VOA: Zulia Jekundu S1 Ep 34: Justin Bieber, Johnny Depp, Taraji Henson & Emmy 2015
↧
↧
SATURDAY, JULY 25, 2015 MCHUNGAJI NATSE AWAAGA JIMBO LA KARATU ,QAMBALA KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki,Joshua Nassari akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya hosteli ya KKKT Karatu na kumpongeza mch.Natse kwa kuamua kuachia nafasi wanachama wengine.
|
↧
KOMBE LA KAGAME: YANGA YAIFUNGA KMKM 2-0
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akimtoka beki wa KMKM, Khamis Ali Khamis wakati wa mchezo wa Kombe la Kagame uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshinda 2-0.
Deus Kaseke akiwatoka wachezaji wa KMKM.
Golikipa wa timu ya KMKM ya Zanzibar, Nassor Abdulla Nassor akiokoa moja ya hatari langoni mwake wakati timu yake ilipopambana na Yanga katika mchezo wa Kombe la Kagame.
Donald Ngoma (kulia) akiwania na beki wa KMKM, Khamis Ali Khamis.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia timu yao.
↧
Dr Shashi Tharoor MP - Britain Does Owe Reparations
↧
KIOTA KIPYA CHA MARAHA CHA JOZI LOUNGE CHAZINDULIWA MSASANI VILLAGE JIJINI DAR ES SALAAM
Kiota Kipya Cha Maraha kimezinduliwa Kimezinduliwa Jijini Dar es Salaam jana Jiioni. Kiota hicho Jozi Lounge, inapatikana Pande za Msasani Village, jirani kabisa na Shule ya Msingi Msasani.
Mmiliki wa Jozi Lounge, Dismass Massawe (kushoto) akifungua Champaign wakati wa uzinduzi wa kiota hicho. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali ambao walikunywa na kucheza mpaka majogoo.Hiyo ndiyo habari ya Mujini.
Mmiliki wa Jozi Lounge, Dismass Massawe (kushoto)huku meneja wake ni Nick Rawlings(Mzungu anayefungua Champaign).
Sehemu ya Counta ya kiota hicho cha Jozi.
Wadau wakipiga picha kabla ya kuzama ndani kwenye kiota cha maraha.
DJ mkali anaeporomosha muzic wa hatari
Wadau kutoka Kampuni ya Executive Solution ya jijini Dar es salaam ambao ndio walikuwa waratibu wakuu wa uzinduzi huo wakishow love.
Ilikuwa ni hatari kuyarudi magoma mwanzo mwisho. Hakuna kulala wala kuchoka ndani ya Jozi Lounge
↧
↧
KUAHIRISHWA SAFARI YA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA HADI LEO JIONI JULAI 25, 2015
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika kuwataarifu wananchi na abiria waliokuwa wasafiri na treni ya leo Ijumaa Julai 24, 2015 kutoka Dar es Salaam kwenda bara kuwa safari hiyo imeahirishwa hadi kesho saa 11 jioni.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa safari hiyo ni ajali ya treni ya mizigo iliyotokea leo Ijumaa Julai 24, 2015 saa 8:15 alasiri maeneo ya Stesheni za Mazimbu –Mkata mkoani Morogoro ambapo ilihusisha mabehewa matano ya treni ya mizigo iliyokuwa inasafiri kwenda Bara, manne yaliacha njia na moja kuanguka kabisa.
Tayari Wahandisi wa TRL wako eneo la ajali kufanya tathmini na kuanza zoezi la uokoaji, ikiwemo kazi ya kuyanyanyua mabehewa yaliyopata ajali na kisha kukarabati njia ili iwezwe kupitika mapema hapo kesho.
Uongozi wa TRL inawaomba radhi wananchi na wateja wake wote nchini kwa usumbufu utakaojitokeza.
-Tamati-
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ,
Mhandisi Elias Mshana
Dar es Salaam,
Julai 24, 2015.
↧
TAARIFA KWA UMMA JUU YA MAKALA ILIYOTOLEWA NA GAZETI LA MWANANCHI
↧
MSAADA TUTANI
MKAZI wa Heka wilayani Manyoni Mkoani Singida Joha Athumani(pichani), anaomba wasamaria wema kumsaidia msaada wa matibabu kwaajili ya mtoto wake Halima Mohamed mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu anayesumbuliwa na tatizo la kutoona.
Akizungumza na ripota wa Globu ya Jamii Kanda ya Kati, Joha alisema kutokana na uchunguzi uliofanyika katika Hospitali ya wilaya ya Manyoni zinahitajika fedha zaidi ya shilingi laki tano (500,000/=) kwaajili kufanyiwa upasuaji mtoto huyo.
Alisema kwasasa hana uwezo wa kumtibia mtoto huyo kutokana kupewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili mtoto huyo aweze kufanyiwa upasuaji.
Hata hivyo alisema kwa sasa hana msaada wowote kutokana na mumewe kumkimbia baada ya kuzaa mtoto mwenye tatizo hilo.
Mkazi huyo wa Heka alisema mwanaye alianza kusumbuliwa na tatizo la kutoona akiwa na umri wa miezi mitatu mpaka sasa, ambapo amezunguka huku na huku lakini hajafanikiwa kupata matibabu ya mtoto wake.
Ameomba wasamaria wema watakaoguswa kumsaidia, wawasiliane na mwandishi wa gazeti hili kupitia namba 0712 561279.
Barua ya rufaa aliyoandikiwa Joha Athumani ya kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya matibabu ya mwanaye Halima Mohamed.
↧
TTCL yaunganisha Ofisi na Kanda za MSD kwenye Mkongo
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto) hati ya makubaliano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania. Hafla hiyo ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania imefanyika leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania inayotolewa na kampuni ya TTCL. Ofisi za Kanda za MSD zimeunganishwa na Makao Makuu na huduma za mkongo wa mawasiliano ili kufanya kazi zake kwa haraka na ufanisi zaidi. Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD Dar es Salaam, kulia ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akishuhudia.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
↧
↧
Kadama Malunde Mwenyekiti Mpya wa Wanahabari Shinyanga
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza muda wake, Shija Felician akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde (mwenye suti) baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa Klabu hiyo. Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga waliomaliza muda wao wakijiuzuru nyadhifa zao kabla ya uchaguzi mkuu kupata viongozi wapya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club- SPC)Msimamizi wa uchaguzi mkuu wa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga David Nkulila akizungumza jambo wakati wa uchaguzi mjini Shinyanga
↧
Rais Kikwete aagana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia
↧
SIMU TV: HABARI TOKA VITUO VYA TELEVISHENI
↧
UZINDUZI WA KAMPENI YA WAZAZI NIPENDENI AWAMU YA PILI WAFANYIKA VIWANJA VYA MWEMBE YANGA TEMEKE JIJINI DAR
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Dk. Seif Rashid (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya Wazazi Nipendeni awamu ya pili katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo mchana. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Anna Bodipo Memba na wa pili kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magema.
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Anna Bodipo Memba (kulia), akitoa hutuba yake kwenye uzinduzi huo.
Mshauri wa masuala ya Afya ya Jamii kutoka Taasisi ya HBC, Mdadike Thabit (kulia), akimuelekeza jambo mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya watoa huduma kabla ya kufanyika uzinduzi huo.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
↧
↧
Kipindi cha Nyumbani Na Diaspora na David Kyungu
↧
J&M VIRGO WASHUSHA MALI MPYA
DUKA LAKO PENDWA LA J&M VIRGO LIMESHUKA MALI MPYA NA ZA UHAKIKA KABISA KWAKO WEWE MTANZANIA ILI UWEZE KUNG'AA
J&M VIRGO WENYE UHODARI WA KUUZA VIWALO VYA NGUVU NA VYA KISASA JIJI LA DAR ES SALAAM ,WANAPATIKANA PALE MIKOCHENI KWA WARIOBA,JENGO LA C&G PLAZA GHOROFA YA KWANZA.FIKA ILI UWEZE KUJIPATIA VITUZZ NA VIWALO VYA KIJANJA,POCHI BABKUBWA,MOKA MATATA NA MICHUCHUMIO YA HAJA KWA KINA DADA.
KWA KUONA MALI ZAIDI TEMBELEA LIBENEKE LAO
↧
KANALI MSTAAFU ISAAC MWISONGO AMUUNGA MKONO DKT MAGUFULI
↧
DR.MARY MWANJELWA USHINDI WA KISHINDO UBUNGE VITI MAALUM MKOWA WA MBEYA
Mgombea ubunge viti maalum mkoa wa mbeya Dr.Mary Mwanjelwa aibuka mshindi katika kura za maoni kutoka kwa wajumbe wa ccm mkoa wa mbeya na kupata ridhaa ya kulejea tena katika kiti cha ubunge viti maalum mkoa wa Mbeya kwa ushindi wa kishindo wa asilimia 97 na kuwashinda wagombea kumi (10) kati ya kumi na moja (11) walio kuwa wakigombea na kutaka kuteuliwa na wajumbe wa ccm mkoa wa mbeya...Picha zote Na Fadhiri Atick, Mbeya.
Mshindi wa ubunge viti maalum kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa mbeya Dr.Mary Mwanjelwa akiwashukuru wajumbe wa ccm mkowa wa mbeya mara baada ya ushindi katika uchaguzi wa kumpata mbunge viti maalum mkoa wa mbeya ulio fanyika tar:24-07-2015, katika ukumbi wa nyerere Musti jijini mbeya.
↧
↧
BASATA YAWATAKA WASANII WAFUATE TARATIBU WANAPOENDA NJE YA NCHI
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambalo ni msimamizi wa sekta ya Sanaa nchini linawakumbusha wasanii wote nchini kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo wanapokwenda nje ya nchi kufanya maonesho au kushiriki shughuli yoyote ya Sanaa ili kuepuka matatizo na mikanganyiko mbalimbali inayoweza kujitokeza.
Kwa mujibu wa taratibu zilizopo, msanii yeyote anapokwenda nje ya nchi anapaswa kujaza fomu maalumu inayotolewa na BASATA na baadaye kupewa kibali bure (bila gharama yoyote) ambacho mbali na kueleza wapi msanii anaelekea kinaeleza kwa kina tarehe ya kuondoka kwa msanii na ile ya kurudi nchini.
Kutokana na kukua kwa sekta ya Sanaa nchini hususan muziki na filamu wasanii wengi wamekuwa wakipata fursa ya kwenda nje ya nchi kufanya maonesho na shughuli zingine za Sanaa hivyo suala la kufuata sheria, kanuni na taratizu za kupata vibali vya kwenda nje ya nchi ni muhimu sana ili kuhakikisha kwanza; safari zao zinakuwa na baraka ya moja kwa moja kutoka Serikalini, pili kusaidia upatikanaji wa takwimu sahihi za wasaniii wanaokwenda nje ya nchi, tatu usalama wa wasanii wetu na mwisho, kuwakabidhi bendera ya taifa kama ishara ya uwakilishi na ubalozi wa nchi yetu katika mataifa wanayoyatembelea.
Kwa mujibu wa taratibu zilizopo, msanii yeyote anapokwenda nje ya nchi anapaswa kujaza fomu maalumu inayotolewa na BASATA na baadaye kupewa kibali bure (bila gharama yoyote) ambacho mbali na kueleza wapi msanii anaelekea kinaeleza kwa kina tarehe ya kuondoka kwa msanii na ile ya kurudi nchini.
Kutokana na kukua kwa sekta ya Sanaa nchini hususan muziki na filamu wasanii wengi wamekuwa wakipata fursa ya kwenda nje ya nchi kufanya maonesho na shughuli zingine za Sanaa hivyo suala la kufuata sheria, kanuni na taratizu za kupata vibali vya kwenda nje ya nchi ni muhimu sana ili kuhakikisha kwanza; safari zao zinakuwa na baraka ya moja kwa moja kutoka Serikalini, pili kusaidia upatikanaji wa takwimu sahihi za wasaniii wanaokwenda nje ya nchi, tatu usalama wa wasanii wetu na mwisho, kuwakabidhi bendera ya taifa kama ishara ya uwakilishi na ubalozi wa nchi yetu katika mataifa wanayoyatembelea.
↧
DKT MAGUFULI AREJEA JIJINI DAR BAADA YA KUJITAMBULISHA MIKOA KADHAA,APOKELEWA KWA KISHINDO
Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mji wa Bagamoyo (hawapo pichani) alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.Dkt Magufuli amejitambulisha vyema kila alikopita na kupokelewa kwa kishindo katika mikoa na vitongoji vyake aliyopita ikiwemo jijini Mwanza,Geita,dodoma,Morogoro,Pwani na jiji la Dar kwa ujumla.
Wakazzi wa Bagamoyo wakimsikiliza Dkt Magufuli wakati alipokuwa akijitambulisha kwao na kuwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea,alipokuwa akitoka mkoani Dodoma kurejea jijini Dar jana jioni.
Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Chalinze wakimsikiliza Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Chalinze alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete akiwasalimia Wananchi wa Chalinze na kumkaribisha Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru Wananchi wa Chalinze (hawapo pichani) pamoja na kujitambulisha kwao alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Chalinze wakimshangilia kwa mayowe Mteule wa Chama cha Mapinduzi CCM kwa nafasi ya Urais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama mjini hapo kuwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi wa Chalinze alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Chalinze,ambaye anawania tena nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo Mh.Ridhiwani Kikwete pamoja na Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli wakifurahia jambo mjini Bagamoyo,aliposimama mjini hapo kujitambulisha na kuwashukuru kwa kujitokeza kwao kwa wingi kumpokea,alipokuwa akirejea jijini Dar jana jioni akitokea mkoani Dodoma.
Mkazi wa Bagamoyo akifurahia jambo
Wananchi wakimshangilia Dkt Magufuli (hayupo pichani) alipokuwa akijitambulisha kwao hapo jana mjini Bagamoyo.
↧
KAMPUNI YA MAFUTA YA ENGEN HAPA NCHINI YAPATA MKURUNGENZI MPYA
Mkurungenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania, Mubita Akapelwa akiwashukuru baadhi ya wafanyakazi wa kampunikwa ushirikiano walio uonesha wakati wa utendaji wake kazi katika hafla ya kumuaga na kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Kampuni hiyo Paul Mhato iliyofanyika katika ukumbi wa Sea criff jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi MtendajiMpya wa Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania, Paul Mhato akifurahia jambo katika hafra ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo na kumuaga Mkurungenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta Engen hapa nchini, Mubita Akapelwa aliee maliza muda wakekatikati kulia ni Meneja Utawala Kampuni ya Mafuta Engin Tanzania Shannel Sihuimba.
Kushoto ni Mkurungenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania, Mubita Akapelwa aliemaliza muda wakeakipeana mkono wa shukurani na Meneja Masoko wa Kampuni ya Mafuta EnginTanzania Shabaani Kajungilo.
Mkurungenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya Engen Tanzania, Mubita Akapelwa aliemaliza muda wake wa kufanya kazi katika kampuni hiyo (kushoto)akipokea zawadi kutoka kwa Msaidizi wa Mkurungenzi wa Kampuni ya Mafuta ya Tanzania ya Engen Donathi Mbarara.
Mkurungenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta ya EngenTanzania, Mubita Akapelwa aliemaliza muda wake akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo.
Picha na Emmanuel Massaka.
↧
More Pages to Explore .....