Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 93 | 94 | (Page 95) | 96 | 97 | .... | 3282 | newer

  0 0
 • 04/07/13--10:30: Article 11


 • 0 0

   Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda akipokea hundi ya shilingi Milioni hamsini kutoka serIkali ya mapinduzi ya Zanzibar kufuatia ajili ya gorofa 16 lilosababisha maafa tarehe 29 march 2013 jijini Dar es salaam. Hundi hiyo imekabidhiwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi ndogo ya waziri mkuu iliyoko Oysterbay  jijini Dar es salaam. Chini Mhe Pinda akitoa shukurani kwa ujumbe kutoka Zanzibar . Kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi. Picha na Chris Mfinanga


  0 0

  Miss Utalii Tanzania hivi sasa wako katika ziara ya kutembelea hifadhi za Taifa za Utalii ikiwa ni katika kujifunza vitu mbalimbali kuelekea Fainali kuu ya Taifa ambayo itapangwa baada ya kushindwa kufanyika kwa kuwa washiriki walikuwa katika matembezi ya kutembelea hifadhi katika Mto huo. 

   Mpaka sasa washiriki hawa wametembelea hifadhi za Taifa za Saadan ambako walijionea Utalii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ule wa Kutumia Boti nkatika Mto Wami ambako waliweza kushuhudia Viboko na Mamba wengi wakiwa katika mto huo, aida katika hifadhi ya Taifa ya Sadani pia waliweza kufanya Onyesho la kutafuta Tuzo ya Utalii wa Ndani ambapo Miss Utalii Mkoa wa Arusha aliibuka mshindi.

  Baada ya onyesho hilo Saadan washiriki Miss Utalii Tanzania 2013 walitembelea hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa ambako walifanikiwa kupanda katika Milima hiyo na kufanikiwa kutazama kivutio kikubwa cha Maporomoko ya maji kwenye Mlima wa Mlima Sanje. 

  Aidha baada ya kujifunza kutoka katika maporomoko hayo washiriki wa Miss Utalii Tanzania walitembelea Hifadhi ya Taifa ya Hifadhi ya Mikumi ambako wamejionea Wanyama mbalimbali wakiwemo Simba, makundi ya Nyati, Makundi ya Tembo, na Swala. hata hivyo kabla ya kuondoka katika hifadhi ya Mikumi wanatarajia kufanya onyesho kwa ajili kupata mwakilishi wa tuzo ya Tanapa na ile ya utalii wa ndani kabla ya kuelekea mlima kilimanjaro na hifadhi zingine. Kambi ya Miss Utalii ambayo imeanza upya baada ya kuvunjwa kutokana na Washiriki wengi kwenda katika mitiani ya vyuo inatarajia kupanga ratiba ya Fainali hizo baada ya washiriki wote kuwasili kambin.

   Mhifadhi Utalii Emmanue Njiku, wa hifadhi ya Sadaan akifafanua jambo kwa Miss Utalii Tz 2013 wakati wa ziara
  Gari la Warembo likiwa limenasa katika hifadhi ya Saadan

   Miss Utalii Tanzania waakicheza na watoto wa kijiji cha Saadan
   Miss Utalii Tanzania wakati wakijiandaa kuondoka Udzungwa
   Miss Utalii Tanzania wakifurahi wakati wa mazoezi katika Fukwe ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
   Miss Utalii Tanzania wakiwa katika Picha na Wakazi wa Kijiji cha Saadan.
   Miss Utalii Tz wakipozi na watoto wa kijiji cha Saadan baada ya baada ya chakula cha Mchana
  Miss Utalii Tz wakiwa katika pozi katika Milima ya Udzungwa

  0 0


  Itazame dunia kwa jicho la 3 utabaini kuwa;

  1). Maisha yamekuwa mafupi
  2). Usaliti umezidi.
  3). Pesa ndio kila kitu.
  4). Mapenzi yamekuwa fasheni.
  5). Uongo ndio silaha.
  6). Upendo wa dhati umekufa...imebaki tamaa tu!
  7). Mawazo yetu yako kwenye pesa na mapenzi tu!
  8). Ibada kwa Mwenyezi Mungu tunafanyia mazoea tu...si kutoka moyoni.
  9). Kigezo cha uzuri kimekuwa shepu na sura si ''Tabia''.
  10). Vizuri machoni ila si ''Imara''.
  11). Ukizubaa katika jambo lolote imekula kwako.....SO TAKE CARE.

  0 0

  Na Mwandishi Wetu, Tanga 
   MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Mkoa wa Tanga ni moja kati ya mikoa maarufu kwa viwanda nchini lakini hivi saa hali ya kimaendeleo katika mkoa huo imekuwa mbaya. Kauli hiyo ameitoa leo mjini hapa alipokuwa akiwasilisha mada inayohusu maendeleo ya uchumi kwa Mkoa wa Tanga katika kongamano lililoandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kwa kushirikiana Taasisi ya Maendeleo ya demokrasi kwa vyama vya siasa ya nchini Denmark (DIPD). 

  Profesa Lipumba alisema kuwa hakuna haki bila kuwa na maendeleo yanamgusa mwananchi wa kawaida. Alisema Mkoa wa Tanga imefanikiwa kuwa na rasimali nyingi ikiwemo zao la Mkonge ambalo kwa sasa limekosa msukomo hali inayochangia umaskini kwa wananchi wa mkoa huo.

   "Pamoja na Tanga kuwa na fursa nyingi za kiuchumi lakini bado kadri siku zinavyokwenda umaskini umekuwa ukiwatesa wananchi. Viwanda vilikuwa zaidi ya 70 lakini sasa hakuna hata kimoja kinachofanya kazi huku zao la mkonge lilikosa msukumo wa makusudi kwa wananchi wake. 

   "Katika soko la dunia inaonyesha kuwa Tanga ilikuwa ikizalisha tani 234,000 kwa mwaka lakini sasa mkonge umeporomoka na kufikia tani 25,000 tu hali ambayo imekuwa ikiongeza umaskini kila kukicha. Kama kungekuwa na msukumo wa makusudi wa kufufu zao hili ni wazi Tanga ingekuwa imepaa kimaendelo kwa wananchi wake kutokana na kuwa na kila aina ya rasilimali zikiwemo za matunda na mbogamboga," alisema Profesa Lipumba Profesa Lipumba, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi duniani.

  Alisema ili kuweza kufikia malengo ya mkoa huo kuweza kupambana na umaskini ni lazima serikali ikubali kwa kufanya uwekezaji hasa katika kufungua bandari ya Tanga ambayo ni lango kuu la kiuchumi. Alisema Bandari ya Tanga imekuwa haitumiki ipasavyo hali inawechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa umaskini na hazorotesha harakati za mkoa na wananchi kwa ujumla.

   "Bandari ya Tanga, zao la mkonge pamoja na kukosekana kwa msukumo wa kuimarisha sekta ya elimu ni moja ya masuala yanayoufanya mkoa huu kuzidi kurudi nyuma kiuchumi pamoja na wananchi wake,” alisema Profesa Lipumba.
  Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigombe Mzee Said, akitoa maelezo kwa Profesa Lipumba kuhusu ujenzi  wa kingo ya Bahari ambao umejengwa kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa thamani ya Sh milioni 108.
  Profesa Lipumba, akiiangalia ukuta uliojengwa na wananchi wa Kijiji cha Kigombe mkoani Tanga, mara baada ya kuuzindiwa, kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho Mzee Said.
  Profesa Lipumba, akipata maelezo ya zahanati ya Kijiji cha Kigombe kutoka kwa Daktari wa zahanati hiyo Dk. Uwesu Mtulia.

  Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), akifuatilia mada kuhusu uchumi wa mkoa  inayowasilishwa na Profesa Lipumba.


  Wananchi wakimsikiliza Profesa Lipumba, akiwasilisha mada katika kongamano la Uchumi wa Mkoa wa Tanga lililofanyika leo katika Mkonge Hoteli . Profesa Lipumba.

  0 0

  Picha na Habari-Mdau Abdulaziz Video,Lindi 
  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeandaa huduma za madaktari bingwa kutoka hospitali ya Rufaa MUHIMBILI watakaotoa huduma katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi (SOKOINE) kuanzia tarehe 8.4.2013 hadi tarehe 13.4.2013. 
  Uzinduzi wa huduma hiZi utafanywa rasmi siku ya jumatatu(KESHO) tarehe 8.4.2013,Mgeni rasmi ni mkuu wa mkoa wa Lindi pia uzinduzi huo utahudhuriwa na Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Ndg Emmanuel Humba. 
  Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa Habari,Meneja wa ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Lindi,Bi Fortunata Kullaya alieleza kuwa hatua hiyo imekuja ili kusaidia huduma kwa wateja wa Mfuko huo na wagonjwa wengine ambapo wagonjwa wasio wateja wa Mfuko watatumia taratibu za kawaida zilizopo katika kupata matibabu.
    Hivi karibuni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Kwa kushirikia na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA)imetoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya wajasiliamali katika wilaya za Lindi na Kilwa ili wajiunge na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) NA Kutoa msaada wa Mashuka kwa Hospital za Wilaya ya Ruangwa na Kilwa
   Meneja wa Ofisi ya Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya-Lindi,Bi Fortunata Kullaya akitoa taarifa ya ujio wa Madaktari Bingwa wanaoletwa na Mfuko huo na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF kesho katika hospital ya Sokoine Lindi
  Viongozi wa mfuko wa NHIF pamoja na WAMA  wakiwa wameketi pamoja chini na waliohudhuria katika Elimu elekezi kwa vikundi vya wajasiriamali kujiunga na CHF Iliyofanyika katika kijiji cha Namangale-Lindi Vijijini

  0 0

  WASANII wa Filamu Mkoani Mbeya wameaswa kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa kuaminiana ili kuifanya kazi zao kujulikana kitaifa na kupata masoko mengi ikiwa ni pamoja na kujiongezea kipato. Mwito huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Muda wa Shirikisho la Filamu Mkoa wa Mbeya, Samwel Mwamboma ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha kusambazia Filamu cha Sam Video Centre cha Jijini Mbeya.

   Mwamboma alisema Mkoa wa Mbeya unawasanii wengi sana na wazuri tofauti na Dar Es Salaam lakini wameshindwa kujulikana kutokana na kukosa ushirikiano na uaminifu unaosababishwa na ubinafsi ndiyo unaosababisha kutofanikiwa wala kujulikana kwa wasanii licha ya kushiriki katika Filamu nyingi.

   “ Wasanii mkiwaamini watayarishaji wa Filamu, Wasambazaji, Waongozaji, Wapiga Picha na Waandaaji kazi zetu zitafika mbali sana lakini mkiwa wabinafsi hatutaendelea kabisa” Alisema Mwenyekiti huyo. 

  Aliongeza kuwa Lengo la Kuanzisha Shirikisho la wacheza Filamu Mkoa wa Mbeya ni kuleta Umoja ili kazi za Wasanii wa Mkoa wa Mbeya zijulikane na kupendwa na watazamaji ili Wasanii wakubwa kutoka Dar Es Salaamu watamani kufanya kazi nao na siyo Wasanii wa Mbeya kutamani kuigiza na Wasanii wakubwa. 

  Kwa Upande Katibu wa Muda wa Shirikisho hilo Sadi Mwang’onda alisema kuwa moja ya vitu vinavyosababisha kazi za wasanii wa Mkoa wa Mbeya kuonekana kutokuwa na ubora ni kutokana na kila mtu kufanya kazi kivyake bila ushirikiano ambapo Watayarishaji, Wasambazaji, Wapiga picha na wadau kutokuwa na umoja. Aliongeza kuwa Wasanii wa Mkoa wa Mbeya wanakutana na Changamoto nyingi ambazo ni ukosefu wa Mitaji hivyo kuwaomba Wakazi wa Mkoa wa Mbeya wenye mitaji kuwekeza katika Soko la Filamu ambapo aliongeza kuwa kama wasanii wako tayari kuhakikisha Mwekezaji ananufaika na hajutii kuwekeza kwenye Filamu za Wasanii wa Mkoa wa Mbeya. 

  Aliitaja Changamoto Nyingine kuwa ni kukosekana kwa Elimu miongoni mwa Wasanii ambapo wengi wao wamekosa elimu ya kawaida ya darasani ili hali wengine kutokuwa na ufahamu juu ya kitu wanachokifanyia maigizo, kutokana na hilo Katibu huyo amewakikishia Wasanii kuwa baada ya Shirikisho hilo kutulia atawatafutia Semina na Mafunzo ili wapate mwanga kuhusu Filamu. 

  Katibu huyo alizitaja changamoto zingine kuwa ni pamoja na Wasanii kutofanya utafiti kuhusu kile anachotaka kukiigiza jambo ambalo linasababisha kazi nyingi kuonekana kama zinafanana,ukosefu wa matangazo na wasanii wenyewe kutojiamini kutokana na kazi wanazozifanya hivyo kuonekana ni wababaishaji tu. 

  Mbali na hayo Mwang’onda aliwasihi Wasanii waliojitokeza katika Mkutano huo uliohudhuriwa na Wasanii zaidi ya 50 kutoka Ndani ya Jiji la Mbeya, Wadau wa Filamu pamoja na Wanahabari kuwa Wasanii wanatakiwa kuishi maisha ya Heshima kama wanavyoigiza kutokana na Jamii kuiamini sana kazi za sanaa. Aidha Katibu huyo alisema ili Shirikisho lao liweze kuimarika na kuendelea watakuwa wakifanya mikutano ya mara kwa mara na kuwataka Wasanii hao kufanya kazi kwa ushirikiano na kukutana kila wanapopata nafasi na sio kubaguana.
  MWENYEKITI WA MUDA WA SHIRIKISHO LA WAIGIZAJI MKOA WA MBEYA SAMWEL MWAMBOMA AKIZUNGUMZA AZMA YA KUWAKUTANISHA WAIGIZAJI WA MKOA WA MBEYA KATIKA KIWANJA CHA CITY PUB MBEYA
  KATIBU WA MUDA WA SHIRIKISHO LA WAIGIZAJI WA MKOA WA MBEYA SADY MWANG'ONDA AKIZUNGUMZIA MIKAKATI YA WASANII KUJIKWAMUA KATIKA KAZI ZAO ZA SANAA YA UIGIZAJI MKOA WA MBEYA

  BAADHI YA WASANII WA SANAA YA UIGIZAJI MKOA WA MBEYA WAKIWA KATIKA MKUTANO ULIOWAKUTANISHA WAIGIZAJI KATIKA UWANJA WA CITY PUB JIJINI MBEYA

  0 0


  *** Application cycle 2014 - 2015 currently open ***
  Deadline for submission of online application and supporting documents June 1, 2013. Only successful candidates will be called for interviews scheduled for mid-July, 2013. 

  The Foreign Language Teaching Assistant (FLTA) Program is funded by the U.S. Department of State. Teaching Assistants are vetted through the J. William Fulbright Foreign Scholarship Board. The program aims to strengthen U.S. foreign language instruction and promote mutual understanding by establishing a foreign language native speaker expertise on U.S. campuses. 

  The program enables the teaching assistants to complete their home country pre-service training by engaging in non-degree studies at accredited post-secondary U.S. educational institutions while teaching one or two language courses. 
  Additionally they serve as resource persons in conversation groups, cultural representatives, attendants in language laboratories, coordinators of extracurricular activities or supervisors of clubs and language houses.Selected teaching assistants will enjoy Fulbright status in the United Status. They are expected to teach their language/culture for up to 20 hours per week while taking two courses per semester. All FLTA's receive room and board, a monthly stipend, and tuition waiver for the required coursework, in addition to Fulbright immigration services. The Fulbright grant is for one academic year and is non-renewable.
  The Institute of International Education (IIE) on behalf of Department of State, USA, would like to place several language teaching assistants at universities and colleges in the US as part of a strategic language initiative.
  Kiswahili is one of the targeted languages. For more visit Makulilo's site CLICK HERE

  0 0

  Mabloga wakiwa wamembeba juu mwanalibeneke na mshambuliaji mkabaji Sufiani Mafoto baada ya kufunga penati  ya mwisho na ya ushindi  iliyowapeleka fainali za michezo hiyo iliyofana sana katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam jana.

  Baada ya kufanya vyema katika TBL Media Day Sports Bonanza, Tanzania Bloggers United hivi sasa wanajipanga ili kushiriki katika michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na NSSF Cup mwakani.

  Pia wanapanga kufanya ziara kibao ndani na nje ya nchi, hasa Marekani ambako wanapanga kupambana na Yanga na Simba za DMV.  Katibu wa muda wa timu hiyo Sufiani Mafoto ametoa shukrani tele kwa kampuni ya SAPHIRE kwa kujitokeza kama wafadhili wake wa  kwanza. Amewashukuru pia waasisi wa wazo la kuwa na timu ya mabloga ambao ni wanalibeneke Francis Godwin wa Iringa na Lukaza wa UDOM ambao wanaingia kwenye vitabu vya historia ya tasnia ya blogu kama waanzilishi wa hili.
   Mshauri wa ufundi wa Tanzania Bloggers United, Ankal, akitoa maelekezo wakati wa mapumziko. Ankal alisikitika sana baada ya kiungo Maggid Mjengwa kucheza nusu ya kwanza tu na kuondoka kwenda kuendelea na kazi. Hata hivyo pengo lake lilizibwa na Mroky Mroky na Francis Dande.
   Kikosi cha Tanzania Bloggers United
   Kipa wa Tanzania Bloggers United Othman Michuzi akipongezwa kwa kazi nzuri
   Mshauri wa ufundi, Ankal, akiwa na furaha kwa matokeo mazuri


  0 0

  BWANA HASHIM NA MAI WAIFU WAKE KURUTHUM MAYA WAMEKULA KIAPO KIPYA BAADA YA MIAKA 26 YA NDOA.HARUSI ILIFANYIKA THE HAGUE,  HOLLAND.
  BWANA HARUSI BI HARUSI NA BWANA HIJA.
  KURUTHUM MAYA BI HARUSI.
   MAYA WIFI YAKE NA MWANAE MAYA.
  MAHARUSI NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI.
  MAHARUSI NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI.

  0 0


  Padri Jean Marie akimbatiza mtoto Rose leo Jumapili April 7, 2013 katika kanisa la Mtakatifu Camillus lililopo Silver Spring, Maryland nchini Marekani na baadae viburudisho viliendelea katika kanisa la Mt. Luke lililopo barabara ya Colesville, Downtown, Silver Spring. Aliyembeba mtoto ni mama wa ubatizo Tabitha Mwita wakiwa pamoja na wazazi wa Rose.
  Picha juu na chini ni Padri Jean Marie akiongoza misa ya ubatizo ya mtoto Rose iliyofanyika leo Jumapili katika kanisa la Mt. Camillus.
   Juu na chini ni Wazazi, mama ubatizo na mtoto Rose katika picha ya pamoja

   Picha juu na chini misa ya ubatizo ya mtoto Rose ikiendelea.
  Wazazi, mama ubatizo na mtoto Rose katika picha ya pamoja na Padri Jean Marie baada ya misa ya ubatizo wa Rose kumalizika.

  Ndugu, jamaa na marafiki waliofika kwenye misa ya ubatizo ya mtoto Rose katika picha ya pamoja
  Wazazi wa Rose na kadogoo wao wakipata picha ya kumbukumbu.

  0 0

   Baada ya kumeremeta wadau Rachel Mfinanga na mai hazbendi wake Mlaki Carlos wakiingia katika ukumbi wa Police Officer's Mess Oysterbay Dar es salaam kwa mnuso wa nguvu walioandaa
  Rachel Mfinanga na mai hazbendi wake Mlaki Carlos wakipozi na mabesti wao. Kwa mapicha ya kumwaga BOFYA HAPA

  0 0
 • 04/07/13--22:00: Article 24


 • 0 0

  Wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari jijini Dar zikiwemo Makongo, Airwing, Mtakuja Beach na Chang'ombe wakiwa Safarini Kulekea katika ziara ya kutembelea Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara ambayo yapo kwenye orodha ya urithi wa Dunia katika safari ya iliyoandaliwa na Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) wakati wa kumbukumbu ya Biashara ya Utumwa na kuwaenzi waliopoteza maisha katika biashara hiyo iliyokuwa imeshamiri katika maeneo hayo.
  Biashara hiyo ya Watumwa ilifanyika kwa miaka 400 na kuhusisha zaidi ya Waafrika milioni 15 na watu wenye asili ya Afrika ambao walikuwa waathirika wa ukatili wa Utumwa na kuendelea kuteseka na madhara yaa biashara ya Utumwa.(Picha na Mo Blog.)
  Kiongozi wa msafara huo Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo (wa tatu kushoto) njiani kuelekea Kilwa Kisiwani.
  Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo akitoa mwongozo wa ziara kwa wanafunzi baada ya kufika katika bandari ya Kilwa kabla ya kuelekea Kilwa Kisiwani kwa ziara ya mafunzo ya kumbukumbu za biashara ya Utumwa.
  Ambapo alisema lengo la ziara hiyo ni kutaka Wanafunzi kujifunza madhara ya biashara ya Utumwa jinsi ilivyofanyika na madhara yake na ili waweze kusaidia katika jitihada za kuitokomeza biashara hiyo ambayo mpaka sasa bado inaendelea kufanyika kimya kimya katika maeneo mbalimbali nchini na kuwataka kuzijua haki zao za kibinadamu na kutogeuzwa bidhaa za kuuzwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa udanganyifu wa kupelekwa kufanya kazi nchini za kigeni.
  Mwl. Mwasi wa shule ya Sekondari Chang'ombe (mwenye nyekundu) akiwa ndani ya boti na wanafunzi kuelekea Kilwa Kisiwani.
  Wanafunzi wakiwasili Kilwa Kisiwani.
  Picha juu na chini' Tour Giude' Dullah akitoa malekezo ya ramani ya sehemu watakazotembelea wanafunzi hao ili kupata ufajamu wa jinsi Historia ya eneo hilo ilivyokuwa hadi kufikia biashara ya Utumwa na majengo yaliyokuwa yakitumika Karne ya 9 baada ya kuzaliwa Kristo.
  Wanafunzi wakichukua maelezo muhimu kutoka kwa Mtaalamu wa masuala ya Historia ya Asali ya Kilwa Kiswani na Songo Mnara wakiwa kwenye makaburi waliyozikwa viongozi waliotawala eneo la Kilwa Kisiwani.
  'Tour Giude' Dullah akiendelea kutoa ufafanuzi wa maeneo mbalimbali yaliyotumika enzi za biashara ya Utumwa ikiwemo Misikiti, Gereza na Nyumba ya Sultan Hassan Bin Sultan ambaye alikuwa mtawala wa eneo hilo.
  Wanafunzi wakielekea kwenye Gereza maarufu lililokuwa likitumiwa na kufunga watumwa.
  Muonekano wa Gereza hilo kwa Nje Lango Kuu la kuingia.
  Mhifadhi Mambo ya Kale Kilwa Kisiwani Yussuph Bakari Said (mwenye shati la zambarau) akionyesha Kisima kilichokuwa kikitumiwa na wafungwa ndani ya Gereza hilo.
  Wanafunzi wakiangalia Kisima kimoja wapo ndani Msikiti wakati huo.
  Mmoja ya wananfunzi wa shule hizo walioitembelea maeneo hayo ya kumbukumbu akishangaa Mzinga uliodumu mpaka leo toka Karne ya 9 baada ya kuzaliwa Kristo.
  Mafunzo yakiendelea kutolewa kwa wanafunzi hao.
  Moja ya Majengo ya Nyumba ya Sultan Hassan Bin Sultan aliyeoa wanawake 77 enzi za utawala wake.
  Mhifadhi Mambo ya Kale Kilwa Kisiwani Yussuph Bakari Said katika picha ya kumbukumbu na Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo aliyeambatana na Phillip Musiba pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam katika siku ya kuwakumbuka wahanga wa biashara ya Utumwa.
  Wanafunzi wakisindikizwa na Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo (mwenye kitenge) kupanda boti kurudi Bandarini baada ya kuhitimisha ziara yao Kilwa Kiswani.
  Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo aliyeambatana na mfanyakazi mwenzake Phillip Musiba, walimu waliojumuika na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kilwa katika ziara hiyo katika picha ya pamoja.

  0 0


  For More Videos of Kid President, please click here.

  0 0


  0 0

  Na Mdau Abdulaziz Video
  Abiria wanaosafiri kati ya Mtwara na Lindi kwenda Masasi na watokao Masasi Tunduru,Nachingwea,Liwale na Ruangwa mnatakiwa kuchukua tahadhali kubwa kufuatia zaidi ya Magari 50 na watu wasiopugua 300 kushindwa kupita katika kijiji cha Chipite/Mkwera kufuatia eneo hilo kujaa maji yaliyotokana na Mvua zinazoendelea,

   Eneo hilo, ambalo lilitokea mafuriko makubwa mwaka 1990/1991, limeanza kujaa maji jana, hali ambayo leo imekuwa zaidi na kusababisha msongamano.
    Taarifa zaidi tutaendelea kuwapatia kadri hali inavyoendelea huku msaada wa haraka unahitajika ili kusaidia msongamano uliopo hapo ili kuepusha maafa mbalimbali 

  0 0


  0 0
 • 04/08/13--00:03: MCHONGO WA KAZI, CHANGAMKIA

 • 0 0

   Msanii wa kizazi kipya Faridi kubanda maarufu kama Fid Q akitumbuiza wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach mwishoni mwa wiki.
   Msanii maarufu wa kizazi kipya Sir Juma Nature akimwaga burudani katika tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki.
   Msaninii maarufu wa Hip Hop Roma Mkatoliki akiwapagaisha wapenzi wake katika tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki.
   Kundi la sarakasi la la jijini Dar es salaam likitoa burdani  kwa maelfu ya watanzania waliohudhuria tamasha la Airtel Yatosha lililofanyika Cocobeach mwishoni mwa wiki.
   Mkuu wa Majaji (JB) aliyemiliki jukwaan na msanii nguli wa bongo fleva Sir, Juma Nature  (hayupo pichani) akitoa burdani wakati tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki.
   Umati wa watu  waliohudhuria tamasha la Airtel yatosha jijini Dar es saalam wakipata burudani huku wakishika mabango ya kuwashangilia wasanii mahiri wa kizazi kipya katika tamasha la Airtel yatosha Fid Q alionekana kung'ara zaidi
   Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Levi Nyakundi akibadilishana mawazo na Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki.
  Msanii wa kizazi kipya miondoko ya Hip Hop maarufu kama  Ney wa Mitego  akimwaga burudani kwa mashabiki na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya wakati wa tamasha la Airtel yatosha lililofanyika Cocobeach jijini Dar es Saalam mwishoni mwa wiki.

  ========  =========  =========
  Fid Q, Ney Wamitego wafunika Tamasha la Airtel YATOSHA COCO Beach Jana, mwisho mwa wiki hii Tamasha kuhamia chalinze.
   Airtel Tanzania imeendeleza ahadi yake ya kuzunguka nchi nzima kutoa elimu kwa wateja wake na watanzania kwa ujumla ili kuifahamu huduma yao ya AIRTEL YATOSHA pamoja na faida zake

  Dokezo lilitolewa na meneja uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando alisema "tunawashukuru sana watanzania wote waliojitokeza Coco beach nakujiunga na huduma yetu nafuu ya Airtel yatosha, wote wameikubali na wameona ukweli wa mambo kwamba kweli Airtel yatosha nyingine ya nini???

  Tuwape mpya ya wiki hii ni kwamba tunahamia zetu chalinze, wateja wetu wa mkoa wa pwani sasa ni zamu yenu kupata burudani na elimu ya faida zilizopo ndani ya hii AIRTEL YATOSHA, tutapiga kambi kwa siku mbili yaani Juma mosi na Jumapili paleee kwenye viwanja vya sokoni Chalinze na wasanii kibao na zawadi kibao zitakuwepo.

  Ni wazi kuwa hii haina kiingilio njoo wewe na mshikaji wako upate burudani na ujifunze kutumia huduma yetu mpya ya Airtel yatosha ambayo ni rahisi kujiunga na kujipatia zawadi ofa kibao ukiunga kwa kupiga *149*99# KISHA utaweza kupata dakika za BURE, Intaneti pamoja na SMS zako za kutuma kwenda mtandao wowote nchini

  Wasanii watakaotumbuiza chalinze mwishoni mwa wiki hii ni Fid Q, Juma Nature na wanaume Halisi, Madee na kundi zima la Tip top Connection, pamoja na Ney wa Mitego anaetambasana katika miondoko ya Hip Hop.

older | 1 | .... | 93 | 94 | (Page 95) | 96 | 97 | .... | 3282 | newer