Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 932 | 933 | (Page 934) | 935 | 936 | .... | 3286 | newer

  0 0
 • 08/07/15--02:27: MSAADA TUTANI
 • Naitwa Ellen Azaria Maduhu, 
  Nimepoteza wallet nyeusi ambayo ilikuwa na vitambulisho vya kazi,  leseni za kuendeshea gari, kadi za benki, health insurance cards na credit cards.

  Naomba kwa ambae ameviokota,  apige simu na 0789223344 au 0753223344 au 0787 636 695.

  ZAWADI ITATOLEWA.

  Natanguliza shukrani zangu za dhati

  0 0

  Wananchi wanaotembelea maonesho ya Kilimo na mifugo Nananane Njiro jijini Arusha wakiwa kwenye banda la Chuo cha Ufundi Arusha kupata maelezo ya namna kinavyotimiza wajibu wake kuelimisha vijana katika taaluma ya ufundi nchini.
  Wanafunzi na wananchi wakipata maelezo kutoka kwa Mkufunzi wa Mitambo,Frank Moshi kwenye banda la Chuo cha Ufundi Arusha(ATC)juu ya matumizi ya nishati ya Nguvu jua.
  ATC pia hutoa mafunzo ya kuongeza thamani madini  hapa nchini badala ya kusafirishwa yakiwa ghafi kwa kuchakata katika mwonekano unaongeza thamani na kuongeza ajira kwa vijana.
  Mkufunzi wa Maabara Lemael Anael wa  ATC akimpa maelezo mmoja wa wananchi waliofika kujifunza,Chuo hicho hutoa mafunzo kwa walimu wa maabara katika Shule za Sekondari nchini katika masomo ya Fizikia,Kemia na Bailojia. 

  0 0

  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake wakati akizindua benki ya maendeleo ya kilimo Tanzania, kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere, jijini Dar es salaam leo.

  0 0

   Mkuu wa Biashara za Kibenki, Rahim Kanjii akipeana mkono na Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Chamanzi, Ancent Shayo  mara baada ya kutoa msaada wa meza 25 na  viti 25.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
   BENKI ya NIC imetoa msaada wa madawati 25 katika shule ya msingi Chamanzi yenye thamani ya Sh.Milioni tatu kutokana na shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya madawati.

  Akizungumza baada ya kukabidhi  madawati  hayo, Mkuu wa Biashara za Kibenki,Rahim Kanjii amesema kuwa shule hiyo waliona ina umhimu wa kusaidiwa sehemu ya madawati katika kupunguza idadi ya wanafunzi wanaokaa chini ardhi wakiwa darasani.

  Amesema shule hiyo inatakiwa kusaidiwa kwa kila hali kwani watoto wanaoandaliwa kuwataifa la kesho hivyo wanatakiwa kuandaliwa mazingira bora ya kupata elimu.

  Kanji amesema kuwa ameguswa sana na benki itaendelea kadri ya uwezo wake kusaidia shule katika kuweza kuondokana na chagamoto ya madawati  katika kujenga mazingira bora ya kusomea watoto kwani wanaandaliwa kuja kuwa wanataaluma mbalimbali.

  Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Ancent Shayo amesema kuwa shule ina wanafunzi 3200 lakini vyumba vya madarasa 11 na kufanya kila darasa kukaa wanafunzi 150.

  Amesema madawati hayo ni kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la nne kutokana na kupungukiwa madwati 175 ambapo NIC imepunguza imetoa madawati 25 hivyo kwa darasa hilo linahitaji madawati 150 ili waweze kukaa katika siku ya mtihani wa taifa.

  Shayo amesesema hitaji katika shule licha ya madawati wanaupungufu wa vyumba vya madarasa  kutokana na idadi ya wanafunzi hao.

   Wanafunzai wa shule ya msingi Chamanzi wakiwa darasani wakiwa wamekaa chini kwa kutokuwa na madawati ya kutosha katika chumba cha darasa la tatu walipotembelewa na wafanyakazi wa Benki ya NIC leo jijini.
  Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Chamanzi, Ancent Shayo akizwa na wafanyakazi wa Benki ya NIC walipowatembelea wanafunzi wa Shule ya Msingi Chamanzi jijini Dar es Salaam walipotembelea chumba cha darasa la kwanza katika shule hiyo. 
   Picha ya pamoja ya wanafunzi wa shule ya msingi Chamanzi na wafanyakazi wa Benki ya NIC baada ya kutoa msaada wa meza 25 na viti 25 vya plastiki katika shule hiyo jijini Dar es Salaam leo.
  Wanafunzi wa shule ya Msingi Chamanzi wakiwa wamekaa kwenye viti na meza walivyopewa msaada na Beni ya NIC jijini Dar es Salaam leo.
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Balozi wa Tanzania, nchini Misri, Balozi Mohammed Hamza, wakati wakitoka kwenye Boti baada ya kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa Mfereji mpya wa Suez Canal, kwa ajili ya meli za mizigo. Hafla hiyo ilifanyika jana Agosti 6, 2015 jijini.
   Picha na OMR

  MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana ameiwakilisha Tanzania katika uzinduzi wa mfereji mpya wa Suez unaounganisha mabara ya Ulaya, Afrika na Asia. Mfereji huu mpya ambao Misri inauita "zawadi mpya kwa Dunia" unalenga kukuza uchumi katika usafiri wa maji na utarahisisha usafirishaji wa mizigo kwa mabara haya matatu, huku Misri ambayo kijiografia iko jangwani ikitegemea kukuza uchumi wake kutokana na meli zitakazopita katika mfereji huo.

  Mradi wa ujenzi wa Mfereji huu mpya umejengwa kwa mwaka mmoja licha ya kupangwa kukamilika baada ya miaka mitatu na umetumia kiasi cha dola za Marekani Bilioni Nane ambazo zimechangwa kwa njia ya Hisa na wananchi wa Misri kwa kipindi kisichozidi siku tisa. Mfereji huu ambao umezinduliwa jana, unatoa fursa kwa Meli kupita bila usumbufu tofauti na zamani ambapo ilipaswa Meli kusimama ili kupishana lakini sasa kila upande wa Meli utapita bila kuathiri upande mwingine.

  Sherehe hizo za aina yake zimehudhuriwa na viongozi kadhaa wa nchi mbalimbali na kupata kuripotiwa na vyombo vyote vikubwa duniani na hivyo kutoa picha ya kuwa Afrika inapiga hatua katika kukuza uchumi wake pamoja na kuonesha dunia kuwa fursa mpya za maendeleo zipo Afrika.

  Sherehe hizo za  aina yake zilipambwa na maonesho ya ndege za kivita zilizotanda anga la Mfereji mpya wa Suez huku zingine zikiruka kwa kasi na kutoa moshi ulioakisi bendera ya Misri, zingine zikipeperusha bendera ya nchi hiyo.

  Katika tukio hilo la kuathimisha tukio hilo la kihistoria   serikali ya Misri ilitangaza kuwa  siku hiyo ni ya mapumziko huku ulinzi mkali ukiimarishwa katika miji yote mikuu ya nchi hiyo huku jiji la Cairo walipofikia  viongozi mbalimbali wa kimataifa likiwa chini ya uangalizi wa kijeshi kwenye maoneo yote muhimu. Barabara ya kwenda eneo la Islamelia zilikofanyika sherehe hizo ilifungwa kwa siku nzima,  walioruhusiwa kupita  ni viongiozi na wageni mbalimbali  waalikwa waliotakiwa kuhudhuria tukio hilo la kihistoria.

   Rais wa Misri Abdel  Fatah  Sisi alisema kufunguliwa kwa Mfereji  ni uthibitisho kwamba Misri inaweza na kueleza kwamba njia hiyo itaimarisha zaidi shughuli za usafirisha na kufungua fursa zaidi kwa mataifa  duniani.

  Katika moja ya matukio ya  uzinduzi huo Rais Fatah na viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo walisafiri katika meli za kifahari huku kiongozi huyo wa Misri akivalia mavazi maalumu ya kijeshi akiwa juu ya sehemu ya uwazi wa meli hiyo pamoja na kijana mdogo mwanafunzi wa miaka tisa aliyevalia kijeshi na kupeperusha bendera ya  Misri kama ishara ya kufunguliwa rasmi kwa mfereji huo.

  Shughuli  ilimazika usiku  kwa  maonesho mbalimbali ya sanaa na utamaduni wa Misri  na kuhudhuriwa na viongozi na wageni wote waalikwa.

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (katikati) akipokea cheti cha ushiriki wa Tanzania kutoka kwa Mmoja wa Washiriki wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma  Barani Afrika Bw. William Budoya yaliyofanyika nchini Congo Brazaville hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Florence Temba (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Aloyce Msigwa (wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. Cosmas Ngangaji (wa pili kutoka kulia).
  Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (wa pili kutoka kushoto) akipokea zawadi ya Tanzania kutoka kwa mmoja wa Washiriki wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika Bw. William Budoya yaliyofanyika nchini Congo Brazaville hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Aloyce Msigwa (kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. Cosmas Ngangaji (wa pili kutoka kulia).
  Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu (katikati) akionyesha cheti cha ushiriki wa Tanzania katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika nchini Congo Brazaville hivi karibuni.  Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Florence Temba (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw.Aloyce Msigwa (wa pili kutoka kushoto),  Mkurugenzi wa Mipango Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. Cosmas Ngangaji (wa pili kutoka kulia)na mmoja wa washiriki wa maonyesho hayo kutoka Wizara ya Uchukuzi Bw. William Budoya (wa kwanza kulia).

  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizindua uvunaji wa matikiti maji kwa wakulima wa shehia ya Donge Muwanda.
   Mkulima wa matikiti maji na pilipili boga Bw. Salum Khamis Kiregu akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais kuhusiana na changamoto zinazowakabili katika kilimo hicho.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa pamoja na badhi ya wakulima wa Donge Mchangani na Muwanda, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “A” (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Affan Othman Maalim (wa pili kushoto). Picha na OMKR.
   
  Na: Hassan Hamad (OMKR)
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesifu juhudi zinazochukuliwa na wananchi wa Donge katika kuendeleza kilimo cha matunda na mboga mboga.

  Amesema iwapo kilimo hicho kitawekeza mikakati imara, kinaweza kuwa mkombozi wa kweli kwa wakulima na kuweza kuweza kuongeza kipato chao.
  Maalim Seif ameeleza hayo wakati akizindua uvunaji wa matikiti maji na pilipili boga katika shehia za Donge mchangani na Muwanda katika Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja.

  Amesema katika siku za hivi karibuni, kilimo hicho kimepata mafanikio makubwa na kupunguza uagiziaji wa bidhaa hizo nje ya Zanzibar kutoka asilimia 80 hadi asilimia 20.

  Amefahamisha kuwa lengo la Serikali ni kuimarisha zaidi kilimo cha matunda na mboga mboga ili kuweza kukidhi soko la ndani na kuacha kuagizia bidhaa hizo kutoka nje ya Zanzibar.
   

  0 0

   Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akizungumza, mmoja waviongozi wa kampuni ya Marmo and Garnito Mines wakati alipokuwa kwenye ziara ya viwanda mkoani mbeya hivi karibuni.
  Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Janet Mbene,akiangalia  baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa na kampuni ya Marmo and Garnito Mines kwa ajili ya matumizi mbalimbali
   Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Janet Mbene, akitembelea sehemu ya kiwanda cha Marmo anda Granito Mines.

  0 0

  Kikosi cha timu ya Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars).

  Kikosi cha timu ya Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kimeodoka leo saa 6 mchana jijini Dar es salaam kuelekea kisiwani Zanzibari, ambapo kitaweka kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) mwezi Septemba.

  Msafara wa Twiga Stars umeondoka na boti ya Azam (Kilimanjaro) ukiwa na watu 32, wakiwemo wachezaji 25, benchi la ufundi 6 pamoja na kiongozi wa msafara, ambapo TFF imegharamia kambi hiyo ya mwezi mmoja

  Wachezaji waliosafiri leo ni Fatuma Omari, Belina Julius, Happiness Hezron, Fatuma Hassan, Anastazia Anthony, Fatuma Bashiru, Fatuma Issa, Fatuma Khatibu, Maimuna Hamis, Donizia Daniel, Sofia Mwasikili, Etoe Mlenzi.

  Wenigine ni Amina Ally, Thereza Yonna, Mwanahamisi Omari, Stumai Abdallah, Shelder Boniface, Asha Rashid, Najiat Abbas, Estha Chabruma, Mwajuma Abdallah na Fatuma Mustapah.

  Twiga Stars itakua kambini kisiwani Zanzibar kwa kipindi cha mwezi mmoja, kujiandaa na fainali hizo za michezo ya afrika, ambapo imepangwa kundi A pamoja na wenyeji Congo – Brazzavile, Ivory Coast na Nigeria.

  Fainali za Michezo ya Afrika  (All Africa Games) zinatarajiwa kuanza kutivua vumbi Septemba 4 – 19 nchini Congo-Brazzavile.

  TOTO AFRICAN KUCHAGUANA OKTOBA 2015
  Klabu ya Toto African ya Mwanza inatarajiwa kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi katika kamati yake ya utendaji ifikapo tarehe 11 Oktoba 2015. Katika barua yake kwa Katibu Mkuu wa Toto African, Katibu Mkuu wa TFF ameuagiza uongozi wa Toto African kuwasiliana na Kamati yao ya Uchaguzi ili tangazo la uchaguzi litolewe si chini ya siku sitini (60) kabla ya tarehe ya kufanyika uchaguzi.

  Kwa muda mrefu kumekuwa na mvutano katika klabu ya Toto na suala kubwa likiwa ni kuhusu ujazaji wa nafasi zilizo wazi. Awali TFF ilipokea maombi ya wanachama na wadau wa Toto African wakitaka ufanyike uchaguzi ili kumaliza mvutano ndani ya klabu.

  TFF ilishauri uchaguzi huo kusubiri klabu kukamilisha mchakato wa usajili.

  Vilevile TFF imewataka wadau wote wa klabu hiyo kongwe ya mjini Mwanza kuheshimu uongozi uliopo madarakani kwani ndio unaotambulika na ndio utaendelea kuiongoza Toto African katika kipindi cha kuelekea uchaguzi uchaguzi.

  NB: Picha za Twiga Stars wakisafiri kuelekea Kisiwani Zanzibar zimeambatanishwa.

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

  Rais wa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' katikati akiwa na mabondia Lulu Kayage kulia na Ramadhani Shauri wakienda kupanda ndege kwenda afrika ya kusini mabondia hawo wanapanda uringoni agost 9.
  Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah Othadhi katikati akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa na mabondia Ramadhan Shauri kushoto na Lulu Kayage kabla awajapaa kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa agost 9.
  Bondia Lulu Kayage.
  Mabondia wakiwa na wadau mbalimbali wa masumbwi kabla ya kupaa kwenda Afrika Kusini kwaajili ya mchezo wao wa Augosti 9.
  Bondia Lulu Kayage kulia  akihakiki nyalaka zake za kusafiria kushoto ni mshauri wake wa karibu Hamisi Berege kutoka kambi ya mchezo wa ngumi Ilala Lulu amenda Afrika ya kusini kwa ajili ya mpambano wake wa Agost 9.
  Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah Othadhi katikati akingia katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa julius nyerere kwa ajili ya safari pamoja na mabondia Lulu Kayage kushoto na Ramadhani Shauri mabondia
  kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa agost 9.
  Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO Yassin Abdallah Othadhi katikati akiwa uwanja wa ndege wa kimataifa na mabondia Ramadhan Shauri kushoto na Lulu Kayage kabla awajapaa kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya mchezo wao utakaopigwa agost 9.
   Picha na SUPER D BOXING NEWS.

  0 0

   Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha kwa wananchi mgombea mwenza Said Miraj (kulia) na mgombea urais wa chama hicho, Zanzibar, Hamad Rashid Hamad  kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Buguruni Sheli Dar es Salaam jana. 
   Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha kwa wananchi mgombea mwenza Said Miraj (kushoto), baada ya kuchukua fomu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dar es Salaam leo. Kulia ni mke wake, Mwanaisha Lutasola.
   Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Hamad Rashid Hamad akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
    Mgombea urais wa Tanzania  kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC),  Lutasola Yemba, akihutubia katika mkutano huo Buguruni Sheli jana.
  Wanachama wa chama hicho na wananchi wakisikiliza sera za viongozi hao watakao peperusha bendera ya ADC kwenye uchaguzi mkuu. 
  (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com.

  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Mb), akiwa ziarani mkoani Mbeya, akizungumza na watendaji wa Mkoa, wa Halmashauri ya jiji, baada ya kuwawajibisha watendaji wawili wa Halmashauri kwa kuwasimamisha kazi na kuwakabidhi kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa tuhuma za kujimilikisha viwanja 25 kinyume na sheria.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Mb), akisisitiza jambo, wakati alipokuwa anatoa maelekezo kwa viongozi wa jiji na Wananchi wa eneo la Sisitira, Lwambi – Mbeya alipokuwa ziarani mkoani humo, Mhe. Lukuvi pia aliwawajibisha watendaji wawili wa Halmashauri kwa kuwasimamisha kazi na kuwakabidhi kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kujimilikisha viwanja 25 kinyume na sheria.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Mb), akikagua mafaili katika masijala ya Idara ya ardhi, halmashauri ya jiji la Mbeya alipokuwa ziarani mkoani humo, Mhe. Lukuvi pia aliwawajibisha watendaji wawili wa Halmashauri kwa kuwasimamisha kazi na kuwakabidhi kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kujimilikisha viwanja 25 kinyume na sheria.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi (Mb), akitoa maelekezo kwa viongozi wa jiji na Wananchi wa eneo la Sisitira, Lwambi – Mbeya, alipokuwa ziarani mkoani humo, Mhe. Lukuvi pia aliwawajibisha watendaji wawili wa Halmashauri kwa kuwasimamisha kazi na kuwakabidhi kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kujimilikisha viwanja 25 kinyume na sheria.

  0 0

   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wa mkoa wa Temeke (NHIF),Constantine Makala akieleza jambo wakati wa kukabidhi mashuka 120 katika hospitali ya Temeke leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk.Edwin Muhondezi.
   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wa mkoa waTemeke (NHIF), Constantine Makala akimuwakilisha kaimu  Mkurungenzi Mkuu wa (NHIF) wa mkoa wa Temeke kumkabidhi msaada wa mashuka 120 Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke Edwin Muhondezi leo Jiji Dar es Salaam.
   Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke,Dk.Edwin Muhondezi akitoa neno la shukarani baada ya hospitali yake kupata msaada wa mashuka 120 kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika hospitalini hapo jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa mkoa wa Temeke (NHIF) wakiwa wameshika shuka ambayo inawasilisha msaada wa shuka 120 zilizotolewa katika hospitali ya Temeke leo jijini Dar es Salaam.
  (picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

  0 0

   Mganga kutoka kitengo cha afya makao makuu ya jeshi la polisi Tanzania, Dk Issa Ndimila akimchukua damu dereva wa magari makubwa, Benedicti Samuel kwa ajili ya kumpima magonjwa katika uzinduzi wa upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro mpango ulioanzishwa na TBL na jeshi la polisi nchini.
   Mganga kutoka kitengo cha afya makao makuu ya jeshi la polisi Tanzania, Dk Issa Ndimila akimchukua damu dereva wa magari makubwa, Kanai John kwa ajili ya kumpima magonjwa katika uzinduzi wa upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro mpango ulioanzishwa na TBL na jeshi la polisi nchini.

   Katibu Tawala wilayaa ya Morogoro, Emmanuel Nzunda akimkabidhi zawadi ya fulana na cheti dereva wa magari makubwa baada ya kupima afya wakati wa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kitucha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro, mpango ulioanzishwa na
  TBL na jeshi la polisi nchini.
   Askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Silve Massawe akijaza taarifa za dereva Edward Sanga baada ya kupima afya katika uzinduzi wa upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro mpango ulioanzishwa na TBL na jeshi la polisi nchini.
  Askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro, Silve Massawe akijaza taarifa za dereva Abdallah Rajabu baada ya kupima afya katika uzinduzi wa upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro mpango ulioanzishwa na TBL na jeshi la polisi nchini.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) mara walipoingia katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo katika kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ya Zanzibar,(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi(kushoto).
  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipokuwa akitoa taarifa ya kikao kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ya Zanzibar kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo kbla ya kukifungua kikao hicho.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akikifungua kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ya Zanzibar leo katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi(kushoto).
  Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ya Zanzibar wakifuatuilia kwa makini ratiba ya kikao hicho kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja.Picha na Ikulu.

  0 0

   Mkurungezi wa Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA, Dk.Ally Simba akizungumza na waandishi wa habari juu ya semina ya kuwapiga brashi wa wasanii wa bongo Movie leo jijini Dar Dar es Salaam.
   Afisa Mwandamizi Mkuu wa Kitengo cha Watumiaji wa Huduma za Bidhaa za Mawasiliano wa TCRA,Thadeo Ringo akizungumza na baadhi na wasanii waliohudhuria semina hiyo hawapo pichani iliyoyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi  Makao Makuu,Kitengo cha Kuzuia Uhalifu ,Kamisheni ya Polisi Jamii,David Mwakalukwa akizungumza na wasaanii juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii katika semina ya wasanii iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
   Msanii Mkongwe wa Filam nchini,Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ akichangia maada katika semina ya kuwanoa wasanii juu ya matumizi ya mitandao katika semina iliyoandaliwa na TCRA leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wasanii walioshiriki semina iliyoandaliwa na TCRA ,leo jijini Dar es Salaam.
  (picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

  0 0

  Meneja Mkuu Shirika la Uendelezaji Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Boniface Njombe (aliyesimama) akielimisha Umma wa Kata ya Swaya wakati walipotembelea eneo la kata hiyo ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya uelimishaji kuhusu manufaa ya Jotoardhi hivi karibuni mkoani Mbeya. Kushoto ni Mkurugenzi wa masuala ya Ufundi wa TGDC, Bwana Karamaeli Mnjokava.
  Mkurugenzi wa masuala ya Ufundi wa TGDC, Bwana Karamaeli Mnjokava.(aliyesimama mbele) akichangia mada kuhusu jotoardhi na manufaa yake kwa wakazi wa Kata ya Swaya hivi karibuni mkoani Mbeya.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  BINTI YETU KWENYE PICHA KWA JINA : NAELIJWA LUTHER KIMBWEREZA (11yrs) wa MOMELA MAJI YA CHAI-ARUSHA. ametoweka nyumbani tangu Jumapili 
  02 Agosti 2015. Alikuwa amevaa shati jeupe na suriali. Tafadhali ukimuona wasiliana nasi
  Tel. 0758335751 /0763066520/0758423766

  0 0

  Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Edgar Senga akieleza uratibu wa shughuli za maafa kwa wananchi waliotembelea Banda hilo katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, Tarehe 7 Agosti , 2015.
  Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wavulana ya Ndada wakipata maelezo juu ya sera baina ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kutoka kwa Mchumi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji , Vedastus Manumbu walipotembelea Banda hilo katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, Tarehe 7 Agosti , 2015.

  0 0

  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati walipokutana Jana, jijini Dar es salaam.
  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwa katika Mazungumzo na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, wakati walipokutana Jana, jijini Dar es salaam.

older | 1 | .... | 932 | 933 | (Page 934) | 935 | 936 | .... | 3286 | newer