Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 936 | 937 | (Page 938) | 939 | 940 | .... | 3353 | newer

  0 0

  Mtumishi wa Nssf Mbeya Niah Almasi   akiwa na nyuso ya furaha baada ya  ya kufunga pingu za maisha na Jackline Bukuku  ndoa iliyofungwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika msikiti wa Forest jijini Mbeya na maulid iliyofanyika nyumbani kwa Bw.Harusi Brock T jijini hapa .
  0 0

  image (3)
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akitia saini kwenye kitabu cha wageni kwenye banda la maonesho la NHC lilikuwapo katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi kulikokuwa kukifanyika maonesho hayo ya Nane Nane kitaifa.
  image (5)
  Wateja wakipata maelekezo kutoka kwa maafisa wa mauzo wa Shirika la Nymba la Taifa kwenye maonyesho ya Nane Nane Kitaifa Ngongo, Lindi.
  image (7)
  Wateja wakipata maelekezo kutoka kwa maafisa wa mauzo wa Shirika la Nymba la Taifa kwenye maonyesho ya Nane Nane Kitaifa Ngongo, Lindi.
  image (9)
  Wateja wakipata maelekezo kutoka kwa maafisa wa mauzo wa Shirika la Nymba la Taifa kwenye maonyesho ya Nane Nane Kitaifa Ngongo, Lindi.
  image (11)
  image (13)image
  0I7A0544
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akihutbia wakazi wa Lindi kwenye uwanja wa Nane Nane Ngongo ambapo alihitimisha kilele cha sikukuu ya wakulima Nane Nane. Maonesho ya nane nane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.
  0I7A0550
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akihutbia wakazi wa Lindi kwenye uwanja wa Nane Nane Ngongo ambapo alihitimisha kilele cha sikukuu ya wakulima Nane Nane. Maonesho ya nane nane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

  0 0

  Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa kituo cha Redio cha EFM,  Denis Ssebo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu  kuendelea kufanyika kwa Tamasha la Muziki Bar kwa Bar baada ya kumalizika kwa tamasha hilo kwa awamu ya kwanza. Kulia ni Mtangazaji, Dina Marios.
   Mtangazaji, Dina Marios akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu  kuendelea kufanyika kwa Tamasha la Muziki Bar kwa Bar baada ya kumalizika kwa tamasha hilo kwa awamu ya kwanza. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa kituo cha Redio cha EFM,  Denis Ssebo.
  Waandishi wa habari wakimsikiliza Meneja Mkuu wa Mawasiliano wa kituo cha Redio cha EFM,  Denis Ssebo katika mkutano uliofanyika makao makuu ya EFM-Mikocheni jijini Dar es Salaam.
  Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

  BAADA ya kumalizika kwa Tamasha la muziki mnene Bar kwa bar awamu ya kwanza, na mashabiki kuomba Burudani hiyo iendelea tena, Uongozi Efm umekubali ombi hilo na sasa Tamasha hilo linarudi tena kwa kishindo likiwa  limeboreshwa kwakuongeza wigo wa kuwafikia watu wengi zaidi.

  Muziki mnene bar kwa bar awamu hii bila kuwasahamu wasikilizaji na mashabiki wa EFM katika wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala kwa umuhimu wake na Wilaya mpya katika mkoa wa Dar es salaam, Muziki mnene sasa utapelekwa pia katika mkoa wa Pwani.

  Maeneo ambayo wanatakiwa kukaa tayari  kwa Muziki mnene bar kwa bar utakaoporomoshwa  na Madjs wakali wa Efm, ni pamoja na Kibaha, Mlandizi, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe,  Kigamboni na maeneo mengine mengi kwa ajili ya kuhakikisha tunakonga nyoyo za mashabiki wetu.

  Muziki Mnene bar kwa bar mwaka huu inatarajiwa kuanza rasmi tarehe 5/09/2015 . Lakini katika kuelekea huko efm imeanza na Muziki mnene bango katika sehemu yako ya biashara ambako bwana E anapita na ukiwa umeweka bango la EFM na unasikiliza matangazo yetu basi utapata kifurushi chenye zawadi kibao.

  Na kama ilivyokawaida yetu, mwishoni tutakuwa na Tamasha kubwa la hitimisho ambalo litafanyika jijini Dar es salaam ambalo safari hii limeboreshwa na kuongezwa vionjo vingi sana.


  “Ninawaomba wasikilizaji wetu wakae mkao wa kula maana tutawafikia na kuwamiminia Burudani ambayo pia itarushwa live kutoka eneo husika kupitia kituo chao cha 93.7 EFM. Njoo tuonane, tufahamiane na tuijenge Radio yetu efm ambayo kwetu Muziki unaongea”.

  LAKINI jambo la pili ambalo ndugu zangu wanahabari tungependa kuwajulisha ni kwamba katika kuhakikisha tunaendelea kukupa kilicho bora zaidi kupitia vipindi vyetu mbalimbali,sanjari na kuwa na watangazaji wenye ushawishi na uwezo mkubwa. leo hii tunamtambulisha kwenu mtangazaji Dina Marios ambaye wengi uwezo wake mnaujua na sasa ameungana na wenzake  wenye uwezo mkubwa katika familia ya Efm.

  Mwisho niwashukuru sana kwa mwitikio wetu na kwakuwa tumeendelea kushirikiana mara nyingi hivyo naomba tuendelee kushirikiana hivi hivi.  Asanteni sana kwakunisikiliza.


  0 0

   Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati kuu ya CCM vitakavyofanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu Dodoma.
  Alhaj Kimbisa amekanusha uvumi uliosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa ameihama CCM. Kushoto ni Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana   (picha na Freddy Maro)
   Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na KAtibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahmana Kinana baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma ambapo ataongoza vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati kuu ya CCM vitakavyofanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu Dodoma. Picha na Freddy Maro


  0 0

  Afisa uhusiano mwandamizi Bw. Fulgence Sebera akitoa maelezo ya shughuli za Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Majid Mwanga (wa tatu kulia) aliyeambatana na viongozi wengine wa TASO walipotembelea banda la SSRA katika sherehe za maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere mkoani Morogoro.
  Mch. Vernon Fernandes (aliyekaa) alipotembelea banda la SSRA katika maonesho ya Nanenane Morogoro, kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji Bi Sarah Kibonde Msika akifuatiwa na mwanasheria mwandamizi Bw. Omar Sururu Khalfan, kushoto ni Afisa matekelezo Bw. David Lyanga.
  Mkuu wa kitengo cha uhusiano na uhamasishaji Bi Sarah Kibonde Msika wa kwanza kushoto akitoa maelezo ya masuala ya Hifadhi ya Jamii kwa wadau waliotembelea banda la SSRA, akifuatiwa na afisa matekelezo Bw.David Lyanga na afisa uhusiano mwandamizi Bw. Fulgence Sebera katika maonesho ya Nanenane Morogoro.
  Maafisa wa Mamlaka wakikabidhi zawadi ya Mfuko wa SSRA kwa mdau aliyetembelea banda la Mamlaka katika maonesho ya Nanenane mkoani Morogoro.

  0 0

  Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF akipokea Kikombe cha Ushindi wa Kwanza kundi la Mifuko ya Jamii Toka kwa Rais Jakaya Kikwete,kushoto na Kulia kwa Rais wakishuhudia tukio hilo Ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mwantumu Mahiza na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika,Stephen Wassira katika Ufungaji wa Maonesho hayo katika Viwanja Vya Ngongo Lindi
  Meneja wa Mfuko wa NHIF Mkoa wa Lindi,Fortunata Kullaya(Alieshika kikombe)Kwa Pomoja na Mkurugenzi wa Masoko ,Rehani Athumani (kulia) na Grace Kisinga Afisa Uhusiano na mawasiliano Nhif wakishangilia Ushindi wa Kwanza Walioupata katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa katika Viwanja vya Ngongo,Manispaa ya Lindi.
  Waziri Mkuu wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania,Mizengo Pinda Akisiliza kwa Makini maelezo ya Huduma zinazotolewa na Mfuko wa Bima ya Afya Toka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Bima ya Afya Makao Makuu,Bw Rehani Athuman.Huku Mkuu wa mkoa wa Lindi na Mtwara wakifuatilia kwa karibu


  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima aliwaalika Mabalozi wa wa nchi mbali mbali kuja kutembelea Tanzania hivi karibuni.
  Mabalozi hao kutoka Kuala Lumpur Malaysia walitembelea mbuga za wanayama za Serengeti, Ngorongoro na walifanya ziara mjini Zanzibar.
  Mabalozi hao ni Waheshimiwa Viorica na Constantin Nistor (Romania), Stephen Mubiru (Uganda), Dkt. AzizPonary Mlima(Tanzania), Isabela Mhlanga( Afrika Kusini), na Bwana Rogatius Shao (Naibu Balozi-Tanzania).
  Mabalozi walipowasili Kibo Palace Hotel, Arusha na kupokelewa na Naibu Waziri wa Maliasili.na Utalii Mheshimiwa Mahmud Mgimwa, Bwana Alan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA na Bwana Pascal Shelutete Meneja wa Mawasiliano na Masoko wa TANAPA.
   
   Tembo mbugani Serengeti
   Simba wa Serengeti
   Kifaru katika mbuga ya Serengeti
   Mabalozi walipowasili kutokea Zanzibar
  Mabalozi hao walikutana na  Balozi Thami Mseleku ambaye ni Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania na Balozi Chabaka Kilumanga na Mkewe katika  Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kabla ya kuondoka na kurejea Kuala Lumpur.
  Sehemu ya mamilioni ya nyumbu na pundamilia Serengeti

  0 0

  Mwandishi wa makala haya Bw. Yusuph Kileo akitoa mada kwenye moja ya vikao vya usalama mitandao jijini Nairobi, Kenya, hivi karibuni
  Nimekamilisha vikao vya usalama mitandao vilivyofanyikia jijini Nairobi kufuatia mualiko maalum nilioupata. Katika vikao hivyo niliwasilisha mada mbili (ya kwanza ikiwa ni namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao na mada ya pili ikiwa ni namna ya uchunguzi wa makosa ya digitali kitaalam) katika mada hizo mbili ambazo zilipokelewa vizuri na kupelekea mijadala ya kipekee kuna mengi  nikajifunza kutoka kwa washiriki.

   Aidha, nilishiriki mijadala duara iliyojikita katika changamototo mbali mbali za uhalifu mitandao na kuiangazia sharia mtandao ya nchi ya Kenya.

  Kenya ni miongoni mwa nchi tatu barani afrika ambazo zimeorodheshwa kuwa na uhalifu mkubwa sana wa kimtandao nyingine ni Nigeria pamoja na Afrika ya kusini. 

  Tukijadili takwimu za kutisha duniani kote, tulishuka na kuangazia bara la Afrika na baadae Afrika mashariki na hatimae kujikita na takwimu za nchi ya Kenya.


  Kwa upande wa Kenya kwa mujibu wa takwimu zilizo wasilishwa katika mkutano, hadi kufikia Mwezi wa saba mwaka huu (2015) kuna simu 34.8 Milioni  huku watumiaji wakiwa ni 26.0 Milioni. Aidha, matumizi ya intaneti ni 29.1 milioni ambayo ni sawa na 65% “penetration”. Takwimu hizo zinasindikizwa na upotevu wa dola za kimarekani 20 milioni ($20 Mil) kila mwaka kutokana na uhalifu mtandao.


  0 0

  Mzee Paul Sozigwa (pichani), aliyewahi kuwa Mwandishi wa Habari  wa Rais katika serikali ya Awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Nyerere, amepotea tangu jana mchana katika mazingira ya kitatanishi. 


  Kwa mujibu wa taarifa ya familia yake ambayo Globu ya Jamii imeletewa, mara ya mwisho Mzee Sozigwa alionekana kanisani Mbezi Beach BCIC (kwa Gamanywa) jana Jumapili saa nane mchana. Kupotea huku kunaleta mashaka hasa kwa kuwa Mzee Sozigwa ni mgonjwa wa Alzheimer, na mara nyingi anapoteza kumbukumbu. Taarifa ya kupotea kwake imeshatolewa polisi na kufunguliwa RB.

  Taarifa hiyo imesema mara ya mwisho Mzee Sozigwa alikuwa amevaa shati jeupe lenye mistari ya bluu na kijivujivu, suruali nyeusi na viatu vyeusi. Anapoulizwa anakaa wapi hujibu Kisarawe ama Vidunda, wilaya ya Kisarawe. Atakayemuona anaombwa kupiga simu zifuatazo:

  Mch. Moses Sozigwa  
  0712 3798180755 716158

  Mrs. Irene Yussuf       
  0784 300418

  Ms. Lucy Paul Sozigwa 
  0755 5640800717 310783

  Mrs. Judith Mlawa      
  0712 834737

  Unaweza pia kuwasiliana nao kwa Whatsapp na Viber
  0 0

  Image result for MNADA WA NYUMBA

                  Na Bashir Yakub
  Sheria  ya  ardhi  Sura  ya  113  imetoa  maelezo  kwa  upana  kuhusu  miamala    kati  ya  mtoa  mkopo , mkopaji na  dhamana  inayohusika katika mkopo  huo. Mara  kadhaa   watu binafsi,  taasisi  za  haki  za  binadamu, asasi  za kiraia, na  makundi  mengine  wamekuwa  wakitoa maelezo  mbalimbali   yanayotokana  na  sheria hii hasa  wakilenga  kupunguza vitendo  vya  ukiukaji  wa  taratibu  ambao  hufanywa  na  baadhi  yua  taasisi  za  mikopo   zikishirikiana  na  makampuni  ya  udalali  ( Brockers/auctioneers). 

  Katika kipindi  hiki  ambapo  taasisi  za  fedha  zinazojihusisha  na  mikopo  zimeongozeka watu  wengi  wamekuwa  wakilalamikia  mienendo  yake hasa  pale  mtu  anaposhindwa  kurejesha  kwa  wakati. Pia wamekuwa  wakilalamikia  namna  taasisi  hizi  zinavyowakokotolea  mahesabu  hasa  yale  ya  riba. Jingine  ni  taratibu  zinazotumika  katika  kuuza/ kunadisha   dhamana  ya  mtu   hasa    nyumba  iwapo  mlengwa  ameshindwa kurejesha.

  0 0

  Habari na picha na Editha Karlo, 
  wa Globu ya Jamii Kigoma


  MTU mmoja ambaye ni raia kutoka nchi ya Burundi amefariki usiku wa kuamkia jana  katika hospitali ya Kigoma  kwa ugonjwa usiojulikana. 
  Mgonjwa huyo amezikwa jana  jioni  kwa tahadhari zote zihusuzo magonjwa hatari ya kuambukiza.
  Nguo, vitanda, mashuka na vitu vyake vyote alivyokuwa akitumia wakati wa uhai wake vimechomwa moto mara tu baada ya mwili wake kuzikwa eneo la Masanga nje kidogo ya mji wa Kigoma.
  (Picha zinaonesha hatua mbalimbali toka mwili wa marehemu ulipoondolewa na wataalamu waliovaa mavazi maalumu hadi mazikoni).

  Akiongea na mtandao huu daktari wa wakimbizi  kutoka shirika la kusafirisha wakimbizi  kwenda nje ya nchi  (IOM) Dkt.  Beda amesema kuwa marehemu ameishi  katika kambi ya wakimbizi ya Nyalugusu Wilayani Kasulu kwa muda wa miaka mitatu  yeye pamoja na familia yake.


  Dkt Beda amesema kuwa marehemu Buchumi Joely  (39) alifika Kigoma mwezi uliopita akiwa yeye pamoja familia yake kwa ajili ya kusafirishwa na shirika la IOM kwenda marekani.

  DK Beda alisema kuwa marehemu alianza  kuugua tarehe 31 ya mwezi uliopita kwa kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili wake kama mdomoni, kwenye fizi na machoni.
  "Ilipofika tarehe juzi Agosti  8 hali yake ilizidi kuwa mbaya ndipo uongozi ulipoamua kumpeleka katika hospital ya mkoa maweni kwaajili ya matibabu zaidi" alisema Dkt Beda.

  Naye Kaimu mganga mkuu wa hospital ya nkoa wa kigoma Dkt Shija Ganai amethibitishia mtandao huu kuwa walimpokea mgonjwa huyo na kumlaza katika wodi namba 8 ya Grade One.

  Alisema kuwa usiku wa kuamkia leo hali ya mgonjwa ilizidi kuwa mbaya na damu zilizidi kuongezeka, na walipompima maralia  alikuwa na joto la kawaida la nyuzijoto 36.


  Dkt. Ganai ameeleza kuwa  ilipofika alfajiri ya kuamkia leo mgonjwa huyo alifariki dunia. Amesema  kwamba mpaka sasa  bado haijadhibitishwa kama mgonjwa huyo amekufa kwa ugonjwa wa  ebola japo alikuwa na dalili zote za ugonjwa huo.


  "Tumeshatuma sampo ya damu  maabara kuu ya Taifa kwa ajili vipimo ili tujue ni ugonjwa gani uliomuuwa"alisema Dkt huyo.

  Aliongezea kuwa hivi sasa madaktari, manesi pamoja na ndugu wote waliokuwa wanamuhudumia mgonjwa hivi sasa wapo chini ya uangalizi maalumu wa madaktari kwa muda wa siku 21.


  0 0

    Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wanachama na wafuasi wa CCM mkoa wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kumpokea,Dkt Magufuli aliwashukuru wanachama hao kwa kujitokeza kwa wingi na walimuahakikishia ushindi wa kishindo na wa mapema katika uchaguzi mkuu utakaofanyika hapo baadae mwaka huu,pia amewata kuwa na umoja wa kushirikiana na kuweka kando tofauti zao kuhakikisha wanailetea CCM ushindi wa kishindo.
   Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Husnain Murji akiwahutubia wana CCM nje ya ofisi ya CCM Mtwara na kuwaambia kuwa ushindi kwa CCM utakuwa wa kishindo .
   Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani akihutubia wakazi wa Mtwara  ambapo alihakikisha kuwa Mtwara itaongoza katika kumpigia kura nyingi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli.
   Wananchana na Wafuasi wa chama cha Mapinduzi (CCM),wakimshangilia  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli  alipokuwa akiwashukuru kwa kumpa udhamni na kujitokeza kwa wingi kumpokea,lakini pia alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwao na kuwaomba wajenge mshikamano na kuweka tofauti zao kando ili kukihakikishia ushindi chama cha CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika hapo baadae mwaka huu.

   Mgombea mteule wa Urais kwa chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara,Ndugu Shaibu Akwilombe mara baada ya kuwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Mtwara kuwashukuru Wanachama na wafuasi wa chama hicho kwa kujitokeza kwa wingi,na pia alitia saini vitabu vya wageni vya ofisi hiyo,kati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Mohamed Sinani pamoja na Naibu Waziri wa Fedha,ambaye pia aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Mwigulu Nchemba.
   Baadhi ya Wanachama na wafuasi wa chama cha CCM wakiwa wamekusanyika nje ya ofisi ya za mkoa huo mjini Mtwara,kabla ya kumsikiliza mgombea Urais wa chama hicho Dkt John Pombe Magufuli,ambaye alifika ofisini hapo kusaini vitabu na pia kuwashukuru wanachama hao kumdhamini na kujitokeza kwa wingi kumpokea

  0 0

  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kuongezeka kidogo kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Mei 2015 leo jijini Dar es salaam.Mfumuko wa Bei wa bei kwa mwezi Julai ,2015 umefikia asilimia 6.4 kutoka asilimia 6.1 iliyokuwepo Juni 2015.

  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai 2015 na kusema kuwa umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.4  kutoka asilimia 6.1 iliyokuwepo mwezi Juni 2015.

  Hii inamaanisha kuwa  kasi ya upandaji wa bei ya  bidhaa na huduma kwa mwezi Julai 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji bei ya bidhaa na huduma  iliyokuwepo mwezi Juni mwaka 2015.  

  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam amesema kuongezeka huko kumesababishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali nchini.

  Amezitaja bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko huo kutokana na upandaji wa bei katika masoko kwa mwezi Julai 2015 kuwa  ni mchele kwa asilimia 27.9,mahindi asilimia 2.3, unga wa muhogo asilimia 9.2, nyama asilimia 4.5, samaki 12.2, na maharage asilimia 5.9.

  Kuhusu Fahirisi za Bei ambacho ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya binafsi hapa Tanzania, Kwesigabo  amesema zimeongezeka hadi kufikia 158.78  kutoka 158:12 za mwezi Juni.

  Amesema kuongezeka kwa fahirisi za bei kumechangiwa na ongezeko la bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula zikiwemo gesi ya kupikia kwa asilimia 3.7, mafuta ya dizeli 5.9, mafuta ya Petroli ailimia 4.9,  unga wa mahindi asilimia 2.5, ulezi asilimia 2.9, samaki asilimia 4.8, viazi vitamu asilimia 2.6 na ndizi za kupika asilimia 3.4.

  Kwesigabo amesema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Julai , 2015 umefikia shilingi 62 na senti 98 ikilinganishwa na kiasi cha shilingi 63 na senti 24  za mwezi Juni 2015. 

  “Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi Julai ,2015 na  umepungua  hii ina maana kuwa sasa mtu anahitaji kuongeza ziada ya shilingi 38 ili aweze kununua bidhaa na huduma sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua katika mwezi Juni"

  Kwa upande wa mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwezi Julai, 2015 Bw.Kwesigabo amesema kuwa una mwelekeo unaofanana , Kenya umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 6.62 na kutoka 7.03 mwezi Juni 2015 huku Uganda ikiwa na mfumuko wa Bei wa  asilimia 5.4  kutoka asilimia 4.9  za mwezi Juni, 2015.

  0 0

  Wapendwa wasomaji wa Modewjiblog tunashughulikia matatizo ya kifundi yaliyojitokeza tangu jana kwenye ‘server’ kiutaalam inaitwa DDOS unaweza kuperuzi link hii  kwa taarifa zaidi https://en.wikipedia.org/wiki/Denial-of-service_attack ambayo yako nje ya uwezo wetu.

  Modewjiblog itarudi hewani hivi punde, samahani kwa usumbufu wowote ule uliojitokeza, tunahitaji ushirikiano wenu zaidi.
  ----------------------------------
  There has been an undergoing DDOS attach on the server https://en.wikipedia.org/wiki/Denial-of-service_attack.

   We have taken measures to lighten the effects of this as much as we can. Unfortunately it is something that we don't have much control over, but we will do all in our power to get the blog back to full functionality.

  Imetolewa na Operation Manager 
  wa Modewjiblog, Zainul Mzige. 


  0 0  0 0

  R&R Insurance Brokers Limited (R&R) in partnership with Jubilee Insurance companies in Tanzania announced the first-ever Investment Plan cover that combines both Life Insurance and Repatriation (Funeral) cover for Tanzanians living in the diaspora.
  The product named Nyumbani Kwetu, Swahili for My Home has been designed to deliver three components; investment, life and repatriation cover.  Nyumbani Kwetu allows access to ones’ funds after the second year, it has a guaranteed life cover, guaranteed funeral cover and a return rate of 4 %.The cover is affordable and accessible with premiums as low as Tsh17,200/-  per year.  The product is available to all Tanzanians living outside the country with a minimum age of 18 years. Unlike other insurance products, Nyumbani Kwetu has no maximum age of entry.
  R&R prides itself on crafting unique insurance solutions. R&R Insurance Brokers Managing Director, Ms. Diana Matondane, said that the firm is thrilled to partner with the number one Insurance Company in East Africa. “This presents us with an opportunity to showcase our products to Tanzanians all over the world. Jubilee’s passion and dedication to underwrite risks and paying claims is well known as the market leaders in Tanzania, It’s an honour to work with them,” said Ms. Matondane.

   “We are delighted to partner with R&R and we look forward to introducing various products to the Tanzanian market, and beyond catering for long term life Assurance packages such as school fees and personal investment policies,” said Jubilee Insurance CEO George Alande. Alande further highlighted that Jubilee also offers short term insurance packages such as domestic package insurances for residential houses and their contents, motor vehicle covers specifically for ladies and individual medical insurance covers among others. “There is a synergy between our two brands that we feel will result in a profitable relationship for both of us,” said Alande.
  R&R provides a full- brokerage service covering General, Life and Health insurance in a wide range of sectors including aviation, marine, mining, oil, gas and energy, credit and political (investment) risks, surety bonds, terrorism and sabotage as well as micro insurance. 

  0 0

  Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akitoa mada katika  Kongamano la Vijana. Wakati wa kongamano hilo Balozi Mushy amewashauri vijana kufanya kazi na Taasisi za Umoja wa Mataifa ili kujipatia uzoefu wa kujielezea ikiwa ni pamoja na kujiamini. Kongamano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam
  Mwakilishi Mkazi wa UNFPA Tanzania Dkt. Natalia Kanem (Wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Vijana Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi (wa kwanza kulia) wakimsikiliza Balozi Mushy (Hayupo pichani) wakati akiwasilisha Mada.
  Juu na Chini ni picha ya Vijana waliohudhuria Kongamano hilo wakimsikiliza Balozi Mushy (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada.
  Balozi Mushy akimwelezea jambo Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi katika Kongamano la Vijana
  Balozi Mushy (Katikati mwenye suti nyeusi) alipokuwa akiwasilisha mada ambapo pia alitaka kujua ni vijana wangapi wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba 2015, huku ikionekana idadi kubwa ya vijana waliohudhuria Kongamano hilo wamejiandikisha.
                                             Picha na Reginald Philip 

  0 0

   Baada ya washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula  Shindano linalo endeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow na kudhaminiwa na Gates and Melinda Foundation,TBS, Cooperative Bank Great Britain na Care Tanzania, baada ya  kuwasili wote sasa wanapangwa makundi makundi kwa ajili ya kuanza mchakato wa siku
   Hapa katika kundi la kwanza washiriki wa Shindano la  Mama Shujaa wa Chakula , Shindano linaloendeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow hapa wakiwahamasisha wanakijiji cha kisanga kilimo cha Biashara na kubadilishana mawazo kuhusu nyenzo , mazao na tathimini ya mapato na matumizi.
   Kundi la pili wakiendelea kutoa Elimu ya Kilimo kwa Wanakijiji. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Libarata Mulamula akizungumza mbele ya Mabalozi na Wageni waalikwa wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga rasmi Balozi wa Finland aliyemaliza muda wa kazi nchini, Mhe. Sinikka Antila. Katika hotuba yake Balozi Mulamula alimshukuru Balozi Antila kwa mchango wake wa  kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Finland. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
  Balozi Mulamula akiendelea kuzungumza.
  Balozi Antila (Wa kwanza Kulia), Balozi wa Demokrasia ya Kongo nchini Balozi Juma Mpango (Wa pili Kutoka kulia), Balozi wa Uingereza Mhe. Dianna Melrose (Wa tatu kutoka kulia), Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Segore Kayihura (Wa tatu kutoka kushoto), Balozi wa Ujerumani nchini Mhe. Egon Kochanke (Wa pili kutoka kulia) na Balozi wa Canada nchini Mhe. Alexandre Leveque wakimsikiliza Balozi Mulamula hayupo pichani 
  Sehemu ya Wageni walioudhuria hafla hiyo wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani).

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Ephraimu Kwesigabo akitoa taarifa ya kuongezeka kidogo kwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi Mei 2015 leo jijini Dar es salaam.Mfumuko wa Bei wa  bei kwa mwezi Julai ,2015 umefikia asilimia  6.4   kutoka asilimia 6.1 iliyokuwepo Juni 2015.


  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
  OFISI  ya Taifa ya Takwimu imetangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwezi Julai 2015 na kusema kuwa umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.4  kutoka asilimia 6.1 iliyokuwepo mwezi Juni 2015.

  Hii inamaanisha kuwa  kasi ya upandaji wa bei ya  bidhaa na huduma kwa mwezi Julai 2015 imeongezeka ikilinganishwa na kasi ya upandaji bei ya bidhaa na huduma  iliyokuwepo mwezi Juni mwaka 2015.  

  Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam amesema kuongezeka huko kumesababishwa na kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali nchini.

  Amezitaja bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko huo kutokana na upandaji wa bei katika masoko kwa mwezi Julai 2015 kuwa  ni mchele kwa asilimia 27.9,mahindi asilimia 2.3, unga wa muhogo asilimia 9.2, nyama asilimia 4.5, samaki 12.2, na maharage asilimia 5.9.

  Kuhusu Fahirisi za Bei ambacho ni kipimo kinachotumika kupima mabadiliko ya bei ya bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya binafsi hapa Tanzania, Kwesigabo  amesema zimeongezeka hadi kufikia 158.78  kutoka 158:12 za mwezi Juni.

  Amesema kuongezeka kwa fahirisi za bei kumechangiwa na ongezeko la bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula zikiwemo gesi ya kupikia kwa asilimia 3.7, mafuta ya dizeli 5.9, mafuta ya Petroli ailimia 4.9,  unga wa mahindi asilimia 2.5, ulezi asilimia 2.9, samaki asilimia 4.8, viazi vitamu asilimia 2.6 na ndizi za kupika asilimia 3.4.

  Kwesigabo amesema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za mlaji kwa mwezi Julai , 2015 umefikia shilingi 62 na senti 98 ikilinganishwa na kiasi cha shilingi 63 na senti 24  za mwezi Juni 2015. 

  “Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma zilezile kwa mlaji kwa mwezi Julai ,2015 na  umepungua  hii ina maana kuwa sasa mtu anahitaji kuongeza ziada ya shilingi 38 ili aweze kununua bidhaa na huduma sawa na zile alizokuwa na uwezo wa kuzinunua katika mwezi Juni"

  Kwa upande wa mfumuko wa Bei kwa nchi za Afrika Mashariki kwa mwezi Julai, 2015 Bw.Kwesigabo amesema kuwa una mwelekeo unaofanana , Kenya umepungua kidogo hadi kufikia asilimia 6.62 na kutoka 7.03 mwezi Juni 2015 huku Uganda ikiwa na mfumuko wa Bei wa  asilimia 5.4  kutoka asilimia 4.9  za mwezi Juni, 2015.


older | 1 | .... | 936 | 937 | (Page 938) | 939 | 940 | .... | 3353 | newer