Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

NAWASHANGAA MAWAZIRI WAKUU WENZANGU WALIOSTAAFU,WAKIDAI CCM MIAKA 50 HAKUNA KILICHOFANYIKA-JAJI WARIOBA

$
0
0
 Waziri Mkuu Mstafu Jaji Joseph Sinde Warioba akihutubia wakazi wa Butiama ambapo aliwaeleza Magufuli anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

WAZIRI Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, ameibuka katika kampeni za mgombea urais wa CCM Dk. John Magufuli na kusema kuwa anashangazwa na hatua ya mawaziri wakuu wenzake kuhama CCM na kudai hakuna kilichofanyika katika miaka 54 ya Uhuru.

Pamoja na hali hiyo amesema anajua wazi huenda hata wanachokifanya hawajui wajibu wao walipokuwa katika madaraka hayo kama washauri wakuu wa rais.alisema  sasa umefika wakati wa watu wanaomtumia kama dira Baba wa Taifa katika kampeni zao wajitafakari zaidi.

"Wengine katika kampeni zao wanatumia maneno ya Mwalimu kama wamechanganyikiwa. Huwezi kumtumia Mwalimu kama dira halafu unasema CCM haijafanya kitu, aliijenga Tanzania kwenye misingi na wote walimfuata wanapita kwenye misingi yake," alisema Jaji Warioba



 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika mjini Bunda leo.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akipokea kifimbo na Chief Japhet Wanzagi kwa niaba ya Wazee wa Butiama.
 Dkt akionesha fimbo hiyo aliyokabidhiwa na Chief wa Wazanaki,Japhet Wanzagi. 
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge kulia ni Nimrod Mkono kutoka jimbo la Butiama Vijijini na  Profesa Sospeter Muhongo ambaye anatoka jimbo la Musoma vijijini.

 Mamia ya Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli.

 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Nyamuswa ambako ndiko alikozaliwa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba,wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Nyamuswa ambako ndiko alikozaliwa Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba,wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli. 



MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA KUKAGUA MAENDELEO YA MRADI YA MAJI KATA YA KIGUNDA WILAYA YA KASKAZINI A UNGUJA.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka kukagua  moja kati ya Visima vinne vya Maji safi na salama wakati alipofika katika Kijiji cha Kigunda Wilaya ya Kaskazini A Unguja kwa ajili ya kukagua mradi huo wa maji, leo Sept 10, 2015. Mradi huo unaosimamiwa na Kijiji hicho umegharamiwa na Mhe. Makamu wa Rais kutokana na maombi ya wananchi hao waliokosa maji kwa miaka mingi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kigunda, baada ya kukagua mradi wa Maji safi na salama katika Kijiji cha Kigunda Wilaya ya Kaskazini A Unguja kwa, leo Sept 10, 2015. Mradi huo unaosimamiwa na Kijiji hicho umegharamiwa na Mhe. Makamu wa Rais kutokana na maombi ya wananchi hao waliokosa maji kwa miaka mingi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Msingi wa Msikiti wa Shule ya Msingi Kigunda, baada ya kukagua mradi wa Maji safi na salama  unaosimamiwa na Kijiji hicho ambao umegharamiwa na Mhe. Makamu wa Rais kutokana na maombi ya wananchi hao waliokosa maji kwa miaka mingi. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Makame Madina.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Bwereu, Juma Nyange Omari, wakati alipofika kukagua moja kati ya Visima vinne vya Maji safi na salama wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi huo katika Vijiji vya Kigunda na Bwereu Wilaya ya Kaskazini A Unguja, leo Sept 10, 2015. Mradi huo unaosimamiwa na Kijiji hicho umegharamiwa na Mhe. Makamu wa Rais kutokana na maombi ya wananchi hao waliokosa maji kwa miaka mingi. Picha na OMR

 

SIMU TV: HABARI ZA USIKU WA LEO

NAWASHANGAA MAWAZIRI WAKUU WENZANGU WALIOSTAAFU,WAKIDAI CCM MIAKA 50 HAKUNA KILICHOFANYA-JAJI WARIOBA

$
0
0
 Waziri Mkuu Mstafu Jaji Joseph Sinde Warioba akihutubia wakazi wa Butiama ambapo aliwaeleza Magufuli anafaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MARA

WAZIRI Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, ameibuka katika kampeni za mgombea urais wa CCM Dk. John Magufuli na kusema kuwa anashangazwa na hatua ya mawaziri wakuu wenzake kuhama CCM na kudai hakuna kilichofanyika katika miaka 54 ya Uhuru.

Pamoja na hali hiyo amesema anajua wazi huenda hata wanachokifanya hawajui wajibu wao walipokuwa katika madaraka hayo kama washauri wakuu wa rais.alisema  sasa umefika wakati wa watu wanaomtumia kama dira Baba wa Taifa katika kampeni zao wajitafakari zaidi.

"Wengine katika kampeni zao wanatumia maneno ya Mwalimu kama wamechanganyikiwa. Huwezi kumtumia Mwalimu kama dira halafu unasema CCM haijafanya kitu, aliijenga Tanzania kwenye misingi na wote walimfuata wanapita kwenye misingi yake," alisema Jaji Warioba
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika mjini Bunda leo.
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akipokea kifimbo na Chief Japhet Wanzagi kwa niaba ya Wazee wa Butiama.
 Dkt akionesha fimbo hiyo aliyokabidhiwa na Chief wa Wazanaki,Japhet Wanzagi
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge kulia ni Nimrod Mkono kutoka jimbo la Butiama Vijijini na  Profesa Sospeter Muhongo ambaye anatoka jimbo la Musoma vijijini.

 Mamia ya Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

RAIS KIKWETE APOKEA TUZO YA UTAWALA BORA

$
0
0
 Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Asha Rose Migiro akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Tuzo maalum ya “Africa Achiever’s Award in The Category of Good governance in Africa,” wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo.Dkt.Migiro alimwakilisha Rais Kikwete katika hafla ya kutunukiwa Tuzo hiyo huko Afrika ya Kusini hivi karibuni.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba fupi baada ya kupokea TuAfrica Achiever’s Award in the Category of Good Governance in Africa,” kutoka kwa Waziri wa katiba na Sheria Dkt.Asha Rose Migiro aliyeipokea kwa niaba ya Rais huko Afrika ya Kusini.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Asha Rose Migiro aliyekabidhi Tuzo kwa Rais(Watatu kushoto),Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Wapili kushoto), Wamasheria Mkuu wa Serikali Mh.George Masaju(wapili kulia), Mwenyekiti wa Tume ya Haki Za Binadamu Mhe.Tom Nyanduga(kulia) na Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mh.Suzan Mlawi(kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya Dkt.Migiro Kumkabidhi Rais Kikwete Tuzo ya “ Africa Achiever’s Award in the Category of Good Governance in Africa” ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)

MFUMO WA KIMTANDAO UNAOWEZESHA KUPOKEA NA KUHAMISHA MIAMALA YA KIFEDHA KUTOKA BENKI MOJA KWENDA NYINGINE UNAORATIBIWA NA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT)

$
0
0
 MFUMO WA KIMTANDAO UNAOWEZESHA KUPOKEA NA KUHAMISHA MIAMALA YA KIFEDHA KUTOKA BENKI MOJA KWENDA NYINGINE UNAORATIBIWA NA BENKI KUU YA TANZANIA (BOT)  YAANI ‘TANZANIA INTER-BANK SETTLEMENT SYSTEM’ (TISS) WAONGEZA UFANISI KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM
 Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga, akibadilishana mawazo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. Gabriel Migire, leo asubuhi kabla Kaimu Katibu Mkuu hajaongea na waandishi wa habari pamoja na wadau kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwa kuongeza muda malipo ya kibenki kupitia mfumo wa TISS.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. Gabriel Migire (wa tatu kutoka kushoto), akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) na wadau mbalimbali, kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwa kuongeza muda malipo ya kibenki kupitia mfumo wa TISS.
 Wadau mbalimbali wa Bandari ya Dar es Salaam na waandishi wa habari wakimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw Gabriel Migire (hayupo pichani) wakati akielezamafanikio yaliyopatikana kwa kuongeza muda malipo ya kibenki kupitia mfumo wa TISS, leo asubuhi katika ofisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA).

 (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

PALESTINA KUPEPESHA BENDERA YAKE MAKAO MAKUU YA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0

   Bendera ya  Palestine itapepea nje ya Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,   hii inafuatia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  kupitisha azimio ambalo linatoa fursa kwa nchi ambazo si  mwanachama kamili wa Umoja huo  kupeperusha bendera yake Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Ubao wa Matangazo ndani ya Ukumbi Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,  ukionyesha matokeo ya kura katika tukio la kihistoria  kufanyika ambapo Baraza hilo  limepitisha azimio linalotoa fursa kwa Palestina kupeperusha bendera yake. Nchi wanachama walipiga makofi kushangilia kupitishwa kwa azimio hilo, ambalo Israel imesema Palestina inatafuta umaarufu kwa njia za mkato badala  ya kurejea kwenye meza ya mazugumzo.
 
Na Mwandishi Maalum New York
BARAZAKuu la Umoja wa Mataifa,  jana Alhamis, limepitisha Azimio ambalo kwa mara ya kwanza   tangu kuanzishwa kwa Umoja huo, litaruhusu nchi ambazo  siyo  mwanachama kamili kupeperusha  bendera yake katika  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Kupitishwa kwa azimio hilo ambalo  limepigiwa kura  za ndiyo 119 za hapana  nane  na zisizofungamana na upande wowote 45 kunaipa   fursa Palestina kupeperusha  bendera yake nje ya Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.

Mara baada ya  matokeo ya kura kutangazwa rasmi, Wajumbe wa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa  Mataifa walipiga makofi kama ishara ya kufurahia kupitishwa kura nyingi azimio hilo.

TANGAZO LA KIFO ROSE RAYMOND SHOGHOLO

$
0
0
FAMILIA YA CHALLY SHOGHOLO WA SINZA (BABA MDOGO), DAR ES SALAAM WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO NDUGU YAO ROSE RAYMOND SHOGHOLO (PICHANI) KILICHOTOKEA JUZI SEPT 9, 2015 KATIKA HOSPITAL YA MAMA NGOMA MWENGE-KWA PROFFESOR NGOMA
MAZISHI YAMEPANGWA KUFANYIKA KESHO JUMAMOSI, WILAYA YA SAME KIJIJI CHA KISIWANI
FAMILIA INATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA PROFFESOR NGOMA  NA WAUGUZI WA HOSPITAL YA MAMA NGOMA MWENGE, KWA MOYO WAO NA UPENDO WALIOTUONYESHA KIPINDI CHA KUMUUGUZA NDUGU YETU
HABARI ZIWAFIKIE NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI POPOTE PALE WALIPO. LEO SAA 3 TUNAMUAGA NDUGU YETU ROSE,  SINZA SAA 3 ASUBUHI NYUMBANI KWA BABA MDOGO CHALLY SHOGHOLO SINZA.
BWANA AMETOA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE!!


MABALOZI MBALIMBALI WAZUNGUMZA KUHUSU MAJUKUMU YAO KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.), akizungumza na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, kuhusu nafasi na majukumu yao katika uchaguzi mkuu ujao, pamoja na jinsi Serikali ilivyojipanga kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani, huru na haki kwa vyama vyote.
Waheshimiwa Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini,wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb), wakati wa mkutano huo uliofanyika leo 10-09-2015 katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIC) jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja.
PICHA NA REUBEN MCHOME.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.
 

TANGAZO LA SHUKRANI

$
0
0
Familia ya Bwana na Bibi Charles Yanga wa Tabata Chang'ombe, Dar es salaam, wanapenda kutoa shukurani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walioshirikiana nao katika mazishi ya mtoto wao mpendwa Abel Charles Yanga aliyefariki tarehe 22 July 2015 na kuzikwa tarehe 25 July 2015 katika makaburi ya Kinondoni, Dar es salaam. Familia inakukaribisha kwenye Misa ya shukurani Jumamosi tarehe 12 Sep. 2015 saa  5.00 asubuhi nyumbani Tabata Chang'ombe. Baada ya Misa tutashirikiana chakula cha mchana. Karibuni sana.
Kwa mawasiliano zaidi simu namba
0653 013 211

UNESCO WAKABIDHI KITABU CHA MAFUNZO YA TEHAMA KWA SERIKALI NCHINI

$
0
0
IMG_8554
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kulia) akitoa neno la ukaribisho kwa wadau wa sekta ya elimu wakati wa hafla ya kukabidhi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Katikati ni mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa aliyemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome. Kushoto ni Ofisa wa Ubalozi wa China, LIU Yun.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_8766
Mgeni rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya Elimu nchini mara baada kupokea kitabu cha mwongozo wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu na walimu kilichoandaliwa na mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wakati hafla ya makabidhiano ya kitabu hicho kilichokabidhiwa kwa Kamishna wa Elimu nchini katika hoteli ya Protea Courtyard Hotel jijini Dar es Salaam.

MAFANIKIO SIYO AJALI SEHEMU YA KWANZA.

$
0
0
WATU wengi wanafikiri mafanikio ni kitu ambacho kinatokea tuu kama ajali lakini mafanikio sio ajali wala sio bahati mafanikio ni mipango dhahiri ambayo inapangwa na mtu anayeyataka na ayenuia kutoka katika vilindi vya moyoni mwake kwamba anataka kutoka katika sehemu moja kwenye maisha ambayo inakuwa ni duni na kwenda sehemu nyingine ambayo ni ya hadhi nzuri.

Wengi wamekuwa wakijidanganya kwamba ipo siku moja watafanikiwa (watatoboa)lakini hawana mpango wowote wa kuwawezesha kufanikiwa katika iyo siku moja na nataka niwaambie kwamba iyo siku moja haitakaa itokee kama hauna mpango dhahiri wa kupata unachokitaka katika maisha yako.

Unatakiwa kuwa na picha halisi ya kitu unachokitaka kwanza ndipo uende ukakitafute, kumbuka kumiliki kunaanzia kwenye akili kwanza acha kusema nahitaji nyumba nzuri,gari zuri,biashara nzuri, wakati hujapata picha halisi katika akili yako kile unachokihitaji unataka kiweje. Vijana wengi wamekuwa wakimaliza chuo Kikuu na kusema nipo tayari kufanya chochote huu ni ujinga na kutokuwa na maono hivi kweli kama upo tayari kufanya chochote nkikuambia ukachimbe vyoo utachimba? Be definate (unataka nini kwanza) na hicho unachokitaka hakikisha una picha yake kwenye akili yako jinsi kitakavyokuwa ndipo unaanza jitihada zote zitakazokupelekea kupata kile unachohitaji.

MHE.ENG.HAMAD MASAUNI AFUNGUA MAFUNZO YA VIJANA WA TUEPO KUWAJENGEA UWEZO VIJANA KUJIAJIRI WENYEWE

$
0
0
Mmoja wa Kijana Wasio na Ajira Tanzania akisoma Quran wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Siku mbili ya kuwajengea Uwezo Vijana wa Jumuiya ya Watanzania Wasuio na Ajira Tanzania (TUEPO) yanayofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Zanzibar.
Mhe Hamad Masauni akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo baada ya ufunguzi wake. 
Picha na Zanzinews.com  
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

WADHAMINI WAKUU WA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA WAZITAKIA KILA LA HERI TIMU 16 ZINAZOSHIRIKI LIGI KUU 2015/2016 INAYOTIMUA VUMBI KESHO

$
0
0

Ferrao.
 NA MWANDISHI WETU
WADHAMINI wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, wamezitakia kila la heri timu zote 16 zinazoshiriki ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Jumamosi hii kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao, alisema kuwa ni fahari kubwa kwao kuona msimu mpya wa ligi hiyo unaanza hivyo kutoa fursa kwa wapenzi wa soka nchini na kwingineko kupata burudani.

Alizitaka timu zote pamoja na mchezaji mmoja mmoja, kucheza kwa kufuata sheria zote 17 za soka ili kuutendea haki mchezo huo, lakini pia mashabiki ambao wamekuwa wakimiminika kwa wingi viwanjani kuzishabikia timu zao.

Ferrao aliwaonya viongozi, wachezaji na hata waamuzi kujiepusha na vitendo vyovyote vinavyoweza kuathiri matokeo ya mchezo husika, zaidi ikiwa ni rushwa na ushirikina ambao mara nyingi umekuwa ukihusishwa katika kupunguza uhondo wa soka kwa wachezaji kutojituma uwanjani wakiamini ‘ushindi ni lazima’.

“Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inapoanza mwishoni mwa wiki hii, wachezaji wa timu zote shiriki, ni vema wakatambua kuwa Vodacom inawajali ndio maana tumeongeza udhamini kutoka Sh bilioni 1.8 hadi bilioni 2.3  ili kuifanya ligi kuwa na msisimko wa aina yake, lakini pia kuboresha maisha ya wachezaji,” alisema.

Juu ya udhamini wao wa miaka mitatu katika ligi hiyo, Ferrao alisema kuwa wameongeza dau kwa kuwa timu zimeongezeka kutoka 14 msimu uliopita hadi 16 msimu huu, lakini pia wakifanya hivyo ili kuiboresha na kuongeza ushindani miongoni mwa wachezaji na timu kwa ujumla.

Ferrao aliwataka mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi viwanjani kuzishangilia timu zao ili kuwapandisha mzuka wachezaji waweze kujituma kadri ya uwezo wao na kupata ushindi.

Timu zinazoshiriki ligi hiyo ni mabingwa watetezi Yanga, Azam na Simba za Dar es Salaam, Mbeya City na Prisons (Mbeya), Toto Africans (Mwanza), Kagera Sugar (Kagera), Mwadui na Stand United (Shinyanga), Coastal Union, African Sports na Mgambo Shooting (Tanga), Mtibwa Sugar (Morogoro), JKT Ruvu (Pwani), Ndanda FC (Mtwara) na Majimaji (Ruvuma).
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, kesho Simba itavaana na African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, Azam watawakaribisha Prisons (Azam Complex), JKT Ruvu na Majimaji (Majimaji, Songea) na Mgambo watakuwa wageni wa Ndanda (Nangwanda Sijaona).

Mbeya City watakuwa wenyeji wa Kagera Sugar (Sokoine), Mwadui wataifuata Toto African (Kirumba), Stand Utd wataikaribisha Mtibwa (Kambarage), wakati mechi nyingine itachezwa Jumapili kwa Yanga kuikaribisha Coastal Union (Uwanja wa Taifa).

JUKWAA LA SANAA LAFANA, MSANII MKONGWE AISHIYE MAREKANI SALMA MOSHI AWALIPIA WASANII BIMA YA AFYA

$
0
0

Jukwaa La Sanaa la BASATA wiki hii lilipata wazungumzaji wa aina yake na kulifanya kuwa jukwaa lililochangamka na kuwa na mazungumzo ya zaidi ya masaa matano. Wasanii takriban 70 walikaa wakichambua maada mbalimbali kuhusu mustakhabari wa sanaa katika nchi yetu. Jambo ambalo liliingiza changamoto katika jukwaa hili, ni kuweko katika meza kuu wasanii wawili ambao walianza sanaa nchini na hatimae kuhamia ughaibuni ambako ndiko wanaishi kwa sasa.

Wasanii Salma Moshi aliyekuwa akijulikana kama Salma Nyoka, msanii wa kwanza wa kike kuchezea nyoka katika jukwaa, na ambaye alikuwa kiongozi wa vikundi vilivyotamba kama DDC Kibisa Cultural Troupe Super Mama Cultural Troupe na Ujamaa Cultural Troupe, na Abbu Omar, mwanamuziki aliyewahi kupigia bendi kama Urafiki na UDA Jazz ambae kwanza alihamia Kenya na kupiga na kurekodi na makundi kama Simba wa Nyika na Les Wanyika na pia kurekodi album kadhaa akiwa na kundi lake ambaye hatimae alihamia Japan ambako amekuwa akiishi kwa kupiga muziki na akiwa na waTanzania wengine kama Lista na Fresh Jumbe.

Mazungumzo yaligusia nyanja mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kuwa na mikataba kabla ya kazi, kuboresha kazi ili kuweza kuuza nje, namna ya kujitambulisha  duniani kwa kuwa na websites na blogs, na pia serikali kubadilika na kuweko mfumo wa uongozi wa sanaa kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa. Katika mkutano huo, John Kitime Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki aliongelea fursa ya Bima ya Afya kwa wasanii, ambapo Salma Moshi alijitolea kuwalipia nusu ya ada wasanii wanne, na kumlipia bima kamili Mzee Kassim Mapili ambaye kwa sasa anasumbuliwa na moyo na figo. Abbu Omar pia aliamua kulipia Bima yake na kueleza kuwa katika nchi ya Japan ni lazima kila mwananchi kuwa na Bima ya Afya, kwani ugonjwa hauji kwa taarifa na matibabu ni gharama kubwa.

Mkutano huo ulianza saa tano na kulazimishwa kusimamishwa saa kumi, kwani wasanii bado walikuwa na mengi ya kuwauliza wasanii hawa nguli walioweza kuendeleza maisha ughaibuni kupitia sanaa

Salma Moshi na Mzee Kassim Mapili

Abbu Omari mwanamuziki aishiye Japan akitoa mada. Kulia ni msanii mkongwe aishiye Marekani Salma Moshi aliyepata kujizolea umaarufu kwa kucheza na nyoka miaka ya nyuma

Picha ya pamoja

Salma Moshi akiwa na baadhi ya wasanii aliowalipia sehemu ya Bima ya Afya IMETAYARISHWA NA www.johnkitime.co.tz
Kwa kusoma zaidi BOFYA HAPA

WATEJA WA AIRTEL WAZIDI KUSHIDA MAMILIONI YA PESA

$
0
0
  Afisa uhusiano na matukio, Bi Dangio Kaniki akiongea na mshindi
aliyepatikana wakati wa kuchezesha droo ya saba ya wiki ya promosheni
ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel kutoka mikoa ya
Kigoma na Dar es Salaam walipatikana akichukua taarifa za mshindi
(kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana
Bakari Majid droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya Airtel
Moroco jijini Dar es saalam, Jumanne Septemba 1 2015.



Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Tanzania, Dangio Kaniki
(kushoto) akimkabidhi mshindi wa droo ya sita ya promosheni ya
“Jiongeze na Mshiko”, Rajabu Mwalapinga (kulia), mkazi wa Dar es
Salaam, shillingi millioni tatu.



Hivyo aliwahimiza watanzania kuchukua fursa hii
waliopatiwa na Airtel kujiinua kiuchumi
Hadi sasa, promosheni ya “Jiongeze na Mshiko” ya Airtel imewafanya
watanzania 16 mamilionea. Mamilionea zaidi wanategemewa kutokea katika
promosheni hii iliyoanzishwa wiki saba zilizopita.
 
 Vile vile Airtelimewazawadia fedha taslimu washidi wa droo ya saba, ambao ni, GeriWilliam kutoka Dar es Salaam na Lui Saulo Karunda, mkazi wa Kigoma.

Wateja wanaweza kujinga na promosheni hii bure kwa kutuma ujumbe wenyeneno "BURE" kwenda namba 15470, na kisha kuanza kupokea maswali kwenyesimu zao na kujibu maswali bure bila gharama yoyote na kujikusanyiapointi.

 Mteja atakapomaliza kujibu maswali ya bure atapata ujumbe
utakaomuuliza kama angependa kujiunga na ngazi ya premier, ili
kuwezeshwa kufunguliwa maswali zaidi na kujikusanyia pointi nyingi kwa
zawadi zenye thamani kubwa.

SERIKALI YAZINDUA UJENZI WA KITUO KIKUBWA CHA TIBA YA MOYO NCHINI

$
0
0
 Mkurugenzi wa Elimu ya juu kutoka Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi, Prof. Sylivia Temu akizungumza wakati wa uzinduzi mradi wa ujenzi wa kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na mishipa ya moyo hapa nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kituo hicho kitakachokuwa na uwezo wa kutoa huduma za kitabibu na kitafiti kwenye magonjwa hayo kwa nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki na kitakuwa chini ya usimamizi wa  Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS).
 Mkurugenzi wa Elimu ya juu kutoka Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi Stadi, Prof. Sylivia Temu (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa chuoChuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS), wawakilishi kutokakutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya afya baada yauzinduzi mradi wa ujenzi wa kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na mishipa ya moyo hapa nchini uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kituo hicho kitakachokuwa na uwezo wa kutoa huduma za kitabibu na kitafiti kwenye magonjwa hayo kwa nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki na kitakuwa chini ya usimamizi wa  (MUHAS).
Na Mwandishi wetu,
SERIKALI imezindua mradi wa ujenzi wa kituo cha ubora wa sayansi ya magonjwa na mishipa ya moyo hapa nchini kitakachokuwa na uwezo wa kutoa huduma za kitabibu na kitafiti kwenye magonjwa hayo kwa nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam jana kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi stadi Bw. Shukuru Kawambwa, Mkurugenzi wa Elimu ya juu nchini, Prof. Sylivia Temu alisema mradi huo unaotekelezwa na serikali kwa ushirikiano na benki ya maendeleo ya Afrika  ni mojawapo ya miradi minne ya afya inayotekelezwa kwenye ukanda wa afrika mashariki ikilenga kutatua changamoto mbalimbali za kiafya.
“Kila nchi ya Afrika Mashariki ina mradi wa aina yake kwenye sekta hii muhimu na kwa upande wetu sisi umejikita katika kukabiliana na magonjwa ya moyo na utakuwa chini ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) na utakwenda sambamba na ujenzi wa kampasi mpya ya chuo hicho unaondelea huko eneo la Mloganzila hapa jijini Dar es Salaam,’’ alibainisha.
Akizungumzia faida za mradi huo Prof Temu alisema utasaidia kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo hapa nchini sambamba na kupunguza gharama zinazolikabili taifa kwa sasa kutokana na kusafirisha idadi kubwa ya wagonjwa wa moyo kwa ajili ya kutafutaa matibabu nje ya nchi. 

IN LOVING MEMORY

$
0
0
Norma Gloria Kemilembe Mushema

 Born: 06-11-1974 – Passed on: 13-09-1990
For the last 25 years:
A million times we've needed you
A million times we've cried
If love alone could have saved you 
You never would have died.

In life we loved you dearly
In death we love you still
In our hearts you hold a special place No one could ever fill.

If tears could build a staircase
And heartache build a lane
We would walk the path to heaven
And bring you back again.

Our family chain is broken
And nothing seems the same
But as God calls us one by one
The chain will link again.



Deeply remembered by your Brothers, Sisters and your loving Mum. Continue resting in peace

The Right Mix: Youth Study Reveals The Music that Makes East Africa Youth One.

Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji cha Umbuji { Masjid Shuraa } Jimbo la Uzini Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja wazinduliwa

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al – Hajj Dr. Ali Mohammed Shein amesema ni jambo la faraja kuona kwamba waumini wa Dini ya Kiislamu waliojalaliwa uwezo wanaendelea kujitokeza katika ujenzi wa majengo ya Misikiti na madrasa za Kisasa katika maeneo mbali mbali hapa Nchini. 
Alisema mwamko huo umesaidia kupata majengo mazuri nay a kisasa kwa mujibu wa maendeleo ya sayansi na teknolojia kiasi kwamba mazingira ya kufanyia Ibada yanaridhisha katika kuwafundisha vijana Quran n a mafundisho mengine ya Dini ya Kiislamu. 
Al-Hajj Dr. Ali Mohammed Shein alisema hayo wakati akizungumza na Waislamu wa mbali mbali mara baada ya kuuzindua rasmi Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji cha Umbuji { Masjid Shuraa } ndani ya Jimbo la Uzini Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. 
Alisema Waislamu na Jamii ni mashahidi katika miaka iliyopita Waislamu wa Zanzibar na maeneo mengine Duniani hawakuwa na sehemu muwafaka wakati walipokuwa wakitaka kutekeleza ibada zao. 
Alisema mazingira ya sasa yamekuwa bora zaidi kwa kuwapa utulivu waumini wa Dini ya Kiislamu ambapo hufanya ibada zao katika maeneo mazuri yanayotoa fursa kuendelea na ibada hizo hata wakati wa usiku. 
Rais wa Zanzibar alisema ujenzi wa msikiti huo ni neema kubwa ambayo waumini wa Kijiji hicho wana wajibu wa kushukuru na kuhakikisha wanautumia vyema katika kutekeleza ibada za sala, kuendesha madrasa, kukuza imani, kuuendeleza Uislamu na kufanya matukio ya Kijamii ambayo yana mnasaba wa kutumia msiki. 
Aliwanasihi waumini hao kuitunza nyumba hiyo ya mwenyezi Muungu kwa kuwaunganisha wakikumbuka kwamba uwepo wa jengo hilo tukufu ujenzi wake umetokana na Umoja na moyo wao wa kujitolea ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya ujenzi. 
Akisoma Risala ya Waumini na Wananchi wa Kijiji cha Umbuji Ustadhi Haji Shauri Issa alisema ujenzi wa Msikiti huo wa Ijumaa wa Kijiji hicho ulioanza Miaka Mitatu iliyopita umekuja kutokana na changamoto ya ongezeko kubwa la Waumini waliokuwa wakifanya ibada katika msikiti wa asili. Ustadhi Shauri alisema waumini wa Kijiji hicho wamepata faraja baada ya kukamilika kwa msikiti huo uliojengwa kwa nguvu za waumini wenyewe na na kuwashukur washirika mbali mbali wa Dini waliojitolea kuchangia ujenzi huo. 
Msjid Shuraa ambao una uwezo wa kusaliwa na waumini zaidi ya 600 kwa wakati Mmoja umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 200,000,000/- za Kitanzania licha ya kuendelea kuwepo baadhi ya changamoto katika kukamilisha msikit
 Haiba ya Msikiti Mkuu wa Ijumaa wa Kijiji cha Umbuji  ulipo Jimbo la Uzinin ndani ya Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja unavyoonekana kwenye picha baada ya kukamilika ujenzi wake na kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohammed Shein.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Umbuji mara baada ya kuuzinduai Msiki wa Ijuma wa Kijiji hicho.
 Naibu Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Thabir Nauman Jongo akitoa mawaidha katika hafla ya uzinduzi wa Msikiti wa Ijumaa wa Kijiji cha Umbuji Jimbo la Uzini ,Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
 Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakisikiliza Hotuba ya Balozi Seif mara baada ya uzinduzi wa Msiku wa Ijumaa wa Kijiji hicho.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Balozi Mpya wa India aliyepo Nchini Tanzania  Bwana Sandeep Arya aliyefika Ofisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi.
Balozi Seif akibadilishana mawazo  na Balozi Mpya wa India Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya aliyekaa kati kati katika azma ya kuimarisha uhusiano wa muda mrefu wa Kihistoria kati ya pande hizo mbili. Aliyekaa  mwanzo kutoka kushoto ni Balozi Mdogo wa India aliyepo hapa Zanzibar Bwana Setandar Kumar. Picha na OMPR – ZNZ.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images