Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 919 | 920 | (Page 921) | 922 | 923 | .... | 3286 | newer

  0 0

  SAM_4394Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima aliyeshinda katika kura za maoni za kutafuta wabunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi ( CCM ).akizungumza katika mkutano wa chama cha mapinduzi jana mtaa wa kati (CCM MKOA)wakati wagombea 12 wa chama hicho walipofanya ziara ya kutembelea kila kata na kujinadi kwa wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho ambapo aliwataka wananchi wasirubuniwe na kama walipewa rushwa na mgombea yeyote wasimchague bali wamchague kiongozi sahihi wa kuleta mabadiliko ya kimaendeleo  katika jimbo la Arusha(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  SAM_4366Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalimaambaye alishinda katika  kura za maoni za kutafuta wabunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi ( CCM ).  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple "A",Mkurugenzi wa Phide entertainment akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Monaban yajijini Arusha,Philemon Mollel ambaye pia ni Mgombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM katika ofisi za (CCM Mkoa) jijini Arusha jana
  SAM_4398Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau akizungumza katika mkutano wa kuwanadi wagombea Ubunge kupitia chama  cha mapinduzi mtaa wa kati jijini Arusha ambapo aliwataka wapambe wawagombea watulize mung'ari zao na kuacha tabia ya kukebihana huku akisisitiza wananchi kuchagua kiongozi bora.

  0 0

  SHIRIKA  la ndege la taifa (ATCL) limeupongeza utawala wa awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete huku likibainisha kuwa licha ya changamoto zilizo likabili shirika hilo katika kipindi cha awamu hiyo bado limefanikiwa kulinda hadhi yake sambamba na kuibua mipango inayolenga kuliibua upya shirika hilo.
  Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusiana na  utendaji wa shirika hilo katika kipindi hicho cha awamu ya nne, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Bw. Johnson Mfinanga aliitaja baadhi ya mikakati iliyoundwa juu ya msingi wa serikali ya awamu ya nne katika kuboresha zaidi huduma za shirika hilo.
   “Ni katika kipindi hiki cha awamu ya nne chini ya Rais Kikwete  ndio tuliweza kuanzisha safari zetu za kwenda visiwa vya Comoro na tumekuwa tukizidi kuongeza safari zetu zaidi kuelekea huko kwa kuwa tumebaini uamuzi huu umekuwa na tija kwa wananchi wa mataifa haya mawili,’’ alibainisha Bw. Mfinanga ambaye shirika lake kwa sasa limeongeza idadi ya safari zake kuelekea visiwa hivyo  kutoka mara tano hadi kufikia mara saba kwa wiki.
  Kwa sasa shirika hilo ndio shirika pekee la ndege hapa nchini linalotoa huduma zake kutoka Dar es Salaam kuelekea visiwa vya Comoro na hivyo kutoa fursa kwa wananchi wa mataifa hayo mawili  kuweza kuunganisha fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye mataifa hayo ikiwemo biashara, kwa mujibu wa Bw. Mfinanga.
  Zaidi Bw. Mfinanga alibainisha mpango wa shirika hilo wa kutambulisha safari zake za moja kwa moja baina ya visiwa vya Comoro na Zanzibar kabla ya mwisho wa mwaka huu kutokana na uhitaji mkubwa wa soko linachochewa na fursa za kibiashara baina ya visiwa hivyo.
  Aliongeza kuwa pamoja na mipango hiyo shirika hilo pia linaendelea kuboresha huduma zake kuelekea mkoani Mtwara na limekuwa likijivunia kuwa kiungo muhimu katika usafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoa huo ambao kwa sasa unajipanga kuchangamkia fursa ya uchumi wa gesi iliyovumbuliwa hivi karibuni.
  “Tumekuwa tukifanya safari zetu kuelekea mkoani Mtwara kwa kipindi kirefu sasa. Fursa ya gesi iliyoibuka mkoani humo inasababisha na sisi pia tujipange kwa kuangalia ni namna gani tutanufaika na fursa hiyo pia. Lakini pia tuna jukumu la kuhakikisha tunatimiza wajibu wetu kama shirika la taifa katika kukabiliana na mahitaji ya wananchi wa taifa hili,’’ alisema.
  Akizungumzia mipango ya shirika hilo katika kujipanua zaidi, Bw. Mfinanga alisema kwa sasa shirika hilo linaandaa mpango mkubwa wa miaka mitano ambao unatarajiwa kukamilika na kuwekwa wazi hivi karibuni.
  Kwa sasa shirika hilo linatoa huduma zake kuelekea mikoa ya Kigoma, Mtwara na visiwa vya Comoro kwa kutumia ndege yake aina ya CRJ-100  wakati ikiendelea kusubiri ndege yake nyingine aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 inayoendelea na ukarabati mkubwa kwenye karakana ya shirika hilo iliyopo kwenye uwanja wa Kimataaifa wa Julius Nyerere (JNIA) , jijini Dar es Salaam.

  “Kukamilika kwa ukarabati wa ndege hiyo kutasaidia tuweze kurejesha huduma zetu kuelekea mikoa ya Mwanza, Tabora, Kilimanjaro na Mbeya,’’ alisema Bw Mfinanga.

  0 0


  Meneja Bidhaa wa benki ya Exim, Bw Aloyse Maro akiokota moja ya kura za wateja wakati wa kuchezesha bahati nasibu ya kwanza ya kampeni ya akaunti ya malengo inayoendeshwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Wanaoshuhudia ni pamoja na mwakilishi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Bw. Humudi Abdulhussein  (kushoto) na mmoja wa maafisa wa beki hiyo Bw George Musetti.

  Benki ya Exim Tanzania imeendesha  droo yake ya kwanza ya kampeni ya akaunti ya malengo inayolenga kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba miongoni mwa watanzania.

  Droo hiyo iliyosimamiwa na Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini iliendeshwa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam ikiwa ni droo ya kwanza kati ya sita zinazotarajiwa kuendeshwa katika kampeni hiyo.

  Akizungumza mara tu baada ya droo hiyo, Meneja bidhaa wa benki hiyo, Bw. Aloyse Maro alisema kampeni hiyo ilizinduliwa ikiwa ni sehemu ya jitahada za benki hiyo kuwapatia wateja wake faida zaidi sambamba na huduma bora.

  Alisema kwa kuanzia, washindi waliopatakina kupitia droo hiyo walifanikiwa kujitwalia zawadi za simu za kisasa aina ya iPhone 6 huku akitoa wito zaidi kwa wateja wa benki hiyo kuwa na mwitikio zaidi kwa kushiriki kwenye kampeni hiyo.

  “Pamoja na kutoa shukrani zetu kwa wateja wetu kutokana na mafanikio tunayoendelea kuyapata ni vema pia tuwe mrejesho wa mafanikio haya  kwao pia. Ni katika mazingira hayo ndio maana tumekuwa na utaratibu wa kutoa zawadi kwa wateja wetu ili kufurahi nao pamoja,’’ alisema Bw. Maro.

   Zaidi Bw. Maro aliwakumbusha wateja wa benki kuendelea kushiriki zaidi kwenye kampeni hiyo kwa kuwa bado wananafasi zaidi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi ya gari kwenye droo tano zilizosalia.

  “Kampeni hii inaendelea kwa kipindi cha miezi mitano na bado kuna zawadi zaidi kwa ajili ya washiriki ikiwemo zawadi kuu ya gari ambayo itakabidhiwa kwa mshindi mwishoni mwa kampeni hii. Hivyo tunaomba watu waendelee kushiriki zaidi,’’ alisema.
   Sambamba na zawadi hizo Bw. Maro aliongeza kuwa kampeni hiyo inatoa riba nzuri zaidi kwa wateja wanaofungua akaunti hiyo ya malengo.  0 0

  Kama ambavyo aliweza kufanya vizuri na singo yake ya kwanza, msanii Galaxy anatarajia kuchomoka na wimbo wake mpya ‘mzuri tu’ ukiwa umeandaliwa na Man Walter chini ya studio za Combination sound hivi karibuni jijini Bongo.

  The smart boy Galaxy Ikanda akiwa maejipanga fresh kwa ujio wake mpya, alielezea sababu zinazompelekea kutumia muda wake mwingi kujipanga na sio kukurupuka 

  “Muziki umekuwa na ushindani mkubwa sana kiasi inampelekea msanii makini kuongeza umakini  na ubunifu kwenye utendaji Otherwise unaweza kujikuta kila siku umesimama sehemu moja huendi mbele, kitu ambacho sikitarajii kulingana na jitihada nilizonazo”.


  Alisema “kinachoturudisha nyuma wasanii wengi ambao tunachipukia ni kutokuwa na nidhamu na kazi zetu wenyewa hata kwa wanaotusimamia (Managers), halikadhalika tuna pupa ya kutafuta shortcut kuyafikia mafanikio kirahisi bila kufanya juhudi, huku mi nasema ni kujidanganya”.


  Galaxy ambaye kwa sasa yuko hewani na wimbo unaojulikana kwa jina la ‘Tam Tam’ amewataka wasanii wenzake kuongeza jitihata kwenye ubunifu na kuepuka kuzihusisha Sanaa zao na maisha yao binafsi ‘KUTENGENEZA KICKI’ kwa maana haiwasaidii na hii inachangia kuudidimiza muziki wetu na Sanaa kwa ujumla.


  “sioni sababu ya msanii kutengeneza story ya uongo ili aweze kutoa wimbo wake, hii inaonesha dhahiri ni kutojiamini na sijawahi kuona imemsaidia msanii kwa kufanya hivyo wimbo ukapata umaarufu mwaka mzima, mara nyingi story za kutengeneza ili kutoa wimbo zikiisha na wimbo umeisha so zinaua muziki wetu kama vipi tukaze” – Galaxy. 

  0 0

  IMG_8896
  Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akielezea mantiki ya warsha ya wadau wa elimu kuhusu viwango vya umahiri wa Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu Tanzania iliyofanyika mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani mwishoni mwa juma.
  IMG_8887
  Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
  SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limesema litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na wananchi wenye uwezo mkubwa wa kuvumbua na kutumia elimu.

  Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Unesco nchini Al Amin Yusuph wakati akizungumza na washiriki wa kongamano maalumu wa kupitia waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.

  Kongamano hilo ni moja ya mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.

  Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
  Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora na Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu ambavyo vitaingizwa.
  IMG_8817
  Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akifafanua jambo kwa wadau wa kongamano la kupitia kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini lililofanyika mjini Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa juma.

  Yusuph aliwataka wadau wanaoshiriki katika kongamano ambalo lilitarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki kutekeleza wajibu wao kwa makini kwa kuwa Watanzania wanasubiri maelekezo yao kufanikisha utoaji wa elimu ya Tehama yenye kuleta mwelekeo mpya wa matumizi kwa kulenga kuvumbua na kutumia elimu kwa manufaa ya taifa.

  Alisema UNESCO ipo tayari kuhakikisha kwamba Tanzania inazalisha wanafunzi ambao watakuwa na uwezo mkubwa katika Tehama ambao utaibua maendeleo endelevu.“Si kutoa walimu wazuri tu bali kuwezesha jamii , wanafunzi na waliopitia mafunzo hayo kuwa na namna mpya ya kufikiri na kuvumbua vitu vipya vya kujiendelea na kuendeleza taifa” alisema Yusuph.Alisema kimsingi elimu inatoa asilimia 5 lakini maisha yanatoa asilimia zilizobaki kama mtu atatumia vyema msingi wa maarifa aliyopewa.
  IMG_8793
  Jaco Du Toit, kutoka ofisi za Unesco kanda ya Nairobi akiendesha majadiliano ya maboresho ya vipengele mbalimbali vya waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu"UNESCO ICT Competency Framework for Teachers in Tanzania" wakati wa kongamano hilo lililomalizika mwishoni mwa juma mjini Bagamoyo.Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.

  0 0

   Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Leticia Nyerere akinyanyua mikono ikiwa ni sehemu ya ishara ya kuondoka katika chama hicho na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati alipokutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam.

   Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere akifafanua jambo kwa waandishi habari juu ya kuondoka katika chama hicho.
   Waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini maelezo ya Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere juu ya kuhama kwake katika chama hicho katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam. 

  Mwandishi akiuliza swali kwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere ambaye leo alikutana na waandishi habari juu kuhama chama hicho na kurejea CCM katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam. 


  Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii.

  MBUNGE wa Viti  Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa  wa Mara ,Leticia Nyerere amengatuka rasmi leo katika chama hicho na kudai kuwa anarudi nyumbani katika chama Cha Mapinduzi (CCM).


  Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam,Leticia amesema kuwa katika suala la kuhamia Chadema hakutafakari kwa kina labda angetafakari asingeweza kwenda huko.


  Amesema mchango wake unatambulika sasa anaweza kutumikia CCM nje  bila ya kuwa mbunge na kuweza kuleta maendeleo kutokana na uwezo wake katika masuala ya siasa.


  “Moyo wangu umekuwa ukisoneneka kutokana na kukaa Chadema na kuacha kukaa katika chama kilichonilea na kunisomesha hadi nje ya nchi ,sasa  nasema narudi  nyumbani kutumikia”amesema Leticia.


  Leticia amesema kwenda Chadema alifanya ujinga bila kutafakari na hawezi kulaumu dhamira yake mpya kurudi katika chama kilichompa makuzi yote na atatumikia CCM kwa kasi mpya na kuleta maendeleo chanya kutokana na kile ambacho amekuwa akitoa katika michango ya bunge.  Amesema wapinzani wote wa zamani walikuwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM)hivyo katika maamuzi yake ya kwenda Chadema hayakuwa  shahihi.


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kijeshi wa Fairbairn mjini Canberra katika siku ya mwanzo ya ziara yake Rasmi ya siku nne ya Kiserikali nchini Australia.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua na kutoa heshima katika kaburi la askari wa Australia wakati alipotembelea jumba la Makumbusho ya Taifa ya vita - Australian War Memorial - mjini Canberra zilikohifadhiwa kumbukumbu mbalimbali ambayo zinazoonesha jinsi Australia ilishiriki kwenye vita mbalimbali  katika siku ya mwanzo ya ziara yake ya Kiserikali nchini Australia.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Watanzania waishio Australia alipkutana nao na kuongea nao katika siku ya mwanzo ya ziara yake ya Kiserikali nchini Australia. 
   

  0 0


  THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone:255-22-2114512, 2116898
  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,
        STATE HOUSE,
                1 BARACK OBAMA ROAD,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Gazeti la Mwananchi la leo, Jumatatu, Julai 27, 2015, kwenye ukurasa wake wa 26 limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Marais watano wanaotajwa kuongoza kwa mishahara minono barani Afrika ni hawa hapa”.

  Katika habari hiyo ambayo gazeti hilo linadai chanzo chake ni “uchambuzi wa mtandao wa African Review” inadaiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, anashilikia nafasi ya tano miongoni mwa viongozi 38 wa nchi za Afrika wanaolipwa mshahara mnono zaidi.

  Gazeti hilo linadai kuwa Rais Kikwete analipwa Dola za Marekani 192,000 kwa mwaka, ikiwa ni malipo ya Dola za Marekani 16,000 kwa mwezi.

  Habari hizi siyo za kweli. Ni uongo na uzandiki. Ni uzushi mtupu na ni uzushi wa hatari.

  Mshahara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwezi ama kwa mwaka haufikii na hata wala kukaribia kabisa kiwango kinachotajwa na Gazeti la Mwananchi.

  Tangu Uhuru, mwaka 1961, Rais wa Tanganyika na baadaye tangu mwaka 1964 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuwa miongoni mwa viongozi wanaolipwa mishahara ya chini kabisa duniani.

  Mshahara wa Rais wa Tanzania kwa mwezi ni wa chini kiasi cha kwamba mshahara wake unazidiwa, tena kwa mbali, na mishahara wanayolipwa baadhi ya watendaji wakuu wa baadhi ya taasisi za umma nchini.

  Aidha, ni jambo la kushangaza kwamba Gazeti la Mwananchi, linalochapishwa hapa nchini, linaweza kupata kiasi cha uongo anacholipwa Rais wa Tanzania katika mitandao ya nje badala ya kuuliza rasmi na kupewa majibu sahihi.

  Kwa kujiingiza katika uzushi wa kupindua kiasi hiki, Gazeti la Mwananchi haliwezi kuwa na nia nyingine yoyote isipokuwa nia ya kuwachochea wananchi na kuwajengea chuki dhidi ya Serikali yao na Kiongozi wao Mkuu.

  Ni matarajio yetu, kuwa Gazeti la Mwananchi litafanya jitihada za makusudi, kama taaluma ya uandishi wa habari inavyoelekeza, kutafuta usahihi wa jambo hili na kuwaambia Watanzania ukweli.

  Imetolewa na;
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu – Dar es Salaam.
  27 Julai, 2015
  0 0

   Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia (pichani kati) akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wengine wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe,Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba na wa pili kulia ni Mwenyekitiwa chama cha NLD Dkt.Emmanuel Makaidi.Katika mkutano huo ulizungumzia pia kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Edward Lowassa na Watanzania Wengine wanaotaka kuleta mabadiliko  kuungana kupitia UKAWA ili kuiondoa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MICHUZI MEDIA GROUP.
   Baadhi ya Wanahabari wakiwa kwenye mkutano wa viongozi wa Umoja wa UKAWA,uliofanyika mapema leo jijini Dar
    Mmoja wa Wahariri wa gazeti la Jamhuri,Deodatusi Balile akitaka ufafanusi kuhusiana na umoja huo wa UKAWA kumkaribisha rasmi Mhe.Lowassa kujiunga na UKAWA,kwenye mkutano wa Wanahabari uliofanyika katika makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar
   Mmoja wa waandishi mahiri kutoka gazeti la Raia Tanzania,Hafidhi Kidogo aikuliza swali kwa viongozi hao wa UKAWA,kwenye mkutano wa Wanahabari na umoja huo,uliofanyika katika makao makuu ya chama cha CUF jijini Dar.
   Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama hicho jijini Dar,akiwa sambamba na baadhi ya viongozi wengine wa wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),ambapo mkutano huo ulizungumzia pia kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mhe.Edward Lowassa na Watanzania Wengine wanaotaka kuleta mabadiliko  kuungana  kupitia UKAWA ili kuiondoa CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu,kulia ni Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia na kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe pamoja na Mwenyekitiwa chama cha NLD Dkt.Emmanuel Makaidi (hayupo pichani)
    Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana kwenye makao makuu ya chama cha CUF,jijini Dar.Mh Mbatia amesema kuwa mtu yoyote ana haki ya kujiunga na UKAWA."Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu,kila chama kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake,watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi,hivyo mwanzoni mwa mwezi wa nane (wiki ijayo) tutamtangaza  mgombea  wetu kwa mbwembwe,mpaka sasa tumeishapiga hatua ambayo ni nzuri",amesema Mhe.Mbatia katika mkutano huo na Wanahabari.
     Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe.James Mbatia akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari mapema leo mchana makao makuu ya chama cha CUF,jijini Dar.Mh Mbatia amesema kuwa mtu yoyote ana haki ya kujiunga na UKAWA."Umoja ni Nguvu na utengano ni udhaifu,kila chama kilichosajiliwa ni mpinzani kwa mwenzake,watanzania wanahitaji kutengenezewa katiba ambayo itaweka mfumo safi,hivyo mwanzoni mwa mwezi wa nane (wiki ijayo) tutamtangaza  mgombea  wetu kwa mbwembwe,mpaka sasa tumeishapiga hatua ambayo ni nzuri",amesema Mhe.Mbatia katika mkutano huo na Wanahabari.
   Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha CUF-Prof.Ibrahim Lipumba akipeana mkono na Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Mhe,Freeman Mbowe mara baada ya kuzungumza na Waaandishi wa Habari  makao makuu ya chama cha CUF,mapema leo mchana jijini Dar,ambapo kwa pamoja kama UKAWA wamemkaribisha rasmi Mhe.Lowassa kujiunga na umoja huo na kwamba watampa nafasi.

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
  UMOJA wa  katiba ya Wananchi  nchini (UKAWA) vinamkaribisha Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa kujiunga katika  na umoja huo pamoja na watanzania wengine katika mapambano ya kuindoa CCM madarakani.


  Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao Makuu ya Chama cha Wananchi (CUF), kwa niaba ya Mwenyekiti wa Umoja huo,Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema wanawalika watanzania wote kujiunga na UKAWA katika kuweza kuleta mabadiliko katika kuhakikisha wanakiondoa Chama cha Mapinduzi (CCM)  katika kuweza kusimamia nchi.

  Mbatia amesema kuwa wanamualika Waziri Mkuu  Mstaafu,Edward Lowassa kutokana na kuwa mchapakazi na mfuatilialiaji katika majukumu ambayo anayatoa na uwezo anao katika kusimamia.Amesema  akiingia Lowassa katika umoja huo watashirikiana kwa karibu kutokana na kutambua kuwa ni mhamasishaji  na  ni mtu mwenye kuthubutu.

  Aidha amesema kuwa watamsimamisha mgombea  mmoja katika kila nafasi kupeperusha bendera  ya UKAWA katika uchuguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka  huu.


  Nae Mwenyekiti wa Chama Cha  Wananchi (CUF),Profesa Ibrahimu Lipumba amesema tuhuma za ufisadi zinazomkabili Lowassa zinatokana na mfumo  uliopo. Amesema  wanatarajia kutaja jina la mgombea Urais Agosti Nne Mwaka  huu  na atapatikana kutokana na taraibu zilizowekwa na umoja huo.

  Mbatia hakuweza kuweka wazi kuwa wanamkaribisha Lowassa kujiunga na chama kipi kutokana na ukawa sio chama kilichosajiliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini.


  Mwenyekiti wa NLD,Dk.Emmanuel Makaidi amesema Lowassa akigombea Urais atamkubali na tuhuma zinazomkabili kiongozi zingekuwa za kweli angepelekwa mahakamani lakini bado yupo na wenye tuhuma wamefikishwa mahakamani .


  Katika mkutano wa UKAWA masuali yalilenga kwa Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa kujiunga huko na  tuhuma zake wakati vyama hivyo vilikuwa vikinadi juu ya kutokuwa na usafi na pamoja na uhusikaji katika tuhuma ya mchakato wa  umeme wa dharula kupitia kampuni ya Richmond.

  0 0

  IMG_8896
  Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph, akielezea mantiki ya warsha ya wadau wa elimu kuhusu viwango vya umahiri wa Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu Tanzania iliyofanyika mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani mwishoni mwa juma.
  IMG_8887
  Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
  SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limesema litaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na wananchi wenye uwezo mkubwa wa kuvumbua na kutumia elimu.

  Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Unesco nchini Al Amin Yusuph wakati akizungumza na washiriki wa kongamano maalumu wa kupitia waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.

  Kongamano hilo ni moja ya mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wenye lengo la kusaidia serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.

  Mradi huo umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
  Ingawa kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora na Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu ambavyo vitaingizwa.
  IMG_8817
  Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo akifafanua jambo kwa wadau wa kongamano la kupitia kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini lililofanyika mjini Bagamoyo, Pwani mwishoni mwa juma.

  Yusuph aliwataka wadau wanaoshiriki katika kongamano ambalo lilitarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki kutekeleza wajibu wao kwa makini kwa kuwa Watanzania wanasubiri maelekezo yao kufanikisha utoaji wa elimu ya Tehama yenye kuleta mwelekeo mpya wa matumizi kwa kulenga kuvumbua na kutumia elimu kwa manufaa ya taifa.
  Alisema UNESCO ipo tayari kuhakikisha kwamba Tanzania inazalisha wanafunzi ambao watakuwa na uwezo mkubwa katika Tehama ambao utaibua maendeleo endelevu.

  “Si kutoa walimu wazuri tu bali kuwezesha jamii , wanafunzi na waliopitia mafunzo hayo kuwa na namna mpya ya kufikiri na kuvumbua vitu vipya vya kujiendelea na kuendeleza taifa” alisema Yusuph. Alisema kimsingi elimu inatoa asilimia 5 lakini maisha yanatoa asilimia zilizobaki kama mtu atatumia vyema msingi wa maarifa aliyopewa.

  0 0
 • 07/27/15--22:05: KIBONZO CHA NATHAN MPANGALA


 • 0 0  Na John Nditi, Morogoro

  MKUU wa Mkoa wa Morogoro pichani kati, Dk Rajab Rutengwe, amewaomba  wanawake kuanzia ngazi ya mitaa, vitongoji,  vijiji na kata  kushiriki katika suala la ulinzi shirikishi kwa  kuwafichua wahalifu  wanaotishia kuhatarisha uvujifu wa amani ndani ya  mkoa.

  Dk Rutengwe alitoa rai hiyo wakati alipozungumza na wajumbe wa mkutano mkuu maalumu wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Morogoro , Julai 24, 2015  wilayani Kilosa baada ya kutangazwa kwa  matokeo ya uchaguzi wa wabunge wa viti maalumu kwa makundi matano , UWT Mkoa, watu wenye ulemavu, Taasisi za Vyuo Vikuu, Wafanyakazi, NGO’s.

  Hivyo aliwaomba  wanawake kuunga mkono juhudi za serikali ya kukabiliana na uharifu wowote kushiriki katika ulinzi shirikishi kwa kutoa taarifa  kwa vyombo vya dola kwa watu wanaoshuku kuwa na  mienendo isiyofahamika  maeneo wanakoishi.

  Pia aliomba kamati ya ulinzi na usalama  mitaa, vitongoji , vijiji na kata ziwajibike katika majukumu ya kufanya kazi zao za kubaini waharifu.

  Mbali na hayo alitumia fursa hiyo kuwaomba  wananchi wa madhehabu mbalimbali ndani ya mkoa kuwafichua watu wanaogeuza nyumba za ibada kuwa ni sehemu ya maficho yao ya kupanga ama  kutekeleza vitendo vya kiharifu  hali inayoweza kutoa taswira potovu.

  0 0

  Dedicated, professional, eager to succeed, innovative and passionate are just some of the words used to describe Krantz Charles Mwantepele. He realized there was a deficiency and opportunity in Internet marketing but did not wait for changes, he made them happen. With no IT background, just a passion for news reporting, he has successfully.

  created three blogs; Mwanaharakati Mzalendo blog, harakati 360 and  Mzalendo Times put as well as an application on Google Play Store for his Mwanaharakati Mzalendo blog. Mwanaharakati Mzalendo has been recognized in the country and in Africa as the one of the best political, news, educational and general blogs. MAN magazine correspondent, Lisa Baraba sat down with Krantz to find out who is the man behind the laptop; his journey, aspirations and the mark he has left in the blogosphere.
  MORE NEWS CLICK HERE.

  0 0

  1
  Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Dr.Ahmed Twaha katikati akifuatilia mkutano wake na kamati ndogo ndogo za klabu hiyo uliofanyika jana,kulia ni Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi,
  23
  Mwenyekiti wa Cpastal Union akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Mipango na Fedha mara baada ya kumalizika kikao hicho.
  ………………………………………………………………………….

  UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union umeitaka kamati ya ulinzi na usalama kuhakikisha inatimiza wajibu wake ipasavyo ikiwemo kuhakikisha vitendo vitakavyoweza kuigharimu timu hiyo wakati wa michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara vinazibitiwa.

  Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao baina ya Kamati ndogo ndogo zilizoundwa,Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union,Dr.Ahmed Twaha alisema kuwa kumekuwa na vitendo vingi ambavyo vinajitokeza kwenye michuano ya Ligi kuu Tanzania bara na kuigharimu timu yetu na kulazimika kulipa faini ambayo ingeweza kufanya mambo mengine ya maendeleo.

  Alisema kutokana na kuwepo kwa tatizo hilo ndio sababu pekee iliyopelekea kuundwa kamati hiyo ili kuweza kukabiliana na vitendo vinayoweza kuisababisha hasara ndani ya klabu hiyo kwani vinakwamisha juhudi za kupiga maendeleo.

     “Ukiangalia msimu uliopita tulipata hasara ya shilingi milioni 3 kwa makosa ya uwanjani na hii inasababishwa na mashabiki kitendo ambacho kinaharibu sura ya mkoa hivyo lazima kamati hii italisimamia suala hilo “Alisema Mwenyekiti huyo.

  Aidha Mwenyekiti huyo aliitwisha mzigo mengine kamati ya Nidhamu na Maadili kuhakikisha watu wanaotukana kwenye mitandaa ya kijamii ikiwemo Facebook, Twiter na mengineyo watachukuliwa hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo.
  Hata hivyo alisema kuwa kamati hiyo itakuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa wakati wa timu hiyo itakapokuwa ikicheza mechi zake kwenye michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.

   “Lakini pia zamani wapo watu walikuwa wakitengeneza vitabu vya tiketi na kufanya mapato kuwa madogo licha ya uwepo wa watu wengi hivyo huu ndio mwisho wao kamati hii pia itasimamia suala hilo kwani hali hii iliifanya klabu kukosa mapato “Alisema Mwenyekiti huyo.
  Mwenyekiti huyo alisema kuwa wameweka mipango mizuri ya kuhakikisha timu hiyo inafungua matawi kwenye mikoa yote timu hiyo itakapokuwa ikienda kushiriki michuano ya Ligi kuu hapa nchini.

  IMETOLEWA NA OFISA HABARI WA COASTAL UNION.
  OSCAR ASSENGA.  0 0
 • 07/27/15--22:43: kipindi cha Jukwaa Langu
 • JUKWAA LANGU ni kipindi ambacho kitakuwa kikikujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015

  0 0
  Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo
  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani.
  Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ?
  Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya
  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa
  ukamilifu


  HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME
  Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya
  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili
  kama  ifuatavyo :
  Hatua  ya  kwanza, ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara
  na  kuwa  mgumu  kama  msumari.

  Na  hatua  ya  pili  ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa
  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo
  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER
  ERECTION
  JINSI  HATUA  ZA  KUSIMAMA  KWA  UUME  ZINAVYO  TOKEA.

  1. HATUA   YA  KWANZA:

  DAMU  KUTIRIRIKA  KWA  KASI KUINGIA  NDANI  YA  MISHIPA  YA  UUME  NA
  KUUFANYA  UUME  KUSIMAMA  NA  KUWA  MGUMU.

  Unapopata  wazo  la  kufanya  tendo  la  ndoa, mishipa  ya  fahamu
  iliyopo  kwenye  ubongo,  hupeleka  ishara  kwenye  mishipa  ya  uti
  wa  mgongo, ambayo  nayo  hupeleka  taarifa  hadi  kwenye  mishipa  ya
   uume. Taarifa  inapofika  kwenye  mishipa  ya  uume  huifanya
  mishipa hiyo  ku-relax  na  hatimaye   kufanya  mishipa  ya  ateri
  kufunguka  na  kutanuka. Mishipa  ya  ateri  inapo  tanuka  na
  kufunguka, huruhusu  damu  kuingia  kwa  kasi  ndani  ya  mishipa  ya
  uume  na  hivyo  kuufanya  huume  kusimama.

  Ni  muhimu  kujua  kuwa, mishipa  ya  uume  inapo relax  hupelekea
  kuisukuma na  hatimaye  kuiziba  mishipa  ya  vena  iliyo  karibu  na
  mishipa  ya  uume  na  hivyo  kuiondolea  uwezo  wa  kunyonya  damu
  iliyomo  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  sehemu  nyingine
   za  mwili.

  N.B: Kazi  kubwa  ya  mishipa  ya  vena  ni  kunyonya  damu  iliyomo
  ndani  ya  mishipa  ya  uume  na  kuipeleka  katika  sehemu  nyingine
  za  mwili.  Au  kwa  lugha  nyingine  unaweza  kusema, kazi  kubwa  ya
   mishipa  ya  vena  ni  kuhakikisha  hakuna  damu  kwenye  mishipa  ya
   uume.

  KWA   MAELEZO  ZAIDI, TEMBELEA


  0 0

  John Pombe Joseph Magufuli alipokuwa kidato cha kwanza katika Seminari ya Katoke mwaka 1975.

  0 0
 • 07/27/15--23:05: MSAADA TUTANI
 • MKAZI wa Heka wilayani Manyoni Mkoani Singida Joha Athumani(pichani), anaomba wasamaria wema kumsaidia msaada wa matibabu kwaajili ya mtoto wake Halima Mohamed mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu anayesumbuliwa na tatizo la kutoona.

  Akizungumza na ripota wa Globu ya Jamii Kanda ya Kati, Joha alisema kutokana na uchunguzi uliofanyika katika Hospitali ya wilaya ya Manyoni zinahitajika fedha zaidi ya shilingi laki tano (500,000/=) kwaajili kufanyiwa upasuaji mtoto huyo.

  Alisema kwasasa hana uwezo wa kumtibia mtoto huyo kutokana kupewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili mtoto huyo aweze kufanyiwa upasuaji.

  Hata hivyo alisema kwa sasa hana msaada wowote kutokana na mumewe kumkimbia baada ya kuzaa mtoto mwenye tatizo hilo.

  Mkazi huyo wa Heka alisema mwanaye alianza kusumbuliwa na tatizo la kutoona akiwa na umri wa miezi mitatu mpaka sasa, ambapo amezunguka huku na huku lakini hajafanikiwa kupata matibabu ya mtoto wake.

  Ameomba wasamaria wema watakaoguswa kumsaidia, wawasiliane na mwandishi wa gazeti hili kupitia namba 0712 561279.
  Barua ya rufaa aliyoandikiwa Joha Athumani ya kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya matibabu ya mwanaye Halima Mohamed.

  0 0

  Usili wa kwanza wa Dance 100% (2015) umefanyika kwa mafanikio makubwa Temeke jijini Dar es Salaam, ambapo makundi ya Team ya Shamba, The WT Group, WD, The Best Boys Kaka Zao na Team Makorokocho wameweza kushinda nafasi ya kuingia katika michuano kutoka wilaya ya Temeke.

  Makundi haya yamechuana vikali na mengine 6 yanayokamilisha idadi ya makundi 11, UNI 6 Crew, GMF Crew, TWC, Dar Crew, Noma Sana Crew, na Viga Stars yaliyojitokeza kuwania nafasi hiyo katika usajili huo wa kwanza.


  Mratibu wa mashindano hayo kutoka East Africa Television na East Africa Radio, Bi Happy Shame, amesema kuwa amefurahishwa na utulivu na amani ambayo wapenda burudani Temeke wameonyesha leo, huku pia kukiwa na vipaji mbalimbali kutoka makundi yaliyojitokeza katika usaili huo wa kwanza.


  Akizungumza baada ya kumalizika michuano ya usaili huo, mratibu wa Dance 100% kutoka BASATA, Kwerugira Maregesi, mbali na kufurahishwa na vipaji vilivyojitokeza, amekumbushia umuhimu wa makundi hususan yale yanayotarajiwa kushiriki usajili unaofuata, kuzingatia vigezo na masharti yaliyowekwa kujiwezesha kushinda, ikiwepo ubunifu katika mitindo ya kudansi, kuburudisha na muonekano, huku akishauri kupunguzwa kwa mitindo ya sarakasi na kuongezwa ladha katika upande wa dansi zaidi.


  Majaji Super Nyamwela, Queen Darleen na Shetta wametumia umakini nkubwa kuhakikisha wanatoa alama zinazostahili kwa mujibu wa vigezo kwa washiriki wote, huku burudani mbalimbali zikijiri zikishereheshwa kikamilifu na watangazaji rasmi wa Dance 100 kwa mwaka huu, T-Bway 360 na mrembo Maggie Vampire.


  Majaji pia kila mmoja kwa nafasi yake wametaka washiriki watakaoendelea kujitokeza kujipanga zaidi wakizingatia vigezo vilivyowekwa, ambavyo ndivyo wanavyovitumia kutoa maksi (alama) zitakazowawezesha kufikia ushindi.


  Usajili wa pili wa mashindano haya makubwa kabisa ya kudansi utafanyika katika viwanja vya Don Bosco Upanga siku ya Jumamosi Tarehe 01 Agosti 2015, ambapo makundi mengine matano yatasakwa kushiriki katika michuano hiyo kwa mwaka huu.


  Usikose kujionea kwa urefu yote yaliyojiri  pale TCC Chang'ombe katika mashindano ya usajili huo, kwa kutazama ting'a namba moja kwa vijana EATV, siku ya Jumamosi, kuanzia saa 12 na nusu jioni.


  East Africa Television na East Africa Radio inaleta Dance 100% kwa kupewa nguvu na mtandao wa Vodacom Tanzania na Coca Cola ambao ndio kinywaji rasmi cha dance 100% (2015).
   Kutoka kushoto -Majaji wa mwaka huu kwenye Dance 100%  ni Super Nyamwela, Shetta na Queen Darleen wakiwa wanajumulisha matokeo ya washiriki kutoka Temeke.


  0 0

  Na Benjamin Sawe,Maelezo

  Mabadiliko katika sekta ya hifadhi ya jamii nchini yamepelekea kuwepo na mabadiliko ya sheria ya mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF). Sheria ya Mfuko wa pensheni wa PSPF sasa inaruhusu kusajili wanachama katika sekta zote za umma na binafsi. Na kwa sasa mfuko una mipango miwili ya uchangiaji wa lazima yaani PSPF Mandatory Scheme na mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSPF Supplementary Scheme

  Akizungumza katika mahojiano maalum na Mwandishi wa Makala hayaBi Mwanjaa Sembe, Meneja Mpangowa Uchangiaji wa Hiari PSPF anasema uwasilishaji michango kwa kutumia huduma ya MaxMalipo itawasaidia wachangiaji kupata huduma za michango yao.

  Anasema huduma ya kulipia kupitia mfumo wa Maxmalipo imeanzishwa na mfuko wa pensheni wa PSPF kwa ajili ya kupanua wigo kwa wanachama wa mfuko huo kuchangia na kujua salio la michango yao popote walipo ambapo huduma hiyo itawarahisishia watumiaji kutosafiri kwa umbali mrefu ili kupata huduma hiyo.
  Mfuko umeona adha na shida walizokuwa wanazipata wateja wetu ndio maana tukaamua pamoja na huduma nyingine zitolewazo na mfuko wetu tujiunge na wenzetu wa Kampuni ya MaxCom inayotoa huduma ya Max Malipo ili kuweza kuwakomboa wateja waweze kuchangia pamoja na kujua kiasi cha michango yao kwa urahisi kwa kutumia huduma hiyo hivyo kuwafanya kuwa na muda mrefu wa kutafuta kipato badala ya kusafiri kwa umbali mrefu kufuata huduma.Anasema Bi. Sembe.


older | 1 | .... | 919 | 920 | (Page 921) | 922 | 923 | .... | 3286 | newer