Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 920 | 921 | (Page 922) | 923 | 924 | .... | 3284 | newer

  0 0

  Mwanariadha wa Polisi Tanzania Fabian Nelson (kushoto) akishangilia na wanariadha wenzake kutoka Zimbabwer baada ya kuvalishwa medali ya fedha baada ya kushika nafasi ya pili katika mbio za kilomita 10000 katika uwanja wa Mavuso nchini Swaziland wakati wa Michezo ya majeshi ya polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika(SARPCCO) inayoendelea nchini Swaziland.nafasi ya kwanza na ya tatu ilikwenda kwa wanariadha kutoka Jeshi la Polisi la Zimbabwe(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi, Swaziland).
  Mwanariadha wa Polisi Tanzania Fabian Nelson (wa pili) akipambana na wanariadha wengine katika mbio za kilomita 10000 katika uwanja wa Mavuso nchini Swaziland wakati wa Michezo ya majeshi ya polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika(SARPCCO) yanayoendelea nchini Swaziland.Fabian Nelson alishinda medali ya Fedha baada ya kushika nafasi ya pili katika mbio hizo.

  0 0

  NA MWANDISHI WETU

  MAHAKAMA Kuu  ya Tanzania imewataka wananchi  wenye malalamiko kuhusu vitendo vya rushwa  mahakamani kutoa ushirikiano ili kuweza kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.

  Hayo yalisemwa katika taarifa  kwa vyombo vya habari  iliyotolewa leo jijini Dar es salaam  na   Afisa Habari  Mary Gwera wa Mahakama hiyo kufuatia gazeti moja la hapa nchini la Julai 21 mwaka huu  kupitia makala yenye kichwa cha habari  “Mtandao wa rushwa Mahakamani huu hapa” .

  Taarifa hiyo imeeleza kuwa, baada ya kufanya uchunguzi juu ya  kesi  zilizoandikwa katika makala hiyo Mahakama haikuweza kupata maelezo sahihi  kuhusu kesi   mbalimbali  za watu  wenye malalamiko hayo ambao ni Muhidini Nguluma ,Kuruthum Majjid, Abadallah Majata, Halima  Abdan, Claudiana  Mbazigwa Mpondela na  Laizer Kaanan.

  “Ili kuondoa  kero  zilizobainishwa katika gazeti la Mwananchi , mahakama inatoa  rai  kwa gazeti  la Mwananchi  au mtu yoyote  mwenye taarifa sahihi  kuipatia ushirikiano ili kupata namba za simu za kesi zilizolalamikiwa  na mahakama zilikofunguliwa,” ilisema taarifa hiyo.

   Aidha mahakama hiyo imeomba wale wote waliotajwa katika makala hiyo wafike Makao Makuu ya Mahakama, Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Namba 11409 Kivukoni Front waonane na Mkurugenzi Msaidizi wa Malalamiko katika Idara ya Ukaguzi wa Huduma za Mahakama na Maadili ili watatuliwe kero zao.

  Mahakama hiyo inasisitiza kwamba imeweka namba za simu 0752–500 400. mitandao ya kijamii,  WhatsApp, na barua pepe info@judiciary. go.tz) ili wananchi na wadau mbalimbali  waweze kutoa malalamiko yao, maoni na mapendekezo. 

  0 0

  Vyama vya Siasa 21 vinavyotarajiwa kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani baadaye mwaka huu vimesaini Maadili ya uchaguzi yatakayotumika wakati wa kampeni, kupiga kura na wakati wa kutangaza matokeo.

  Maadili hayo yanayohusisha Serikali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Vyama vya Siasa yalisainiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dr. Florence Turuka, Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva na Wawakilishi wa vyama vya Siasa 21 nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume hiyo amesema Chama cha Wananchi (CUF) hakikusaini Maadili hayo kutokana na kuwa na kazi nyingine lakini akasisitiza kuwa Chama hicho kitasaini Maadili hayo wakati wowote.

  Akifafanua kuhusu Maadili hayo, Jaji Lubuva alisema Maadili yanapaswa kuanza kutumika rasmi Agosti 22 mwaka huu wakati kampeni za uchaguzi zitakapoanza, katika kipindi cha kupiga kura na wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo. 

  Alisema Maadili hayo pia yatahusu wajibu wa vyama vya siasa na wagombea na mambo yasiyotakiwa kufanywa na vyama vya siasa na wagombea. 

  Maadili pia yatahusu masuala yanayotakiwa kufanywa na yasiyotakiwa kufanywa wakati wa kupiga kura.Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa maadili yaliyosainiwa pia yatahusu maadili kwa Tume ya Uchaguzi yaani mambo yanayotakiwa na yasiyotakiwa kufanywa na Tume hiyo. 

  Aidha, maadili hayo yatahusu mambo yanayotakiwa na yasiyotakiwa kufanywa na watendaji wa serikali katika kipindi chote cha uchaguzi. 

  0 0


  0 0

  Katibu Mkuu, Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akiwa na Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
  Katibu Mkuu, Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akiwa na Mkuu wa Utawala, Bi Lilian Munanka, ambaye Balozi amemwelezea kama Afisa Mkuu Mwandamizi, mweledi, mchakapakazi, anayejituma na mwajibikaji, mwenyeuzoefu mkubwa na nguzo ya kutegemewa na ambaye amewapokea Mabalozi wengi.
  Katibu Mkuu, Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Liberata Mulamula akiwa na baadhi ya maafisa na wafanyakazi wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa wakiongonzwa na Balozi Ramadhani Mwinyi.

  Katibu Mkuu, Wizara ya  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, amewaaga watanzania waishio nchini  Marekani,  kwa kuwataka kujivunia utanzania wao na kutoionea aibu lugha yao ya taifa,   Kiswahili.

  Mwishoni mwa wiki,   Ubalozi wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania nchini Marekani,  uliandaa hafla ya aina yake  ya  kumpongeza, kumshukuru na kumuaga  Balozi Liberata  Mulamula ambaye sasa ni  Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  Hafla hiyo iliyowajumuisha  watanzania wa kada mbalimbali wakiwamo maafisa na  wafanyakazi wa Uwakilishi wa Kudumu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, wakiongozwa na   Balozi  Ramadhan  Mwinyi,  ilipambazwa kwa nasaha mbalimbali na salamu za kumtakia kheri Balozi Mulamula katika  jukumu lake jipya.


  0 0

  Simba SCAfisa Mtendaji Mkuu wa Eaggroup Iman Kajula Akizungumza wakti wa Kuzindua Mpango wa Kuuza Vifaa vya simba Kupitia Duka la Mtandao akiwa Sambama na Rais wa Simba  Evans Aveva Pamoja na Msemaji wa Simba Sport Club

  Klabu ya Simba kwa kushirikiana na Jumia wamezindua huduma ya kununua jezi za Simba 2015 – 2016 kupitia duka la mtandao la Jumia www.jumia.co.tz . Dhumuni la huduma hii ni kuwapatia wapenzi wa klabu ya Simba njia bora ya kuweza kununua jezi popote walipo Tanzania.
  Kupitia mtandao imara na wenye uzoefu wa Jumia, klabu ya Simba inapanga kuongeza upatikanaji wa vifaa vyake ya michezo nchi nzima. 

  BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

  0 0


  Mbunge wa Ilala mheshimiwa Mussa Zungu leo amefungua mashindano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Dar es Salaam na kuwataka vijana kucheza kwa kujituma ili kuwa wachezaji bora na hatimaye kulinusuru taifa na matokeo mabaya katika medani ya kimataifa.

  Zungu amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kuhakikiha kwamba timu zote za ligi kuu na daraja la kwanza zinakuwa na timu za vijana. “Kwa bahati nzuri, mashindano ya Airtel Rising Stars yamewapa fursa nzuri na ni vema makocha wa ligi kuu wakayatumia kupata vijana wenye vipaji na kuwaendeleza”, alisema.

  Alisema mbali ya kuwa jukwaa la kubaini wachezaji wenye vipaji, Airtel Rising Stars pia yanawahamasisha vijana kushiriki mazoezi hivyo kuwa na afya njema ili kukabiliana na masomo yao.

  Aliwaambia vijana kwamba kwa dunia ya leo mpira ni chanzo cha kutumainiwa cha ajira kwa mamilioni ya vijana ambao wanaishi maisha mazuri kwa kuwa wanalipwa mishahara mizuri.

  Aliwataka viongoizi wa soka kuchagua wachezaji watakaoshiriki fainali za taifa kwa kuzingatia uwezo na siyo upendeleo wa aina yoyote. Wakati mashindano ya mkoa yakiendelea makocha watateua vijana wenye vipaji kuwakilisha mikoa yao kwenye fainali ya taifa.

  Kwa upande wake Rais wa TFF Jamal Malinzi ameishukuru kampuni ya Airtel kwa kubuni programu hii ili kutumika kama jukwaa linatotumika kubaini vipaji vya wanasoka chipukizi. Alisema kuwa mashindano ya Airtel Rising stars yameifanya kazi ya TFF ya kutafuta vipaji vya soka kuwa rahisi zaidi.

  Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi wa IT wa Airtel Tanzania Franky Filman amewashukuru wadau wote wa soka kwa kuyaunga mkono mashindano ya Airtel Rising Stars na kuyapa umuhimu yanaostahili. Pia amewataka makocha kutumia mashindano hayo kuimarisha vikosi vyao.

  Mashindano ya Airtel Rising yanajumuisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke, Ilala Morogoro, Mbeya, Mwanza na Arusha itahitimishwa kwa michuano ya taifa itakayofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 11 hadi 21.

  Mbunge wa Ilala Musa Zungu akisalimiana na wachezaji wakati akifungua rasmi mashindano ya Airtel Rising Stars. Leo Jijini Dar-es-Salaam.
  Mbunge wa Ilala Musa Zungu akiongea na wachezaji wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars Mbeya, Leo jijini Dar-es-Saam.
  Mbunge wa Ilala Musa Zungu akipiga mpira kuashiria ufunguzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars Mbeya, Leo jijini Dar-es-Saam.
  Mkurugenzi wa IT wa Airtel Frank Filman akiongea wakati wa ufunguzi wa mashindano ya Airtel Rising Stars Mbeya, Leo jijini Dar-es-Saam.

  0 0


  Je umekwishawahi kukwama kwenye foleni ukajutia kutobeba gazeti walau likusaidie kusogeza muda mbele? Je umekwisha wahi kutafuta chanzo cha habari za uhakika kwenye simu yako ukakikosa?

  Je umekwishawahi kuambiwa kuna tangazo la kazi au tenda ila ukashindwa kuliona kwa vile lipo kwenye gazeti la siku za nyuma?
  Je umeshawahi kulazimika kuchoma au kutupa magazeti ya siku za nyuma kwa sababu yamejaa sana nyumbani kwako? Au je umeshawahi kuhisi kuna umuhimu wa kuona watoto wako wanachojifunza shuleni?

  Je umekwishaona maktaba inayokupa magazeti, majarida au vitabu vyote toka tulipopata uhuru, mahali popote wakati wowote ulipo?

  Kama jibu la swali lolote kati ya hayo ni ndio, basi M-Paper inaweza kukupa hayo yote.

  Kabla hatujaendelea, tazam video hii ya sekunde thelathini tu  https://www.youtube.com/watch?v=x00FXMqY-jg

  M-Paper ni programu ya simu za mkononi, inayokuletea magazeti, majarida na vitabu vyote kwenye simu yako ya mkononi.  Programu hii ya kipekee itakufanya usome gazeti, jarida au kitabu chote kama kilivyo kwenye makaratasi na si vichwa vya habari pekee.

  Kama hiyo haitoshi, watengenezeji wa programu hii watakupa shilingi 10,000 pale utakapodownload app hii ambayo utaitumia kununua magazeti, vitabu na majarida kabla hujaanza kutumia pesa zako.

  Oh, jambo jingine la kipekee kuhusu program hii ni kuwa, magazeti, majarida na vitabu vyote vinauzwa kwa nusu bei. Faida mara mbili.
  Unaweza kudownload app hii hapa http://www.mpaper.co.tzkisha ukaniandikia maoni yako hapa chini, umeionaje? Kumbuka unadownload BURE, unawekewa 10,000 kwenye akaunti yako hivyo huna cha kupoteza.

  0 0

  Maafisa Vijana Nchini wametakiwa kutumia elimu wanayopata katika kuwaendeleza vijana kiuchumi ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali. 

  Hayo yamesemwa leo Jijini Arusha na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi wakati wa Ufunguzi wa awamu ya kwanza ya mafunzo ya Ujasiriamali na ubunifu.

  Bw. Kajugusi alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa kuwaendeleza vijana nchini Wizara kwa Kushirikiana na Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) wameanzisha mradi unaolenga kuwawezesha vijana kijasiriamali nakiubunifu kwa kupitia mafunzo wanayowapa Maafisa Vijana.

  “tunawaomba kushiriki kikamilifu katika mafunzo haya ya ujasiriamali na ubunifu kwa kuwasikiliza wawezeshaji kwa makini kwa dhumuni la kutumia elimu hiyo kuwainua vijana nchini kiuchumi na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika ujasiriamali”. Alisema Kajugusi.

  Naye Mkurugenzi wa Ujasiriamali na Ubunifu kutoka Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Bw. Leon Malisa alisema kuwa dhumuni la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo Maafisa Vijana katika eneo la  ujasiriamali na ubunifu ili kuwawezesha kuitumia Elimu hiyo kwa vijana vijana nchini kwa kuwawezesha kujiajiri wenyewe.

  Aidha Bw. Malisa ametaka vijana nchini kuunda vikundi na kubuni miradi itakayowaendeleza ili Wizara kwa kushirikiana na ESAMI waweze kuwasaidia kujiendeleza ikiwa ni njia moja wapo ya kukabiliana na tatizo la Ajira Nchini.

  Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo Afisa Vijana toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Eliackim Mtawa alisema kuwa watatumia mafunzo haya kuwatayarisha vijana kuwa wajasiriamali wazuri na kuwasimamia katika utekelezaji wa Miradi hiyo ili kuwawezesha kushiriki katika uzalishaji mali na kukuza uchumi kupitia ujasiriamali.

  Mafuzno hayo ya Ujasiriamali na Ubunifu yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI)
  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi akiongea na Maafisa Vijana waliohudhuria Mfunzo ya Ujasiriamali na Ubunifu kutumia elimu na uzoefu watakaoupata katika mafunzo hayo kuwainua vijana kiuchumi kwa kutoa elimu itakayowajenga na kuwafanya vijana kujitegemea na kuwa wajasiriamali, wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi wa Ujasiriamali na Ubunifu kutoka Chuo cha Uongozi cha ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute) Bw. Leon Malisa.
  Baadhi ya Maafisa Vijana wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo.


  0 0

  africapractice, a strategic advisory and communications consultancy that advises clients on identifying opportunity, managing risk and overcoming communications challenges, has announced the appointment of Jeff Aludo as the new Managing Director for East Africa.

  ​A former ​Director​ ​of​​  Strategy and Operations practice​ ​at top consultancies such as Deloitte and PwC where he ​ has advised senior executives across the world on major strategic, commercial and regulatory decisions and led hundreds of projects, his appointment is in line with africapractice's new growth and market positioning as a leading market entry risks an​d strategy ​advisory firm in East Africa, ​

  ​Jeff Aludo's appointment is preceded by the firm’s new partnership with Alkebulan, a firm that identifies liquid structured credit opportunities in Sub-Saharan Africa. The partnership will help africapractice further improve perceptions of Africa and client’s operating environment in multi-asset deal and project structuring and commercial risk analysis.

  africapractice
  ​ has been operating in Tanzania for the past five years and provides advisory services to firms in the extractives, agriculture, infrastructure, and corporate sectors.

  Jeff who holds an MBA in strategic management
  ​ ​is a seasoned, strategic and results focused leader who will drive the firm’s new prospects in East Africa forward, while ensuring that africapractice continues to provide high impact and high value intelligence, analysis and engagement solutions to clients.

  0 0

  Fatilia Mkutano wa Mh. Edward Lowassa leo Jumanne tar 28/07/2015, kuanzia saa 9 alasiri kwa saa za Afika Mashariki. itakuwa live kupitia hapa http://live.wogmedia.co.tz/channel/view/karibu-1

  0 0

   .Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Tabata ya jijini Dar es Salaam,Tumaini Kabuta akikabidhiwa msaada wa madawati 100 na Meneja Biashara wa Benki ya KCB Tanzania, Tawi la Mlimani City, Benjamin Mgonja(kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo.Benki hiyo imetoa msaada wa matawati 1000 kwa shule kumi za jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi Tabata.Wakati wa hafla ya  kukabidhiwa msaada wa madawati 100 na Benki hiyo jana.


  0 0

   Mwenyekiti wa QAML Mwenyekiti,Yusuf Manji wa kwanza kulia, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa  Kampuni ya magari ya General Motors East Africa (GMEA) Limited,Mario Spangenberg wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Isuzu uzinduzi huo uliofanyika jiji Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya General motors (GMEA) Bi. Rita Kavashe  akisaini makubaliano ya kibiashara na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Quality automotive Vinay Upadhyay.

   Mkurugenzi mtendaji wa GMEA Rita Kavashe alisema Kampuni ya General motors kuingia katika soko la Tanzania ilikuwa ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu katika kampuni hiyo ili kuimarisha uwepo wake Afrika Mashariki. Kulia ni Rais na Mkurungenzi Mtendaji wa (GM) Africa  Mario Spangenberg.


  0 0

  Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimkabidhi kadi ya uanachama wa chama hicho,Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa leo katika hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
   Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akizungumza na mamia wakati wa kutangaza adhima yake ya kujiunga na Chadema katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
   Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya kujunga kwake katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
   Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa (mwenye umvi) akiwa na viongozi wa UKAWA katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akimpa kadi ya uanachama Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu,Regina Lowassa leo katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
   Mh.Lowassa akiingia kwenye Hoteli Bahari Beach  kwa ajili ya kutangaza adhima yake ya kujiunga na UKAWA. Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa ametangaza kujiunga rasmi na Umoja wa Katiba (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) .
  .
   Mh.Edward Lowassa akiwa katika hadhara ya mamia kujibu maswali katika Hoteli ya Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.
   Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli akiingia kwenye ukumbi wa mikutano ndani ya hotel ya Bahari Beach jijini Dar,kwenye mkutano wa Wanahabari jioni ya leo.
   Mh.Lowassa akiwa na viongozi wa UKAWA  katika Hoteli ya Bahari Beach Hoteli jijini Dar es Salaam jioni ya leo mara baada ya kutangaza rasmi azma yake ya kujiunga na ukawa.
   Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika Hoteli ya Bahari Beach Jijini Dar es Salaam jioni hii alipokuwa akitangaza azma yake ya kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA.
  Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba  katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

  0 0

   KLABU ya Simba kwa kushirikiana na Kampuni ya kuuza vitu kwa njia ya Mtandao ‘Jumia’ wamezindua huduma ya kununua jezi za Simba 2015-2016 ‘Jumia – Simba Online Shop’ kupitia katika duka la mtandao la Jumia Iiitwayo la www.jumia.co.tz.
  Akizungumza jijini Dar es Salaam, Rais wa Simba, Evans Aveva, alisema dhumuni la huduma hiyo ni kuwapatia wapenzi wa klabu ya Simba njia bora ya kuweza kununua jezi popote walipo nchini.
  Aveva alisema klabu ya Simba inapanga kuongeza upatikanaji wa vifaa vyake vya michezo nchi nzima, hivyo mkataba huo abu ya Simba inapanga kuongeza upatikanaji wa vifaa vyake vya michezo nchi nzima, hivyo mkataba huo utaongeza usaambazaji wa vifaa vya michezo vya klabu hiyo.

  “Klabu ya Simba inafahamu umuhimu wa kuvifanya vifaa vyake vya michezo kuweza kupatikana kiurahisi kwa wateja wake, hivyo leo tunajivunia kuzindua huduma hii kwa ajili ya kutumia mtandao wa Jumia kuwezesha wapenzi wa Simba popote walipo kuweza kununua mavazi na bidhaa za Simba kiurahisi na kwa bei nafuu” alisema Aveva. 

  Meneja wa Jumia nchini Tanzania Jean –Philippe Boul alisema uzinduzi wa jezi za mpira wa miguu siku zote ni tukio muhimu kwenye maisha ya klabu maarufu na inayopendwa kama Simba.

  Alisema katika msimu wa 2015 – 2016 klabu ya Simba imeamua kuwa wabunifu kwa kutoa fursa kwa wapenzi wake kununua jezi za msimu huo, kupitia njia ya mtandao hivyo wanajivunia kwa Aveva kuwachagua wao kwa kazi hiyo.

  “Kupitia huu umoja wetu wa Simba na Jumia tumeamua kutoa ofa kwa wanachama na wapenzi wa Simba kuagiza jezi kuanzia leo(jana) mpaka Alhamisi Julai 31 kupitia www.jumia.co.tz kabla ya kuanza rasmi kwa mauzo ya kimtandao kupitia Jumia na kuanzwa kuuzwa rasmi kwa rejareja”. 


  “Tunawahamasisha wapenzi wa Simba popote walipo Tanzania kuagiza jezi kupitia mtandao huu, kuona urahisi katika kufanya manunuzi. Popote walipo wapenzi wa Simba wanaweza kuagiza jezi kupitia tovuti ya jumia na kuletewa mzigo wako mpaka mlangoni. 


  Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EAGgroup Limited, Imani Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya kibiashara wa klabu ya Simba alisema “kwa mapinduzi haya makubwa yataiwezesha klabu ya Simba kuongeza mapato yake pia kudhibiti bidhaa feki,”.


  0 0

  Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akipokea maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) kutoka kwa Ofisa wa HESLB Bi. Veneranda Malima katika maonesho ya vyuo vikuu yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Ofisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa ELimu ya Juu (HESLB) Bw. Saleko Mandara (kushoto) akimwelekeza namna ya kujaza fomu ya kurejesha mkopo Bw. Suleiman Zidi Hisabu ambaye ni mwajiriwa wa Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait Zanzibar na mnufaika wa mkopo aliopewa na HESLB. Bw. Hisabu alitembelea banda la HESLB katika maonesho ya vyuo vikuu yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Elimu ya Juu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sylvia Temu akimkabidhi Ofisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bi. Veneranda Malima cheti cha ushiriki katika maonesho ya vyuo vikuu yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Ofisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa ELimu ya Juu (HESLB) Bi. Joyce Mgaya (kulia) akijibu maswali ya Bi. Dorah Kusiri, mkazi wa jijini Dar es Salaam kuhusu huduma za HESLB. Bi. Kusiri alitembelea banda la HESLB katika maonesho ya vyuo vikuu yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
  Ofisa wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa ELimu ya Juu (HESLB) Bi. Joyce Mgaya (kulia) akimwelekeza Bw. Sheha Semtawa (aliyekaa) namna ya kujaza fomu ya kuomba mkopo kwa njia ya mtandao. Bw. Semtawa alitembelea banda la alitembelea banda la HESLB katika maonesho ya vyuo vikuu yaliyomalizika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Mwisho wa kuwasilisha maombi ya mkopo ni Julai 31, 2015. (Picha na HESLB).

  0 0

  Mkurugenzi wa Taasisi ya Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki na Kusinin(ESAURP) Prof,Ted Maliyamkono akzungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wajasiliamali  wadogo wa mkoa wa Kilimanjaro yanayofanyika katika chuo cha VETA Moshi.
  Mjumbe wa  Bodi ya Taasisi ya fedha ya FSDT ,Erick Masinda akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
  Baadhi ya wajasiliamali hao.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015) inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa michezo miwili kuchezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku macho na masikio yakiwa kwenye mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.
  Mechi hiyo ya pili inatarajiwa kuanza saa 10:15 jioni inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvute kufuatia timu hizo mbili zinatotokea jijini Dar es salaam kuwa na upinzani mkali kuanzia katika Ligi Kuu a Vodacom Tanzania na michuano mingine.

  Kocha mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amesema hana cha kuogopa katika mchezo huo dhidi ya Yanga, vijana wake amewandaa kupambana katika hatua hiyo ya robo fainali na ana imani wataibuka na ushindi.

  Stewart ameongeza kuwa ana wigo mpana wa kikosi chake, katika hatua ya makundi wameweza kushinda michezo yao yote mitatu na kufunga mabao 8, huku ukuta wake ukiwa haujaruhusu bao hata moja kuingia wavuni kwake.

  Kwa upande wa Yanga, kocha Hans Van der Pluijm amesema naaiheshimu klabu ya Azam, na katika mchezo wa kesho hana cha kupoteza, kikosi chake kimemalilika kila idara kuelekea katika hatua ya robo fainali.

  Hans anajivunia kikosi chake ambacho kimeonyesha mabadiliko makubwa kutoka mchezo wake wa awali iliyoupoteza, na kushinda michezo mitatu mfululizo iliyofuatia katika hatua ya makundi.

  Mchezo wa kwanza wa robo fainali utazikutanisha timu za KCCA ya Uganda dhidi ya Al Shandy ya Sudan, mechi itakayoanza saa 7:45 mchana uwnaja wa Taifa jijini Dar es aalaam.

  Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB nchini Tanzania Ineke Bussemaker anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa robo fainali kesho kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.

  0 0

  Rais Mstaafu Alhaj Dkt Ali Hassan Mwinyi alizuru Jamhuri ya Watu wa China kufuatia mualiko uliomhitaji ashiriki na kutoa hotuba katika ufunguzi wa mkutano wa kuadhimisha miaka sabini ya kuundwa kwa Umoja wa Mataifa tarehe 20 Julai 2015. 

  Katika ziara hiyo, Rais Mwinyi pia alipata fursa ya kutembelea Ubalozi wetu na kupata chakula kilichoandaliwa na Balozi wa Tanzania nchini China, Jenerali (Mstaafu) AbdulRahman Shimbo pamoja na Mama Shimbo.
  Rais Mstaafu Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi na wadau wengine wakiwa ziarani Guangdong

  Rais Mwinyi pia alipata fursa ya kuzuru maeneo mbalimbali jijini Beijing pamoja na Zhuhai na Guangzhou katika jimbo la Guangdong. Katika ziara hiyo, Mwinyi alikutana na viongozi waandamizi katika maeneo yote aliyotembelea katika ziara yake na pia alipata fursa ya kutembelea Mamlaka inayosimamia ujenzi wa daraja la Hongkong – Zhuhai – Macau miongoni mwa maeneo mengine. 

  Daraja la Hongkong – Zhuahi – Macau litakuwa na urefu wa zaidi ya kilomita hamsini na linavuka bahari kuunganisha Bara ya China na visiwa vya HongKong na Macau halitokuwa kivutio tu, bali linaonesha umahiri wa watu wa China katika fani za ubunifu na uhandisi.
  Rais Mstaafu Mwinyi akisaini kitabu cha wageni cha makumbusho ya mipango miji jijini Beijing.

  Rais Mwinyi aliondoka China kurudi nyumbani usiku wa tarehe 26 mwezi Julai 2015 akiwa ameambatana na Mama Sitti Mwinyi. Ziara hii ya Rais Mwinyi ni ishara kuwa mataifa haya marafiki (China na Tanzania) yanaendelea kuuthamini urafiki wao usio wa msimu na kuwa uhusiano huo utadumishwa ili uwe urithi wa vizazi vijavyo na wao wauendeleze. 

  Tanzania na China wana uhusiano wa miongo mingi ambapo China ilivutiwa na kujenga reli ya TAZARA – reli ya pekee iliyojengwa Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.

  Imetolewa na Ofisi ya Rais Mstaafu Dkt Ali Hassan Mwinyi

  0 0

  WASANII nchini wametakiwa kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba katika mifuko mbalimbali ya jamii kwa kuwa kufanya hivyo kuna kumuhimu mkubwa katika maisha yao baada kuwa wamestaafu kazi zao au wanapokuwa hawana tena uwezo wa kufanya kazi.

  Hayo yalisemwa na msanii mkongwe wa maigizo hapa nchini Bakari Mbelemba maarufu kwa jina la Mzee Jangala wakati akizungumza katika Jukwaa la na Sanaa lililofanyika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) mwanzoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam.

  Mzee Jangala alikuwa akijibu hoja iliyotolewa na msanii Christian Kauzeni ambaye alitaka kujua ni kwa nini wasanii wakongwe wengi wanakuwa na maisha magumu licha ya kuwa walifanya kazi nzuri zilizo wahengea umaarufu mkubwa hapa nchini.

  Alisema wasanii wengi wakonge hawakuwa na utaratibu wa kuweka akiba, lakini kwa sasa kuna mifuko mingi na mifumo mingi ya kujiwekea akiba hivyo ni muhimu kwa sanii kujiwekea akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

  Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza alisema huu si wakati wa msanii kupata shida baada ya kustaafu au kuzeeka kwa kuwa kuna mifuko mingi ya kuweka akiba na hata ya huduma za afya ambayo kwa mchango kidogo inatoa unafuu mkubwa wahuduma.

  “Haipendezi kwa msanii aliyekuwa na jina kubwa au umaarufu katika nchi anapokuwa amepatwa na maradhi kusubili harambee ipite ili apate matibabu, msanii akijiunga na mfumo wa bima ya Afya kwa mfano NHIF analipa fedha kidogo sana na anapata uhakika wa matibabu kwa muda mrefu wa maisha yake,” alisema Mngereza.

older | 1 | .... | 920 | 921 | (Page 922) | 923 | 924 | .... | 3284 | newer