Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

SAKATA LA MTU KUSHAMBULIA WATU KWA KISU KWENYE DALADALA JIJINI DAR ES SALAAM


SIMU TV: HABARI TOKA TELEVISHENI USIKU HUU

MAKALA YA SHERIA: NI MUHIMU SANA MFANYABIASHARA/MJASIARIAMALI/MNUNUZI WA BIDHAA KUYAJUA HAYA.

$
0
0
Na  Bashir  Yakub


Ipo  sheria moja  iitwayo  Sheria  ya Uuzaji  wa  bidhaa Sura  ya 354. Ni  sheria  ambayo  hutoa majibu  ya  miamala ya  kibiashara  hasa  kwa namna  ya  kimikataba. 

Ni  muhimu  sana  kwa  wajasiriamali  kujua  mambo  yaliyo  kwenye sheria  hii  ili  kuepuka  migongano  na  migogoro  ya  kibiashara.

Sheria  hii hueleza  jambo  fulani likitokea  hivi  kati  ya  muuzaji  na  mnunuzi  nani  ana  haki  na mengine  mengi  kama  nitakavyoonesha  hapa. Ili  ujumbe  kufika  vyema  nitaeleza  kwa  mtindo  wa  masomo. 

BAADA YA UCHAGUZI WA AMANI, BURUNDI BAN KI MOON ATAKA KUTEJEA KWA MAZUNGUMZO

$
0
0
Na Mwandishi Maalum, New York.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amezitaka pande zinazopingana nchini Burundi kubaki watulivu na kurejea mara moja katika meza ya majadiliano jumuishi ya kisiasa ili kumaliza tofauti zao na kujadili changamoto zinazolikabili taifa lao.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Katibu Mkuu, Julai 23, Ban Ki Moon ametambua hali ya Amani na utulivu iliyotawala wakati wa uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo ( Burundi )uliofanyika Julai 21 na kuwataka wadau wakuu kurejea katika meza ya majadiliano.

Taarifa hiyo imebainisha kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, anazikumbusha mamlaka za Burundi wajibu wao wa kuwahakikishia usalama pamoja na kuwalinda raia wake na kumalizwa kwa matukio ya uvunjifu wa Amani na uwajibikaji kwa wa ukiukwaji wa haki za binadamu.

“ Katibu Mkuu anatoa wito kwa wadau wote wa Burundi kushiriki kwa nia njema katika majadiliano ya kisiasa kwa kuweka mbele maslahi ya Burundi kwanza, na kutekeleza kikamilifu vipengele vilivyoainishwa katika tamko la Julai 6 la Mkutano wa Kilele wa Jumuiya ya Afrika Mashariki chini ya usimamizi wa Rais Yoweri Museven wa Uganda” Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa, Umoja wa Mataifa utaendelea kufanya kazi kwa karibu na Jumuiya ya Afrika Mashariki ( EAC) na Umoja wa Afrika ( AU) katika kusaidia upatikanajji wa suluhu ya kudumu nchini Burundi.

Katika muktadha huo, Katibu Mkuu anakaribisha kupelekwa watazamaji wa haki za binadamu kutoka AU na wataalam wa masuala ya kijeshi kwa lengo la kusaidia na kupunguza kujitokeza kwa vitendo vya uvunjifu wa Amani na kuwezesha suluhu la Amani la kisiasa kwa matatizo yanayoiathiri nchi hiyo.
" Nimepiga kura ndivyo anavyoelekea kusema mama huyu Raia wa Burundi mara baada ya kupiga kura ya uchaguzi wa rais uliofanyika Julai 21. ( picha kwa hisani ya Umoja wa Mataifa. Ban Ki Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ametoa wito kwa pande zinazopingana kurejea katika meza ya mazugumzo mara moja baada ya kuwa uchaguzi huo umefanyika kwa amani ili kujadiliana na kumaliza tofauti zao kwa maslahi ya wananchi wao na nchi yao.

Kampeni ya " Ndio ! Fuso ni Faida " kwa mikoa zaidi ya 11 Kuanza leo tarehe 24 July ,2015 ,Jijini Dar

$
0
0
Diamond Motors Limited is the country’s leading automobile distributor and the sole distributor of Mitsubishi Fuso Truck and Bus Corporation (MFTBC) in Tanzania. They will once again be launching the campaign, Ndio! FusoniFaida where over a 26-day 11 region Test Drive andRoad Show in which they will be showcasing the FJ and launching the FZ; Fuso medium and heavy-duty truck which are suitable for the purpose of mining, agriculture, construction, logistics and haulage.

During the road show that is set to begin on 24th July 2014 in Dar Es Salaam. The trucks will be available for test drive during to the road show.

The sales and technical teams will accompany the vehicles during the 26-day 11 region Test Drive and Road Show and will pass by key towns in each district. The objective of the roadtrip is to bring the trucks closer to its customers in the region and to showcase the vehicles' efficiency and capability which will lead to high productivity for their customers. The Ndio! Fuso niFaida campaign will kick off its journey in Dar es Salaam and then head to several strategic townssuch as Tanga – Moshi – Arusha – Mwanza – Kahama- Shinyanga – Dodoma – Iringa – Mbeya – Songea and back to Dar Es Salaam.

USHIRIKIANO NI MUHIMU KATIKA UTHIBITI WA UHALIFU MTANDAO

$
0
0
 Itakumbukwa Mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu katika hotuba yangu niliyo iwasilisha kwa wanausalama mitandao tulipo kutana  jijini Johannesburg mbali na mambo mengine nilihimiza sana ushirikiano baina yetu kwani wahalifu mtandao wameendelea kua mbele yetu kutokana na ushirikiano mkubwa waliokua nao. Ushirikiano unao mabatana na kusambaza vitendea uhalifu mtandao bure auu kwa gharama nafuu mitandaoni.

Baada ya kulizungumza hili laushirikiano wazungumzaji wengine wote walionekana kuniunga mkono na hatimae kuonekana ni swala muhimu lakufanyiwa kazi mapema. Nafarijika kuona Uingereza tayari mukuu wake wa CERT ametilia mkazo kauli hii (Ya ushirikiano) kupitia kikao kilicho malizika London ambapo taarifa kamili kuhusiana na hili inaweza kusomeka kwa “KUBOFYA HAPA

Aidha, Marekani na Israel baada ya kutia saini makubaliano ya kuboresha ushirikiano katika maswala ya usalama mitandao paliambatana na kuhimiza mataifa mengine kuona umuhimu wa kushirikiana katika vita hii ya uhalifu mtandao.
Nilipata kuzungumza tena katika mkutano wa wanausalama Nchini Cyprus ambapo pia nilizungumza kwa mara ya kwanza kuhusiana na ushirikiano huku nikipongeza umoja wa ulaya kwa kuungana kwao katika hili la usalama mitandao kupitia chombo chao kiitwacho ENISA kinacho hudumia mataifa yote yaliyo ndani muungano wa nchi za ulaya katika maswala ya Usalama mitandao.

CAG AONGOZA KIKAO CHA BODI YA UKAGUZI YA UMOJA WA MATAIFA

$
0
0
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa, Bw.Mussa Juma Assad akizungumza wakati wa hitimisho la mkutano wa siku mbili wa Bodi hiyo uliofanyika hapa Umoja wa Mataifa kuanzia Julai 22-23. Kushoto kwake ni Bw. Fransis Kitauli, Mkurugenzi wa Ukauzi wa Nje na Mwenyekiti wa Kamati ya Operesheni za Ukaguzi ( AOC) Akiwa Mwenyekiti wa AOC Bw. Kitauli ambaye alishika nafasi hiyo tangu mwaka 2012 amefanikisha utoaji wa ripoti za ukaguzi za Umoja wa Mataifa kwa miaka mitatu mfululizo.
Wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi kutoka kushoto, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ya India, Bw. Shashi Kant Sharma, Sir Amyas Morse, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka Serikali ya India na Bw. Mussa Juma Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu kutoka Serikali ya Tanzania wakitia saini zao katika ripoti 28 za ukaguzi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa zilizorejewa na kupitishwa na Bodi hiyo wakati wa mkutano wake wa siku mbili. ripoti hizo ni matokeo ya kazi kubwa ya Bodi hiyo.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Bodi wakiwa pamoja na wataalamu wao na wajumbe kutoka Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa.

JARIDA LA WIKI NISHATI NA MADINI TOLEO LA 77


Rais Kikwete amfariji Nehemia Mchechu kwa kufiwa na baba yake

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Marehemu John Edward Mchechu ambaye ni baba wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Bwana Nehemia Mchechu. Rais Kikwete alikwenda nyumbani kwa Mkurugenzi huyo Mbezi Beach jana kumpa pole kufuatia kifo cha Baba yake aliyekuwa anaugua ugonjwa wa kiharusi.Kulia aliyesimama ni Mtoto wa Marehemu Bwana Nehemia Mchechu.
Rais  Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiifariji familia ya marehemu John Edward Mchechu Mbezi beach Dar es Salaam jana jioni.aliyeketi wapili kushoto ni mtoto wa Marehemu ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bwana Nehemia Mchechu. Picha na Freddy Maro

If you are in Arusha arusha today.....

$
0
0
This evening from 06:30pm - 10:30pm Arusha Poetry Club will happen @ the loft of Taste Of Mexico restaurant located opp. Nakumat Supermarket.
Do come with your poems to recite on APC audience and your instruments for a jam session, while your donations are absolutely welcome since its free event.

Karibu sana!

WASIMAMIZI, WAHARIRI NA WADADISI WA UTAFITI WA AFYA YA MAMA NA MTOTO NA MALARIA WA MWAKA 2015,WAPEWA MAFUNZO

$
0
0
Mkurugenzi wa Kinga kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wasimamizi,wahariri na wadadisi wa utafiti wa afya ya mama na mtoto na Maralia yanayofanyika kwa siku 36 katika ukumbi wa YMCA mjini Moshi.
Baadhi ya washiriki.
Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akizindua matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.




Mkurugenzi wa Kinga ,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Neema Rusibamanyila akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Afya ,Zanzibar Halima Maulid Saleh  matokeo muhimu ya utafiti wa tathmini ya utoaji wa huduma za afya nchini Tanzania 2015.

SIMU TV: Uchambuzi wa Magazeti Asubuhi hii

Wafanye Watabasamu kutembelea kituo cha yatima Bagamoyo

DK. MAGUFULI ALIVYOPOKELEWA KIBAIGWA ASUBUHI HII

$
0
0
 Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Mji wa Kibaigwa, Mkoani Dodoma asubuhi hii, wakati akiwa njiani kurejea jijini Dar es Salaam akitokea Mkoani Geita.

KUMBUKUMBU

$
0
0
MODEST SABINUS KWEKA.
14-04-1968 -  25-07-1999

Ni  miaka 16 leo,tokea ulipotuacha gafla baada ya kuitwa a Mungu Baba wa Mbinguni.Hatuna cha kusema ila ni kushukuru kwa kila jambo.

Mdogo wetu Modest, tokea hapo maisha ya Familia yetu hayajawa tena mazuri machache Mungu alitukumbuka lakini kubwa kuliko yote, ni  kuwa tulimpoteza mama yetu mpenzi mwaka jana, mwezi kama huu, tunaamini upo pamoja naye huko juu nyumbani kwa Bwana.Unakumbukwa sana na Mkeo Mpenzi Constancia, Mwanao wa pekee Kelvin,Shangazi yako Sr. Devotha Kweka, Ndugu zako 
Jane, Festo, Eugenia, Elizabeth, Cecilia, na Thadei;Mashemeji zako wote, WaKweka wote wa Narumu, Wamallya wa Manushi, Wafanyakazi wenzako wa Temeke Hospital, wakazi wote wa Temeke Mikoroshini,Ndugu,Jamaa na Marafiki na wote waliokufahamu 

Misa ya Kumbukumbu Itasomwa mwanza leo  Kanisa la Mt. Augustino – Mkolani Mwanza na Burka – Arusha.

“ RAHA YA MILELE UMPE Ee BWANA”

RAIS JAKAYA KIKWETE MGENI RASMI MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na waandishi wa habari kuhusu sherehe za maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa zitakazofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa katika mazoezi katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ya sherehe za Kumbukumbu ya Mashujaa. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

BALOZI WA AFRIKA KUSINI ASHIRIKI KUFANYA USAFI MUHIMBILI

$
0
0
 Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini, Thami Mseleku akifanya usafi katika Wodi (A) ya Watoto iliyopo katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI),ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela.
Muunganishi wa Makazi katika Umoja wa Mataifa,Alvaro Rodriguez (wa kwanza kutoka kushoto),Balozi wa Afrika Kusini nchini,Thami Mseleku (wa pili) wakiwa na baadhi ya wawakilishi wakipokea misaada kwa niaba ya walezi wengine.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI),Dkt.Othman Kiloloma akizungumza na waandishi wa habari juu ya msaada waliopokea kutoka kwa Umoja wa Mataifa,,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela.
Baadhi ya wadau wakiendelea na usafi katika sehemu ya maadhimisho ya  ya siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela. 
 Baadhi ya washiriki waliofanya usafi hospitali ya  Mhimbili Wakiwa katika picha ya pamoja. 

PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII. 


WATANZANIA WATAKIWA KUANGALIA UBORA WA ELIMU YA VYUO VIKUU VYA NJE NA SIO MAJINA-MOLLEL

$
0
0
Na Mwandishi Wetu
Watanzania wametakiwa kuangalia ubora elimu katika vyuo vya nje na sio kuangalia majina ya vyuo hivyo ili ukuweza kupata wataalamu wataosaidia nchi kupata maendeleo.

Hayo aliyasema jana,Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link,Abdulmaliki Mollel katika maonesho ya  Elimu ya Vyuo Vikuu vya Ndani na Nnje ya nchi yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mollel amesema yeye akiwa wakala wa vyuo vikuu vya nje anatambua vyuo walivyoenda watanzania kusoma hawakumuangusha kutokana na kujituma kwao pamoja na mazingira rafiki ya kusomea katika vyuo hivyo.

Amesema watu wanaokwenda katika vyuo kwa kuangalia majina wanarudi na kuwa hawana msaada wa elimu walioipata nje na kulazimika nchi kuchukua wataalam kutoka nje wenye uwezo kutokana na vyuo vyao na kuacha watanzania waliopata elimu katika vyuo vyenye majina lakini havina elimu bora.

Mollel amesema kuna vyuo vingi nje lakini suala la kuangalia ubora wa elimu inayotolewa na mazingira ya kusomea kutokana na baadhi ya watu waliosoma wamekuwa wakiiga utamaduni mwingine na kuingiza nchini na kushindwa kuendana na utamaduni wa ndani na kusababisha kukosa ajira.

Mollel amewataka watanzania kutumia Global Education Link katika kuweza kuwapa vyuo bora ambavyo itasaidia vijana kupata elimu bora kutokana na uwezo wa vyuo husika.

Aidha amesema Global Education Link imekwenda mbali zaidi kwa baadhi ya vyuo vya nje kuingiza kozi katika vyuo vya ndani ikiwemo kozi ya Petrol ,Gesi.

Amesema  anafanya kazi na vyuo 10 vya nje ambavyo vinazalisha elimu bora yenye kumsaidia mtanzania katika kuweza kuongeza uwezo wa kitaalam katika nchi.

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa shirika la taifa la bima (NIC), Sam Kamanga akipata maelezo kutoka kwa afisa masoko mwandamizi wa shirika la taifa la bima (NIC),Joyce Mswia katika maoneho ya wiki ya elimu ya vyuo vikuu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Da es Salaam.
Mkurugenzi mtendaji wa Global Education  Link akiwapa maelezo wananchi alipotembelea banda la Global Education  Link katika maoneho ya wiki ya elimu ya vyuo vikuu katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Da es Salaam.

Rais Kikwete aongoza mahafali ya Tatu ya Chuo Cha Ulinzi wa Taifa (NDC) Jijini Dar leo

$
0
0
Amiri Jeshi Mkuu ,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kozi ya Tatu ya Chuo Cha Ulinzi wa Taifa (National Defence College NDC) huko Kunduchi jijini Dar es Salaam leo.Aliyeketi Pembeni ya Rais kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange na aliyeketi pembeni ya Rais Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Gaudence Salim Milanzi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na medali ya dhahabu ya mwanafunzi bora katika kozi ya tatu ya National Defence College(NDC) Brigedia Jenerali Aloyce Damian Mwanjile wakati wa mahafali iliyofanyika chuoni huko Kunduchi jijjini Dar es Salaam leo.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange baada ya kutunuku vyeti na zawadi kwenye mahafali ya kozi ya tatu ya National Defence College iliyofanyika Kunduchi jijini Dar es Salaam leo ambapo jumla ya wanafunzi 42 walihitimu masomo yao.(picha na Freddy Maro).

Tabora Wanufaika na Mafunzo ya ULINGO – Tanzania Women Crossparty Platform (TWCP)

$
0
0
ULINGO WA WANAWAKE WANASIASA – Tanzania Women Crossparty Platform (TWCP) ni shirika lisilo la kiserikali lililoendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watia nia wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu katika nyadhifa mbalimbali za uongozi wa nchi ikiwa ni kuchangia kutoa elimu inayolenga kuleta usawa kama haki msingi ya Mtanzania. 
Mafunzo hayo yamedhaminiwa na UNWomen.
Mafunzo hayo yamewanufaisha walengwa husika kwa kujipatia elimu hiyo huku wawezeshaji wakiwa ni Hilda Stuart Dadu na Emmiliana Msaguka waliohakikisha wanawafikia watiania katika mkoa wa Tabora na kuendesha mafunzo hayo pale Student Center.
t-wcp (2)
Wanufaika na watia nia za kugombea nafasi mbalimbali na wa vyama tofauti tofauti wakifuatila mafunzo hayo yaliyotolewa na Hilda Stuart Dadu kutoma TWCP
t-wcp (3)
Watia nia wakichukua kumbukumbu za mafunzo hayo mapema leo hii
t-wcp (9)
Picha ya pamoja ya wanufaika wa mafunzo ya ULINGO na wawezeshaji wa mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo watia nia za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi. Mafunzo hayo yamekuja wakati huu ambao ndiyo haswa muda mwafaka wa uchaguzi mkuu wa ngazi za udiwani, ubunge na Urais.


Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images