Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

WASANII WAMUUNGA MKONO SAID FELLA

$
0
0
 Mgombea wa nafasi ya udiwani katika kata ya Kilungule Said Fella (kushoto) akiteta jambo  na mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Mbagala Issa Mangungu, wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani ambazo zimezinduliwa jana.
Msanii Richard  Maviko, (katikati) akiwa na wasanii wenzake  wakitoa salamu maalum ya kumuunga mkono mgombea wa udiwani katika Kata ya Kilungule Said Fella, ambaye  amezindua rasmi kampeni katika kata hiyo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Lameck Ditto akiongea kwa niaba ya wasanii wenzake  ambao walikuwepo katika uzinduzi wa mgombea wa udiwani kata ya Kilungule iliyopo.


MWINYI LAUNCHES THE UDSM ENTREPRENEURSHIP CENTRE

$
0
0
 Bank M’s deputy CEO Ms. Jacqueline Woiso speaking during the official launch of the UDSM refurbished learning centre last Saturday at the UDSM library grounds. The learning centre has been built by the Rotary Clubs of Dar es salaam in partnership with Bank M Tanzania plc.

 The former president of Tanzania Hon. Ally Hassan Mwinyi cuts the ribbon marking the launch of the state of the art learning Resource Centre at the University of Dar es salaam last Saturday, the centre has been refurbished by the Rotary Clubs of Dar es salaam in partnership with Bank M. Others in the photo from left are The UDSM library Director Dr. Amina Kabudi, Bank M’s Deputy CEO Ms. Jacqueline Woiso,The Rotary Dar Marathon Board Chair Ms. Sharmila Bhatt and the Rotary District 9211 governor Robert Wagga Nsibirwa (Right).

BANK OF AFRIKA TANZANIA YAKUSANYA ZAIDI YA MILIONI 210 KUSAIDIA MATIBABU YA WATOTO WANAOZALIWA NA MIGUU ILIYOPINDA

$
0
0
  Mkurugenzi Mkuu wa Bank of Africa nchini Bw. Ammishadai Owusu-Amoah akimkabidhi Ofisa Mtendaji Mkuu wa hospitali ya CCBRT mfano wa hundi wenye ya dola za kimarekani 100,000 kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda. Nyuma ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mhe. Ali Hassani Mwinyi na Mwenyekiti wa Bodi ya Bank of Afrika Mwanaidi Majaar.
 Balozi Mwanaidi Majaar,Mwenyekiti wa Bodi Bank of Afrika akihutubia wadau mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo. Balazo anasema BOA wamejizatiti kurudisha kwa jamii wanayoihudumia na harambee ya kutibu watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda ni moja ya mafanikia ya taratibu wao.
 Matembezi ya hisani ya pamoja yaliyoandaliwa na BOA na CCBRT hospitali kutoka Leaders clup mpaka CCBRT kuadhimisha kilele cha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya matibabu ya watoto wanaozaliwa na miguu iliyopinda.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akihutibia na kupongeza kwa dhati juhudi zilizofanya na zinazoendelea kufanywa na  Bank of Africa kwa kujali jamii na kuhusia wadau wengine pia kuiga mfano wa BOA
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mh. Ali Hasssan Mwinyi akimsalimia mtoto aliyeshiriki katika matembezi hayo.
Matembezi ya hisani  kuadhimisha kilele cha ukusanyaji fedha yakiendelea kueleka hospital ya CCBRT

NA  FRANCIS DANDE

RAIS wa Awamu ya Pili, Ali Hssan Mwinyi, jana aliongoza  matembezi ya hisani ya kilometa tatu kutoka Leaders Club, Kinondoni hadi Hospitali ya CCBRT Msasani kwa ajili ya kuchangia  matibabu ya watoto waliopinda miguu.

Matembezi hayo yaliyodhaminiawa  na Benki ya Afrika - Tanzania, lengo kuu lilikuwa ni kukusanya dola za marekani laki moja kwa madhumuni ya kugharamia watoto wenye miguu iliyopinda nchini kote. Ilikuwa ni kilele cha kampeni ya  ukusanyaji wa dola za Marekani laki moja iliyozinduliwa mwezi Aprili mwaka  huu.
Kupatikana kwa fedha hizo kutawezesha  CCBRT kutoa matibabu ya gharama nafuu kwa watoto  400 wenye ugonjwa wa kupinda miguu nchini kote,ilikuyabadili  maisha  yao na kuwa  ya kawaida.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo jana,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Benki ya Afrika – Tanzania, Mwanaidi Maajar, alisema: “Benki ya Afrika – Tanzania imedhamiria kurejesha kwa jamii kile  inachopata  kwa kuwa inaendesha  shughuli  zake, kwa kuchangia mahitaji mbalimbali ya jamii husika. Tumeona umhimu wa kuhimiza  usaidizi katika suala hili jema, kwa kuwa  CCBRT inatoahuduma kawa jamii maskini kwa kuondoa vikwazo mbalimbali ili jamii husika iweze  kupata  matibabu,” alisema Mwanaidi .

Aidha , Ofisa Mendaji mkuu wa CCBRT,Erwin Telemans alisisitiza: “ CCBRT inatoa shukrani za pekee kwa  Benki ya Afrika –Tanzania kutokana na ukarimu wao katika kipindi chote  cha kampeni hii. Maisha ya  a mamia ya  watoto wenye ugonjwa wa kupinda miguu watapona kwa uhakika kutokana na matibabu watakayopatiwa na CCBRT, na hatutaweza kuya badili maisha  ya watoto hao bila  kupata msaada kutoka kwa washirika wetu wakarimu kama Benki ya Afrika – Tanzania.”

MAGUFULI ALIVYOPOKELEWA NDANI YA JIMBO LA PERAMIHO MKOANI RUVUMA LEO.

HIVI NDIVYO MAGUFULI ALIVYOITIKISA RUVUMA LEO,MAELFU YA WATU WAJITOKEZA KUMSIKILIZA

$
0
0
Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Mgufuli akiweka shada la Maua kwenye kaburi la Marehemu Kapteni Komba aliyezikwa kijijini kwao Lituhi mkoani Ruvuma.

 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Songea waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Maji Maji mjini  humo mkoani Ruvuma,Mgombea huyo ambaye anawaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano,amewaambia kuwa katika serikali yake wakulima hawatokopwa mazao yao, mbolea zitapatikana kwa wakati, barabara zitaboreshwa ,elimu bure mpaka kidato cha nne, kuongeza maslahi ya walimu pamoja na kuboresha huduma za afya. 
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa mji wa Songea, ambapo alisema katika serikali yake wakulima hawatokopwa mazao yao, mbolea zitapatikana kwa wakati, barabara zitaboreshwa ,elimu bure mpaka kidato cha nne, kuongeza maslahi ya walimu pamoja na kuboresha huduma za afya. 
 Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akipokea Ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mgombea Urais kupitia chama hicho, Dk Magufuli wakati wa mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha mkoani Ruvuma.
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Nyasa, Stelah Manyanya katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Lituhi,ambapo pia alimkabidhi Ilani ya chama hicho.

 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge wa Jimbo la Mbinga Ndugu Sixtus Mapunda kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mbinga mjini.
 Dk Magufuli akishuka kwenye Kivuko cha Mto Ruhuhu akitokea Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe kwenda Mbinga  mkoani Ruvuma kuendelea na kampeni za urais ubunge na udiwani. Dk Magufuli ameahidi kujenga daraja la mto huo.

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mkazi wa mji wa Peramiho ambaye ni mlemavu wa ngozi,jioni ya leo mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa mji huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Dk Magufuli akimsalimia mmoja wa walemavu waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga.


 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCm Dk. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Songea mjini ambapo aliwataka wananchi hao kumpa kura nyingi Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli kwenye uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25,kwa sababu ni Muaminifu,muadilifu na ni mchapa kazi.
 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Ndugu William Lukuvi akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Maji Maji jioni ya leo.
 Maelfu ya Wananchi wakiwa wamefurika ndani ya uwanja wa maji maji mjini Songea jioi ya leo kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,mkoani Ruvuma jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe aliwahutubia wananchi hao.


HALI YA KIPINDUPINDU MOROGORO BADO TETE IDADI YA WAGONJWA YAONGEZEKA.

$
0
0

Hali ya ugonjwa wa kipindupindu mkoani Morogoro imeendelea kuwa tete baada ya idadi ya wagonjwa wa kipindupindu kungezeka hadi  kufikia wagonjwa 45 ambao wanaendelea na matibabu katika kambi maalum katika hospitali ya sabasaba mjini Morogoro.

 
Akizungumza na mtandao huu afisa afya mkoa wa Morogoro Carlesilas Lyimo amesema kutokana na kasi ya ongezeko la kipindupindu maafisa afya wamefanya operesheni katika maeneo mbalimbali yanayotoa huduma za chakula na vinywaji na kufanikiwa kukamata na kumwaga pombe za kienyeji zaidi ya lita 770, kuwachukulia hatua wafanyabiashara wa chakula wanauza vyakula bila utaratibu pamoja na kutoa dawa za kuwakinga na kipindupindu majumbani kwa watu 410 wengi wao wakitokea kata ya kilakala.
 

Nao wananchi wa mji wa Morogoro wameeleza wasiwasi wao juu ya kuongezeka idadi ya wagonjwa wa kipindupindu ambapo wametupia mamlaka ya maji safi na maji taka Moruwasa kushindwa kutoa huduma ya maji kwa wananchi katika baadhi ya maeneo hali inayosababisha wananchi kulazimika kutumia maji ya mito ambayo si salama.

RAIS KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA KIMBAU MAFIA

$
0
0
 Baadhi ya wanajeshi wakiwa wamebeba jeneza la Marehemu Kanali Mstaafu Ayub Kimbau aliyewahi kuwa mbunge wa Mafia wakati wa Mazishi yake huko Kilwa leo jioni.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la aliyewahi kuwa Mbunge wa Mafia Kanali Mstaafu Marehemu Ayub Kimbau huko Mafia leo jioni.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo na watoto wa marehemu Kanali Mstaafu Marehemu Ayub Kimbau wakiomba dua wakati wa mazishi ya Mbunge huyo wa Zamani wa Mafia yaliyofanyika huko Mafia leo jioni.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma(aliyeketi na mke wa Marehemu kushoto) wakimfariji mke wa Marehemu Kanali Mstaafu Nyumbani Kwake Mafia wakati wa mazishi ya Mbunge huyo wa zamani wa Mafia leo jioni.
(picha na Freddy Maro)

TANGAZO KWA UMMA: KWA WAHITIMU WA SHAHADA, STASHAHADA, ASTASHAHADA NA WENYE UJUZI KATIKA KADA MBALIMBALI


BBC DIRA YA DUNIA JUMATATU 31/08/2015

UZINDUZI WA KAMPENI JIMBO LA MOROGORO MJINI

$
0
0
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini wakiwaasa wakazi wa Jimbo la Morogoro Mjini Kumchagua MH John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mgombea Ubunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh aziz Abood Akiwahutubia wananchi na wakazi wa Jimbo la Morogoro Mjini waliojitokeza kwenye uzinduzi wa Kampeni za  Ubunge za Jimboni humo.


Wakazi wa Jimbo la Morogoro Mjini waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa Kampeni za Ubunge na Madiwani wa Jimbo hilo. 

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

DC PAUL MAKONDA AZINDUA VITABU VYA MWL.LILIAN NDEG

NITASHIRIKI UCHAGUZI KWA AMANI

$
0
0
 Wanahabari wakimsikiliza Mkurugenzi  Mtendaji wa Baraza la Dini Mbalimbali la Amani  Tanzania  Thomas Godda  juu ya kuwahimiza wanachi kwenda kupiga kura kwa amni  na kumchanguwa kiongozi bora leo jiji Dar es Salaam   
 Mkurungenzi  Mkuu wa Global Peace Foundation Tanzania Martha Nghambi juu ya wananchi kupiga kula kwa amani nautulivu  na  kujitokesa kwa wingi  siku ya kupiga kula kikao hicho kimefanyika  leo Jiji Dar es Salaam
Mkurugenzi  Mtendaji wa Baraza la Dini Mbalimbali la Amani  Tanzania  Thomas Godda na Mkurungenzi  Mkuu wa Global Peace Foundation Tanzania Martha Nghambi wakiwa katika picha ya pamoja leo jiji Dar es Salaam  Picha na Emmanul Massaka wa Globu ya Jamii

TANGAZO KWA UMMA:JESHI LA POLISI TANZANIA LINAWAITA KWENYE USAILI

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA POLISI TANZANIA

 

RPC.                                                                                              Ofisi ya Kamanda wa Polisi,                                                                                                                                                                                                                                                                                                   Mkoa  wa  Mbeya,                                                                                    

Namba ya simu 2502572                                                                                              S. L. P. 260,

Fax - +255252503734                                                                                            MBEYA.             

              tanpol.mbeya@gmail.com

                

TANGAZO KWA UMMA.

JESHI LA POLISI TANZANIA LINAWAITA KWENYE USAILI WAHITIMU WALIOORODHESHWA WA SHAHADA, STASHAHADA NA ASTASHAHADA. USAILI UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE 03.09.2015 HADI TAREHE 04.09.2015 KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI HADI SAA KUMI JIONI KATIKA MAENEO YAFUATAYO:-

·         FANI YA UTAWALA, UCHUMI, USIMAMIZI WA SHERIA NA UTEKELEZAJI [BALE], UALIMU, UANDISHI HABARI, UHANDISI MADINI [MINING ENGINEERING], UGAVI, LUGHA, USHAURI NASIHI, KATIBU MUKTASI, LAND SURVEY CATHOGRAPHER NA GEOMATICS WATAFANYA USAILI KATIKA CHUO CHA TAALUMA YA POLISI DAR ES SALAAM [DPA] KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM.


·         MAFUNDI MAGARI, MATENGENEZO YA PIKIPIKI, MAFUNDI MATENGENEZO YA UMEME WA MAGARI [AUTO ELECTRICAL], MAFUNDI RANGI ZA MAGARI, MAFUNDI MAGARI, MAFUNDI USHONAJI,MAFUNDI BODY ZA MAGARI NA MADEREVA. USAILI WA KADA HIZI UTAFANYIKA KIKOSI CHA POLISI UFUNDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.



·         MATENGENEZO YA KOMPYUTA, FAX & PHOTOCOPY MACHINES NA MAWASILIANO YA REDIO [DIPLOMA IN RADIO COMMUNICATION], USAILI WAO UTAFANYIKA NYUMA YA KIKOSI CHA UFUNDI YAANI TEHAMA KEKO CHINI.


·         WAKEMIA, BAILOJIA [MOLECULAR BIOLOGY] USAILI UTAFANYIKA MAKAO MAKUU YA POLISI YALIYOPO MAKUTANO YA BARABARA YA OHIO NA GHANA JENGO LINALOTAZAMANA NA POSTA HOUSE.



·         KADA ZA AFYA USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA AFYA KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.


·         MANAHODHA NA MAFUNDI MITAMBO WA MELI, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA WANAMAJI KILICHOPO KARIBU NA JENGO LA MAHAKAMA YA RUFAA.


·         DAKTARI WA WANYAMA, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA MBWA NA FARASI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.


·         MAFUNDI AC ZA MAJUMBANI, ARCHITECTURE DRAFTMAN, QUANTITY SURVEYORS, CIVIL ENGINEER, WELDING & FABRICATION, UMEME WA MAJUMBANI, PAINTING, ALUMINIUM & GLASS WORK, PLUMBING, MOSONRY, MOTOR REWINDING, HYDRO GEOLOGY DRILLING WELL, REFRIGERATION & AIR CONDITIONING. USAILI WA KADA HIZI UTAFANYIKA KIKOSI CHA POLISI UJENZI NDANI YA KAMBI YA POLISI BARRACKS KURASINI KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.


·         FANI ZA BENDI, BRASS BENDI, WOODWIND, STRING JAZZ NA PERCUSSIVE, USAILI WAO UTAFANYIKA KIKOSI CHA BENDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.


·         FANI YA URUBANI,USAILI  UTAFANYIKA  KIKOSI CHA ANGA KILICHOPO UWANJA WA NDEGE NDOGO WA ZAMANI WA J.K.NYERERE DSM.

MUHIMU:

1.      MWOMBAJI AFIKE KWENYE USAILI AKIWA NA NAKALA HALISI YA VYETI VYOTE VYA MASOMO/TAALUMA [ACADEMIC TRANSCRIPT (S)/CERTIFICATE (S) YAANI KIDATO CHA NNE, SITA, CHUO NA CHETI CHA KUZALIWA. KIAPO CHA KUZALIWA HAITAKUBALIWA.

2.      MWOMBAJI ALIYEITWA KWENYE USAILI ATALIPIA GHARAMA ZA UPIMAJI AFYA SHILINGI ELFU KUMI (10,000/=), USAFIRI, CHAKULA NA MALAZI KWA MUDA WOTE WA ZOEZI LA USAILI.

3.      AMBAYE HATAHUDHURIA USAILI KUANZIA SIKU YA KWANZA HATAPOKELEWA.

ILI KUPATA/KUONA ORODHA YA MAJINA, TEMBELEA www.policeforce.go.tz

Imetolewa na:

[AHMED Z. MSANGI – SACP]


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

JOTO LA ASUBUHI LA EFM 93.7 Jumanne septemba 1, 2015

LOWASSA KATIKA KAMPENI MJINI MAKAMBAKO NA NJOMBE

$
0
0
Umati wa wananchi wa Mji wa Makambako, Mkoani Njombe wakiwa wamekusanyika kwenye Uwanja wa Polisi Makambako, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa

Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Lawrence Masha akihutubia kwenye Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja Polisi Makambako, Leo Agosti 31, 2015.
Taswira zikichukuliwa.

Waziri Mkuu wa Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Polisi, Makambako leo Agosti 31, 2015.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Makambako, waliofurika kwa wingi wenye Polisi Makambako, Mkoani Mkoani Njombe leo Agosti 31, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwasili Njombe. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA



CCM JIMBO LA KAWE YAZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU YAMNADI KIPPI WARIOBA

$
0
0
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (katikati mbele), akisindikizwa na wanachama wa chama hicho, alipowasili katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati CCM ilipozindua kampeni kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kulia) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni kwaajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ (kulia) akimpongeza Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba baada ya kumkabidhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’ (kushoto) akimtambulisha Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Kippi Warioba baada ya kumkadhi Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba (kulia), akiusalimia umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, baada ya kutambulishwa na kukabidhiwa Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, wakati wa uzinduzi wa kampeni jimboni humo, jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Katibu Mwenezi wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gadafi’.
Mgombea  Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kippi Warioba akizungumza umati wa wanachama wa CCM na wananchi waliofurika katika viwanja vya Shule ya Msingi Boko Kata ya Bunju, wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

HUBIRINI AMANI, USALAMA, DEMOKRASIA NA MAENDELEO ENDELEVUWATU -BAN KI MOON

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, New York 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amewaasa Maspika wa Mabunge Duniani kuhakikisha kwamba wanakuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa Malengo na Ajenda Mpya za Maendeleo Endelevu, kwa kushirikiana na Serikali zao na Asasi za Kijamii. 
“ Mnakutana katika kipindi ambacho dunia inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo ya wimbi kubwa la wakimbizi wanaokimbia vita na machafuko katika nchi zao, wimbi ambalo halijawahi kutokea tangu vita kuu ya pili ya dunia”. 
Ban Ki Moon ameyasema hayo siku ya jumatatu wakati akifungua mkutano wa Nne wa Maspika wa Mabunge Duniani ambao hufanyika kila baada ya miaka mitano. Mkutano huu wa siku tatu unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na umeandaliwa na Chama cha Kimataifa cha Wabunge ( IPU). Na kuongeza. 
“ Tunachagizwa kuimarisha jitihada na juhudi za kuhubiri Amani, usalama, maendeleo endelevu na haki za binadamu duniani kote. 
“ Watu wanataka elimu, wanataka huduma bora za afya, na fursa zaidi za ajira. Wanataka kuishi pasipo kuwa na hofu. Wanataka kuziamini Serikali zao na Taasisi zake. Wanataka kuheshimiwa kwa haki za binadamu na haki ya kuzungumza na kusikilizwa katika maamuzi yanayohusu maisha yao” akasema Ban ki Moon. 
 Maspika wanaohudhuria mkutano huu, wanatoka katika mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea. Ujumbe wa Tanzania, unaongozwa na Mhe. Ann Mapinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
“Na pengine jambo muhimu kwenu na ambalo linawiana na majukumu yenu ni hili. Hiki ni kipindi ambacho mifumo ya kiserikali katika sehemu kubwa ya dunia inakabiliwa na changamoto ya kukosa kuaminiwa, uwakilishi na ushiriki” anaeleza katibu Mkuu 
Akizungumzia kuhusu ajenda na malengo mapya ya maendeleo, Ban Ki Moon amesema kuwa malengo hayo ambayo yapo 17 yamelenga zaidi katika maisha ya watu na sayari dunia. Na yanatoa mpango wa utekelezaji katika kumaliza umaskini, njaa na kujenga maisha yenye hadhi kwa wote bila ya kumwacha yeyote nyuma. 
 Aidha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema lengo namba 16 linazungumzia demokrasia, kwa kutoa wito jamii na taasisi jumuishi. Na kwamba suala la demkorasia limetawala katika andiko lote la malengo mapya ya maendeleo kama upinde wa fedha kwa kutia msisitizo wa upatikanaji wa raslimali, huduma za afya, elimu na fursa za ajira na zenye hadhi kwa wote. 
Akasisitiza kwamba kazi ya kutekeleza na kusimamia malengo haya ni kubwa, inayohitaji Serikali kufanya kazi na kwa ushirikiano wa karibu na Asasi za Kijamii, uhusiano ambao anasema ama unatoweka ama haupo kutokana na baadhi ya nchi kuweka masharti magumu dhidi Asasi za Kijamii.
 Mbali ya Ban Ki Moon, viongozi wengine waliozungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huu wa Maspika wa Mabunge ni pamoja na Rais wa Baraza Kuu la 69 la Umoja wa Mataifa. 
 Baada ya ufunguzi Maspika waliendelea na majadiliano ya jumla yaliyojikita katika maudhui ya Amani, demokrasia na maendeleo endelevu.
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon,  akifungua mkutano wa Nne wa  Maspika wa Mabunge  Duniani, siku ya Jumatatu, kulia kwake ni Rais wa IPU   Bw.  Saber Chowdhury na Katibu Mkuu wa IPU Bw. Martin Chungong  
 Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ann Makinda akiwa na ujumbe wake  akifuatilia kwa makini hotuba za  ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Maspika wa  Mabunge Duniani ulioanza siku ya jumatatu hapa Makao  Makuu ya Umoja wa mataifa
Maspika wa Mabunge kutoka  Mataifa yanayoendelea na  yaliyoendelea wakiwa katika  ufunguzi wa Mkutano wao wa Nne ambao  hufanyika kila baada ya miaka  mitano. Ufunguzi wa Mkutano huu umefanyika katika Ukumbi Mkuu wa  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

MO DEWJI FOUNDATION YAKABIDHI MATUNDU NANE YA CHOO BORA KWENYE SHULE YA MSINGI KIBAONI

$
0
0
DSC01579
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, Sundi Samike, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni zilizotolewa na MO Dewji Foundation (shilingi 14 milioni) na Doris Mollel Foundation shilingi 2.3 milioni).
DSC01583
Mwakilishi wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, chenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16. Duda amewataka wakazi wa manispaa ya Singida, kujenga utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali, uboreshaji wa mazingira ya shule, ili kuvutia wanafunzi kupenda shule.

JK ALIPOZINDUA RASMI AZAM TV

JK UNATUACHAJE??

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>