Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 959 | 960 | (Page 961) | 962 | 963 | .... | 3284 | newer

  0 0
  0 0


   Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Songea waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Maji Maji mjini  humo mkoani Ruvuma,Mgombea huyo ambaye anawaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-RUVUMA
  Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa mji wa Songea, ambapo alisema katika serikali yake wakulima hawatokopwa mazao yao, mbolea zitapatikana kwa wakati, barabara zitaboreshwa ,elimu bure mpaka kidato cha nne, kuongeza maslahi ya walimu pamoja na kuboresha huduma za afya. 

   Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akipokea Ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mgombea Urais kupitia chama hicho, Dk Magufuli wakati wa mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha mkoani Ruvuma.
   Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Nyasa, Stelah Manyanya katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Lituhi,ambapo pia alimkabidhi Ilani ya chama hicho.

   Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge wa Jimbo la Mbinga Ndugu Sixtus Mapunda kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mbinga mjini.
   Dk Magufuli akishuka kwenye Kivuko cha Mto Ruhuhu akitokea Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe kwenda Mbinga  mkoani Ruvuma kuendelea na kampeni za urais ubunge na udiwani. Dk Magufuli ameahidi kujenga daraja la mto huo.

   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mkazi wa mji wa Peramiho ambaye ni mlemavu wa ngozi,jioni ya leo mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa mji huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
  Dk Magufuli akimsalimia mmoja wa walemavu waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga.


   Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCm Dk. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Songea mjini ambapo aliwataka wananchi hao kumpa kura nyingi Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli kwenye uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25,kwa sababu ni Muaminifu,muadilifu na ni mchapa kazi.
   Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Ndugu William Lukuvi akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Maji Maji jioni ya leo.
   Maelfu ya Wananchi wakiwa wamefurika ndani ya uwanja wa maji maji mjini Songea jioi ya leo kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,mkoani Ruvuma jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe aliwahutubia wananchi hao.
    Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mbinga.
   Waanchi wakifuatilia hotuba ya Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha-Peramiho mkoani Ruvuma jioni ya leo.
   Wananchi wakishangilia 
   Umati wa wakazi wa Peramiho wakisikiliza hotuba ya Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni katika uwanja wa Tamasha ndani ya jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma. 
   Baadhi ya Wananchi wa Peramiho wakifurahia jamo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
   Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM,, dK John Magufuli akiwa na watoto aliowapatia zawadi alipokuwa akiondoka baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma
    Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa Mbinga.
   Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni za ccm leo jioni ndani ya uwanja wa Maji Maji mjini Songea.

   Wananchi wa Songea mjini wakishangilia jambo wakati mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Maji maji mjini humo.

  0 0

   Ndugu Wandishi wa Habari, 
  Mabibi na Mabwana,

  Napenda nichukue fursa hii kuwashukuru nyote hasa waandishi wa habari kwa kutenga muda wenu na kujumuika nasi kwa lengo la kutangaza rasmi kuanza kutumika kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 ambayo ilitangazwa kwenye gazeti la Serikali  la tarehe 14/08/2015 na kupewa Na. 328. Pia Sheria ya Miamala ya Kielektroniki, 2015 ambayo  ilitangazwa kwenye Gazeti la Serikali la tarehe hiyo hiyo na kupewa Na.329.


  Ndugu Wananchi,

  Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni nyenzo ya kisasa inayotumika kubeba na kusafirisha ujumbe, taarifa, takwimu, picha na sauti kwa kutumia njia na mifumo mbalimbali ya mawasiliano iliyopo, kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine au eneo moja kwenda eneo lingine kwa uharaka, ufasaha, kwa wakati na kwa kiwango cha ubora ule ule bila kujali umbali na mipaka iliyopo ya kijiografia. Matumizi ya TEHAMA yameleta mafanikio katika kuharakisha, kuboresha na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kuchangia kukuza uchumi na kuleta maendeleo nchini. Mathalani, wananchi walio wengi sasa wanapata huduma mbalimbali za kifedha, kulipia huduma (leseni, kodi, Ankara), matumizi ya mitandao ya kijamii, barua pepe na huduma mtandao kama vile Serikali mtandao, afya mtandao, kilimo mtandao, biashara mtandao, Elimu mtandao, n.k


  Ndugu Wananchi

  Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo kumekuwepo na changamoto mbalimbali kama vile wizi wa fedha kwa njia ya mtandao, uvujaji wa taarifa, kusambazwa kwa ujumbe wa matusi, picha chafu, uchochezi, udhalilishaji, vitisho kupitia mitandaoni. Vile vile kuna watu wachache ambao wanaharibu miundombinu ya mawasiliano, kwa mfano wanakata mkongo wa Taifa wa mawasiliano na mikongo mingine ya mawasiliano na hili lina athari kubwa sana kwa nchi yetu na kwa nchi za jirani ambazo zimeunganishwa kwenye mkongo wa Taifa wa mawasiliano.


  Ndugu Wananchi 

  Mtakumbuka kuwa, mnamo tarehe 1 Aprili 2015 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 na Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya Mwaka 2015. Pamoja na masuala mengine, sheria hizi zinabainisha makosa, kutambua ushahidi wa nyaraka za kielektroniki na pia kuainisha adhabu zinazokwenda pamoja na makosa mbalimbali ya kimtandao. Sheria hizi ni muhimu sana na zina manufaa makubwa kwenye jamii yetu haswa katika nyakati hizi ambapo matukio ya uhalifu wa mtandao yamekuwa yakiongezeka na kukosekana kwa Sheria hizi kumefanya Wananchi kutokuwa na mahala pa kukimbilia pale wanapokumbana na uhalifu kupitia mitandaoni.


  Aidha, ninatambua ya kuwa Sheria hizi zimepokelewa kwa hisia tofauti kutokana na uelewa mdogo kwa wengi wetu kuhusu sheria hizi. Vilevile ni ukweli usiopingika kuwa kumekuwa na tafsiri hasi kwa baadhi ya wananchi juu ya maudhui ya sheria hizi na kuzifanya zitafsiriwe kama kandamizi zaidi kitu ambacho ni tofauti na dhana na maudhi ya sheria hizi.  


  Kwa kutambua hilo, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia mara baada ya kupitishwa kwa SHERIA  hizi  ilianza kuwaelimisha wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya habari na kuwa na mikutano na makundi mbalimbali ya watekelezaji wa Sheria hizi ili kuwajengea uelewa ikiwemo Jeshi la Polisi, Waendesha Mashtaka, Wachunguzi, Wapelelezi, Mahakimu na Majaji kuhusu Sheria hizi kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaani Bara na Zanzibar. Aidha, ili kuhakikisha kuwa usimamizi na utekelezaji wa Sheria hizi unakwenda vizuri, Wizara itaendelea kuwajengea uelewa Wadau mbalimbali. 


  Ndugu Wananchi

  Tanzania siyo nchi ya kwanza kutunga sheria kama hizi. Kuna nchi mbalimbali duniani ambazo zimetunga sheria kama hizi, kwa mfano nchi ya Uingereza (UK Computer Misuse Act, 1990), India (IT Act, 2000), Malaysia (Computer Crime Act), Uganda (Computer Misuse Act, 2010), Korea ya Kusini (Information and Communications Network Act na Information and Communication Infrastructure Protection Act), Singapore (The Computer Misuse and Cyber security Act), Mauritius (Computer Misuse and Cybercrime Act, 2003), Marekani (Computer Fraud and Abuse Act, 1984) na nyingi nyenginezo. 


  Ndugu Wananchi,

  Serikali baaada ya kujiridhisha kuwa maandalizi yote muhimu ikiwemo elimu kwa umma na kujenga uelewa kwa watekeleza wa sheria hizi yamefanyika. Sasa, Sheria hizi zitaanza kutumika rasmi tarehe 01/09/2015. 


  Kwa hivyo, natoa rai na wito kwa wananchi wote kuwa tuzingatie “Matumizi Salama na sahihi ya Huduma za Mawasiliano na Mtandao kwa manufaa ya kila  mmoja  na kwa maendeleo ya Taifa letu. Mitandao ikitumiwa vema ina faida kubwa sana katika jamii yetu.


  AHSANTENI KWA KUNISIKILIZA

   Wanahabari kazini wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kuanza kutumika rasmi kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao na ya Miamala ya Kieletroniki za mwaka 2015. 
   Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (Mb), akiongea na waandishi wa habari kuhusu kuanza kutumika rasmi kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao na ya Miamala ya Kieletroniki za mwaka
  2015. Anayeangalia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bwana John Mngodo


  0 0


  0 0

  Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano Kampuni ya Tumbaku Tanzania na Kiwanda cha Kusindika Tumbaku (TTPL), Bw.Richard Sinamtwa (Kulia) akifafanua jambo kwa wadau wa tumbaku kutoka Zimbabwe walipotembelea kiwanda hicho kwa ziara ya mafunzo Mjini  Morogoro.
  Meneja Uhusiano wa Kiwanda cha Kusindika Tumbaku (TTPL), Bw. Mazehiew Folleto (Kulia) akifafanua jambo kwa wadau wa tumbaku kutoka Zimbabwe walipotembelea kiwanda hicho kwa ziara ya mafunzo Mjini  Morogoro.


  0 0

  Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo, baada ya kukaa kimya kingi sana tangu mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia  Chama cha Demokrasia na Maendeleo  chini ya mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa kuhamia chama hicho. Leo ameibuka na kusema  ya moyoni kuwa amejivua uanachama  rasmi wa chama cha Chadema pamoja na Ukatibu Mkuuu wa Chama hicho na kuachana  kabisa na siasa  kutokana na mambo yaliyokuwa yakifanyika ndani ya chama chake hayakumridhisha na hakukubaliana nayo.

  Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa pia amesema kuwa mambo yaliyotokea katika chama chake ndio maana ameamua kuachana na siasa  rasmi hii leo.
   Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika harakati za kupata taswira nzuri za aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.

  Baadhi ya wananchi pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dk.  Wilbroard Slaa leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Magreth Kinabo- maelezo
  SERIKALI imesema kwamba imeshalipa madeni ya walimu  ya kiasi cha Sh. bilioni 5.7 ambayo yaligungulika kihalali kati ya Sh. bilioni 19.6 zilizokuwa zinadaiwa kudaiwa,hivyo  kwa  sasa hakuna  malalamiko mwalimu ambaye hajalipwa.

  Aidha Serikali imependekeza kwamba   halimashauri  zilizowasilisha  madeni ambayo si  halali, yenye shaka, au watumishi wasio na madai, madai ya watumishi wasio na madai, madai ya watumishi waliokwishalipwa na waliowasilisha madai ya mishahara kama madai yasiyo ya mishahara wawajibishwe.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya  Fedha, Dkt. Servacius Likwelile wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

  Dkt.  Likwelile  alisema hayo wakati akitoa taarifa  ya  uhakiki wa madeni ya  walimu wa shule za msingi, sekondari na  Watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya  Ufundi Stadi.


  0 0


   
  Wanawake wameaswa kukipenda chama cha mapinduzi kwakuwa ndicho chama pekee kitakachowaletea maendeleo yanayotakiwa kwakuwa kinajua changamoto zinazo wakabili wananchi katika kipindi hiki. 

    
  Akizungunguza na  wanawake wa wa Kata ya Makolongoni Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa Rose Tweve  aliwataka wananchi kutobabaishwa na wapinzani kwani hawana nia njema na watanzania  na kusema kuwa chama hicho kina misingi ya kutetea amani ya Nchi.
   
  "sisi sote ni wanawake niwaombeni sana tukipigie kura chama cha mapinduzi kiweze kupata ushindi wa kishindo leo katika chama kuna mgombea mwenza mwanamke tazama hamsini kwa hamsini wahamasisheni vijana wenu pia waelezeni mazuri yalimo ndani ya ccm bila kuwaambia wataendelea kurub uniwa na kutumiwa kwa faida za wachache" alisema rose
    

  Alisema huu ndiyo wakati wa wanawake kujitokeza kwa wingi kukiunga mkono chama cha mapinduzi kwa kuwapigia kura wagombea wanaotokana na chama hicho kwakuwa kukipa nchi chama cha Upinzani ni kujisaliti wenyewe hiyo aliwaomba wanawake kuhakikisha wanakisaidia chama cha mapinduzi kiweze kushinda.


  0 0
 • 09/01/15--13:30: GO TAIFA STARS! GO!


 • 0 0


     Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Masasi kwenye uwanja wa Bomani ambapo aliwaambia kama atapewa ridhaa na wananchi hao ya kuiongoza Tanzania basi atahakikisha utendaji, ufanisi katika kuleta maendeleo nchini unaongezeka ikiwa pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata haki ya msingi.
    Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Masasi kwenye uwanja wa Bomani ambapo aliwaambia kama atapewa ridhaa na wananchi hao ya kuiongoza Tanzania basi atahakikisha utendaji, ufanisi katika kuleta maendeleo nchini unaongezeka ikiwa pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata haki ya msingi.

   Wakazi wa Masasi wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Bomani wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mjini humo,Magufuli aliwaambia wananchi hao kuwa kama atapewa ridhaa na wananchi hao ya kuiongoza Tanzania basi atahakikisha utendaji, ufanisi katika kuleta maendeleo nchini unaongezeka ikiwa pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata haki ya msingi.
   Mgombea wa Urais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe akimsikiliza Mwenyekiti wa CCM mkoani Mtwara Ndugu Mohamed Sinan wakati alipokuwa akimkaribisha ili kuzungumza na wakazi wa Nanyumbu mkoani Mtwara. 
   Wananchi wa Nanyumbu wilayani Masasi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
    Wananchi wa Nanyumbu wilayani Masasi wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mapema leo wilayani humo.
   Wananchi wa Nanyumba wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili na kuwahutubia
   Umati wa watu ndani ya uwanja wa Bomani wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia ndani ya mji huo.  0 0

   Mkurungenzi Mtendaji wa Chama cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA) Edda Sanga akizungumza na wananchi juu ya uzinduzi wa ilani ya uchaguzi ya mtandao wa wanawake na katiba na uchumi leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurungenzi Mtendaji wa Chama cha waandishi wa habari wanawake (TAMWA) Edda Sanga akizidua ilani ya uchaguzi ya mtandao wa wanawake na katiba na uchumi leo jijini Dar es Salaam.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0


  0 0

    
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikutana, kufanya mazungumzo ya faragha na kisha kuagana na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wakati Rais huyo aliposimama kwa muda katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam leo mchana na kisha kurejea Kongo.(picha na Freddy Maro)

  0 0


  Dear All,

  Come join the Embassy of Tanzania and Childbirth Survival International (CSI) for CSI’s first annual fundraising on September 12th at 4:30pm to 7pm, at the Embassy of Tanzania, Washington DC.

  In Tanzania, many of the lives lost during pregnancy, childbirth, and immediately after birth, are often 100% preventable. We are calling upon You to join us and help save lives. This fundraising is to kickoff CSI’s saving lives at birth project in Biharamulo District in northwest Tanzania. Biharamulo is one of Tanzania’s poorly performing Districts that deserves immediate support and attention – We thank you for answering the call. Visit www.childbirthsurvivalinternational.org for more information.

  There’s a registration fee of $100 and it includes a raffle ticket. All donations are tax deductible and will be used to implement project activities in Biharamulo. Registration link here.

  Light Refreshments | Entertainment | Raffle Prizes | Networking

  For information about the event, please contact
  Sandra Kiyonga at sandra.kiyonga@childbirthsurvivalinternational.org or call 202-763-2100.

  Tuko Pamoja!

  0 0

  Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajiwa kuondoka nchini leo usiku kuelekea nchini Congo-Brazzavile kwenye michuano ya Michezo ya Afrika (All Africa Games) inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 3, mwaka huu.
  Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa TFF, Twiga Stars haikuondoka leo kuelekea nchini Congo – Brazzavile, Shirikisho bado linasubiri mwongozo wa Wizara ya Habari,Viajana, Utamaduni na Michezo.
  Imani ya TFF ni kuwa timu itasafiri na kuwahi mechi ili kuepuka hatari ya kuadhibiwa na CAF ikiwa ni pamoja nan a kulipishwa fainai au kuondolewa kwenye michuano hiyo.
  Mchezo wa kwanza wa Twiga Stars katika michuano hiyo  utakua dhidi ya Ivory Coast tarehe 6, Septemba, mchezo wa pili dhidi ya Nigeria Septemba 9 na mchezo wa mwisho katika kundi hilo utakua dhidi ya      Congo-Brazzavile Septemba 12, 2015.
  Timu mbili kutoka kundi A zitaungana na timu mbili nyingine kutoka kundi B kucheza hatua ya nusu fainali.

  0 0

  ITS now 5 yrs Since You left Us On 02/09/2010.Thursday 15:45 Pm!!!!!!

  We thought of you with love today,
  But that is nothing new.
  We thought about you yesterday.
  And days before that too.
  We think of you in silence.
  We often speak your name.
  Now all we have is memories.
  And your picture in a frame.
  Your memory is our keepsake.
  With which we'll never part.
  God has you in his keeping.
  We have you in our heart.
  We as family will remember all you taught us
  We are hurt but we won't be sad
  Because he'll send us down the answers
  And he'll always be OUR DAD
  R.I.P. Mzee Mng’anya.

  0 0


  0 0

   Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akizungumza siku ya Jumanne, wakati  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipopitisha Azimio linalowasilisha kwa Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali  Malengo na Ajenda mpya za Maendeleo Endelevu ( Ajenda 2030)   Anaonekana pia Rais wa Baraza Kuu la 69, Bw. Sam Kutessa .
  Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  akiwa na Afisa Mkuu Siongelael Shilla wakati wa upitishaji wa Azimio  namba A/69/L.85   kuhusu Ajenda 2030  ambapo baada ya kupitishwa  kwa kauli moja azimio hilo wazungumzaji  wanaowakilisha  makundi ya kikanda walipata fursa ya kuelezea misimamo yao juu ya  baadhi ya   mambo ambayo walikuwa wakitofautiana kimtizamo na kimsimamo.

  Na Mwandishi Maalum,   New York

  AFRIKA,  imesisitiza  na kubainisha kwamba  itatekeleza malengo mapya ya maendeleo endelevu kwa  kuzingatia  maslahi, vipaumbele, sera,   mila na tamaduni ambazo nchi za Afrika  zimejiwekea.


  Aidha  Afrika inasema kuwa,  utekelezaji wa  malengo hayo    pia utazingatia  sheria za kimataifa  na ambazo nchi  za Afrika  zimeridhia na si vinginevyo.


   Hayo yameelezwa na  Balozi Fode Seek,  Mwakilishi wa Kudumu  wa Senegal katika Umoja wa Mataifa ambaye ni  Mwenyekiti wa    nchi za Afrika   kwa mwezi Septemba.


    Alikuwa  akizungumza  kwa  niaba ya  nchi   za Afrika wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipokutana  siku ya jumanne, kupitisha Azimio namba A/69/L.85  ambalo linawasilisha  ajenda ya  Maendeleo Endelevu (ajenda 2030) itakayotekelezwa kwa miaka   15 ijayo.

  Ajenda 2030 inachukua nafasi ya   Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs) yanayofikia ukingoni  mwishoni mwa  mwaka huu.  0 0

  Aliyekuwa Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa Frank Leonard (Kulia) akifungua mkutano mkuu wa IPC jana katika ukumbi wa Maktaba ya Iringa katikati ni Daud Mwangosi ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa IPC akifikiri jambo.
  Aliyekuwa mwenyekiti wa IPC Daud Mwangosi (kushoto) akihojiwa na mzee wa matukio daima Bw Francis Godwin  ambaye alikuwa ni katibu msaidizi wa IPC juu ya wanahabari kudumisha umoja na mshikamano wakati wa uhai wake.


  Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa cha chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi tarehe Kama ya leo miaka mitatu iliyopita aliuwawa  katika vurugu za Polisi  na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa .
  Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .
  Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

  0 0

   Marehemu Mzee Anyosisye Mwakyusa enzi za uhai wake.
   Mwili ukiondolewa kanisani.
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA


older | 1 | .... | 959 | 960 | (Page 961) | 962 | 963 | .... | 3284 | newer