Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 956 | 957 | (Page 958) | 959 | 960 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NextGen Solawazi Ltd ya kutoka Marekani, Bw. Mayank Bhargava. Katika mazungumzo hayo ambayo yalifanyika katika Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Bhargava alimjulisha Balozi Mulamula kuwa kampuni hiyo imeshaanza kazi ya kufunga mitambo ya kuzalisha umeme wa nishati ya jua wa MW 5 kwa ajili ya mkoa wa Kigoma. Aidha, alitoa taarifa kuwa hivi karibuni kampuni hiyo itaanza mchakato wa kufunga umeme wa nishati ya jua wa MW 16 kwa ajili ya mkoa wa Shinyanga.

  Bw. Bhargava akisisitiza jambo huku Balozi Mulamula akisikiliza kwa makini. Wa kwanza kushoto ni Bw. Cyril Batalia ambaye ni Mshauri Mwelekezi wa Kampuni ya NextGen Solawazi Ltd.

  mazungumzo yakiendelea.

  0 0

  Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwasikiliza akinamama wakimuelezea kero ya maji baada ya kumsimamisha na kumpa kero hizo Jimboni Longido.
   Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwasikiliza akinamama wakimuelezea kero ya maji baada ya kumsimamisha na kumpa kero hizo Jimboni Longido.Wakinamama wilayani Longido wakiendelea kuteka maji kwa zamu baada ya kumaliza kumueleza kero zao Bi. Samia Suluhu aliepita maeneo hayo. Wakinamama wilayani Longido wakiendelea kuteka maji kwa zamu baada ya kumaliza kumueleza kero zao Bi. Samia Suluhu aliepita maeneo hayo.Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.Baadhi ya wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Monduli wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM, Bi. Samia Suluhu.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Wasanii wa Filamu nchini Wema Sepetu na Steven Nyerere wakimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam kuzindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao illi aipigie kura CCM.Kampeni hiyo imeratibiwa na Wasanii wa filamu wakuongozwa Wema Sepetu na Steven Nyerere.
  Msanii wa Filamu Bi.Wema Sepetu akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete tuzo maalum kwa kutambua mchango wake katika kulinda na kuthamini kazi za wasanii nchini ambapo katika kipindi chake cha uongozi wamepata manufaa makubwa.Wema alikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya baadhi wasanii wa filamu na Muziki nchini wanaoshiriki katika kampeni ya Mama Ongea na Mwanao yenye lengo la kuwahimiza wanawake kuwahimiza watu kuipigia kura CCM kwa kuwachagua wagombea wake katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao.
  Baadhi ya Wasanii wa Filamu nchini, wakimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya picha ya kuchorwa ya Mama.picha na Freddy Maro


  0 0

  Na Dotto Mwaibale

  BOHARI ya Dawa (MSD) imezindua rasmi taarifa yake ya mwaka 2013/2014 (Annual Report), ambayo ilizinduliwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia.

  Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa taarifa hiyo, Profesa Mtulia alisema kupanda kwa huduma za usambazaji dawa, upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 55 hadi 85 ni jambo la kujivunia.

  Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani alisema mpango wa MSD kwa sasa ni kuanzisha maduka ya dawa ambayo yataendeshwa na MSD ambapo kwa kuanzia hivi karibuni litazinduliwa mkoani Mbeya na baadae itafuatia mikoa Kanda za  Dar es Salaam, Mwanza na Moshi. 
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia (kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa taarifa ya MSD ya mwaka 2013/2014 uliofanyika Ofisi za MSD Keko jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani.
   Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Johnson Mwakalitolo, akizungumza katika uzinduzi huo.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Profesa Idris Ali Mtulia, akizungumza katika uzinduzi huo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

   Muandaaji wa matamasha hapa nchini Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na maandalizi ya tamashala kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. pia amesema kuwa katika tamasha hilo litahuzuliwa na watu mbalimbali akiwemo mwimbaji mahili wa nyimbo za Injili hapa nchini Rose Mhando pamoja na Solomoni mwimbaji wa nyimbo hizo Solomon Mkubwa ameyasema hayo katika ofisi zake zilizopo kinondoni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya tamasha la kuombea amani,Beno Chelele.
  Muandaaji wa matamasha hapa nchini Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na maandalizi ya tamashala kuombea amani kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. Pia amewaomba watanzania kumuunga mkono katika tamasha hilo litakalofanyika Oktoba 4 mwaka huu  jijini Dar es Salaam.Msama alisema, mbali ya kuuombea uchaguzi mkuu, Tamasha hilo pia litatumika kumuaga rasmi Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ambaye amekuwa mdau mkubwa wa muziki wa injili hapa nchini.

  0 0

  WACHEZAJI watano kutoka katika kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) wanaondoka leo jijini Dar es salaam kuelekea nchini Afrika Kusini katika klabu ya Orlando Pirates kwa ajili ya kufanya majaribio.
  Vijana hao wanakwenda katika klabu ya vijana ya Orlando Pirates kufanya majaribo ambapo makocha wa vijana wa klabu hiyo watapata nafasi ya kuwatazama katika mazoezi na michezo ya kirafiki.
  Nafasi hiyo imepatikana kufuatia mazungumzo ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Rais wa klabu hiyo Irvin Khoza kuomba vijana hao kupata nafasi ya kufanya majaribio katika klabu hiyo na endapo watafuzu, watajiunga na timu ya vijana ya Orlando Pirates.
  Msafara huo wa wachezaji utaongozwa na Mkurugenzi wa Ufudndi wa TFF, Salum Madadi ambaye atakua na vijana hao katika kipindi chote cha majaribio nchini Afrika Kusini.
  Wachezaji hao ni Asaad Ali Juma (Zanzibar), Maziku Aman (Dodoma), Issa Abdi (Dodoma), Kelvin Deogratias (Geita) na Athumani Maulid (Kigoma).
  Shirkisho la Mpira wa Miguu nchini linawatakiwa kila la kheri vijana hao katika majaribio yao huko nchini Afrika Kusini.

  0 0


  Abdallah Waziri - ambaye ni mmoja wa watoto wa mitaani aliyerudishwa shule kwenye kikao cha leo.
  Abdallah Waziri, Asia Mtibua na Mwalimu Gaudensia Igoshalimo wakimkaribisha Abdallah Waziri shuleni.
  Mmoja wa wajumbe akitoa maoni yake katika kikao  cha bunge katika shule ya oysterbay mkoani manyara.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi Irene Florence Mkwama alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais leo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi Irene Florence Mkwama alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais leo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mpya wa Jamhuri ya watu wa Algeria Belabed Saad alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi kwa Rais leo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi Mpya wa Jamhuri ya watu wa Algeria Belabed Saad alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi kwa Rais leo,[Picha na Ikulu.]

  0 0

   Mtaalam kutoka  Kitengo cha Leseni, Wizara ya Nishati na Madini, Charles Gombe akielezea hatua za Wizara katika  kuboresha huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao (Online Mining Cadastre Transactional Portal; OMCTP) kwa wachimbaji wa madini (hawapo pichani) mjini Mtwara. Lengo la mafunzo hayo lilikuwa ni kuwapa uelewa  wachimbaji wa madini kuhusu  huduma hiyo pamoja na kuwasajili.
   Baadhi ya wachimbaji wadogo  wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini (hawapo pichani).
   Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Aidan Mhando ( wa pili kutoka kushoto, waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo.
   Mtaalam kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mtwara, Juma Namuna akielezea umuhimu wa wachimbaji wa madini kujiunga na mfuko huo  ili kunufaika kwa kupata mikopo.


  0 0  0 0


   Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia (kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa taarifa ya MSD ya mwaka 2013/2014 uliofanyika Ofisi za MSD Keko jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani.
   Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Johnson Mwakalitolo, akizungumza katika uzinduzi huo.

  Na Dotto Mwaibale
  BOHARI ya Dawa (MSD) imezindua rasmi taarifa yake ya mwaka 2013/2014 (Annual Report), ambayo ilizinduliwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia.

  Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa taarifa hiyo, Profesa Mtulia alisema kupanda kwa huduma za usambazaji dawa, upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 55 hadi 85 ni jambo la kujivunia.

  Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani alisema mpango wa MSD kwa sasa ni kuanzisha maduka ya dawa ambayo yataendeshwa na MSD ambapo kwa kuanzia hivi karibuni litazinduliwa mkoani Mbeya na baadae itafuatia mikoa Kanda za  Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.


  0 0

  Katibu Mkuu  wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, na Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania, Mhe. Filiberto Sebregondi, wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya kuruhusu waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kuingia nchini kufuatilia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.
  Hati hiyo ya makubaliano imesainiwa leo, 28-08-2015, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo.
   Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregondi, akisaini Hati ya Makubaliano ya kuruhusu waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kuingia nchini kufuatilia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, naye akisaini Hati hiyo.
  Zoezi la kusaini likiendelea.

   Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga,(kulia) akizungumza katika hafla hiyo ya kusaini hati ya Makubaliano ya kuruhusu waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kuingia nchini kufuatilia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.

   Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregondi, akijibu maswali ya Waandishi wa habari. 

  Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe.Filiberto Sebregondi, akiagana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, muda mfupi mara baada ya kusaini hati hiyo.
  =================
  NA REUBEN MCHOME.
  Umoja wa Ulaya (EU) utatuma timu ya waangalizi yenye wajumbe 128 nchi nzima katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015. Hayo yalibainishwa wakati wa uwekaji saini wa Makubaliano ya awali ya kuruhusu timu hiyo kati ya EU na Serikali ya Tanzania uliofanyika kwenye Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tarehe 28 Agosti 2015. Uwekaji saini huo umefanywa na Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na kwa upande wa EU ulifanywa na Mhe. Filiberto Ceriani Sebregondi, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania.
  Akizungumza baada ya uwekaji saini wa Makubaliano hayo,  Balozi Sebregondi alieleza kuwa EU imekuwa ikituma timu hiyo kwa nchi washirika ambazo zina historia nzuri ya demokrasia. Aidha, nchi hizo zina dhamira ya dhati ya kukuza mahusiano na EU kwa kuruhusu waangalizi wafanye majukumu yao katika hatua zote za uchaguzi kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa wa haki na huru.

  Balozi Sebregondi aliendelea kueleza kuwa timu kama hiyo ambayo wajumbe wake wanakuwa Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya, ilitumwa katika uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo iliutangaza kuwa ni huru na haki.   Timu pia ilitoa ushauri na maelekezo ya namna ya kufanya maboresho katika hatua mbalimbali za uchaguzi.
  Kwa upande wake, Balozi Mulamula aliikaribisha timu hiyo kuja Tanzania na alisema kuwa  jukumu la Wizara yake ni kuratibu na kuhakikisha kuwa wajumbe wa timu hiyo wanatekeleza majukumu yao kama ilivyokubalika kwenye Makubaliano ya Kimataifa. Aliongeza kuwa maelezo ya undani wa shughuli ya timu hiyo wakati wa uchaguzi yatatolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambao pia watasaini makubaliano ya utekelezaji wa kazi ya timu hiyo. 
  Taasisi zingine za Kimataifa zinazotarajiwa kutuma timu za uangalizi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 ni pamoja na Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR).

  0 0

   Mwandishi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Tanzania ambae pia ni Mkurugenzi wa Internews Tanzania Valerie N. Msoka akifafanua kitu kwa wandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo juu ya kuripoti uchaguzi Mkuu.
   Mkurugenzi wa Shirika la Internews kanda ya Afrika Ian Noble akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari juu ya kuripoti habari za Uchaguzi, alipotembelea katika mafunzo hayo huko ukumbi wa watu wenye ulemavu Kikwajuni Weles Mjini Zanzibar.
  Mkurugenzi wa Shirika la Internews kanda ya Afrika Ian Noble (wakatikati) katika picha ya pamoja na washiriki na wasimamizi wa mafunzo hayo (kulia) aliekaa ni Afisa Mwandamizi Baraza la Habari Tanzania Ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan na kushoto ni Mwandishi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Zanzibar Salim Said Salim.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.


  0 0

   Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Njombe mjini katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa saba saba.Magufuli amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataendeleza juhudi zake za kujenga barabara kwa kiwango cha lami,amesema dhamira yake aliokuwa nayo ya Uwaziri wa Ujenzi katika kujenga barabara za lami katika maeneo yote hapa nchini.

  Amesema tangu kupewa kuwa waziri wa ujenzi ameweza kujenga barabara  zaidi kilomita 7000 nchi nzima,ambapo ilipelekea kuongeza kuongeza pato la mfuko wa barabara kutoka bilioni 73,3 hadi kufikia bilini 866 kwa mwaka huu hivyo ameahidi akiwa rais atajenga zaidi barabara za lami.

  Dkt MAGUFULI ambae anaendelea na mikutano ya kampeni za Urais mikoa ya nyanda za juu kusini , amelalamikia udanganyifu wa baadhi ya mitandao ya kijamii  na baadhi ya vyombo vya habari kuripoti  kuwa amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali ya mkoa wa mbeya wakati sio kweli.

  Aidha pia Magufuli  amewaomba wananchi waweke imani kubwa kwake kwa  kumpa kura nyingi  zitakazomwezesha kuwa raisi wa awamu ya tano,na kIsha alipe fadhira hizo kwa kutatua kero zinazowakabili hasa wananchi wenye kipato cha chini

   Mgombea Urais wa CCM Dkt Joh Pombe Magufuli akipeana mkono na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,Ndugu Phillip Mangula mara baada ya kumkaribisha mgombea huyo jukwaani kuwahutubia wananchi wa njombe na kuzinadi sera za chama chake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano
   Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,Ndugu Phillip Mangula akiwashukuru wananchi wa Njombe waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa sabasaba mjini humo,ambapo pia Ndugu Mangula alimkaribisha mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kuwahutubia wananchi wa njombe na kuzinadi sera za chama chake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano
   Wananchi wa Njombe wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa sabasaba mjini Njombe.
   Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM na Mgombea Ubunge wa jimbo la Kyela,Mh Harrison Mwakyembe akiwahutubia wananchi wa Njombe jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
   Waanchi wakishangilia jambo kwenyemkutano wa kampeni wa CCM.

   Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe Mh. Gerson Lwenge kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe
   Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM mgombea Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe Mh. Gerson Lwenge kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe kwa ajili ya kuwaambia wananchi ni namna gani wataiongoza Tanzania katika awamu ya tano. 
    Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Makete Dkt Norman Msigala kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe
   MKutano wa Kampeni ukiendelea. 
   Wananchi wakisikiliza sera za mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,hayupo pichani alipowahutubia jioni ya leo mjini Njombe. 
   Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni.  0 0


  0 0


  0 0

  Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kwa Chama cha Mapinduzi Bi.Samia Suluh akisalimiana na Mh;Mwigulu Nchemba ambaye ni mgombea Ubunge jimbo la Iramba hii leo,Bi.Samiah suluhu katika ziara yake ya kampeni ndani ya mkoa wa Singida,hii leo amefika Kata ya Kyengege Jimbo la Iramba kwaajili ya kunadi Ilani ya CCM ya uchaguzi ya Mwaka 2015 na kuomba kura za kishindo kwa nafasi zote za Udiwani,Ubunge na Urais ifikapo Tar.25.10.2015

  Bi.Samiah Suluhu ambaye ni Mgombea Mwenza wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi akizungumza na Wananchi wa kata ya kyengege mambo mbalimbali anayodhamiria kuwafanyia mara baada ya kushinda hapo October 25.Kubwa amewaahidi kutatua kero ya Maji kwa Tanzania nzima ,Kujenga mabweni kwaajili ya watoto mashuleni,Kuinua Uchumi wa akina mama kupitia Mikopo mbalimbali na kupitia Utekelezaji wa Ilani ya CCM inayosema kila kijiji kimetengewa Milion 50 kwaajili ya maendeleo.Mgombea mwenza wa nafasi ya Urais Bi.Samiah Suluhu akimuombea Kura Mh;Mwigulu Nchemba kwa wananchi wa kata ya kyengege hii leo wakati wa mkutano wa kampeni za kuelekea Uchaguzi Mkuu 2015.Kushoto ni Mgombea Ubunge jimbo la Mkalama kupitia CCM ambaye pia alihudhuria mkutano wa Kata ya Kyenge wilaya ya Iramba.Makamu wa Rais mtarajiwa wa Kwanza Mwanamke Nchi Tanzania akimnadi Mgombea Udiwani wa kata ya Kyengege wilaya ya Iramba.Hapa akiwanadi washindi wa Ubunge Viti Maalum Mkowa wa Singida,Kushoto ni Ashyrose na Kulia ni Bi.Martha Mlata.
   Picha na Sanga Festo Jr.


  0 0

  Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake nchini (TWFA)  umemalizika ambapo Amina Karuma amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho, kufuatia uchaguzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
  Nafasi ya katibu msaidizi imekwenda kwa mwandishi wa habari za michezo Someo Ng’itu, na nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya TFWA imekwenda kwa Debora Mkemwa na Theresia Mng’ongo.
  Mgeni rasmi katika uchaguzo huo alikuwa ni katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine ambapo na uchaguzi ulisimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya uangalizi wa Jeremia Wambura kutoka kamati ya Uchaguzi ya TFF.
  TFF inawapongeza viongozi wapya waliochaguliwa na kuwatakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya, na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika maendeleo ya mpira wa miguu ya wanawake nchini.

  0 0

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji wakiwasili kwenye viwanja vya Jangwani Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, leo Agosti 29, 2015. PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
   Umati wa wakazi wa Jijini Dar es salaam, ukiwa umefurika kwa wingi kwenye viwanja vya Jangwani kuwalaki Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza, Mh. Juma Duni Haji, walipokuwa wakiwasili viwanjani hapo, kulikofanyika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 956 | 957 | (Page 958) | 959 | 960 | .... | 3284 | newer