Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110091 articles
Browse latest View live

uwanja wa michezo wa Kirumba Mwanza toka hewani


Habari za Tanzania kwa kina toka TBC

Mzee Hamza Kasongo atwaa tuzo ya maisha ya mafanikio katika tasnia ya habari usiku huu

$
0
0
Mzee Hamza Kasongo (kati) akibadilishana mawazo na Balozi Christopher Liundi (shoto) na mwandishi wa habari mkongwe Mzee Fred Jim Mdoe katika hafla ya siku za nyuma. Mzee Kasongo usiku huu ameibuka kidedea kwa kutwaa TUZO YA MAISHA YA MAFANIKIO KATIKA TASNIA YA HABARI kwenye hafla inayoendelea hivi sasa katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijin Dar es salaam, mgeni rasmi akiwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Ali Shein. 

Mzee Hamza Kasongo mwenye umri wa miaka 74, ni mtangazaji mkongwe wa radio na TV, alikuwapo kama mtangazaji wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwa mara ya kwanza kwa kutajwa Tanzania badala ya Mungu Ibariki Tanganyika siku ya uhuru mwaka Desemba 9, 1961, ambapo aliwasiliana moja kwa moja na Alex Nyirenda wakati akipandisha mwenge mlima Kilimanjaro.

Mzee Hamza Kasongo alikuwa miongoni mwa vijana saba waliochaguliwa  kupata mafunzo ya utangazaji wa Sauti ya Dar es salaam, kabla ya RTD miaka ya 60. 

Baada ya Uhuru, akiwa na hayati  Salim Seif Mkamba na David Wakati (RiP) January 1962 walipata nafasi ya kwenda kupata mafunzo ya utangazaji jijini London, Uingereza, katika Shirika la Habari la BBC na kutangaza. Mwaka 1965 alirejea na kuwa mkuu wa habari na matukio RTD. Baada ya miaka kupita akajiunga na Africa Media Group na kuwa Mkurugenzi wa Habari wa Channel Ten ambapo hadi leo anaendesha kipindi cha Wasaa wa Hamza Kasongo, akimuachia Jenerali Ulimwengu kundesha kipindi kilichochukua nafasi ya Hamza kasongo Hour.

Mshindi wa jumla ya uandishi wa habari umeenda kwa mpiganaji Lucas Liganga wa The Citizen. Tuzo hizi za kila mwaka zimeandaliwa na Baraza la Habari Tanzania.

COMORO YAHIMIZA UHUSIANO ZAIDI NA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

$
0
0

Mhe.Lily Munanka (kulia) akisalimiana na Balozi Roubani Kaambi wa Visiwa vya Comoro Ubalozini Tanzania House Washington DC.
Mhe.Balozi Roubani Kaambi wa Visiwa vya Comoro katika picha ya pamoja na Mhe.Lily Munanka, Kaimu Balozi.
Mhe.Balozi Roubani Kaambi wa Visiwa vya Comoro akisalimiana na Suleiman Saleh,(kulia) Afisa Ubalozi wa Tanzania,Washington DC.
Mhe.Balozi Roubani Kaambi wa Visiwa vya Comoro (katikati) katika picha ya pamoja na Suleiman Saleh,(kulia) Afisa Ubalozi wa Tanzania,Washington DC. Kushoto ni Mhe.Lily Munanka Kaimu Balozi.

Balozi wa visiwa vya Comoro nchini Marekani Mhe. Roubani Kaambi jana alitembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania (Tanzania House) Washington DC na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi Mhe. Lily Munanka ambayo yalilenga katika kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizo mbili. Balozi Roubani ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Visiwa vya Comoro katika Umoja wa Mataifa alisisitiza umuhimu wa Tanzania na Comoro kuimarisha zaidi mahusiano yao kihistoria na kuyatafsiri mahusiano hayo katika mashirikiano zaidi kiuchumi. Balozi Roubani alibainisha kwamba nchi yake inafahamu mafanikio mbali mbali katika sekta za uwekezaji pamoja na utalii na hivyo kuomba nchi yake isaidiwe kuwavutia wawekezaji kutoka Marekani pamoja na kukuza utalii kutokana na mazingira ya nchi yake kufanana na yale ya Tanzania Bara na Visiwani.

Kwa upande wake Kaimu Balozi Mhe. Lily Munanka alimshukuru Balozi Kaambi kwa kumtembelea na kumweleza kwamba kimsingi ameyapokea maombi yake hayo na atayawasilisha katika mamlaka husika ili yatolewe maamuzi stahili. Kwa ujumla Kaimu Balozi Munanka alimhakikishia Balozi Kaambi kwamba Tanzania inathamini mahusiano baina ya nchi zao na kuona umuhimu wa kujenga mashirikiano zaidi kiuchumi baina ya nchi zao mbili kwa faida ya wananchi wao.

Ngoma azipendazo Ankal

$
0
0

Ngoma ya 'Pesa Position Na Yo' ya Madilu na Franco wakiwa na Le T.P. O.K. Jazz mwaka wa 1986 ni balaa!!

Faida za Kujua kuvuta pumzi- Video fupi na freddy macha

$
0
0

Moja ya nguzo kuu za kiafya ambazo hazizungumziwi sawasawa kwetu Afrika ni umuhimu wa kuvuta pumzi. Mwandishi Freddy Macha anaanza msururu wa maelezo juu ya shughuli hii muafaka sana kwetu wanadamu.

Countdown towards Global 2013-Week of 1st April

Article 19


yale yale....

$
0
0

Michuzi,
Tukiwa katika maswala ya ujenzi usiofuata viwango na masharti ya ujenzi, nilikumbana na hoteli iliyoko Shinyanga mjini ambayo imemalizika na wateja wanaishi. Cha kushangaza ni kuwa ngaziimechomoza katika kila corridor ya hoteli hii. Pia ngazi hizo hazilingani. Utakuta nyingine ndoogo na zingine kubwa, kiasi inatia wasiwasi kuhusu usalama wa watumiaji wa hili jengo. Mathalan ikitokea dharura ama hatari yoyote kaam vile moto na majanga mengine matokeo yanajulikana kwa kuangalia design failure hii.

Halimashauri ya Shinyanga mjini mpooo?
Ni mimi mdau SHY TOWN

JOSEPH SENGA MPIGA PICHA BORA WA 2012

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akimkabidhi tuzo ya Mpiga Picha Bora 2012, Joseph Senga kutojka Kampuni ya Free Media inayochapisha magazeti ya Tanzania Daima na Sayari. SDEnga amepata tuzo hiyo baada picha aliyopiga ikimuonesha askarti Polisi akimsurubu Mwandishi wa Habari, Marehemu Daudi Mwangosi wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten.
 Hongera, ulistahili
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akimkabidhi mfano wa hundi mshindi wa jumla wa tuzo za EJAT 2012, Lucas Liganga.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akimkabidhi mfano wa hundi mwandishi mkongwe aliyepata mafanikio. 
Mpiga Picha Bora 2012, Joseph Senga (kulia) akiwa na mpiga picha wa magazeti ya Uhuru na Mazalendo, Emmanuel Ndege ambaye aliingia katika fainali za kinyang'anyilo cha kumtafuta mpiga picha bora.
 Mwandishi wa Habari wa Mwananchi Communications, Anthony Mayunga akipokea tuzo yake.
Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akimkabidhi tuzo ya mwandishi bora wa habari za watoto, Shadrack Sagati kutoka TSN.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI TMA

$
0
0
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba ( kati kati) akifafanua jambo mbele ya wajumbe ( hawapo pichani) jana ( Aprili 5) wakati wa hotuba yake ya kufungua mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ( TMA), ( kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi na ( kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk Agnes Kijazi.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba ( kulia)akimpongeza Mtabiri Mwandamizi na Msimamizi mkuu wa shughuli za utabiri , Wilberforce Kikwasi, ambaye amechanguliwa na Uongozi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuwa ni mfanyakazi bora mwaka huu kutokana na ubunifu katika matumizi ya teknolojia ya kisasa na utafiti kwa kubuni mfuno wa ICT ‘ Software’ ( Digital Meteorological Observatory) inayosaidia kurahisisha mawasiliano na uhifadhi wa taarifa za hali ya hewa, Naibu Waziri huyo jana ( Aprili 5) alikuwa ni mgeni rasmi ufunguzi wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa TMA.
Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi akitoa ufafanuzi wa jambo kabla ya kukaribishwa mgeni rasmi , Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba ( hayupo pichani) wakati wa mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa TMA.
Picha ya Pamoja.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii.

Bloggers Fc yatia fora Media Day

$
0
0
 Kikosi kazi cha Mablogger a.k.a waendeshaji wa mitandao ya kijamii kilichopo chini ya Ankal Issa Michuzi (Shoto) kikiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya mtanange wao wa nusu fainali dhidi ya Timu ya DSJ ulipigwa jioni hii ikiwa ni sehemu ya kunogesha Bonanza hilo la waanahabari lililodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).Bonanza hilo linaendelea hivi sasa kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam.Timu ya Bloggers imetinga hatua ya fainali baada ya kuwatoa DSJ kwa Mikwaju ya Penati.
 Beki wa Bloggers Fc,John Dande (kulia) akichuana vikali na mshambuliaji wa timu ya Radio Maria wakati wa Bonanza hilo.
Strika wa Bloggers Fc,Saleh Ali (chini) pamoja na kuchezewa rafu lakini hakukubali hata kidogo kuruhusu mpira uchukuliwe na adui ambao ni Radio Maria.
 Nyanda Machachari wa Bloggers Fc,Othman Michuzi akiondosha mpira langoni mwake japo alikuwa kazongwa na Mshambuliaji wa timu pinzani ya DSJ.
hatari langoni mwaoo....

Prayer for Tanzania and Neighboring Countries

$
0
0

Hello Tanzanians and Friends,

Please join me to pray for our beloved country Tanzania and its neighboring counties Uganda, Kenya, Zambia, Malawi, Democratic Republic of Congo, Rwanda, Burundi and Mozambique.

We will be praying for just one hour every 1st Saturday of the month starting on May 4, 2013 at 9pm Eastern time or 8pm Central time, or 7pm Mountain time or 6pm Pacific time.

God’s blessings to you all and may God use you as the Daniel of our time who will dare stand in the gap so that His name could be gloried as Tanzania and its neighbors seek God than never before. God responded to a prayer by just one person Daniel for the entire nation of Israel. How about when me and you join hands for the sake of our countries?

Please stay tuned for more details.

Evangelist Frank Mwakasisi, Ph.D.
Founder and President
Mighty Outreach International - "Helping Churches Reach More People for Christ"
PO Box 1655
Portage, MI 49081
USA

DKT. MWAKYEMBE AWAASA WANAHABARI KUWA MAKINI NA KAZI YAO

MHE PHILIP MANGULA NA YOLANDA KABEREGE WAMEREMETA LEO HUKO NJOMBE

$
0
0

Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Njombe Isaya Mengele akiwafungisha ndoa Mhe Philip Mangula na Yolanda Kaberege leo. Katika neno lake, Askofu Mengele amekumbusha Maneno ya Mungu na Kuwataka Wanandoa Kuishi Kwa Misingi ya Dini Kama Ilivyoelekezwa Kwenye Vitabu Vya Dini.
 Waziri mkuu Mhe. Mizengo Pinda katikati akifuatiwa na Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mku wa Wilaya ya Njombe Mhe Sarah Dumba.
 Kushoto ni msemaji wa familia ya mzee Philip Mangula Dr.Lechion Kimilike ambaye ni Mhadhiri wa chuo kikuu huria cha Tanzania Tawi la Njombe[NJOMBE OPEN UNIVERSITY].


 Waziri mkuu Mizengo pinda akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa wilaya ya Njombe bwana Lupyana Fute[Jacky's]ambaye ni diwani wa kata ya Njombe mjini leo wakati wa Harusi ya Mzee Philip Mangula.
 Hapa ni ndani ya kanisa la KKKT Dayosisi ya kusini Njombe Mjini ambako pingu za maisha kwa mzee wetu Mangula zimefungwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana Katika harusi ya mzee Mangula leo Njombe.
Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Philip Mangula na Mkewe Yolanda Kaberege leo baada ya kufunga pingu za maisha. 
Picha na Gabriel Kilamya

Habari za Tanzania toka TBC

Article 10

Ziara ya Balozi Kamala Oostende, Ubelgiji

$
0
0
Mhe Balozi Dr. Diodorus B. Kamala Balozi wa Tanzania Ubelgiji akiwa wenyeji wake wa Oostende Ubelgiji wakiwa wamepanda usafiri wa farasi tayari kuanza safari ya kuutembelea mji wa  Oostende baada ya mkutano wake na Watanzania wanaoishi Oostende Ubelgiji.

TFF Technical Development Plan 2013 - 2016

Sherehe za mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwa kikundi cha Island Exercise Group

$
0
0
 Baadhi ya wana michezo wa vikundi vya mazoezi wakiwa katika maandamano ya kusherehekea mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwa kikundi cha Island Exercise Group zilizofanyika hapo katika uwanja wa makao makuu ya Brigedia nyuki Migombani.
 Vijana wa kitambi noma wakiwa makini katika mazoezi yao ya viungo wakionyesha umahiri wao kwa vile wao ni chem Chem ya kuenea kwa vikundi vyengine vya mazoezi hapa Zanzibar.
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akiwa mwenye furaha akiambatana na Mumewe Balozi Seif wakiingia kwenye uwanja wa michezo wa Brigedia nyuki Migombani mara baada ya kuyapokea maandamano ya wana vikundi vya mazoezi. Nyuma ya Mama Asha ni Waziri wa Habari, Said Ali Mbarouk , Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameri Kificho na aliyevaa track Suit ya Kijani ni mwakilishi wa jimbo la Rahaleo Nassor  Al-Jazira.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho ambae  naye alialikwa katika hafla hiyo na kushiriki pia kwenye maandamano hayo. Katikati yao ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Island Exercise Group Brigedia General Sharif Sheikh Othman.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza katika maadhimisho ya mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwa kikundi cha mazoezi cha Island Exercise Group hapo Migombani. Kulia ya Balozi Ni Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michazo Said Ali Mbarouk na Kushoto yake ni Mwenyekiti wa Kikundi hicho Brigedia General Sharif Sheikh Othman. Picha na Hassan Issa wa OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis Ame
Jamii Nchini inawajibu wa kuzingatia zaidi matumizi bora ya vyakula vinavyopunguza mafuta  kwa nia ya kujijengea afya bora sambamba na maisha marefu yenye kuambatana na akili iliyotulivu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo mara baada ya kuyapokea maandamano ya wanamichezo wa mazoezi wa vikundi mbali mbali vilivyoshiriki katika uzinduzi rasmi wa Kikundi cha mazoezi cha Island Exercise Group  ambacho tayari kimeshatimiza mwaka mmoja hapo katika uwanja wa michezo wa Makao makuu ya Brigedia Nyuki Migombani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Balozi Seif alisema upo muamko wa kutosha wa watu wengi kujiunga katika vikundi vya mazoezi jambo ambalo huleta faraja kwa afya zao lakini wakati huo huo baadhi yao wanashindwa kuzingatia mfumo mzuri wa matumizi ya vyakula wanavyotumia.
Alieleza kwamba si vyema kwa mtu kusubiri ushauri wa Daktari  wakati anapobainika kusumbuliwa na maradhi mbali mbali mengi kati ya maradhi hayo husababishwa na  ukosefu wa mazoezi.
“ Pamoja na mazoezi  yanayoendelea kuchukuliwa na wana michezo walio wengi  lakini bado wanapaswa kuepuka vyakula  vyenye kuleta athari kwenye miili yao”. Alisisitiza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Balozi Seif alifahamisha kwamba inavutia na kutia moyo kuona mazoezi yanayofanywa na wanamichezo katika sehemu tofauti yamekuwa yakishirikisha watu wa rika tofauti wakiwemo pia watoto wadogo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaasa wana michezo hao kuhakikisha wanadumisha suala la amani na Utulivu wa Nchi uliopo ambao kutokuwepo kwake maana yake hata muda wa kufanya mazoezi ambayo ni muhimu kwa afya za wanaadamu utatoweka kabisa.
Balozi Seif alisema zipo baadhi ya Nchi Duniani zikiwemo pia jirani na Tanzania  huadhimisha siku maalum ya kumbu kumbu ya mauaji yaliyotokea kwenye nchi zao kwa sababu  ya kuichezea amani.
Aliupongeza Uongozi wa taasisi inayosimamia vikundi vya mazoezi Zanzibar         { ZABESA } kwa juhudi zake mbali mbali zinazoendelea kuhamasisha kundi kubwa la watu hasa Vijana kujiunga na vikundi vya mazoezi.
Alisema mikusanyiko inayojumuisha wanamichezo hao mara nyingi huleta Umoja na upendo miongoni mwao na hatimae kuchangia kuondoa kwa makundi katika maisha yao ya kawaida.
Mapema katika Risala yao iliyosomwa na Mohd Ahmad wenyeji wa hafla hiyo Kikundi cha Island Exercise Group walisema kikundi chao kimelenga kuwakusanya wanamichezo tofauti hasa vijana katika harakati hizo.
Walisema vijana wengi ambao ndio wanaounda kundi kubwa katika jamii hujiingiza katika vitendo viovu vinavyosababisha kupata maradhi na hatimae kupoteza nguvu kazi  inayotegemewa na taifa.
Wana kikundi hao wa Island Exercise Group pia walieleza changamoto wanazopambana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa maeneo maalum ya kufanyia shughuili zao pamoja na sehemu za mazoezi.
Akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk alisema Wizara hiyo tayari imeshaliagiza shirika la Utangazi Zanzibar { ZBC } kuanzisha vipindi maalum vya mazoezi kutokana na umuhimu wake.
Waziri Mbarouk alisema hatua hizo itasaidia kuipa fursa Jamii majumbani kufuatilia vipindi hivyo kwa vile utafiti unaonyesha kwamba wengi wa wananchi hao wanakosa  muda wa kufanya mazoezi ya viungo.
Hafla hiyo ya kutimia mwaka mmoja tokea kuanzishwa kwa kikundi cha mazoezi cha Island Exercise Group iliyoongozwa na Brass Bendi ya Chuo cha Mafunzo Zanzibar na kupambwa na ngoma maarufu ya kibati ilijumuisha pia mchango wa papo kwa papo uliolenga kutunisha mfuko wa Kikundi hicho.
Zaidi ya shilingi milioni 2.8 zimeahidiwa kutolewa  kutoka kwa viongozi, maafisa pamoja na wana vikundi mbali mbali katika kusaidia kikundi hicho cha Island Exercise Group kinachoongozwa na Mwenyekiti wake Brigedia General Sharif Sheikh Othman. Balozi Seif naye aliahidi kuchangia shilingi Milioni 1,000,000/-.
Vikundi vipatavyo 39 kati ya 40 vya Mkoa Mjini Magharibi vilialikwa katika hafla hiyo vikiwemo vya Kizimkazi Wilaya ya Kusini,Mpapa na Pagali Wilaya ya Kati pamoja na kikundi maarufu cha Barafu kutoka Mkoani  Dar es salaam.


Viewing all 110091 articles
Browse latest View live




Latest Images