Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 937 | 938 | (Page 939) | 940 | 941 | .... | 3348 | newer

  0 0

  Marehemu Mzee SK George Mallya
  Familia ya  Mallya inasikitika kutangaza kifo cha Mzee SK George Mallya aliyefariki kwenye hospitali ya KCMC siku ya Jumamosi tarehe 8 Agosti. Taarifa ya familia inaeleza kuwa marehemu  anatarajiwa kuzikwa siku ya Alhamisi tarehe 13 Agosti, nyumbani kwake Maili-Sita, Moshi, ambako mipango ya mazishi inafanywa kwa sasa.
  Marehemu Mzee SK George Mallya atakumbukwa kama mmoja wa wanajeshi shupavu wa Kings African Rifles (KAR) wa  Tanganyika Battalion nyakati za Vita Kuu vya Pili (World War Two) ambapo alienda kupigana na Wajapani kule Burma (siku hizi Myanmar).
  Baada ya Vita kuisha mwaka wa 1945, alishika nyadhifa mbalimbali katika Serikali za Mitaa, hadi kuwa kiongozi mkuu wa kwanza wa Kiafrika wa Jiji la Dar es Salaam. Baada ya kutoka Serikalini, aliiongoza kampuni ya Lonrho Tanzania hadi alipostaafu na kuhamia Moshi.
  Ameacha watoto wanne wa kike na mmoja wa kiume, pamoja na wajukuu na vitukuu kadhaa.

  Mungu Ailaze Roho yake 
  mahala pema Peponi.

  AMINA

  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  Wasanii nchini wametakiwa kurejesha kwa jamii sehemu ya faida wanayoipata kupitia kazi zao za Sanaa kwa kuwakumbuka watoto wenye mahitaji maalum ili kujijengea mtandao wa kudumu wa masoko, uhalali na taswira nzuri kwa jamii.

  Wito huo umetolewa mapema wiki hii na mtengeneza filamu wa Tanzania mwenye makazi yake nchini Marekani Bi. Honeymoon Mohamed wakati akiwasilisha mada kuhusu Filamu za Kitanzania na Masoko kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa inayoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

  “Wasanii wanaitegemea jamii kama chanzo cha mapato yao hivyo ni lazima wajenge utamaduni wa kurejesha kile kidogo wanachokivuna kutoka kwa jamii kupitia kusaidia watu wenye uhitaji maalum” alisema Honeymoon ambaye filamu yake ya Daddy’s Wedding  imeshinda tuzo kwenye tamasha la kimataifa la filamu la Zanzibar (ZIFF) lililomalizika hivi karibuni eneo la Ngome Kongwe, Zanzibar.

  Aliongeza kwamba watoto wenye uhitaji maalum wanapata faraja na kuhisi kupendwa na jamii pale wanapotembelewa mara kwa mara na watu mbalimbali wenye umaarufu na nafasi kubwa katika jamii hivyo wasanii wetu hawana budi kuwa sehemu ya kujenga faraja hii kwa watoto hawa.

  Kwa mujibu wa Honeymoon wasanii wa Tanzania wako nyuma katika kuikumbuka jamii hususani kutembelea makazi ya watoto wenye uhitaji maalumu na kuchangia huduma mbalimbali zinazokuwa zinahitajika.

  “Watoto wenye utindio wa ubongo wako wengi, kuna wale wenye ulemavu wa ngozi na wengine wanaishi wakiwa yatima kwenye vituo mbalimbali lakini wasanii wetu wamekuwa wazito kuwakumbuka. Wasanii hawana budi kuyakumbuka makundi haya maana wako kwa ajili ya jamii” alisisitiza.

  Awali kabla ya uwasilishaji wa mada hiyo, watoto wanaoandaliwa kupitia programu ya BASATA ya ‘Sanaa kwa Watoto’ kutoka Shule ya Msingi wa Msimbazi iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam walitoa burudani mbalimbali za Sanaa wakisaidiana na Kikundi cha Sanaa cha Jivunie chenye maskani yake neo la Mbagala Manispaa ya Temeke.
  Afisa Habari wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Aristides Kwizela (Kushoto) akifuatilia burudani zilizokuwa zikitolewa na watoto wanaondaliwa na Baraza hilo kupitia programu ya ‘Sanaa kwa Watoto’ wakati wakitumbuiza kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii. Watoto hao wanatoka shule ya Msingi ya Msimbazi iliyoko Ilala jijini Dar es Salaam. Katikati ni Msanii wa filamu Honeymoon Mohamed na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Stadi za wasanii Bi. Vick Temu.
  Sehemu ya watoto wanaoandaliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kupitia programu yake ya Sanaa kwa Watoto wakicheza igizo kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii. Watoto hao wanaosoma Shule ya Msingi Msimbazi walikuwa kivutio kikubwa kwa wadau wa Sanaa.
  Wasanii kutoka Kundi la Ngoma za Asili na Maigizo la Jivunie lenye makazi yake eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam wakionesha ufundi wao katika kuchenza ngoma za asili kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA mapema wiki hii.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwenye Jukwaa la Sanaa la BASATA linalofanyika makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba kwa mwezi mara mbili siku za Jumatatu.

  0 0

  Katibu tawala mkoa wa Arusha Ado Mapunda jana alizindua mashindano ya kuibua vipaji vya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars jijini Arusha na kuwataka vijana wanaoshiriki mashindano hayo kujituma na kucheza kwa bidii ili kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji nyota.

  Hafla ya ufunguzi ilihudhuliwa na viongozi wa shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) mkoa wa Arusha, mdhamini wa mashindano Airtel Tanzania na wadau wengine wa soka. Ufunguzi huo uliufanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

  “Tumepewa nafasi ya kuwa washiriki katika mashindano haya ya Airtel Rising Stars 2015. Hivyo inatupasa tudhihirishe kuwa mkoa wetu una vipaji na tunaweza kuchangia katika maendeleo ya soka kwa kutoa wachezaji kwenye timu za vijana za taifa”, alisema Mapunda Arusha inashirikisha timu ya wasichana ambapo timu kombaini kutoka mkoa huo itasafiri kuelekea Dar-es-Salaam mwezi ujao kushiriki mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa.

  Timu nyingine kwa upande wa wasichana ni Ilala, Temeke, Kinondoni, Mbeya na Mwanza. “Naamini vijana hawa wanaoibuliwa katika Airtel Rising Stars kila mwaka wanahitajika sana katika kuongoza nchi yetu kufika mbali katika Mafanikio”, alisema Mapunda na kuwapongeza Airtel katika kuwekeza katika maendeleo ya Mpira.

  Programu hii ya soka la vijana ilianzishwa nchini Tanzania na sehemu nyingine barani Afrika mnamo mwaka 2011 na ime0nyesha kwa vitendo na imekua chombo muhimu katika maendeleo ya soka hasa katika soka la wasichana. Timu ya Taifa ya wasichana inaundwa na wachezaji kutoka Airtel Rising Stars.

  Alisema katika soka wachezaji wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira. “ Soka imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na mishahara wanayopata”, alisema na kuwataka wasichana kuwa na malengo ya mbali.

  Akiongea katika ufunguzi huo Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde aliwashukuru viongozi wa shirikisho la mpira wa miguu TFFA) na chama cha soka mkoa wa Arusha kwa muda wao na ushirikiano wao katika mashindano. “ Pia natoa shukrani zangu za dhati kwa mgini rasmi kuja kuungana nasi katika uzinduzi huu.

  Matinde amewataka wasichana kufanya vizuri na wayatumia mashindano ya Airtel Rising Stars kufanikisha ndoto zao kupitia soka. Mechi ya ufunguzi iliwakutanisha Chriss FC na Future Stars ambapo mechi ilikwenda sare ya bila kufungana.
  Katibu tawala Jiji la Arusha Ado Mapunda (RAS) akikagua timu katika ufunguzi wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars jijini Arusha jana.
  Katibu tawala jiji la Arusha Ado Mapunda (RAS) akiongea na wachezaji katika ufunguzi wa mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars jijini Arusha jana.

  0 0

  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Ndugu Erasmus Rugarabamu kwa niaba ya Menejimenti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa akitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya ambaye pia ni Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma kwa ushindi mnono alioupata katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kutafuta mgombea wa ubunge Jimbo la Mbinga Magharibi. Eng. Manyanya alishinda kwa kura 13,276 ambapo mshindi wa pili alikua na kura 3,466. Jumla ya wagombea walikua 10 ambapo tisa kati yao walikuwa ni wanaume.

   Awali Jimbo hilo lilikuwa nimeshikiliwa na hayati Capt. John Komba. Kwasasa imebaki hatua ya mwisho ya majina ya wagombea kupitishwa na Uongozi wa juu wa Chama kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Chama  cha Mapinduzi majimboni katika uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba mwaka huu 2015. Uongozi na Watumishi wote wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa unamtakia kila la heri Eng. Manyanya katika safari yake hiyo na hatimae aweze kushinda katika Jimbo hilo. 

  Akitoa shukurani kwa niaba ya watumishi Katibu Tawala Msaidizi Kitengo cha Serikali za Mitaa Ndugu Albinus Mgonya alimpongeza Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa kwa msukumo mkubwa wa maendeleo aliouweka katika kipindi cha uongozi wake hususani katika sekta ya elimu ambapo alianzisha Azimio la Kasense kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya elimu mashuleni, Kuboresha afya ya mama wajawazito na watoto wachanga, usafi wa mazingira ambapo alianzisha kampeni ya Sumbawanga Ng'ara iliyozinduliwa na Mhe. Makamu wa Rais, Kampeni ya upandaji miti, kuboresha mazingira ya utalii katika maporomoko ya Mto Kalambo, kuboresha hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa, Kuwaunganisha watumishi na viongozi katika kufanya kazi kwa pamoja n.k 

  (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa  0 0

   THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS   TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joseph B. Masikitiko kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi huo Ndugu Masikitiko alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo (TBS).

  Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Balozi mmoja na kuwabadilishia vituo vya kazi Mabalozi wawili kama ifuatavyo:

  (i)    Lt. Gen. Charles L. Makakala, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Kabla ya uteuzi huo Lt. Gen. Makakala alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College).
  (ii)Balozi Wilson Masilingialiyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi amehamishwa kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Liberata Mulamula aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa. Atakuwa pia anaiwakilisha Tanzania nchini Mexico.

  (iii)                 Balozi Irene Kasyanjualiyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi kushika nafasi inayoachwa wazi na Balozi Wilson Masilingi.

  Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Agosti 11, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Uteuzi na uhamisho huu unaanzia tarehe 07 Agosti, 2015.
  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.
  11 Agosti, 2015


  0 0
 • 08/11/15--07:22: TAIFA STARS YAANZA MAZOEZI
 • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 142
  TAREHE 11 AGOSTI 2015
  KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kimeanza mazoezi katika uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

  Wachezaji wa Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Mkwasa watakua wakijifua mara mbili kwa siku asubuhi na jioni katika uwanja wa Karume katika kujiweka fit na maandalizi ya mchezo huo.

  Kufuatia baadhi ya wachezaji kuwa na majukumu na timu zao kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Hisani utakaochezwa Agosti 22, Mkwasa amewaongeza wachezji wengine kumi (10) kutoka katika orodha yake ya akiba.

  Lengo la kambi hii ya awali ya siku tano, ni kocha mkuu pamoja na benchi lake la ufundi kupata nafasi ya kuwaona wachezaji katika mazoezi hayo kabla ya safari ya kuelekea nchini Uturuki Agosti 23 mwaka huu kwa kambi ya siku kumi.

  Wachezaji walioitwa na kuanza mazoezi leo ni Said Mohamed, Vicent Andrew (Mtibwa Sugar), Mohamed Hussein, Ibrajim Hajibu (Simba SC), Hamis Ali, Juma Mbwana (KMKM), Tumba Sued (Coastal Unioni), Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Ibrahim Hilka (Zimamoto– Zanzibar) na Mohamed Yusuf (Prisons).

  Wachezaji wengine waliopo kambini ni Said Ndemla, Hassan Isihaka, Abdi Banda(Simba SC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Orgeness Mollel (Aspire Academy) na Abdulhaman Mbambi (Mafunzo).


  TWIGA STARS KUIVAA HARAMBEE STARLETS
  Timu ya Taifa ya  Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) iliyopo kambini kisiwani Zanzibar, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Wanawake kutoka Kenya (Harambee Starlets) Agosti 23, 2015.

  Mchezo huo wa kirafiki utachezwa katika uwanja wa Aman Kisiwani Zanzibar, ikiwa ni sehmu ya maandalizi ya kikosi hicho kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofayika nchini Congo-Brazzavile kuanzia Septemba 4 – 19, 2015.

  Twiga Stars inaendelea na mazoezi kutwa mara mbili katika viwanja vya Aman na Fuoni chini ya kocha wake mkuu Rogasian Kaijage kujiandaa na fainali hizo za michezo ya afrika, wachezaji wote waliopo kambini wapo katika hali nzuri wakiendelea kujifua na michezo ya Afrika.


  USAJILI                                                                                         Dirisha la usajili limeongezwa toka tarehe 06 Agosti hadi tarehe 20 Septemba, baada ya muda huo klabu itakayochelewesha kuleta usajili wake itatozwa kiasi cha shilingi laki tano (Tsh 500,000) kwa kila mchezaji itakayemsajili mpaka siku ya tarehe 30 Agosti.
  Mwisho wa kufanya uhamisho wa kimataifa wa wachezaji kwa njia ya mtandao TMS ni tarehe 6 Septemba.
  Kikao cha kamati ya sheria kitakaa tarehe 28 kwa ajili ya kuupitisha usajili na kitakaa tena tarehe 8/9/2015 kwa ajili ya kupitisha usajili.
  Kuanzia tarehe 21 hadi 27 itakuwa ni wiki ya pingamizi, ambapo majina yatabandikwa TFF Karume na kuwekwa kwenye mtandao ili kuwezesha vilabu vyenye pingamizi kuwawekea wachezaji mapingamizi.
  Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza tarehe 12 Septemba 2015, Daraja la kwanza (FDL) ikitarajiwa kuanza Septemba 17 na Ligi Daraja la pili inatarajiwa kuanza Oktoba 16 mwaka huu.


  MICHUANO YA COPA COCA-COLA 2015
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) bado linaendelea na mazungumzo na wadhamini wa michuano hiyo (Coca-Cola). Kutokana na mazungumzo hayo, ratiba ya michuano hiyo itachelewa kutoka.

  Hivyo, tunawaomba kuwa na uvumilivu wakati mchakato wa mazungumzo hayo yanayokaribia ukingoni ukiendelea.  UAMUZI WA KAMATI YA RUFAA YA TFF JUU YA RUFAA YA DR. DEVOTA JOHN MARWA,YA MAAMUZI YA KAMATI YA UCHAGUZI WA SOKA LA WANAWAKE (TFF)

  Mwomba rufani, Dr. Devota John Marwa, (Mrufani) ni msomi mbobezi katika taaluma ya michezo, akiwa ni mhadhiri katika kitengo kinachojihusisha na taaluma ya michezo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Akiamini kwamba anakidhi vigezo vilivyowekwa kwa nafasi ya mgombea uenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake(TWFA), alichukua fomu ya kuomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho.

  Maombi hayo yalikumbana na pingamizi zilizoletwa na wakereketwa wawili wa soka la Wanawake, Bi. Chichi Mwidege na Bi. Mwajuma Noty, ambao kwa pamoja walimwekea pingamizi Mrufani, kwamba hakidhi matakwa ya kanuni za ugombea wa nafasi ya Mwenyekiti.

  Waleta mapingamizi walidai kuwa Mrufani hakuwa na sifa zilizoainishwa katika Kanuni za Uchaguzi za T.F.F. (TFF Electoral Code) Ibara ya 9 (tisa) kipengele cha 3 (tatu), kinachomtaka mgombea awe amejihusisha na uongozi wa mpira wa miguu kwa muda usiopungua miaka mitano.

  Aidha Ibara ya 28 (ishirini na nane) kipengele cha 3 (tatu), kinamtaka mgombea awe amejihusisha japo miaka 2 (miwili) katika shughuli za maendeleo ya mpira wa miguu nchini.  Kamati ya Uchaguzi iliridhia mapingamizi hayo na kuliondoa jina la Mrufani katika orodha ya wagombea wa nafasi hiyo ya Mwenyekiti. Rufani hii ni matokeo ya uamuzi huo wa Kamati ya Uchaguzi uliotolewa taraehe 22 Julai, 2015.

  Kwa ujumla, sababu za kupinga maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi zinaweza kuhesabiwa kuwa ni mbili. Moja ni iliyojikita juu ya hitilafu katika kuamua kwamba Mrufani hakuwa na uzoefu katika uongozi wa soka kwa muda ulioainishwa. Sabau nyingine ni kwamba Kamati ya Uchaguzi illibua sababu ambayo haikuwa katika Hati ya pingamizi iliyoletwa na Mleta pingamizi.

   Wakati ambapo Mleta pingamizi alijikita katika kipengele cha 28(3), Kamati iliibua kipengele cha 28(8), cha Katiba ya TWFA kinachomtaka mgombea awe ametimiza uzoefu wa uongozi wa miaka mitano, ambacho hakikuwemo katika hoja za pingamizi zilizowasilishwa na mleta pingamizi.

  Katika kufikia uamuzi wake, Kamati ya Rufani ilizipitia sababu za Mrufani kama zilivyoletwa, na baada ya kusikiliza maelezo ya Mrufani na hoja za Mwakilishi wa TFF, Wakili Msomi Edward Augustino, na imeamua kama ifuatavyo. Tutaanza na hoja ya mwisho.

  Je, Kamati ilikuwa sahihi kuibua kipengele ambacho hakikuletwa katika hati ya mapingamizi? Kamati inaweza kuibua kipengele hicho endapo kwa kufanya hivyo, itakuwa imejielekeza katika nia njema ya maslahi ya suala linalozungumziwa.

  Sharti jingine ni kwamba hoja hiyo inyoibuliwa isiwe na athari hasi(prejudicial) kwa mhusika. Kaika suala hili hata hivyo, hoja iliyoletwa na Mleta pingamizi, yaani hoja chini ya kifungu cha 28 (3), imeainisha kipindi kifupi cha uzoefu
  (miaka 2), na hoja iliyoibuliwa na Kamati inahitaji uzoefu wa miaka 5.

  Endapo Mrufani angekuwa na uzoefu wa miaka 3 hadi 4, bado angekwama kutokana na hoja iliyoibuliwa na Kamati. Hii kwa vyovyote ingekuwa ni athari hasi (negative impact) katika harakati za Mrufani. Ni vema

  Kamati zinazosikiliza malalamiko zikajikita kwenye malalamiko yaliyoletwa na wahusika wenyewe. Kama pigamizi lingekuwa liko juu ya kipengele hicho tu, tusingesita kukubaliana na sehemu hii ya rufani. Hata hivyo, takwa la uzoefu wa miaka 5 limeainishwa pia katika Ibara ya 9 (3), ambayo ilikuwa ni sehemu ya mapingamizi yaliyokuwepo kwenye hati ya mapingamizi.

  Kwa sababu hiyo, Kamati ya Rufani haioni kama hoja hiyo ina mashiko. Haitaitilia maanani. Hoja kuu ndani ya rufaa hii ni je, Kamati ya Uchaguzi ilijielekeza vema kuhusu suala la uzoefu wa uongozi ulioainishwa na Katiba?

  Mrufani ameieleza Kamati ya Rufani mlolongo wa shughuli ambazo amekuwa akizifanya, nyingi zikiwa zimejikita zaidi katika taaluma. Miongoni mwa shughuli hizo ni kuandaa Mpango Mkakati wa kuendeleza soka la wanawake. Mpango huu uliridhiwa na kuwasilishwa Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira Duniani, yaani FIFA.

  Maelezo mengine ni kushiriki katika kuongoza timu mbali mbali kule Chuo Kikuu, zingine zikiwa za watoto wadogo ambao baadhi ya matunda yake ni wachezaji walioibukia kwake kama vile Simon Msuva. Alisema zaidi kuwa alishiriki kuandaa warsha ilizoandaliwa kwa ushirikiano kati ya FIFA na TFF.

  Aidha. Alisema kuwa amekuwa kiongozi tangu akiwa bado kwenye vyuo vya ualimu, na baadaye alipohitimu na kufanya kazi kama Mwalimu, kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliko mpaka sasa. Akasema, hata alipokuwa Sweden kwa masomo ya juu pia lijihusisha na programu za maendeleo ya soka la wanawake.

  Wakili msomi wa TFF akijibu hoja hizo, alikubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi kuwa Mrufani hajaonesha popote kwamba amewahi kuongoza soka, akasema Mrufani ni mtaalamu tu kama msomi, jambo linaloweza kufanywa na msomi yoyote. Akamalizia kwa kuiomba Kamati ya Rufani za Uchaguzi kuitupilia mbali rufaa ya Mrufani kwa kukosa mashiko.

  Tofauti na Kamati ya Uchaguzi, Kamati ya Rufani imeona kuwa kwa maslahi mapana ya mchezo wa soka katika ujumla wake, ni vema kuweka tafsiri pana (wide interpretation) juu ya sifa zinazozungumzwa, badala ya kuweka tafsiri finyu (restricted/narrow interpretation) kama ilivyofanya Kamati ya Uchaguzi.

  Baada ya kufanya hivyo, kuhusiana na Mrufani, Kamati imeona kuwa ana sifa zinazostahili. Kupitia sababu alizozitoa, na vielelezo vyake, Kamati ya Rufani haina wasiwasi kuwa Mrufani ana uzoefu mbali mbali sio katika soka tu, bali pamoja na michezo katika ujumla wake.

  Tumeshuhudia katika maelezo yake kwetu kwamba ushiriki wake katika hatua mbali mbali, japo hakuwahi kuchaguliwa, sio ushiriki wa kitaaluma tu, kama msomi mwingine yeyote. Ni ushiriki wenye dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko/maendeleo katika soka la wanawake. Maelezo

  yake kuwa aliaandaa programu ya maendeleo ya soka la wanawake, hayakupingwa. Kamati ya Uchaguzi ingeangalia namna ambavyo “visheni” iliyomo katika programu ile ambavyo ingeweza kutekelezwa na mtu aliyeaiandaa. Kwa hiyo, katika hoja hii, Kamati inakubaliana kuwa Mrufani

  anazo sifa stahiki, na kukatwa kwa sababu hii, Kamati ya Uchaguzi haikujielekeza vema. Kwa hiyo, Mrufani ameshinda rufaa yake? Kamati ya Rufani inachelea kujibu swali hili moja kwa moja. Utaratibu wa kuwasilisha rufani ulikiukwa, na hapa ndipo rufaa hii inapokwaa kisiki.  Chini ya Ibara ya 13 (1) cha Kanuni ya
  Uchaguzi (Electoral Code), mgombea ambaye hakuridhika na maamuzi, atawasilisha rufaa yake ndani ya siku 3 (tatu) tangu uamuzi anaoupinga ulipotolewa.

  Kipengele cha 3 (tatu) cha ibara hiyo kinasema kwamba Mrufani yoyote atakuwa na uhalali endapo rufaa yake imewasilishwa kwa mujibu wa kanuni hizo.  Uamuzi unaolalamikiwa ulitolewa tarehe 22 Julai 2015, sababu za rufaa ziliandaliwa tarehe 27 Julai na sababu hizo za rufaa zililipiwa tarehe 28 Julai, 2015. Ni dhahiri kwamba rufaa ililetwa nje ya muda uliowekwa na kanuni, na kwa hiyo inakosa uhalali kisheria na kikanuni.

  Japo katika mwenedo na maamuzi yake Kamati ya Rufani za Uchaguzi haifungwi na taratibu za kimahakama, suala la muda wa kuwasilisha rufani sio miongoni mwa mambo ambayo Kamati inaweza kutoyazingatia. Kwa sababu hiyo, Rufaa hii imetupwa, lakini kwa sababu tofauti na zile za Kamati ya Uchaguzi.

  Pamoja na uamuzi huu, Kamati ya Rufani za Uchaguzi inapenda kwa namna ya kipekee kumpongeza Mrufani kwa jitihada alizozionesha kutaka kuitumikia TWFA. Ni matumaini ya Kamati kuwa hatokata tama, na kwamba atakuwa tayari, akitakiwa kufanya hivyo, kupitia taalum yake, kushirikiana na wenzake katika jitihada za kuendeleza soka la akina mama lililo na changamoto lukuki.

  Imetolewa na,
  JULIUS M. LUGAZIYA
  Mwenyekiti-Kamati ya Rufani za Uchaguzi


  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

  Shindano la kuibua na Kusaka Vipaji vya Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo limedumu kwa takribani Miezi Minne hatimaye shindano hilo linakaribia kufika tamati mnamo tarehe 22 August 2015 huku Mshindi Mmoja Akiondoka Na Kitita Cha Shilingi Milioni Hamsini Za Kitanzania. Na Washiriki waliofanikiwa kuingia Hatua ya Kumi bora watapata kifuta jasho huku wakiwa na mkataba mnono wa kufanya kazi na Kampuni namba moja ya Kutengeneza na Kusambaza filamu za Kitanzania ambao pia ndio waratibu wa Shindano Hilo la Tanzania Movie Talents (TMT) ya Proin Promotions Ltd.
  Shindano la TMT lilianza mapema mwezi wa Nne kwa kutafuta vipaji katika Kanda ya Ziwa ambapo usaili ulifanyika Mkoani Mwanza na kuhitimishwa Kanda ya Pwani Mkoani Dar Es Salaam kwa kupatikana Jumla ya Washindi 20 kutoka Kanda sita za Tanzania.
  Washindi wa kanda sita walipata fursa ya kuingia ndani ya mjengo wa TMT huku wakipatiwa mafunzo ya sanaa kutoka kwa Walimu wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam huku mchujo ukiendelea na kupelekea kila wiki Washiriki wawili kuaga shindano, takribani wiki tano jumla ya washiriki 10 waliweza kuaga shindano hili ambalo limefikia hatua ya kuwapata washiriki 10 waliofanikiwa kuingia hatua ya Kumi bora huku wakingojea fainali itakayotoa mshindi wa kitita cha shilingi milioni hamsini za kitanzania
  Mpaka sasa washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya Kumi bora wanaendelea na kujifua Kwaajili ya fainali ambayo imebaki wiki moja tu kwa fainali hiyo kuliteka jiji la Dar huku hofu na presha zikiwapata Washiriki hao.
  Fainali ya TMT itafanyika Siku ya Jumamosi ya tarehe 22 August 2015 katika ukumbi wa makumbusho ya taifa karibu na Chuo cha IFM kwa viingilio vya shilingi Elfu 50 kwa VIP na Elfu 30 kwa viti vya kawaida.
  TMT 2015 inapigwa tafu na Precious Air, Cam gas, ITV na Radio One, Global Publishers, I-View Studio, Paisha na Hussein Pamba Kali

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati kuu ya CCM kilchofanyika katika ukumbi wa White house, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo.
  Wajumbe wa Kamati kuu ya CCM.

  0 0


  Vijana wakitoka kukata nyasi kwa ajili ya mifugo huko Kaliua mkoani Tabora ikiwa ni sehemu ya biashara yao 

  Kijana Ephrahim Maksoni akipita  juu ya reli kwa  baiskeli maeneo ya Nguruka Mkoani Kigona
  Abiria wakiteremka toka ndani ya Basi la Saratola likitokea Nguruka kwenye kituo kipya cha mabasi kilichopo Masanga Gungu mkoani kigoma

   Wafanya biashara wa chumvi wakiwauzia abiria waliokuwa wakisafiri na basi lililokuwa likitoka Nguruka kuelekea Kigoma 
   Wakichota maji eneo  katika kituo cha mabasi mjini  Kaliua mkoani Tabora
  Wananchi wakikata  tiketi katika kituo kipya cha Stendi ya mabasi ya Mikoani kilichopo Masanga Gungu mkoani kigoma, ambapo kuingia huingia bure na kutoka huwalazimu kutoa sh. 200. Picha na Khamisi Mussa

  0 0  CUSTOMIZED DRESS from scrach….ikiwa imedhaminiwa  na ze stylist ROSE KOKUHILWA ‘FASHION JUNKII’
  Ni kwa neema tuuuuuu na rehemaaa, ni kwa neema tuu……ndo nyimbo ilikuwa inaunguruma kwa spikaaa na mabiharusi na mwenzie akawa wanaingia kwa kunesanesa. Kwa mapicha exclusive ya kumwaga toka 8020fashionblog.com

  0 0

  Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania Limited leo imemtangaza Mkurugenzi wake mpya Bw. Ian Ferrao anayechukua nafasi ya Mkurugenzi anayeondoka Rene Meza ambaye hivi karibinu aliteuliwa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Ooredoo Myanmar kuanzia mapema mwezi ujao. 
  Bw. Ferrao kwa sasa hivi ni Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Lesotho.Ana uzoefu mkubwa wa uongozi katika sekta ya mawasiliano katika nchi mbalimbali za Ulaya na Afrika.Kabla ya kjiunga na Vodacom Lesotho alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu anayesimamia biashara za kampuni ya Vodacom barani Afrika na alikuwa na hisa katika kampuni ya Africonnect ya nchini Zambia.
  Ujio wake kuongoza Vodacom Tanzania ni kama vile amerejea nyumbani kwa kuwa wazazi wake waliwahi kuishi nchini tangu mwaka 1952 kabla ya kuhamia nchini Uingereza mwaka 1970. 
  Akiongelea uteuzi wake alisema “mimi ni mzoefu na nina ujuzi wa kuongoza sekta ya mawasiliano na nina imani sekta hii ni zaidi ya mwasiliano bali imeonyesha mabadiliko makubwa katika kuchangia kuleta mabadiliko kwenye jamii kwa kuboresha maisha ya watu na kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri ya kuishi.
  Nina imano Vodacom ina uwezo wa kuendelea kuboresha mawasiliano nchini na kuzidi kufanya maisha ya watanzania kuwa murua” 
  Naye Rene Meza Mkurugenzi aliyeiongoza Vodacom Kuanzia mwaka 2011 alisema kuwa katika kipindi cha uongozi wake Vodacom Imefanya mabo mengi katika kuboresha sekta ya mawasiliano nchini ikiwemo kukua kwa mtandao huo na kuwa na wateja zaidi ya milioni 12 na kuanzishwa kwa huduma ya M-PESA ambayo inatumiwa na wananchi wengi Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zenye watumiaji wengi kwenye huduma hii kwenye makampuni ya Vodacom Group.
  Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akiongea na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wa hafla fupi ya kujitambulisha kwao iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akiongea na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wa hafla fupi ya kujitambulisha kwao iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam,Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo aliyemaliza muda wake, Rene Meza.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania aliyemaliza muda wake, Rene Meza(kulia)akimtambulisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kampuni hiyo, Ian Ferrao kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wa hafla fupi ya kumtambulisha kwao iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

  Vodacom Tanzania Announces 
  New Managing Director
   Vodacom Tanzania Limited today announced the appointment of  Ian Ferrao  as the new Managing Director of the company. He replaces Rene Meza who is moving on to assume the position of Chief Executive Officer of Ooredoo Myanmar on September 1, 2015.
  Ferrao is currently the Managing Director of Vodacom Lesotho.  He has over 10 years international experience in Europe and Africa and has held senior leadership positions in various technology  businesses.  Prior to Vodacom Lesotho, he was the Chief Commercial Officer for Vodacom Business Africa and before that he was the commercial director and a shareholder at AfriConnect Zambia. Ferrao’s move to Tanzania is a homecoming of sorts – his grandfather emigrated to Tanzania in 1952 and some of his family members were born in Dar es Salaam, before relocating to the UK in 1970. 
  The new Vodacom MD is in his own words, “ a passionate telecoms leader who enjoys creating positive change. I believe that our industry plays a transformational role in the communities in which we operate - we are not simply just about connecting people. Our products & services change lives, create brand new opportunities and make the world a better place. 
  I am a firm believer that technological innovation moves the world forward and Tanzania cannot be left behind. We are entering an era where being connected is now a necessity, and we as Vodacom Tanzania have a massive role to play in ensuring all Tanzanians can access the internet, enjoy digital content and create a brighter future for both themselves and the Country.”
  For his part, Meza joined joined Vodacom Tanzania in October 2011 as Managing Director. He introduced many firsts in the telecoms sector in Tanzania during his tenure. 
  Meza’s most notable achievements include the fact that under his leadership; the network doubled in size,  customer  numbers rose  to over 12 million and Tanzania went on to become the biggest M-PESA customer base in the Vodacom Group.


  0 0

  Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
   Mwanahabari Gordon Kalulunga akichangia mada
   Mwanahabari Michael Katona akiwasilisha kazi waliyopewa kwa niaba ya kundi lake
   Mafunzo kwa vitendo yakiendelea
  Waandishi wa habari wa kanda ya nyanda za juu Kusini wamepatiwa mafunzo ya nanma ya kuandika na kutangaza habari za uchaguzi ili waweze kutumia taaluma yao iifikie jamii

  Semina hiyo inaendeshwa kwa pamoja na shirika la utangazaji la Uingereza BBC na baraza la habari Tanzania MTC.(Picha na Edwin Moshi wa Eddy Blog)

  0 0


  0 0

  Airtel Tanzania imetanga washindi  wa droo yake ya nne ya promosheni  ya "Jiongeze na Mshiko" katika ofisi za makao makuu ya Airtel zilipo Morocco jijini Dar Es Salaam, ambapo wateja wanaweza kushinda zawadi ya fedha kila wiki ya shilingi tatu , milioni  moja na mwisho wa promosheni mteja ataweza kuondoka na kitita cha shilingi milioni 50.

  Akiongea wakati wa droo hiyo, Afisa uhusiano na matukio wa Airtel  Dangio Kaniki alisema leo tunatangaza washindi wawili wa  promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo watajishindia pesa taslim shilling milioni tatu na milioni moja kila mmoja. Ninayo furaha kutangaza washindi hao ambao  ni  Josephat Mahinda(25) Askari Magereza wa wa Mkoa wa Manyara yeye amejishindi shilingi milioni 3 , na  mshindi wa pili ni Daudi Ally Kingonji (31) mfanya biashara  na mkazi wa Kiwalani Dar Es Salaam yeye amejishindi shilingi milioni 1.”

  Kaniki aliongeza kwa kusema, mpaka sasa Airtel imeshakabidhi zawadi kwa washindi mbali mbali hapa nchini. Na leo hii tumewakabidhi washindi wa droo ya tatu  ambao ni Shangai Rodger (53) mkazi wa Tanga yeye amejishindi shilingi milioni 3 , na  mshindi wa pili ni Afrillious Kapinaa  (21) mwanafunzi na mkazi wa mkoa wa Dar Es Salaam yeye amejishindi shilingi milioni 1 waliopokea zawadi zao leo  hii asubuhi.

  Akiongea na waandishi wa habari Afrillious Kapinaa mwenye umri wa miaka 12, aliishukuru Airtel kwa kuanzisha promsheni hii. Ushindi wake ulikuja kama bahati na msaada mkubwa sana katika maisha yake ya uanafunzi. “Wazazi wangu wako Songea, ushindi huu wa milioni moja utanisaidia kutimiza mahitaji  yangu nikiwa hapa chuoni. Nawahimiza Wateja wengine wa Airtel kujiunga na prmosheni hii kwani ya ukweli kabisa”.

  "Tunawashukuru wateja wetu na watanzania wote walioshiriki mpaka sasa katika promosheni hii. "Tunaamini ushindi huu utawawezesha wateja wetu kupata fedha za kuendesha shughuli zao za kiuchumi na kuboresha maisha yao, hilo ndilo lenge letu kama Airtel.  Natoa wito kwa watanzania kujiunga na kushiriki bure kwa kutuma ujumbe wenye neno BURE kwenda namba 15470 na kupata nafasi ya kushindia kupitia droo zetu za kila wiki." alimalizia Kaniki.
  Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (katikati) akiwasiliana na mmoja wa washindi wakati wa kuchezesha droo ya nne ya promosheni ya Airtel "Jiongeze na Mshiko" iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo wateja wawili, Daudi Kingonji wa Dar na Josephat Mahinda wa Manyara waliibuka washindi. Kushoto ni Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Majjid Bakary na Afisa Huduma za Ziada wa Airtel, Fabian Felician.
  Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kulia) akikabidhi zawadi ya kitita cha shilingi milioni 1, kwa mshindi wa droo ya tatu ya promosheni ya Airtel "Jiongeze na Mshiko", Agricius Kapinda katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati) ni Afisa Huduma za Ziada wa Airtel, Fabian Felician.
  Meneja mauzo wa Airtel Tanga Aluta Kweka (kulia) akikabidhi zawadi ya kitita cha shilingi milioni 3, kwa mshindi wa droo ya tatu ya promosheni ya Airtel "Jiongeze na Mshiko" Shangai Rodger, katika hafla iliyofanyika jijini Tanga jana.

  0 0

  Na Lorietha Laurence-Maelezo

  Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini(RFB) imefanikiwa kufanya maboresho ya barabara kwa kiwango cha lami katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Serikali ya awamu ya nne wa Mhe. Jakaya Kikwete.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Jana Bw. Joseph Haule amesema kuwa matengenezo hayo yamefanikisha ujenzi wa barabara kuu zinazounganisha mikoa mbalimbali nchini kukamilika kwa asilimia 89 huku zile za Wilaya na Miji kwa asilimia 57.

  “ kazi kubwa ya Mfuko huu ni kukusanya mapato kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo tozo za barabarani na ushuru wa mafuta na baadaye kuzigawa kupitia taasisi zinazohusika na ujenzi wa barabara ikiwemo TANROADS, Wizara ya Ujenzi na Ofisi ya Waziri Mkuu “ alisema Bw. Haule

  Aidha aliongeza kuwa Mfuko huo umefanikisha ujenzi wa daraja la Mabatini jijini Mwanza ,daraja la Mwanhunzi na daraja la Mbutu linalounganisha Igunga na Shinyanga pamoja na ununuzi wa vivuko kikiwemo kile cha Mv Malagarasi.

  Mbali na hayo Bw.Haule aliongeza kuwa Bodi hiyo inaendelea kuhakikisha barabara zinatunzwa kwa kudhibiti magari ya mizigo yanayozidisha uzito unaochangia uharibifu wa barabara kwa kuanzisha mfumo wa kisasa wa kamera utakaokuwa unaratibiwa na mfuko huo.

  Mfuko huo umefanikiwa kuanzisha ujenzi wa barabara kwa kutumia mawe ambao ni wa gharama nafuu na wa kudumu kwa muda mrefu,hata hivyo miradi hiyo imeanza kutekeleza katika mikoa ya Kigoma na Mwanza.

  Kutokana na mtandao wa barabara kufanyiwa matengenezo ya mara kwa mara imesaidia kuongeza ubora wa barabara na kupanua wigo wa biashara kati ya Tanzania na nchi za jirani ikiwemo Zambia,Malawi,Burundi,Rwanda na Uganda.

  Mbali na mafanikio hayo Mfuko huounakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa bajeti kutokana na fedha zinazopatikana kutokukidhi mahitaji.

  0 0

  The Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) Director General Dr. Ally Yahaya Simba (right), e-Government Agency Chief Executive Officer (CEO) Dr. Jabiri Kuwe Bakari (centre) and of Dar Es Salaam Teknohama Business Incubator (DTBi)CEO, Eng. George Mulamula address a news conference during the 3rd Annual Cyber Defense East Africa Summit held in Dar Es salaam on 11-08-2015. Dr. Bakari opened the summit on-behalf of the Chief Secretary, Ambassador Ombeni Sefue.
  The Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) Director General Dr. Ally Yahaya Simba (left), addresses the 3rd Annual Cyber Defense East Africa Summit held in Dar Es Salaam on 11-08-2015. The event was opened by e-Government Agency Chief Executive Officer (CEO) Dr. Jabiri Kuwe Bakari (right) on-behalf of the Chief Secretary, Ambassador Ombeni Sefue. . (Photo by Courtesy TCRA)

  0 0

  Tanzania inaingia katika kipindi kigumu na cha muhimu sana kwenye historia yake. Ni kipindi ambacho kitasaidia kuamua muelekeo wa nchi kwa miaka mitano inayokuja. Mara nyingi ifikapo wakati wa uchaguzi kuna mambo mengi hubadilika. Biashara huanza kuwa ngumu kutokana na hofu miongoni mwa watu. Pia, ushiriki wa watu kwenye kampeni hufanya muda mwingi kutumika huko hivyo kutoa muda mchache kwenye shughuli kama kazi.
  Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, mwaka huu tutashuhudia mabadiliko makubwa sana, mabadiliko haya siyo tu aina ya watu wanaoshiriki kwenye kugombea nafasi mbalimbali, bali pia mfumo utakaotumika kwenye kampeni hadi upigaji kura. Mwaka huu tutashuhudia matumizi ya Tehama kwa kiwango kikubwa sana kwenye kampeni za uchaguzi na hata utangazaji na uchungaji wa matokeo ya chaguzi.Tutegemee kupata updates za matokeo ya kura toka kila kituo ndani ya dakika punde tuu wanapomaliza kuhesabu.

  Kwa chama chochote kinachotaka kufikia watu na hatimaye kushinda, ni ngumu kufanikisha hilo bila kutumia Tehama. kwa maneno mengine, Tehama ndiyo itakayoongoza uchaguzi wa mwaka huu. Tumeona mfano wa Obama mwaka 2008. Akiongozwa na kauli mbiu yake ya pamoja tunaweza (Yes we can) na matumizi ya mitandao, Obama aliweza kufikisha ujumbe kwa vijana wengi kama ilivyo sasa kwa Tanzania, na hatimaye kushinda uchaguzi wa kihistoria.


  0 0
 • 08/12/15--01:51: TANZIA
 • Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu anasikitika kutangaza kifo cha Bw. Boniphace Haule - Mhasibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Pichani) kilichotokea nchini India tarehe 10.08.2015.
  Mwili wa Marehemu utawasili leo, uwanja wa ndege wa J.K. Nyerere. Mazishi yatafanyika Ijumaa tarehe 14/08/2015. Msiba uko nyumbani kwa marehemu Tegeta Ununio, Mtaa wa Mwaitende.

  Maziko yanatarajia kufanyika katika makaburi ya KINONDONI.

  Taarifa na taratibu za msiba zitafuata.

  0 0

  The world is presently witnessing brutality & annihilation of one of the most charismatic mammals on earth, the African Elephant at a shocking rate in human history. Poaching, habitat loss and other cruelty are alarming. Tanzania being a treasure of elephants in Africa has recently revealed its catastrophe. 

  The recent elephant census conducted in the main elephant ecosystems for seven months consecutively from May to November 2014, indicates   a significant decline of current elephant population in Tanzania from 2009 to 2014 survey by 60%. At independence in 1961 there were 350,000 elephants and in 2009 were 110,000 and by 2014 the number dwindled to about 43,521.
        
  ‘The increase in elephant poaching is highly linked to an increase of ivory prices and illegal markets in the Far East and South East Asia’ Says Dr. Amani Ngusaru, WWF Tanzania Country Director on marking the World Elephant Day, 12th August 2015, in Dar es Salaam. Elephant poaching and trafficking of wildlife has increased dramatically in recent years, threatening the three pillars of life on earth: - sustainable development, peace and human rights.

  It is now more urgent and important to come up with interventions that address the root causes of elephant poaching through more and improved international cooperation in source, transit and consumer countries as well as to identify and address any gaps in the current anti-poaching strategies for better protection of wild elephants. 

  READ MORE HERE

  0 0


older | 1 | .... | 937 | 938 | (Page 939) | 940 | 941 | .... | 3348 | newer