Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

JOTO LA ASUBUHI LA 93.7 EFM JUMATANO KUANZIA SAA 12


TTCL YASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA WADAU WA MAWASILIANO

0
0
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na tekinolojia, Selina Lyimo akimkabidhi cheti cha shukrani, Mkuu wa Idara ya Mkongo wa Taifa, wa Kampuni ya TTCL, Adin Mgendi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa ya siku mbili ya wadau wa mawasiliano wa mkongo huo iliyoanza jijini Dar es Salaam Julai 28, 2015.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na tekinolojia, Selina Lyimo akimkabidhi cheti cha shukrani, Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Huwawei, Jimmy Liguo Jin wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa ya siku mbili ya wadau wa mawasiliano wa mkongo Taifa iliyoanza jijini Dar es Salaam.
Adin Mgendi akonesha ramani ya mtandao wa Mkongo wa Taifa wakati wa mkutano jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Extensia, Tariq Malik (katikati) akifrahia jambo na wadau mbalimbali wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Kulia ni Naibu Waziri wa ICT, Postali na Huduma Uchukuzi wa Zimbabwe, Win Mlambo na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, Selina Lyimo.

Wafanyakazi wa Hospitali ya wanawake na watoto ya Centenary ya mjini Canberra wameonyesha nia ya kufanya kazi nchini Tanzania

0
0
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mama Elizabeth Chatham, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Caniberra nchini Australia inayotoa huduma ya Afya ya Mama, vijana na watoto mara baada ya kufika eneo la hospitali kwa madhumuni ya kujionea namna bora yautoaji huduma.  Mama Salma yupo nchini Australia akifuatana na mumewe Rais Jakaya Kikwete kwenye ziara rasmi ya kiserikali nchni humo.
Mke wa Rais na Mama Salma Kikwete na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CaniberraMama Elizabeth Chatham wakibadilishana mawazo wakati walipokuwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma ya mama, vijana na watoto.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaangalia baadhi ya watoto wanapatiwa huduma ya matibabu katika hospitali ya Caniberra wakijishughulisha na michezo mbalimbali wakiwa na wazazi wao.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Na Mwandishi wetu – Canberra, Australia 

Wafanyakazi wa Hospitali ya wanawake na watoto ya Centenary ya  mjini Canberra wameonyesha nia ya kufanya kazi nchini Tanzania ili kumuunga mkono Mke wa Rais Mhe. Mama Salma Kikwete katika juhudi zake za kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia afya za wanawake, vijana na watoto wa Hospitali hiyo Liz Chatham wakati akiongea na Mhe. Mama Kikwete na ujumbe wake walipotembelea Hospitali hiyo.
Liz  alimshukuru Mama Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) kwa kutembelea Hospitali hiyo na kujioneka kazi wanazozifanya pia alimpongeza kwa juhudi zake anazozifanya za kuhakikisha wanawake na watoto wa Tanzania wanapata huduma bora ya afya.

Mkurugenzi huyo alisema katika Hospitali hiyo wafanyakazi wengi  wa sekta ya afya wanapenda kwenda kufanya kazi Tanzania  ili waweze kutoa huduma ya afya kwa ajili ya mama na mtoto pamoja na watu wengine  na kubadilishana ujuzi wa kazi na wenzao.

Kwa upande wake Mhe. Mama Kikwete alisema  ni jambo la kufurahisha kuona katika Hospitali hiyo wanawake wenye afya njema wanajifungua katika mazingira mazuri na watoto ambao ni wagonjwa wanapewa matibabu na  uangalizi wa hali ya juu.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuwahudumia kinamama wajawazito na watoto, kujifungua iwe sababu ya kuwa na  furaha na kusherehekea lakini siyo tofauti na hapo, nasema hivi kutokana na mazingira halisi ya kule ninakotoka”.

Pamoja na kuwa jitihada za makusudi zinafanywa na Serikali bado wanawake na watoto wanapoteza maisha wakati wa kujifungua kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika”, alisema Mama Kikwete.

Akiwa katika Hospitali hiyo Mama Kikwete alipata nafasi ya kuongea na watoto ambao ni wagonjwa  ambao kwa wakati huo walikuwa darasani wanasoma na aliwaona  na kuwajulia hali wazazi waliojifungua Hospitalini hapo.

Utaratibu wa Hospitali ya wanawake na watoto ya Centenary mtoto akiwa amelazwa kipindi ambacho shule hazijafungwa anafundishwa masomo ambayo wenzake wanafundishwa darasani kwani Hospitalini hapo kuna madarasa na walimu wanaofundisha watoto wagonjwa.

Mama Kikwete ameambatana na mmewe Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete nchini Australia kwa ajili ya ziara rasmi ya Kiserikali ya siku nne.

DIRA YA DUNIA YA BBC SWAHILI, LONDON

TASWIRAZ KUTOKA MJINI BUKOBA LEO

0
0
Mji wa Bukoba na kwa mbali ni Kisiwa cha Msila mojawapo ya kivutio na kielelezo cha Mji wa Bukoba. Picha zote na Faustine Ruta/Bukoba
Sehemu ya Bandari ya Bukoba

Mahojiano na Balozi Amina Salum Ali kwenye kipindi cha JUKWAA LANGU

0
0
Mhe. Balozi Amina Salum Ali akifafanua jambo ndani ya Kilimanjaro Studio
Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Katika kipindi hiki utasikia mahojiano yetu na watu mbalimbali kuhusu DEMOKRASIA kuelekea uchaguzi nchini Tanzania
Katika kipindi cha wiki hii tumebahatika kuungana na Balozi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali
Karibu

Mradi mkubwa wa kuinua vijana kiuchumi nchini waja

WAGOMBEA UBUNGE CCM WAKAMILISHA KAMPENI ZAO KATIKA KATA 25 JIJINI ARUSHA

0
0
SAM_4554Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju ambaye ni mtia nia ubunge wa jimbo la Arusha kwa tiketi ya CCM akinadi sera zake mbele yawananchi na wanachama wa chama hicho katika kata ya Themi viwanja vya Trans Foma jijini Arusha katika mkutano wa wagombea 12 wa chama cha mapinduzi ,kuomba kura katika kata 25 ambapo katika kura ya maoni atapatikana mmoja wa kupeperusha bendera ya CCM Arusha mjini(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_4518Kijana aliyejitokeza kusikiliza sera za wagombea 12 wa CCM akisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi wa Bushback Safaris Mustafa Panju akimwaga sera zake kwa wananchi wa kata ya Themi viwanja vya Trans Foma jijini Arusha
SAM_4552Wananchi  na wananchama waliojitokeza kuwasikiliza wagombea Ubunge jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi
SAM_4512Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Monaban yajijini Arusha,Philemon Mollel ambaye pia ni Mgombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM akimwaga sera zake kwa wananchi na wanachama wa chama hicho kuomba ridhaa ya kuwatumikia katika nafasi ya Ubunge.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA AUSTRALIA NA GAVANA MKUU WA NCHI HIYO

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai 2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo rasmi na Waziri Mkuu wa Australia Mhe. Tonny Abbot asubuhi ya tarehe 28 Julai 2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la lililoandaliwa kwa heshima yake huku akipigiwa mizinga 21 alipowasili asubuhi ya tarehe 28 Julai 2015 katika makao Makuu ya kiongozi huyo jijini Sydney.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

SIMU TV: MAPITIO YA MAGAZETI

0
0

SIMUtv: Lowassa mazima mazima UKAWA. Aingia kwa mbwembwe na kupokelewa kwa shangwe. Tazama Magazeti yalivyoandika. https://youtu.be/RZUtLRHWHDY
SIMUtv: Je wajua nini kimejiri katika habari za Magazeti ya Leo baada ya Lowassa kujiunga CHADEMA? Tazama hapa. https://youtu.be/07JFxNMOEV0
SIMUtv: Lowassa azamia CCM na kuibukia UKAWA. Je hayo ndiyo maamuzi magumu? Jibu hili hapa katika Magazeti ya Leo. https://youtu.be/G5Z5ne8np2c
SIMUtv: Tazama uchambuzi wa habari za Michezo zilizojiri Kitaifa na Kimataifa katika Magazeti ya Leo July 29 2015. https://youtu.be/foWkTR-X8FE
SIMUtv: Watu wanne wafariki na wengine watano kujeruhiwa katika ajari iliyotokea huko Kagera baada ya basi la abiria kugongana na Cruiser.    http://youtu.be/wWk60vR57pU
SIMUtv:  Aliekuwa Waziri Mkuu Mh Edward Lowassa ajiunga rasmi na Ukawa kupitia Chadema na kusema safari ya matumaini inaendelea.     http://youtu.be/3iVcnkGCJ6U

Airtel Yatangaza Washindi wa Draw ya Pili ya Promosheni ya “Jiongeze na Mshiko”

0
0
Afisa Uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kati) akiongea na mshindi aliyepatikana wakati wa kuchezesha droo ya pili ya wiki ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel kutoka mikoa ya Musoma na Tabora walipatikana akichukua taarifa za mshindi (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Humudi Abdul Hussein na Afisa huduma za ziada Airtel bwana Fabian Felician. Droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya Airtel Moroco jijini Dar es saalam, Jumanne 28 Julai 2015, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imechezesha droo ya pili ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" nakutangaza washindi wawili wa pili wa wiki waliojishindia kila mmoja pesa taslimu.
Afisa Uhusiano na matukio wa wa Airtel, Dangio Kaniki (kati) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika droo ya pili ya wiki ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" ambapo wateja wawili wa Airtel kutoka mikoa ya Musoma na Tabora walipatikana akisikiliza (kushoto) ni mkaguzi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Humudi Abdul Hussein na Afisa huduma za ziada Airtel bwana Fabian Felician. Droo hii imechezwa jana katika makao makuu ya Airtel Moroco jijini Dar es saalam, Jumanne 28 Julai 2015, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imechezesha droo ya pili ya promosheni ya "Jiongeze na Mshiko" nakutangaza washindi wawili wa pili wa wiki waliojishindia kila mmoja pesa taslimu.

Airtel Tanzania leo imefanya droo yake ya Pili kwa wateja wake katika kampeni ijulikanayo kama “Jiongeze na Mshiko”. Kampeni hii ilianza rasmi tarehe 13 July 2015 na itaendelea hadi tarehe 10 Novemba 2015

Akiongea na waandishi wa habari Afisa Uhusiano wa Airtel, Dangio Kaniki amesema; “kila wiki, droo hii itawapatia wateja wawili nafasi ya kujishindia hadi shilingi milioni tatu za kitanzania, mmoja shillingi milioni moja kila wiki na mwingine milioni tatu kila wiki.

Kwa wale watakaoingia katika droo ya milioni moja watajiunga na kushiriki bure na kupata nafasi ya kujishindia shilingi milioni moja kila wiki na mwishoni mwa droo hii kuweza kujishindia shilling milioni 2. Na kwa wale washindi wa wa milioni tatu, mteja anaweza kuamua kuingia na kushiriki kwa tozo ya shilingi 300 kwa siku na mwisho wa promosheni mteja ataweza kujishindia milioni 50.

Akitangaza washindi Dangio alisema" Leo tumechezesha droo ya wiki ya
pili tangu kuzinduliwa kwa promosheni ya ”Jiongeze na Mshiko" wiki
mbili zilizopita. Ninayo furaha kutangaza washindi hao ambao ni 
Gabriel Fernandis(18) mwanafunzi na mkazi wa wa Mkoa wa Musoma Mara yeye amejishindi shilingi milioni 1 , na  mshindi wa pili ni Hamis Rashid(52)na mkazi wa mkoa waTabora Sikinge yeye amejishindi shilingi milioni 3.

“Ushiriki upo wazi kwa wateja wote wa malipo ya awali. Wanachotakiwa kufanya ni kujiunga na promosheni hii  kwa kutuma ujumbe wenye neno “BURE” kwenda namba 15470, na kisha kuanza kupokea maswali kwenye simu zao na kujibu maswali bure bila gharama yoyote na kujikusanyia pointi.

TANESCO IMEPATA MAFANIKIO MAKUBWA YA UTOAJI WA HUDUMA YA UMEME NCHINI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA 10 -MHANDISI MRAMBA

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme (Tanesco),Mhandisi Felchesmi Mramba akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio ya miaka 10 ya shirika hilo katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waandishi wa habari wakifatilia taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco,hayupo pichani katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

SHIRIKA la Umeme (Tanesco) limesema kuwa limepata mafanikio katika kipindi cha miaka 10 na kuwa  ziada ya umeme kutokana na utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Mhandisi Felchesmi Mramba amesema kuwa walipoanza 2004 walikuwa na Megawati 891 na kufikia 2014 wamekuwa na Megawati 1501.

Amesema mahitaji ya umeme kwa sasa nchini ni Megawati 934 hali hiyo inaonyesha kuwa kutokana na miradi mbalimbali kutakuwa na ziada kubwa ya umeme na kuongeza uchumi katika nyanja mbalimbali.

Mramba amesema kuwa hivi karibuni wataunganisha Megawati 150 za Kinyerezi namba moja katika Gridi ya Taifa na  katika kuunganisha huko kutakuwa na tatizo la umeme katika maeneo mbalimbali.

 Amesema tatizo la umeme la kuunganisha litafanyika usiku Agosti 31 na wananchi wametakiwa kununua umeme katika siku mbili hizi ili waweze kuondokana na tatizo la umeme na hakuna manunuzi yatakafanyika kwa Agosti 1 mwaka huu.

Amesema  kuna mazungumzo na Serikali ya China katika mradi wa umeme wa Kilowati 400 kwa Chalinze pamoja na kilowati 400 zingine kutoka Chalinze hadi Segera mkoani Tanga. 

MICHEZO YA MAJESHI YA POLISI YAENDELEA NCHINI SWAZILAND

0
0
Mshindi wa kwanza katika mbio za Kilomita 21, Josepat Joshua (katikati) na wa pili Osward Revelian kutoka Jeshi la Polisi Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa baada ya kukabidhiwa medali zao katika uwanja wa Mavuso mjini Mbabane Swaziland katika michezo ya majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika(SARPCCO) inayoendelea nchini Swaziland.
Mchezaji wa Polisi Tanzania, Mohamed Ibrahim kutoka Jeshi la Polisi Tanzania akirusha tufe katika uwanja wa Mavuso mjini Mbabane Swaziland katika michezo ya majeshi ya Polisi kwa nchi za Kusini mwa Afrika(SARPCCO) inayoendelea nchini Swaziland.Mohamed alichukua nafasi ya tatu katika mchezo wa kisahani na hivyo kufanikiwa kupata medali ya shaba.(Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi-Swaziland).

BENKI YA EXIM YAKABIDHI ZAWADI KWA MSHINDI WA DROO YA KWANZA YA KAMPENI YA AKAUNTI YA MALENGO

0
0
Meneja wa benki ya Exim tawi la Exim Tower, Bi. Rose Kanijo (kushoto), akikabidhi zawadi ya iPhone 6 kwa mshindi wa droo  ya kwanza ya kampeni ya Akaunti ya Malengo inayoendeshwa na benki hiyo, Bw, Prabhjot Singh, mkazi wa Dar es Salaam katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika makao makuu ya benki ya Exim jijini Dar es Salaam jana. Kampeni hiyo inayoendelea kwa miezi mitano zaidi, inalenga kuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba miongoni mwa Watanzania.

Serikali yahimiza unyonyeshwaji wa watoto

0
0
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Dkt. Neema Rusibamayila toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji inayotarajiwa kuanza Agosti Mosi hadi Saba ambapo kitaifa itafanyika mkoani Dodoma.

Na. Eliphace Marwa – Maelezo.

Katika kuzingatia na kuboresha afya ya mtoto, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeendelea kuwahimiza wanawake kuzingatia utunzaji na ustawishaji wa watoto kwa kuwapa haki ya kunyonya maziwa ya mama.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Dkt. Neema Rusibamayila amesema wakati Tanzania inategemea kuungana na mataifa mengine duniani ni vema jamii ikatambua umuhimu wa lishe kwa mtoto.

“Jamii inapaswa kutambua umuhimu wa unyonyeshaji maziwa ya mama pekee katika miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto na kuendelea kunyonyeshwa mpaka umri wa miaka miwili au zaidi” alisema Dkt. Neema.

Kwa upande wa mtoto, Dkt. Neema alisema maziwa hayo yana faida nyingi ikiwemo kumpatia virutubisho vyote anavyohitaji kwa uwiano sahihi kwa afya na ustawi kwani viini vya kingamwili vinavyofanya kazi kama chanjo dhidi ya maradhi humeng’enywa na kufyonzwa kirahisi zaidi mwilini tofauti na vyakula vingine.

Aidha aliongeza kuwa maadhimisho ya mwaka huu yataenda sanjari na kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Azimio la Innocenti la mwaka 1990ambalo linasisitiza umuhimu wa kulinda, kuendeleza na kusaidia unyonyeshaji na ulishaji bora wa watoto.

Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo yanayotarajiwa kuanza Agosti Mosi na kufikia kilele chake Agosti 7 mkoani Dodoma katika viwanja vya Nanenane ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi yakiwa na kauli mbiu “Unyonyeshaji na kazi, hakikisha inawezekana” yenye lengo la kuwasaidia wanawake wote wenye ajira rasmi na zile zisizo rasmi waweze kutunza watoto wao ipasavyo pasipo kuathiri ajira zao zinazowapatia kipato.

Wachimbaji madini watakiwa kuendana na mabadiliko ya teknolojia

0
0
Na Greyson Mwase, Handeni-Tanga

Wachimbaji wa madini nchini wametakiwa kuendana na teknolojia inayokua kila kukicha ili kuwezesha sekta ya madini kuwa na mchango zaidi katika pato la taifa.

Rai hiyo ilitolewa na Afisa Madini Mkazi kutoka Ofisi ya Madini- Handeni mkoani Tanga, Frank Makyao kwenye ufunguzi wa mafunzo juu ya matumizi ya huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao yaliyokutanisha wachimbaji wa madini katika kanda ya mashariki yanayoendelea mjini Handeni.

Lengo la mafunzo hayo lilikuwa ni kuwapa uelewa wa matumzi ya huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao ijulikanayo kama online mining cadastre transactional portal.

Makyao alisema kuwa ni vyema wamiliki wa leseni za madini wakaachana na mfumo wa zamani wa kutumia makaratasi katika huduma za leseni kwani mfumo wa kisasa wa huduma za leseni kwa njia ya mtandao utawawezesha kupata leseni kwa wakati na uwazi zaidi.

“ Kwa mfano kuanzia sasa mtaweza kufanya malipo ya leseni zenu kwa njia ya M-Pesa, Airtel Money na Tigo Pesa hali itakayowezesha ofisi za madini kupata mapato zaidi.” Alisisitiza Makyao

Makyao aliendelea kusema kuwa wachimbaji wa madini wanatakiwa kuchangamkia mafunzo yanayotolewa na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na kuanza kutumia huduma hiyo mara moja ili kurahisisha utendaji wao wa kazi.

Alisema biashara katika nchi nyingi duniani imekuwa ikifanyika kwa njia ya mtandao na kuwataka wachimbaji wa madini kuchangamkia fursa hiyo ili waweze kuendana na ushindani wa biashara ya madini duniani.

Aidha aliwataka wachimbaji wa madini kufuata sheria za madini katika uombaji na umiliki wa leseni za madini pamoja na kushirikiana na serikali kwa kulipa kodi na tozo mbalimbali kama Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 inavyowataka ili sekta hiyo iwe na mchango zaidi katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Afisa Madini Mkazi- Ofisi ya Madini Handeni, Frank Makyao (kulia) akifungua mafunzo kuhusu huduma za leseni za madini kwa njia ya mtandao yaliyokutanisha wachimbaji wa madini kanda ya mashariki mjini Handeni. Kutoka kushoto ni wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Pendo Elisha na Charles Gombe.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Charles Gombe (kushoto) akisisitiza jambo katika mafunzo hayo. Kulia ni Afisa Madini Mkazi- Ofisi ya Madini Handeni, Frank Makyao.

UAP Tanzania; one of the leading InsuranceGroup in East Africa is launching its two newproducts

0
0
DSC_1783Catherine Joshua Assistant Claims Manager UAP Insurance Tanzania (cnt) during the conference with media (not in picture). message about the launch of their two products UAP Jikinge and UAP Family Kinga. In (left) Mr. Raymond Komanga Business Development Manager UAP and Right is Michael Itimu Kiruti General Manager Operations UAP.

MAALIM SEIF AKUTANA NA MUWAKILISHI WA UN ANAESHUGHULIKIA MASWALA YA MADAWA YA KULEVYA NA UHALIFU

0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Muwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) Afrika Mashariki Bw. Jose Castillo, walipokutana kwa ajili ya mazungumzo ofisini kwake Migombani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Muwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) Afrika Mashariki Bw. Jose Castillo, ofisini kwake Migombani.
Muwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) Afrika Mashariki Bw. Jose Castillo, akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej, baada ya mazungumzo yaliyokuwa chini ya Maalim Seif. Katikati ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. Omar Dadi Shajak.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) Afrika Mashariki, pamoja na baadhi ya watendaji wa Tume ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya Zanzibar. (Picha na Salmin Said, OMKR).

KAMATI YA HARAMBEE KUWASAIDIA WAANDISHI WA HABARI YAKABIDHI MILIONI 20 KWA WAANDISHI WENYE MAHITAJI YA MATIBABU

0
0
 Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani), ndani ya Idara ya Habari MAELEZO,mapema leo jijini Dar kuhusiana na matokeo ya harambee ya Media Car Wash for Cancer Campaign, inayoendelea nchini.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani), ndani ya Idara ya Habari MAELEZO,mapema leo jijini Dar na pia akiwa ameambatana na baadhi ya
Waandishi wa habari watatu, Adolf Simon Kivamwo, Athumani Hamisi na Danstan Bahai (hayupo pichani) ambapo leo wamekabidhiwa jumla ya TZS 20m/- kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu  yao.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.Milioni 10 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari ZA Ukimwi (AJAAT), Adolf Simon Kivamwo kutokana na kusumbuliwa na Kansa ya Utumbo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.Milioni Tano kwa aliyekuwa mwandishi wa magazeti ya Habari leo na Daily News ambaye alipata ajali  na kumsababishia ulemamvu,Athman Khamis .

 
Waandishi wa habari watatu, Adolf Simon Kivamwo, Athumani Hamisi na Danstan Bahai wamekabidhiwa jumla ya TZS 20m/- kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu  yao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson alisema kuwa fedha hizo ni matunda ya harambee ya Media Car Wash for Cancer Campaign, inayoendelea nchini.

Kama tujuavyo, kwa kuanzia, wanahabari kutoka vyombo mbalimbali Jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau wengine waliosha magari kwenye viwanja wa Leader Club Julai 4, 2015.

Alisema katika harambee hiyo jumla ya 31m/-, zilipatikana, ambapo kati ya fedha hizo, ndizo wagonjwa wamegawiwa.

“Malengo yetu ya awali yalikuwa kwamba tuwachangishe fedha kwa ajili ya wenzetu wagonjwa, pia kiasi kingine kitumike kuwaingiza baadhi ya wanahabari kwenye mifuko rasmi ya Bima ya Afya. Na ndivyo tulivyofanya leo hii,” alisema.

Bw Thompson alisema kiasi kilichosalia kitatumika kuwaingiza waandishi wa habari 100 katika mpango wa kulipia matibabu kupitia mfuko wa Bima ya Afya, yaani  NHIF.” Alisema.

Alisema lengo la harambee hiyo ni kukusanya jumla ya 100m/- kabla ya mwezi Disemba 2015 na kazi yake kubwa itakuwa kuwahudumia wanahabari wasiojiweza kwa sababu ya kusumbuliwa na maradhi mbalimbali.

Pia pesa zitokanazo na harambee hiyo zitasaidia kuanzisha mkakati wa mkubwa wa kuhakikisha wanahabari wote nchini wanaingizwa kwenye mfuko wa Bima ya Afya.

“Lengo letu ni kuhakikisha wanabari wana kinga za afya zao,ili tukomeshhe huu mtindo wa kuchangiana mara kwa mara kila mmoja anapougua,”alisema na kuongeza kuwa  watakaohusika katika zoezi hilo, ni wale wasioajiriwa pamoja na wasioajiriwa lakini hawana huduma ya Bima ya Afya.

Ili kuendeleza mchakakato wa kufikia lengo kuu, wanahabari Kanda ya Ziwa kwa kushirikiana na wenzao wa Jijini Dar es Salaam, Agost 15 mwaka huu, wataosha magari kwenye viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza.

Tunaomba wadau mbalimbali waungane nasi kwenye hili,ikiwemo kulipia gharama mbalimbali ukiwemo usafiri kwenda na kurudi Mwanza,hoteli, matangazo ya radio na mabango.

Wakati huo huo Bw Thompson amesema kutakuwa mkutano wa wadau habari Jumamosi Agost 1, mwaka huu utakaofanyika Msimbazi Centre Jijini Dar es Salaam kwa jili ya kuanzisha mchakato wa usajili wa rasmi wa kampeni hii.

“Tunaomba wanahabari wote nchini watakaoweza kuhudhuria wasikose kufika, maana hapa ndipo juhudi za ukombozi wa kiafya kwa wanahabari zitakapoanzishwa rasmi,” alisema.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo alisema kuwa Kamati yake imewashirikisha wahariri wote nchini katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na kwamba viongozi hao wa vyumba vya habari ndio waliotoa majina hayo kwa kamati.


CCM MKOA WA DAR ES SALAAM WAITAKA TUME KUONGEZA VIFAA ILI KUFANIKISHA ZOEZI

0
0
 
 Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Juma Hamis 'Gadafi' akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hotel ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakielezwa na Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Juma Hamis 'Gadafi' alipozungumza nao mapema leo mchana  kwenye hotel ya Peacock jijini Dar es Salaam.


Chama Cha Mapinduzi  mkoa wa  Dar es Salaam kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuongeza,vifaa na rasilimali watu ili wananchi wengi waweze kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura bila usumbufu.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Bw. Juma Simba Gadafi  alisema anawashukuru waandishi kwa ushirikiano waliounesha  kwenye mkutano wa kumtambulisha mgombea wa urais  kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli uliofanyika tarehe 14 Julai 2015 katika viwanja vya Mbagala Zakheem.


Aidha aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 1 Agosti 2015, kupiga kura za maoni kuchagua wagombea Udiwani na Ubunge .Katika mkutano huo ambao waandishi wengi walionekana kuwa na  shauku ya kutaka kujua maoni ya  CCM juu ya kuondoka kwa Edward  Lowassa , Katibu wa Siasa na Uenezi  wa CCM mkoa wa Dar es Salaam alisema “Lowasa aliingia mwenyewe CCM bila shinikizo na kutoka mwenyewe hivyo maamuzi yake hayaifanyi CCM ishindwe kuendelea kutekeleza majukumu yake”. 
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images