Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 971 | 972 | (Page 973) | 974 | 975 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, (kushoto), na Afisa wa Fedha Mwandamizi wa Mfuko huo, Angel Mukasa, (kulia), na Mfanyakazi mwingine wa Mfuko huo, Omari Bundile, (wapili kushoto), wakigawa mafuta maalum yanayotumiwa na watu wenye ulemavu wa ngozi, pamoja na sare za shule na viatu kwa wanafunzi hawa wenye ulemavu wa ngozi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam leo Septemba 11, 2015. Katika kutekeleza sera ya mfuko ya kusaidia jamii, PPF, imetoa vifaa mbalimbali ikiwemo, sare za snhule, viatu na mafuta hayo maalum, Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Lulu Mengele aliwaambia waandishi wa habari. 
  (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)

   Latifa Musa,(kulia), akitoa shukrani kjwa niaba ya wenzake baada ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam, kupatiwa msaada na Mfuko wa Pensheni wa PPF

   Watoto wenye ulemavu wa ngozi kwenye shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa msaada kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF, shuleni hap oleo Ijumaa Septemba 11, 2015

  Watoto wenye ulemavu wa ngozi, wakiteta jambo, baada ya kupatiwa msaada wa vifaa yakiwemo mafuta maalum yanayotumiwa na watu wenye ulemavu wa ngozi
   Picha ya pamoja ya maafisa wa PPF, Walimu na wanafunzi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0  Director of Sports from Ministry of Information Youth Culture & Sports Mr. Leonard Thadeo

  Representatives from UN Agencies

  Representatives from various Organizations

  Media people

  Distinguished Guests

  Ladies & Gentlemen


  On behalf of Agape Television Network and World Agape Ministries, it is my privilege and pleasure to welcome you all to this special occasion we have today.


  I am honored this morning to stand before you to briefly share about the official launch of our new programs on Agape Television Network.


  Agape Television Network was founded and began broadcasting 14 years ago today on September 2001. It is an Educational and Inspirational Channel in Tanzania.


  Agape Television Network has ever since then impacted our society within Tanzania and across borders throughout all of Africa where it is watched.

  Our heart is truly to serve our society around us. We exist to meet the needs of our people and to be a blessing to our viewers.


  With the Digital migration, ATN is watched within 10 Terrestrial sites, all over Tanzania via DTH platform, in over 42 African countries via AMOS 5 satellite, via Cable TV Networks and reaching to over 400,000 homes.


  Through research and development, along with major requests from our viewers; we have taken the next strategies to launch new programming which will meet the needs and benefit our viewers even further. Our top requests were for football programs, music and local news.

  For our news programs, we have established our network with reporters from various regions who will be able to provide us with ‘breaking news’ and also for the coming election campaign.

  Furthermore, 24 community radio stations in Tanzania are working hand in hand and will be rebroadcasting our news and the football matches.


  Hence I am proud to announce that we are officially launching the following new programs which are:


  English Premier League (EPL)

  UEFA European Champions League

  La Liga

  News

  Top 10 Gospel Music


  I thank you all for coming out today, lets join hands together in bringing economical changes in our country by using this media, Agape Television Network. I encourage you to take the next step uniting together with us in making positive inspirational and educational progress for our society as a whole. God bless you.


  Thank you.  REV. DR. ANNY FERNANDES D.D.


  SEPTEMBER 11, 2015

  0 0

   Baadhi ya nyota wa Bongo Movie wakiwa katika basi lao kwenye msafar wa kampeni za mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli. Wasanii hawa na wengine wengi wa kiume na fani ya muziki wanamunga mkono mgombea wa CCM 


  0 0

  KWAYA tatu za muziki wa Injili Tanzania zinatarajia kuwa mojawapo ya wadau watakaoiombea amani Tanzania kuelekea uchaguzi Mkuu kupitia Tamasha la Amani linalotarajia kufanyika Oktoba 4.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama pamoja na kwaya hizo maombi hayo ya amani yatashirikisha waimbaji wengine wa Tanzania na nje.
  Msama alizitaja kwaya hizo ni pamoja na Kwaya ya Uinjilisti ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam, Kwaya ya Mtakatifu Andrew Anglican ya Dodoma sambamba na kwaya ya Wakorintho wa pili ya Mafinga mkoani Njombe.

  Msama alisema Watanzania wajiandae kupata neno la Mungu lenye lengo la kuombea amani nchi yao kupitia viongozi wa dini na wadau wengine.
  "Suala la amani linatakiwa kuzungumzwa na kila mmoja, hivyo ni wakati wa kuunganisha nguvu pamoja kwa lengo hilo," alisema Msama.

  Msama alisema kamati yake inaendelea na mchakato wa kufanikisha tamasha hilo ambalo litaunganisha nguvu kumfikia Mungu kwa maombi.

  Aidha Msama alisema baada ya kumalizika kwa tamasha hilo jijini Dar es Salaam, Oktoba 6 tamasha hilo litafanyika Morogoro, Oktoba 8 (Iringa), Oktoba 10 (Makambako), Oktoba 11 (Mbeya), Oktoba 13 (Dodoma), Oktoba 14 (Singida), Oktoba 15 (Tabora), Oktoba 16 (Shinyanga) na Oktoba 18 (Mwanza).

  0 0

                                                                                                                                11  SECOND 

  AVENUE           
                                                                                                                                      
  COVENTRY CV3 1HP


  9/9/2015


  TO

  ISSA MICHUZI


  RE: CONGRATULATIONS


  It’s  been  ten  years   now  since  you  left  Helsinki  after meeting  a  Mr  Macha, a Tanzanian  blogger who  sowed   the  seed  that  later  became  an  idea and  this  idea  is  now a nyomi; it’s  now  a  movement, a  media  house... I  later  met  you  that  week  in  London  after  the  Helsinki  process meeting  in  London  and  you  told  me  about  the  idea.

  I  know  it  has  been  an uphill task  to  introduce  a  new  media  product  in a  predominantly  print  world. You kept your cool   and now we are celebrating 10 years.

  Your  media  has  been  a  source  of  information, entertainment and education for  us  especially  in  the  Diaspora. It’s been an inspiration and a Home away platform.

  Happy ten years. Long live Michuzi media group.

  I’m proud to be associated with Michuzi media group.


  Thank you

  Yours respectfully

  Ayoub  Mzee

  DIRECTOR

  NEWDEAL  AFRICA

  LONDON


  TEL +447556130219


  0 0

  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akinadi sera zake kwa umati wa wakazi wa Mji wa Dodoma waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini humo leo Septemba 11, 2015, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Mikutano yake ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Benson Kigaila, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma leo Septemba 11, 2015.

  Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa mji wa Dodoma waliofurika kwa wingi wao kwenye Uwanja wa Barafu mjini humo, kwa ajili ya kusikiliza sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.

  Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu akiwaga cheche zake katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma.

  KUONA PICHA ZAIDI 
  BOFYA HAPA

  0 0
 • 09/11/15--14:12: DIRA YA DUNIA YA BBC, LONDON

 • 0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda akihutubia kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa unahusu masuala ya Lishe na Chakula uliofanyika jijini Arusha.
  Mhe. Pinda akihutubia 
  Mfalme wa Lesotho Mhe. Letsie III ambaye nae alihudhuria mkutano huo  akihutubia wadau mbalimbali na wageni waalikwa walioshiriki katika mkutano huo (hawapo pichani).
  Balozi wa Tanzania anayeiwakilisha nchini Lesotho, Mhe. Radhia Msuya (kulia) akifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikiendelea kutolewa kwenye hafla hiyo ya ufunguzi wa mkutano huo  

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0
  0 0


  0 0

  Kada wa CHADEMA  Bw. Nyakarungu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa chama hicho mara baada ya kukihama chama hicho na kwenda CCM na kuvalishwa sare za CCM.
  Msanii wa Bongo Movie Wema Sepetu akizungumza na Umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni leo.
  Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Mama Samia Suluhu Hassan  (kulia) akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Kisarawe, Seleman Said Jafo (kushoto) na katikati ni mgombea udiwani, Mwishehe Mlao mkoani Pwani,   Mgombea mwenza wa urais tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimtambulisha mgombea ubunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Koka Francis (kulia) katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kibaha Mkoa wa Pwani .
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0  0 0

  Mgombea Ubunge Jimbo la Mbeya kwa tiketi ya CCM Mjini Sambwee Shitambala akishangiliwa na baadhi ya WanaCCM  Kata ya Maanga Jijini Mbeya alipokuwa katika kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini. 
  Meneja kampeni wa Mgombea Ubunge Jimbo la Mbeya Mjini Kupitia Chama Cha Mapinduzi  ndugu Charles Mwakipesile akizungumza jambo katika mkutano wa adhara wa kampeni Ulio fanyika katika Kata ya Maanga Jijini Mbeya.
  Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi Ccm Mh.Sambwee Shitambala akizungumza na Wananchi wa kata ya Maanga Jijini Mbeya, katika mkutano wa adhara wa kampeni ya kumba kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi Ccm.
  WanaCCM  na Wananchi wa Kata ya Maanga wakipunga mikono. 
  Picha Zote na Fadhiri Atick a.k.a Mr.Pengo Mbeya.


  0 0


  Ms. Afua Atta-Mensah is the Director of Litigation and Policy Safety Net Project at Urban Justice Center. She works to resolve affordable housing issues helping both Americans and immigrants to both know their rights and to be able to get justice if required.

  She has been working as an attorney for ten years specializing in housing issues here in New York. At the moment she is running for an unpaid position as a district representative of one of the districts of Harlem and she asks you to vote for her in the coming election. 
  In this interview, Ms. Atta Mensah explains what she does to help tenants get their rights and how she fits in a position she is running for. For those who are interested in knowing more about the housing issues of New York, they may learn a lot from this interview.
  .
  You are welcome to watch this show on Friday September 18th from 4:00 pm to 5:00 pm (New York Time) on the following channels depending on who your service provider is. Total Duration: 60 Minutes. The above video has only 36 minutes of the 60 minutes. To watch the entire 60 minutes of the show please see the details below.  Provider Channel
  Times Warner Cable (TWC) 67 and 1998
  FiOS 36
  RCN 85  To stream online tune to channel 4 @ www.mnn.org/4-culture-channel%20 every friday from 4:00 pm to 5:00 pm (New York Time).  Thank You and Stay Tuned.

  0 0


  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kutoa taarifa kuwa kuanzia leo tarehe 10 Septemba 2015, na katika kipindi chote cha kampeni za uchaguzi mkuu 2015, watu ambao sio wagombea wa udiwani, ubunge, urais, wasemaji rasmi wa vyama au watu wasioteuliwa na vyama vya siasa kama wawakilishi hawataruhusiwa kushiriki katika vipindi vya moja kwa moja (Live Programmes) vinavyohusu shughuli za uchaguzi vitakavyorushwa na vituo vya utangazaji.


  Utaratibu huu unazingatia Kanuni Za Huduma Za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji Wa Uchaguzi Wa Vyama Vya Siasa), 2015, Kanuni ya 4 (f), (h), (i),  5(b), (d), (e) and (f).

  Hatua hii inachukuliwa na Mamlaka ili kuweka utaratibu mzuri wa kufanya kampeni za uchaguzi ziwe za amani na utulivu.


  Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya kituo cha utangazaji kitakacho kwenda kinyume na utaratibu huu..  IMETOLEWA NA:

  Mkurugenzi Mkuu

  MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA


  Tarehe 11/09/2015      


  0 0

  UNAJUA watu wengi hawajawahi kujiuliza maswali kama haya hapa... Kwa nini Mungu aliumba mito? Kwa nini Mungu aliumba Miti? Kwa nini Mungu aliumba chuma? Mungu hakukupa vitu vilivyotimia kwa sababu anajua una asili ya uumbaji ndani yako maana umeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, hivyo basi hakukupa vitu vilivyokamilika ila alikupa vitu ambavyo vitakupelekea kutengeneza vitu vingine ili uendeleze ule uumbaji ambao yeye aliuanzisha ,tunajua kabisa kwamba Mungu ni asili ya uumbaji.

  Nataka nikwambie hivi binadamu kawekewa uwezo wa ajabu sana ndani yake na Mwenyezi Mungu wa kutenda mambo makubwa na ya ajabu ndio maana Mungu hakukupa vitu vilivyokamilika kama magari,nyumba, ndege,umeme,meza, n.k ili aliweka ndani yako uwezo wa kutumia mito ukatengeneza madaraja juu yake na magari yakapiti lakini pia alijua kabisa unao uwezo wa kutumia mito ukatengeneza mitumbwi ikapita, lakini pia alijua unao uwezo wa kutumia maji ukatengeneza umeme na ukautumia huo umeme kwa matumizi mbalimbali kama kwenye viwandani,manyumbani,maofisini na kadhalika.

  Pia Mungu aliumba miti hakuumba meza, wala vitanda ,wala viti,wala mkaa kwa sababu anajua unao uwezo wa kubadili hivi vitu kuwa vitu vingine kwa ajili ya matumizi yako na pia ukaendeleza uumbaji wake.

  Hebu angalia tena fikiri kwa kina Mungu kaumba chuma lakini hakuumba gari ila ndani yako wewe kama mwanadamu aliweka uwezo wa kutengeneza magari kwa kupitia zile chuma. Sasa swali nakuuliza katika vitu vyoote Mungu alivyotupa bure kabisa kuna ardhi,kuna maji, kuna anga,kuna hewa, kuna bahari, kuna maziwa na vingine vingi wewe umetumia kipi kuendeleza uumbaji wa Mungu hii ni changamoto kwangu na kwako.

  Hebu tazama Wright Brothers waliweza kutumia anga kutengeneza ndege, Hivi unajua kwamba katika kikao cha mwisho kilichojumuisha wanasayansi 64 wote walisema kwamba haiwezekani kutengeneza ndege ikapaa hewani? Na je unajua kwamba hao wenyewe tuu ndio walibakia katika kikao kile wakisema kwamba inawezekana? Na je unajua Baba yao aliwaambia wakifa watachomwa moto kwa kuwa na wazo kwamba inawezekana kutengeneza ndege na kuirusha angani? Leo ndege zipo au hazipo?

  Nafurahi hawakumsikiliza yeyote walisimamia wazo lao waliamini inawezekana na kweli mwisho wa siku waliweza Leo hii tunasafiri kwenda sehemu mbalimbali duniani pasipo shida ya aina yoyote kwa sababu ya Wright Brothers, ushawahi kujiuliza kama kungekuwa hakuna ndege watu wakasafiri kwa mabasi au meli ingekuchukua mda gani kutoka hapa Tanzania kufika Marekani au Brazil au Canada au Wingereza? Bila shaka ungesafiri hata miezi miwili mitatu na bado usingefika. Mungu awapumzishe pepa peponi asante Mungu kwa kuwaumba.

  Nakuja kwako wewe je una mipango mingapi umeiacha kisa watu wamekuambia haiwezekani? usiwasikilize nakwambia maana watu wengi wameshindwa kutimiza ndoto zao kwa kusikiliza watu hata kama ni mzazi wako, hata kama ni rafiki,hata kama ni ndugu ivi kweli jaribu kutafakari haya maneno kwa kina kama tungefanya kama wazazi wetu walivyofanya mabadiliko yangekaa yatokee? 

  Wright Brothers wangemsikiliza baba yao leo tungekuwa na ndege?anza kushughulikia mpango wako maadamu unauona katika fikra zako ina maana unaweza kuutimiliza mimi nakuhakikishia hakuna kitu kitakachoweza kukuzuia kupata kile unachokitaka labda tuu uamue kujizuia mwenyewe ila kama kweli umenuia kukitafuta kwa moyo wako wote na ukafuata taratibu zote za kukitafuta utakipata tuu na sina wasiwasi katika kusema hivi.

  Naomba nimalizie kwa kusema hivi kitu pekee kitakachokuzuia kupata kile unachokitaka ni wewe mwenyewe na kingine ni kuruhusu maoni ya watu wengine kutawala mawazo yako kwamba huwezi ukafanikiwa katika hilo unalotaka kufanya.
   IMEANDALIWA NA HUMPHREY MAKUNDI NA ALLARD MINJA.

  0 0

  LEO ASUBUHI, MWANDISHI AMBAYE PIA NI MPIGAPICHA WA MAGAZETI YA UHURU, MZALENDO NA BURUDANI YANAYOCHAPISHWA NA KAMPUNI YA UHURU PUBLICATIONS, CHRISTOPHER LISSA, ALIPATA TAARIFA ZA MAANDAMANO YA WALIOTAJWA KUWA WAFUASI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) WALIOKUWA WAMEKUSUDIA KUANDAMANA KWENDA MAKAO MAKUU YA CHAMA CHAO.


  LISSA ALIMFAHAMISHA MHARIRI WAKE JUU YA TAARIFA HIZO, AMBAPO MHARIRI ALIMTAKA KUFUATILIA TUKIO HILO.


  MWANDISHI HUYO ALIONDOKA OFISINI SAA 2:50 ASUBUHI MPAKA KINONDONI ENEO  AMBAKO WAANDAMANAJI WALIKUWA WAMEPANGA KUANZIA MAANDAMANO YAO.

  WAANDAMANAJI WALICHELEWA KUFIKA ENEO TAJWA NA ILIPOTIMU SAA 5.00

  NDIPO WALIFIKA WAKIWA KWENYE BASI NA KUSHUKA KUANZA MAANDALIZI YA MAANDAMANO HUSIKA.


  WAANDAMANIJI HAO WALIANZA MAANDAAMO MUDA MFUPI BAADAYE KUELEKEA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA CHADEMA ZILIZOPO MTAA WA UFIPA, KINONDONI.


  HUKU WAKIWA NA MABANGO YALIYOKUWA NA UJUMBE TOFAUTI AMBAPO MWINGI ULIKUWA UKIKEMEA KITENDO CHA MGOMBEA URAIS WA CHADEMA, EDWARD LOWASSA, KUTUMIA UDINI KUOMBA KURA KANISANI. ITAKUMBUKWA KWAMBA LOWASSA ALIOMBA KURA HIVI KARIBUNI ALIPOKUWA MJINI TABORA, AMBAPO ALIFANYA HIVYO KATIKA KANISA LA KILUTHERI.


  BAADA YA KUNDI HILO LA WAANDAMANAJI KUFIKA, LILIKWENDA MOJA KWA MOJA HADI KATIKA MLANGO WA KUINGIA KWENYE OFISI ZA CHAMA HICHO, AMBAPO MWANDISHI WETU ALIANZA KUTEKELEZA JUKUMU LAKE AKIWA NA WAANDISHI WENGINE.


  HATA HIVYO KATIKA HALI YA KUSHANGAZA LISSA PAMOJA NA WAANDISHI WENZAKE WA HABARI, WALIKAMATWA NA WALINZI WA CHAMA HICHO, AMBAPO WENZAKE WALIACHIWA BAADA YA KUJITAMBULISHA KUWA WANATOKA VYOMBO VYA HABARI.  LAKINI CHA KUSHANGAZA LISSA ALIPOJITAMBUSHA KUWA ANATOKA GAZETI LA UHURU NDIPO WALIPOSEMA KWAMBA ‘HUYU NDIYE TULIYEKUWA TUNAMTAFUTA’ NA KUANZA KUMPIGA KWA NGUMI MAGONGO NA VYUMA NA KUMSABABISHIA MAJERAHA NA KUHARIBU KAMERA, HUKU WAKIMPORA SIMU YAKE YA MKONONI NA ‘WALLET’ ILIYOKUWA NA JUMLA YA SH. 80,000.


  AIDHA ALIPOKUWA AKIPIGWA WAHUSIKA WALISIKIKA WAKISEMA TUWASUBIRI WAKUBWA NA MUDA MFUPI BAADAYE ALIINGIA MSEMAJI WA CHAMA HICHO, BONIFASCE MAKENE, DIWANI WA UBUNGO CHADEMA,  AMBAYE PIA ANATUHUMIWA KUMSHAMBULIA MLINZI WA  DK. WILLIBROD SLAA,  MUDA HUO HUO PIA ALIPITA  MHE. JOHN MNYIKA ALIYEKUWA NA KIKAO NA WAANDISHI WA HABARI.


  KWA MUJIBU WA MWANDISHI LISSA ALIYEELEKEZA NA KUMUINGIZA KWENYE CHUMBA CHA MATESO NI DIWANI HUYO WA UBUNGO AKIWA PAMOJA NA WALINZI WENGINE AMBAO WALIKUWA WAKIMPIGA.


  AKIWA KATIKA CHUMBA HICHO ALIENDELEA KUPIGWA NA BAADAYE ALIPEWA KADI ZA CHADEMA NA KUANZA KUSHURUTISHWA KUSHIKA HIZO KADI NA ATAMKE MBELE YA KAMERA YA VIDEO ILIYOKUWA IKIMREKODI KWAMBA YEYE AMETUMWA NA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), ABDULRAHMAN KINANA NA VIONGOZI WA CCM KUANDAA MAANDAMANO HAYO, AMBAPO PAMOJA NA KUSHURUTISHWA HUKO ALIKATAA NA KUSHIKILIA MSIMAMO WAKE KWAMBA ALIKUWA AKITETEJELEZA MAJUKUMU YAKE YA UANDISHI WA HABARI NA SI VINGINEVYO.


  WAKIWA WANAAENDELEA KUMSHURUTISHA GHAFLA WALIINGIA POLISI NA WATEKAJI WALISTUKA NA KUMWELEZA ASISEME KWAMBA ALIKAMATWA NA YUKO NDANI, HIVYO WALIMTOA NA KUTOKA NAYE NJE PAMOJA NA WATU WENGINE HUKU AKILINDWA NA WALINZI WA CHADEMA.


  POLISI WALIPOFIKA NA KUOMBA KUFANYA UPEKUZI KUTOKANA NA TAARIFA ZA KUWEPO MWANDISHI WA UHURU, ANAYESHIKILIWA NDANI YA OFISI, WALIRUHUSIWA KUFANYA HIVYO HUKU LISA AKIWA NJE NA WALINZI WA CHADEMA WALIOMTAKA KUTOJITAMBULISHA AU KUSEMA CHOCHOTE WAKATI POLISI WAKIWEPO ENEO HILO.


  BAADA YA POLISI KUONDOKA WALISIKIA WAKISEMA KWAMBA ‘DILI’ YETU HAIJAFANIKIWA NA KUINGIA NAYE NDANI TENA NA KUMWELEZA MNYIKA ALIYEKUWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KWAMBA WAMEMKAMATA MWANDISHI WA UHURU AMBAYE NI MUANDAAJI WA MAANDANAMO HAYO.


  BAADA YA KUPATA TAARIFA HIYO, MNYIKA ALIWAAMBIA WAANDISHI WA HABARI WAKATI HUO LISA AMBAYE ALIOKUWA AMESHIKISHWA KADI NYINGI ZA CHADEMA , ALISHURUTISHWA KUSEMA KWAMBA NDIYE ALIYEANDAA MAANAMANO HAYO NA KWAMBA ASIPOSEMA HIVYO HATATOKA MZIMA.


  PAMOJA NA VITISHO HIVYO, LISSA ALIKATAA NA KUSHIKILIA MSIMANO WAKE KWAMBA ALIFIKA ENEO HILO KUFANYA KAZI YAKE YA UANDISHI WA HABARI NA SI VINGINEVYO. BAADHI YA WAANDISDHI WALISIKIKA WAKISEMA KWANINI MWENZAO ALIKUWA AKISHURUTISHWA KUSEMA MANENO HAYO.


  WALINZI HAO WAONEKANA KUKIRI KWAMBA ZOEZI LAO LIMESHINDIKANA NA WENGINE WALITAKA APIGE NA HADI KUFA ILI KUPOTEZA USHAHIDI, LAKINI WENGINE WALIGOMA WAKISEMA HAPO NI MAKAO MAKUU YA CHAMA.


  BAADA YA KUTOFAUTIANA WENYEWE KWA WENYWE WALIMRUHUSU LISSA AONDOKE NA NDIPO ALIPOONDOKA NA GARI LILILOKUWA NA WAANDISHI WA HABARI WA AZAM MOJA KWA MOJA KWENDA KITUO CHA POLISI, OYSTERBAY AMBAKO ALITOA MAELEZO YAKE.


  TUNASIKITIKA KWAMBA CHADEMA WAMEAMUA KUFANYA SIASA CHAFU ZINAZOTUHUSISHA KATIKA HARAKATI ZAO AMBAZO ZIMESHINDWA KUFANIKISHA KUWASHAWISHI WATANZANIA ILI WAWACHAGUE.


  AIDHA, TUNALAANI VIKALI KITENDO HICHO KILICHOFANYWA NA KUNDI LA MAOFISA NA WALINZI WA CHAMA HICHO, KUINGILIA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI. CHADEMA WAMEFANYA UNYAMA HUO DHIDI YA MWANDISHI WETU, LAKINI CHAMA CHA MAPINDUZI HAKIJAWAHI KUFANYA HIVYO. HIVYO TUKIO HILI LIMEONYESHA PICHA HALISI CHA CHAMA HICHO AMBACHO KINALILIA KUWAONGOZA WATANZANIA.


  WAKATI TUNALAANI UNYAMA HUO, TUNAAMINI VYOMBO VYA HABARI VITAKEMEA TUKIO HILI, LAKINI PIA TUNAAMINI HATUA STAHIKI ZA VYOMBO VYA DOLA IKIWEMO POLISI VITACHUKUA HATUA DHIDI YA WALIOHUSIKA NA UNYAMA HUO.


  DAIMA CCM IMEKUWA IKIENDESHA KAMPENI ZA KISTAARABU KATIKA KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI MKUU TOFAUTI NA CHADEMA. UONGOZI WA UPL UNATOA POLE KWA LISSA NA KUMTAKIA MATIBABU MEMA.

  RAMADHANI MKOMA,

  KAIMU MHARIRI MTENDAJI,

  UHURU PUBLICATIONS LIMITED


  0 0

   Mufti Mkuu mpya wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi bin Ally  akiongea na mamia ya Waislamu waliojitokeza kumkaribisha rasmi makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu la Tanzania (BAKWATA) Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam Ijumaa jioni.
    Rais Mstafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza wakati wa hafla ya kumkaribisha rasmi Mufti Mkuu mpya wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi bin Ally   makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu la Tanzania (BAKWATA) Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam Ijumaa jioni.
   Sehemu ya mamia ya waislamu wakati wa hafla ya kumkaribisha rasmi Mufti Mkuu mpya wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi  bin Ally   makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu la Tanzania (BAKWATA) Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam Ijumaa jioni.
  Mamia ya Waislamu katika  wa hafla ya kumkaribisha rasmi Mufti Mkuu mpya wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuberi  bin Ally   makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu la Tanzania (BAKWATA) Kinondoni Muslim jijini Dar es salaam Ijumaa jioni.

  0 0

   Mkurugenzi wa Taasisi ya Natural Resource Forum (TNRF), Joseph Olila, akizungumza na wanahabari wakati akitoa taarifa chokozi katika uzinduzi wa mfululizo wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini uliofanyika Hoteli ya New Africa Dar es Salaam leo asubuhi.
  Mshauri wa Ufundi Weizara ya Maliasili na Utalii, Thomas Sellaine (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
   Balozi wa Mama Misitu, Asha Salimu (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo.
  Na Mwandishi wetu.
   MFULULIZO wa vipindi vipya vya runinga kuhusu uzalishaji endelevu wa mkaa vitarushwa hewani kupitia televisheni mbalimbali nchini. Kampeni ya Mama Misitu (MMC), inazindua mfululizo wa vipindi vya kuelimisha jamii kuhusu uzalishaji na faida za mkaa endelevu kijamii, kimazingira na kiuchumi.


  Vipindi hivyo mfululizo vimetengenezwa katika wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya jitihada za pamoja kati ya Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA), Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG), Shirika la Kuendeleza Teknolojia  za Asili (TATEDO) na Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ili kuleta mabadiliko na kurasimisha sekta ya mkaa iweze kutoa ajira endelevu na kipato kwa jamii za vijijini na mijini.


  Inakadiriwa kuwa mkaa na biashara za kuni huzalisha takriban (dola bilioni 1) za mapato kwa zaidi ya wazalishaji, wasafirishaji na wafanyabiashara laki tatu (300,000) katika mwaka 2012. Mahitaji ya mkaa nchini Tanzania yameongezeka kwa kasi na kwa kiasi kikubwa. 

  Kusoma zaidi bofya HAPA


  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
  JESHI LA POLISI TANZANIA

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  JESHI LA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAAM LAHIMIZA AMANI NA MSHIKAMANO KATIKA MCHAKATO WA UCHAGUZI MKUU WA 25.10.2015
          Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam Suleiman Kova amewakumbusha watanzania hususani wananchi wanaoishi jijini Dar es Salaam kukumbuka wajibu wao wa kudumisha amani wakati wote wa mchakato wa uchaguzi mkuu.

  mchakato huo ni pamoja na wakati wa kampeni, siku ya kupiga kura tarehe 25.10.2015 na baada ya kutangazwa kwa matokeo  mablimbali katika ngazi za udiwani, ubunge na urais.

  Kamishna ameyasema hayo katika uwanja wa mpira wa karume jijini dsm alipoenda kukaguwa mazoezi ya pamoja yanayowashirikisha viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo Masheikh, Maaskofu, mapadre wachungaji na mabalozi wa nchi mbalimbali.

  Mabalozi na wawakilishi wa Nchi zao walioshiriki mazoezi hayo ni pamoja na Ujerumani, Uholanzi, Urusi, na Denmark ambao Kamishna aliwashukuru kwa ushiriki wao ulilenga kudumisha amani ya Tanzania.

  Aidha watanzania wamekumbushwa kuwa wavumilivu katika kipindi hiki  kuelekea uchaguzi mkuu  kwani muda huu ni mfupi sana ukilinganisha  na muda mrefu  ambapo Tanzania imekuwa na amani. Wanatakiwa washirikiane bila kujali itikadi zao au tofauti zozote zile kwa madhumini ya kudumisha amani iliyopo.

  Jeshi la Polisi limejiandaa kikamilifu katika kulinda amani na usalama wa Nchi na kutoa onyo kwa wale watu wachache watakaovuruga amani na usalama kwani wakibainika watashughulikiwa kikamilifu kwa mujibu wa sheria.

  Katika zoezi hilo hapo uwanja wa karume Kamishna Kova alikabidhi mipira mitano kwa Mwenyekiti wa timu ya Amani na mshikamano Sheikh Alhad Mussa Salum ambaye pia ni Sheilk wa Mkoa wa Dar es Salaam akisaidiwa na Mchungaji FUPE -Makamu Mwenyekiti, na Katibu wa timu PADRE JOHN SOLOMONI ili kuwapa hamasa katika kazi yao ya pamoja iliyo nzuri na muhimu kwa taifa hili. Aidha Kamishna alipata fursa ya kupuliza filimbi katikati ya uwanja ikiashiria kuanzisha mazoezi kwa madhumuni ya kuhamasisha amani na mshikamano.

  Kamishna Kova amewambia watanzania kupitia shughuli hiyo kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu "kipaumbele cha kwanza ni  amani cha pili ni amani na cha tatu ni amani"

  SULEIMAN H. KOVA
  KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
  DAR ES SALAAM


older | 1 | .... | 971 | 972 | (Page 973) | 974 | 975 | .... | 3272 | newer