Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 938 | 939 | (Page 940) | 941 | 942 | .... | 3353 | newer

  0 0

   Meneja bidhaa wa Benki ya Barclays,Valence Lutegavya akizungumza wakati wa uzinduzi wa kadi ya ATM ya dola za kimarekani katika mkutano wa uzinduzi uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Bwana Kumaran Pather.
     Meneja bidhaa wa Benki ya Barclays,Valence Lutegavya akionyesha kadi ya ATM ya Dola za Kimarekani katikati ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays Tanzania, Bwana Kumaran Pather na wamwisho ni
  Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Vimal Kumar.
   Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Bwana Kumaran Pather, akitoa msisitizo juu ya faida za ATM kadi ya dola za kimarekani kwa wateja watakao zitumia kazi hizo wakati wa manunuzi ya bidhaa mbalimbali haoa nchini na kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Vimal Kumar.
  Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Vimal Kumar akifafanua juu ya matumizi ya ATM kadi za dola za kimarekani katika matumizi ya kawaida katika kununua bidhaa mbalimbali kwenye maduka yanayotumia kadi za ATM hapa nchini, katika mkutano wa uzinduzi kadi ya ATM ya dola, uliofanyika makao makuu ya benki jijini Dar es Salaam leo.
   
  BENKI ya Barclays hapa nchini imezindua kadi ya ATM ya dola hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Barclays Tanzania, Bwana Kumaran Pather wakati akizungumza wakati wa uzinduzi, uliofanyika makao makuu ya benki jijini Dar es Salaam leo.

    alisema “wateja wa Barclays wenye akaunti ya Dola za kimarekani wataweza kutumia kadi hizo mpya wakiwa ndani na nje ya Tanzania kupitia huduma za VISA.”

  Kadi hizi mpya zimewekwa kwenye mfumo mpya wa teknohama ambao unawapa wateja usalama zaidi wanapofanya huduma zote za kibenki. Mteja atapata fedha za ndani atakapoitumia kadi hiyo akiwa nchini. Miamala yote ya nje ya nchi itafanyika kwa dola za Kimarekani tu.

  Pia amezitaja faida za Kadi za dola kutoka Benki ya Barclays hapa nchini,  Inarahisisha malipo ya bidhaa na huduma madukani, hotelini, vituo vya mafuta n.k. nchini na dunia nzima,Utakupo toa hela nje ya nchi kupitia ATM utapata noti za dola za kimarekani,
  Inakupa amani ya akili baada ya kukamilisha muamala kwa mtandao na pia inakupa nafasi ya kupata punguzo la bei mtandaoni unapotumia kadi ya matumizi ya Barclays.

  Aliendelea kusema “Barclays inawasaidia wateja kunufaika kwa kulenga kuwapatia uzoefu rahisi na kuwasikiliza mahitaji yao.” Barclays inazingatia kila wakati kuwapa wateja wake huduma timilifu za hali ya juu na kwa uzoefu wa hali ya juu.

  0 0  0 0

   Mkurungenzi Mtendaji wa kituo cha msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) Theosia Nshala akuzungumza kwenye mdahalo na wanawake wenye ulemavu (TAMAWA) juu ya taratibu mbarimbari za Uchanguzi hususani hari za mwanamke katika Uchanguzi hapa nchini katika mdahalo uliofanyika  Jijini Dar es Salaam.
   Mwanaharakati na Mtaaramu wa Jinsia na Haki za Binadam Gema Akilimali, akuzungumza kwenye mdahalo na wanawake wenye ulemavu(TAMAWA) juu Kuwajengea wanawake ufahamu na ujasiri wa kushiriki katika Uchanguzi kama wagombea,wapiga kura wafutiliaji na waangalizi katika mdahalo uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
  Sehemu ya   wanawake wenye ulemavu (TAMAWA) wakiwa katika mkutano leo Jijini Dar es Salaam.
   Picha na Emmanuel Massaka.

  0 0

   Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.

  Kabla  hatujaangalia  namna  suala la upigaji  punyeto linavyo  maliza  nguvu  za  kiume, ni  vyema  tukafahamu  kwanza  kuhusu  SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
  Kufahamu   kuhusu   SAYANSI  YA  MFUMO  WA  NGUVU  ZA  KIUME  tafadhali  tembelea :


  MAWASILIANO :  WASILIANA  NASI   KWA  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84.
  Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kwenye  blogu  yetu :


  0 0

   Bendi ya jeshi la polisi ikiongoza Maandamano ya siku ya vijana Duniani ,yaliyofanyika Agost 12 kila mwaka yaliyoanzia katika Shule ya Sekondari Jangwani na kuishia katika  viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
   Naibu Katibu  Mkuu wa Wizara ya habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo,Profesa Gabriel Ole Sante akizungumza  katika maadhimisho ya Siku ya Viajna Duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja,jijini Dar es Salaam.
   Vijana wakionyesha ujuzi wao katika mchezo wa sarakasi katika siku vijana duniani yaliyofanyika katika viwanja vya manzai mmoja leo jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Profesa Gabriel Ole Sante akipata maelekezo kutoka Afisa Maendeleo wa Vijana wa Wizara hiyo,Dora Meena katika maadhimisho ya Siku vijana Duniani yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo,Profesa Gabriel Ole Sante akipata maelezo katika banda la Asasi ya Vijana wa Umoja wa Matiafa (YUNA), katika maadhimisho ya Siku Vijana Duniani yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Vijana walioshiriki Maadhimisho ya Siku Vijana Duniani yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  (Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii)

  0 0

  Na Mwandishi wetu-MAELEZO-Dar es salaam

  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Pichani) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michezo ya Wizara, Idara zinazojitegemea ,Wakala wa Serikali  na Ofisi za wakuu wa Mikoa (SHIMIWI) itakayoanza Jumamosi ijayo(15.8.2015) mjini Morogoro.

  Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Katibu Mkuu SHIMIWI Moshi Makuka, mashindano ya mwaka huu yatafanyika kwa wiki mbili.

  Amesema kuwa siku ya ufunguzi kutakuwa na michezo ya mpira wa miguu kati ya Elimu na Hazina kwa wanaume , mpira wa pete utazikutanisha timu ya Afya na Mambo ya Ndani.

  Makuka ameongeza kuwa siku hiyo pia kutakuwepo mchezo wa kuvuta kamba kati ya Wakala wa Jiolojia Tanzania na Mambo ya Nje  kwa wanaume na kamba kwa wananwake kati ya Ikulu na Bunge.

  Amezitaja timu zilizothibitisha kushiriki kuwa ni Ikulu, Utumishi, Waziri Mkuu, Afya, Ardhi, Elimu, Hazina, Kilimo,TAMISEMI, Mifugo, Maji, Afika mashariki, Maliasili, Mambo ya Nje, Mambo ya Ndani, Ulinzi, Nishati, Maendeleo ya Jamii, Viwanda, Uchukuzi, Ujenzi na Tume ya Mipango.

  Timu nyingine ni Mahakama, Tume ya Utumishi wa Umma, Bunge, Tume ya Kurekebisha Sheria, Tume ya Mahakama, Ukaguzi, tume ya ushirika , Wakala wa Jiolojia Tanzania, Wakala wa Ukaguzi wa Madini, Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula, Mkoa wa Lindi, Katavi, Mwanza, Kagera, Rukwa, Dar es salaam, Mtwara, Iringa, Geita, Kigoma, Manyara , Arusha, Mara, na Tanga

  0 0


  Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (katikati), akihutubia wakati akizindua kampeni ya kupambana na ujangili viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam leo asubuhi. Kampeni hiyo imeanzishwa na watu wa China kwa ajili ya kuunga jitihada za watanzania katika mapambano hayo ya kuwalinda wanyama dhidi ya ujangili hasa tembo.
  Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (kulia), akimpa zawadi ya mpira kwa niaba ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kinondoni, Faudhia Eddy katika uzinduzi huo. Balozi huyo alitoa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za Manispaa ya Kinondoni.
  Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (kulia), akimpa zawadi ya mpira, Mwalimu Flora Lukali kutoka Shule ya Mount Pleasant kwa ajili ya shule hiyo.
  Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing akionyesha umahiri wa kuchezea mpira katika uzinduzi huo kabla ya kutoa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za Manispaa ya Kinondoni.
  Wanafunzi wakiwa na vipeperushi vya bendera ya nchi ya china wakati wa uzinduzi huo.
  Wasanii wa kundi la makhirikhiri wakitoa burudani katika 
  uzinduzi huo.
  Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
  Wimbo wa taifa ukiimbwa.
  Wanahabari wakichukua taarifa za uzinduzi huo.
  Wanafunzi ndani ya uzinduzi huo. 

  0 0
 • 08/12/15--06:00: DRIVE YOUR DREAMS


 • 0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi ya Ushindi wa Tatu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe ambaye alipokea kwa niaba ya Ofisi ya Uhamiaji walioibuka washindi wa tatu katika Maonesho hayo ya Kilimo Nane nane yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi,
   Wafanyakazi wa Idara ya Uhamiaji wakiwa katika Picha ya Pamoja wakishangilia Ushindi walioshinda katika Maonesho ya Kilimo ya Nane nane yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Lindi na Kufungwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete.
   Afisa Uhamiaji Mkoa waLindi Abdallah Towo akiwa na Martin Mhagama,Mkaguzi wa Uhamiaji Lindi wakiwa wameshikilia kikombe cha Ushindi wa Tatu walichokabidhiwa na Rais Kikwete katika Maonesho ya Nane nane
  Mratibu wa Uhamiaji kutoka Makao makuu Bi. Tatu Burhani (mwenye Hijabu) akiwa sambamba na Sofia Maunda ambaye ni Konstebo wa Uhamiaji Lindi (mwenye Kofia) wakiwa katika Banda lao la Maonyesho katika sherehe za Nane nane Mkoani Lindi.

  0 0

  Waziri wa Afrika Mashariki Dk. Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa amgeni rasmi katika semina kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  akifungua rasmi semina hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akitoa hotuba yake wakati wa semina kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini.

  Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Beki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei kutoa hotuba yake wakati wa semina kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  iliyoandaliwa na benki hiyo na kufanyika jijini Mbeya.
  Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Beki ya CRDB, Tully Mwambapa akiwaongoza wageni waalikwa kuimba wimbo maalumu wa Benki hiyo.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  CRDB Dk. Charles Kimei akifurahia jambo na Waziri wa Afrika Mashariki Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) wakati wa semina ya Benki ya CRDB kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  iliyofanyika jijini Mbeya. Kushoto ni Mkuu Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Nyirembe Munasa.
   Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika semina ya Benki ya CRDB kwa viongozi wa Halmashauri za Kanda za Nyanda za Juu Kusini  iliyofanyika jijini Mbeya. 

  PICHA ZAIDI INGIA HAPA

  0 0

  unnamed (100)
  Meneja Mfuko wa Barabara Bw.Joseph Haule akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni alipokuwa akiwasilisha ripoti ya mafanikio ya utekelezaji wa Mfuko wa Barabara kwa  Serikali ya awamu ya nne.
  unnamed101
  Naibu Meneja Masuala ya Kiufundi Bw. Ronald Lwakatare kutoka Taasisi ya Mfuko wa Barabara akizungumza na waandishi  wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
  ……………………………
  Na Lorietha Laurence-Maelezo
  Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini(RFB) imefanikiwa kufanya maboresha ya barabara kwa kiwango cha lami katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Serikali ya awamu ya nne wa Mhe. Jakaya Kikwete.

  Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam Jana Bw.  Joseph Haule amesema kuwa matengenezo hayo yamefanikisha ujenzi wa  barabara kuu  zinazounganisha mikoa mbalimbali nchini kukamilika kwa asilimia 89 huku zile za Wilaya na Miji kwa asilimia 57.  

  “ kazi kubwa ya Mfuko huu ni kukusanya mapato kupitia vyanzo mbalimbali   ikiwemo tozo za barabarani na  ushuru wa mafuta na baadaye  kuzigawa kupitia taasisi zinazohusika na ujenzi wa barabara ikiwemo TANROADS, Wizara ya Ujenzi na Ofisi ya Waziri Mkuu “ alisema  Bw. Haule

  Aidha aliongeza kuwa  Mfuko huo umefanikisha ujenzi wa daraja  la Mabatini jijini Mwanza ,daraja la Mwanhunzi  na daraja la Mbutu  linalounganisha Igunga na Shinyanga   pamoja na ununuzi wa vivuko  kikiwemo kile cha Mv Malagarasi.Mbali na hayo Bw.Haule aliongeza kuwa Bodi hiyo inaendelea kuhakikisha barabara  zinatunzwa  kwa  kudhibiti magari ya mizigo yanayozidisha uzito unaochangia uharibifu wa barabara  kwa kuanzisha mfumo wa kisasa wa kamera  utakaokuwa unaratibiwa na mfuko huo.

  Mfuko huo  umefanikiwa  kuanzisha ujenzi wa barabara kwa kutumia mawe ambao ni wa gharama nafuu na wa kudumu kwa muda mrefu,hata hivyo miradi hiyo imeanza kutekeleza katika mikoa ya Kigoma na Mwanza.

  Kutokana na mtandao wa barabara  kufanyiwa matengenezo ya mara kwa mara imesaidia kuongeza ubora wa barabara na kupanua wigo wa biashara kati ya Tanzania na nchi za jirani ikiwemo Zambia,Malawi,Burundi,Rwanda na Uganda.  Mbali na mafanikio hayo Mfuko huounakabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa bajeti kutokana na fedha zinazopatikana kutokukidhi  mahitaji.

  0 0

   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (wa pili kushoto) akitembelea soko la wamachinga la Rehema Nchimbi Complex Mjini Dodoma wakati wa ziara yake ya ukaguzi sokoni hapo mapema leo, Wengine ni viongozi wa soko hilo.
   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akikagua eneo la vyoo vya soko la wamachinga la Rehema Nchimbi Complex Mjini Dodoma wakati alipotembelea soko hilo mapema leo.

   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa (katikati) akibadilishana mawazo juu ya changamoto za biashara na wamachinga wa soko la Rehema           Nchimbi Complex wakati wa ziara yake ya ukaguzi sokoni hapo mapema leo, wengine ni viongozi wa Wilaya ya Dodoma na viongozi wa soko hilo.

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akiwa kwenye Picha ya pamoja na wafanyabiashara wa soko la machinga la Rehema  Nchimbi Complex baada ya kumalizika kwa ziara yake ya ukaguzi sokoni hapo mapema leo, wengine ni viongozi wa Wilaya ya Dodoma.


  0 0


  0 0

   Rais wa shirikisho la mpira wa  miguu Tanzania(TFF) Jamali Malinzi(kushoto)na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo Kelvin Twissa(kulia)wakielekezwa na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu jinsi ya kusaini mkataba wa makubaliano ya udhamini wa ligi Kuu ya  Vodacom Tanzania  bara kwa msimu wa 2015/16.

   Rais wa shirikisho la mpira wa  miguu Tanzania(TFF) Jamali Malinzi(kushoto)pamoja na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo Kelvin Twissa(katikati)wakisaini mkataba mpya wa miaka(3) kwa Vodacom Tanzania kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa ligi Kuu ya  Vodacom Tanzania  bara 2015/16. Anayeshuhudia kulia ni Ofisa Mkuu mtendaji wa ligi Boniface Wambura
   Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na mkataba mpya wa miaka(3) wa udhamini wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliosainiwa baina ya shirikisho la mpira wa  miguu Tanzania(TFF)na kampuni hiyo,kushoto ni Rais wa shirikisho la mpira wa  miguu Tanzania(TFF) Jamali Malinzi pamoja na Ofisa Mkuu mtendaji wa ligi Boniface Wambura(
    Rais wa shirikisho la mpira wa  miguu Tanzania(TFF) Jamali Malinzi(kulia)akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba mpya wa miaka(3) wa kudhamini ligi Kuu ya  Vodacom Tanzania  bara kwa msimu wa 2015/16.Katikati ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo Kelvin Twissa na kushoto ni Ofisa Mkuu mtendaji wa ligi Boniface Wambura.

  Rais wa shirikisho la mpira wa  miguu Tanzania(TFF) Jamali Malinzi(kushoto) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(kulia)wakibadilishana nyaraka za mkataba wa makubaliano ya kampuni hiyo kuendelea kuwa mdhamini mkuu wa ligi kuu  ya  Vodacom Tanzania  bara 2015/16 kwa miaka(3) anayeshuhudia katikati ni Ofisa Mkuu mtendaji wa ligi Boniface Wambura.


  0 0


  Kwa mara ya kwanza katika historia
  inakuletea Khanga Party siku ya Jumamosi Aug 29, 2015 ndani ya kiota THE VAULT AT PALACE

  ANUANI
  1104 BROAD ST
  DURHAM NC 27705

  Khanga Party ndani ya Durham North Carolina
  Kiingilio ni $ 20
  Couple $15
  Ladies with Khanga outfit $10 B4 11pm
  Music By Dj Luke

  KaRiBuNi

  0 0


  Wadau wa Diaspora mnakaribishwa ku record kijiwe cha Ughaibuni siku ya jumapili tarehe 23 kuanzanzia saa 10 jioni. nyumbani kwa Dr Temba maudhui ya Kijiwe hicho ni kuzungumzia mchakato mzima wa siasa ya nchi yetu ya Tanzania kuelekea kwenye uchaguzi Oct 25. 

  Mtu yeyote anakaribishwa kuja kuchangia hoja ya mtazamo na uelewa wake juu ya yote yanayoendelea Tanzania kwa sasa kuelekea kwenye uchaguzi. Piga simu hii #347 -475 -4313 kupata usaili wa jinsi ya kuhudhuria kijiwe hicho. Watu 10 wanaotakiwa watano kila upande ilikutengeneza hoja.
  Licha ya kijiwe kutakuwa na nyama choma kutoka kwenye jiko la kisasa kabisa kama bite wakati kijiwe kinaendelea.
  Tembelea web hii kuona picha zenye ubora za matukio yote ya kwenye community za Watanzanai.

  0 0

  Tukielekea kukamilisha maandalizi ya kongamano la Diaspora litakalofanyika kesho tarehe 13 hadi 15 Agosti, 2015 napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru kwa kukubali mwaliko wetu wa kushiriki kongamano hilo na pia kuwakumbusha yafuatayo:

  1. Kujiandaa kikamilifu kwa kupitia "brief concept Note" ya Kongamano hilo ambayo nimeambatanisha;
  2. kupitia ratiba ya masuala yatakayojiri katika kongamano hilo ambayo pia nimeambatanisha; na 
  3. kuhakikisha kuwa mmejiandikisha kushiriki kongamano hilo kupitia tovuti za www.tzdiaspora.com na www.tzdiaspora.org.

  Endapo mtakwama ama kukumbana na changamoto yeyote musisite kuwasiliana na waandaaji kupitia kwenye email ya Idara: diaspora@nje.go.tz ama ubalozi@tanzaniaembassy-us.org
  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akifungua warsha ya uelimishaji juu ya usimamizi uendelezaji wa mji wa Dodoma kwa viongozi wa kata na mitaa wa Manispaa ya Dodoma iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Morena Mjini Dodoma.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA Ndg. Paskasi Muragili akitoa maelezo ya ufafanuzi juu ya warsha ya uelimishaji juu ya usimamizi uendelezaji wa mji wa Dodoma kwa viongozi wa kata na mitaa wa Manispaa ya Dodoma iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Morena Mjini Dodoma.
  Baadhi ya viongozi wa kata na mitaa wa Manispaa ya Dodoma wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa warsha ya uelimishaji juu ya usimamizi uendelezaji wa mji wa Dodoma kwa viongozi hao wa serikali za mitaa iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Morena Mjini Dodoma.
  Picha ya pamoja baina ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Serikali na Viongozi wa Kata na Mitaa ya Manispaa ya Dodoma muda mfupi baada ya ufunguzi wa warsha ya uelimishaji juu ya usimamizi uendelezaji wa mji wa Dodoma iliyofanyika leo kwenye hoteli ya Morena.

  0 0  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Makamu Mwenyekiti Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein,Makamu Mwenyekiti Bara Ndugu Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakipiga makofi pamoja na wajumbe wengine muda mfupi baada ya kuingia katika ukumbi wa White House Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma tayari kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM leo jioni.
  Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai Nahodha wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Halmashauri kuu ya CCM mjini Dodoma leo.
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dkt.John Pombe Magufuli wakiteta muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Halmashauri kuu ya CCM mjini Dodoma leo.(picha na Freddy Maro).

older | 1 | .... | 938 | 939 | (Page 940) | 941 | 942 | .... | 3353 | newer