Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 933 | 934 | (Page 935) | 936 | 937 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0


  0 0  Na Mwandishi Wetu, Dar 
  Kwa miaka mingi upatikanaji wa wataalamu wa Afya na matibabu ya uhakika unakabiliwa na changamoto kuu mbili inayowakumba wagonjwa wengi Tanzania.Watanzaniawamekuwa wakisafiri nje ya nchi kupata matibabu ya Figo na magonjwa yanayohusiana na kibofu. Hivyo wataalamu wawili waliobobea katika magojwa ya Figo na Kibofu kutoka Hospitali za Apollo walitembelea nchini Tanzania wakishirikiana na madaktari kutoka Hospital ya Hindu Mandal ili kuwafanyia uchunguzi, kutoa tiba na kutoa ushauri kwa wagonjwa mbalimbali Tanzania. Dkt V. Rajagopal ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya njia ya mkojo na mfumo wa uzazi wa kiume na amekuwa mshauri mwandamizi wa magonjwa ya kibofu katika Hospitali za Apollo huko Hyderabad India tangu mwaka 1994. Dkt. Sanjay Maaitra ambaye ni mtaalamu wa magonjwa ya Figo kwa kutoa huduma za matibabu ya figo na magonjwa yanayoambatana na Figo ikiwa lengo kuu la ujio wao ni kuhakikisha wagonjwa wanapata uchunguzi sahihi bila kuingia gharama kubwa za kwenda nje ya nchi.
  Kwa tarifa kaamili BOFYA HAPA

  0 0

   MSAIDIZI Mkutubi Mkuu wa Shirika la Huduma za Maktaba Zanzibar, Abdalla Omar akielezea namna ya uzinduzi wa tamasha la uhamasishaji wa kusoma vitabu, kwa wanafunzi na wananchi wa wilaya ya Micheweni Pemba, lililofanyika juzi.
   AFISA Elimu na Mafunzo ya Amali wilaya ya Micheweni Pemba Mbwana Shaame, akielezea faraja yao, kwa Shirika la Huduma za Maktaba Zanzibar, tawi la Pemba kuanza wilaya hiyo, uzinduzi wa tamasha la uhamasishaji wa usomaji wa vitabu kwa wananchi na wanafunzi lililofanyika skuli ya Micheweni.
   AFISA Uendeshaji kutoka wizara ya elimu na mafunzo ya amali Pemba, Salim Ali Mata, akisoma hutuba kwenye uzinduzi wa tamasha la uhamasishaji wa usomaji wa vitabu, lililoandaliwa na Shirika la Huduma za Maktaba Pemba na kufanyika skuli ya Micheweni.
   BAADHI ya vitabu vilivyotayarishwa na Shirika la Maktaba Zanzibar kisiwani Pemba, kwa ajili ya kusomwa na wananchi na wanafunzi wa wilaya ya Micheweni, kwenye tamasha la uhamasishaji wa usomaji wa vitabu hivyo lililodumu kwa muda wa siku mbili.

   AFISA Uendeshaji kutoka wizara ya elimu na mafunzo ya amali Pemba, Salim Ali Mata, (kushoto) akionyeshwa baadhi ya vitabu vilivyotayarishwa na Shirika la Maktaba Pemba na Msaidizi Mkutubi Mkuu Abdalla Omar, kwenye tamasha la uhamasishaji wa kusoma vitabu lililofanyika skuli ya Micheweni Pemba.
  BAADHI ya wanafunzi wa skuli za sekondari za wilaya ya Micheweni wakisoma na wengine kuchagua vitabu, kwenye tamasha la uhamasishaji wa usomaji wa vitabu lililoandaliwa na Shirika la Maktaba Pemba na kufanyika skuli ya Micheweni, (Picha na Haji Nassor, Pemba).    

  0 0

   Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha kwa wananchi mgombea mwenza Said Miraj (kulia) na mgombea urais wa chama hicho, Zanzibar, Hamad Rashid Hamad  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Buguruni Sheli Dar es Salaam jana. 
   Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha kwa wananchi mgombea mwenza Said Miraj (kushoto), baada ya kuchukua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dar es Salaam leo. Kulia ni mke wake, Mwanaisha Lutasola.
   Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Hamad Rashid Hamad akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
    Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba, akihutubia katika mkutano huo Buguruni Sheli jana.
  Wanachama wa chama hicho na wananchi wakisikiliza sera za viongozi hao watakao peperusha bendera ya ADC kwenye uchaguzi mkuu. 

  0 0

  Kwa habari zaidi BOFYA HAPA
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli(wapili kushoto),Balozi wa Kuwaiti nchini Tanzania Mhe.Jassem Ibrahim Al Najem(kulia) pamoja na mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait Bwana Abdulrahman Al Hashim(wapili kulia) wakifunua kitambaa katika jiwe kuashiria kufungua rasmi barabara ya kilometa 60 ya Ndundu-Somanga wakati wa hafla ikiyofanyika katika kijiji cha Marendego Wilaya ya Kilwa leo.Barabara hiyo imefadhiliwa na mfuko wa Kuwait.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambi na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa sherehe ya ufunguzi wa Barabara ya Ndundu Somanga leo


  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na mwakilishi wa mfuko wa Kuwait Bwana Abdulrahman Al Hashim wakati wa sherehe ya ufunguzi wa Barabara ya Ndundu-Somanga iliyofadhiliwa na mfuko huo.Kulia ni Balozi wa Kuwaiti nchini Tanzania Mhe.Jassem Ibrahim al Najem

  0 0


  0 0
 • 08/07/15--23:00: UMAARUFU WA LIGI KUU ENGLAND

 • 0 0


  0 0

   Mafundi wa Hospitala wakiunganisha kitanda cha kujifunguliwa kilicholetwa na Mh Janet Mben kwa ajili  ya hospitalai za ieleje.
   Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janet Mbene,akionyesha baadhi ya vifaa vinavyotumika katika hospital ambavyo avimetolewa na Karemjee Foundation kwa ajili ya Hospital ya Ileje.
   Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akimkabidhi Vitanda vya Kujifungulia Katibu wa CCMwilaya ya Ileje kwa ajili ya Hospitali za wilaya hiyo.
   Mganga mkuu wa Wilaya ya ilje akiangalia kwa furaha sehemu ya msaada wa vitanda uliotolewa na Mhe. Janet Mbene


  0 0

  Tunawatangazia wananchi wote waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR kujitokeza katika vituo walipojiandikisha ili wahakiki taarifa zao. Ambako daftari la mpiga kura limebandikwa. (Display)  
  NA.
  MIKOA
  TAREHE YA KUANZA
  TAREHE YA KUMALIZA
  1
  Njombe, Iringa,  Mtwara, Lindi, Ruvuma, Katavi, Rukwa, Mbeya, Dodoma, Singida, Tabora, Kigoma, Kagera, Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Morogoro.

  07/08/2015
  11/08/2015
  2
  Pwani na Zanzibar
  11/08/2015
  15/08/2015
  3
  Dar es Salaam
  13/08/2015
  17/08/2015

  Mashine zitakuwa katika OFISI YA AFISA MTENDAJI WA KATA  kwa ajili ya kusahihisha makosa yaliyojitokeza wakati wa kujiandikisha.

   Kwa waliohama wakahamishe taarifa zao ziwepo mahali watakapopigia kura tarehe 25/10/2015
  Siku ya UCHAGUZI MKUU. 

  Tangazo hili limetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
  S.L.P. 10923, Dar es Salaam

  Tunza kadi yako, Usimpe Mtu.
  JITOKEZE SASA, NENDA KAHAKIKI TAARIFA ZAKO.


  0 0

   Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid akiongea na wageni waalikwa  na kuwashukuru wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kupambana  na ugonjwa wa tezi dume iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dares Salaam.
   Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo  (WAMA) Daudi Nassib  akiwakilisha mchango wa Sh. milioni tano ambazo ni mchango wa hospitali za mkoa huo pamoja na halimashauri tatu   kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa tezi dume iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dares Salaam                                                             
   Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Grace  Magembe – Mugisha akiwakilisha mchango wa Sh. milioni 10,800,000/=ambazo ni mchango wa hospitali za mkoa huo pamoja na halimashauri tatu   kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa tezi dume 
   Baadhi ya  wadau mbalimbali  wakurafahia wakati wa wa hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kupambana  na ugonjwa wa tezi dume iliyofanhyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dares Salaam
  Baadhi wa wadau waliokuwa wa hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kupambana  na ugonjwa wa tezi dume iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dares Salaam. Picha zote na Magreth Kinabo- Maelezo

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akiangalia bidhaa zinazozalishwa na mjasiriamali anayesaidiwa na benki ya NMB kwenye banda la Benki hiyo kwenye Maonesho ya NaneNane mkoani Lindi
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akipata maelezo juu ya  bidhaa zinazozalishwa na mjasiriamali anayesaidiwa na benki ya NMB kwenye banda la Benki hiyo kwenye Maonesho ya NaneNane mkoani Lindi
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akipata huduma za ATM za  benki ya NMB kwenye banda la Benki hiyo kwenye Maonesho ya NaneNane mkoani Lindi
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akisindikizwa na maafisa wa  NMB baada ya kutembelea  banda la Benki hiyo kwenye Maonesho ya NaneNane mkoani Lindi

  0 0

  NA RAMADHANI ALI-MAELEZO

  CHUO cha Uongozi wa Fedha Zanzibar (ZIFA) kitaanzisha Tawi lake Kisiwani Pemba kuanzia mwaka huu  wa masomo na kitaanza kufundisha  masomo ya   uongozi wa fedha ngazi ya cheti.

  Akizungumza na waandishi wa Habari Makao Makauu ya ZIFA Chwaka, Kaimu Mkuu wa Taaluma Dkt. Iddi Salum Haji amesema wameamua kufungua Tawi  Pemba ili kuzipunguzia gharama  familia zenye  kipato cha chini.

  Amesema utafiti uliofanywa na Chuo  umegundua  kuna vijana wengi Kisiwani Pemba waliomaliza kidato cha nne na wanazo  sifa za kujiunga na chuo kwa masomo ya cheti  lakini wanashindwa kutokana na familia zao kukosa uwezo wa kuwasomesha.

  Ameongeza kuwa chuo kimejipanga  na kukamilisha taratibu zote za kutoa mafunzo hayo  katika Mji wa Wete na wanafikiria kuanzisha Tawi  Mjini Dar es salaam hapo baadae.

  Dkt. Iddi  amesema lengo la Chuo hicho ni kujipanua zaidi hasa kufuatia matokeo mazuri ya mitihani ambapo mwaka huu asilimia 98.3 ya wanafunzi   870 waliofanya mitihani kuanzia  ngazi ya cheti mpaka shahada ya kwanza wamefaulu vizuri.

  “Wanafunzi waliohitimu fani ya Uhasibu wamepasi asilimia mia,  IT asilimia 97 na  fani ya Ugavi na Ununuzi wamefaulu kwa asilimia 98,” amesema Kaimu Mkuu wa Taaluma.
  Amesema mafanikio hayo yamepatikana  kutokana  na wanafunzi kujituma zaidi na walimu  kujitolea  kwa uwezo wao wote na  kuwa  wabunifu  katika kufundisha.

  Ameeleza kuwa baadhi ya fani   zinzofundishwa na chuo cha Uongozi wa Fedha  yanaelekeza zaidi  kwa vitendo na yanawasaidia  wahitimu kuweza  kujiajiri wenyewe.

  Dkt.  Iddi amewashauri  wazazi kuwa waangalifu  wakati vijana wao wanapotafuta  nafasi za kujiunga na Taasisi za elimu ya juu  na kuwataka wahakikishe wanawapeleka kwenye vyuo vyenye sifa na vilivyosajiliwa na  kutambuliwa na Bodi za elimu ya juu NACTE na  TCU.

  “Hivi sasa kumeibuka  msururu wa vyuo vinavyojitangaza vinatoa mafunzo ya Elimu ya juu lakini wanafunzi wanapomaliza na kutafuta ajira ama masomo ya juu inakuwa vigumu kupata kutokana na kuwa havitambuliki,” alisema Dkt. Iddi.

  Kaimu Mkuu wa Idara ya Masomo ya jumla  ZIFA Maalim Said Mohd amesema chuo hivi sasa kimejipanga kuteremka ndani ya jamii kwa kutoa elimu kwa wajasiriamali  ili waweze  kujiendesha  wenyewe.

  “Kwa kuanzia chuo tayari kimeendesha mafunzo ya ujasiriamali  kwa vikundi vya   Wilaya ya Kaskazini A, Wilaya ya Kati  na Wilaya Kusini kwa Unguja na Chake chake na Micheweni  Pemba na lengo ni kumaliza Wilaya zote za Zanzibar,” alisisitiza Maalim Said.

  Mmoja wa wanafunzi waliomaliza masomo  mwaka huu Bakar Omar Hamad  ameishauri Wizara ya elimu kufanya mapitio ya Taasisi zinazotoa elimu ya juu nchini ili kuhakikisha  uhalali wa usajili wao,  mitaala inayotumika  inalingana  na masomo na  kuhakikisha walimu  wanazo sifa zinazokubalika.

  Amesema wazazi wamekuwa wakiwekeza   fedha nyingi kuwasomesha watoto  wao lakini baadhi  ambao mwamko wa kielimu ni mdogo wanawapeleka vijana wao katika vyuo ambavyo  pamoja  na kupata usajili lakini masomo  yanayotolewa yanakosa ithibati ya kufundishwa.

  0 0

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa kilomita 60, hafla hiyo imefanyika jana Agosti 7 2015 mkoani Lindi.Wengine pichani ni Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al Najem,Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait, Abrahman Al- Hashim,Mkuu wa Mkoa wa Pwan, Eng. Evarist Ndikilo, wengine kushoto ni Waziri wa ujenzi Mhe.John Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazia Dkt.Jakaya Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kufunguarasmi barabara ya Ndundu - Somanga.
   Rais Kikwete akimshukuru  Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim mara baada kuweka jiwe la msingi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika   kwenye kijiji cha Marendego ,wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
   Rais wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kwa pamoja na mkewe Salma  Kikwete akimwagia maji mti wa kumbukumbu alioupanda baada ya ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga mkoani Lindi.
  Wafadhili wa ujenzi wa barabara ya Ndundu-Somanga, Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al Najim na   Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim mara kwa pamoja wakishiriki kupanda mti wakati wa sherehe fupi zilizofanyika   kwenye kijiji cha Marendego ,wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
   Rais Kikwete akiwasalimia na kuwaaga wananchi wa kijij cha Nangurukulu na kumtambulisha Mgomea Urais kwa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akielekea mkoani Lindi.
  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akijitambulisha kwa wakazi wa mji wa Nangukurulu,mara baada ya sherehe fupi za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga kukamilika mkoani Lindi.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mgombea mteule wa Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Marendengo Wilayani Kilwa mkoani Lindi kufungua barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 6.Barabara hiyo imejengwa na Serili ya Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa Mfuko wa Kuwait pamoja na mfuko wa OPEC .
   Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa na  Mkuu wa mkoa wa Lindi,Mh.Mwantumu Mahiza mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Marendengo Wilayani Kilwa mkoani Lindi kushiriki ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 6.Barabara hiyo imejengwa na Serili ya Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa Mfuko wa Kuwait pamoja na mfuko wa OPEC .
   Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa,Mh.Bernad Membe mara baada ya kuwasilia katika kijiji hicho  Marendengo,ambapo sherehe za uzinduzi wa barabara ya Ndundu-Somanga zilifanyika na mgeni Rasmi alikuwa ni Rais Dkt Jakaya Kikwete.

  PICHA NA MICHUZI JR-LINDI- 

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Mkuu wa Magereza Mkoani Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Antonino Kilumbi akiwa ameshika vikombe vya ushindi katika Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Kati kwa Mwaka 2015. Wengine ni Maafisa Washiriki wa Jeshi la Magereza wa Maonesho ya Wakulima ya Nane Nane Kanda ya Kati, Dodoma.

  Jeshi la Magereza nchini limeibuka Mshindi wa kwanza kwa upande wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika Maonesho ya Nane Nane yaliyofanyika katika Kanda ya Kasikazini(Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara), Kanda ya Magharibi(Mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga na Dar es Salaam) pamoja na Kanda ya Magharibi(Mikoa ya Tabora, Kigoma na Shinyanga) ambapo Jeshi la Magereza limeibuka kidedea katika upande wa Uzalishaji Taasisi za Serikali pamoja na Taasisi za Serikali upande wa Teknolojia na Maonesho Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

  Jeshi la Magereza ni Miongoni mwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi likiwa na jukumu lake la kuwahifadhi na kuwarekebisha Wafungwa wa aina mbalimbali wawapo Magerezani ili pindi wamalizapo vifungo vyao waweze kuwa raia wema katika jamii. Pia hushiriki kikamilifu katika Maonesho ya Nane Nane Kitaifa na Kikanda kwa lengo la kutoa elimu kwa umma kupitia shughuli zake mbalimbali za uzalishaji katika Sekta za Kilimo na Mifugo.

  Mbali na ushindi huo wa Kikanda, Jeshi la Magereza limeshiriki kikamilifu katika Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Kitaifa(Maarufu kama Nane Nane) katika Mkoa wa Lindi ambapo Jeshi hilo limeibuka Mshindi wa Pili kwa upande wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama katika Kilele cha Maonesho hayo huku Jeshi la Kujenga Taifa likibuka Mshindi wa Kwanza wa Jumla na Mgeni rasmi katika Kilele cha Maonesho hayo Kitaifa alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

  Kutokana na Ushindi huo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja amewapongeza Maafisa na Askari wote walioshiriki kikamilifu katika Maonesho hayo hadi kufanikisha ushindi huo na amewapa changamoto ya kuongeza bidii zaidi katika utendaji wao wa majukumu ya kazi ili katika Maonesho yajayo waweze kufanya vizuri zaidi.

  Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa Jeshi la Magereza kuibuka Mshindi wa kwanza kwa upande wa Taasisi za Majeshi ya Ulinzi na Usalama katika Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika Kikanda hapa nchini tangu Mwaka 2013.

  Maonesho ya Wakulima Nane Nane Kitaifa yamefunguliwa rasmi Agosti 04, 2015 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Kayanza Pinda ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu ni "Matokeo Makubwa Sasa" - Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Wakulima na Wafugaji.

  Imetolewa na Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje,
  Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
  Agosti 08, 2015.

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na wakulima na wananchi wa  mikoa ya Kanda ya Nyanda za juu kusini wakati akifunga maonesho ya sherehe za wakulima Nanenane katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Agost 8 ,2015b .Picha Jamiimojablog.
  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza katika sherehe hizo za wakulima Nanenaneb Kanda ya Nyanda za juu kusini katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
  wananchi na wakulima wa mikoa ya Kanda ya Nyanda za juu kusini wakimsikiliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda (hayupo pichani)  wakati akifunga maonesho ya sherehe za wakulima Nanenane katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Agost 8 mwaka huu.


  0 0

  Dkt John Pombe Magufuli kwa pamoja akicheza wimbo wa Adinselema uliokuwa ukiimbwa na wanachama hao mara baada ya kumpokea na kuamsha shamra shamra na shangwe za hapa na pale.Pichani kulia ni Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mama Salma Kikwete akishuhudia.
  Mgombea Uraisi wa chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa kwa shangwe na shamra shamra kutoka kwa wanachama na wafuasi wa chama cha CCM waliokuwa wamekusanyika nje ya ofisi za CCM mkoa wa Lindi,alipofika kusaini vitabu,kuwashukuru na kujitamulisha kwao.

  Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mama Salma Kikwete akizungumza jambo na Wanachama wa chama hicho nje ya Ofisi za CCM mkoa wa Lindi
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wanachama wa CCM na wafuasi wa chama hicho waliofika kumlaki alipowasili kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kusaini vitabu pamoja na kuwashukuru na kujitambulisha kwa wanachama hao mapema leo Agosti 8 2015.Dkt Magufuli amewataka wananchama hao kushikamana kuwa wamoja katika kipindi hiki muhimu cha uchaguzi,ambacho anaamini kitaipatia ushindi chama cha CCM.
  Dkt John Pombe Magufuli akitia sahihi vitabu ndani ya ofisi ya CCM mkoa wa Lindi,pichani kati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa,Ndugu Ali Mtopa pamoja na
  Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mama Salma Kikwete.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi,Ndugu Ali Mtopa alipowasili  kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kusaini vitabu pamoja na kuwashukuru na kujitambulisha kwa wanachama na wafuasi wa chama cha CCM mkoani humo mapema leo Agosti 8 2015.

  PICHA NA MICHUZI JR-LINDI

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0


older | 1 | .... | 933 | 934 | (Page 935) | 936 | 937 | .... | 3272 | newer