Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

NITABORESHA MASLAHI YA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA-MAGUFULI

$
0
0
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk.John Magufuli akifafanua jambo kwa msisitizo huku akibainisha kuwa iwapo atachaguliwa kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu, basi Serikali yake itahakikisha inaboresha maslahi ya watumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini kutokana na kutambua mchango wao katika kulinda amani ya nchi yetu.

Dkt Magufuli alisema kuwa anataka kuona watumishi wa jeshi hilo wanakuwa na mishahara mizuri na hiyo itawezesha kufanya kazi ya ulinzi na usalama wa nchi kwa ufanisi zaidi huku akitumia nafasi hiyo kuomba Watanzania kudumisha amani ya nchi kwani ikipotea hakutakuwa na maendeleo ya aina yoyote.

Dk.Magufuli alitoa kauli hiyo leo  katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Korogwe, Mkinga na Lushoto ikiwa ni sehemu ya mikutano ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa rais ambapo alisema anatambua kazi nzuri inayofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama na kuongeza kuwa serikali yake itaboresha maslahi ya wanajeshi wa majeshi yote Nchini . PICHA NA MICHUZI JR-LUSHOTO,TANGA
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Bumbuli Ndugu January Makamba kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Togotwe.
Mgombea Ubunge jimbo la Bumbuli Ndugu January Makamba akisisitiza jambo kwa Wananchi wake katika jimbo la Bumbuli jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Togotwe.
 Wakazi wa Jimbo la Bumbuli wakifuatilia kwa makini mkutano wa Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jioni ya leo.
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM pamoja na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini Ndugu Stephen Ngonyani aka Profesa Maji Marefu kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kwamazandu, Korogwe Vijijini.




MAGUFULI ALIVYOUNGURUMA MJINI LUSHOTO

BBC DIRA YA DUNIA JUMATANO 09/09/2015

ACT WAZALENDO WASEMA MCHUANO IRINGA NI CHIKU ,MWAKALEBELA NA MASASI ,MCHUNGAJI MSIGWA ASICHAGULIWE KASHINDWA KAZI

$
0
0
Na Matukiodaimablog
CHAMA Cha ACT wazalendo kimewataka wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kuwapima wagombea watatu waliojitokeza kuomba kuchaguliwa kupokea  nafasi ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa ( Chadema)kwa madai kuwa hapaswi tena kupewa kura katika jimbo hilo.

Katibu Wilaya  wa ACT wazalendo Wilaya ya  Iringa Bw Zhenepa Ally leo wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea Ubunge wa jimbo la Iringa mjini Chiku Abwao ( ACT wazalendo) kwenye kata ya Kitwiru .

Alisema kuwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Msigwa wakati wa Ubunge wake awali alikuwa akipambana na ujangili kwa kupambana na wauwaji wa Tembo na kila mkutano wake alikuwa akionyesha kupiga vita ujangili ila baada ya kushikamana na Waziri Lazaro Nyalandu ( CCM ) kwa kusafiri pamoja katika Ziara za nje aligeuka ghafla na kuacha kabisa kuzungumzia ujangili.

Hivyo aliwataka wananchi wa jimbo la Iringa Mjini kuwapima wagombea watatu. Waliojitokeza kuwania nafasi ya Ubunge jimbo hilo ambalo Mchungaji Msigwa kashindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.

Aliwataja waliojitokeza kugombea nafasi hiyo ya Ubunge ambao wananchi wanapaswa kuwachuja kuwa ni Chiku Abwao ( ACT wazalendo) ,Frederick Mwakalebela(CCM) na Daud Masasi (ADC)na sio kupoteza kura kwa kumpa tena mchungaji Msigwa ambae ametelekeza jimbo hilo kwa miaka yote mitano.

" Katika uchaguzi huu wananchi wa Iringa tunaomba muwapime watu watatu waliojitokeza kumpokea Ubunge Mchungaji Msigwa"

Kwa upande wake Mgombea Ubunge jimbo hilo la Iringa Mjini Bi  Abwao alisema jimbo la Iringa Mjini ni moja kati ya majimbo ambayo yalikuwa rahisi zaidi upinzani kuendelea kuongoza tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ila kutokana na kushindwa kwa Mchungaji Msigwa jimbo hilo wananchi wamepoteza imani na upinzani.

Abwao aliwaomba wananchi wa jimbo la Iringa mjini kumchague yeye kuwa mbunge wao kwani sera nzuri za kuwakomboa wananchi hao

" Mbunge  Msigwa aliahidi kuwapa nyavu kwa maana ya mitaji ila kipindi chake chote kaishia kufanya mikutano ya vurugu na kutukana wananchi wake kuwa ni wavivu wanaopenda kucheza bao wakati nae ni miongoni mwa wavivu hao na wacheza bao wazuri"

Hivyo alitaka wananchi wa jimbo la Iringa ili kurejesha heshima ya upinzani jimbo la Iringa Mjini ni wakati wa kuchagua chama cha ACT wazalendo kuanzia Udiwani Ubunge na Urais na sio Chadema kupitia mwamvuli wao wa Ukawa ambao wamesimamisha mgombea ambae yupo katika orodha ya mafisadi.

Akizungumzia kuhusiana na Mgombea Urais wa Ukawa Chiku ,alisema kuwa Mgombea huyo hana sifa ya kuwakomboa watanzania kwani ni genge la walanguzi linalotaka kwenda kutumia Ikulu kwa kurejesha mamilioni ya pesa waliotumia kununua Ikulu.

Hata hivyo alisema watanzania wasidanganyike na safari ya matumaini ya Ukawa kwani safari hiyo haipo tena na hivyo ni vema kuchukua hatua kwa kukataa wagombea hao wa Ukawa.

NHIF YAINGIA MAKUBALIANO YA UDHAMINI WA BIMA VPL

$
0
0
Mfuko wa Bima ya Afya nchini (NHIF) umeingia makubaliano ya udhamini wa bima ya afya kwa wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi kwa vilabu 16 vya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo ofisi za TFF zilizopo Karume, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema wanaishukuru NHIF kwa kuwapa udhamini huo ambao utavisaidia vilabu vya Ligi Kuu katika matibabu ya wachezaji na bechi ka ufundi.

Tumekua na kilio cha muda mrefu juu ya vilabu vya Ligi Kuu kuwa na Bima za afya kwa wachezaji, kitu ambacho kipo kikanuni lakini vilabu vilikuwa vinashindwa kutimiza hitaji hilo la kikanuni na sasa TFF kwa kushirikian na NHIF tutakua tumeiondoa tatizo hilo.

Naye Mkuu wa Mawasiliano wa NHIF, Sungi amesema udhamini huo wa bima ya matibabu kwa wachezaji na benchi la ufundi utatolewa kwa matibabu yote yatakayofnayika ndani ya nchi.
Mchezaji au kiongozi pindi atakapopata tatizo la kuumwa, basi ataweza kutibiw akatika hospitali yoyote yenye huduma ya Bima katika eneo alilopo, lengo ni kuhakikisha wanakua na afya njema kwa ajili ya kushiriki vizuri mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom.

Lengo letu ni kuona wachezaji wanapata huduma ya afya popote wanapokuwa na kuweza kushiriki vizuri katika michuano ya Ligi Kuu, na kuweza kuzitumikia vyema timu zao kwenye mashindano.
Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura kwa niaba ya vilabu vya Ligi Kuu amesema wanashukuru kupata udhamini huo wa bima ya afya, uwepo wa NHIF umevipunguzia vilabu mizigo wa matibabu na sasa vilabu vitaweza kushiriki vizuri kwenye michuano ya msimu huu.

JKT KUENDELEA KUBORESHA CHANGAMOTO MBALIMBALI

$
0
0
Mkuu wa kambi ya JKT Burombola Luteni Kanali Mketo akizungumza katika sherehe ya kufunga mafunzo ya mujibu wa sheria kwa vijana waliomaliza kidato cha sita mafunzo yaliyofanyika kwenye kambi ya Burombola wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.

Baadhi ya vijana waliomaliza mafunzi ya JKT kwenye kambi ya Burombola wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma
picha na editha Karlo
   
           
   Na Editha Karlo,Kigoma
MKUU wa Jeshi la kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael Muhuga alisema kuwa jeshi hilo litaendelea kuboresha changamoto mbalimbali zinazojitokeza ili kuwezesha vijana wote wanaomaliza masomo ya kidato cha sita kujiunga na mafunzo hayo kwa wakati mmoja.

Muhuga alisema hayo  kwenye kambi ya JKT Burombola kikosi cha 821 katika sherehe za kumaliza mafunzo kwa vijana wa mujibu wa Taifa kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita katika mafunzo yaliyojulikana kama Operesheni Kikwete.

DKT JOHN POMBE MAGUFULI ALIVYONGURUMA MTWARA

DIAMOND PLATNUMZ, SAUTI SOL AND PATORANKING ROCKS VUZU AMP 1st ANNIVERSARY #ONLYTHEBEST

$
0
0
IMG_8160
Diamond Platnumz with his dancers!
IMG_8167
...Onanana baby oh onananana baby oh onanana onananananana Baby oh onanana baby oh onananana baby oh onanana onananananana Kama nguna ntakulaga (mmhh) tukipata burger (mmhh) tukikosa dagaa (mmhh) Njaa nitalala nayo (oyorima) mirungi kwa kusaga (mmhh) mbege kwa wachagaa (mmhh).
IMG_8255
sankoro sankororo sankoro sankororo Tanzania sankoro sankororo tah (oyorima) Kama Ronaldo Nigeria sankoro sankororo (umunwanyi) sankoro sankororo (everybody) Sankoro sankororo taah! Kama Ronaldo...

WACHIMBAJI WADOGO SHINYANGA WAPATIWA MAFUNZO KUHUSU MFUMO MPYA WA UTOAJI LESENI ZA MADINI KWA NJIA YA MTANDAO

$
0
0
 Kamishna Msaidizi wa Madini, Kanda ya Kati – Magharibi, Humphrey Mmbando akitoa ufafanuzi wa baadhi ya masuala muhimu yaliyojitokeza wakati wa semina kwa wachimbaji wadogo wa madini kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji wa leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP). Semina hiyo imefanyika leo mjini Shinyanga na ni mwendelezo wa Mafunzo yanayotolewa nchi nzima kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini nchini. Wengine pichani (mstari wa mbele) ni baadhi ya Maofisa kutoka Ofisi ya Madini – Shinyanga.
 Baadhi ya akina mama ambao ni wachimbaji wadogo wa madini mkoani Shinyanga wakiwa katika semina kuhusu mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP). Kutoka Kushoto ni Amina Mtoro, Hafsa Issa, Halima Mohamed, Khadija Salum na Nusura Juma. Semina hiyo imefanyika leo mjini Shinyanga na ni mwendelezo wa Mafunzo yanayotolewa na Wizara ya Nishati na Madini kwa wachimbaji wadogo na wamiliki wa leseni za madini nchi nzima.
 Mtaalamu kutoka Kitengo cha Leseni cha Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Nuru Shabani, akitoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa utoaji wa leseni kwa njia ya mtandao wakati akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya mfumo mpya wa huduma za utoaji leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal – OMCTP) kwa wachimbaji madini wadogo, wakati wa Semina maalumu iliyofanyika leo Septemba 9, 2015 mjini Shinyanga.

NCCR-MAGEUZI WAZINDUA KAMPENI JIMBO LA MWANGA KUMNADI MSUYA

$
0
0
Baadhi ya wananchi katika kata ya Kifula ,jimbo la Mwanga wakifuatilia uzinduzi wa mkutano wa kampeni wa chama cha NCCR-Mageuzi.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi na Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA,James Mbatia akihutubia katika mkutano huo.
Mke wa mgombea Ubunge katika jimbo la Mwanga,Youngsevier  Msuya,Dorcas Youngsevier akizungumza katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi na Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA,James Mbatia akimtamburisha Mkurugenzi wa mambo ya nje wa chama hicho na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki ,Ndelakindo Kessy wakati wa uzinduzi wa mkutano wa kampeni katika jimbo la Mwanga. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Mh. Hamad Rashid afungua kampeni za urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADC kisiwani pemba

$
0
0
 Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADC (DAIADAIA) Mhe Rashid Hamad akihutubia umati wakati akizindua rasmi kampeni za chama hicho katika kiwanja cha Gombani ya Kale Kisiwani Pemba na kunadi sera zake
 Sehemu ya umati wa wananchi ukimsikiliza  Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADC (DAIADAIA) Mhe Rashid Hamad akihutubia umati wakati akizindua rasmi kampeni za chama hicho katika kiwanja cha Gombani ya Kale Kisiwani Pemba na kunadi sera zake
Sehemu ya umati wa wananchi ukimsikiliza  Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADC (DAIADAIA) Mhe Rashid Hamad

MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI WA KATI NA WAFANYAKAZI‏‎

$
0
0

Je umekwama kifedha?,Hujui wapi pa kwenda? Je unahitaji kutimiza ndoto na malengo yako? usihangaike
Kampuni ya mikopo ya wezesha mzawa microfinance ltd inatoa mikopo kwa wajasiriamali wa kati na wafanyakazi wa sekta zote ikiwemo biashara,viwanda na ufugaji.
Kiwango cha mkopo kinaanzia 500,000/= hadi 50,000,000/=
Mkopo unatolewa ndani ya masaa 24


Sifa za mkopaji
.uwe ni mtanzania mwenye umri usiopungua miaka 18
.uwe n uzoefu wa biashara usiopungua
.uwe na namba ya utambulisho wa kodi (TIN)
.Uwe na mkataba wa kazi (kwa mfanyakazi)
.Uwe umeajiriwa na kampuni inayotambulika na kusajiriwa na serikali(kwa mfanyakazi)
Ofisi zetu zipo Bamaga ,jengo la Global publishers.Tupigie kwa simu namba
0715 620824
Nyote mnakaribishwa

KUMBUKUMBU YA FLORA (MAPENDO YA FLORA)

$
0
0
TUNAPOADHIMISHA MIAKA MIWILI YA KUMBUKUMBU

YA KIFO CHA MPENDWA WETU

FLORA FLOWIN MKANULA

(1993 – 2013)

Tunaona ni vema kumshukuru MUNGU hasa kwa mapendo aliyotushirikisha kupitia maisha ya FLORA, nasi tukabakiwa kwa namna ya pekee tunamuenzi kwa matukio mbalimbali hasa kupitia Misa Takatifu katika kanisa kuu la Mtakatifu Joseph Jimbo Kuu la Dar es Salaam. 

Siku ya tarehe 10/09/2015, saa 12.30 asubuhi.  Baada ya hapo tunazuru makaburi ya Kinondoni.

Sote tuzidi kuyaenzi haya: 
Pendaneni kindugu Rum 12:10
“APUMZIKE KWA AMANI”

SHUKRANI FAMILIA YA MCHECHU

$
0
0
New Picture
Familia ya marehemu Dr. John Edward Mchechu wa Ukonga Dar es salaam wanapenda kutoa shukrani zao za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki walioshirikiana nao na kuwafariji kwa hali na mali katika kumuuguza na mpaka kumlaza katika nyumba ya milele mpendwa baba yao Dr. John Edward Mchechu aliyefariki tarehe 21/07/2015 nyumbani kwake Ukonga na kuzikwa tarehe 26/07/2015 Muheza, Tanga.
Shukrani za pekee zimfikie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. JakayaMrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, WaziriMkuu, Mh. Mizengo Peter Pinda, Mawaziri, Wabunge, Wakuu wa Mashirika na Wafanyakazi wa Serikali kwa kutufariji kipindi chote cha kuumwa kwake mpaka alipotwaliwa kutoka ulimwengu huu.
Shukrani za pekee pia ziwafikie wafanyakazi na wajumbe wa bodi ya NHC, Serengeti Breweries, DAWASCO, KCB, Rafiki Club, Soul Sisters, New Millenium Women Group, Beach Ladies, Sisters Club, Madaktari na wauguzi wa hospitali za Muhimbili, Hindu Mandal, Apollo Hydrabadna Dispensary yaArafa.
Mapadri na wachungaji wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Mbezi Beach, Makanisa ya Anglikana ya Mtakatifu Paulo la Ukonga, Dar es Salaam na Mtakatifu Petro la Mkuzi,Tanga, kwaya mbalimbali na vikundi vya maombi kwa msaada wao wa kiroho.
Tunawakushukuru mtu mmoja mmoja lakini haiwezekani kwani watu ni wengi sana, tunaomba tu mpokee shukrani zetu za dhati kutoka moyoni mwetu kwajinsi mlivyotufariji katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa baba yetu.
Misa ya Shukrani
Familia ya marehemu Dr. John Edward Mchechu wanapenda kuwakaribisha wote katika misa ya shukrani itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 12/09/2015 kuanzia saa mbili asubuhi katika kanisa la Mtakatifu Petro Mkuzi, Tanga. Karibuni sana mjumuike nasi.
Raha ya milele umpeeeh Bwana wamilele umwangazie apumzike kwa amani, Amina
MR. & MRS. NEHEMIAH MCHECHU.

MAHOJIANO YA ANKAL NA VIJIMAMBO BLOG WASHINGTON DC, MAREKANI, MIAKA 7 ILIYOPITA


sherehe ya kuadhimisha miaka 10 ya Michuzi blog - Globu ya jamii...Libeneke oyeeeeee!!

EKARI 7000 ZA MASHAMBA KUGAIWA KWA WANANCHI WA ARUSHA.

$
0
0
SERIKALI imetwaa jumla ya Ekari 7000 baada ya ubatilishwaji wa Mashamba ya Tanzania plantatition limited yaliyokua yakimilikiwa na mwekezaji  kutoka nje ,mashamba hayo yanatajiwa kugawanywa kwa wananchi 2000 wenye uhitaji wa ardhi ya makazi na mashamba .

Aidha baada ya ubatilishwaji wa mashamba hayo Arusha imepata ekari 6176.5 na Halmashauri ya Meru ekari 925  hivyo kufikia ekari 7101 ambazo zitagawanywa kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi,Wiliam Lukuvi wakati akitoa taarifa ya usuluhishi wa migogoro ya ardhi  katika mikoa ya Arusha na Manyara katika mkutano wake na Waandishi wa Habari,Lukuvi amesema kuwa mashamba hayo yalikua na migogoro kwa kipindi kirefu kati ya mwekezaji na Wananchi hivyo kutokana na uhitaji mkubwa wa ardhi serikali imeamua kubatilisha mashamba hayo.

“Nimekuja Arusha na timu yangu ambayo itafanya uhakikiki wa watu 2000 wenye uhitaji na baada ya kujiridhisha watafanya zoezi la ugawaji na pia wananchi watapatiwa hati ya kumiliki ardhi zao safari hii hatutagawa ardhi kienyegi” Alisema Lukuvi

Lukuvi amesema kuwa mbali na shamba hilo pia wamepata ekari 100 katika shamba la Imani Estate na pia Shamba la Noors  lenye Ekari 2296  lililokua na mgogoro kati ya Mwekezaji na wananchi wa Kijiji cha Laroi na Kisima cha Mungu litagaiwa kwa wananchi baada ya mazungumzo kati ya Mwekezaji kukubali kuachia shamba hilo

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC ,Fidelis Lumato amesema kuwa ugawanywaji wa mashamba hayo utasaidia kupunguza migogoro mikubwa ya ardhi iliyokua inakabili wilaya hiyo kutokana na uhaba mkubwa wa ardhi.

Jumla ya migogoro 80 iliyowasilishwa kwa Waziri Lukuvi kutoka katika Halmashauri ya Jiji la Arusha ,Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na Halmashauri ya Meru imepatiwa ufumbuzi hivyo kupunguza migogoro ya ardhi ilikua ikilisakama jiji la Arusha.

LISHE DUNI YACHANGIA VIFO VYA WATOTO NA KIMAMA WAJAWAZITO

$
0
0
 
Na Woinde Shizza,Arusha.
LISHE duni kwa kinamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano imekua chanzo cha vifo vya watoto wadogo pamoja na kinamama hao hali ambayo  hali ambayo inazorotesha maendeleo ya kiafya na kitaaluma hivyo watanzania wametakiwa kutumia lishe bora yenye vitamin na virutubisho ili kujenga jamii yenye afya bora kwa ustawi wa nchi.

Hayo yameelezwa na Naibu waziri wa Afya Dokta Kebwe S.Kebwe akitoa takwimu za vifo vya watoto na kinamama vinavyosababishwa na lishe duni amewataka kinamama kuzingatia lishe bora hasa katika kabla ya ujauzito na baada ya kujifungua katika siku 1000 za kuzaliwa kwa mtoto ili aweze kukua vizuri kiafya  hususan afya ya akili na kufaulu kitaaluma.


Kebwe amesema kuwa Mtoto aliyezaliwa na uzito pungufu (chini ya kilo 2.5) ana uwezekano wa kufa katika mwezi wa kwanza baada ya kuzaliwa, mara nne kuliko mtoto aliyezaliwa na uzito wa wastani au zaidi.Mtoto mwenye uzito mdogo sana ana uwezekano wa kufa kutokana na ugonjwa wa kuambukizwa mara nane kuliko mtoto aliye na hali nzuri ya lishe.


“Lishe duni inahatarisha maisha ya watoto wa Tanzania kama ilivyo katika nchi zinazoendelea.Tafiti zinaonyesha kuwa upo uhusiano mkubwa kati ya kiwango cha udumavu na vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka 5, katika ngazi ya mikoa nchini” Kebwe

Naibu Waziri wa Afya Dokta Kebwe S.Kebwe amesema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa Masuala ya Lishe ulioandaliwa na Taasisi ya GAIN (Global Alliance for Improved Nutrition)  unaondelea jijini Arusha huku akiwaagiza maafisa afya walioko katika Halmashauri kufanya kazi zao za kuwaelimisha wananchi na kuwashauri juu ya masuala ya lishe badala ya kupangiwa majukumu mengine na Wakurugenzi wa Halmashauri.

Kusoma zaidi bofya HAPA.

Article 21

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI 10/09/2015

Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images