Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 918 | 919 | (Page 920) | 921 | 922 | .... | 3284 | newer

  0 0


  0 0

  Chuo cha  Waislam Morogoro kimeshiriki maonyesho ya vyuo vikuu yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere maarufu kama Sabasaba jijini Dar es Salaam kilianzishwa mwaka 2005 na mpaka sasa kina miaka 10 kinatoa kozi mbalimbali kwa wanafunzi wanaojiunga katika chuo hicho.Afisa mahusiano wa chuo cha Waislam Morogoro, Ngaja Mussa akimwonyesha Mkufunzi mkuu wa chuo cha Waislam Morogoro, Faraji Tamim wakati wa maonyesho ya wiki ya vyuo vikuu yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu nyerere jinini Dar es Salaam.
  Mkufunzi wa chuo cha Waislam Morogoro wa Lugha ya Kichina katika chuo hicho, Sun Xiaofei akizungumza na wateja mbalimbali waliotembelea katika maonyesho ya vyuo vikuu vya hapa nchini na nje ya nchi.

  0 0

   Hatua ya makundi ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015) inatarajiwa kukamilika kesho jumapili kwa michezo miwili kupigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku macho na masikio ya wapenzi wa soka yakiwa katika mchezo kati ya Yanga SC dhidi ya Kahrtoum ya Sudan.

  Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 10 kamili jioni, ambapo Yanga SC watashuka dimbani kusaka ushindi wake wa tatu mfululizo katika michuano hiyo, hali kadhalika timu ya Khartoum ikihitaji ushindi wake wa tatu katika mechi hiyo inayosuburiwa kwa hamu kubwa.

  Kuelekea katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa wa vuta ni kuvute kufuatia timu ya Yanga SC kuhitaji ushindi katika mchezo huo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuongoza kundi lake, huku pia Khartoum wakihitaji ushindi katika mchezo huo ili kuweza kuongoza kundi A.
   Utamu wa mchezo huo unaletwa na makocha wa timu hizo mbili, Hans Van der Pluijm wa Yanga na James Kwesi Appiah wa Khartoum ambao wote wamewahi kufanya kazi nchini Ghana kwa vipindi tofauti.

  Hans ambaye ametwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanznaia msimu huu, anasifika kwa kucheza soka safi la kasi na kushambulia muda wote, huku akiwa na mafanikiko nchini Ghana baada ya kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na timu ya Berekum Chelsea miaka miwili iliyopita.

  Kwa upande wa James Appiah alikuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ghana, ambapo alikua kocha wa kwanza mwafrika kuipeleka timu ya Afrika katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Brazil mwaka 2014.
   Licha ya kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia, Appiah pia aliwahi kuichezea timu ya Taifa ya Ghana kwa miaka 7 akiwa nahodha, pia aliiwezesha timu ya Vijana ya Ghana chini ya miaka 23 kufuzu kwa fainali za Michezo ya Afrika na kutwaa Ubingwa huo mwaka 2011.

  Katika kikosi chake cha Khartoum kinachoshiriki michuano ya Kagame, Appiah amejumuisha wachezaji wa kimataifa kutoka nchini Cameroon na Ghana, na malengo yake ni kutwaa Ubingwa wa Kagame Cup kwa mara ya kwanza.

  Mpaka sasa Khartoum inaongoza kundi A ikiwa na pointi 7 sawa na Gor Mahia lakini Wasudani hao wakiwa juu kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, huku Yanga wakishika nafasi ya tatu wakiwa na pointi sita.

  Kabla ya mchezo huo kati ya Yanga SC dhidi ya Khartoum kutakua na mchezo wa kwanza utakaoanza majira ya saa 8 kamili mchana kati ya Gor Mahia ya Kenya dhidi ya  Telecom ya Djibout.

  Mpaka sasa timu zilizofuzu hatua ya robo fainali ni Khartoum, Gor Mahia na Yanga kutoka kundi A, huku APR na Al Shandy zikitoka kundi B, na Azam FC ikiwa timu ya kwanza kufuzu kutoka kundi C, na timu mbili kati ya Adama City, KCCA na Malakia zitaingia hatua ya robo ya fainali.

  Hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Kagame itachezwa Jumanne, Julai 28 na Jumatano Julai 29 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

  0 0

  Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Kakuni wilayani Mlele wakitoka kufanya usafi wa barabara zinazozunguka shule yao mpya waliyojengewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye kijiji cha Kibaoni Julai 25, 2015.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  0 0

  MTOTO  mwenye kipawa cha ajabu katika kutoa ushauri  wa kujijengea uwezo wa kujiamini  anayezidi kujipatia umaarufu mkubwa duniani,  Lonnie Hudson  maarufu kama ‘King Nahh’(Pichani), ametua  jijini Dar es Salaam , leo.
  King Nahh aliambatana na baba yake mzazi , Nyeeam Hudson  ambapo wapo nchini kwa mwaliko wa  taasisi isiyo ya kiserikali ya Wisdom Partners.
  Kesho mtoto huyo atafanya  kongamano kubwa  la watoto na wazazi  katika Ukumbi wa Urafiki ambapo nia na madhumuni ni kuamsha hisia za  watu ambao wamekata  tamaa katika masuala mbalimbali na kukosa kujiamini katika maamuzi.
  “Najisikia furaha kuja Tanzani. Ninaamini nina jukumu kubwa la kufanya hapa. Hususani  kwa watoto ambao bado hawaamini kuwa wanaweza kubadili hisia zao, kujiamini na  kushiriki katika masuala mazima ya maendeleo,” alisema.
  King Nahh aliongeza kwamba, hisia za watu wengi hivi sasa zimelemaa kutokana na kuishia kulaumu  matatizo na vikwazo bila kutafuta suluhu ya matatizo yao.
  “Kila mtu analaumu. Wa kwanza atalaumu, wa pili, wa tatu, wa nne, wa tano mpaka wa sita. Wote wanaishia kulaumu jambo moja. Wengine wanaamini kuwa hawezi kitu. Ila ukweli ni kwamba pale unapokuwa huwezi kitu kuna kitu unaweza kufanya. Jamii ibadilike. Iache kulaumu,”alisema mtoto huyo na kushangaza watu waliokwenda kumlaki.
  Mkurugenzi wa taasisi ya Wisdom Partners, Cynthia Henjewelle, alisema kuwa dhamira kubwa ya kumleta mtoto huyo nchini ni kusaidia kubadili hisia za jamii hasa watoto ili waweze kujiona kuwa sehemu ya jamii.
  “King Nahh ni miongoni mwa watoto wanaosifika hivi sasa duniani kutokana na  kipawa  alichonacho. Wazazi wawalete watoto kesho  Urafiki,  ili waweze kubadilishana mawazo. Pia wazazi wanakaribishwa kumsikiliza mtoto huyu kuanzia saa tano asubuhi,”alieleza Henjewele.

  0 0

  Mtaalamu wa Mradi wa Kilimo chenye tija Tanzania (TAPP ), Mussa Madurufu ( anayenyosha mikono) akitoa elimu ya namna ya kuendesha wa kilimo cha bustani ya nyanya kwa njia ya teknolojia mpya ya umwagiliaji kwa njjia ya matone wakati wa maadhimisho ya siku ya wakulima Julai 20, 2015 katika bustani ya vipando vya mboga na matunda ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), maonesho yaliyodhaminiwa na Asasi kilele ya sekta binafsi yenye lango kuu la kuhamasisha maendeleo ya kilimo cha mazao ya horticulture Tanzania (TAHA),TAPP ,Mradi wa Tafiti Bunifu za Kilimo (iAGRI), na SUA.
  Ulaji wa matunda ni muhimu kwa afya ya mwili wa binadamu.
  Baadhi ya Wakulima waliokuwa wakihudhuria maonesho ya wakulima na teknolojia mpya ya umwagiliaji kwa njjia ya matone wakipita kuangalia kipando cha bamia , maonesho hayo yalifanyika julai 20, 2015 , SUA na yalidhaminiwa na Asasi kilele ya sekta binafsi yenye lango kuu la kuhamasisha maendeleo ya kilimo cha mazao ya horticulture Tanzania (TAHA),TAPP ,Mradi wa Tafiti Bunifu za Kilimo (iAGRI), na SUA.


  0 0

   Kutoka kushoto ni One Mic akiwa pamoja na Dj MO ndani ya studio ya Kilimanjaro zilizopo Beltsville, Maryland nchini Marekani.
   Mcheza sinema wa Bongo Movi, Charles Magali ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za dansi(kushoto) akiwa na mwenyeji wake Kenyatta wakiwa ndani ya Studio ya Kilimanjaro.
   Charles Magali akifanyiwa mahojiano na matangazaji mahairi wa Radio Mubelwa Bandio ndani ya studio ya Kilimanjaro iliyopo Beltsville, Maryland.
   Mtangazaji mahiri wa Radio na muuliza maswali tata, Mubelwa Bandio akimfanyia mahojiano mcheza sinema wa Bongo movi Charles Magali siku ya Ijumaa July 24, 2015 alipotembelea studio hiyo iliyopo Beltsville, Maryaland.
  Mahojiano yakiendelea.

  0 0


  0 0


  SAM_4216Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akizungumza katika uchaguzi wa kumpata Mbunge pamoja na Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA)jijini Arusha ambapo aliibuka kidedea kwa kura 255 sawa na asilimia 93.06% (Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

  SAM_4210Mbunge viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joyce John Mukya alipata kura 39 sawa na asilimia 73.6% katika kinyang'anyiro hicho hivyo kumfanya kuwa Mbunge wa viti maalum,aliwataka wajumbe wa mkutano huo kuvunja makundi ili kuhakikisha chama kinashinda katika uchaguzi wa Urais,Ubunge na udiwani 
  SAM_4212 Mgombea kupitia chama cha Demokrasia na maendelao (CHADEMA)Noel Olevaroya akizungumza mara baada ya kutangazwa kushika nafasi ya pili  kwa kupata kura 13 sawa na asilimia 4.74% katika kinyang"anyiro hicho ambapo aliwashukuru wajumbe wa mkutano huo na kuhaidi kumpa Mbunge Lema shilingi laki tano kwaajili ya kampeni ya kuhakikisha  chama hicho kinapata ushindi wa kishindo
  SAM_4147Wagombea ubunge viti maalum Mkoa wa Arusha wakisubiria kuingia kujinadi kwa wajumbe wa mkutano. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0

  After more than 20 years of successful operations in Europe and Africa distributing Two-Way Radio Communications, Airsys is expanding its operations to Africa to work with dealers serving private and public sector customers as well as UN and Humanitarian organisations. 
  Airsys therefore is setting up office in East Africa to serve as a distribution point of its Two-Way Radio Communication Equipment and Solutions in East Africa Region and will serve dealers on the Eastern African market.
  Airsys will distribute a complete range of Two-Way Communication Technology. In addition Airsys will offer sales, marketing and technical support to dealers. This will including training and capability building in partnership with the dealers serving customers in the Eastern African market. For more CLICK HERE

  0 0

  Na Willliam Kaijage

  UTANGULIZI (PREAMBLE)
  •Mwanzoni mwa mwezi wa 7 ndio nusu ya mwaka. Zinakuwa zimepita siku 182 (au 183 kwa mwaka mrefu) na kubaki siku 182.
  •Yafuatayo ni matukio makubwa ya muziki wa dansi kwa nusu ya kwanza ya mwaka huu wa 2015

  BENDI MPYA
  •Tarehe 31-Jan-2015, BMM Classic Band, ilizinduliwa katika ukumbi wa BMM Mwenge, opposite TRA.
  •Tarehe 21-Feb-2015,  JJ Band yazinduliwa katika ukumbi wa. JJ Band ni bendi dada ya Skylight Band itakayokuwa inatumbuiza mjini Mwanza katika hotel ya Jembe ni Jembe Resort.
   •Tarehe 06-Mar-2015 (Ijumaa), Ruby Band ilitambulishwa rasmi katika ukumbi wa Coco Beach Pub ambapo pia ilizindua video ya wimbo mpya wa “Noma”.
  •Tarehe 18-Jul-2015 (Jumamosi), Stars Band yazinduliwa katika ukumbi wa Mzalendo Pub. Bendi hiyo inaongozwa na mwanamuziki Aneth Kushaba aka “AK47” aliyekuwa Skylight Band. Meneja wa bendi ni mpiga drums James Kibosho.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Julai 25, 2015.
  Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey akiweka sahihi kwenye hati baada ya kuapishwa kuwa kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Julai 25, 2015.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Charles Magali akiwa ndani ya Kilimanjaro Studio zinazomilikiwa na Vijimambo Radio, Kwanza Production na NesiWangu Media
  Ijumaa ya Julai 24, 2015, mwigizaji na mwimbaji wa muziki nchini Tanzania Charles Magali alipata fursa ya kutembelea studio zetu zilizopo Beltsville Maryland. Hapo akazungumza nasi kwa ufupi
  Karibu umsikilize akihojiwa na Mbunifu na Mtayarishaji wa kipindi hiki Dj Luke Joe na Mubelwa Bandio

  0 0

  Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini Priscus Tarimo akijinadi mbele ya wajumbe wa CCM kata ya Mawenzi.
  Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Edmund Rutaraka akiomba kura mbele ya wajumbe wa CCM kata ya Mawenzi.
  Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Davis Mosha aijinadi mbele ya wajumbe wa CCM kata ya Mawenzi.
  Baadhi ya wajumbe wa Chama cha Mapinduzi kata ya Mawenzi wakiwasikiliza wagombea.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wilaya ya Moshi mjini wakiwa katika mkutano maalumu wa kumchagua mtia nia atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi mjini.
  Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro na Mbunge anayemaliza muda wake,Philemoni Ndesamburoakizungumza wakati wa mkutano huo.
  Jafary Michael aliye chaguliwa na Chadema kupeperusha Bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba katika kuwania kiti cha Ubunge jimbo la Moshi mjini.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Rais wa Jumuiya ya Watanzania Washinton Ndg Iddi Sandaly akiutambulisha Ujumbe wa Madaktari 17 Diaspora, waliofika Zanzibar kutoa Tiba ya Maradhi ya Saratani ya Matiti, Kisukari na Meno akitowa maelezo wakati walipofika katik Chuo cha Elimu ya Afya Mombasa Zanzibar, na kutowa Elimu ya kutambua Saratani ya Matiti kwa Kinamama. na kutowa huduma ya uchunguzi wa Meno.
  Rais wa Jumuiya ya Wanawake Afrika Washington (Africa Womens Cancer Awereness Association ) Dr Ify Anne Nwabukwu, akiutambulisha ujumbe wa Madaktari wa maradhi mbalimbali waliowasili Zanzibar kwa ajili ya kutowa huduma kwa wananchi wa Zanzibar ikiwa ni kusaidia Wafrika wenzao walioko Afrika.    

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe akishangilia kwa staili ya aina yake baada ya kuifungia timu yake bao pekee katika mchezo wa Kombe la Kagame uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kushoto ni  mshambuliaji wa timu hiyo, Malimi Busungu. (Picha na Francis Dande).
   Golikipa wa Khartoum ya Sudan, Mohamed Ibrahimakiokoa moja ya hatari langoni mwake.
   Simon Msuva akichuana na beki wa Khartoum.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  MKURUGENZI wa Msama Promotions, Alex Msama  amewaita Maaskofu na viongozi wengine wa dini katika uzinduzi wa albamu tatu za mwimbaji nguli Bonny Mwaitege zinazotarajia kuzinduliwa Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Kwa  mujibu  wa  Msama  ambaye  ni  mdhamini  wa  uzinduzi  huo, Maaskofu watafikisha  ujumbe wa neno la Mungu  kwa karibu zaidi baada ya waimbaji kumaliza kazi yao jukwaani.

  Msama alisema uzinduzi huo unatarajia kusindikizwa na waimbaji mbalimbali wa Tanzania na nje lengo likiwa ni kufanikisha uzinduzi mahiri wa albamu hizo. Msama alisema pamoja na uzinduzi huo kusindikizwa na waimbaji mahiri pia, waimbaji chipukizi watamsindikiza Mwaitege ambaye hivi sasa anaendelea na mazoezi kuelekea uzinduzi huo.

  Aidha Msama alisema hivi sasa muimbaji huyo pia anamalizia kurekodi baadhi ya nyimbo zilizomo kwenye albamu hizo katika majiji ya Mwanza, Arusha, Mbeya  na Nairobi. Msama alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa mashabiki wa muziki wa injili kujiandaa na uzinduzi huo ambao utakuwa ni wa aina yake.

  "Maandalizi makubwa kuelekea uzinduzi wa Mwaitege yameshafanyika, kilicho mbele ni uzinduzi wa hali ya juu, mashabiki wakae mkao wa kula," alisema Msama na kuongeza. "Uzinduzi wa Mwaitege utakuwa ni wa aina yake kwa sababu maandalizi yake kwa sababu yamefanywa kwa ustadi mkubwa, mashabiki watarajie kazi bora zaidi kutoka kwa muimbaji huyo," alisema.    Bonny Mwaitege anatamba na nyimbo mbalimbali kama Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, Fungua Moyo wako, Njoo  uombewe na  Yesu yupo.

older | 1 | .... | 918 | 919 | (Page 920) | 921 | 922 | .... | 3284 | newer