Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

UN YAKANUSHA UZUSHI WA JAMII FORUM NA INDIAN OCEAN NEWSLETTER

$
0
0
IMG_7871
Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mipango ya maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez.

UMOJA wa Mataifa umetaka vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa kuhakikisha vinatoa taarifa zao kwa usahihi kuhusu maandalizi ya uchaguzi na uchaguzi wenyewe.

Kauli hiyo imetolewa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa Dar es salaam, kufuatia taarifa iliyochapishwa na jarida moja kwamba UN inataka kujitoa katika kusaidia mandalizi ya uchaguzi nchini Tanzania.

Aidha alisema kwamba si kweli kuwa Umoja wa Mataifa haujaridhishwa na mwenendo wa maandalizi ya uchaguzi nchini Tanzania na kwamba Umoja huo utaendelea kushirikiana na serikali na vyombo vingine vya uchaguzi kuhakikisha uchaguzi unakwenda vyema.

Indian Ocean Newsletter ya Julai 10 mwaka huu ilichapisha habari iliyoandikwa na kichwa cha habari “State is facing electoral commissions negligence” na kusema kwamba Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mipango ya maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bw. Alvaro Rodriguez, haridhishwi na mwenendo wa maandalizi ya uchaguzi na uchaguzi wenyewe na kutishia kuondoa msaada wa mamilioni unaoratibiwa na UNDP kutoka kwa wahisani mbalimbali.

Aidha Julai 15, 2015, mtandao wa Jamii Forum ilitafsiri habari hiyo kwa Kiswahili na kuitawanya kwa wasomaji wake.

Taarifa ambayo sio sahihi iliyochapwa na Jamii forum hii hapa link: http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/885659-un-yaeleza-kutoridhishwa-kwake-na-vurugu-za-uchaguzi-nchini-tanzania.html#post13289399
Ukweli ulivyo
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini hajawahi kukutana wala kuzungumza na watu wa Indian Ocean Newsletter .

Aidha taarifa zilizotolewa na kijarida hicho na tafsiri yake iliyowekwa mtandao wa kijamii wa Jamii Forums hazikujengwa katika ukweli.

Pia Umoja wa Mataifa utaendelea kufanyakazi na mamlaka za Tanzania na wananchi wake na kuwa Uhusiano kati ya Umoja wa Mataifa na mamlaka za uchaguzi nchini Tanzania na Jumuiya ya kimataifa inayofadhili mradi wa DEP unawasilisha mahusiano muhimu miongoni mwa wadau mbalimbali wanaotaka kuwapo na uchaguzi huru na wa amani.

Alisema katika makubaliano kuna kamati ya mradi inayojumuisha wadau wote na ina wajibu kuongoza na kutoa mwongozo wa utekelezaji mradi huo kimkakati.

Maamuzi ya mradi huo hufanywa na kamati hiyo na kamati ya ufundi ya mradi iliyopo Bara na Zanzibar.

Kutokana na ukweli huo Umoja wa Mataifa unavitaka vyombo vya habari vya kitaifa na Kimataifa kuhakikisha kwamba inatoa taarifa za ukweli na za usahihi kipindi hiki cha maandalizi na uchaguzi wenyewe.
Biometric Voter Registration (BVR)   Machines operator, Kheri Mkali attends Rebeca Kimu at Bunju A in Dar es Salaam yesterday during the trial registration. PHOTO|VENANCE NESTORY Biometric Voter Registration (BVR) Machines operator, Kheri Mkali attends Rebeca Kimu at Bunju A in Dar es Salaam yesterday during the trial registration. (LIBRARY PHOTO|VENANCE NESTORY).


NMB YATOA MSAADA WA MADAWATI 570

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya  ya Busega Mkoani Mwanza Bw. Paulo Mzindakaya , akimpa mkono wa shukurani Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB Bw. Waziri Barnabas(kulia), baada ya kukabidhi  madawati 240 yenye thamani ya shilingi milioni .... yaliyotolewa na benki ya NMB ukiwa ni msaada kwa  Shule za Msingi Nyashimo na Nasa Wilayani Busega pamoja na Sukuma na Simakitongo Wilaya ya Magu ili kupunguza uhaba wa madawati katika shule hizo. Kila shule imepata madawati sitini.
 Mkuu wa Wilaya  ya Musoma Mkoani Mara Bw. Zelothe Stephen , akimpa mkono wa shukurani Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB Bw. Waziri Barnabas(kushoto), baada ya kukabidhi  madawati 330 yaliyotolewa na benki ya NMB ukiwa ni msaada kwa  Shule za Msingi Bwai, Kiriba, Chanyahuru na Busumi pamoja na shule ya Sekondari Kiriba zilizopo Musoma vijijini ili kupunguza uhaba wa madawati katika shule hizo. Kila shule imepata madawati hamsini na tano.
Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Kwibara wakiwa wameki kwenye madawati waliyokabidhiwa na NMB.

FASTJET KUZINDUA SAFARI YA LILONGWE-MALAWI JULAI 27 MWAKA HUU

$
0
0
DSC_0263Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro (kulia) akifafanua jambo kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa mkutano wa wandishi wa habari akielezea kampuni hiyo ilivyoweza kusaidia sanaa kwa Tanzania na Afrika. Kushoto kwake ni CEO wa ZIFF, Prof. Martin Mhando.
Na Andrew Chale.
Shirika la ndege la Fastjet limeendelea kupanua wigo wake kwa kuanzisha ‘rout’ zaidi za safari zake ikiwa ni kuunganisha Afrika kuwa moja.

Kwa mujibu wa Afisa Mahusiano na Masoko wa Fastjet, Lucy Mbogoro anasema kampuni hiyo inatarajia kuizindua rasmi safari zake kwa kwenda, Malawi.
“Julai 27, Fastjet tutazindua rasmi safari ya kutoka Dar es Salaam-Lilongwe Malawi. Hii inakuwa ni ‘rout’ yetu ya tano katika safari zetu za Kimataifa ndani ya Afrika lengo ni kufikia nchi mbalimbali za Afrika.” Anabainisha Lucy Mbogolo.

Hata hivyo anabainisha kuwa, wanaendelea kutoa elimu mbalimbali kwa wateja wao juu ya huduma ya Fastjet Ambayo imeendelea kuwa bora zaidi kila kukicha huku akisisitiza kwa wateja kufanya ‘booking’ mapema pamoja na kuzielewa sheria na taratibu za usafirishaji wa anga.

Awali Fastjet ilianzia na safari za ndani za kusafirisha abiria ‘rout’ za Mwanza – Dar, Kilimanjaro – Dar na Mbeya – Dar sasa hivi wamevuka mipaka zaidi kwa nchi za Afrika zikiwemo, kati ya Dar – Johannesburg, Dar – Lusaka, Dar – Harare,Dar – Entebbe nah ii inayotarajiwa kuzinduliwa wiki ijayo ya Dar-Lilongwe.

Aidha, Lucy Mbogoro alibainisha kuwa Fastjet itaendelea kusaidia kukuza sekta ya sanaa nchini na Bara la Afrika kwa kuwaunganisha wadau wa sekta hiyo ikiwemo wasanii wa filamu, muziki na sanaa kwa ujumla.

Lucy Mbogoro anasema hayo ambaapo kwa mwaka huu ni mwaka wa pili mfululizo wakiendelea kudhamini tamasha la Filamu za nchi za majahazi maalufu kama ZIFF. 

TAARIFA KWA UMMA KUHUSIANA NA TAARIFA ZISIZO NA UKWELI DHIDI YA WASHIRIKI WA TMT 2015

$
0
0
Picha ya Post iliyopostiwa na Kijana ajulikanae kama Raffayel Mombury.
Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao ni waandaaji na waendeshaji wa shindano la Kusaka vipaji vya Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo linaendelea kufanyika huku washiriki watano Wakiwa washaenguliwa katika shindano hilo Kutokana na Kutokupata kura za kutosha kutoka kwa watazamaji wa Kipindi hiko mahiri kinachorushwa na kituo cha runinga cha ITV siku ya jumapili saa tatu na nusu usiku.
Proin Promotions tunasikitika kusema kuwa kuna habari ambazo sio za kweli ambazo zimepostiwa katika ukurasa wa facebook wa kijana mmoja ajulikanae kwa jina la Raffayel Mombury ambae amepost taarifa hiyo yenye kichwa cha Habari "WASHIRIKI WA TMT 2015 WAFUMANIWA WAKINGONOKA" kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu, Sisi kama Proin Promotions ltd tunapenda kusema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na sura hizo hatuzitambui na wala sura zinazoonekana katika post hiyo sio za washiriki wetu wa TMT 2015 na hazijawahi kuwa. 
Kutokana na post hiyo ambayo yenye mlengo wa kuichafua Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao ndio waandaaji na waendeshaji wa shindano pamoja na mradi mzima wa TMT ambao unaaminika Tanzania Nzima na Nje ya Tanzania tumepata usumbufu mwingi kutoka kwa wapenzi wa Shindano hilo pamoja na wazazi wa Washiriki waliobakia. Tunapenda kusema kuwa kiukweli taarifa hizo zimetuletea usumbufu mkubwa sana na kupelekea kuvunja imani kwa watazamaji wetu na wapenzi wa vipindi vyetu, Sisi kama Proin Promotions tunawaomba Watanzania na Wapenzi wa TMT  kuzipuuza taarifa hizo na hakuna kitu kama hiko kwasababu Nyumba wanayoishi washiriki wa TMT 2015 imezingatia maadili makubwa na kuwepo kwa usimamizi wa matron katika kambi hiyo.
Proin promotions tunasema kutokana na taarifa hizi kutokuwa na ukweli wowote tunaahidi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu huyu aliyesambaza taarifa hizi za uongo na zilizotuletea usumbufu mkubwa sana katika jamii inayofuatilia shindano hili na kupelekea kupoteza imani kwa jamii.

Imetolewa na
Idara ya Mahusiano ya Umma
Proin Promotions Ltd

IN LOVING MEMORY OF OUR BELOVED FATHER ON HIS 4TH DEATH ANNIVERSARY

$
0
0
Dear Dad, our heart still aches in sadness, our silent tears still flows,
For what it meant to loose you, No one will ever know.
Even though you can’t be with us, were truly not apart,
Until the final breath we take, you will be living in our hearts.
Dearest Dad, to hear your voice and see your smile and to just sit and talk to you would be our dearest wish. 

Just know that we are thinking about you on your 4thAnniversary since you left us.
Still remembered by your Dearest Wife, all your Children, relatives, Family and Friends.
May your Spirit continue 
to live on forever, Amen

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI.

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
                                                 JESHI LA POLISI TANZANIA

“PRESS RELEASE” TAREHE 23.07.2015.

·    MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBARALI.

·        JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA POMBE KALI NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU.

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE KATIKA SHULE YA SEKONDARI MSHIKAMANO ILIYOPO KATIKA WILAYA YA MBARALI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GIDION MPUGI (20) MKAZI WA UHAMBULE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.618 CQH AINA YA MITSUBISHI FUSO ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA FRANK EVARISTO NYOTA (36) MKAZI WA UBARUKU.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 22.07.2015 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAJEN, KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA NA UPELELEZI UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA NA WATUMIAJI WENGINE VYA VYOMBO VYA MOTO KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO MVYA MOTO IKIWA NI PAMAOJA NA KUFUATA NA KUZINGATIA SHERIA, ALAMA NA MICHORO YA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


KATIKA TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA MAKUNGURU JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA AGATHON SANGA (18) AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NCHINI AINA YA DOUBLE PUNCH KATONI 04, BOSS KATONI 02 NA CHARGER KATONO 01.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 22.07.2015 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MAENEO YA KABWE, KATA YA MAANGA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.

KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LIMEKAMATA VIPODOZI MBALIMBALI VILIVYOPIGWA MARUFUKU NCHINI BAADA YA KUFANYA MSAKO KATIKA NYUMBA MOJA HUKO KATIKA MAENEO YA ITEZI, KATA YA ITEZI, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA  MKOA WA MBEYA.

KATIKA MSAKO HUO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 22.07.2017 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI, VIPODOZI AINA YA BUTA SOAP PIECE 50, EXTRA CLAIR PIECE 18 NA CAROLOGHT PIECE 12 VILIKAMATWA BAADA YA MTUHUMIWA KUWAONA POLISI NA KUKIMBIA NA KUVITELEKEZA VIPODOZI HIVYO. MSAKO MKALI UNAENDELEA KUMTAFUTA MTUHUMIWA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA UINGIZAJI/USAMBAZAJI NA UUZAJI WA POMBE KALI NA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU NCHINI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.

Imesainiwa:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

KONGAMANO LA TAMASHA LA 20 LA UTAMADUNI WA MZANZIBAR LAFANYIKA JANA

$
0
0
Mshereheshaji katika Kongamano la Tamasha la 20 la Utamaduni wa Mzanzibar Otman Mohd (Makombora ), akitoa maelezo mafupi ya kongamano litakavyokuwa katika Ukumbi wa Suza mjini Zanzibar.
 Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Tamasha la 20 la Utamaduni wa Mzanzibar wakisikiliza kwa makini mada inayowasilishwa katika Ukumbi wa Suza mjini Zanzibar.
 Katibu mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar Bimwanahija Ali Juma ambae ni mgeni rasmi akitoa hotuba ya ufunguzi wa Tamasha la 20 la Mzanzibari katika Ukumbi wa Suza mjini Zanzibar.
 Mtoa mada Bimwanahamisi Hamadi akiwasilisha mada ya Athari za Utalii katika kuendeleza  Utamaduni katika Tamasha la 20 la Mzanzibari katika Ukumbi wa Suza mjini Zanzibar.
Mmoja kati ya washiriki wa Tamasha la 20 la Mzanzibari Abdalla Alawi akichangia mada iliowasilishwa katika Tamasha hilo  katika Ukumbi wa Suza mjini Zanzibar.

PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

SAFARI YA KUJITAMBULISHA YA MGOMBEA URAIS WA CCM DKT MAGUFULI KUTOKA CHATO MPAKA DODOMA

$
0
0

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Rajab Luhwavi akimkaribisha  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  awasalimie wananchi,awashukuru na kujitambulisha kwa wananchi hao waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM Manyoni mkoa wa Singida.
  Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli  akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwa wingi nje ya ofisi za CCM Manyoni mkoa wa Singida. 
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli(kulia) akisalimiana na aliyekuwa Mbunge wa Nzega Vijijini Dk. Hamisi Kigwangala
 Hussein Bashe ambaye ametia nia ya kugombea ubunge jimbo la Nzega Mjini akisalimiana na Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli mjini Nzega.
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasalimu wakazi wa Nzega kwenye mkutano uliofanyika nje ya ofisi ya CCM wilayani hapo, ambapo aliwaambia Wananchi kuwa amefarijika na mapokezi mazuri na amewaahidi kurudi tena wakati wa kampeni zitakapoanza..
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisaini vitabu vya  wageni Ofisi za CCM ndani ya mji wa Manyoni  mkoani Singida alipokuwa akipita kuwashukuru Wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea na kujitambulisha kwao akiwa anatokea jimboni kwake Chato akirejea jijini Dar kwa njia ya barabara.
 Wananchi wa Igunga wakiwa na Bango lao wakimkaribisha Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili maeneno hayo kuwashukuru na kujitambulisha kwao akiwa anatokea jimboni kwake Chato akirejea jijini Dar kwa njia ya barabara.

Wananchi wa Ikungi wakiwa wamelizunguka gari la Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi CCM Dk.John Pombe Magufuli na kufunga barabara wakimtaka awasalimie tu ndipo aendelee na safari yake.



YALE YALEEE.....

$
0
0
 Kameya ya Globu ya Jamii ilifanikiwa kuzinasa taswira hizi za vijana hawa wakining'inia kwenye madirisha ya Daladala huku Kondakta wake akiunana nao. Hatuombei mabaya yatokee lakini yakitokea itakuwa ni jambo la bahati mbaya kwe??? Wazee wa Feva liangalieni jambo hili kwa jicho la ziada.

WIZARA YA MAMBO YA NJE YAMUAGA RASMI BALOZI WA UBELGIJI ALIYEMALIZA MUDA WA KAZI NCHINI

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akitoa hotuba wakati wa kumuaga Balozi wa Ubelgiji ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Adam Koeler huku Balozi huyo (wa kwanza kulia waliketi) na wageni waalikwa wakimsikiliza. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Julai, 2015. Katika hotuba yake Balozi Kasyanju alimsifu Balozi Koeler kwa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji.
Balozi Koeler nae akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga. Katika hotuba yake Balozi huyo aliishukuru Serikali ya Tanzania  kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini  na kusifu ukarimu wa Watanzania.

Balozi Kasyanju kwa pamoja  na Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Congo (DRC), Mhe. Juma Halfan Mpango na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodrigues wakimsikiliza Balozi Koeler (hayupo pichani) akihutubia.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bunndala (katikati) akiwa na wageni waalikwa wengine wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.



















WAZIRI MKUU PINDA KUTANA NA WANANCHI WA MLELE

$
0
0
 Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akifafanua jambo kwa kutumia  kompyuta ndogo (Ipad) wakati alipozungumza  na wanafamilia wa Mzee Katinda wa kitongoji cha Tupindo wilayani Mlele akiwa katika mapumziko mafupi nyumbani kwake  Kibaoni, Katavi julai 22, 2015.
 Watoto  wa familia ya  mzee Katinda wa  Kitongoji cha Tupindo wilayani Mlele  wakicheza ngoma ya Kisukuma mbele ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda .   Mheshiiwa Pinda yuko katika mapumziko mafupi kijijini kwake Kibaoni, katavi.
7027  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana  na  wasichana wa Kisukuma  nyumbani kwa Mzee Katinda kwenye kitongoji cha Tupindo wilayani  Mlele  akiwa  katika mapumziko mafupi  nyumbani kwake Kibaoni, Katavi   Juai 22, 2015.
  Mke wa Waziri Mama Tunu Pinda  akiwaonyesha picha mbalimbali alizopiga vijana wa kabila la Kisukuma aliokutana nao nyumbani kwa Mzee  Katinda katika kitongoji cha Tupindo wilayani Mlele  ambako yeye na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wako katika mapumziko mafupi  kijijini Kibaoni. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONESHO YA 10 YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA VYUO VYA ELIMU YA JUU NCHINI.

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua  rasmi Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.  Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mvumbuzi wa mashine ya kuchujia maji safi, Dkt. Askwar Hilonga, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, Atilio Raphael (kushoto kwake) na William Sambera (kulia) kuhusu Kompyuta ya mezani waliyoibuni maalum kwa ajili ya kufundishia somo la Kompyuta, wakati Makamu alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 :- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, William Sambera (kulia) kuhusu Kompyuta ya mezani iliyobuniwa maalum kwa ajili ya kufundishia somo la Kompyuta, wakati  Makamu alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MICHUANO YA KAGAME, APR YAICHAPA LLBA FC YA BURUNDI 2-1

$
0
0
Beki wa timu ya LLBA ya Burundi, Hakizimana Issa akijaribu kumzuia mchezaji wa timu ya APR ya Rwanda, Mubumbyi Barnabe katika mchezo wa Kome la Kagame uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijioni Dar es Salaam. APR imeshinda 2-1. (Picha na Francis Dande)
Beki wa LLBA FC ya Burundi, Manirakiza Aruna akioko hatari langoni mwake. 
 Heka heka katika lango la timuya LLBA FC.
 Simbomana Patrick wa APR ya Rwanda (kulia) akichuana na mchezaji wa LLBA FC ya Burundi, Ndaye Chancel.
 Uwimana Messo akimiliki mpira uku akizongwa na mchezaji wa APR, Simbomana Patrick.
Picha na Francis Dande

BENKI YA NMB YAKABIDHI MADAWATI KWA SHULE ZA MSINGI MWANZA NA MUSOMA

$
0
0
 Wanafunzi  wa Shule ya Msingi Kiseke Wilaya  ya Ilemela Mkoani Mwanza,  wakiwa wameketi kwenye madawati  64 yenye thamani  ya shilingi milioni 5 waliyokabidhiwa na Benki ya NMB kama sehemu ya msaada kwa shule hiyo.
Bw. Daniel Makorere, Afisa Elimu Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza  akimshukuru Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB Bw. Waziri Barnabas(kushoto) baada ya kupokea madawati yenye thamani ya shilingi milioni 5 kutoka benki ya NMB. Msaada huo wa madawati ulikabidhiwa kutoka NMB kwa Shule ya Msingi Kiseke ili kupunguza uhaba wa madawati unaoikumba shule hiyo. Wakishuhudia kutoka kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa Bw. Abraham Augustino pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kiseke Bw, Denitrus Wima.
 Mkuu wa Wilaya  ya Busega Mkoani Mwanza Bw. Paulo Mzindakaya , akimpa mkono wa shukurani Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB Bw. Waziri Barnabas(kulia), baada ya kukabidhi  madawati 240 yenye thamani ya shilingi milioni .... yaliyotolewa na benki ya NMB ukiwa ni msaada kwa  Shule za Msingi Nyashimo na Nasa Wilayani Busega pamoja na Sukuma na Simakitongo Wilaya ya Magu ili kupunguza uhaba wa madawati katika shule hizo. Kila shule imepata madawati sitini.
 Wanafunzi wa shule ya Msingi ya Kwibara wakiwa wameki kwenye madawati waliyokabidhiwa na NMB

Mkuu wa Wilaya  ya Musoma Mkoani Mara Bw. Zelothe Stephen , akimpa mkono wa shukurani Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB Bw. Waziri Barnabas(kushoto), baada ya kukabidhi  madawati 330 yaliyotolewa na benki ya NMB ukiwa ni msaada kwa  Shule za Msingi Bwai, Kiriba, Chanyahuru na Busumi pamoja na shule ya Sekondari Kiriba zilizopo Musoma vijijini ili kupunguza uhaba wa madawati katika shule hizo. Kila shule imepata madawati hamsini na tano.

Wakazi wa Kijiji cha Kingwang’oko Tabora wapatiwa huduma za mawasiliano na Airtel

$
0
0
Wakazi wa Kijiji cha Kingwang’oko Tabora wapatiwa huduma za mawasiliano na Airtel WAKAZI wa Kijiji cha Kigwang’oko Wilaya ya Ulyankulu,wameipongeza kampuni ya Airtel kwa kuwajengea mnara wa mawasiliano na hivyo kuondokana na tatizo sugu la mawasiliano lililokuwa likiwakabili. 
 Wakazi hao wamekuwa wakifanya shughuli zao bila ya mawasiliano ya uhakika kwa muda mrefu jambo linalotajwa kukwamisha shughuli nyingi za maendeleo kijijini hapo. 
 Wanakijiji hao wameeleza kuwa, wamekuwa wakipata tabu ya kufanya mawasiliano wakati mwingine wakilazimika kupanda kwenye miti au vichuguu kupata mawasliano kabla ya kujengwa kwa mnara huo. 
 “Tunawashukuru sana Airtel kwa kutukumbuka na kutuleta mnara huu ambao hapa kijijini kwetu ni mkombozi mkubwa katika sekta ya mawasiliano” walisema wananchi hao Akiongea na waandishi wa habari mkazi wa Kigwang’oko, Juma Magema alisema 
“Kabla ya Airtel kuweka mnara hapa kijiji kwetu tulikuwa tunapanda katika miti na hata vichuguu ili kupata mawasiliano, lakini sasa hatupati tena shida hiyo” Akiuzindua mnara huo,aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, John Kadutu, amewataka wananchi kuutumia mnara kuboresha shughuli zao za kijamii na kiuchumi na kuboresha maendeleo ya kijijini hapo na jamii kwa ujumla. 
 “Muutumie mnara huu kujiletea maendeleo kwani hivi sasa mnaweza kutumia mawasiliano ya Airtel na huduma zote zinazoenda sambamba na uwepo wa mnara huo kijijini hapo” alisema Kadutu 
 Awali meneja wa Airtel Mkoa wa Tabora,Fidelis Lugangira,alisema wamepeleka mnara huo ili kuboresha za kiuchumi ,lengo likiwa ni kuzidi kuwafanya wanufaike kwa kutumia mawasiliano. 
 “Mnara huu umejengwa kijijini hapa ikiwa ni hatua ya Kampuni yetu kusogeza karibu huduma za mawasiliano hivyo ni fursa ya kipekee kwenye kujiletea maendeleo” alisema Lugakingira. 
 Airtel imezindua huduma ya mawasiliano katika Kijiji cha Kigwang’oko Wilayani Ulyankulu mikoani Tabora mara baada ya kuzindua huduma kama hizo katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida na katika kijiji cha Nduruma wilayani Arumeru mkoani Arusha. Mpango mkakati ni kufikia maeneo mengi zaidi husasani yaliyoko pembezoni mwa nchi
 Msimamizi wa Mnara wa Airtel Tabora, Bwana Phidelis Lugangila akimwonyesha sehemu za mnara , aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, John Kadutu baada ya uzinduzi wa mnara huo wa mawasiliano wa Airtel, utakaowawezesha wakazi wa kijiji cha
Kingwang’oko wilayani Uyankulu mkoani Tabora kupata mawasiliano bora. Akishuhudia ni Diwani wa kata ya Kona nne Bwana Japhael Lufungija akifatiwa na Afisa Masoko wa Airtel Tabora, Godfrey Kigata
 Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa mnara huo wa mawasiliano wa Airtel, utakaowawezesha wakazi wa kijiji cha Kingwang’oko wilayani Uyankulu mkoani Tabora kupata mawasiliano bora.
Wanannchi wakifurahia baada ya uzinduzi wa mnara huo wa mawasiliano wa Airtel, utakaowawezesha wakazi wa kijiji cha Kingwang’oko wilayani Uyankulu mkoani Tabora kupata mawasiliano bora.

YANGA ILIPOILAZA TELECOM 3-0 CECAFA KAGAME CUP NA KUFUFUA MATUMAINI YA KUSONGA MBELE

Twanga Pepeta waibuka na onesho maalumu la "juzi, jana na leo", kuanza kurindima mwisho wa mwezi huu

$
0
0
Bendi ya muziki wa dansi ya African Stars “Twanga Pepeta’ itafanya maonyesho maalum mwishoni mwa mwezi  huu yaliyopewa jina la juzi, jana na leo.
Katika maonyesho hayo, bendi hiyo itapiga nyimbo zao maarufu katika albamu zake kuanzia "Kisa cha Mpemba" mpaka albamu ya mwisho kuzinduliwa ijulikanayo kwa jina la "Nyumbani ni Nyumbani". 
Pia itapiga nyimbo zake mpya ambazo bado hazijaingia kwenye albamu.
Mratibu wa onyesho hilo, Nasib Mahinya alisema kuwa onyesho la kwanza litafanyika kwenye ukumbi wa Escape One ambapo onyesho la pili litakuwa Agosti Mosi kwenye ukumbi wa Dar West, Tabata na la tatu AGosti 2 kwenye ukumbi wa TCC, Chang’ombe.
Mahinya alisema kuwa sababu kubwa ya kufanya maonyesho hayo ni kuwakumbusha mashabiki wao wapya na wa zamani, wapi walianzia na walipo sasa.  Alisema kuwa wanajua kuwa mpaka sasa kuna mashabiki wa bendi hiyo hawazijui nyimbo zao za zamani.
“Bendi kwa sasa ipo kambini kujiandaa na maonyesho hayo yaliyodhaminiwa na Salut5, CXC Africa, Astery Insurance, EF Outdoor, Master’s club na Clouds Media group, hii ni fursa pekee kwa mashabiki kuona shoo za zamani, ungo, mchi nayo itakuwepo,” alisema Mahinya.

JK aagana na Mabalozi waliomaliza muda wao wa India,Ubelgiji na Sweden Ikulu jijini Dar es salaam

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo ameagana na mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania baada ya kumaliza muda wao wa kazi . Mabalozi walioagana na Rais leo ikulu jijini Dar es Salaam ni pamoja na Mhe.Debnath Shaw wa India,Balozi Koenraad Adam wa Ubelgiji na balozi Lennarth Hjelmaker wa Sweden.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na balozi wa India anayemaliza muda wake Mhe.Debnath Shaw wakati balozi huyo alipokwenda kumuaga ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na balozi Koenraad Adam wa Ubelgiji ikulu jijini Dar es Salaam leo alipokwenda kumuaga.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Sweden nchini aliyemaliza muda wake Mhe.Lennarth Hjelmaker ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Freddy Maro

FRIENDS OF DEVELOPMENTS (FOD) na Bigright YAANDAA MAPAMBANO ya NDONDI JIJINI DAR ES SALAAM mwezi ujao

$
0
0
Kampuni ya bigright promotion inategemea kuandaa pambano la masumbwi litakalopigwa tarehe 6/9/2015 katika ukumbi wa vijana , kinondoni jijini Dar es salaam.
Katibu wa ngumi za kulipwa ambaye  ndie mratibu wa mpambano huo Ibrahim Kamwe (Bigright) amesema pambano hilo limeandaliwa kwa ajili ya kuamsha vijana kujituma na kujijengea mazingira ya kupenda kufanya kazi na sio kukaa vijiweni na kujiingiza katika utumiaji wa madawa na ukabaji.
Bigright promotion ikishirikiana FRIENDS OF DEVELOPMENTS (FOD) yaani rafiki wa maendeleo wanaandaa pambano hilo kwa kuwachezesha mabondia toka sehemu tofauti za Tanzania. 
Katika mapambano hayo  Mbena Rajabu atazipiga na Twalibu Mchanjo katika pambano la ubingwa wa Taifa kilogram 57. ambapo bondia Dula Mbabe atazipiga na Ambukile Chusa, wakati Haidary Raju atapambana na Mtango Salum kutoka Tanga
Mapambano mengine ni ya Yona Miyeyusho ataezipiga na Hemedi hemed, huku George Allen wa Tanga akizipiga na Mwinyi Mzengela wa Dar es salaam ana Mau Champion wa Tanga atazipiga na Epson John wa Morogoro
Bondia Mohamed Alkaida atapambana na Guzo Hassan 
Mapambano hayo ni kutimiza lengo la FoD kushirikiana na bigright katika kuandaa mapambano hayo ili kuhakikisha Tanzania inakuwa  na mabingwa wengi wa ngumi katika mikoa yote, na kuhakikisha wanamichezo wengine na wasanii wanafanya vizuri katika fani zao.
"Kwa kuwa FOD ina wafuasi kila kona ya Tanzania imelenga kupigana vilivyo kuhakikisha majiji yanakuwa safi, wasanii na wanamichezo wanafika mbali kuwasaidia wasiojiweza mitaani na mahospitalini. 
"Kwa ufupi yatakuwa ni mapambano ya aina yake kutokana na hao mabondia wenyewe kuwa na uchu wa ushindi kwani  ni mabondia wazuri, wazoefu na wana wapenzi wengi.
Mratibu wa mapambano hayo  Ibrahim Kamwe (Bigright)
Ibrahim Kamwe (Bigright) akiwa na mabondia wanawake anaowapromoti

Erick Omondi, Sarabi Band, Grace Matata na Leo Mkanyia kutumbuiza kwenye East African Vibes Concert, Tarehe1 Agosti 2015, Dar es Salaam

Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images