Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 973 | 974 | (Page 975) | 976 | 977 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Maandamano  ya  askari  polisi kuelekea katika  maadhimisho  ya  wiki ya nenda kwa usalama
  Maadhimisho ya wiki ya  nenda  kwa  usalama mkoa  wa Iringa  leo
  Askari  wa FFU  wakiwa katika maadhimisho hayo.  

  Mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Amina Masenza akiongoza kupokea maandamano leo.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

   

  0 0

   Krini ya ujenzi wa upanuzi wa eneo la Tawaf ulipo msikiti wa Makkah ambao uliangukiwa na kusababisha vifo vya mahujaji 107. 


  Kufuatia mvua  ilioambatana na upepo mkali na kusababisha kuanguka kwa mashine ya ujenzi wa upanuzi wa eneo la Tawaf ulipo msikiti wa Makkah, msikiti huo umeanguka na kusababisha vifo vya mahujaji.  

  Kwa mujibu wa Televisheni ya Saudi Arabia, Saudi TV hadi sasa watu 107 wamefariki dunia na wengine takriban 200 wamejeruhiwa. 

  Kufuatia ajali hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kupitia Ofisi za Ubalozi Riyadh unathibitihsa kuwa Mahujaji wa Tanzania wameanza kuwasili Jeddah kuelekea Makkah leo tarehe 12 Septemba 2015 wakitokea Madina. 

  Hadi sasa Wizara haijapokea taarifa ya Watanzania waliopoteza maisha wala kujeruhiwa kwenye ajali hiyo.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,

  12 Septemba, 2015
   Mmoja wa viongozi wa Mahujaji wa Tanzania akiongea katika kikao cha dharura na mahujaji hao baada ya krini la ujenzi na katika eneo la Tawaf ulipo msikiti wa Makkah  kuanguka  na kusababisha vifo vya mahujaji 107 na majeruhi zaidi ya 200. Hakuna Mahujaji wa Tanzania walioathirika katika ajali hiyo.

   Baadhi ya Mahujaji wa Tanzania wakiwa Makkah salama salimini baada ya ajali hiyo
  Msanii King Majuto akiwa na Mahujaji wenzake wakiwa salama salimini baada ya ajali hiyo
  Taswira la eneo la ajali huko Makkah

   


  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Deo Mutasiwa asisitiza jambo jana jioni  wakati wa ufungaji wa mkutano mkuu wa  mwaka wa sekta ya afya ambao uliambatana na maadhimisho ya miaka 40  ya Mpango wa Taifa wa Chanjo  uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam. 
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando na  wakipongezana mara baada ya kumaliza   jana jioni mkutano mkuu wa  mwaka wa sekta ya afya ambao uliambatana na maadhimisho ya miaka 40  ya Mpango wa Taifa wa Chanjo  uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam.
  Picha namba 3367 ni Baadhi ya wanganga wakuu wa mikoa na wilaya wakiwa katika  huo.

  Na Magreth Kinabo
   SERIKALI imewataka watendaji wote  afya  wa halmashauri ,mikoa wilaya  kusimamia suala la usafi wa mazingira ilikuizesha jamii kuepukana na matatizo ya milipuko ya magonjwa likiwemo suala la ugonjwa wa kipindupindu.
   
   Aidha Serikali pia imewataka watendaji hao, kuanzisha siku maalum ya usafi katika maeneo wanayotoka.
   
  Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Donan Mmbando wakati akifunga mkutano mkuu wa  mwaka wa sekta ya afya ambao uliambatana na maadhimisho ya miaka 40  ya Mpango wa Taifa wa Chanjo  uliofanyika kwenye hoteli ya kuanzia Septemba 8 hadi 11, mwaka huu Ubungo Plaza jijini Dares Salaam.  
   

  0 0

  lemonMo Lemon Mint imefika hadi Santorini, Greece! Umeifikisha wapi Mo soda yako kutoka hapo Dar? Tutumie picha yako 'smile emoticon' ikichaguliwa tutaiweka kwenye ukurasa wetu wa facebook.
  Na Andrew Chale, modewjiblog
  Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL GROUP), imeendelea kufanya vizuri sokoni kupitia upande wa vinywaji vyake mbalimbali vikiwemo: MO Cola, MO Portello na, MO Malt, MO Lemon Mint, MO chungwa na MO Bomba (Energy drink).

  Kupitia ukurasa wa Facebook wa MeTL GROUP, (https://www.facebook.com/MeTLGroup) wamebainisha kuwa kampuni hiyo yenye kauli mbiu ya ‘The People’s Brand’, imeendelea kuwa karibu na wateja wao ilikuweza kushirikisha mawazo mbalimbali katika kufikia malengo ya kimaisha.

  Mbali na kushirikishana mawazo hayo na wateja wao waliopo kwenye ukurusa huo maalum wa facebook, pia imeweza kutoa elimu na namna ya hatua za kufuatwa kwa watu ikiwemo mazoezi, vyakula vinavyofaa kuliwa na mambo mengine.
   KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Mwinyiussi Hassan Abdalla kuwa Mkuu wa Wilaya Magharibi A Unguja katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi hati ya kiapo Nd,Mwinyiussi Hassan Abdalla baada ya kumuaapisha kuwa Mkuu wa Wilaya Magharibi A  katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipeana Mkono wa Shukurani na Nd,Mwinyiussi Hassan Abdalla baada ya kumuaapisha kuwa Mkuu wa Wilaya Magharibi A  katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
   Baadhi ya Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Magharibi A Unguja iliyofanyika lero Ukumbi wa Ikulu,(kutoka kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu (Utawala Bora) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji na Naibu Kadhi Hassan Othman Ngwali
   Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Magharibi A Unguja Nd,Mwinyiussi Hassan Abdalla,iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu,(kutoka kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu(Utawala bora)


  Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Magharibi A Unguja Nd,Mwinyiussi Hassan Abdalla,iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu,(kutoka kulia)Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum Haji Omar Kheir,Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,Meya wa Manispaa ya Mji wa ZanzibarMr.Khatib na Mshauri wa Rais wa Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Bw.Abrahman Mwinyi Jumbe
  Picha na Ikulu


  0 0


  0 0

  ????????????????????????????????????
  Wasanii wenye vipaji vya kuimba wakihakiki majina yao kwa DJ Haazu, wa Radio 5 wakati wa mchakato wa RADIO 5 KAMATA KIPAJI uliofanyika katika viwanja vya TP SINZA Jijini Dar es salaam Septemba 12, 2015.wenye lengo la kusaka vijana wenye vipaji na kuwainua kutokana na vipaji vyao.
  PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
  Katika kuonyesha kuwa wapo karibu na vijana wa kitanzania katika kuwasaidia kuwainua kiuchumi na kiuwezo,kituo cha Radio maarufu kutoka kaskazini mwa Tanzania ARUSHA Radio 5 kimenzisha mchato maalum wa kusaka vipaji kwa vijana wa kitanzania mchakato ambao umeanzia Jijini Dar es salaam ukiwa na lengo la kuhakikisha kuwa wanamuwezesha kijana mwenye kipaji kufikia malengo na ndoto zake
  3
  DJ Haazu akiwajibika.
  Radio 5 imekuwa na michakato mbalimbali ili kusaidia vijana katika secta tofauti tofauti zinazohusu maisha yao ya kiuchumi huku ikiwa inawaunga mkono vijana wenye shughuli mbalimbali ambao hufika radioni hapo kuomba saport ikiwa ni pamoja na vijana wa sarakasi,ujasiriamali na fani nyingine. Mchakato ambao sasa unatajwa kuwa utakuwa msaada mkubwa kwa vijana ambao umezinduliwa Jijini Dar es salaam na kupewa jina la RADIO 5 KAMATA KIPAJI katika viwanja vya TP sinza darajani ilishughudiwa vijana wengi wakijitokeza kuonyesha vipaji vyao ili waweze kuibuka na zawadi mbalimbali ambazo zinatolewa na waandaji hao.

  0 0

   Viongozi waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Magharibi A Unguja Nd,Mwinyiussi Hassan Abdalla,iliyofanyika leo Ukumbi wa Ikulu,(kutoka kulia)Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum Haji Omar Kheir,Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis,Meya wa Manispaa ya Mji wa ZanzibarMr.Khatib na Mshauri wa Rais wa Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Bw.Abrahman Mwinyijumbe.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Mwinyiussi Hassan Abdalla kuwa Mkuu wa Wilaya Magharibi A Unguja katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi hati ya kiapo Nd,Mwinyiussi Hassan Abdallabaada ya kumuaapisha kuwa Mkuu wa Wilaya Magharibi A  katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
   [Picha na Ikulu.]

  0 0

   Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini(TFDA) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi  imefanya operesheni katika maeneo 243 na kufanikiwa  kukamata bidhaa bandia na zile zilizomaliza muda wa kutumika ambapo zina thamani  zaidi ya shilingi milioni 135. katika mkutanono uliofanyika leo jijini Dar es Salaam kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Dawa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Henry Irund.
   Naibu Kamishina wa Polisi (DCI) Makao Mkuu ya Upelelezi na Jinai, Hezron Gyimbi akuzungumza na wanahabari hawapo pichani juu ya Operesheni GIBOIA II iliyofanyika sanjari katika nchi nane zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara ambazo ni Afrika Kusini, Zimbabwe, Malawi na Msumbiji. Operesheni GIBOIA II ameyasema hayo katika mkutano ulifanyika jijini Dar es Salaam kulia ni  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo.

  Mkaguzi wa Dawa Mwandamizi, Sonia Mkumbwa akiwaonesha  Bidhaa bandia  katika mkutano jijini Dar es Salaam.
  Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya  Jamii.

  0 0

   KATIKA kuhakikisha kuwa inamshirikisha msikilizaji wake kwenye kila jambo na hatua inayopiga 93.7 efm, kupitia kipindi chake kipya cha Uhondo ambacho huruka hewani kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa sita mchana hadi saa tisa Alasiri, Kikiwa na watangazaji mahiri Dina Marios na Swebe Santana (Rais wa Wanaume) kimeandaa shindano la Kanga kwa ajili ya wanawake wote wasikilizaji wa Efm 93.7
  Lengo la shindano hilo, linaloanza leo Septemba 14 na kuishia Oktoba 5 mwaka huu, kwanza ni kuwahamasisha wanawake wote wakione Kipindi cha Uhondo kuwa kimekuja kwa ajili yao, pili kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini pia tatu kumwonyesha njia nyingine mwanamke itakayomkomboa badala ya kukaa nyumbani mwisho wa siku atajifunza ujasiriamali kupitia biashara ya Kanga. 
   Mfumo wa shindano lenyewe utakuwa kama ifuatavyo: Wasikilizaji wa E fm ambao ni wanawake wanakaribishwa kushiriki shindano la kubuni maneno ya Kanga kupitia kipindi cha UHONDO na maneno hayo yawe na neno UHONDO . 
  “Mfano Uhondo wa Ngoma uingie Ucheze” na Mshindi atajinyakulia kitita cha Shilingi za Kitanzania milioni moja Hata hivyo shindano hilo halitaishia hapo, kwani baada ya kupata mshindi neno lake la Ushindi zitatengenezwa kanga zitakazoandikwa neno hilo ikiwa ni hatua ya pili sasa ya kumwezesha mwanamke kujikwamua kiuchumi.
  "Zikishatengenezwa kanga hizo, Efm kupitia kipindi hicho cha Uhondo, itatatoa nafasi kwa wanawake kutengeneza pesa na kujikwamua kwa kuuza Kanga hizo na Mwanamke yoyote hasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani atachukua kanga hizo na kuziuza ambapo kwa kila doti moja ya kanga atapata asilimia 30% ya pesa. 
  “ Ndugu zangu waandishi wa habari naomba kusisitiza tu hapa kuwa shindano hili litashirikisha wanawake pekee”. Alisema Dina Marios 

   Mkurungenzi wa Mawasiliano wa( EFM) Denis Ssebo akizugumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya Wasikilizaji wa  E fm  ambao ni wanawake wanakaribishwa kushiriki shindano la kubuni maneno ya Khanga kupitia kipindi cha UHONDO na maneno hayo yawe na neno UHONDO . “Mfano  Uhondo wa Ngoma uingie Ucheze” na Mshindi atajinyakulia kitita cha Shilingi za Kitanzania milioni moja. Kulia ni Mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Uhondo wa EFM Dina Marios leo Jijini Dar es Salaam
   Mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Uhondo wa EFM Dina Marios zungumza na waandi wa habari hawapo pichani kuhusu shindano hilo leo Jijini Dar es Salaam
  Wanahabari wakimsikiliza kwa makini Mkurungenzi wa Mawasiliano wa
  (EFM) Denis Ssebo leo Jijini Dar es Salaam.
  Picha na Emmanuel Massaka.

  0 0

  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiongozana na aliekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Hamis Mngeja wakiwapungia wananchi wa Mji wa Kahama, wakati wakiwasili kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo. Katika hotuba yake, Mgombea huyo amesema iwapo atafanikiwa kuwa Rais wa Tanzania, ataunda Serikali itakayochangamkia Maendeleo yatakayowanufaisha Watanzania wote kwa Ujumla.
  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokelewa na Mwenyeji wake, Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA, Mh. James Lembeli, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.
  Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia Mkutano wa Kampeni wa hadhara wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015.
  Mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia CHADEMA, Mh. James Lembeli, akihutubia Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015.
  Sehemu ya Umati wa wananchi wa Mji wa Kahama, wakiwa wamefurika kwenye Uwanja wa Stendi mpya, Nyasubi, Kahama Mjini leo Septemba 14, 2015, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.

  KUONA PICHA ZAIDI

  BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA


  0 0

   Timu ya soka ya Muziki Mnene ya EFM 93.7 (jezi nyeupe) wikiendi iliyopita ilikuwa Mlandizi mkoani Pwani kucheza mchezo wa kirafiki na Mlandizi Veteran ambapo matokeo yalikuwa 0-0. Hiyo ni katika mwendelezo wa kupeleka muziki mnene wa kituo hicho machachari cha redio kwa wananchi,
   Nahodha wa Muziki Mnene Dennis Ssebo akiongoza kikosi kazi chake kusalimiana na wenyeji wao Mlandizi veterans kabla ya kuanza kwa mtanange wao huko Mlandizi
  Wananchi wakishudia mpambano wa Muziki Mnene na Mlandizi veterans.

  0 0
  0 0

  Taswira ya Uwanja wa Kaitaba ulivyo kwa sasa.

  Mwakilishi kutoka shirikisho la soka Duniani (FIFA) baada ya kukagua maendeleo ya uwekaji nyasi bandi katika uwanja wa mpira wa Kaitaba Amewaomba mafundi kuongeza kasi ili ukamilike kwa muda uliopangwa. Mwakilishi huyo wa FIFA Mhandisi Kelvin Macklain, alitua Bukoba wiki iliyopita na kukagua hatua kwa hatua uwanja huo na alifika hapo kukagua hatua za mwisho kabla ya nyansi husika kuanza kutandazwa, ambazo tayari zipo katika uwanja huo. 
  Hata hivyo Katibu wa chama cha Soka Wilaya ya Bukoba Malick Tibabimale, alisema kuwa sehemu ya kati ya uwanja itakamilika ndani ya mwezi mmoja, na timu ya Kagera sugar itaanza kuutumia uwanja huo baada ya mechi zake nne za mzunguko wa kwanza. 
  Timu ya Kagera Sugar kwa sasa itaendelea kutumia Uwanja wa Musoma kama uwanja wake wa nyumbani katika Ligi kuu ya vodacom iliyoanza kutimua vumbi jumamosi septemba 12, 2015.
  Nyasi bandia zikiwa zimewekwa pembeni ya Uwanja tayari kwa kutandikwa katika Uwanja huo

  Mhandisi kutoka kampuni ya Artificial Grass africa, wanaojenga uwanja huo Pierre De Groote baada ya kuukagua Uwanja huo alisema watamaliza kazi yote mwezi Desemba mwaka huu 2015.Mhandisi Kelvin Macklain Mwakilishi kutoka FIFA akifanya vipimo katika Uwanja wa Kaitaba unaoendelea kujengwa mpaka sasa. Picha zote na Faustine Ruta wa bukobasports.com
  Sehemu ya katikati ya Uwanja wa Kaitaba ambayo itakamilika mwezi huu wa tisa.
  Picha zote na Faustine Ruta wa bukobasports.com

  0 0


  0 0

   KIWANJA KINAUZWA NUSU HEKARI, KIMEPIMWA, KIPO, TEGETA WAZO, DAR ES SALAAM.  BEI NI TSH 70M, 
  KWA MAWASILIANO PIGA, No.0784-577087 Kisali.


  0 0

   Viongozi  wa ACT  wazalendo Iringa  wakijiandaa kwa  wimbo  wa Taifa jukwaani wakati wa uzinduzi wa kampeni  zao kwenye uwanja wa Mwembetogwa jana  mjini Iringa jana

  Mgombea ubunge  jimbo la Iringa mjini Chiku  Abwao  akiwahutubia  wananchi  katika  uzinduzi wa kampeni kwenye uwanja wa Mwembetogwa jana

  Mgombea ubunge  jimbo la Iringa mjini Chiku  Abwao  akiwahutubia  wananchi  katika  uzinduzi wa kampeni kwenye uwanja wa Mwembetogwa jana
  Msanii Baba  Revo  akiwa na Chiku Abwao

  0 0

   Mwanaharakati wa kutetea wanawake na mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bonah Kaluwa (kulia), akizungumza na wanawake wakati akifungua kampeni ya kupinga ukatili wa jinsia dhidi ya wanawake katika Soko la Tabata Muslim lililopo mtaa wa Msimbazi,  Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa mtaa huo, Tatu Lazaro na Mwenyekiti wa mtaa huo, Beatries Mkama.

  Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wadau wapinga ukatili wa kijinsia masokoni.
  Mgeni rasmi Bonah Kaluwa akiwa katika picha ya pamoja na wanawake wapinga ukatili wa kijinsia wa Tabata Muslim.
  Mgeni rasmi akiondoka eneo la mkutano.
  Maofisa wa Shirika la Equality for Growth (EfG), wakiwahamasisha wananchi kujaza fomu za kuwa mabalozi wa kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake masokoni. 

  0 0

  TIMU ya Maafande wa JKT Oljoro ya jijini Arusha inayoshiriki ligi daraja la kwanza imeshindwa kuonyesha makali yake mbele ya wadogo zao  timu ya AFC Arusha inayoshiriki ligi daraja la pili baada ya kutoka suluhu ya bao 1-1 katika ufunguzi wa michuano ya Nyerere Cup 2015.

  Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, uliwashuhudia maafande hao wa Oljoro wakianza kucheka na nyavu za AFC baada ya kujipatitia bao lake kupitia kwa mchezaji Swalehe Idd alilofunga kwa njia ya Penalti mnamo dakika ya 58, iliyosababishwa na mabeki wa timu pinzani kunawa mpira katika eneo la hatari.

  Vijana wa AFC walionyesha juhudi zao kwa kulishambulia lango la Oljoro ambapo walifanikiwa kusawazisha bao mnamo dakika ya 88 kupitia kwa mshambuliaji wao Wandima Malechela baada ya kuachia  shuti kali lililokwenda moja kwa moja vyavuni.
  Ufunguzi huo ni utangulizi tu wa Mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 13 yaliyoandaliwa na kampuni ya BIMO Media yenye kauli mbiu "Uchaguzi wa Amani  2015, ndio taifa moja kwa maendeleo ya utalii nchini" na yatafikia kilele siku ya kilele tarehe 19 mwezi huu katika viwanja vya Makumbusho Arusha.

  Akifungua mashindano hayo kwa niaba ya mkurugenzi wa jiji la Arusha Idd Juma,  Afisa Elimu jiji la Arusha kwa shule za sekondari Josephat Ntabindi alieleza kuwa mashindano hayo ni humimu hasa kwa watoto hao wenye vipaji kuonyesha uwezo wo huku wakikuza uelewa kwa vijana wadogo na kumuenzi hayati baba wa taifa Mwl Julias Nyerere ambaye pia alikuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha michezo hadi kugharamia kambi za timu ya Taifa kitendo ambacho kwa sasa hakipo.

  Naye mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano ya Bimo Media Bertha Ismail alisema  maadhimisho hayo yataambatana na mashindano ya kila mwaka ya ki- elimu  ya uandishi wa insha,makala pamoja na uchoraji  picha juu ya masuala ya utalii  kwa wanafunzi wa shule za msingi 25 zilizopo  Arusha.

  “ Lengo ni  kuhamasisha uchaguzi wa mwaka huu  kufanyika kwa amani vile vile kuhamasiha watu  kuhudhuria hifadhi za utalii zilizoasisiwa na Mwl Nyerere na tunategemea Zaidi ya wanafunzi 700 watashiriki  katika shindano hilo la isha.”ismail alifafanua.

  Timu za nyota academy,Future Stars,Kijenge Youth,Rolling Stone,Young Life na palloti zitachuana na washindi watakabidiwa zawadi mbalimbali ikiwemo vikombe na fedha.

  0 0


older | 1 | .... | 973 | 974 | (Page 975) | 976 | 977 | .... | 3272 | newer