Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 989 | 990 | (Page 991) | 992 | 993 | .... | 3270 | newer

  0 0


  0 0

  dickson busagaga & salome mhozya wedding (9)
  Mwakilishi wa Globu ya Jamii Kanda ya Mshariki  Mpiganaji Dickson Busagaga (Blogger) na Salome Mhozya katika picha baada ya kufunga ndoa iliyowafanya kuungana na kuwa mwili mmoja tukio lililofanyika katika kanisa la Mt. Teresia wa Mtoto Yesu jimbo kuu la Tabora mnamo tarehe 23 Sep, 2015.
  dickson busagaga & salome mhozya wedding (8)
  Waharusi (Dickson na Salome) wakionesha pete zao mara baada ya kuungana na kuwa kitu kimoja.
  dickson busagaga & salome mhozya wedding (2)
  Hakika ilikuwa ni siku ya furaha sana kwao, hata walipoingia ukumbini katika sherehe ya usiku walidhihirisha kuto kubahatisha kuungana kwao.
  dickson busagaga & salome mhozya wedding (3)
  Furaha ilitawala sana miongoni mwao na waalikwa wote.

  0 0


  Katibu wa TUICO  Mkoa wa Mbeya Ndugu Merboth Kapinga akizungumza na wajumbe wa Tuico siku ya uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Otu jijini Mbeya.(JAMIIMOJABLOG)
  Wajumbe wa mkutano wakiimba wimbo wa pamoja.

  Na Emanuel Madafa,Mbeya
  CHAMA cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri Mkoa wa Mbeya, kimefanikiwa kupata viongozi wapya watakao kiongoza chama hicho katika kipindi cha miaka mitano 2015  hadi 2020.

  Uchaguzi umefanyika katika chuo cha wafanyakazi (Otu) jijini Mbeya na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka Taasisi za serikali na binafsi ambao wanawakilisha chama hicho cha (Tuico) mkoa wa Mbeya.

  Akizungumzia uchaguzi huo, Katibu wa TUICO  Ndugu Merboth Kapinga, amesema uchaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za chama hicho ambacho zinaeleza kuwa kila baada ya miaka mitano ni lazima chama kichague viongozi wapya.

  Amesema, wafanyakazi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye vituo vyao vya kazi lakini matatizo hayo yanashindikana kutatuliwa kutokana na mambo madogomadogo ambayo yanahitaji kupatiwa ufumbuzi kwa pande zote mbili.

  Amesema, wafanyakazi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye vituo vyao vya kazi lakini matatizo hayo yanashindikana kutatuliwa kutokana na mambo madogomadogo ambayo yanahitaji kupatiwa ufumbuzi kwa pande zote mbili.

  Hata hivyo amewataka viongozi hao kujenga uwezo wa kupambana na migogoro ya kifedha kwani ndio changamoto kubwa inayowakabili wafanyaazi na waajiri.

  Aidha amesisitiza kuwa , wafanyakzi ni lazima wawajibike kwanza halafu ndio tudai haki nzetu kama vile nyongeza ya mshahara na motisha mbalimbali.

  Viongozi hao waliopatikana ni Mwenyekiti wa chama hicho, Willium Mhando pamojana na wajumbe wa kamati tendaji, Boniface Mwanyamba kutoka kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi , Joyce Mwakifuna kutoka kampuni ya Coca Cola kwanza.

  Wengine ni Mwanaidi Thadei na Michael Msovakumwao wajumbe kitengo cha biashara,  sekta ya fedha, Winifrida Kinyakisu na Mohamed Tangulia.

  0 0

   Mwenyekiti Mpya wa Mashindano ya Miss Tanzania Juma Pinto akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni msemaji wa kamati hiyo na Miss Tanzania namba 2 mwaka 2006 Jokate Mwegelo.

  Allen Mhina Na Ally Daud – Maelezo
  KAMATI inayosimamia mashindano ya Miss Tanzania Lino International Agency imepata Mwenyekiti na wajumbe wapya watakaoandaa ,kuratibu na kusimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.

  Akiwatambulisha wajumbe hao mbele ya waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania iliyomaliza muda wake  Hashim Lundenga amesema  kuwa kamati  mpya ndiyo itakayowajibika na shughuli zote zilizokuwa zikifanywa na kamati ya awali.

  Amesema kamati hiyo itafanya kazi zake kwa kuzingatia sheria na vigezo vyote vya kimaadili ili kuepuka  ukiukwaji wa taratibu za mashindano hayo.

   “Hatutamvumilia mwanakamati yeyote atakayevunja miiko ya mashindano haya, sisi tutakuwa nyuma tukiangalia kwa umakini”, amesema Bw. Lundenga.

  Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa kamati hiyo  Juma Pinto ametoa pongezi za dhati kwa kamati iliyomaliza muda wake na kuhaidi kukubaliana na mfumo unatumika kuratibu  mashindano hayo .

  “Namshukuru  Lundenga kwa  kunikabidhi nafasi hii ya mwenyekiti wa kamati ya miss Tanzania,  naahidi kuratibu mashindano haya kwa kuzingatia vigezo na masharti yaliyowekwa ili kamati yangu iweze kukidhi haja ya mashindano haya”. Amesema.

  Naye Msemaji Mkuu wa kamati hiyo na aliyekuwa Miss Tanzania namba mbili  mwaka 2006 Jokate Mwegelo, ametoa rai kwa wasichana wa kitanzania wajitokeze kushiriki mashindano hayo kwa kuonesha vipaji walivyonavyo na kupata ajira.

  Mwishoni mwa mwaka  jana Mashindano  ya Miss Tanzania  yalikumbwa na mtafaruku wa ukiukwaji wa maadili na vigezo vya mashindano na kulazimika kusimamishwa kwa muda na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).

  0 0

   Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia gharika ya wananchi wa Makambako mkoani Iringa ambako alipita leo kumalizia viporo vya mkoa huo kwenye kampeni zake.
   Wananchi kwa maelfu wakimsikiliza Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia huko  Makambako mkoani Iringa ambako alipita leo kumalizia viporo vya mkoa huo kwenye kampeni zake.

   Wagombea wa nafasi mbalimbali wa Mafinga wali-Magufulika mbele ya Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli katika jimbo la Mafinga mkoani  Iringa ambako alipita leo kumalizia viporo vya mkoa huo kwenye kampeni zake.
  MGOMBEA ubunge jimbo la Mafinga Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Cosato Chumi, aki-Magufulika
  Mgombea Ubunge Jimbo la Mufindi Kaskazini, Mahamudu Mgimwa akidhihirisha kuwa yupo fiti. Picha na Ahmad Michuzi Jnr.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0
 • 09/27/15--13:23: Article 14


 • 0 0

  ·          Tanzania imetimiza masharti yote ya kupatiwa raundi ya pili ya fedha za maendeleo kutoka Shirika la Maendeleo ya Milenia la Millennium Challenge Corporation (MCC) la Marekani na itaanza kupata na kunufaika na mabilioni hayo ya fedha baada ya wajumbe wa Bodi ya MCC kupiga kura ya kuidhinisha kutolewa kwa fedha hizo chini ya Mpango wa MCC-2.
  Habari hizo njema zimetangazwa Jumamosi, Septemba 26, 2015, kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, na Mtendaji Mkuu wa MCC, Bi. Dana J. Hyde katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya JW Marriot Essex House, New York, na kuhudhuriwa na watumishi waandamizi wa MCC akiwamo Bwana Kamran Khan, Makamu wa Rais wa Operesheni za MCC. Rais Kikwete yuko New York kuhudhuria shughuli za mwaka huu za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

  “Hongera Mheshimiwa Rais kwa sababu nchi yako, Tanzania imetimiza masharti yote ya kupata fedha nyingine chini ya mpango wa MCC - 2, ikiwa ni pamoja na uongozi wa MCC kuridhika kuwa Tanzania inachukua hatua za dhati kupambana na rushwa,” Bi. Hyde amemwambia Rais Kikwete na viongozi wengine wa Tanzania akiwamo Waziri wa Nchi za Fedha wa Zanzibar, Mheshimiwa Yusuf Omar Mzee.

  Bi. Hyde amemwambia Rais Kikwete kuwa Bodi ya MCC, katika mkutano wake wa Septemba 17, mwaka huu na chini ya Mwenyekiti wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Bwana John Kerry, imeafiki kuhusu kipengele pekee kilichokuwa kimebakia katika masharti ya kupata fedha za MMC kuwa ni kweli Tanzania inakabiliana ipasavyo na rushwa na kuchukua hatua stahiki kukabiliana na janga hilo la rushwa.

  MCC imetoa taarifa ya kuthibitisha kuwa Tanzania imetimiza masharti ya kuiwezesha kufaulu kupata raundi ya pili ya fedha za maendeleo na pia imetoa taarifa ya kuthibitisha kuwa ni kweli Bodi ya MCC imeridhishwa na hatua zinazochukuliwa kukabiliana na rushwa.

  Tofauti na fedha nyingi zinazotolewa na wafadhili wengi duniani, fedha za MCC hazitakiwi kurudishwa na nchi inayopewa fedha hizo na pia nchi husika hupewa uhuru wa kuchagua aina ya miradi ya maendeleo ambayo inaitaka igharimiwe na fedha hizo.

  Miongoni mwa wajumbe wengine wa Bodi ya MCC ni pamoja na Waziri wa Fedha wa Marekani ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Mwakilishi wa Biashara wa Marekani duniani, Mwendeshaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), nafasi ambayo kwa sasa anaikaimu Bwana Alfonsi Lenhardt, Mtendaji Mkuu wa MCC Bi. Hyde na Rais wa Taasisi ya International Republican Institute (IRI) Balozi Mark Green.

  Mabalozi Lenhardt na Green walikuwa mabalozi wa Marekani katika Tanzania wakati wa majadiliano, upitishaji na utekelezaji wa MCC–1.

  Bi Hyde amesema sasa linalobakia ni kwa wajumbe wa Bodi kupelekewa muhtasari wa kuidhinisha mabilioni hayo kwa Tanzania ambayo chini ya mpango wa uwekezaji wa MCC–2 yatakwenda katika kuboresha huduma za umeme katika Tanzania ikiwa ni pamoja na kusambaza umeme katika vijiji vingi zaidi nchini. Kiasi cha asilimia 46 ya Watanzania kwa sasa wanapata umeme kutoka asilimia 10 ya mwaka 2005 na sehemu kubwa ya asilimia hiyo imetokana na msaada wa MCC-1.

  Chini ya Mpango huo wa pili wa MCC, Tanzania itapatiwa kiasi cha dola za Marekani milioni 472.8 (sawa na sh. bilioni 992.80). Kwa kutilia maanani kiasi cha dola milioni 698 (sawa na sh. trilioni 1.46) ambazo zilitolewa chini ya MCC-1 basi Tanzania itakuwa imepata jumla ya dola za Marekani trilioni 2.45 za maendeleo kutoka Marekani katika kipindi cha miaka 10 tu iliyopita. Fedha za MCC-2 zitaanza kutolewa mwakani, 2016.

  Kiasi kilichotolewa kwa Tanzania wakati wa MCC-1 ndicho kilikuwa kiasi kikubwa zaidi ambacho kimepata kutolewa na Marekani chini ya Mpango huo wa Millennium Challenge Corporation na kwa kupita MCC-2 Tanzania itakuwa ni nchi ambayo itakuwa imepata kiasi kubwa cha fedha za maendeleo chini ya MCC duniani.

  Fedha zilizotolewa chini ya MCC -1 zilitumika kujenga Barabara za Tunduma-Sumbawanga, Tanga-Horohoro na Namtumbo-Songea-Mbinga.

  Aidha, fedha hizo zilitumika kujenga upya mfumo wa huduma za maji kwa ajili ya miji ya Dar es Salaam na Morogoro na zilitumika kusambaza umeme katika vijiji vya mikoa 10 ya Tanzania Bara.

  Fedha hizo vile vile zilitumika kutandaza njia ya pili ya kusafirisha umeme chini ya Bahari ya Hindi kati ya Bara na Tanzania Visiwani na pia zilitumika kujenga barabara zote kuu za Kisiwa cha Pemba na baadhi ya barabara za Unguja kwa kiwango cha lami.


  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.

  27 Septemba, 2015


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na  Mtendaji Mkuu wa MCC, Bi. Dana J. Hyde katika mkutano wao uliofanyika katika Hoteli ya JW Marriot Essex House, New York
  Rais  Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa MCC, Bi. Dana J. Hyde katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya JW Marriot Essex House, New York, na kuhudhuriwa na watumishi waandamizi wa MCC akiwamo Bwana Kamran Khan, Makamu wa Rais wa Operesheni za MCC.
  Rais  Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa MCC, Bi. Dana J. Hyde katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya JW Marriot Essex House, New York. Picha na Freddy Maro

  0 0

  In line with her focus on making the case for children's education across Africa, especially Girls Education, 13 year old education advocate and the worlds youngest film maker has visited one of the lesser known IDP's  (Internally Displaced Persons) camp near Abuja city. It was formed informally as a result of the Boko Haram challenges in North East Nigeria.

  Accompanied by her small team of volunteers, she made he unscheduled visit to the IDP Camp near Games Village - Abuja, to meet the children and encourage them despite their very difficult circumstances. She spent the afternoon teaching them the alphabets, and they in turn taught her some of their local games they play to while away time. For the younger children, she gave then "Angry Bird" Themed toothbrushes and toothpaste sets - something simple to remind them they are still children, and have not been totally forgotten. The camps are seldom visited by children, and she was a refreshing sight to the camp residents.

  A few days earlier in Abuja, she was received by various envoys to Nigeria in their Embassy's, including the Ambassadors of Tanzania, Cuba, Trinidad & Tobagoand the USA. Her discussions centered on various areas of the Education subject, including ways these governments could assist her Dream Up, Speak Up, Stand Upproject, in making a measurable difference to the lives of the more than 10 million Nigerian children, currently out of school.

  On arrival in Lagos, she was a guest at one of the slum2school students programs in Makoko - Lagos, where she donated books, spoke to the children, encouraged them to dream, and showed them a video clip of some of her work.
   Zuriel with Cuba's envoy to Nigeria
   Zuriel with Tanzania's envoy to Nigeria
   Zuriel with the ambassador of Trinidad & Tobago in Nigeria
   Zuriel with the US Ambassador to Nigeria
  Zuriel at one of the slum2school students programs in Makoko - Lagos, where she donated books. For more photos CLICK HERE

  0 0

  Na John Gagarini, Chalinze 
  WAZAZI wa watoto wa wafugaji kwenye Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo wametakiwa kuachana na tabia ya kuwafanya watoto wao kuwa wachungaji wa mifugo huku wakikosa haki ya kupata elimu. 
  Hayo yalisemwa kwenye na Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwani Kikwete Mazizi kata ya Msata wakati wa mkutano wa kampeni na kusema kuwa baadhi ya wazazi wa watoto wa wafugaji wanaendeleza utamaduni wa kutowapeleka watoto wao shule na kuwaacha wakichunga mifugo ya wazazi wao. 
  Ridhiwani alisema kuwa nyakati hizi siyo za kuwaacha watoto wasipate elimu kwani zimepitwa na wakati na urithi wa mtoto ni elimu na siyo mali kwani bila ya elimu mali hupotea bila ya faida yoyote kwa mtoto na familia nzima. 
  “Hapa hatupaswi kuonyesha umahiri wa mtoto kuonyesha ufundi kujua anatunzwaje kikubwa ni kuwasomesha ili baadaye hata kama watakuja kuwa madaktari basi watawasaidia kuwatibia mifugo yenu kwa utaalamu,” alisema Ridhiwani. 
  Alisema kuwa tamaduni kama hizo hazipaswi kupewa nafasi wakati kama huu wakati uliopo ni watoto kwenda shule ili kuwajengea maisha bora ya baadaye ambayo yatawasaidia kuliko kumnyima elimu. 
  “Namshukuru Mungu pamoja na wazazi wangu kwa kunipatia elimu ambayo imenisaidia na kuweza kunifikisha hapa nilipo lakini nisingepata elimu ningekuwa wapi kwani urithi niliopewa ni elimu ambayo itanisadia katika maisha yangu yote kwani hata kama una mali huna elimu ni kazi bure lazima wazazi wabadili mitazamo na kutoa kipaumbele kwenye elimu,” alisema Ridhiwani 
   Aidha alisema kuwa moja ya vitu ambavyo anavipigania katika kipindi kijacho endapo atachaguliwa kuwa mbunge ni suala la elimu kwani anataka Jimbo hilo liwe na wasomi wengi ili waweze kuisaidia jamii ya Chalinze. 
  Naye mkazi wa Msata Shaban Mtambo alisema kuwa jamii ya wafugaji bado inaona watoto kuchunga mifugo kuwa ni kazi yao jambo ambalo ni makosa kwani mtroto anakosa haki zake za msingi ikiwa ni pamoja na elimu.
   Mtambo alisema kuwa licha ya baadhi ya wazazi wa watoto wa wafugaji lakini wameendelea kuwahamasisha wazazi wenzeo kuachana na utamaduni huo ambapo wengine tayari wameshaaanza kubadilika na kuwapeleka watoto wao shule.
  Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Msoga wakimsikiliz amgombea Ubunge Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete hayupo pichani kwenye mkutano wa kampeni.

  Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kwa CCM Ridhiwani Kikwete akizungumza na wakazi wa kijiji cha Makombe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.

  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo Almas Maskuzi kulia akimnadi mgombea wa CCM Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete kwenye Kijiji cha Pongwe Kiona.
  Wakazi wa Lugoba wakimsikiliza mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete hayupo pichani.

  0 0

     Msanii John Kitime akipokea kadi ya matibabu itakayomwezesha kupata huduma kote nchini.
    Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Rehani Athumani akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawako pichani) kuhusiana na utaratibu wa kujiunga na Mfuko huo
      Baadhi ya wasanii waliohudhuria hafla hiyo pamoja na waandishi wa habari.

  0 0

  Na Dotto Mwaibale
  WATANZANIA wenye asili ya India wa dhehebu la Hindu (Baniani), leo wameadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Mungu wa mdogo wa kiume mwenye daraja kubwa (Ganpati Bappa Morya) na mwenye sura ya tembo.

  Mungu huyo hufanyiwa sherehe baada ya kufanyika kwa ibada ya siku tisa ambapo siku yake ya kuzaliwa alipelekwa baharini kwaajili ya kuungana na Mungu wa kike walio kwenye mito mitatu mitakatifu iliyopo nchini India ambayo ni Sarasgad, Amba na Raigad.

  Sherehe hizo zilianza kwa ibada ambapo pia walitumia fursa hiyo kuiombea amani ya nchi hii katika maadhimisho ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa iliambatana na utoaji wa sadaka za vyakula mbalimbali na maombi hupelekwa baharini kwa ajili ya kuungana na Mungu kike.

  Katika sherehe hizo jijini hapa zilianzia katika nyumba zao za ibada ambapo kulikuwa na msafara mkubwa ambao ulihusisha na magari yaliyobeba Mungu huyo huku wanawake wakijipamba kwa mavazi mazuri huku wakitembea na kucheza kwa furaha kumsindikiza wakipita barabara kadhaa za katikati ya jiji la Dar es Salaam zikiwemo za Azikiwe na Kivukoni hadi Baharini.

  Baada ya kufanyika kwa sherehe hizo pia baada ya miezi miwili kutakuwa na maadhimisho ya mwaka mpya ambao ni Diwali ambapo mwaka ujao wataadhimisha tena sherehe hizo.

  Mungu huyo ambaye pia hujulikana kwa majina zaidi ya 125 na ndiye Mungu mdogo na mwenye daraja kubwa zaidi.Baadhi ya majina hayo ni Ganesh Chaturthi, Vinayaka Chaturthi

  Inaaminika kuwa unapoomba kitu chochote kutoka kwake unafanikiwa. Ambapo mungu huyo ambaye ni mwanaume aliyetengenezwa kwa aina ya udongo maalumu huyeyuka anapowekwa baharini ikiwa na maana ya kwenda kuungana na Mungu wa kike waliokatika mito hiyo.
   Mungu huyo wa mdogo wa kiume mwenye daraja kubwa anayejulikana kwa zaidi ya majina 125 (Ganpati Bappa Morya)  mwenye sura ya tembo akiwa amewekwa juu ya gari maalumu wakipita mitaa kadhaa ya jiji la Dar es Salaam leo mchana akipelekwa Baharini ili kuungana na mungu wa kike waliopo kwenye mito mitatu mikubwa mitakatifu iliyopo nchini India.
   Mungu huyo akiwa amewekwa juu ya paa la gari akiwa katika uangalizi wa heshima.
   Hapa ni furaha tupu ya maadhimisho hayo.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  D3A_5097
  Mkurugenzi M-Net Kanda ya Afrika Magharibi, Wangi Mba-Uzoukwu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka nchi za Afrika waliokusanyika kwenye jukwaa kubwa la kuonesha vitu mbalimbali vinavyoburudisha katika chaneli za DStv na GoTv kupitia MultiChoice hivi karibuni nchini Mauritius.
  D3A_5116
  Mkurugenzi wa M-Net kwa nchi za Afrika Mashariki na SADC, Theo Erasmus akifurahi jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

  Na Modewjiblog, Mauritius
  Moja ya makampuni yanayoongoza katika utoaji wa vipindi vya burudani barani Afrika M-Net imesema kwamba itazindua chaneli maalumu kwa ajiri ya wakazi wa Tanzania itakayojulikana kama maisha Magic Bongo.
  MAISHA MAGIC BONGO itaruka hewani kupitia chaneli 160 ya DStv kuanzia Alhamisi ya Oktoba Mosi mwaka huu na itapatikana katika vifurushi vyote vya Access, Family, Compact, Compact Plus na Premium.

  Imeelezwa kuwa ingawa mambo yametengenezwa mahsusi kwa ajili ya Watanzania mataifa jirani yaAfrika Mashariki ikiwamo Kenya, Uganda, Ethiopia na DRC wanaweza kuona.

  Uamuzi huo wa M-Net umefanyika wakati mchakato unaendelea wa kuboresha zaidi ulaji kwa wateja wake.

  Hata hivyo wamesema kwamba MAISHA MAGIC EAST ambayo kwa sasa inaruka kupitia chaneli 158 itajiimarisha zaidi katika soko la Kenya huku ikiendelea na mara moja kwa wiki kwa ajili ya soko la Uganda ndani ya Luganda.

  0 0

  1.     Viko Mbweni  usalama  wa  taifa, vina  hati miliki, viko  karibu na  barabara  ya  lami na viko  karibu  na  beach,  vipo  Sqm  600 – 1500, bei  ni  kuanzia  milioni 35 mpaka  45.

  2.     Nyumba 3 zinauzwa, zipo Mwananyamala “A”, moja vyumba 12, nyingine vyumba  6 na  nyingine vyumba 4. Zote  zina  leseni  ya  makazi, gari  mpaka mlangoni, umeme  upo. Kila  moja  bei  milioni 65.

  3.     Nyumba yenye geti  la  gari, vyumba 4, kimoja master, umeme, sebule, dining, jiko, stoo, na  hati miliki inauzwa. Ipo Mbagala  Kuu, bei  milioni  65.

  4.     Pia  nyumba  za  milioni 65 – 70  zipo  Mbweni  na  boko.
  Mawasiliano  0784482959.


  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akisaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia kifo cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Kombani kilichotoke Nchini India juzi, wakati Makamu wa Rais alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mikocheni.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akifariji watoto wa Familia ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Marehemu Celina Kombani wakati alipofika nyumbani marehemu Mikocheni     Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akizungumza na Mume wa Marehemu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Kombani, alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mikocheni Dar es salaam leo Sept 27,2015 kwa ajili ya kusaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo na kuifariji familia ya marehemu.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal,  akizungumza na Mume wa Marehemu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Kombani, alipokwenda nyumbani kwa marehemu Mikocheni Dar es salaam leo Sept 27,2015 kwa ajili ya kusaini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo na kuifariji familia ya marehemu.

  0 0


  0 0

   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Mgombea Ubunge wa jimbo la Makambako Ndugu Deo Sanga wakiwaiambisha wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Polisi Mwembetogwa mkoani Iringa Jumapili  Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mafinga katika uwanja wa Mafinga mkoani Iringa Jumapili  Septemba 27 kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni. 
   Mmoj wa Waangalizi wa Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu,akifuatilia mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli mjini Makambako jioni ya Jumapili  Septemba 27 mkoani Iringa
  ????????????????????????????????????
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Ndugu Mahmoud Mgimwa akipiga push up mbele ya wakazi wa Mafinga waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni wa kumnadi mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli  ambaye anashuhudia tukio hilo katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vyaWambi  mjini Mafinga mkoani Iringa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi.

  Dk. John Pombe Magufuli amewaambia wakazi hao wasihadaike na maneno ya kisiasa yanayotolewa na vyama vingine kuwa nchi ya Tanzania haijapiga hatua ikiwa chini ya utawala wa CCM wakati maendeleo yanaonekana wazi na nchi inazidi kusonga mbele kwa mambo mengi ikiwemo amani na utulivu wa nchi.
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Chimala,Mbarali mkoani Mbeya alipokuwa akielekea mkoani Iringa kuendelea na kampeni zake.
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akionesha hisia zake mara baada ya kuonana uso kwa uso na Waziri Mkuu Mstaafu na Kada Mkongwe wa chama cha CCM. Samwel Malecela mjini Mbarali kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni
   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu na Kada Mkongwe wa chama cha CCM, Samwel Malecela mjini Mbarali kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni,huku Mjumbe wa kamati kuu ya CCM Ndugu  Bulembo akifuatilia kwa makini
   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Rujewa mjini katika viwanja vya Barafu mjini Rujewa,wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya Jumapili  Septemba 27 kwenye mkutano hadhara wa kampeni.
    Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Rujewa mjini wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya Jumapili  Septemba 27 kwenye mkutano hadhara wa kampeni.

  PICHA NA MICHUZI JR-IRINGA

  PICHA ZAIDI INGIA HAPA

  0 0

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii aliyekuwa Kahama.
  BUZWAGI imeanzisha mkakati wa kukuza na kuboresha hali ya utendaji kazi kwa wafanyakazi wake kwa kuanzisha utaratibu wa kuwakutanisha wafanyakazi wa mgodi huo na familia zao mara moja kwa mwaka katika siku maalumu ya familia ambayo hutoa fursa kwa familia za wafanyakazi wa mgodi huo kuweza kujionea namna ambavyo shughuli za uchimbaji wa madini hufanyika na hivyo kuwa mabalozi wazuri wa kampuni kwa ujumla.

  Mwaka huu wafanyakazi wa kampuni hiyo wamepata fursa ya kukutana na kujionea shughuli mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanyika mgodi hapo. Pamoja na mambo mengine wafanyakazi hao pia walipata fursa ya kutembelea eneo ambapo shughuli za uchimbaji zinafanyika.
  Sherehe hizo zilihudhuliwa na Afisa mkuu wa masuala ya uendeshaji  Michelle Ash, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulur-Graham Crew na meneja mkuu wa masuala ya ufanisi wa kampuni Janet Ruben pamoja na meneja mahusiano na mawasiliano wa Acacia Nector Foya, pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali..
  Eng.Philbert Rweyemamu akifafanua jambo katika moja ya mabanda ya maonyesho kwa baadhi ya maafisa wa uhamiaji walipokuwa wakitembelea mabanda ya maonyesho.
  Eng.Philbert Rweyemamu akifafanua jambo katika moja ya mabanda ya maonyesho.
  Wageni wakijionea namna mradi wa matofali ya gharama nafuu ulivyowanufaisha wenyeji wanaozunguka mgodi wa Buzwagi.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

   Mkurugenzi mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akiangalia bidhaa aliyopokea kutoka kwa Marius Mutashobelwa  mkazi wa Mbeya, ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa na Airtel FURSA walipotembelea ofisi za Airtel jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya kuendeleza biashara zao mwishoni mwa wiki hii.
   Mkurugenzi mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akisalimiana na vijana waliowezeshwa na Airtel Kupitia mradi wake wa Airtel Fursa walipotembelea ofisi za Airtel jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya kuendeleza biashara zao mwishoni mwa wiki hii.
   Mhandisi wa Airtel Gabriel Mshiu akiongea na vijana 13 waliowezeshwa na Airtel kupitia mradi wake wa Airtel FURSA walipotembelea ofisi za Airtel jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya kuendeleza biashara zao mwishoni mwa wiki hii.
    Mkurugenzi mkuu wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akiongea na vijana 13 waliowezeshwa na Airtel kupitia mradi wake wa Airtel FURSA walipotembelea ofisi za Airtel jijini Dar es Salaam na kupata mafunzo ya kuendeleza biashara zao mwishoni mwa wiki hii.Akishuhudia ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano (katikati) and  (kushoto) Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi.
   

  KAMPUNI  ya simu za mikononi ya Airtel kwa kupitia mradi wake wa  Airtel FURSA imewakaribisha vijana wajasiriamali 13 katika Makao makuu yake yaliyopo Morocco na kujifunza uendeshwaji wa shughuli zake na kupatiwa mafunzo zaidi ya kibiashara kwa muda wa siku tatu mwishoni mwa wiki iliyopita.

  Meneja uhusiana na huduma kwa jamii  wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akizungumzia hilo alisema, “Airtel kwa kupitia mradi wake wa Airtel FURSA imeendelea kuwa mstari wa mbele kushirikiana na vijana katika kutatua changamoto wanazozipata katika kujikwamua kiuchumi.

  Alisema, “Tunayofuraha kuwakaribisha vijana wetu 13 tuliowawezesha katika biashara zao nakujikwamuakiuchumi kwa kuwapa nyenzo za kisasa zinazosaidia kukuza biashara zao na kujiongezea mapato.

   Pia ndani ya siku tatu wameweza kupatiwa mafunzo zaidi yatakayo wafanya waweze kuendesha biashara zao kwa njia ya kisasa na kuona ni jinsi gani wanaweza kuboresha biashara zao”
  Pia walifanikiwa kukutana na Meneja wa Airtel Tanzania Bwana. Sunil Colaso na kumuelezea mafanikio waliyopata katokana na kuwezeshwa na Airtel FURSA.

  Bwana Sunil Colaso aliwaasa kutumia nafasi waliopata kujiendeleza katika biashara zao na Airtel iko pamoja na vijana ili kuhakikisha malengo yao yanatimia.

  Iddi Chilumba mwakilishi wa vijana hao alisema, “Airtel FURSA ilinikuta nikiwa na nauwezo wa kubanjua korosho chache kutokana na vifaa duni, ila toka nimewezeshwa kwa mashine za kisasa na usafiri, sasa nabanjua korosho nyingi na kusafirisha kwenye masoko mbalimbali kwa haraka Zaidi. 

  Nawashukuru sana Airtel kwa fursa walionipa na nawahasa vijana wenzangu wajishughulishe kuliko kukaa kijiweni na kujishughulisha na vitendo viovu”.

  “Tunafurahishwa sana na juhudi zinazofanywa na vijana za kujitafutia maendeleo kwa njia zilizo halali na tuko tayari kushirikiana nanyi katika kutatua changamoto mnazozipata kwa kupitia mradi wa Airtel FURSA” alisema bwana Sunil Colaso. 

  0 0

   Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF) Bwana Michael Mhando akizungumza na wafanyabiashara   wa wasamaki katika Soko la  feri  hawapo pichani juu ya vikundi  vya    wajasiliamali wadogo na wakubwa  kujiunga na  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF) Bwana Michael Mhando  akimkabidhi kadi ya uanachama ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF)  Mvuvi wa Samaki wa Soko Kuu la Feri Bwana Mohamed Ally Masoud mwishoni mwa wiki Jijini Dara es Salaam.

  MFUKO  wa Taifa wa Bima ya Afya  NHIF leo umekabidhi bima ya Afya kwa Wavi wadogowadogo (UWAWADA) wa mkoa wa Dar es Salaam,na Kaimu Mkurugenzi  wa mfuko huo,Michael Mhando .

  Mhando amekabidhi Bima hizo leo kwenye soko kuu la kuuzia samaki Jijini Dar es Salaam maarufu ‘soko la feri’ ambapo awali ua kukabidhi bima hizo alisema kuwa anawapongeza wanachama wote wa uwawada waliojikusanya kwa vikundi vya watu kumi na kuhitaji siku ya leo kukabidhiwa Bima zao za NHIF kwa wanachama 10 waliojiunga na mfuko huo.

  Alisema wanachama hao baada ya kukaa na kusikiliza huduma zinazotolewa na shirika hilo, namna ambavyo wamefanikiwa kufikia hatua hiyo ya kukabidhiwa bima zao kupitia mpango wa KIKOA ambao unawalenga hasa wajasiliamali wadogowadogo.

  Aidha alisema kuwa vikundi husika kujiunga na mfuko huo ,hunufaika  na mafao ya matibabu sawa  na wanachama  wanaochangia kupitia mishahara yao ya kila mwezi.

  Mhando alisisitiza kuwa lengo kubwa la mpango wa Mfuko wa Taifa wa Biama ya Afya ni kuyafikia makundi yote ya wajasiliamali wadogo na wakubwa ili kuwajumuisha katika mpango huo.

  ”Lengo letu kubwa la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ni kuyafikia makundi yote ya wajasiliamali wadogo na wakubwa ili kuweza kuwajumuisha katika mpango huu”alisema Mhando.


  0 0

  Na Ally Daud –Maelezo
  Dar es salaam

  MWILI wa marehemu wa aliyekuwa Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais ,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina Ompeshi Kombani (56) umeagwa leo Katika Viwanja vya Karemjee jijini Dar es salaam.


  Waziri  huyo ambae pia alikuwa mgombea ubunge Jimbo la Ulanga Mashariki amefariki dunia Septemba 24, mwaka huu katika hospitali ya Apollo Nchini India kutokana na ugonjwa wa saratani ya kongosho.


  Maelfu ya waombolezaji yakiongozwa  na Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Galib Bilal pamoja na Mke wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere na Mke wa Rais wa Tanzania Mama Salma Kikwete katika hafla fupi ya kuaga mwili wa marehemu kabla ya kusafirisha kuelekea Morogoro kwa ajili ya mazishi .


  Wawakilishi wa mashirika na viongozi mbalimbali wa nchi walihudhuria katika viwanja hivyo wakiwemo mawaziri wa Tanzania Bara na Visiwani wakiongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Makinda ili kutoa heshima za mwisho kwa marehemu.


  Marehemu Kombani anatarajiwa kuzikwa kesho katika shamba lake huko Morogoro baada ya waombolezaji kupata nafasi ya kutoa heshima za mwisho katika viwanja wa Jamhuri mjini humo.


  Aidha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anna Makinda ametoa pole kwa wafiwa na kusisitiza kwamba jamii iendeleze  ya yaliyoachwa na marehemu kwa ajili ya kujenga Taifa letu kwani alikuwa mstari wa mbele katika kupigania kuondoa malipo hewa ya watumishi wa Umma, kufanyakazi kwa bidii na kujawali watu .


  Mbali na hayo Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar Balozi  Seif Ali Iddi amesema wamepokea taarifa hizo kwa mstuko mkubwa kwani hawakutarajia kuachiwa pengo na Celina Kombani.


  Vile vile Mwenyekiti na mwakilishi wa kituo cha kulelea yatima Good Hope Family ya Kigamboni Bw. Omari Rajabu amewaasa viongozi waliobakia kutowasahau kwani wamepoteza mama yao wa dunia ambaye alikuwa mstari wa mbele kuwapigania watu wasiojiweza.


  Marehemu Kombani ameacha mume , watoto watano na wajukuu wanne pia ameacha pengo kubwa katika Serikali ya Jamhuri wa Muungano Wa Tanzania.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,  marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,  marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mama Maria Nyerere,  wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kushiriki kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa  mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,  marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro.
   Spika wa Bunge la Jamhuri, Mama Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma,  marehemu Celina Kombani, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Septemba 28, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Kombani alifariki Agosti 24 huko nchini India na anatarajia kuzikwa kesho mkoani Morogoro. 
  Picha na OMR

older | 1 | .... | 989 | 990 | (Page 991) | 992 | 993 | .... | 3270 | newer