Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

mkataba wa uchimbaji madini wa kampuni ya MorogoroRegional Mining Company Ltd wasainiwa leo

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo akisaini mkataba wa uchimbaji madini wa kampuni ya MorogoroRegional Mining Company Ltd wanaotarajia kuanza shughuri hizo mwishoni mwaka 2013 kulia kwake ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo ndugu, Protase R.G. Ishengoma.
Waziri wa Nishati na Madini (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji katika sekta ya madini baada ya kusaini mkataba wao ili waweze kuanza shughuri za uchimbaji. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo akifuatiwa na Kamishna wa Madini.

UNDP kupitia mradi wa LEGISLATIVE SUPPORT PROJECT yazidi kuwajengea Uwezo waheshimiwa Wabunge

$
0
0
Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na UNDP kupitia mradi wa Legislative Support Project, umeandaa semina ya siku moja kwa waheshimiwa Wabunge kuhusu Haki za wanawake katika nyanza za kiuchumi, kijamii na kisiasa, kwa lengo la kuwajengesa uwezo waheshimiwa Wabunge katika maeneo hayo hususani katika kipindi hiki ambacho Tanzania ipo katika mchakato wa Kuandaa katiba Mpya.

Semina hii ni mwendelezo wa semina za kutoa elimu kwa waheshimiwa Wabunge na Watumishi wa Ofisi ya Bunge katika maeneo mbalimbali ya kibunge ili kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao ya Kibunge. Jumla ya Kamati Tano, za Kilimo, PAC, LAAC, Miundombinu, Maendeleo ya Jamii na Katiba Sheria na Utawala zimeshiriki semina hii.

Mradi huu wa Legislative Support Project, ambao upo chini ya Shirika la Maendeleo Duniani (UNDP) uliingia ubia na Ofisi ya Bunge mwaka 2011 kwa lengo la kujenga uwezo kwa Wabunge na Watumishi katika maswala mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Shughuli za Kibunge.

Mpaka Sasa mradi huu umekwisha toa mafunzo mbalimbali kwa wabunge ambayo yamewasaidia kuongeza uelewa wa mambo mbalimbalu katika sekta hapa nchini hivyo kuweza kutekeleza majukumu yao ya uwakilishi, usimamizi wa serikali pamoja na kutunga sheria kwa ufanisi mkubwa.
Mtaalam kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt.Modesta Opiya akiwanoa Waheshimiwa Wabunge katika Semina hiyo kuhusu haki za kijamii na Uchumi kwa wanawake
waheshimiwa Wabunge mbalimbali wakichangia mada iliyowasilishwa na Dkt.Modesta Opiya.

SALAAM ZA RAMBIRAMBI TOKA JUMUIYA YA WATANZANIA WANAOISHI GUANGNDONG CHINA

$
0
0
Kwa niaba ya watanzania wote wanaoishi katika mji wa Guangzhou china tunapenda kuwataarifu kwamba tumeshitushwa na kuhuzunishwa sana na taarifa za vifo vya ndugu zetu vilivyotokea kwa kudongokewa na ghofofa.

Jumuiya kwa niaba ya watanzania wote nchini China, tunatoa pole kwa wahanga wote, aidha tunawatakia watanzania wote pamoja na ndugu jamaa na marafiki wote wawa wafiwa moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi.

Tunaomba mwenyezi Mungu azipumzishe mahala pema peponi roho za marehemu wote, tuko pamoja na familia za marehemu wote katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Mwenyezi Mungu Azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi

Amen.

Imetolewa na
Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Guangzhou China.

wanahabari wapewa mafunzo kuhusu ripoti ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012

$
0
0
Mchambuzi wa mifumo ya kompyuta kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ariv Severe akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kutumia tovuti ya NBS ambayo inataarifa mbalimbali ikiwemo ya ripoti ya sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012 wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyofanyika leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Sensa Zanzibar, Mayasa Mwinyi (kushoto) akimuelekeza mwandishi wa habari wa gazeti la Majira Darlin Said (kulia) jinsi ya kutumia takwimu za sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Idadi ya watu kwa ngazi za utawala , matokeo muhimu wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Sensa ya watu na takwimu za jamii Ephraim Kwesigabo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) umuhimu wa kuripoti kwa usahihi taarifa ya Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Idadi ya watu kwa ngazi za utawala, matokeo muhimu wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa Habari wa Televisheni ya Zanzibar (ZBC) Khamisuu Ally (kushoto) na Mohamed Mohamed (kulia) wakisoma ripoti ya Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Idadi ya watu kwa ngazi za utawala, matokeo muhimu wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo jijini Dar es Salaam. NBS iliandaa mafunzo hayo ya siku moja ili vyombo vya habari viweze kuripoti kwa usahihi taarifa ya sensa.
Mhariri wa Habari Msaidizi Stella Nyemenohi kutoka gazeti la Habarileo akitoa maoni yake jinsi waandishi wa habari wanavyoweza kutumia ripoti ya sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012 kupata majibu mbalimbali ikiwa ni pamoja na totauti ya idadi ya watu kati ya mkoa mmoja na mwingine wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mpiga picha wa kampuni ya New habari (2006) Anthony Siame na kulia ni mwandishi wa Habari wa Televisheni ya Zanzibar (ZBC) Khamisuu Ally.
Meneja wa Takwimu za watu na Jamii kutoka ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Aldegunda Komba akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu uwiano wa idadi ya watu kijinsia unavyotofautiana kimkoa kuanzia wanaume 88 kwa kila wanawake 100 kwa mkoa wa Njombe hadi wanaume 101 kwa kila wanawake 100 kwa mkoa wa Manyara. NBS iliandaa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyofanyika leo jijini Dar es ili vyombo vya habari viweze kuripoti kwa usahihi taarifa za sensa.
Mratibu wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Irenius Ruyobya (kushoto) akiongea jambo na mtaalamu wa mawasiliano ya umma Said Ameir wote kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu jinsi ya kutumia takwimu za sensa yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa Habari wa Televisheni ya Zanzibar (ZBC) Mohamed Ally (kulia) akiuliza swali wakati wa mafunzo ya siku moja ya waandishi wa habari yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam jinsi ya kutumia takwimu za Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Idadi ya watu kwa ngazi za utawala, matokeo muhimu yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) . Kushoto ni Mustapha Musa mwandishi wa habari kutoka Zenj FM. Picha na Anna Nkinda – Maelezo

Mbunge Mwidau, ahamasisha miradi ya Maendeleo Tanga

$
0
0
Mbunge Mwidau akikabidhi mifuko kumi ya saruji kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Msambweni Bahati Marungu kwa ajili ya ujenzi shule ya Sekondari ya Kata ya Msambweni.

Mbunge Mwidau akisalimia na wanawake wa kikundi cha wajasiriamali wafugaji wa kuku wa Kata ya Pongwe kijiji cha Marizara.
Mbunge Mwidau, akisalimia na wanawake wa Kata ya Mafuriko, ambao walifika kumlaki katika ziara yake ya Wilaya ya Tanga.
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), akipata maelezo ya mradi wa kisima cha maji kutoka kwa Diwani wa Kata ya Mwera Maisha Mkaidi (CUF), wengine ni baadhi ya viongozi na wananchi wa kata hiyo.

MBUNGE wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), awametaka wananchi wa mkoa wake kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Kauli hiyo aliitoa kwa nyakati tofauti alipokuwa akizungumza katika ziara yake hiyo katika kata za halmashauri ya jiji la Tanga na Wilaya ya Pangani, ambapo alisema ni muhimu kwa kila mwanajamii kutambua wajibu wake.

“Suala la amaendeleo halina itikadi na sasa sio wakati wa kampeni za uchaguzi, ni jukumu letu kwa viongozi wa Mkoa wa Tanga, kuhakikisha tunashiriki katika miradi ya maendeleo kwa dhati.

“Ni wazi Mkoa wa Tanga tuna kila sababu ya kuhakikisha tunaimarisha uchumi wetu hasa baada ya miaka kadhaa viwanda vyake kufa kutokana na kutokuwepo na usimamizi mzuri. Ikiwa kila mtu atatambua wajibu wake ni wazi tutafanikiwa kufikia lengo letu,” alisema Mwidau.

Alisema kutokana na hali hiyo kila mara amekuwa akishiriki katika kuhamasisha maendeleo katika maeneo yote ya mkoa huo bila kujali uongozi wa kaa upo chini ya chama cha CUF au CCM.

“Tanga tuna ardhi nzuri na tuna kila sababu ya kujivunia jambo hili ingawa kukosekana kwa usimamizi madhubuti kwetu imekuwa ni kilio kikubwa kwa wananchi wetu tunaowaongoza, wabunge wote wa mkoa huu tuna wajibu wa kuliangalia hili,” alisema Mbunge Mwidau.

Katika ziara hiyo akiwa wilayani Pangani Mwidau, alisema kuwa amefurahishwa kuona wananchi na viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mwera kuamua kuchimba kisima kikubwa zaidi ya kilichopo sasa na katika hilo amefurahishwa kuona mchango wa awali wa mashine aliyoitoa imewezesha kujengwa kwa kisima kisima kingine kikubwa cha futi 45 na kipenyo cha nchi sita.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA BECOMES CHAIR OF THE AFRICAN UNION PEACE AND SECURITYCOUNCIL (AUPSC) FOR THE MONTH OF APRIL 2013

VIDEO YA BONANZA LA WANAHABARI LILILOFANYIKA LEO VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR

Wizara ya Elimu Yapiga Marufuku Walimu Kutumia Wanafunzi Kusahihisha Madaftari


Serikali kupambana na matumizi mabaya ya TEHAMA

$
0
0
Serikali imesema itachukua hatua kali za kisheria kwa atakayebainika kutumia vibaya simu za mikononi, na mitandao ya kijamii kuleta uchochezi au kwenda kinyume na maadili ya nchi.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutaka kukomesha vitendo hivyo hatari vinavyoonekana kukua siku hadi siku.

“Hatua hizo zitachukuliwa dhidi ya kampuni au mtu yoyote atakayetoa kashafa na kuitukana serikali, viongozi wa serikali, dini, siasa na watu binafsi,” alisema na kuongeza kuwa vitendo hivyo vinakiuka sheria za nchi.

Alisema hatua hizo pia zitawakumba watu wote wanaojihusisha na uonyeshaji kwenye mitandao hiyo picha za ngono, unyanyasaji wa watoto na ukiukaji wa maadili na kutoa taarifa zenye lengo la kuvunja utulivu na amani.

“Matumizi mabaya haya ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kama za simu za mikononi, barua pepe, na mitandao ya kijamii yanafanywa na watu wachache kwa kusambaza taarifa zenye nia ya kuchafua taifa letu,” alisema.

Alisema pamoja na kwamba teknolojia hiyo katika miaka ya karibuni imechangia kuleta maendeleo makubwa nchini, baadhi ya watu wanaitumia kwa mambo yasiyofaa.

Aliendelea kusema kuwa watu wengine wamekuwa wakiitumia kwa kufanya wizi, ujambazi,ubakaji, biashara ya madawa ya kulevya na ukahaba na kusambaza siri za watu binafsi bila idhini ya wahusika.

Alisema matumizi yasiyofaa yanafanywa na watu wachache yanaelekea kuharibu maadili ya watanzania na yanaweza kuhatarisha utulivu na usalama wa nchi kwa kutumia TEHAMA.

Aidha alisema pia hatua kali zitachukuliwa kwa wakala au kampuni ya simu yoyote itakayouza SIM kadi kwa mtu yeyote bila ya kuwa na kitambulisho kinachotambulika kisheria.

Alisema pia ni kosa la jinai kutoa taarifa za uwongo wakati wa usajili wa SIM kadi na serikali imejipanga kuzima sim kadi zote ambazo hazijasajiliwa kama inavyotakiwa kisheria.

TPSF yapania kuendeleza vijana, kinamama nchini

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Geofey Simbeye (kulia) akizungumza jambo kwa wanachama wa taasisi hiyo kanda ya nyanda za juu kusini (hawapo pichani) mwishoni mwa wiki mjini Mbeya katika mkutano maalumu wa uelimishaji na uhamasishaji wa muundo wa uwakilishi katika kongano ( clusters). Katikati ni mjumbe wa Bodi ya TPSF Bw. Gideon Kaunda na Bw. Jumbe Menye (kushoto), pia mjumbe wa bodi ya taasisi hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Geofey Simbeye (kulia) akizungumza jambo na mjumbe wa Bodi ya TPSF Bw. Gideon Kaunda wakati wa mkutano na wajumbe wa taasisi hiyo kanda ya nyanda za juu kusini mwishoni mwa wiki mjini Mbeya katika mkutano maalumu wa uelimishaji na uhamasishaji wa muundo wa uwakilishi katika kongano ( clusters).

NAPE AFUNGUA SEMINA YA HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA WA KILIMANJARO

$
0
0
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akifungua Semina ya Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Kilimanjaro,Aprili 6, 2013, katika ukumbi wa VETA mjini Moshi.
Wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro, wakijitambulisha kwenye semina ya Halmashauri Kuu mkoa wa Kilimanjaro, katika ukumbi wa VETA mjini Moshi. Kutoka kushoto ni, Charles Mlingwa (Siha), Novatus Makunga (Hai), Elinas Pallangyo (Rombo), Shaibu Ndemanga (Mwanga), Helman Kapufi (Same) na Dk. Ibrahim Msengi (Moshi Mjini). 
Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kazidi akizungumza wakati semina hiyo.
Wajumbe wakimshangilia Nape alipofungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCm, mkoa wa Kilimanjaro katika ukumbi wa VETA mjini Moshi.

LIBENEKE JIPYA TOKA MAKETE

$
0
0

Habari za leo wadau, Napenda kuchukua fursa hii kuitambulisha kwenu blog yangu mpya ambayo ina lengo la kutoa habari mbalimbali kutoka Makete na sehemu za jirani ili kuendelea kuwajuza wasomaji waliopo kila pembe ya Dunia hii kwa muda wote bila kuchoka. Jina la blog hiyo ni EDDYMOBLAZE BLOG unaweza kuipitia kwa kubonyeza link ifuatayo:-  


asante kwa ushirikiano wenu

Edwin Moshi
Mmiliki wa Blog
Eddymoblaze Blog 

TEAM TANZANIA OFF TO CHINA FOR TOURISMPROMOTION MISSION

VIONGOZI MBALI MBALI WASHIRIKI HITMA YA KARUME LEO CCM KISIWANDUI MJINI ZANZIBAR LEO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiungana na waumini wa dini ya Kiislamu na Wananchi,katika kumuombe dua kwa Kisomo cha Hitma iliyosomwa leo katika Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar,wakiwemo Rais wa Tanzania Alhaj Dk.Jakaya Mrisho Kikwete,(wa pili kushoto).
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akiweka shada la mauwa katika kaburi la Marehemu Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume,wakati wa Hitma na Dua iliyoombwa na wananchi wa Zanzibar huko Kisiwandui Mjini Zanzibar leo.

PPF YATOA VIFAA KUMALIZIA UJENZI KITUO CHA POLISI NYAKOTO MWANZA

$
0
0
Meneja wa PPF Kanda ya ziwa Meshack Bandawe akimkabidhi mifuko ya simenti Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu, mchango wenye thamani zaidi ya shilingi milioni 2, kwaajili ya kuchangia uharakishwaji wa ujenzi wa kituo cha polisi Nyakato jijini Mwanza. 
Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kituo cha polisi Nyakato Bw. Alfred Wambura, amesema kuwa kamati yake imenuia kuhakikisha ujenzi wa kituo hicho unakamilika mwishoni mwa mwezi wa 5 na kukabidhiwa kwa jeshi la polisi.
Mikakati mingine iliyowekwa na kamati hiyo ni kukamilisha ujenzi wa nyumba ya makazi ya OSS wa Nyakato pamoja na watendaji wengine watatu wanaomfuata kwa cheo, ili kurahisisha utendaji wa kila siku wa shughuli za usalama wa jeshi hilo. 
Meneja wa PPF Kanda ya ziwa Mesharck Bandawe amesema kuwa ulinzi kwa maisha ya baadaye ya mwananchi uko ndani ya  mfuko wa uwekezaji wa PPF,  na ulinzi wa wananchi na mali zao uko chini ya jeshi la polisi hivyo amewataka wadau wengine wa mashirika mbalimbali kujitokeza kulisaidia jeshi hilo kukamilisha shughuli za utendaji kwa manufaa ya ustawi wa jamii.


Wadau wa PPF wakisikiliza kwa makini yanayojiri kwenye makabidhiano hayo.

picha na G. Sengo Blog

SBL YAMKARIBISHA BALOZI WA IRELAND NCHINI KATIKA KIWANDA CHAKE CHA MOSHI

$
0
0

 Meneja wa kiwanda cha bia cha Serengeti Moshi Colman Hannah akitoa maelezo mafupi kwa wana habari juu ya ugeni kiwandani hapo kulia kwake ni Balozi wa Ireland nchini Fionnuala Gilsenan na kushoto kwake ni Msambazaji mkuu wa bidhaa za Kampuni ya Bia ya Serengeti mkoani Kilimanjaro
 Balozi wa Ireland nchini  Fionnuala Gilsenan kushoto akiwa na mwenyeji wake Meneja wa Kiwanda cha Bia cha Serengeti Moshi Colman Hannah akitembelea kiwanda hicho mwishoni mwa wiki hii.
  Balozi wa Ireland nchini  Fionnuala Gilsenan akionja bia ya Guinness inayozalishwa kiwandani hapo(kulia) akiwa pamoja na katibu wake Nicholas Michael(katikati) na mwenyeji wake Meneja wa Kiwanda cha bia cha Serengeti Moshi Colman Hannah(kushoto).
    Balozi wa Ireland nchini  Fionnuala Gilsenan akipata maelekezo kutoka kwa mtaalamu wa maabara ya kiwanda hicho Jemima Mwambungu.
 Mpishi mkuu wa bia za Kampuni ya Bia ya Serengeti Moshi Julius Nyaki akitoa maelekezo kuhusu upikaji wa bia ya Guinness kwa Balozi
Mazungumzo ya hapa na pale pia yalikuwepo.

vikwangua anga vya dar es salaam kutoka angani leo

$
0
0
Baada ya serikali kutoa siku 30 kwa mjenzi wa ghorofa karibu na lile lililoporomoka na kuua watu zaidi ya 20 siku ya Ijumaa kuu mwaka huu, mtazamo umekuwa tofauti kwa vikwangua anga ambavyo vinazidi kume akila kona kama uyoga. Serikali pia imeziagiza halmashuri za Dar es salaam za Ilala, Kinondoni na Temeke kutathmini ubora wa ujenzi wa kila ghorofa na litaloonekana limejengwa chini ya kiwango libomolewa...
 Maeneo ya Gerezani. Uwanja wa Kidongo Chekundu juu shuto kuleeeeee...
 Maeneo ya Gerezani
 Maeneo ya mtaa wa Lumumba Kariakoo. Shoto ni 'Central Park' yetu - Bustani ya Mnazi Mmoja garden
Maeneo ya mtaa wa Ohio kupitia Serena Inn

KARUME DAY SPECIAL

$
0
0

Hapa ndipo alipopigwa risasi na kuuwawa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Makamu wa pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mzee Abeid Amani Karume wakati akicheza bao na marafiki zake katika makao makuu ya CCM Kisiwandui, Unguja. Matundu yanayookekana kwenye ukuta ni ya risasi zilizomiminwa na muuwaji ambaye naye aliuwawa na walinzi wa Mzee Karume, mnamo Aprili 7, 1972. Chini wanafunzi wakiiangalia sehemu hiyo ambayo haijaguswa wala kuondolewa kitu na  imewekwa uzio kuihifadhi kama kumbukumbu

Sanamu ya Mzee Abeid Amani Karume ikiwa mbele ya Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar, Kisiwandui,

MUASISI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR MZEE ABEID AMANI KARUME AKUMBUKWA LEO

$
0
0
Na Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein leo ameongoza hitma ya kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu mzee Abeid Amani Karume, iliyofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui mjini Zanzibar. Hitma hiyo pia, ilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Kharib Bilal, Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Ali Hassan Mwinyi pamoja na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.

 Viongozi wengine ambao walihudhuria katika hitma hiyo ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabhi, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Sheikh Alhad  Mussa Salum kutoka Mkoa wa Dar-es-Salaam nae pia, alihudhuria. 

Wengine ni viongozi wa serikali zote mbili na viongozi wastaafu, viongozi wa vyama vya siasa, Masheikh kutoka Zanzibar na Tanzania Bara, Wabunge na Wawakilishi, wananchi kutoka sehemu mbali mbali pamoja na Mabalozi wadogo waliopo hapa Zanzibar. 

Hitma hiyo ilitanguliwa na Qur-an tukufu, iliyosomwa na Ustadh Sharif Muhidin na kuongozwa na Sheikh Yussuf Mohammed Khamis. Mara baada ya hitma hiyo, Sheikh Mkoa wa Dar-es-Salaam, Sheikh Alhad  Mussa Salum alitoa mawaidha na kumuelezea marehemu mzee Abeid Amani Karume kuwa ni kiongozi aliyepigania maendeleo ya wananchi wa Zanzibar na kumuombea MwenyeziMungu ampe makaazi mema Peponi. 

Akieleza kuhuhu umauti, Sheikh Mussa alisema kuwa umauti ni jambo ambalo litafika kwa kila kiumbe alichokiumba Mwenyezi Mungu na kusisitiza kuwa ni vizuri mwanaadamu akakumbuka asili yake na hatma yake. Baada ya kisomo hicho cha hitma ambacho hufanyika kila mwaka inapofika tarehe 7, Aprili,

Viongozi hao na wananchi waliohudhuria katika hitma hiyo walimuombea dua, marehemu mzee Abeid Karume katika kaburi lake lililopo pembezoni mwa afisi hiyo ya CCM Kisiwandui dua iliyoongozwa na viongozi wa dini tofauti akiwemo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Kabhi, Askofu Michael Hafidh kutoka Kanisa la Anglikana Zanzibar. 

Viongozi na wanafamilia waliweka mashada ya maua katika kaburi la marehemu mzee Abeid Amani Karume akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Ramadhan Haji Faki aliyeweka shada la maua akiwakilisha wazee walioshiriki Mpinduzi ya Januari 12, 1964. 

Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania Meja Jenerali Hassan Vuai Chema, Balozi Ali Karume aliyewakilisha watoto wa Marehemu Karume na Balozi mdogo wa Misri anayefanya kazi zake hapa Zanzibar Balozi Walid Mohamed Ismail aliyewawakilisha Mabalozi wenzake wa hapa nchini na Ahmed Amani Karume aliyewakilisha wajukuu. 

Aidha mjane wa marehemu mzee Abeid Karume, Mama Fatma Karume, alishiriki katika hitma hiyo akiongozana na Mama Salma Kikwete, Mama Asha Balozi na Mama Pili Balozi, Mama Shadya Karume na viongozi wengine wanawake wa kitaifa wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Wawakilishini na wananchi kutoka sehemu mbali mbali ya Zanzibar na Tanzania Bara. April 7, 1972 ndiyo siku aliyouawa Rais wa Kwanza wa Zanzibar marehemu Mzee Abeid Amani Karume na wapinga maendeleo nchini ambapo hivi leo imetimia miaka 41 tokea utokee msiba huo. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Dkt Mohamed Ali Shein na viongozi wengine wa juu wakisoma dua wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo April 7, 2013 .
 Shekhe wa Mkoa wa Dar es salaam Alhaj Alhad Mussa Salum akitoa mawaidha wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo April 7, 2013.
  Askofu Michael Hafidh kutoka Kanisa la Anglikana Zanzibar.  akiomba dua wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo April 7, 2013.
 Kiongozi wa Kihindu  akiomba dua wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo April 7, 2013 .PICHA NA IKULU
Wake za vionvgozi mbalimbali pamoja na mabalozi wakiwa katika dua wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa (Karume Day) katika Makao Makuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo April 7, 2013

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WAPANDA PANTONI

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongea na watoto waliokutana nao kwenye pantoni ya MV Magogoni walipokuwa  wakitoka Mji Mwema, Kigamboni, jijini Dar es salaam leo April 7, 2013   walikomtembelea Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakishuka kutoka  kwenye pantoni ya MV Magogoni walipokuwa  wakitoka Mji Mwema, Kigamboni, jijini Dar es salaam leo April 7, 2013 walikomtembelea Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi. PICHA NA IKULU.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images