Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 935 | 936 | (Page 937) | 938 | 939 | .... | 3353 | newer

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kusini Mashariki, Bw. Joseph Kibehele kikombe cha ushindi baada ya VETA kuibuka Mshindi wa Kwanza katika eneo la Taasisi za Mafunzo na Utafiti kwenye Kilele cha Maonesho ya Kilimo (Nanenane) kitaifa,  iliyofanyika viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi, tarehe 8 Agosti, 2015.
   Wafanyakazi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wakiwa katika picha ya pamoja kufurahia ushindi baada ya VETA kuwa Mshindi wa Kwanza kwenye eneo la Taasisi za Mafunzo na Utafiti katika kilele cha Maonesho ya Kilimo (Nanenane) Kitaifa, kwenye viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi. Aliyeshika kikombe ni Mwenyekiti wa Bodi ya VETA Kanda ya Kusini Mashariki, Br. Sixtus Luoga.
   Wafanyakazi wa VETA wakishangilia kikombe cha ushindi baada ya VETA kutunukiwa Ushindi wa Kwanza kwenye eneo la Taasisi za Mafunzo na Utafiti katika kilele cha Maonesho ya Kilimo (Nanenane) Kitaifa, kwenye viwanja vya Ngongo, mkoani Lindi.

  0 0

  Na Mubelwa  Bandio
  MAISHA. Nimejifunza kuwa hayako sawa, na naamini huo ndio usawa wake, kwani humu tuishimo hakuko sawa.

  Hivyo, haitakuwa sawa kwa maisha kuwa sawa katika "uwanja" usio sawa kwa waishimo.
  Na...
  Najua nililoanza nalo na nitakaloendeleza halitaeleweka sawa, na huo ni udhihirisho wa usawa wetu, ambao nao hauko sawa.

  Leo, Agosti 10,  ninapoadhimisha mwaka mwingine katika maisha yangu, naitumia siku hii KUAKISI maisha yangu kuliko kusherehekea.
  UKWELI ni huu.....

  Unasoma hapa kwa kuwa "umekua" na kufikia umri wa kusoma na kuelewa. Huu ni umri wa kusherehekea ama kuadhimisha siku kadhaa za kuzaliwa kwako.

  Na, kama unasoma hapa, jambo moja ninaloweza kukuhakikishia ni kuwa UTAKUFA.

  Kwa hiyo, kama wanadamu, haya mawili yanakuwa ya lazima. Ukizaliwa, utakufa, tofauti ya maisha yetu ipo katikati ya haya mawili.

  Kama nilivyowahi kuandika, kuwa UTAKUMBUKWA KWA DESHI YA MAISHA YAKO (rejea hapa).

  Maishani, nimehudhuria KUMBUKUMBU ZA KUZALIWA WATU MBALIMBALI  na MISIBA mingi tu, na kote nimejifunza mengi kuhusu maisha yetu ya sasa, tuyatakayo na namna tunavyojitahidi kuifikia tamatuti yetu.

  Labda funzo kuu nililowahi kushiriki nanyi ni lile nililoliandika hapa Agosti 22, 2011 baada ya kuhudhuria msiba wa Dada yetu hapa Washington DC.
  Maisha yetu ya sasa yanaonekana kuwa ya mchakamchaka, twayakimbiza matumaini na (katika hali ya kushangaza) hata siku zaonekana kuwa fupi kuliko awali. 

  Kabla hujajipanga, ni kesho, ni juma lijalo, ni mwezi ujao na mwaka bila kukamilisha mengi uliyoamini ungependa kuyakamilisha katika muda uliojipangia.

  Ninapoangalia miaka hii niliyoishi, naiona kuwa mingi sana, si kwa kuwa nimeishi mingi kuzidi wote, bali kwa kuzingatia ni mara ngapi nimekuwa nikiamini nimefika mwisho wa uhai.

  Nakumbuka kusoma makala ya Kaka Eric Shigongo, iliyosema kuuona mwaka mpya ni nafasi ya ziada, na naamini katika hilo.

  Mara kadhaa (na ni zaidi ya moja) nimekuwa kwenye nafasi ya kuona kama kesho ilikuwa mbali na isiyofikika kwangu nikiwa hai, siku ambayo hunijia akilini zaidi juu ya hilo, ni  hii..

  Lakini leo wasoma niandikalo.
  NI NAFASI YA ZIADA katika kuikimbiza "siku ya mwisho"
  Nikirejea kwenye kichwa cha bandiko hili,fikra kwamba maisha yetu ya sasa ni kama kuikimbiza kesho kuliko kuifikiria leo na hata jana, kunatufanya tuonekane kuyawaza yajayo kuliko tulikotoka.

  Ni hili linalonifanya niamini kuwa, maisha yetu ya sasa yamewekeza katika yajayo na kama nilivyoeleza kabla, jambo pekee ambalo sote tuna hakika nalo, ni kifo.

  Na ndio maana nikasema, maisha ya sasa,ni kukimbiza DEATHDAY kuliko kuikimbia BIRTHDAY.

  Nisijesahau kujitakia EARTHday njema.
  Najua fika kuwa hongera na shukrani za maisha yangu nazipokea kwa sababu ni Mungu aliyeniweka hai mpaka sasa. 

  Na ndiye aliyenipa WAZAZI wangu ambao sina ninanloweza kueleza kuhusu nafasi yao maishani ikalingana na walilotenda.

  Labda jambo moja tu, kwamba walinibariki na NDUGU ambao uwepo wao umekuwa kama egemeo la kukua kwangu. Hawa ndugu wameniwezesha kuambatana na JAMAA ambao kwa muongozo wa ndugu, wameniwezesha kuwa nilivyo. 

  Si unakumbuka kuwa Twachagua maongezi, maongezi yachagua mawazo na mawazo yatuchagulia jamii? (Isome hapa)
  Nina maRAFIKI ambao wananisaidia katika kukua kwangu. Hawa nawajumusha na wale wanajiona kama maadui kwangu, ambao mara nyingi wamenifanya kujitahidi kukamilisha mambo ili wasipate la kusema.

  Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa
  Kipekee, namshukuru mke wangu mpenzi Esther na wanangu Paulina na Annalisa kwa kuwa wavumilivu kwenye harakati zangu (nyingine hazielewekagi yaani)

  Hahahaaaaaaaaaaaaaa
  Ni siku nyingine ya kukumbuka kuzaliwa kwangu. Nalikaribia hitimisho la maisha, na nikilijongelea, najitahidi kukamilisha dhumuni yangu ya kuwa humu duniani.

  Mungu akubariki na kuonyeshe namna muafaka ya kutenda kila lililo jema, kadhi uikaribiavyo.

  0 0

  Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi taifa ,Hemed Msabaha akizungumza wakati wa mikutano wa kutamburisha wagombea wa nafasi ya udiwani inayofanyika katika jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro.
  Baadhi ya viongozi wa NCCR-Mageuzi jimbo la Vunjo wa kiwa katika moja ya mikutano hiyo kata ya Makuyuni.
  Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi taifa na Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia ,Bw Hamis Athuman akitoa salamu za mwenyekiti huyo wakati wa mkutano wa utamburisho wa wagombea wa nafasi za udiwani kupitia chama hicho.
   
  0 0

  IMG-20150721-WA0084

  0 0

  BONDIA wa Kike Lulu Kayage mwishoni mwa wiki iliyopita alibuka kidedea nchini Afrika ya kusini baada ya kumdunda vibaya   Lizbeth Sivhaga wa nchini humu huu ni mpambano wake wa kwanza Lulu kucheza nje ya nchi na kufanikiwa kushinda kwa T.K.O ya raundi ya pili mchezo uho ulioanza kwa kasi ya mashambulizi ya uku na kule kila mmoja kutaka kumpiga mwenzie raundi za awaliata hivyo ilivyofika raundi ya pili bondia Lulu Kayage alimwelemea sana mpinzani wake kwa makonde mfululizo na wasaidizi wake kumuokoa kwa kumtupia taulo hivyo kusababisha Lulu kushinda T.K.O ya raundi ya pili.

  ushindi wa Lulu Kayage ulichagizwa na kocha maarufunchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambapo siki mbili kabla ya kuondoka nchini alimzawadia vifaa mbalimbali vya mchezo wa masumbwi na kumwaidi ushindi kwa asilimia zote.

  bondia huyo anatarajia kurudi nchini agost 11 kwa ajili ya maandalizi ya mapambano yake mengine ya kimataifa wakati uho uho bondia Ramadhani Shauri amepoteza mpambano wake kwa kupigwa K.O ya raundi ya nne na bondia mzoefu Philip Ndlovu wa Afrika ya Kusini ambapo mpambano uho wa raundi nane ulijikuta ukisha katika raundi ya nne.
  Bondia Lulu Kkayage akiwashukuru mashabiki walio udhulia kwa kuwapigia magoti na kuwapungia mikono baada ya kumchakaza bondia Lizbeth Sivhaga wa Afrika ya Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita Picha na SUPER D BOXING NEWS           

  Refarii akiwa katikati uku akiwashika mikono mabondia Llulu Kayage na Lizbeth Sivhaga wa Afrika kusini kwa ajili ya kutangaza mshindi Lulu alishinda kwa TKO ya raundi ya pili kushoto ni Yassini Abdallah
  Picha na SUPER D BOXING NEWS.

  0 0

   Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Mhe. Hawa Ghasia (MB) (kulia), akiweka sahihi alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania katika Wiki ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane) eneo la Ngongo, Mkoani Lindi.
   Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Mhe. Hawa Ghasia (MB) (kulia), akipokea zawadi kutoka Meneja wa Mawasiliano TPDC, Bi. Marie Msellemu (kushoto) alipotembelea banda la Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) katika Wiki ya Maonesho ya Wakulima (Nanenane).
   Mhandisi wa Petroli, Yusufu Risasi, (kulia) akitoa maelezo ya kitalaam kwa watu waliotembelea banda la Shirika la Maendeleo Petroli Tanzania kujionea shughuli zinazo fanywa na Shirika la TPDC

    Afisa Masoko wa TPDC, Elias Mziray (kulia), akitoa maelezo ya shughuli za Shirika kwa Wananchi waliotembelea banda la Shirika katika Wiki ya Maonesho ya Wakulima.

  0 0

  1
  Richard Rugimbana Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi waliosoma katika shule ya (St Joseph Cathedral High School Alumn )kuanzia mwaka 1940 - 2014 akizungumza katika mkutano wao uliofanyika shuleni hapo jana wakati wa kikao chao kikilchojadili mipango mbalimbali ikiwamo kuanzisha mfuko wa Elimu utakaosaidia kuwasomesha wanafunzi wa shule hiyo wenye mahitaji maalum ikiwemo kuwapatia Scholaship katika vyuo mbalimbali.
  Chama hicho kinatarajiwa kuzinduliwa rasmi Septemba 26 kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam , Katika kufanikisha uzinduzi huo kadi maalum zimeandaliwa ambazo zitauzwa shilingi 50.000 kwa mtu mmoja , 100.000 kwa watu wawili na meza za watu kumi kila moja zitakazouzwa kwa kiasi cha shilingi 1.000.000. Katika Picha kushoto ni Katibu wa Chama hicho Bwa.Collins Rutenge.
  2
  Richard Rugimbana Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi waliosoma katika shule ya (St Joseph Cathedral High School Alumn )kuanzia mwaka 1940 - 2014 akisisitiza jambo katika mkutano huo uliofanyika jana.
  3
  Mariam Ziaror mmoja wa wanachama hao akizungumza jambo wakati wa mkutano huo uliofanyika jana (St Joseph Cathedral High School .
  4
  Chief Edward Makwaia akichangia jambo katika mkutano huo
  5
  Bw. Hassan Ndumbaro mmoja wa wanachama hao akizungumza jambo katika mkutano huo kutoka kushoto ni Leaticia Mukarasa, Mariam Zialr na Chief Edward Makwaia.
  6
  Dr. Zubeida Tumbo kutoka taasisi ya Room To Read Tanzania ambaye pia alisoma katika shule hiyo akichangia mawazo yake wakati wa mkutano huo.
  7
  Baadhi ya wanachama wakiwa katika mkutano huo
  9
  Mkutano ukiendelea.
  10
  Mkuu wa shule ya (St Joseph Cathedral High School )Sr. Theodeta Faustin akizungumza na wanachama hao wakati wa mkutano huo.

  0 0

   Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akikata utepe kuashiria kumkabidhi kijana Jonathan Tarimo (wa pili kulia), msaada wa Zizi jipya na Ng’ombe wawili wa maziwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence Tarimo na Mratibu wa Masoko wa Airtel wilaya ya Monduli, Polas Emmanuel.
  1) Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akifafanua jambo kwa kijana Jonathan Tarimo (wa pili kulia), kabla ya kumkabidhi msaada wa Zizi jipya na Ng’ombe wawili wa maziwa, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. Wanaoshuhudia ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence Tarimo (kushoto) na maafisa wa Airtel wa Mikoa ya Arusha na Manyara.
   Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akimpongeza Jonathan Tarimo (wa pili kulia), baada ya kumkabidhi msaada wa Zizi jipya na Ng’ombe wawili wa maziwa kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence Tarimo, Mratibu wa Masoko wa Airtel wilaya ya Monduli, Polas Emmanuel na Meneja wa Airtel mkoa wa Manyara, Peter Kimaro.
  Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa tatu kushoto), akikabidhi Ng’ombe wa maziwa kwa kijana Jonathan Tarimo, ikiwa ni sehemu ya msaada wa Ng’ombe wawili wa maziwa na zizi jipya, alivyomkabidhi kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Baba mzazi wa kijana huyo, Clemence Tarimo na Mratibu wa Masoko wa Airtel wilaya ya Monduli, Polas Emmanuel.
  Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kushoto), akikabidhi Ng’ombe wa maziwa kwa kijana Jonathan Tarimo, ikiwa ni sehemu ya msaada wa Ng’ombe wawili wa maziwa na zizi jipya, alivyomkabidhi kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’ wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana.

  AIRTEL Tanzania kwa kupitia mpango wake wa Airtel
  Fursa “Tunakuwezesha” imemkabidhi kijana Jonathan Clement mkazi    Migungani kata ya Mto wa Mbu wilaya ya Monduli mkoani Arusha ng’ombe wawili, banda la kisasa pamoja na mafunzo ya biashara   ambayo itamsaidia kuinua biashara yake ya ufugaji na kumuongezea kipato chake.
  Jonathan kijana mwenye umri wa miaka 21 na elimu ya kidato cha nne  amekabidhiwa mtaji huo ambapo awali alikuwa na ngomb’e wawili na banda  lililochoka  na  alikuwa na changamoto ya elimu ya ufugaji na madawa ya mifugo.
  Jonathan ameishukuru kampuni ya simu za mikononi ya Airtel kwa kumpatia msaada huo amesema  “biashara yangu ya ufugaji sasa itapiga hatua. Naamini miaka michache ijayo nitakuwa na mifugo mingi sana na soko langu la maziwa litakuwa kwa kasi. Na vile vile itaniwezesha kuinua familia na biashara yangu kwa ujumla”.

  “Hii ni bahati ya peke kwangu kutoka Airtel, kwani ni vijana wengi sana wanatamani kupata hivi nilivyovipata lakini hawakupata bahati hii. Nawahimiza vijana wengine wasikate tamaa na  wajitokeze kwa wingi kwani Airtel Fursa ipo kutuwezesha vijana”.

  Akizungumza baada ya makabidhiano, Meneja huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, alisema “mpango huu ulibuniwa ili kuwawezesha vijana na kuwakwamua kiuchumi. Jonathan amepitia changamoto nyingi kufikia hapa alipo alianza na ngombe wa kukopeshwa kutoka kwa mjomba wake kwa makubaliano kwamba atakapopata ndama wa kwanza atakuwa wa kwake. Lakini leo hii tumemuwezesha kuwa na jumla ya ng’ombe watatu kwenye zizi lake”.
  “Airtel kupitia mradi wake wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” imempatia msaada huu Jonathan baada yakuridhishwa na hatua ya ufugaji pamoja na kuonyesha nia yakuwa mfugaji bora hapa nchini” alisema.

  Bayumi aliwataka vijana wachangamkie fursa hiyo na kuongeza kuwa mpango huu unawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ambao watapokea misaada ya vifaa au thamani ili kuweza kutimiza malengo yao..
  “Program hii inahusisha vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini alisema.
  Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma
  ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:-
  Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao
  kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com<mailto:airtelfursa@tz.airtel.com>. ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara. Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com

  0 0

  OFISI ya Makamu wa Rais inasikitika kuwepo kwa taarifa ambazo zimesambaaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo vya habari kuhusu msimamo wake ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi.
    Tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais hajapanga tukio lo lote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.
  Tunatumia nafasi hii kuwataka wale wote wenye tabia ya kuvumisha taarifa zisizo sahihi waache kufanya hivyo kwa kuwa ni kosa kisheria. Tunawaomba waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi na kutafuta taarifa sahihi kwenye vyombo vinavyotambulika.
  Boniphace Makene
  Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais.

  0 0

  Wananchi wakimsindikiza Waziri mkuu msaafu Edwald Lowassa (CHADEMA) wakati akielekea kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Demokrasioa na Maendeleo (CHADEMA) wakitokea ofisi za chama hicho kupitia ofisi za CUF na kuhitimisha katika ofisi za NEC jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  PRESS RELEASE” TAREHE 10.08.2015.

  ·         MTU MMOJA AUAWA KWA KUKATWA PANGA SHINGONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA WILAYANI KYELA.

  ·         MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KUTOKANA NA TUHUMA ZA WIZI.


  ·         MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBOZI.

  ·         JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATATU KWA MAKOSA MBALIMBALI.
   
  KATIKA TUKIO LA KWANZA:
  MTU MMOJA MKAZI WA NSANSA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA DAVID MWAKIPESILE (60) ALIUAWA KWA KUKATWA PANGA KICHWANI NA SHINGONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. 

  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 09.08.2015 MAJIRA YA SAA 21:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA NSANSA, KATA YA NGONGA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA.

  INADAIWA KUWA MHANGA ALIVAMIWA NA WATU HAO WAKATI ANARUDI NYUMBANI AKITOKEA KWENYE MATEMBEZI KISHA KUMJERUHI. MAREHEMU ALIFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA KWA MATIBABU.  

  CHANZO CHA MAUAJI HAYO INASADIKIWA KUWA NI IMANI ZA KISHIRIKINA. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA AJILI YA MAZISHI. UPELELEZI UNAENDELEA PAMOJA NA MSAKO WA KUWATAFUTA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILO.

  KATIKA TUKIO LA PILI:
  MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA, JINSI YA KIUME, MIAKA KATI YA 20-27, ALIUAWA KWA KUPIGWA NA KUNDI LA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BAADA YA KUKAMATWA AKIWA AMEIBA PILIPIKI MC 811 AFJ AINA YA T-BETTER MALI YA THOBIUS ALLANUS YENYE THAMANI YA TSHS 1,800,000/=.

  TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 09.08.2015 MAJIRA YA SAA 19:45 USIKU HUKO ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.

   MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. UPELELEZI UNAENDELEA.

  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA. 

  AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO LA KWANZA KUZITOA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.


  KATIKA TUKIO LA TATU:
  MPANDA BAISKELI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MICHAEL KIBONA (55) MKAZI WA MLOWO ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LISILOFAHAMIKA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.

  AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 09.08.2015 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA ENEO LA MLOWO, KATA YA MLOWO, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUMTAFUTA DEREVA ALIYEHUSIKA KATIKA TUKIO HILI.

  TAARIFA ZA MISAKO:
  WATU WATATU WAKAZI WA KIJIJI CHA MASIANO WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. SHAMLA MAHUNDOLA (20) 2. YUNGE LUHUNZA (25) NA WANGU D/O MKUWA (21) WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI UZITO WA KILO 09.
  WATUHUMIWA WALIKAMATWA KATIKA MSAKO MKALI ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 09.08.2015 MAJIRA YA SAA 08:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MASIANO, KATA YA CHOKAA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

  Imesainiwa na:
  [AHMED Z.MSANGI – SACP]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

  0 0

   Kwaya Maalum ya Jangwani kutoka Shinyanga ikitumbuiza wakati wa Sherehe za Makambi ya Mtaa wa Kanisa la Waadventista Wasabato Manzes.
   Muhubiri Mkuu wa Sherehe za Makambi mtaa wa Manzese Mch. Idelphonce Tirumanywa akihutubia watu waliohudhuria sherehe hizo. Ujumbe Mkuu "Mtizame Yesu Ukaishi".
    Kikosi maalum cha vijana wadogo wa Kanisa la Waadventista Wasabato Manzese (Wavumbuzi) wakitembea kwa mwendo wa gwaride kuelekea jukwaani kwa ajili ya program maalum kwenye sherehe za makambi.
   Baaadhi ya washiriki wa sherehe za makambi wakisikiliza kwa makini vipindi vinavyoendelea kwenye Makambi ya Mtaa wa Manzese.
   Mch. Idelphonce Tirumanywa akinyoosha mkono juu kuomba  wakati wa kufanya huduma maalum ya ubatizo kwa watu walioamua kujiunga na kanisa la waadventista wasabato ulimwenguni.


   Picha zote na Sarah Reuben.
   
  SHEREHE za Makambi kwa mwaka 2015 katika Mtaa wa Manzese zimemalizika kwa kishindo cha kubatiza waumini ishirini na saba (27) ambao wameamua kumpokea Yesu kwa kujiunga na kanisa la Waadventista Wasabato Manzese.

  Akizungumza na waumini wa kanisa hilo wakati wa kuhitimisha sherehe hizo mwishoni mwa wiki, Mchungaji Idelphonce Tirumanywa amesisitiza kuwa kanisa kuendelea kuwalea vyema waumini wapya waliojiunga na kanisa hilo. Mch. Tirumanywa pia ameendelea kuwaasa waumini wote wa kanisa la waadventista wasabato kuwa mfano bora kwa jamii kwa kuonesha matendo mema yatakayo warudisha watoto wa Mungu waliopotea nyumbani.

  “Ni wakati wakurudi nyumbani, dunia ipo kwenye hatari kubwa, tena kubwa sana. Tunapoishukuru serikali yetu kwa uhuru wa kuabudu, waadventista wasabato wote amkeni muumtangaze Mungu ili watoto wa Mungu waache dhambi na kurudi nyumbani”, alisistiza Mch. Tirumanywa.

  Sherehe za makambi ya mtaa wa Manzese yalihudumiwa na kwaya maalum kutoka Sauti ya Jangwani Shinyanga wakishirikiana na kwaya tatu (3) zinazounda mtaa huo yaani Angaza, Mbiu na Sauti ya Nyikani zote kutoka Dar es Salaam.


  0 0

   UKOSEFU  ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani. 

   Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda  mrefu.

  Katika  makala  yetu  ya  leo, tutaangalia  namna   suala  la  upigaji  punyeto linavyo  athiri  nguvu  za  kiume.
  Kusoma zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Ziito Kabwe  akiwa na mume  wa Chiku Abwao na Chiku Abwao  na kada wa ACT wazalendo.
  Zitto kabwe  akiwa na wapambanaji
  Zitto kabwe  akiwahutubia  wananchi wa jimbo la Iringa mjini
  Chiku  Abwao  akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini
  Mgombe  udiwani wa kata ya Mvinjeni Abuu Majeck akimpongeza mgombea  ubunge jimbo la Iri nga mjini Chiku Abwa.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa  Vodacom Tanzania, Bi. Rosalynn Mworia  kwa niaba ya kampuni yake  kwa kuwa mdau mkubwa wa  kuhamasisha wananchi kuhusiana na suala la kuzuia ajali barabarani. Makabidhiano hayo yalifanyika katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama  iliyomalizika hivi karibuni mjini Tanga.

  0 0

   Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu, akiwa ameongozana na mkuu wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Col mstaafu Issa Njiku,  kutoka kulia ni kamanda wa Polisi mkoa wa Rukwa, SACP Jacob Mwaruanda na kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi SACP Dhahir Kidavashari, akiwa mkoani humo, jana katika ziara ya kikazi
   Mkuu wa Jeshi la Polisi  (IGP) Ernest Mangu, (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa katavi,(hawapo pichani) kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa katavi, Dkt Ibrahimu Msengi, na kamanda wa Polisi mkoani humo, kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi (SACP) Dhahir Kidavashari, akiwa mkoani humo katika ziara ya kikazi. 
  Mkuu wa Jeshi la Polisi  (IGP) Ernest Mangu, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Katavi, jana akiwa mkoani humo katika ziara ya kikazi. Picha na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi

  0 0

  TWIGA STARS YAENDELEA KUJIFUA ZANZIBAR
  Kikosi cha timu ya Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa Amani na uwanja wa Mafunzo vilivyopo kisiwani Zanzibar. 
  Twiga Stars iko kambini kisiwani Zanzibar kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofanyika nchini Congo- Brazzavile kuanzia Septemba 04 – 19 mwaka huu. 
  Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage ameendelea kukinoa kikosi chake cha wachezaji 25 waliopo kambini kisiwani Zanzibar kujiandaa na michuano hiyo ya Afrika. 
  Twiga Stars itakua kambini kisiwani Zanzibar kwa kipindi cha mwezi mmoja, kujiandaa na fainali hizo za michezo ya afrika, ambapo imepangwa kundi A pamoja na wenyeji Congo – Brazzavile, Ivory Coast na Nigeria.

   KIHANGA MWENYEKITI FA MOROGORO
  Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Morogoro (MRFA) jana kilifanya uchaguzi wa viongozi wake katika nafasi ya mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu, mweka hazina, mjumbe wa mkutano mkuu pamoja na wajumbe wa Kamati ya Utendaji. 
  Katika uchaguzi huo Paschal Kihanga aliibuka na ushindi katika nafasi ya mwenyekiti, huku Gracian Max Makota  akishinda nafasi ya makamu mwneyekiti, nafasi ya katibu mkuu imechukuliwa na Charles Mwakambaya na katibu msaidizi Jimmy Lengme. 
  Nafasi ya Mweka Hazina imechukuliwa na Peter Mshigati, Mjumbe wa mkutano mkuu ni Hassan Mamba na mwakilishi wa vilabu ni Ramadhani Wagala, Kamati ya utendaji wamechaguliwa Mrisho Javu, Rajabu Kiwanga na Boniface Kiwale. 
  TFF inawapongeza viongozi wapya waliochaguliwa kuongoza chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kazi za kila siku za maendeleo ya mpira wa miguu nchini.

  TFF YATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI MALAWI
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salam za rambi rambi kwa Rais wa Chama cha Soka nchini Malawi (FAM), Walter Nyamilandu kufutia kifo cha aliyekua Rais wa chama hicho John Zingale. 
  John Zangale alifariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi wiki iliyopita katika hospitali ya  Mlambe iliyopo Blantyre nchini Malawi na kuzikwa mwishoni mwa wiki alikuwa Rais wa FAM mwaka 1998- 2002. 
  Katika salam zake kwenda kwa Rais wa FAM, Malinzi amewapa pole familia ya marehemu pamoja na chama cha soka nchini Malawi kwa msiba huo, na kusema TFF kwa niaba ya Watanzania iko pamoja nao katika kipindi hicho cha maombelzo. 

  WATANZANIA SABA WAULA KAMATI ZA CAF
  Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la mpira barani Afrika (CAF ) kilichokutana mwishoni mwa wiki jijini Cairo nchini Misri, kimewateua watanzania saba kuwa wajumbe wa kamati zake mbali mbali kwa kwa kipindi cha miaka miwili 2015-2017. 
  Walioteuliwa pamoja na kamati zao katika mabano ni:

  1. Leodeger Tenga- (Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Fedha, Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN), Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, na Mjumbe wa Kamati ya Ushauri na Vyama Wanachama).

  2. Jamal Malinzi - (Mjumbe kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 20)

  3. Mwesigwa Selestine - (Mjumbe Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya Miaka 17).

  4. Richard Sinamtwa -(Mjumbe Kamati ya Rufaa)

  5.Dr Paul Marealle -(Mjumbe Kamati ya Tiba)

  6. Lina Kessy -(Mjumbe ya Soka la Wanawake)

  7. Crescentius Magori-(Mjumbe Kamati ya Soka la Ufukweni na Soka la Ndani)

  Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania - TFF linawapongeza wajumbe wote walioteuliwa kuingia katika kamati mbali mbali na linawatakia kila la kheri wanapoiwakilisha nchi yetu.
  TFF. 
  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA 
  MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

    HALMASHAURI ya Wilaya ya Mufindi  Mkoani Iringa ni mingoni mwa  Wilaya saba nchini, zilizochaguliwa na shirika la kimataifa linaloshughulikia mazao ya viazi (CIP) kutekeleza mradi  wa uzalishaji wa viazi lishe vyenye asilimia kubwa ya vitamini “A” ukilinganisha na  aina nyingine ya vyakula kama Mboga, Matunda na Mizizi.

  Taarifa iliyotolewa na Afisa ya Habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Ndimmyake Mwakapiso, imeeleza kuwa, viazi lishe hivyo ni aina ya viazi vitamu vyenye asilimia 90 ya vitamini A vinavyohitajika katika mwili wa binadamu ili kujenga ubongo wa watoto walio chini ya miaka 05, kuimarisha afya ya wajawazito pamoja na uwezo wa kuona kwa kila mwanadamu.  Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi  Mkoani Iringa ni mingoni mwa  Wilaya saba nchini, zilizochaguliwa na shirika la kimataifa linaloshughulikia mazao ya viazi (CIP) kutekeleza mradi  wa uzalishaji wa viazi lishe vyenye asilimia kubwa ya vitamini “A” ukilinganisha na  aina nyingine ya vyakula kama Mboga, Matunda na Mizizi.


  Katika kutekeleza adhima hiyo, mradi huo umeanza kutekekelezwa katika vikundi vya wakulima kwa kuotesha mbegu kwenye maeneo yenye miundombinu ya umwagiliaji yaliyopo katika viijiji vya Igomaaa na Lugolofu pamoja bustani zilizopo kwenye vijiji vya Lugema, Mabaoni na Makungu.
   
   Taarifa hiyo imeongeza kuwa mbegu zitakazozalishwa zitagawiwa kwenye vijiji 18 ambayo vimechaguliwa kutekeleza mradi huo kwa kipindi cha miaka mitatu na utekelezaji mara babada ya kwa kipindi cha mvua.

  Aidha, endapo Viazi hivyo vitazalishwa kwa wingi na kuongezwa thamani   vitaboresha  kipato kwa mkulima kwani soko lake linapatikana kwa urahisi huku vikiwa na uwezo wa kuzindikwa kwa utengenezaji wa Kripsi, Mkate, Chapati, Biskuti, Juisi na unga wa lishe.  Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi  Mkoani Iringa ni mingoni mwa  Wilaya saba nchini, zilizochaguliwa na shirika la kimataifa linaloshughulikia mazao ya viazi (CIP) kutekeleza mradi  wa uzalishaji wa viazi lishe vyenye asilimia kubwa ya vitamini “A” ukilinganisha na  aina nyingine ya vyakula kama Mboga, Matunda na Mizizi.

  0 0

  Na Mubelwa T Bandio
  MAISHA. Nimejifunza kuwa hayako sawa. Na naamini huo ndio usawa wake, kwani humu tuishimo hakuko sawa.
  Hivyo, haitakuwa sawa kwa maisha kuwa sawa katika "uwanja" usio sawa kwa waishimo.
  Na...
  Najua nililoanza nalo na nitakaloendeleza halitaeleweka sawa, na huo ni udhihirisho wa usawa wetu, ambao nao hauko sawa.
  Leo, Agosti 10,  ninapoadhimisha mwaka mwingine katika maisha yangu, naitumia siku hii KUAKISI maisha yangu kuliko kusherehekea.
  UKWELI ni huu...
  Unasoma hapa kwa kuwa "umekua" na kufikia umri wa kusoma na kuelewa. Huu ni umri wa kusherehekea ama kuadhimisha siku kadhaa za kuzaliwa kwako.
  Na, kama unasoma hapa, jambo moja ninaloweza kukuhakikishia ni kuwa UTAKUFA.
  Kwa hiyo, kama wanadamu, haya mawili yanakuwa ya lazima. Ukizaliwa, utakufa. Tofauti ya maisha yetu ipo katikati ya haya mawili.
  Maishani, nimehudhuria BIRTHDAY(s) na MISIBA mingi tu, na kote nimejifunza mengi kuhusu maisha yetu ya sasa, tuyatakayo na namna tunavyojitahidi kuifikia TAMATI yetu.
  Labda funzo kuu nililowahi kushiriki nanyi ni lile nililoliandika HAPA Agosti 22, 2011 baada ya kuhudhuria msiba wa Dada yetu hapa Washington DC.
  Maisha yetu ya sasa yanaonekana kuwa ya mchakamchaka, twayakimbiza matumaini na (katika hali ya kushangaza) hata siku zaonekana kuwa fupi kuliko awali.
  Kabla hujajipanga, ni kesho, ni juma lijalo, ni mwezi ujao na mwaka bila kukamilisha mengi uliyoamini ungependa kuyakamilisha katika muda uliojipangia.
  Ninapoangalia miaka hii niliyoishi, naiona kuwa mingi sana. Si kwa kuwa nimeishi mingi kuzidi wote, bali kwa kuzingatia ni mara ngapi nimekuwa nikiamini nimefika mwisho wa uhai.
  Nakumbuka kusoma makala ya Kaka Eric Shigongo, iliyosema kuuona mwaka mpya ni nafasi ya ziada. Na naamini katika hilo.
  Mara kadhaa (na ni zaidi ya moja) nimekuwa kwenye nafasi ya kuona kama kesho ilikuwa mbali na isiyofikika kwangu nikiwa hai. Siku ambayo hunijia akilini zaidi juu ya hilo, ni HII
  Lakini leo wasoma niandikalo.
  NI NAFASI YA ZIADA katika kuikimbiza "siku ya mwisho"
  Nikirejea kwenye kichwa cha bandiko hili,fikra kwamba maisha yetu ya sasa ni kama kuikimbiza kesho kuliko kuifikiria leo na hata jana, kunatufanya tuonekane kuyawaza yajayo kuliko tulikotoka.
  Ni hili linalonifanya niamini kuwa, maisha yetu ya sasa yamewekeza katika yajayo. Na kama nilivyoeleza kabla, jambo pekee ambalo sote tuna hakika nalo, ni kifo.
  Na ndio maana nikasema, MAISHA ya sasa. Ni kukimbiza DEATHDAY kuliko kuikimbia BIRTHDAY
  Anyway!
  Nisijesahau kujitakia EARTHday njema.
  Najua fika kuwa hongera na shukrani za maisha yangu nazipokea kwa sababu ni Mungu aliyeniweka hai mpaka sasa.
  Na ndiye aliyenipa WAZAZI wangu ambao sina ninanloweza kueleza kuhusu nafasi yao maishani ikalingana na walilotenda.
  Labda jambo moja tu, kwamba walinibariki na NDUGU ambao uwepo wao umekuwa kama egemeo la kukua kwangu. Hawa ndugu wameniwezesha kuambatana na JAMAA ambao kwa muongozo wa ndugu, wameniwezesha kuwa nilivyo. Si unakumbuka kuwa Twachagua maongezi, maongezi yachagua mawazo na mawazo yatuchagulia jamii? (Isome hapa)
  Nina maRAFIKI ambao wananisaidia katika kukua kwangu. Hawa nawajumusha na wale wanajiona kama maadui kwangu, ambao mara nyingi wamenifanya kujitahidi kukamilisha mambo ili wasipate la kusema.
  Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa
  Kipekee, namshukuru mke wangu mpenzi Esther na wanangu Paulina na Annalisa kwa kuwa wavumilivu kwenye harakati zangu (nyingine hazielewekagi yaani)
  Hahahaaaaaaaaaaaaaa
  Ni siku nyingine ya kukumbuka kuzaliwa kwangu. Nalikaribia hitimisho la maisha, na nikilijongelea, najitahidi kukamilisha dhumuni yangu ya kuwa humu duniani.

  Mungu akubariki na kuonyeshe namna muafaka ya kutenda kila lililo jema, kadhi uikaribiavyo.
   

  0 0

  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mhe. Clara Diana Mwatuka(Mb), aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, kupitia Chama cha Wananchi, (CUF) Mkoa wa Mtwara, kilichotokea jana Jumapili tarehe 9 Agosti 2015 kwa ajali ya gari katika Kijiji cha Miyuyu, Newala, Mkoani Mtwara.


  Mipango ya Mazishi inaendelea kufanywa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho siku ya Jumanne tarehe 11 Agosti, 2014 saa 9:00 Alasiri, kijijini kwake Nanganga, Wilayani MASASI, Mkoa wa MTWARA. Taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kadri zitakavyopatikana.


  MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU 
  MAHALI PEMA PEPONI - AMINA!

  Imetolewa na:

  Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa

  Ofisi ya Bunge

  DAR ES SALAAM


  10 Agosti, 2015


older | 1 | .... | 935 | 936 | (Page 937) | 938 | 939 | .... | 3353 | newer