accidents which put the livelihood of migrating animals at high risk. Drowning in Mara River is one of the occurrences during the migration in the Serengeti-Mara ecosystem and it is estimated that more than 250,000 wildebeest die during the journey. 
Other causes of deaths include stampede and other predators. However, wildebeest deaths during migration are replenished with more than 350,000 births per year. 
In view of the above, Tanzania National Parks would like to inform the public that the deaths are purely natural and not much could be done to prevent. 
In the National Parks and other protected areas nature is always left to take its own course. 
Issued by 
Corporate Communications Department 
Tanzania National Parks 
29th September, 2015 
dg@tanzaniaparks.com 
www.tanzaniaparks.com

BEI YA MADAFU LEO

Mkasi | S13E12 with BBC's Salim Kikeke Extended Version.

Viewing all 109570 articles
Browse latest View live




Latest Images