Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110139 articles
Browse latest View live

I SHOT BI. KIDUDE FILM FOR ZIFF SUNDAY


Rais Kikwete akabidhiwa Joho na Cheti cha Shahada ya Doctor of Laws

$
0
0
Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala akimkabidhi Rais Dkt .Jakaya Mrisho Kikwete cheti cha Shahada ya Heshima ya Doctor of Laws(Honoris Causa) wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi Rais joho na cheti iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na maprofesa waandamizi wa chuo hicho.Tayari Rais Kikwete alishatunukiwa shahada hiyo katika mahafali ya 41 ya UDSM yaliyofanyika Octoba mwaka 2011.
Profesa Agnes Mwakaje wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimvika kofia ya kitaaluma Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi Rasmi Rais Joho na cheti cha shahada ya heshima ya Doctor of Laws(Honoris Causa) ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandala akisoma maelezo mafupi baada yeye na jopo la maprofesa waandamizi wa chuo hicho kumkabidho Joho la taaluma na cheti cha Shahada ya heshima ya Doctor of Laws(Honoris Causa) ya chu kikuu cha Dar es Salaam wakati wa hafla iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandakla pamoja na maprofesa waandamizi wa chuo hicho muda mfupi baada hafla fupi ya kumkabidhi Rais Joho na Cheti cha Shahada ya Heshima ya Doctor of Laws(Honoris Causa) ikliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)

MUSIC AND FILM COMBINE AT ZIFF 2015 / ZIFF ANNOUNCES CLOSING FILM

$
0
0


 Monday was a special day at ZIFF 2015, with a unique and memorable day of film and music in perfect harmony. July 20th saw the screening of the Moussa Diallo biopic, Sound Tracks of Life Moussa Diallo – followed by a live performance from Moussa Diallo himself. 
The film screening was introduced by Diallo himself, and filmmaker Helle Toft, who elaborated on the personal yet universal themes in the film; reconciliation and forgiveness. Diallo’s story may be unique, having left Mali at age 17 and landing up in Denmark, soon becoming a major star, however the themes of the film resonate for most people. 
The live performance from Diallo that followed the screening was even more powerful with the audience having experienced his story through the medium of film. The interconnectedness of these two mediums of communication and their ability to touch people is one of the cornerstones of ZIFF, as Martin Mhando explains. 
It is very important to recognise the synergies of the links between sound and images. ZIFF has always had a component of music in the festival, which we have cultivated over the years. If you want to see how many filmmakers grew out of video clips, just go and ask them to give you a copy of their CV, then you will see that they started from video clips and then graduated to making feature films,” he said. 
 “What we want to do at ZIFF is show the links between business and film, between sound and film,” he added. 
Sound Tracks of Life: Moussa Diallo will screen again at ZIFF on Thursday evening at Zan Cinema at 19:00. 
The festival, in fact, is screening a host of films with music related content, including Shehnai about the journey of a Pakistani musician, Abazezi about a Ugandan dance crew Tabu Flo, and Maramosa that follows young musician, Mandela, and his band as they struggle to promote peace ahead of the hotly contested 2013 Kenyan presidential election.

ZIFF ANNOUNCES CLOSING FILM
 ZIFF is also proud to announce as its closing film, another perfect example of the synergies between film and music – I Shot Bi Kidude, Andy Jones’ follow up to, As Old as my Tongue, his biographical documentary on this legendary Zanzibari artist. 
Jones will arrive at ZIFF on Thursday, fresh from this year’s Durban International Film Festival where the film previewed last year.  “Getting the film in front of audiences at DFM was a huge leap forwards in the film’s development” says Jones. “Obviously we had to hold back the official premiere for Zanzibar, but it’s fantastic to be here mentoring projects [for Doc Station, and the Hot Docs Blue Ice Fund] and then heading to Zanzibar in one trip. It’s a great symbol of the growing collaboration between festivals in the region.” 
After visiting Zanzibar every year for almost a decade, Jones hadn’t seen Kidude for almost three years.  In August 2012, word reached the UK that East Africa’s most famous musical icon had been kidnapped. It wasn’t long before Andy was back in Zanzibar, to get to the bottom of the story.  He began to untangle a web of rumours, started by a jealous nephew who had taken Kidude from her home in the belief that unscrupulous music promoters were making millions from his ageing aunt. 
Just weeks after the drama unravelled before the camera, with South African Natalie Haarhoff behind the lens, the world’s oldest singer died, at a reported age of over a hundred years old.  Jones frantically departed his home in Newcastle arriving at Heathrow just minutes before the  last flight to Nairobi was scheduled to leave. He arrived in Zanzibar just in time to be at her funeral which brought the island to a standstill. 
“I Shot Bi Kidude, is my account of what happened at the end of Bi Kidude’s life.  As with any story, there are many versions of the truth.  There are of course elements that are hard for an outsider to grasp, but I hope that there is also an insight which fresh eyes can bring. What emerges for me is a sense of the celebratory power of music, and the importance of doing those things which bring us happiness while we still can.”  Explains Andy Jones. 
I Shot Bi Kidude screens Sunday July 26th. 7:15pm  at the Old Fort Amphitheatre.

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, (TCRA) Dk. Ally Yahaya Simba

$
0
0
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa hivi karibuni alimteua Dk. Ally Yahaya Simba (pichani) kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, (TCRA) kufuatia mchakato wa kumpata Mkurugenzi Mkuu kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mawasiliano ya 2003 kifungu cha 9 na kifungu cha 13. (TCRA Act, 2003). 

Dk. Simba aliteuliwa rasmi kushika wadhifa huo mnamo tarehe 6 Jula1 2015 kwa kipindi cha miaka mitano. Kabla ya uteuzi huo, Dk. Simba alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia tangu Agosti 2013. 

Dk. Simba ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16 katika Sekta ya Mawasiliano ambapo amefanya kazi kwa watoa huduma, Taaluma ya Utafiti, Udhibiti pamoja na Serikali Kuu. 
Dk. Simba ana Shahada ya B.Sc. (Hons.) Shahada ya Sayansi ya Elektroniki na Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, aliyopata mwaka 1998. Pia ana Shahada ya Uzamili ya Uhandisi aliyoipata mwaka 2003 na Shahada ya Uzamivu (Ph.D) ya Uhandisi wa Kielektroniki kutoka Chuo Kikuu cha Hokkaido, Sapporo, nchini Japan, aliyoipata mwaka 2006. 
Kuanzia mwaka 2006 mpaka 2011, alikuwa Mtaalamu Mtafiti katika Taasisi ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (NICT), huko Tokyo, Japan, ambako alihusika katika kufanya utafiti wa madhara ya ya kiafya kwa mwanadamu kwa kutumia simu za mikononi na kwa kuwa karibu na minara ya mawasiliano. 
Mnamo mwaka 2011 hadi mwaka 2013, alifanya kazi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kama Meneja Mipango na Utafiti wa Mamlaka. 
Dk. Simba ametoa machapisho kadhaa katika majarida ya kimataifa na amewasilisha matokeo ya tafiti zake katika zaidi ya mikutano Zaidi ya 30 ya kimataifa. Aidha Dk. Simba alikuwa Kiongozi wa Timu ya wataalamu wa Kitanzania iliyoandaa Sheria za Uhalifu wa Mitandao nchini iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni. 
Dk. Simba ni Mhandishi Mahiri (Chartered Engineer), aliyesajiliwa nchini Uingereza  katika Baraza la Uhandisi nchini humo na ni “Fellow”  wa Taasisi ya Uhandisi na Teknolojia ya nchini Uingereza (IET), ambako alikuwa Mshauri wa Kimataifa  wa Usajili wa Wanataaluma Wahandisi kutoka Aprili 2011 mpaka Machi 2014. Pia Dk. Simba ni Mwanachama Mwandamizi wa “Institute of Electrical and Electronics Engineers” (IEEE). Hali kadhalika Dk. Simba amechapishwa katika jarida la “Marquis Who's Who in Science and Engineering” katika toleo la 11, la mwaka 2011–2012.

 Dr. Simba ni miongoni waliopata Udhamini wa Serikali ya Japan (Monbusho Scholarship) kutoka mwaka 2000 mpaka 2006.

Rais kikwete apokea hundi ya Bima ya Maisha

$
0
0
 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hundi ya malipo ya Bima ya Maisha(Flexi Provider) kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa(National Insurance Corporation of Tanzania Limited) NIC Bwana Sam Kamanga Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Akimkabidhi hundi hiyo,  Bw. Sam Kamanga amesema uwepo wa Mheshimiwa Rais kama mteja wa NIC imesaidia kukuza uelewa na shughuli za shirika hilo.
“Kitendo cha Serikali kukatia Bima mali zake na taasisi zake, kumeongeza uwezo wa kifedha wa shirika na soko la Bima” amesema na kuwataka watu binafsi, taasisi mbalimbali na mashirika ya kiserikali kukata Bima kwa ajili ya maendeleo na akiba ya baadaye. 
Rais Kikwete ameitaka NIC kuongeza juhudi katika kuhamasisha na kuelimisha watanzania umuhimu na manufaa makubwa yanayopatikana kutokana na Bima.
Picha na Freddy Maro

MAGUFULI AENDELEA KUJITAMBULISHA NA KUWASHUKURU WANACHI WA CHATO MPAKA DODOMA KWA KISHINDO.

$
0
0
   Baadhi ya Wananchi wa mji wa Kahama mkoani Shinyanga na vitongoji vyake wakiwa wamefunga barabara wakitaka kumsalimia kwa  furaha kubwa Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa kwa wananchi hao akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
  Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru na kujitambulisha kwa Wananchi ndani ya mji wa Ushirombo,wilayani Bukombe,mkoa wa Geita mapema leo mchna alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
 Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akisaini vitabu vya ofisi ya CCM juu ya gari ndani ya mji wa Ushirombo,wilayani Bukombe,mkoa wa Geita alipopita kuwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji Bukombe mchana huu alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
 Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji wa Masumbwe wilayani Mbogwe mkoa wa Geita mchana huu alipokuwa akipita njiani kuwashukuru na kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
    Baadhi ya Wananchi wa mji wa Kahama mkoani Shinyanga na vitongoji vyake wakimsikiliza Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli  mara baada ya msafara wake kusimamishwa na wananchi hao alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi  alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.
Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia na kuwashukuru Wananchi wa mji wa Kahama mchana huu alipokuwa akipita njiani kujitambulisha kwa wananchi alipokuwa akielekea mkoani Dodoma na baadae kurejea jijini Dar.

PICHA NA MICHUZI JR-CHATO-DODOMA

TAHADHARI MUHIMU DHIDI YA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO

$
0
0
Kumekua na wimbi la uhalifu Mtandao aina ya (Clickjacking unao fanana na cross-site scripting) - Unao sambaza picha zisizo rafiki katika walls za wengine ( Mara nyingi Muhusika anakua haoni hadi aambiwe) Ushauri ni Kua Uonapo Video Hizo Mjulishe muhusika ili aweze kubadili Password yake na kutoa taarifa facebook.

Pia Wewe uonae Usi Click (Bonyeza) kwani Kwa kufanya hivyo na wewe utakua umeathirikia.

Siku Njema - Yusuf Kileo

Hapo chini kuna post Mbili zenye Picha Tofauti katia Facebook ikiwa ni kufuatia Wimbi kubwa la waathirika na Aina ya uhalifu unaokua kwa kasi nchini. Jihadhari nazo sana!



Prof. John Nkoma Awarded at EACO Congress in Kampala

$
0
0
Hon. Nyombi Thembo, Minister of State for Information and CommunicationsTechnologies (ICTs) Uganda gives an award of appreciation to Prof. John S. Nkoma for having served as a Founding Executive Committee Member of the East African Communications Organization (EACO) and "Eleven years of excellent service and development with Tanzania Communications Regulatory Authority!(TCRA)" as Director General, from 2004 to June 2015. The award was presented to Prof. Nkoma during the 21st EACO Congress and Assemblies held in recently Kampala, Uganda.

WIZARA YA MAMBO YA NJE YAMUAGA BALOZI WA SWEDEN ALIYEMALIZA MUDA WA KAZI NCHINI

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha mchana kilichoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga Balozi wa Sweden hapa nchini ambaye amemaliza muda wake wa kazi, Mhe. Lennarth Hjelmaker. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Balozi wa Sweden anayemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Lennarth Hjelmaker akimsikiliza Balozi Kasyanju (hayupo pichani) wakati akitoa hotuba ya kumuaga Balozi huyo. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine.
Balozi Sokoine akizungumza kuwakaribisha Wageni waalikwa kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Sweden aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Balozi Hjelmaker nae akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa kumpatia ushirikiano mkubwa katika kipindi chote cha miaka mitano aliyokuwepo hapa nchini kama Balozi wa Sweden
Picha ya pamoja
Balozi Kasyanju akiagana na Balozi Hjelmaker mara baada ya hafla ya kumuaga kukamilika. Picha  na Reginald Philip
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF), WAKUTANA NA WAHARIRI, DAR ES SALAAM

$
0
0

 MKURUGENZI Mkuu wa kwanza wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Masha Mshomba, akiwasilisha mada wakati wa warsha iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa Wahariri kwenye Hoteli ya Court Yard jijini Dar es Salaam, Julai 22, 2015
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, (SSRA), Irine Isaka, akifungua warsha hiyo
 Mhariri Shemax Ngahamera akizungumza kwenye warsha hiyo
 Mhariri wa vipindi wa ITV/Radio One, Steven Chuwa, (kulia), na Mhariri Mtendaji wa EFM, Scolastica Mazula, wakipitia mada zilizokuwa zikitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF
 Baadhi ya Wahariri, wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa juu ya kazi na huduma zitolewazo na WCF
Mhariri  wa kujitegemea Mzee Wence Mushi akiuliza swali.
Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

Dk. Willibroad Slaa atua mwanza kuwatambulisha lembeli na bulaya leo

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Willibroad Slaa akiwa kwenye gari katika msafara wa mapokezi kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa kuwatambulisha Mbunge wa Kahama, James Lembeli na Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Bulaya waliohamia Chadema wakitokea CCM jana jijini Mwanza.
 Msafara ukiendelea kuelekea uwanjani sasa
Mbunge wa Jimbo la Kahama, mkoani Shinyanga, James Lembeli (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, John Mnyika, wakiwapungia wananchi mikono walipokuwa kwenye msafara wa mapokezi ya Viongozi Wakuu wa Chama hicho wakiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya mkutano mkubwa wa hadhara.

JUMUIYA YA WATANZANIA WA DMV NA WASHIRIKA WAO WATOA HUDUMA ZA KIMATIBABU NA MADAWA BURE KATIKA HOSPITALI YA MWANAYAMALA JIJINI DAR‏‎

$
0
0
Mkurugenzi wa Taasisi ya kinamama wa Kiafrika inayohusika na ugonjwa wa Saratani ya matiti Bi. Ify Nwabuku(kushoto) akizungumza na wakina mama (hawapo picha) wakati wa utoaji wa matibabu bure kwa wakina mama katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar. Kushoto ni Bi Asha Nyang'anyi ambaye ni mwanakamati wa ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumiwa jumuiya ya Watanzania DMV.

 Wakina mama wakimsikiliza kwa makini Bi. Ify Nwabuku wakati akitoa maelezo juu ya upimaji wa Saratani kwa wakina mama waliofika kupima afya zao katika hospitali ya Mwananyamala zilizokuwa zikitolewa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao walioamua kutoa huduma za kitabibu na madawa bure.
 Dk. George Quintero(kushoto) kutoka Marekani akimtibu meno mtoto Living Andrew aliyeshikwa na mama yake huku akisaidiana na Dk. Emilton Ndashau(kulia) wakatia wa utoaji wa uduma bure iliyodhaminiwa na Jumuiya ya Watanzania DMV pamoja na  washirika wao katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar.
Rais wa Jumuiya ya Jumuiya ya Watanzania DMV, Bw. Iddi Sandaly(kustoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Bi. Adama Gibateh(katikati) pamoja na Kushoto ni Bi Asha Nyang'anyi ambaye ni mwanakamatiwa ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumiwa jumuiya ya Watanzania DMV.
Picha zaidi BOFYA HAPA

JOTO LA ASUBUHI LA 93.7 EFM ALHAMISI KUANZIA SAA 12

JOSHUA NASSARI ACHAGULIWA KUPEPERUSHA BENDERA YA CHADEMA JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI

$
0
0
`Aliekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki mkoani Arusha,Joshua Nassari akizungumza namna alivyotekeleza ahadi zake katika kipindi kilichopita wakati wa mkutano Mkuu wa Jimbo uliofanyika kwenye Mji mdogo wa Usa River ambao  alichaguliwa bila kupingwa ili kupeperusha bendera ya Chadema katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Wanachama wa Chadema wakipiga kura za maoni kwaajili ya kumchagua mgombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki katika Mji Mdogo wa Usa River,Joshua Nassari alipata kura 387  na kura 2 za hapana.

Wanachama wa Chadema wakifurahia jambo katika mkutano huo

Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini ambaye alikua Mbunge wa Chadema jimbo la Karatu mkoa wa Arusha,Israel Natse(kulia)na Katibu wa Chadema mkoa wa Arusha,Kalist Lazaro wakimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari(kati)baada ya kutangazwa mshindi.

Ibada ya kumuaga Mhe. Balozi Liberata Mulamula -- JUMAPILI HII....Washington DC

uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya wazazi nipendeni

$
0
0
 Mkurugenzi wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ali Mohamed Ali (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, wakati akitoa tamko kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando katika uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya wazazi nipendeni uliofanyika Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Georgina Msemo na Mshauri wa Kiufundi wa Malaria kutoka  Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID)
 Ofisa Uzazi Salama,  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Heavengton Mshiu (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
 Mshauri wa Masuala ya Afya ya Uzazi wa Taasisi ya Center for Comminication Programs Johnns HopKins University, Dk,.Rosemarie Madinda (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo. Taasisi hiyo ndiyo inayoendesha kampeni hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Georgina Msemo (kulia), akizungumza kwenye uzinduzi huo.

  
Mwanamuziki Nyoshi Al-Saadat wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM Academia "Wana wa Ngwasuma" itakayotoa burudani katika maonyesho mbalimbali yatakayokwenda sanjari na uzinduzi huo yatakayofanyika kuanzia kesho viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam kuanzia kesho, akizungumza katika uzinduzi huo utakaopambwa na burudani za kumwaga.

Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imesema imepiga hatua katika kupunguza vifo vya watoto waliochini ya miaka mitano toka 157 mwaka 1990 hadi kufikia 54 kwa mwaka 2013.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ali Mohamed Ali wakati akitoa tamko kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando katika uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya wazazi nipendeni uliofanyika Dar es Salaam leo
Alisema kati yua watoto hai 1,000 wanaozaliwa na kufikia lengo la Melenia (MDG) 4 waliojiwekea kufikia mwisho wa mwaka huu Disemba, 2015.
"Pamoja na mafanikio hayo bado hari si shwari kwa upande wa vifo vinavyotokana na uzazi kwani vimepungua kutoka 770 mwaka 1990 na kufikia 410 kwa mwaka 2014 kwa kila vizazi hai 100,000 tofauti na lengo tulilojiwekea kufikia Disema 2015 kuwa vipungue kufikia 193 kwa kila vizazi hai 100,000" alisema Dk.Ali.
Alisema Kampeni ya Wazazi Nipendeni awamu ya kwanza ilitengenezwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na msaada toka watu wa Marekani kupitia taasisi ya USAID, Mfuko wa Malaria wa Rais wa Marekani na taasisi ya Kukinga na kuzuia Magonjwa.
Dk. Ali alisema programu hiyo ilihusisha kutuma ujumbe uliolenga kuimarisha afya ya mjamzito na mtoto na kuwa ilizinduliwa hapa nchini jijini Mwanza kwa mara ya kwanza mwezi Novemba, 2012.
Alisema katika kampeni hiyo ya masuala ya afya na ustawi wa jamii vyombo vyote vya habari ni muhimu zaidi kuhabarisha na kuwa ujumbe mfupi wa simu za kiganjani wenye taarifa anwai zitakuwa zinatumwa wakati wowote wa ujauzito mpaka mwaka mmoja baada ya kujifungua.

Aliongeza kuwa ili kujiunga mhusika, ndugu, jirani au rafiki atatuma ujumbe "mtoto" kwenda namba 15001 jambo litakalosaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, mtoto mchanga na mtoto alie chini ya miaka mitano.
Alisema uzinduzi wa kampeni hiyo unakwenda sanjari na maonyesho mbalimbali, upimaji wa damu, masuala ya huduma ya VVU na Ukimwi yatakayoanza leo asubuhi viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam.


Benki ya NBC yazindua ’Hamia Kwako’ ni huduma ya mikopo ya nyumba

$
0
0
  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Edward Marks wakionyesha mfano wa funguo kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma ya mikopo ya nyumba iliyopewa jina ya ‘Hamia Kwako’ ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Edward Marks (wa pili kushoto), akibadishana mawazo na Ofisa Fedha Mkuu wa Shirika la Mikopo ya Nyumba la Tanzania Mortgage Refinance (TMRC), Oswald Urassa (wa tatu kushoto) katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya mikopo ya nyumba iliyopewa jina ya ‘Hamia Kwako’ ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NBC, Mussa Jallow, Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Rejareja cha benki hiyo, Isdory Msaki na Mkuu wa  Rasilimali Watu wa benki hiyo, Flora Mollel Lupembe.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki (wa pili kushoto), akibadilisha mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Edward Marks (kulia) na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rukia Mtingwa (katikati yao), wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya mikopo ya nyumba ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam leo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo ya Makampuni wa Benki ya NBC, Salehe Mohamed (kushoto), akiagana na Ofisa Fedha Mkuu wa Shirika la Mikopo la TMRC, Oswald Urassa baada ya hafla hiyo. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Mussa Jallow na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Edward Marks.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angela Kairuki (wa pili kulia), akizungumza na Ofisa Fedha Mkuu wa TMRC, Oswald Urassa (kulia) wakati wa hafla hiyo. Wengine kutoka kushoto ni maofisa mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Joseph Haule na Michael Mbago.

SIMU TV: HABARI MBALIMBALI TOKA VITUO VYA TELEVISHENI

SAKATA LA MAMA MJANE KUTIMULIWA KATIKA NYUMBA SINZA, DAR ES SALAAM

Viewing all 110139 articles
Browse latest View live




Latest Images