Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 957 | 958 | (Page 959) | 960 | 961 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Tina Kakolaki is a Tanzanian born musician who resides in the United States. She sings in Haya, Swahili and English. With two albums already in the market and one still a work in progress, Tina has attracted a significant number of fans worldwide. 
   As a member of the Tanzanian Diaspora, Tina has embraced both the Tanzanian and the American cultures and her music speaks for itself carrying the message of love. 
  Moreover, Tina has become one of the musicians in the United States who still have connections with their African roots and whose messages advocate for the power of love. In this interview, we will hear Tina explaining to us how she started and how she is still aspiring to reach the higher heights in her career. 
   You are welcome to watch this show on Friday September 4th from 4:00 pm to 5:00 pm (New York Time) on the following channels depending on who your service provider is. Total Duration: 60 Minutes. 
  The video below has only 36 minutes of the 60 minutes. To watch the entire 60 minutes of the show please see the details below. 
   Provider Channel Times Warner Cable (TWC) 67 and 1998 FiOS 36 RCN 85 
   To stream online tune to channel 4 @ www.mnn.org/4-culture-channel%20 
  every friday from 4:00 pm to 5:00 pm (New York Time). Thank 
  You and Stay Tuned.

  0 0

  Fuatilia kwa kina habari zilizoandikwa katika magazeti ya leo kuanzia kitaifa, kimataifa na michezo. SIMUtv; https://youtu.be/_saEPMJUrWA
  Leo ni siku ya Jumapili unajua magazeti ya leo yameandika nini juu ya kampeni za vyama? Tazama uchambuzi wa habari za magazetini. SIMUtv;http://youtu.be/WI24T51a5TI
  Pata dondoo za vichwa vya habari vilivyopewa umuhimu wa kwanza katika magazeti ya leo.http://youtu.be/KjNuFq3fqts
  Tazama udondozi wa kina wa habari zilizopewa kipaumbele katika magazeti ya juma pili ya  leo. SIMUtv; http://youtu.be/SGAKW8V160A
  Usisite kutazama uchambuzi wa habari motomoto za michezo zilizopewa uzito wa juu katika magazeti ya leo. SIMUtv; https://youtu.be/KjNuFq3fqts

  0 0

   Wakazi wa jiji la Dar es Salaam kutoka kushoto Anna Msinde,Mwanaidi Khaji na Mariam Rajabu wakielekezwa na Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Athuman Mwakipesile(kulia)  jinsi ya kujiunga na huduma ya M-Pawa inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupata riba na mikopo ya bei nafuu kupitia simu zao za mkononi  wakati wa kongamano la wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji(Financial and Investment Service fair) lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
   Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Athuman Mwakipesile(kushoto) akiwafafanulia jambo baadhi ya wateja wa Vodacom Tanzania waliofika katika banda la kampuni hiyo wakati wa kongamano la wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji(Financial and Investment Service fair) lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya Mbagala jijini Dar es Salaam,Idd Mawe akitoa semina ya mafunzo ya huduma ya M-pawa na M-pesa kwa Mawakala na wateja wa kampuni hiyo wakati wa kongamano la wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji(Financial and Investment Service fair) lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakitembelea mabanda ya Vodacom Tanzania na kupatiwa mafunzo mbalimbali ya kujiunga na huduma ya M-Pawa inayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kupata riba na mikopo ya bei nafuu kupitia simu zao za mkononi  wakati wa kongamano la wiki ya huduma za kifedha na uwekezaji(Financial and Investment Service fair) lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

  0 0


  Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira (kushoto), akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya chama hizo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala jijini Dar es Salaam leo.
  Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Mhe.  Zitto Kabwe akihutubia katika uzinduzi huo uliofanyika leo katika uwanja wa Zakheem Mbagala jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

  Mshauri wa chama cha ACT-Wazalendo, Prof. Kitila Mkumbo akihutubia kwenye uzinduzi huo.


  Viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiimba wimbo wa taifa.
  Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akiwatambulisha wagombea ubunge wa majimbo yote ya Dar es Salaam.
  Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akigawa ilani ya chama hicho kwa mgombea urais na mwenza wake.
  Mgombea Mwenza, Hamad Mussa Yusuph akihutubia kwenye uzinduzi huo.
  Mwana muziki Bwana misosi, akitoa burudani katika uzinduzi wa kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam leo.
  Umati wa Wananchi ukiwa katika uzinduzi wa kampeni wa chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem Magala Dar es Salaam leo.

  0 0


  0 0

  This Sunday morning Colonel Ayubu Shomari Mohamed Kimbau has passed away.  The Wake is being held at his home in the Victoria neighbourhood of Dar es Salaam.
  He had been a stalwart member of our Club for many years until his health deteriorated and kept him away.   His burial is planned for tomorrow evening on the island of Mafia.
  The late Col. Kimbau had for many years been the Member of Parliament for CCM in Mafia, up until 2000 when he stepped down to end a distinguished political career.  His son Omari is now poised to represent Ukawa from CUF there, after recently switching over from CCM to challenge an incumbent who was his father's successor.
  May Colonel Ayubu Kimbau's soul be Blessed to rest in eternal peace, and may our Almighty Father Bless and Strengthen his family, with their relatives, neighbours and friends to be able to bear the burden of grief in coming to terms with his departure from their lives, Amen.

  0 0

  Mwaka huu tumeshuhudia uhamaji wa wanachama  na viongozi  wa vyama kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine kuliko kipindi chochote katika historia ya vyama vingi  nchini Tanzania. Wengi wametafsiri hali hiyo kuwa ni ukuwaji wa demokrasia. Jambo ambalo lina ukweli wa aina fulani. 
  Lakini ukiangalia kwa undani wahamaji wa pande zote wamekuwa wakitoa sababu zinazofanana, na yumkini kuhama baada ya matukio yanayofanana kutokea katika  vyama vyao. Wengi wamehama mara baada kukosa nafasi ya kupeperusha  bendera za vyama vyao  katika  uchaguzi wa  urais, ubunge au udiwani. Mara wanapokosa nafasi wanahama  vyama vyao  wakidai demokrasia imebanwa au imebakwa. 
  Nimekuwa nikijiuliza , Je? Wangefanikiwa kupata nafasi ya kupeperusha bendera za vyama vyao katika nafasi walizoomba hizo sababu zingekuwepo? Maana najua wengine wamekuwa viongozi wakuu kwenye vyama  vyao na wameshiriki katika utaratibu huo huo wa kuteuana na kuchaguana katika nafasi mbalimbali na hata kushiriki kukata majina ya watu wengine, lakini kipindi hicho chote demokrasia haikubakwa. Hapa inaonyesha walivyokuwa wamekaa kwenye vyama kimaslahi zaidi na maslahi yao au matakwa yao  yasipofanikiwa wanatoa sababu mbalimbali  za kuhama, na wanapohamia kwenye vyama vingine wanataka wapewe nafasi za kugombea uongozi moja kwa moja. Watanzania tujiulize kweli hawa watu wana nia nzuri na watanzania au wanataka tu kukidhi  maslahi yao.
  Nilishawahi kuguswa na mbunge mmoja aliyehama  chama  tawala akiwa mbunge karibu na bunge kumaliza muda wake. Watu walimshangaa, na baadhi ya wenzake wakamwambia  mbona unahama kipindi hiki na kuacha kiinua mgongo cha ubunge.  
  Yeye alisimamia msimamo wake na  alichokuwa anakiamini na sio maslahi. Aligombea  ubunge kwa chama cha upinzani  katika jimbo  moja la Dar es Salaam  kula zake hazikutosha na nasikia mwaka  huu anagombea ubunge nyumbani kwao. Huyu hakusubiri mpaka  jina lake likatwe ndio ahame. Alifanya alichokiamini  sio maslahi kama wengine wanavyofanya sasa. Kuna watu wamehama  vyama vitatu kwa wiki moja wakitafuta nafasi ya ubunge. Kuna watu wamehama vyama  kwa makubaliano tu wapewe nafasi ya kugombea uongozi. Mimi najiuliza watu hawa kweli wana nia ya dhati ya kuwatumikia watanzania au ni wanachama maslahi?

  Utagundua wanachama maslahi katika vitu vingi, kwanza wanakuwa wanatanguliza agenda zao na si za chama, pili hawathubutu kuvaa mavazi rasmi ya  vyama vyao. hawataki kupambanuliwa kuwa wanachama wa chama walichojiunga nacho kupitia  vyazi rasmi la chama hicho. 
  Wote tunajua CCM wanavaa mashati ya kijani, na Chadema wanavaa kombati kama  vyazi rasmi la vyama vyao. Lakini leo hii ukiona mtu anadai kuwa yeye ni mwanachama wa Chadema au CCM au NCCR au TLP au NLD na amepewa dhamana ya kupeperusha  bendera ya   chama lakini anaogopa kuvaa  vazi rasmi   la chama husika(hata kofia tu), ujue hapo kuna tatizo. Watanzania  tuangalie kwa makini, wanachama tuangalie kwa makini tusije tukakuta  tumealika mamluki katika vyao vyetu. Kazi kwetu kutafakari na kufanya uamuzi sahihi tarehe 25/10/2015.

  0 0
 • 08/30/15--12:42: Blogu kuhusu kampeni za CCM
 • CCM Number One ni blogu maalumu iliyoanzishwa kwa ajili ya kuripoti habari zinazohusu mikutano ya kampeni ya mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan wanayoifanya katika mikoa mbalimbali nchini. 

  Lengo la blogu hii ni kuwafahamisha Watanzania na watu wengine duniani wanaofuatilia uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, nini ambacho wagombea hao wanakizungumza na kuwaahidi Watanzania kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020. 

  Pia imesheheni picha lukuki za wagombea hao wakiwa kwenye mikutano mbalimbali. Lengo ni kuwapa picha halisi Watanzania juu ya kile kinachotokea kwenye mikutano hiyo. 

  0 0

  Uongozi wa kitengo cha kimataifa cha makasha (TICTS) umepongeza juhudi zinazoendelezwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) za kuimarisha bandari ya Dar es Salaam. 
   Akiongea wakati wa kukaribisha kuwasili kwa meli kubwa kabisa kuwahi kufika katika bandari hiyo, Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) wa TICTS, Bw. Bw. Paul Wallace aliuita ujio huo kuwa wa muhimu sana kwa maendeleo ya bandari hapa nchini. 
   “Tunaona maendeleo makubwa ya kiutendaji katika bandari yanayopelekea mashirika makubwa kama Maersk Line kuleta meli zake katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki,” alisema mwishoni mwa wiki. 
   Alisema ujio wa meli hiyo pia ni uthibitisho wa ushirikiano wa wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa bandari ya Dar es Salaam inafunguka zaidi kimataifa. 
   Meli hiyo yenye urefu wa mita 255 ilitia nanga nchini 26 Agosti 2015 na kufunga gati katika kitengo cha Kontena kinachoendeshwa na Kampuni binafsi ya TICTS katika bandari ya Dar es salaam siku iliyofuata. Meli hiyo iliyoongozwa na nahodha Vladislav Barisovscy inajulikana kama Clemens Schulte ina uwezo wa kubeba makontena 5466. 
   Wakati wa safari hiyo ya kwanza, MV. Clemens Schulte yenye ukubwa wa Postmanax ilishusha makontena 250 na kupakia mengine 1300. Bandari ya Dar es Salaam iko katika mageuzi makubwa kuifanya ya kisasa zaidi ambapo moja ya maboresho yaliyofanyika hvi karibuni ni pamoja na kuanzisha mfumo wa malipo ya huduma za bandari kwa njia ya kielektroniki na kufunga mifumo mipya ya kisasa ya ulinzi ikiwa ni pamoja na CCTV. “Tunajivunia bandari yetu, tumeongeza ufanisi na tuko tayari kupanua zaidi huduma zetu,” alisema. 
   Bw. Wallace alisema TICTS iko katika harakati za kununua mashine kubwa zaidi za kubebea mizigo zenye thamani ya Tshs bilioni 46 zitakazowezesha kampuni hiyo kuhudumia meli kubwa zaidi ya Clemens Schutle na hivyo kuifanya bandari ya Dar kuwa shindani katika ulimwengu unaobadilika kwa kasi. 
   Kaimu Meneja Mawasiliano wa TPA, Bi. Janeth Ruzangi alisema ujio wa meli hiyo toka bandari ya Laem Chabang ya nchini Thailand ni uthibitisho wa kuzidi kuaminika kwa bandari hiyo kimataifa. 
   “Uaminifu huu unatokana na kuimarika kwa huduma tunazotoa,” alisema. Mkurugenzi wa Maendeleo TICTS, Bw. Donald Talawa alisema ujio wa meli hiyo ni kielelezo cha ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi ambao unatakiwa kuigwa na wadau wengine nchini. 
   Mara ya mwisho Kitengo hicho kupokea meli kubwa ilikuwa mwezi Februari 2014 ambapo meli iliyoitwa Msc Martina iliyokuwa na urefu wa mita 242. Pamoja na kuhudumia wateja wa ndani bandari ya Dar es Salaam pia inahudumia nchi za DRC Congo, Zambia, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi na Zimbabwe.
  Meli kubwa kabisa kuwahi kuingia katika bandari ya Dar es Salaam, Clemens Schulte.  Meli hiyo yenye urefu wa mita 255 ilitia nanga nchini 26 Agosti 2015 na kufunga gati katika kitengo cha Kontena kinachoendeshwa na Kampuni binafsi ya TICTS katika bandari ya Dar es salaam siku iliyofuata.
  Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi. Apolonia Mosha (katikati) akiwa na nahodha Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Capt. Abdul Mwingamno (kulia) na Kaimu Meneja Mawasiliano wa mamlaka hiyo, Bi. Janeth Ruzangi wakati wa tukio la kukaribisha kuwasili kwa meli kubwa kuwahi kufika katika bandari ya Dar es Salaam.  Meli hiyo, MV. Clemens Schulte, yenye urefu wa mita 255 ilitia nanga nchini 26 Agosti 2015 na kufunga gati katika kitengo cha Kontena kinachoendeshwa na Kampuni binafsi ya TICTS katika bandari ya Dar es salaam siku iliyofuata.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kimataifa cha Makasha (TICTS), Bw. Paul Wallace (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Maendeleo wa kampuni hiyo, Bw. Donald Talawa (kushoto) wakimsikiliza nahodha Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA), Capt. Abdul Mwingamno (kulia) wakati wa tukio la kukaribisha kuwasili kwa meli kubwa kuwahi kufika katika bandari ya Dar es Salaam.  Meli hiyo, MV. Clemens Schulte, yenye urefu wa mita 255 ilitia nanga nchini 26 Agosti 2015 na kufunga gati katika kitengo cha Kontena kinachoendeshwa na Kampuni binafsi ya TICTS katika bandari ya Dar es salaam siku iliyofuata.


  0 0
 • 08/30/15--13:30: SIMU TV: HABARI ZA USIKU HUU
 • 0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete , Jumamosi, Agosti 29, 2013, ameungana na mapadre na waumini wa Kabisa Katoliki na wananchi wa mji mdogo wa Lugoba, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, kusherehekea miaka 50 ya utawa wa Sista Perpetua Mlamwaza. 
   Rais Kikwete aliwasili kwenye Ukumbi wa Mkulima, Lugoba kiasi cha saa saba unusu mchana kuungana na wananchi hao katika sherehe ambako pia alikuwa anapongezwa Sista Ponsiana wa Paroko hiyo hiyo ya Lugoba kwa kufikisha miaka 25 ya nadhiri ya usista. 
   Miongoni mwa waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na baba mzazi wa Sista Perpetua, Mzee Ariseni, pamoja na dada yake mkubwa na wadogo zake. Masista hao wawili wanatoka Parokia ya Lugoba, eneo ambako shughuli za Kanisa Katoliki ziliingia kiasi cha miaka 100 iliyopita na Sista Perpetua alikuwa msichana wa kwanza wa Paroko ya Lugoba kujiunga na utawa wa Kanisa Katoliki alipoweka nadhiri ya kwanza mwaka 1965 kuwa Mtawa wa Shirika la Moyo Safi wa Maria Mgolole na kuweka nadhiri ya kudumu, miaka tisa baadaye, mwaka 1974. 
   Katika risala yao kwa Sr Perpetua, wananchi wa Lugoba wamempongeza Sista huyo kwa “safari ndefu ya maisha ya kumtumikia Mungu kwa kuwa sababu safari hiyo siyo ya mchezo…ina mabonde na milima, furaha na machungu na yote wewe Sr umeyashinda yote hayo katika miaka 50 iliyopita. Tunakupongeza sana kwa kututoa kimasomaso” 
   Sista Perpetua mwenye umri wa miaka 72, alizaliwa katika Kijiji cha Msoga, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani baba yake akiwa Mzee Ariseni na mama yake akiitwa Maria Nyau (Mama wa Mungu) ambao kwa pamoja walimpa binti yao jina la Marystella. 
   Akizungumza katika sherehe hizo, Rais Kikwete amempongeza sana Sr. Perpetua kwa ujasiri wake wa kuingia katika utawa katika kipindi na nyakati ambako uelewa wa watu wa eneo hilo ulikuwa tofauti sana na sasa. 
  “Wakati huo, uamuzi wa namna hiyo haukuwa uamuzi rahisi hata kidogo. Ulikuwa uamuzi mgumu lakini dada yangu Perpetua aliufanya uamuzi huo.” 
   Aidha Rais Kikwete ameongeza: “Nakupongeza pia kwa kuchagua maisha ya kujinyima na kuwatumikia watu. Ungeweza kabisa kuchagua maisha ya kubadili magauni kila siku na kwenda saloni, lakini hukuyataka maisha ya namna hiyo. Umetuletea heshima sana kwa uamuzi wako huu. Tunakushukuru na kukupongeza.”
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Sista.Perpetua(kushoto) aliyekuwa anaadhimisha miaka 50 ya utawa na Sista Ponsiana(kulia) aliyekuwa anaadhimisha miaka 25 ya utawa .Maadhimisho hayo yalifanyika katika kanisa Katoliki Lugoba jana. 
  Picha na Freddy Maro

  0 0

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kuombeleza kifo cha mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa mbunge wa muda mrefu wa Jimbo la Mafia, Mkoa wa Pwani, Kanali (mst) Ayubu Shomari  Mohamed Kimbau, ambaye aliaga dunia asubuhi ya leo,  Jumapili, Agosti 30, 2015 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam. 
  Katika salamu za rambirambi alizomtumia Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Eng. Evarist Ndikilo, Rais Kikwete ameeleza kusikitishwa kwake na taarifa za kifo cha Mzee Kimbau ambaye kwa miaka mingi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Mafia kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). 
  Amesema Rais Kikwete katika salamu zake: “Nimesikitishwa na taarifa za kuaga dunia kwa Mzee Ayubu Kimbau ambaye nimejulishwa kuwa amefariki asubuhi ya leo katika Hospitali ya Muhimbili. Mzee Kimbau atakumbukwa sana kwa utumishi wake wa umma na uzalendo wake kwa taifa lake kuanzia alipokuwa katika Jeshi  la  Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambako alipanda nafasi hadi kufikia cheo cha Kanali na baadaye katika uwakilishi wa wananchi wa Mafia katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.” 
  “Kupitia kwako, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, naungana na wananchi wote wa Mafia na wa mkoa wa Pwani kuomboleza kifo cha mmoja wa magwiji wa siasa na wauwakilishi wa wananchi katika nchi yetu. Nawaombeni mpokee salamu zangu za dhati ya moyo wangu katika kuomboleza kifo hiki,”amesema Rais Kikwete na kuongeza: 
  “Aidha, kupitia kwako naitumia familia ya Kanali Kimbau salamu zangu nyingi za pole. Wajulishe kuwa niko nao katika msiba huu mkubwa na kuwa msiba wao ni msiba wangu. Naelewa machungu yao katika kipindi hiki kigumu na nawaombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kuwapa nguvu, uvumilivu na subira. Naungana nao pia kumwomba Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Kanali Ayubu Shomari  Mohamed Kimbau. Amen.”


  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.


  30 Agosti, 2015


  0 0

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatarajia kuweka Wazi Daftari la Awali la Wapiga Kura katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba kuanzia tarehe 03/09/2015 hadi tarehe 07/09/2015 ili Umma uweze kupata nafasi ya kulikagua Daftari la Awali na kutoa taarifa za kufanyiwa marekebisho pale inapostahili.

  0 0

   Makundi kumi kati ya makundi 15 yaliyoshiriki katika kinyang’anyiro cha kuingia katika nusu fainali ya mashindano yanayokuwa kwa kasi hapa nchini ya Dance 100% yanayoandaliwa na kituo cha televisheni cha East Africa(EATV) chini ya udhamini wa kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania,yanaendelea ambapo mwishoni mwa wiki tulishuhudia hatua ya robo fainali kufanyika katika uwanja wa Don Bosco Oysterbay jijini Dar es Salaam na kushirikisha makundi 15 kutoka wilaya 3 za mkoa wa Dar es Salaam. 
   Makundi yaliyofanikiwa kuingia nusu fainali ni Wazawa Crew,Majokeri,Quality boys,The best,The best boys kaka zao,Team Makorokocho,The winners, The W.D, Cute babies na Team ya shamba. Mratibu wa mashindano hayo,Happy Shame,alisema kuwa katika kinyang’anyiro cha robo fainali hiyo walipata makundi 10 hayo ambayo yameingia moja kwa moja katika ngazi ya nusu fainali. 
  “Huu ni mwaka wa nne East Africa Televisheni tunaandaa mashindano haya chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania na mwaka hadi mwaka mashindano haya yamekuwa yakiongezeka kupata umaarufu na kuwavutia vijana wengi kila kona ya nchi yetu ambao wamekuwa wakijitokeza kushiriki”Alisema Shame. 
   Shame, aliongeza kwamba kundi litakaloibuka na ushindi katika mashindano haya ambayo pia yamekuwa yakionyeshwa na kituo cha televisheni cha East Afrika kila jumatano saa moja kamili usiku,litajishindia kitita cha shilingi milioni 5. 
  Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano haya,Matina Nkurlu alisema kuwa Vodacom inatoa udhamini kwa kutambua kuwa muziki na michezo ni maeneo ambao yanaweza kutoa ajira kwa vijana na kuweza kuwakwamua kimaisha. Alisema kuwa Vodacom inatambua kuwa jukumu la kukabiliana na tatizo la ajira hapa nchini sio la serikali peke yake bali pia ni la watu wote ikiwemo makampuni,taasisi za umma na za binafsi na ndio maana siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za kupambana na tatizo la ajira kupitia nyanja mbalimbali ikiwemo michezo , burudani na huduma mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo. 
  “Vodacom tunaamini kuwa vijana wanaweza kuleta mapinduzi makubwa katika sekta mbalimbali iwapo watawezeshwa,hivyo tunadhamini mashindano haya tukiamini kuwa vijana wenye vipaji wanaoshiriki wataweza kujitangaza na kujulikana ambapo katika siku za usoni ni rahisi kujiajiri kupitia katika sanaa”Anasema Nkurlu. 
   Aliwataka vijana waamke hususani wasichana wasibaki nyuma na watumie fursa kama hizi ili waweze kujikomboa kiuchumi 
  “Suala la ajira sio kufanya kazi ofisini tu bali kuna njia nyingi za kujiajiri na kujipatia mapato mojawapo ikiwa ni kupitia michezo,muziki na sanaa nyingine na Vodacom siku zote tutakuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za vijana kujikwamua kiuchumi”Alisisitiza Nkurlu.
   Vijana wanaunda kundi  la  Timu Makorokoro  wa  wilaya ya Temeke  jijijini Dar es Salaam, wakikongo nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la robof wa shininali ya shindano la Dance100%2015,lililofanyika kwenye viwanja vya Don bosco Oysterbay mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.
   Vijana wanaaunda kundi la  timu ya Shamba kutoka Temeke wakionyesha umahiri wa  kusakata dansi wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100% lililofanyika kwenye viwanja vya Donbosco Oysterbay jijini Dar es Salaam ,mwishoni mwa wiki.Shindano hilo  iliandaliwa  na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania. Makundi 10 kati ya 15 yalifanikiwa kuingia nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni.


   Vijana wanaounda kundi la The Winner Crews kutoka Kiwalani  jijini  Dar es Salaam, wakikongo nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la robofainali ya  shindano la Dance100%2015,lililofanyika kwenye viwanja vya Donbosco  Oysterbay jijini Da res Salaam  ambapo makundi 10 yalitinga nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni. Shindano hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

   Kundi la wasichana pekee la Cute Babies  kutoka Keko  wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wakionyesha umahiri wao  wa kudansi wakati wa robo fainali ya shindano la Dance 100% lililofanyika katika viwanja Don bosco Oysterbay  jijini ambapo makundi 10 yalitinga nusu fainali zitakazofanyika hivi karibuni, Shindano hilo liliandaliwa na  EATV na kudhaminiwa  na Vodacom Tanzania.
  Mashabiki wakifuatilia mashindano hayo

  0 0

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Ludewa mjini kabla ya kuanza kuwahutubia ,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo na kuhudhriwa na maelfu ya watu.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Ludewa waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika mjini humo.
  Mgombea Ubunge wa jimbo la Ludewa,aliyepita bila kupingwa Mh Deo Filikunjombe ,akisoma ilani ya CCM aliyokabidhiwa na Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,wakati alipokuwa akihutubia wananchi wa kijiji cha Mlangali wilayani Ludewa
  Wananchi wa mji wa Ludewa wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa mpira mjini Ludewa wakimshangilia mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
  Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiwa umezuiwa na Wananchi wa kijiji cha Mavanga wilayani Ludewa huku wakishangilia na kuimba  "JEMBE LA KAZI LIMEINGIA",ambapo Magufuli akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo hilo la Ludewa,Mh Deo Filikunjombe walisimama na kuzungumza na wananchi hao ikiwemo pia kuwaomba kura za kutosha ili wapate ridhaa ya kuwaongoza Watanzania katika awamu ya tano.
  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya walemavu waliokuwa wamefika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni kumsikiliza sera zake,Dkt Magufulia alieleza kuwa katika Ilani ya CCM,kwa awamu ya tano itawajali walemavu na kuwapa vipau mbele hasa katika masuala ya elimu,ya kijamii pamoja na kuwawezesha kiuchumi ili waweze kujishulisha vyema katika maisha yao ya kila siku
  Wananchi wa jimbo jipya la Madaba wakimsikiliza kwa makini mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia jukwaani  kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
  Wananchi wa Mlangali wilayani Ludewa wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hdahara wa kampeni,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia.
  Mmoja wa wakazi wa mji wa Ludewa akiwa na bendera yake,huku akimisikiliza mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano kwa nafasi ya Urais.
  Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukiwasili wilayani Ludewa kutoka mkoani Njombe.

  PICHA NA MICHUZI JR-LUDEWA

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba Gangilonga, Mkoani Iringa, Agosti 30, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, IRINGA.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia maelfu ya wananchi wa Iringa Mjini waliofurika kwenye Uwanja wa Sabasaba Gangilonga, Agosti 30, 2015. Katika Hotuba yake Mh. Lowassa alizungumzia namna atakavyotoa kipaumbele kwa wakulima ambapo amesema atafuta ushuru wa mazao kwa wakulima na kufuta kodi kwa vifaa vya michezo na burudani ili vijana waweze kunufaika na vipaji vyao.
  Umati wa Wakazi wa Mji wa Iringa Mjini ukiwa umefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Sabasaba Gangilonga, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, Agosti 30, 2015.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimsalimia kijana mwenye ulemavu (jina lake hakupatikana kwa haraka) aliyehudhulia Mkutano wa Kampeni ya Mgombea huyo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba Gangilonga, Iringa Mjini, Agosti 30, 2015. Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye.

  KUONA PICHA ZAIDI

  BOFYA HAPA AU BOFYA HAPA

  0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka (mwenye miwani) akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, Patrick Karangwa wakati alipokagua ujenzi wa nyumba za waathirika wa maafa Kijijini Mwakata, Kahama, tarehe 30 Agosti, 2015.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka akimsikiliza mwenyekiti Kijiji cha Mwakata wilayani Kahama, Ezekieli Ramadhani akitafsiri kwa Kiswahili shukrani zizokuwa zikitolewa kwa kisukuma na Bi. Rugumba Msenga kwa serikali kumjengea nyumba kutokana na nyumba yake ya awali kuathirika na maafa ya Mvua, wakati Katibu Mkuu huyo alipokagua ujenzi wa nyumba za waathirika hao zilizojengwa na SUMA JKT, tarehe 30 Agosti, 2015.
  Muonekano wa nyumba mpya ya muathirika wa maafa ya mvua kijijini Mwakata Kahama. Rugumba Msega (hayupo pichani ) ambayo amejengewa na serikali kupitia Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa usimamizi wa SUMA JKT, kulia ni makazi ya muda aliyokuwa amejengewa na serikali na mbele ya nyumba hiyo ni mabaki ya nyumba yake ya awali iliyoathirika na maafa hayo, tarehe 30 Agosti, 2015.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka akiagana na mwenyekiti Kijiji cha Mwakata wilayani Kahama, Ezekieli Ramadhani mara baada ya kukagua ujenzi wa nyumba za waathirika wa maafa ya mvua zilizojengwa na SUMA JKT, tarehe 30 Agosti, 2015, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji SUMA JKT, Kanali Felix Samillan na Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Gen, Mbazi Msuya (mwenye kofia ).
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka (mwenye miwani) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama ( kulia kwake), Benson Mpesya wakiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa shughuli za maafa Mwakata kutoka; Ofisi ya Waziri Mkuu, SUMA JKT, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kahama na Halmashauri ya Msalala mara baada ya kikao cha ujenzi wa nyumba za waathirika wa maafa ya mvua Mwakata, tarehe 30 Agosti, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa CCM wakati alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Uguja kuhudhuria katika Kikao cha Siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibar kilichofanyika leo katika ukumbi Ofisi hiyo Mjini Unguja.
  Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibar wakipitia makabrasha ya kikao hicho kabla ya kuanza leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiendesha kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) Zanzibar kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.


  0 0

  Daktari wa Kwanza Bingwa Mshauri wa Maradhi ya Moyo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Morogoro nchini Tanzania Dr.Harun Elmada Nyagori azawadiwa Tuzo ya Kimataifa na kutambuliwa na Baraza la Madaktari Bingwa wa shirikisho la Nchi za Ulaya(European Society of Cardiology) -London Uingereza'
  Akipewa hiyo Tuzo ya Heshima na Rais wa Shirikisho Hilo Prof.Pinto alimwelezea imekuwa Historia kubwa kumpata Daktari aliyewakilisha Mada za Utafiti wa Maradhi ya Moyo kutoka Tanzania na hawajawahi kumpata Mtanzania aliyewahi kuingia kwenye Shirikisho Hilo 
  Hivyo Dr Nyagori amefungua mlango kwa Madaktari wengine kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu hiyo taaluma ya magonjwa ya Moyo.
  Dr Nyagori akiwa na muasisi wa Kimataifa na Mwandishi wa Vitabu vikuu wa taaluma hiyo Prof.Eugine Brawnward 
   Dr Nyagori na Rais wa Shirikisho Hilo la Madaktari Bingwa wa Maradhi ya Moyo prof.Pinto Dr Nyagori amealikwa na Shirika la Utangazaji BBC kwa mdahalo maalumu kuhusu hiyo Tuzo,taarifa kamili zitarushwa Focus on Africa
  Dr Nyagori akiwa na wajumbe wenza walioteuliwa kuingia kwenye Shirikisho Hilo la Madaktari Bingwa wa Ulaya wakiwa na Rais wa Shirikisho Hilo Prof.Pinto

  0 0

  Kamishna wa Bima nchini Bw. Israel Kamuzora.

  Jovina Bujulu-MAELEZO
  WATANZANIA theluthi mbili hawana ufahamu wa kutosha kuhusu namna Bima inavyofanya kazi nchini hasa Bima ya Maisha na Mali.

  Hayo yamesemwa na Kamishna wa Bima nchini Bw. Israel Kamuzora alipokuwa akifunga mafunzo ya wiki ya huduma kifedha na uwekezaji mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

  Kamuzora aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kueneza ujuzi na ufahamu waliopata ili wananchi walio wengi waweze kunufaika na huduma za bima nchini.

  “Ninawaomba muwe mabalozi wazuri wa kueneza ufahamu juu ya faida za Bima kwa ndugu, jamaa na marafiki ambayo ni mojawapo ya mbinu za kujilinda kimaisha na kujikwamua katika umasikini”. Alisema Kamuzora.


older | 1 | .... | 957 | 958 | (Page 959) | 960 | 961 | .... | 3284 | newer