Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

IDARA YA MIPANGO MIJI NA VIJIJI ZANZIBAR YAANDAA MRADI WA KUBORESHA MAENEO MATANO YA WAZI YA MJI WA ZANZIBAR CHINI YA UFADHILI WA SHIRIKA LA SDC LA SWITZERLAND.

$
0
0
 Mkuu wa Ushirikiano wa  Ubalozi wa Switzerland nchini Tanzaania Romana Tedeschi akizungumza na wananchi (hawapo pichani) walioshiriki uzinduzi wa Mradi wa kuboresha maeneo matano ya wazi ya Mji wa Zanzibar kwa kuanzia na  Kiwanja cha Demokrasia Kibandamaiti utakaofadhiliwa na Shirika la SDC la nchi hiyo.
 Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis akizindua  Mradi wa kuboresha maeneo ya wazi ya Mjini  Zanzibar katika hafla iliyofanyika Idara ya Ardhi na Upimaji Forodhani Mjini Zanzibar, (kulia) Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Muhamad Juma.


DKT MAGUFULI ALIVYOITEKA MUSOMA, ASEMA MABADILIKO BORA NDIYO WANAINCHI WANAYOHITAJI NA SIO BORA MABADILIKO

$
0
0
 Baadhi ya Wakazi wa mji wa Musoma waliojitokeza kwa wingi wakimsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa  akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Mkendo,Dkt Magufuli aliwaambia wananchi hao ifikapo oktoba 25 wajitokeze kwa wingi wakampigie kura kwani anataka kuwatumikia Watanzania kwa kuwaletea maendeleo.
   Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Mkendo ambapo aliwaambia wananchi hao ifikapo oktoba 25 wajitokeze kwa wingi wakampigie kura kwani anataka kuwatumikia Watanzania kwa kuwaletea maendeleo. 

 Dkt. Magufuli amewaomba wananchi hao kumpigia kura za ndiyo ili aweze kuingia ikulu na kuwatumikia watanzania kwa ajili ya kuleta mabadiliko bora kwa watanzania na siyo bora mabadiliko.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Mkendo ambapo aliwaambia wananchi hao ifikapo oktoba 25 wajitokeze kwa wingi wakampigie kura kwani anataka kuwatumikia Watanzania kwa kuwaletea maendeleo.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akipiga Drums Ngoma za muziki wakati alipofika Utegi wilaya ya Rorya na kufanya mkutano wa kampeni.


 Sehemu ya nyomi la watu mjini Nyamongo wilayani Tarime
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akishangiliwa na uati wa watu mara baada ya kuwahutubia wakazi hao mji wa Nyamongo,wilayani Tarime.
 Wananchi wa Tarime wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa kampeni za CCM
 Jaji Mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba akizungumza na wananchi wa mjini Tarime wakati alipokuwa akimpigia debe Dr. John Pombe Magufuli. 


WIZARA YA AFYA KWA KUSHIRIKIIANA NA SHIRIKA LA HELPAGE INTERNATIONAL WAMEANDAA MKUTANO WA SIKU MBILI WA KUTATHMINI HUDUMA BORA ZA WAZEE ZANZIBAR KATIKA HOTELI YA OCEAN VIEW.

$
0
0
 Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akifungua Mkutano wa kutathmini huduma za Wazee Zanzibar ulioandaliwa na Wizara yake kwa ufadhili wa Shirika la HelpAge International katika Hoteli ya Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Mkutano huo uliohudhuriwa na Wakuu wa Wilaya za Zanzibar, Madaktari dhamana wa Hospitali kuu za Wilaya, Jumuia ya Wazee  na Taasisi za kiraia baadhi ya maofisa wa Wizara ya Afya.

KAMATI ZA MAAFA MKOANI DODOMA WAFANYA TATHMINI YA MPANGO WA KUJIANDAA NA KUKABILIANA NA MAAFA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa Dodoma, LuteniMstaafu, Chiku Galawa akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano wa kuwasilisha Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa kwa Halmashauri za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa mjini Dodoma,  tarehe 12 Septemba, 2015.
 Mjumbe wa Kamati ya Maafa wilayani Mpwampwa, Shekh, Sabah Seif akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa kujadili Taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Mpango ya Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa kwa Halmashauri za Chamwino, Kondoa na Mpwapwa mjini Dodoma,  tarehe 12 Septemba, 2015.

Taarifa za uongo kuhusu Rambirambi za Msiba wa Mama yake Aslay

$
0
0
Kuna mtu anatumia akaunti feki ya msanii wa Yamoto Band Enock Bella akiomba kutumiwa rambirambi ya msiba wa mama mzazi wa Aslay Isihaka Ambaye amefariki Dunia leo asubuhi.

Mtu huyo anatumia namba 0716281999 na amesajili kwa jina la Aslay Isihaka tunawaomba wadau na mashabiki wa Yamoto Band na Aslay wapuuze tariifa siyo za ukweli na hakuna utaratibu wa kutuma rambirambi katika simu.

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA SHIRIKISHO LA VYUO VIKUU ZANZIBAR

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Shirikisho la  Wasomi wa  Vyuo Vikuu Zanzibar kupitia CCM  Khamis  Ali Ameir alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar kuzungumza na Shirikisho hilo leo.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi  mkutano wa shirikisho la Wasomi wa Vyuo Vikuu vya Zanzibar CCM  uliofanyika leo katika ukumbi wa Mkutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.]
 

BASATA YAONYA LUGHA CHAFU, MAADILI HUSUSAN KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

$
0
0
KATIKA siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi la wasanii kuvunja maadili, kukaidi adhabu na kutumia lugha chafu kwa makusudi katika kazi za Sanaa hususan muziki hali ambayo imezua malalamiko, masikitiko na hofu kwa jamii ambayo ni walaji wa kazi za Sanaa.

Lugha hiyo chafu ambayo inajidhihirisha kwa matusi ya wazi, maneno ya uchochezi, kashfa, kejeli, dharau na udhalilishaji wa kada mbalimbali za kijamii wakiwemo viongozi wa kitaifa inaonesha wazi kulenga katika kuigawa jamii na kufifisha amani, upendo, uzalendo na ustaarabu tuliokuwa nao watanzania.

Ieleweke kwamba kwa mujibu wa misingi ya Sanaa Duniani kote kazi zote za Sanaa zinapaswa ziwe ni zenye kuonya, kuelimisha, kuadabisha, kukosoa, kuburudisha, kuhamasisha na kuchochea maendeleo chanya katika jamii na siyo kuigawa au kuivuruga jamii.

Ndiyo maana msanii anayefanya kazi zake kwa kuzingatia misingi ya Sanaa anatambuliwa kuwa ni kioo cha jamii, kiongozi na pia ni mwalimu wa yale yote yaliyo mema katika jamii inayomzunguka.

Kinyume na misingi hiyo ya Sanaa, baadhi ya Wasanii, studio za kurekodia na kutengenezea muziki, vyombo vya habari vya kielektroniki na mitandao ya kijamii ama kwa kutumiwa au kwa utashi wao binafsi wamekuwa wakijihusisha na Sanaa zenye viashiria vya uchochezi na kuvunja misingi ya weledi katika Sanaa hususan katika kipindi hiki cha kampeni na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.

Aidha, baadhi ya Wasanii wamekuwa wakitumiwa na baadhi ya vyama vya Siasa au wagombea na kujikuta wakitumiwa vibaya na kuvunja misingi ya Sanaa kwa faida za kisiasa. BASATA linapenda kutoa maagizo yafuatayo:
1.    Wasanii wana haki zote za kikatiba na kidemokrasia kushiriki shughuli za Siasa lakini wanawajibika kwa kiwango cha hali ya juu kulinda misingi ya weledi,  maadili, miiko na hadhi yao kama inavyofanyika katika tasnia zingine.

2.    Wasanii wanapaswa kutambua kwamba kuna maisha na Taifa baada ya uchaguzi mkuu. Umoja wa kitaifa na umoja baina ya wasanii wa kada zote za Sanaa ndiyo utakuwa msingi mkuu wa kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya Sekta ya Sanaa na Taifa kwa ujumla pasipo kugawanyika katika misingi ya itikadi za kisiasa

3.    Wasanii wasitumie nafasi na umaarufu wao kuligawa taifa, kukashifu viongozi wa kitaifa, kudharau mamlaka, vyama na makundi mbalimbali katika jamii kwa kile kinachoitwa ushabiki wa kisiasa. Ieleweke kuwa Serikali haitafumbia macho wale wote watakovunja sheria, kanuni na taratibu. Tukumbuke kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria. 

4.    Ijulikane kuwa wasanii kama kundi muhimu katika kipindi cha kampeni za kisiasa ni sawa na watu wengine wanaopewa kazi ili kutimiza lengo lililokusudiwa. Wasanii wasitumiwe kama vyombo tofauti na watu wengine.
BASATA linatoa onyo kali kwa msanii yeyote atakayeendelea kukaidi, kuvunja maadili na kusambaza kwa njia yoyote ile kazi ya Sanaa yenye ukengeufu wa maadili. 

BASATA linawatakia wasanii wote utekelezaji mwema wa maagizo haya lakini kubwa kuliko yote kutambua kwamba tunatakiwa kujenga mshikamano, umoja wa kitaifa na kustawisha amani tuliyonayo ambapo ikitoweka itaathiri ufanisi wa Wasanii na kuirejesha itatugharimu sana.
Sanaa itumike kulinda amani, kujenga upendo, umoja wa kitaifa na mshikamano baina ya makundi mbalimbali ya kijamii.
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI

Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA

DRFA YAZINDUA KOZI YA WIKI MBILI YA MKOCHA WA LESENI C’

$
0
0
CHAMA cha soka mkoa wa Dar es salaam, DRFA kwa kushirikiana na shirikisho la soka nchini TFF,leo imezindua rasmi kozi ya ukocha wa leseni C’ inayotambuliwa na shirikisho la kandanda barani afrika CAF.
Kozi hiyo ya wiki mbili inaendeshwa na mkufunzi, Salum Madadi ambaye ni mkurugenzi wa ufundi wa TFF,ikiwa na jumla ya washiriki 31 wengi wao wakiwemo makocha wa vilabu vya ligi daraja la pili,daraja la kwanza na ligi kuu.
Miongoni mwa washiriki hao ni pamoja na kocha msaidizi wa Simba,Suleiman Matola,katibu mkuu wa zamani wa Simba Muhina Kaduguda,kocha wa Ruvu shooting Tom Olaba,kocha wa makipa wa Yanga Juma Pondamali,nyota wa zamani wa Taifa Stars, Ally Mayai na Peter Tino.
Mgeni rasmi katika ufunguzi wa kozi hiyo ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF,Msafiri Mgoy,ambaye amewapongeza washiriki kwa uamuzi wao wa kutaka kujiongezea maarifa ya ufundishaji wa soka ,kwa kuwa tanzania inakabiliwa na upungufu mkubwa wa makocha ikilinganishwa na mataifa mengine ya Afrika ambayo yamepiga hatua kisoka.
Aidha amesema TFF imeweka mpango maalum wa kutunza kumbukumbu za makocha hao na wengine watakaopatikana,pamoja na kufuatilia kazi zao kwenye vilabu mbalimbali watakavyofundisha ili iwe rahisi kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao.
Naye mwenyekiti wa DRFA,Almasi Kasongo wakati akimkaribisha mgeni rasmi,amesema chama chake kinataraji pia kuendesha kozi za madaktari pamoja na kuendeleza mpango wake wa kuinua soka la vijana,ili taifa liwe na wachezaji wenye uwezo wa kushindana na mataifa mengine.
Kasongo amesema licha ya chama chake kuwa na mikakati ya kuhakikisha soka la mkoa wa Dar es salaam na nchi kwa ujumla linanyanyuka,lakini bado nguvu kumbwa inahitajika kutoka TFF pamoja na wadau wenye mapenzi mema na mpira wa nchi hii.
 
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO YA DRFA,
Omary Katanga,
Mkuu wa habari na mawasiliano DRFA.

WASANII BONGO MOVIE WANOGESHA KAMPENI ZA MGOMBEA MWENZA CCM

$
0
0
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakizungumza na wanaCCM na wananchi katika mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.

Baadhi ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.

Baadhi ya wananchi na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika kampeni za mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Azimia Jimbo la Kibaha Vijijini jana mkoani Pwani.
*Imeandaliwa/www.thehabari.com 

UZINDUZI WA CHEZA KWA MADOIDO WAFANA DAR LIVE!

$
0
0
1.3.
Yamoto Band wakizindua rasmi video yao mpya inayofahamika kwa jina la Cheza kwa Madoido katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala, Zakhem jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
 Wasanii wa Yamoto Band, Enock Bella (wa kwanza kushoto) akifanya yake na Aslay (kulia).
(HABARI/ PICHA: DENIS MTIMA/GPL)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA KUKAGUA NA KUKABIDHI MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA WA CHWAKA, UNGUJA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Chwaka, Unguja, wakati alipofika kutembelea kukagua na kukabidhi Mradi wa Maji safi na salama wa Chwaka, leo Sept 12, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi wa Kijiji cha Chwaka baada ya kutembelea kukagua na kukabidhi mradi ya Maji safi na salama wa Chwaka, leo Sept 12, 2015 Unguja. Picha na OMR
 

LOWASSA ATUA SINGIDA MJINI LEO, APATA MAPOKEZI MAKUBWA

$
0
0
Wananchi wa Mji wa Singida wakiishangilia Chopa ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati ikiwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye wakiwapungua wananchi wa mji wa Singida, mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu akimuonyesha Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, mfano wa funguo wenye ujumbe, aliopewa na wananchi wa Singida, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akionyesha mfano wa funguo kwa umati wa wananchi wa Singida, waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini humo leo Septemba 12, 2015. 
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Peoples, Mjini Singida leo Septemba 12, 2015.

KUONA PICHA ZAIDI

UZINDUZI WA KAMPENI YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SEGEREA

WANAFUNZI 70 WA UHANDISI NA UDAKTARI KUONDOKA NCHINI SEPTEMBA 22, 2015 KWENDA KWA MASOMO NCHINI CHINA

$
0
0
Mkurugenzi wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Abdulmaliki Mollel akitoa maelezo katika semina ya kuwajengea uwezo wazazi na wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya China leo katika ofisi zao zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakilipia tisheti kwa ajili ya sare ya kutambuana wakati wa safari ya kwenda katika vyuo vya China katika semina ya kuwajengea uwezo wazazi na wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya China leo katika ofisi zao zilizopo viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. 
Wanafunzi wakipata maelekekezo mbali mbali kutoka kwa Mkurugenzi wa Global Link Education (GEL) ambao ni Mawakala wa Vyuo Vya Nje ya nchi, Abdulmaliki Mollel katika semina ya kuwajengea uwezo wazazi na wanafunzi wanaokwenda kusoma Vyuo Vikuu vya China.

Solly Mahlangu kuwasha moto Tamasha la Amani

$
0
0
MUIMBAJI nguli wa muziki Afrika, Solly Mahlangu anatarajia kuwasha moto kwenye jukwaa la Tamasha la Amani ambalo litarajia kufanyika Oktoba 4 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama mwimbaji huyo ndiye atakayekoleza maombi ya amani ya Tanzania ambayo inapigiwa chapuo la kulindwa kila kukicha.
 
Msama alisema hivi sasa Kamati yake inaendelea na maandalizi ya kufanikisha tamasha hilo ambalo ni chachu ya amani hasa kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 kwa nafasi za urais, Ubunge na Udiwani.
 
Aidha Msama alisema Kamati yake inaendelea na mawasiliano na waimbaji wa nchi za Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi na Uingereza ambazo ni mojawapo ya nchi ambazo ni kichocheo cha  amani ya Tanzania.
 
“Kwa kuwa tumejipanga kumpigia magoti Mungu ili kuilinda amani yetu, hatuna budi kuwashirikisha pia wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali  sambamba na waimbaji ambao watakaoimba nyimbo ambazo zitachochea amani,” alisema Msama. 
 
Msama alisema tamasha hilo litahudhuriwa na viongozi wa kada ya siasa ambao watakuwa ndio walengwa ambao wanatakiwa kutoa somo kwa vijana ambao wamejikita katika siasa bila ya kuwa na weledi wa siasa.“Tutakuwa na matukio mengi ambayo ni viashiria vya kuombea amani Tanzania ambako pia kutakuwa na tuzo maalum ambazo watakabidhiwa baadhi ya viongozi ambao mchango wao katika jamii,” alisema Msama.

Mwisho      

Raisi Kikwete atunuku Kamisheni kwa maafisa wapya wa Jeshi katika Chuo cha Jeshi Monduli, JWTZ wamzawadia

$
0
0
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili  kutunuku Kamisheni kwa maafisa wapya wa Jeshi katika Chuo cha Jeshi Monduli leo.
 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride muda mfupi kabla ya kutunuku Kamisheni kwa maafisa wapya wa Jeshi katika Chuo cha Jeshi Monduli leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi Afisa mwanafunzi bora Luteni Usu Antony Shija wakati wa sherehe za kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya leo katika chu cha jeshi TMA Monduli leo.


 Amiri Jeshi Mkuu Rasi Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa akimpa zawadi afisa mwanafunzi bora wa kike Luteni Usu Martina James Shija  wakati wa sherehe za kutunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi katika chuo hca jeshi Monduli leo.
  Amiri Jeshi Mkuu Rasi Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi katika chuo hca jeshi Monduli leo.
 Maafisa wapya wa Jeshi wakila kiapo mbele ya Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
  Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akimkabidhi Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya  chuoni hapo, na kitara pamoja na nembo maalum ya jeshi kwa kutambua mchango wake katika kuliboresha na kulifanya la kisasa Jeshi la Wananachi wa Tanzania wakati wa Sherehe za kutunuku l\kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi katika chuo cha jeshi Monduli leo.
  Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akimkabidhi Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya kitara pamoja na nembo maalum ya jeshi kwa kutambua mchango wake katika kuliboresha na kulifanya la kisasa Jeshi la Wananachi wa Tanzania wakati wa Sherehe za kutunuku l\kamisheni kwa maafisa wapya wa jeshi katika chuo cha jeshi Monduli leo.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akimkabidhi Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya picha ya kuchorwa Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
  
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiiangalia picha ya kuchora ya Mkewe Mama Salma Kikwete aliyoipokea kwa niaba yake. Picha zote na Freddy Maro.

DKT MAGUFULI AFANYA MIKUTANO YA KAMPENI WILAYA YA BUSEGA,BARIADI,ITILIMA NA MEATU MKOANI SIMIYU LEO.

$
0
0
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliyenyanyua kofia (katikati) akiwasili katika uwanja wa  CCM mjini Bariadi kwa ajili ya kuwahutubia kwenye mkutano wa kampeni mkoani Simiyu.
 Wananchi wakishangilia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi
 Wananchi wa Nanga wilaya ya Itilima wakishangilia ujio wa Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita kuwasalimia
 Umati wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu jioni ya leo
 Wananchi wakimsiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufui alipokuwa akiwahutubia mjini Meatu jioni ya leo.Dkt Magufuli leo ametembelea wilaya ya Busega,Bariadi,Itilima pamoja na wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dk.Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa Mwanhunzi jioni ya leo mjini Meatu mkoani Simiyu,Dkt Magufuli alisema kuwa atakapokuwa Rais atakuwa karibu na wananchi wanyonge na kuwa yeye anatoka katika familia ya watu maskini na anajua nini maana ya umaskini,Alisema anatoka kwenye familia ya wakulima na wafugaji  hivyo anajua nini ambacho anatakiwa kufanya kuboresha maisha ya makundi hayo mawili na kwenye hilo atahakikisha anaweka mazingiza mazuri ya matumizi bora ya ardhi.

Alisema Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.

"Nitakuwa upande wenu wananchi wanyonge.Serikali yangu ni marufuku watu wa bodaboda kushikwa na polisi.Serikali yangu haitakuwa ya kunyanyasa mama ntile na kudaiwa kodi za hovyo.Hivyo sitakuwa tayari kuona mama ntile wanatozwa kodi.Najua nitaimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali yangu lakini nitawabana wafayabiashara  wakubwa ambapo baadhi yao hawalipi kodi,"alisema Dk.Magufuli.

Aliwataka wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.

Dk.Magafuli aliweka wazi anapenda mabadiliko yenye tija na kwamba Serikali yake itasimamia nidhamu kwa watumishi wa umma ili wafanye kazi ya kuwatumikia waanchi usiku na mchana na ndio maana atawalipa vizuri na kuongeza hapendi watu wavivu kwenye kazi.

 Umati wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu jioni ya leo.

 Wananchi wa Mwanhunzi mjini Meatu wakifuatilia mkutano huo wa hadhara wa kampeni. 


Tahadhari ya upepo mkali na mawimbi makubwa 13-15/09/2015.

KAGERA SUGAR YAIBUKA MSHINDI WA 1-0

$
0
0
Kikosi kazi cha Timu ya Mbeya City fc kikiongwozwa na Gorikipa mahiri Juma Kaseja katika picha waki mwomba Mwenyezi munu kabla ya kuanza Mtanange, ambapo Kagera Sugar iliibuka mshindi kwa kuitundika Mbeya City fc Gori Moja kwa bila (1,0) Dakika ya 41, Mchezaji Poul Ngaiyoma Jezi Nambari 8, Mgongoni kuipatia ushindi Timu ya Kagera Sugar katika Mechi ya Kwanza Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Mtanange ulio chezwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Juma Kaseja Jezi Nambari Moja Mgongoni akiwa makini Lango la Mbeya City katika Mtanange wa Mbeya City fc na Kagera Sugar, ambapo Kagera Sugar iliibuka kidedea kwa Gori moja kwa Sifuli (1,0).
Mashabiki wa Mbeya City fc wakishangilia katika Mtanange uliopigwa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kagera moja huku Mbeya City fc Mama kajabwela Tumbo kamsokota Tumbaku Bilaaa..

KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU BW. FROLENCE TURUKA AITEMBELEA NEC KUONA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 25, 2015

$
0
0
Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Sisti Chriati akimpatia maelezo Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka akimpatia maelekezo juu ya NEC inavyoweza kutunza kumbukumbu za wananchi mapema leo alipoitembelea kuona maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ambapo alishuhudia vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vikiwasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam.
Vifaa mbalimbali vya Uchaguzi vilivyowasili na Kupokelewa katika ofisi ya NEC kitengo cha Daftari Bohari Kuu jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Dk. Sisti Chriati akimuonyesha Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Frolence Turuka moja ya vifaa vilivyowasili kwa ajili ya kusaidia Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, 2015. 

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images