Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 934 | 935 | (Page 936) | 937 | 938 | .... | 3282 | newer

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mwakilishi wa shirika la misaada la Ujerumani KFW Bi.Katrin Brandes na mkuu wa mkoa wa Lindi Bibi Mwantum Mahiza wakifunua kitambaa kuzindua ujenzi wa mradi wa maji wa mji wa Lindi eneo la Ng’apa mjini Lindi leo.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael Muhuga kombe la ushindi baada ya taasisi anayoiongoza kuibuka mshindi wa taasisi iliyofanya vyema kuliko zote(Overall Best Exhibitor) wakati maonyesho ya sikukuu ya wakulima nanenane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini lindi leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi Benki ya Maendeleo ya kilimo huko eneo la Ngongo yalikofanyika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima kitaifa Nanenane leo.

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya sikukuu ya wakulima nanenane yaliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi leo.Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuagana na wananchi wa mkoa wa Lindi.(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Jeshi la Magereza nchini limeibuka Mshindi wa kwanza kwa upande wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika katika Kanda ya Kasikazini(Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara), Kanda ya Magharibi(Mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga na Dar es Salaam) pamoja na Kanda ya Magharibi(Mikoa ya Tabora, Kigoma na Shinyanga) ambapo Jeshi la Magereza limeibuka kidedea katika upande wa Uzalishaji Taasisi za Serikali pamoja na Taasisi za Serikali upande wa Teknolojia na Maonesho Vyombo vya Ulinzi na Usalama. 
  Jeshi la Magereza ni Miongoni mwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi likiwa na jukumu lake la kuwahifadhi na kuwarekebisha Wafungwa wa aina mbalimbali wawapo Magerezani ili pindi wamalizapo vifungo vyao waweze kuwa raia wema katika jamii. Pia hushiriki kikamilifu katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa na Kikanda kwa lengo la kutoa elimu kwa umma kupitia shughuli zake mbalimbali za uzalishaji katika Sekta za Kilimo na Mifugo.
  Mbali na ushindi huo wa Kikanda, Jeshi la Magereza limeshiriki kikamilifu katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Kitaifa(Maarufu kama Nane Nane) katika Mkoa wa Lindi ambapo Jeshi hilo limeibuka Mshindi wa Pili kwa upande wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Kilele cha Maonesho hayo huku Jeshi la Kujenga Taifa likibuka Mshindi wa Kwanza wa Jumla na Mgeni rasmi katika Kilele cha Maonesho hayo Kitaifa alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete. 
  Kutokana na Ushindi huo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja amewapongeza Maafisa na Askari wote walioshiriki kikamilifu katika Maonesho hayo hadi kufanikisha ushindi huo na amewapa changamoto ya kuongeza bidii zaidi katika utendaji wao wa majukumu ya kazi ili katika Maonesho yajayo waweze kufanya vizuri zaidi.
  Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Jeshi la Magereza kuibuka Mshindi wa kwanza kwa upande wa Taasisi za Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika Kikanda hapa nchini tangu Mwaka 2013. Maonesho ya Wakulima Nane Nane Kitaifa yamefunguliwa rasmi Agosti 04, 2015 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Matokeo Makubwa Sasa" - Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Wakulima na Wafugaji. 
   Imetolewa na Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje, 
   Afisa Habari wa Jeshi la Magereza, Agosti 08, 2015.
  Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Antonino Kilumbi akiwa ameshika vikombe vya ushindi katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati kwa Mwaka 2015. Wengine ni Maafisa Washiriki wa Jeshi la Magereza wa Maonesho ya Wakulima ya Nane Nane Kanda ya Kati, Dodoma.

  0 0

   Ofisa elimu wa jiji la Mbeya Protas Mpogole akimkabidhi nahodha wa timu ya Mbaspo Academy Biva Stiven baada ya timu yake kuibuka bingwa wa michuano ya Airtel Rising Star, jana jijini Mbeya. 

  Wachezaji wa timu ya Mbaspo Academy wakishangilia baada ya kuwa mabingwa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars. Michuano hiyo ilimalizika jana jijini Mbeya.


  0 0
  0 0

  Karibu katika uzinduzi wa Albamu ya injili kesho ktk kanisa la Umoja la Dallas, Texas, Marekani.
  Mtumishi wa Mungu kaka Morris Swai ambae ni mtoto wa mchungaji Ragate Swai wa Kinondoni Assemblies (TZ)atazindua Albamu yake ya kwanza.
  Morriss anaishi Houston Texas kwa sasa.
  Karibuni wote bila kukosa. 
  Ps.Absalom-Umoja Church.


  0 0
 • 08/08/15--20:30: KUMBUKUMBU

 •  MAMA MAGRETH LUTHER NANZA 
  09.08.2001-09.08.2015

  Leo ni miaka 14 tangu umeitwa mbinguni! Mama ulikuwa nguzo na tegemeo la maisha yetu. Haupo machoni lakini upo katika mioyo yetu. 

  Daima utakumbukwa na wanao Jane, Hellen, John, Samson, Gyumi na Ruth. Wakwezo Sultan, Levison, Rachel, Monalisa na Sham. Wajukuu zako, ndugu, jamaa na majirani zako. MAMA TULIKUPENDA LAKINI MUNGU ALIKUPENDA ZAIDI JINA LA BWANA LIHIDIMIWE AMEN.

  0 0


  Kijana ABEL MACHANG'A, mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Ukonga Mombasa Jijini Dar es Salaam, ambae anasumbuliwa na maradhi ya macho, akiwa amejipumzisha nyumbani kwao baada ya kuzungumza na waandishi wa habari ili kuomba msaada wa kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kupatiwa matibabu.  

  Na Mwandishi Wetu

  Kijana Abel mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa Ukonga Mombasa jijini Dar es Salaam anakabiliwa na maradhi ya macho na mishipa ya fahamu hali iliyosababisha apoteze uwezo wa kuona, na hivyo kuhitaji msaada wa wasamaria wema ili apelekwe nchini India kwa matibabu zaidi.

  Ama kweli kabla hujafa hujaumbika! Kijana ABEL MACHANG’A aliyezaliwa miaka 23 iliyopita alikuwa na uwezo wa kuona kama kawaida na alisoma mpaka kidato cha nne na baadaye kujiunga na elimu ya biashara katika chuo cha biashara cha CBE cha jijini Dar es Salaam.

  Lakini hivi sasa kijana huyo haoni tena baada ya kupata maradhi ya macho yaliyosababisha macho yake kuvimba na kutoka nje licha ya kupatiwa matibabu.
  Baba wa kijana huyo amesema jitihada za kutibiwa nchini zimeonekana kutokuwa na mafanikio na kuomba wasamaria wema na mashirika mbalimbali yajitokeze kumsaidia kijana huyu gharama za matibabu takribani milioni Hamsini.

  Kwa yeyote atakayeguswa na maradhi ya kijana huyu, awasiliane na Chumba cha Habari Clouds Tv Mikocheni jijini Dar es Salaam au awasiliane na baba mzazi wa kijana huyo kwa namba 0713 275740 au 0784 275740.


  0 0


   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji safi katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji safi katiaka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

   Sehemu ya Chotea kama inavyoonekana pichani katika mradi mkubwa wa maji safi katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi,mradi huu ukikamilika utaweza kutoa lita milioni 750 ambapo utakuwa umetosheleza mahitaji ya maji, kwa sasa wakazi wa Manispaa ya lindi wanapata lita milioni 250 na mahitaji yao ni lita milioni 500.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ujenzi wa mradi wa maji safi uliopo Ng'apa mkoani Lindi.

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali ,Wahisani na Wakandarasi mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji safi wa halmashauri ya Manispaa ya Lindi.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Ng'apa waliojitokeza kwa wingi kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa mradi wa maji safi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Lesotho is one of the smallest African countries. Being one of the smallest countries doesn't necessarily favor Lesotho when it comes to serious issues affecting the African economy in general. Regardless of its size, Lesotho like any other African country has to tackle all its economic issues and what impedes its economic growth. 
   A quarter of its population is HIV positive. The majority of the people living with HIV/AIDS are women. Almost 40 per cent of the population works in textile industries, with the rest working in Agricultural sector or mines in South Africa, etc. Nalane, an NGO, created to support the HIV infected people shares its story in this interview. 
  I realize that other NGOs elsewhere would also benefit in many ways from the story shared to us by Nalane. You may also learn some of the challenges facing the HIV/AIDS NGOs in Lesotho and may be in Africa. 
   You are welcome to watch this show on Friday August 14th from 4:00 pm to 5:00 pm (New York Time) on the following channels depending on who your service provider is. Total Duration: 58 Minutes. 
  The  video below has only 31 minutes of the 58 minutes. To watch the entire 58 minutes of the show please see the details below. 
   Provider Channel Times Warner Cable (TWC) 67 and 1998 FiOS 36 RCN 85 To stream online tune to channel 4 @ www.mnn.org/4-culture-channel%20 every friday from 4:00 pm to 5:00 pm (New York Time). 
   Thank You and Stay Tuned.

  0 0

  TBC: Pata dondoo za vichwa vya habari vilivyopewa umuhimu wa kipekee katika magazeti ya Jumapili ya leo.https://youtu.be/aH3bqEH_7RI
   AZAM TV: Tazama udondozi wa kina wa habari zilizopewa kipaumbele katika magazeti ya juma pili ya leo. SIMUtv;http://youtu.be/RhvP6EYLk94
   STAR TV: Usisite kutazama uchambuzi wa habari motomoto zilizopewa uzito wa juu katika magazeti ya leo Agosti 9. SIMUtv.  http://youtu.be/RAe-c2la5tM

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akimpongeza Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali, Mbazi  Msuya kwa ofisi hiyo kuwa mshindi wa kwanza kwa Wizara za Huduma za Jamii zilizoshiriki maonesho ya Nane Nane Kitaifa mkoani Lindi, Tarehe 8 Agosti , 2015.
   Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifurahia  kombe la kuwa mshindi wa kwanza kwa Wizara za Huduma za Jamii zilizoshiriki maonesho ya Nane Nane Kitaifa mkoani Lindi, Tarehe 8 Agosti , 2015, walioshika kombe hilo katikati ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali, Mbazi  Msuya, kulia kwake ni Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maadhimisho ya Kitaifa  Ofisi ya Waziri Mkuu, Flora Mazilengwe.
  Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi  akipata maelezo ya bidhaa zinazotengezwa na vikundi vya wajasiriamali kutoka Zanzibar waliowezeshwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) na kushoto kwake ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maadhimisho ya Kitaifa  Ofisi ya Waziri Mkuu, Flora Mazilengwe, walipotembelea banda hilo Tarehe 8 Agosti , 2015.

  0 0

  Na Benedict Liwenga, Maelezo-Mbeya
  Kutokana na ongezeko la mahitaji ya nishati ya umeme nchini, nishati ya jotoardhi imetajwa kuwa ni muhimu kwa kuwa itaisaidia Tanzania kuondokana na tatizo la umeme usiokuwa na uhakika pamoja na kupunguza gharama kubwa zitokanazo na matumizi ya mitambo ya uzalishaji umeme yenye kutumia mafuta. 
   Kauli hiyo imetolewa 8 Agosti, 2015 na Mjiolojia Mkuu toka Wizara ya Nishati na Madini, Bwana. Jacob Mayalla wakati wa Kampeni endelevu ya kuelimisha umma kuhusu nishati hiyo katika Kata za Swaya Mjini, Nzovwe pamoja na Igale jijini Mbeya. 
   Mayalla ameeleza kuwa, kwa kawaida utafiti wa nishati ya jotoardhi unahusisha hatua kuu tatu zikiwemo ya utafiti wa maeneo yenye upatikanaji wa nishati hiyo, uchimbaji pamoja na uzalishaji ambapo kwa mkoa wa Mbeya, tayari hatua ya utafiti ilishakwishafanyika katika miaka ya nyuma ingawa bado zoezi hilo ni endelevu ili kujidhihirisha na sehemu ya uchimbaji na kwasasa hatua zinazofata ni uchimbaji pamoja na uzalishaji ili kuongeza nguvu ya uzalishaji wa umeme ikiwemi kuwezesha matumizi ya moja kwa moja ya nyumbani. 
   “Maeneo yaliyofanyiwa utafiti na kubainika kuwepo na kiwango cha juu cha jotoardhi nchini ni pamoja na Ziwa Manyara, Ziwa Natron, Ngorongoro Crater, pia katika Mkoa wa Mbeya, na maeneo mengine ya Ziwa Eyasi na Mara (Maji Moto) yalibainika kuwa na kiwango cha chini cha joto”, alisema Mayalla. 
  Naye Afisa Mawasiliano toka Kampuni ya Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Bi. Johari Kachwamba ameeleza juu ya hali ya uzalishaji wa umeme ilivyo hapa nchini hususani katika mkoa lengwa wa Mbeya kuwa inatumia Megawati 40 jambao ambalo umeme umekuwa usio wa uhakika, hivyo TGDC ina mkakati wa kuongeza uzalishaji huo hadi kufikia Megawati 200 jambao ambalo litaweza kusaidia na mikoa mingine ya pembezoni. 
   “Kampuni ya TGDC ni Kampuni tanzu iliyopo chini ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) na tuna majukumu mengi ikiwemo kuharakisha uzalishaji wa nishati hii ya jotoaardhi ili iwe nishati mbadala na kupunguza mgao wa umeme kwani nishati hii pindi ikianza kutumiwa haitarajiwi kuisha, ni nishati endelevu”, alisema Kachwamba. 
   Kwa upande wake Afisa Sayansi ya Jamii toka TGDC, Bi. Eva Nyantori amezitaja baadhi ya fursa mbalimbali ambazo jamii itashirikishwa na mradi huo zikiwemo fursa za ajira ili kuwaongezea vipato wakazi wa maeneo ambayo nishati hiyo itapatikana, elimu juu ya afya hususani elimu dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwani pindi mradi utakapoanza kuna uwezekano wa kuwa na mahusiano baina ya wageni na wenyeji. 
   Kuhusu athari za mazingira ambazo zinaweza kujitokeza pindi mradi huo utakapoanza, Afisa Mazingira toka TGDC, Bi. Esther Range amefafanua kuwa kabla ya mradi kuanza Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) litafanya ukaguzi wa maeneo husika ili kujiridhisha juu ya athari zinazoweza kutokea katika eneo husika. 
   “Nishati hii ya jotoardhi hatutegemei kuwa italeta atahri katika mazingira yetu kwani kampuni itachukua hatua madhubuti ili kuepusha athari zozote zinazoweza kujitokeza ikiwemo kuwahusisha watu wa NEMC kwani wao ndo watatupatia kibali cha kuweza kuendelea na mchakato wa uchimbaji wa nishati hii, hivyo niwatoe wasiwasi wananchi kuhusu athari”, alisema Range. 
   Naye Mhandisi Mazingira toka Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Bwana. Fikirini Mtandika amesema kuwa TGDC iko mbioni kuandaa Sheria zinazohusu nishati ya jotoardhi ili Kampuni iweze kufanya kazi zake kwa umakini na kwa kuzingatia Sheria, akaeleza pia kutakuwa na masuala ya fidia kwa wahanga ambao mradi huo ikitokea umeangukia katika maeneo yao na hapo aksema kuwa ikitokea hivyo Sheria Na. 4 na N. 5 ya mwaka 1999 zitatumika katika masuala ya fidia lakini kabla ya fidia jamii husika itapewa elimu ya kutosha kuhusu fidia ili kuijengea uelewa wa kutosha. 
   “Hii Sheria itambuliwe kuwa sisi kama Kampuni hatutohusika katika kufanya tathmini ya mali ya Mhanga isipokuwa kutakuwa na Mtathmini kutoka Serikalini ambaye yeye ndiyo atafanya kazi hiyo na sisi kazi yetu itakuwa kufanya malipo tu kwani itakuwa sio vema sisi kufanya tathmini kwani tunaweza kumpunja mhanga, na fidia hii itafanywa kwa kipindi kisichozidi miezi Sita, hviyo jamii iondoe wasiwasi kuhusu suala la fidia” alisema Mtandika. 
  Mkurugeniz Mkuu anaeshughulikia masula ya Ufundi wa Kampuni ya Uendelezaji Nishati ya Jotoardhi (TGDC), Bwana, Taramaeli Mnjokava akiwaelimisha Viongozi wa Kata ya Swaya Mjini kuhusu faida za jotoardhi mapema 8 Agosti, 2015 mkoani Mbeya.
  Mjiolojia Mkuu toka Wizara ya Nishati na Madini, Bwana. Jacob Mayalla akiwaeleza Viongozi wa Kata ya Swaya Mjini kuhusu historia ya nishati ya jotoardhi kuanza kufanyika hapa nchini miaka ya 1976 hadi 1978 mapema 8 Agosti, 2015 mkoania Mbeya.
  Afisa Sayansi ya Jamii toka Kampuni ya Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Bi. Eva Nyantori akiwaeleza Viongozi wa Kata ya Swaya Mjini kuhusu namna gani jamii itahusishwa na mradi huo hususani katika suala la upatikanaji wa ajita kwa wakazi wa maeneo yenye mardi huo, mapema 8 Agosti, 2015 mkoania Mbeya.
  Afisa Mawasiliano toka Kampuni ya Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Bi. Johari Kachwamba akiwaeleza Viongozi wa Kata ya Swaya Mjini kuhusu dhamira na majukumu ya Kampuni ya TGDC hususani masuala yote yanayohusiana na nishati ya jotoardhi mapema 8 Agosti, 2015 mkoania Mbeya.
  Mhandisi Mipango toka Kampuni ya Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Bwana Chagaka Kalimbia akiwaeleza Viongozi wa Kata ya Swaya Mjini kuhusu faida za moja kwa moja za nishati ya jotoardhi, mapema 8 Agosti, 2015 mkoania Mbeya.

  0 0

  Mgeni rasmi katika ufungaji wa Mafunzo ya awali ya skari Polisi,NaibuWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Pereira Ame Silima akizungumza wakati wa sherehe za ufungaji wa mafunzo hayo zilizofanyika Chuo Cha Taaluma ya Polisi Moshi,
  Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya awali ya Askari Polisi na Uhamiaji.
  Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi ,Abdulrahman Kaniki akitoa hotuba yake katika siku hiyo.
  Mkuu wa Chuo cha Polisi ,Commandant ,Matanga Mbushi akitoa hotuba yake katika sherehe hizo.
  Baadhi ya wahitimu.
  Askari Polisi wahitimu wakionesha umahiri wa kucheza Karate.

  Askari wahitimu wa kike wakionesha namna ambavyo walivyofundishwa matumizi ya Bastola.
  Askari Polisi wahitimu wakionesha nmna ya kushusha wagonjwa kutoka gorofani.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema kwamba wakati Serikali inaendelea na jitihada za kuimarisha sekta ya Kilimo ili ikue kwa kasi ya asilimia Tano Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wanapaswa kuitumia fursa ya uzalishaji wa mazao ya Kilimo kuwekeza katika miundombinu na viwanda kwa lengo la kuyaongezea thamani mazao hayo. 
  Alisema uwekezaji huo utawapa nguvu zaidi za uzalishaji wakulima na hatimae kuongeza kipato chao kutokana na uzalishaji wa bidhaa zilizo katika kiwango kinachokubalika Kimataifa na hivyo kupunguza umaskini kwa Wananchi nchini ambao wengi wanategemea sekta hiyo mama kuendesha maisha yao ya kila siku. Balozi Seif Ali Iddi alitoa rai hiyo wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku Kuu Wakulima iliyoambatana na Maonyesho ya Wakulima Nane Nane Mwaka 2015 Kanda ya Mashariki yanayofanyika katika uwanja wa Taifa wa Mwalimu J.K. Nyerere uliopo Mkoani Morogoro. 
  Alisema juhudi hizo za Serikali Kuu zimehusisha kuendeleza miundombinu ya umwagiliaji maji ili kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua, kuondoa kodi katika zana mbali mbali za sekta ya kilimo sambamba na uimarishaji wa bara bara za vijijini ili kuongeza tija. 
  Balozi Seif alisema Serikali imeamua kutekeleza Mpango wa matokeo Makubwa  sasa  kuanzia mwaka 2013/2014 ukilenga kuleta matokeo makubwa na ya haraka, ambapo Kilimo kikitegemewa kuwa miongoni mwa sekta sita zilizopewa kipaumbele kutekelezwa kwa mpango huo. 
  Ujumbe wa maadhimisho ya siku kuu ya Wakulima Nane nane mwaka huu wa 2015 unasema ” Matokeo makubwa sasa { BRN } uchague Viongozi bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji “.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiingia katika eneo la Maonyesho ya Siku Kuu ya Wakulima Nane nane zilizoadhimishwa katika Uwanja wa Mwalimu J.K. Nyerere Kanda ya Mashariki uliopo Mkoani Morogoro akiwa na Viongozi wa Kanda hiyo.
   Luteni Mtui wa JKT akimfahamisha Balozi Seif hatua inayochukuliwa na Jeshi hilo katika kuimarisha kilimo cha mazao mbali mbali kwa kutumia Utaalamu wa
  Kisasa.
   Mmoja wa Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar jitihada wanazochukuwa wakulima katika kuendesha kilimo kwa njia ya kisasa. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Tanzania
  Bwana Salum Mwakuginda.
   Balozi Seif akiridhika na kazi kubwa inayoendelezwa na Shrika la Mzinga linalojishughulisha na utengenezaji wa samani za Majumbani na Ofisini na kushawishika kutajka kuweka oda ya ununuzi kwa ajili ya baadhi ya skuli za Jimbo lake

  Watendaji wa Kampuni ya kigeni ya uuzaji wa vifaa vya Mtandao wa kisasa vya simu ya FFTG kutoka Nchini Jamuhuri ya Watu wa China nayo ni miongoni mwa taasisi zilizoshiriki maonyuesha ya wakulima Nane nane Mkoani Morogoro ambapo Balozi Seif alipata wasaa wa kuitembelea.
  Balozi Seif akikabidhi Kikombe cha ushindi wa Pili wa Jumla kwenye maqonyesho na wakulima Nane nane Mjini Mrogoro uliochukuliwa na Chuo Kikuu cha Kilimo Morogoro. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Tanzania Bwana Salum Mwakuginda na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Said Meck Sadiq. Picha na OMPR – ZNZ.

  0 0


    JK akipata picha na Mgombea Ubunge Moshi Mjini Davies Mosha na mwendesha talk show Mboni Mashimba kwenye hafla ya Wasanii wa fani mbalimbali ya kumuaga usiku wa Alhamisi Agosti 6, 2015
   JK akisalimiana na msani Cassim Mganga
   Ommy Dimples akipata selfie na JK
   Wasanii wakipata selfie na JK
   Kila msanii aliomba selfie na JK
   Selfie kila meza na JK hakufanya hiyana
   JK akipata selfie toka kwa Salma Jabir na Madame Rita
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

   Rais Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi  katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi zinazojengwa  na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu pamoja na Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo.
   Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,Ndugu Nehemia Mchechu akizungumza jambo na Rais  Dkt Jakaya Kikwete mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30za makazi zinazojengwa  na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4,Kulia ni Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais mteule wa chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli wakiondoka eneo la tukio mapema leo mchana.
   Sehemu kivuko hicho kilichozinduliwa Rais Dkt Jakaya Kikwete mapema leo mkoani Mtwara.
  Waziri wa Ujenzi na Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt Jonh Pombe Magufuli akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini baada ya uzinduzi wa  kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3,Dkt Magufuli amesema kuwa Rais Jakaya Kikwete katika utawala wake ndani ya maiaka kumi amefanikiwa kujenga vivuko vipya 15 na vingine 7 vimekwishakarabatiwa na vinafanya kazi mpaka sasa
   Rais Dkt.Jakaya Kikwete akizungumza jambo mbele ya wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini kuzindua kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
   Bango la mradi huo
   Mkuruegenzi Mkuu wa NHC,Nehemia Mchechu akizungumza jambo mbele ya mgeni rasmi Rais Dkt Jakaya Kikwete pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na wananchi kwa ujumla katika mradi wa ujenzi wa nyumba 30 za makazi zinazojengwa  na NHC Shangani mkoani Mtwara zenye thamani ya shilingi bilioni 4.4.
  Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi wa Msanga Mkuu-Mtwara vijijini waliofika kwenye uzinduzi wa kivuko cha MV Mafanikio chenye uwezo wa kubeba watu 100 na magari sita,chenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 3.3
  0 0

   Wasanii wa Kundi la Quality Boys kutoka Temeke jijini Dar es Salaam, wakionyesha umahiri wao wa kusakata dansi  wakati wa usaili wa tatu wa shindano la Dance 100% 2015 uliofanyika kwenye viwanja vya Leaders  Clup Kinondoni  jijini  Dar es Salaam.Shindano hilo limeandaliwa na EATV na   kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
   aadhi mashabiki waliojitokeza kwenye viwanja vya Leaders Club  jijini Dar es Salaam, wakifuatilia usaili wa tatu  wa shindano la  Dance 100% 2015 lililoandaliwa na EATV nakudhaminiwa na  Vodacom Tanzania mwishoni mwa wiki.
   Vijana wanaounda kundi  la Wazawa kutoka Tandale  jijijini Dar es Salaam, wakikongo nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la usaili wa tatui wa shindano la Dance100%2015,lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kkinondoni , shindano hilo limeandaliwa na EATV na Kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
    Baadhi ya vijana wanaounda kundi la Pambana Fasaha Kiwarani  jijiji Dar es Salaam, wakionyesha umahiri wao wa kusakata dansi wakati wa usaili wa tatu waiwanja vya shindano la Dance100% 2015 lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania lilifanyika katika  v Leaders Club  mwishoni mwa wiki.
  05&006.Vijana wanaoaunda kundi la Fresh Crews la Kinondoni wakionyesha vionjo vyao vya kusakata dance  kwa mashabiki waliojitokeza kwenye viwanja vya Leaders Club  jijini Dar es Salaam, wakati wa usaili wa Tatu wa shindano la Dance100%l lilioandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.

  Vijana wanaoaunda kundi la Fresh Crews la Kinondoni wakionyesha vionjo vyao vya kusakata dance  kwa mashabiki waliojitokeza kwenye viwanja vya Leaders Club  jijini Dar es Salaam, wakati wa usaili wa Tatu wa shindano la Dance100%l lilioandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
   Majaji wa shindano la Dance 100%  2015,kutoka kushoto Super Nyamwela, Sheta  na Queen Darling  wakiwa katika mchakato wa usaili wa tatu wa shindano hilo lililoandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania, lilifanyika katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni  jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Vijana wanaounda kundi la Pambana fasaha la Kiwalani  jijini  Dar es Salaam, wakikongo nyoyo za mashabiki waliojitokeza kwenye onyesho la usaili wa tatui wa shindano la Dance100%2015,lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kkinondoni , shindano hilo limeandaliwa na EATV na Kudhaminiwa na Vodacom Tanzania

  0 0

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akikumbatiana na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kabla ya kuelekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF. 
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad na Wenyeviti wenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia na Dkt. Emmanuel Makaidi wakitembelea kuelekea Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakiwapungia wafuasi wa Vyama vinavyounda UKAWA wakati wakielekea kwenye Makao Makuu Chama cha Wananchi CUF, Buguruni jijini Dar es salaam leo August 9, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi CUF. Wengine walioambatana nao ni Wenyeviti wenza wa UKAWA, Mh. James Mbatia na Dkt. Emmanuel Makaidi.

  KUONA PICHA ZAIDI


older | 1 | .... | 934 | 935 | (Page 936) | 937 | 938 | .... | 3282 | newer