Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAVUNJWA, RAIS MWINYI ALIMWAGIA SIFA

$
0
0
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akizungumza na madiwani na watendaji wa Manispaa hiyo wakati wa kikao maalum cha kuahirisha Baraza hilo kilichofanyika jana Dar es Salaam. Wengine ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manipss hiyo, Eng. Mussa Nati (kulia).
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akimtambulisha Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi kwa Madiwani wa Manispaa hiyo baada ya kuwasili kwenye ofisi za Manispaa hiyo kuhudhuria hafla maalum ya kuahirisha Baraza hilo Dar es Salaam jana.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akionesha cheti cha Freeman alichokabidhiwa na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi (kushoto kwake) katika hafla hiyo. Cheti hicho kinachotolewa na Baraza la Madiwani hutolewa mara chache kwa Meya aliyefanikiwa kutekeleza miradi ya wananchi kwa kiwango kikubwa na kina maana ya ‘Raia Huru’. Kushoto ni Naibu Meya, Songoro Mnyonge na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mushi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

FUATILIA HOTUBA YA RAIS KIKWETE WAKATI AKIFUNGA BUNGE MUDA HUU

$
0
0
UNAWEZA KUFATILIA LIVE HOTUBA YA RAIS KIKWETE WAKATI AKIFUNGA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MJINI DODOMA LEO.

SEHEMU YA HOTUBA YA JK WAKATI WA UFUNGUZI WA JENGO LA KISASA LA MIKUTANO DODOMA

BBC DIRA YA DUNIA ALHAMISI JULAI 9, 2015

TANGAZO KUTOKA TANZANIA ASSOCIATION GREATER MANCHESTER (TAGMA).

$
0
0
Tungependa kuwatangazia wanajumuiya wetu, Watanzania wanaoishi Manchester na Watanzania wanoiishi miji ya karibu kama Liverpool, Leeds, York na Newcastle kwamba utakuja Kamati kutoka Ubalozi wa Tanzania kwa hapa Uingereza kwa ajili ya zoezi la ku renew pasipoti.

Hili zoezi litafanyika Jumamosi hii inayokuja, tarehe 11 / 07 / 2015 kuanzia saa sita mchana mpaka saa tatu za usiku ( 12:00pm - 9:00pm / 12:00hrs - 21:00hrs). 

Hili zoezi litafanyika anuani ifwatayo:
Trinity House Community,
Resource Centre,
Grove Close,
Rusholme,
Manchester,
M14 5AA.

Tafadhali wasiliana nasi kwa 
maelezo zaidi au bonyeza link ifwatayo:


Tafadhali mjulishe na mtanzania mwenzako.
Asanteni Sana.
Bravo Mkony
Mwenyekiti
TAGMA
Kwa maelezo zaidi tafadhali piga simu zifwatazo:
Bravo Mkony ( Mwenyekiti, TAGMA) - 07740 980525
Tilumanywa Mkama ( Makamu Mwenyekiti, TAGMA) - 07747 181630
Lilian Mkocha ( Katibu Mkuu, TAGMA) - 07880 994315
Ally Mtiga ( Naibu Katibu, TAGMA) - 07553 282798

UBALOZI WA MAREKANI DAR ES SALAAM: MNADA WA HADHARA JUMAMOSI JULAI 11, 2015

$
0
0
  UNIVERSAL AUCTION CENTRE Kwa idhini waliyopewa na Ubalozi wa Marekani watauza kwa mnada wa hadhara gari, generator, fanicha za ofisi na nyumbani,  makontena na mashine za gym   tarehe 11 Julai, 2015 Jumamosi saa 3:00 asubuhi. Mnada utafanyika Golden Resort Sinza,  Lion Street.
MALI ZITAKAZOUZWA:sofa sets, chest drawer, recliner, dressers, coffee table, book shelve, meza za ofisi/viti, dining table/chairs, carpet, hoover,  vitanda, magodoro, fridges, freezer, cookers, TV set, washer, dryer, computer set, photocopy m/c,  A/c split units, portable toilets, Gym equipments:Stairmaster Eliptical, Comber, Kettler Butterfly,Treadmill, na vingine vingi

Gari, Genereta & Makontena yatakayouzwa:



Idadi

Aina

Model

Mwaka

Ushuru

1

Ford Everest  S/ Wagon

WL  Diesel Engine

2007

Bado

2

Generator

60 & 81 KVA  Silent


Bado

   3

Empty Container

40 & 20 Fts

2012, 2011,1995

Bado

Mali zote zinaweza kukaguliwa Golden Resort Sinza,Lion Street tarehe 9 na 10 Julai,  2015 kuanzia saa 4.00. asubuhi mpaka saa 10.00 jioni.
MASHARTI YA MNADA:

  1. Mnunuzi  wa furniture na genereta atatakiwa kulipa malipo yote kwa keshia (cashier). Na mnunuzi wa gari atatakiwa kulipa 25% pale pale na salio lilipwe ndani ya siku 5 za kazi, ukishindwa kulipa kwa muda huo gari litauzwa  kwa mshindi mwingine aliyefwata  na dhamana haitarudishwa. 
  2. Mali zote zitauzwa kama zilivyo bila dhamana.
  3. Mnunuzi atawajibika kulipa ushuru na kodi zingine zote.
  4. Mali yote iliyouzwa itatakiwa kuondolewa baada ya kulipa malipo yote pamoja na kodi.Kwa maelezo zaidi waone:
  5. Kwa maelezo zaidi waone:

UNIVERSAL AUCTION CENTRE

NKRUMAH STREET
MKABALA NA CO-CABS

SIMU NA:  0754-284 926, 0757 284 926               Email : universalauction@hotamail.com

DAR ES SALAAM.

BIMA YA RESOLUTION YAFUTURISHA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

$
0
0
 Picha ya baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kufutari katika ukumbi wa hoteli Serena, futari iliyoandaliwa na Bima ya Resolution.
 Baadhi wa waumini wa dini ya kiislam wakimsikiliza mgeni rasmi Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam .
  Meneja Mkuu wa Bima ya Resolution, Oscar Osir, na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salim wakiwaongoza wa umini wa Dini ya kiislamu katika mwezi Mtukuru wa Ramadhani kuchukua futari iliyoandaliwa na Bima ya Resolution jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 kushoto ni  Meneja Mkuu wa Bima ya Resolution, Oscar Osir wakifutari na Shehe mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh, Alhadi Mussa Salim katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mkuu wa Bima ya Resolution, Oscar Osir, akiwatambulisha wageni waliaalikwa wa dini ya kiislam waliojumuika na Bima ya Resolution katika futari iliyoandaliwa na Bima ya Resolution katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Nape azungumzia sababu za kuchelewa kwa Vikao vya CCM, Mjini Dodoma

$
0
0
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo asubuhi Julai 10, 2015. 

Nape amesema, leo hii majina matano ya makada wa chama hicho walioomba kuteuliwa na CCM kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yatajulikana, na kufuatia majina matatu ya makada hao ambayo yatapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu utakaofanyika Jumamosi Julai 11, 2015. 

Nape amesema vikao vyote vinaanza leo saa nne, na hakuna kikao chochote kilichokwisha fanyika ikiwa ni pamoja na kile kinachozungumzwa sana na vyombo vya habari yaani kikao cha kamati ya maadili ya chama hicho ambacho ndicho kinachokata majina na kutoa mapendekezo Kamati Kuu. 

Alipoulizwa ucheleweshwaji huo umetokana na nini, Nape alisema "Nyote mmeshuhudia, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amekuwa na kazi nyingi katika kipindi cha siku mbili hizi na hivyo asingeweza kusimamia vikao hivyo kama ilivyotarajiwa ingawa amedokeza kuwa "wakubwa" hao walikuwa wakikutana kwa majadiliano na wadau kingawa hakueleza ni wadau gani.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa White House, Mjini Dodoma leo Julai 10, 2015.

SEND OFF YA TUMPALE JOHN MWAISANGO, YAFANA KATIKA UKUMBI WA MKAPA JIJINI MBEYA

$
0
0
Tumpale John Mwaisango(kulia) Bi. Harusi mtarajiwa akiwa pamoja na Mume wake Mtarajiwa Jeofrey Daniel Shipela (kushoto) katika nyuso za Furaha wakati wa sherehe za kumuaga .
Bi Harusi mtarajiwa Tumpale John Mwaisango akimpa zawadi Mume wake Mtarajiwa Jeofrey Shipela wa kwanza kulia ni mpambe wa Bwana harusi mtarajiwa Venance Matinya
 Bi. Harusi Mtarajiwa Tumpale John Mwaisango (kushoto) Akikata keki kulia ni Mpambe wake Monica.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

RATIBA YA VIKAO VYA CCM LEO

JK ALIPOHUTUBIA BUNGE LA KUMI LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MJINI DODOMA

$
0
0
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozw na Spika Anne Makinda akiingia Bungeni mjini Dodoma tayari kuhutubia wabunge Alhamisi Julai 9, 2015
b10
 Sehemu ya ukumbi wa bunge wakati Rais Kikwete akiingia bungeni kuhutubia  waheshimiwa wabunge.
 Sehemu ya wabunge wakimsikiliza Rais Kikwete
Rais Kikwete akihutubia waheshimiwa wabunge. 

NEWZZ ALERT:KITUO CHA POLISI BUNJU CHACHOMWA MOTO.

$
0
0
Baadhi ya Polisi wakiwatawanya watu (hawapo pichani) kwa mabomu ya machozi mara baada ya tukio la kuchomwa moto kituo cha polisi Bunju, tukio hilo limetokea.Kituo cha polisi Bunju kilichopo nje kidogo ya jiji la Dar kimechomwa moto na baadhi ya Wananchi kufuatia tukio la kudaiwa kwa Mwanafunzi mmoja kugongwa na gari na kufa papo hapo.
 Sehemu ya kituo hicho cha Polisi Bunju kikiteketea kwa moto mara baada ya kuchomwa moto na wananchi kufuatia tukio la kudaiwa kwa Mwanafunzi mmoja kugongwa na gari na kufariki papo hapo.
 Muonekano wa kituo hicho cha Polisi Bunju mara baada ya kuchomwa moto.
 Moja ya Gari iliyokuwepo kituoni hapo ikiwa imenyofolewa vifaa vyake wakati wa vurugu hizo
 Mmoja wa askari akikagua uharibifu mkubwa uliofanywa katika gari hilo kufuatia vurugu za kuchomwa moto kituo hicho cha Polisi Bunju mapema leo na wananchi.
 Imevunjwa kioo chote cha nyuma
Baadhi ya polisi wakiangalia uharibifu uliofaywa na baadhi ya watu waliovamia kituo  hicho cha polisi Bunju,kufuatia tukio la kudaiwa kugongwa na gari mwanafunzi mmoja na kufa papo hapo.

TUTAWALETEA HABARI ZAIDI YA KADIRI ZITAKAVYOPATIKANA.

SIKU YA PSPF YAFANA SABASABA WENGI WAJIUNGA NA MFUKO

$
0
0
·         ORIGINAL KOMEDI WAWA KIVUTIO

Siku ya PSPFiliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF ilifana na kuvutia mamia ya wananchi waliotembelea maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Siku hiyo ni maaluma kwa ajili ya kutoa elimu ya Mfuko wa PSPF kwa umma ili waweze kupata uelewa mpana wa sekta ya Hifadhi ya Jamii hususan bidhaa na huduma zinazotolewa na PSPF, kwa mwaka huu, PSPF ililenga kuhimiza watanzania kujiunga na Hifadhi ya Jamii kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari unaoendeshwa na PSPF.

Kwa mujibu wa takwimu zilizipo zaidi ya asilimia 90 ya watanzania hawapo katika Hifadhi ya Jamii, hivyo jukumu kubwa la siku ya PSPF mwaka huu ni kuhakikisha watanzania wengi wanajiunga na PSPF, jambo hilo lilifanikiwa kwani zaidi ya watu 500 walijiunga na PSPF katika maonesho ya sabasaba ya mwaka huu.

Siku hiyo ilitumika kuwahamasisha wanachama wa PSPF kuwa na utaratibu wa kuhakiki taarifa zao mbalimbali ikiwawemo, historia ya michango, historia ya pensheni, kufuatilia mafao, kujisajili katika Mfuko na pia PSPF ilikuwa ikitoa vitambulisho vipya kwa wanachama wake.

Katika kunogesha siku ya PSPF, Mfuko uliwaalika, Balozi wa PSPF Mjomba Mrisho Mpoto, waigizaji wote wa kikundi cha Original Komedi na Mboni Masimba mtangazaji na mwaandaaji wa kipindi cha The Mboni Show kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha TBC, kwa udhamini wa PSPF.

Baadhi ya wageni mashuhuri waliotembelea banda la PSPF wakati wa maonesho hayo ni pamoja na Mheshimiwa Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda, Waziri Mkuu, Mheshimiwa Gaudentia Kabaka, Waziri wa Kazi na Ajira, Mheshimiwa Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi, Mheshimiwa Shaaban Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na wengine wengi.

Kwa mwaka wa pili mfululizo Mfuko wa Pensheni wa PSPF umekuwa ukitenga siku maalum wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam (sabasaba) kwa ajili ya kutoa elimu juu ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii na huduma zinazotolewa na PSPF.

 Msanii mahiri wa kughani mashairi Mrisho Mpoto akiwa ameambatana na baadhi ya wasanii wa kundi la Original Komedi walipokuwa wakikatiza viunga vya saba saba.
 Baadhi ya wasanii wa kikundi cha Original Komedi wakionesha mbwembwe zao
 Baadhi ya wadau wakiendelea kujiunga na mfuko huo wa PSPF ndani ya viunga vya saba saba.

VIONGOZI NCHINI WATAKIWA KUSHIRIKI MKUTANO MABADILIKO YA TABIA YA NCHI NCHINI ETHIOPIA

$
0
0
 Na Chalila Kibuda ,Globu ya Jamii

VIONGOZI nchini wametakiwa kushiriki katika mkutano wa mabadiliko ya tabia ya nchi utakaofanyika Julai 13 na 16 Addis Ababa Ethiopia.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia ya Nchi (CAN),Sixsbaty Mwanga amesema mkutano huo ni muhimu kutokana hali iliyopo sasa katika mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kuongezeka ukame ,njaa pamoja na mafuriko, hivyo viongozi wanaweza kushawishi mkutano katika kuongeza bajeti katika eneo hilo katika kukabiliana na majanga hayo.


Amesema fedha ya kuweza kupambana na mabadiliko hazitoshi kufikia mwaka 2020, Tanzania kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi itatumia Trilioni mbili  kwa mwaka kutokana na ambayo itakuwa imefikia katika mabadiliko ya tabia.


Mwanga amesema fedha za mabadiliko ya tabia ya nchi zinatakiwa ziwekwe wazi ili kusaidia wananchi kuweza kupata msaada pale panapotokea majanga ya ukame na mafuriko na waketi mwingine fedha hizo zinapotea na kushindwa kutatua matatizo yanayotokana  na mabadiliko hayo .


Amesema mikutano iliyopita haikuwa na changamoto ya tabia ya nchi lakini sasa tatizo limezidi kukua kutokana na hali iliyopo kufikia mwaka 2020 vifo vitakuwa vya kila siku vinavyotokana na mabadiliko hayo.


Amesema katika malengo 17 ya maendeleo endelevu ya masuala ya tabia ya nchi yanatakiwa kuangaliwa kwa katibu katika kila kpengele katika kuweza kukabili hali hiyo.


Hata hivyo CAN inatarajia kufanya maandamano  ya matembezi  amani Julai 12 ambayo itashirikisha zaidi ya wadau 400 wa mazingira kushiriki na kupaza sauti, na matembezi hayo yataanzia katika chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) na kuishia katika kiwanja cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia ya NCH I(CAN) ,Sixsbaty Mwanga akizungumza na waandishi  wa habari (hawapo pichani)  katika mkutano wa mabdiliko tabia nchi katika kuelekea mkutano wa viongozi utaofanyika nchini Addis Ababa,Ethiopia uliofanyika leo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
Baadhi ya waandishi wakifatilia taarifa Mratibu wa Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia ya NCHI(CAN) ,Sixsbaty Mwanga hayupo pichani katika mkutano uliofanyika leo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

NHIF YAKABIDHI MSAADA WA MASHUKA 200 KWA HOSPITALI YA MKOA MJINI SINGIDA

$
0
0
DSC00136
Meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Singida, Alli Amanzi msaada wa mashuka 200 kwa ajili ya hospital ya mkoa mjini hapa.(Picha na Nathaniel Limu).
DSC00132
Mkuu wa wilaya ya Singida,Alli Amanzi (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoa wa Singida, Agnes Chaki (katikati) muda mfupi kabla Meneja NHIF hajakabidhi mashuka 200 kwa hospitali ya mkoa mjini hapa.Kushoto ni Afisa uthibiti ubora wa huduma NHIF mkoani hapa, Dk.Edwin Mwangajilo.

Na Nathaniel Limu, Singida
HOSPTALI ya mkoa wa Singida iliyopo mjini hapa,inakabiliwa na uhaba mkubwa wa mashuka kitendo kinachochangia wagonjwa kutumia mashuka yao binafsi wakati wote wanapokuwa wamelazwa hospitalini hapo.

Hayo yamesemwa na Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Henry Mgetta, wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya msaada wa mashuka 200 yaliyotolewa msaada kwa hospitali ya mkoa na mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mkoani Singida.Alisema hospitali hiyo yenye vitanda 300 vya kulaza wagonjwa,inakabiliwa na uhaba wa mashuka 2,400 na magodoro 230.

“Hali ni mbaya mno,shuka 100 tulizonazo,ni chakavu na kwa ujumla nazo hazifai kwa matumizi ya binadamu.Wagonjwa wanaolazwa inawalazimu kutumia shuka zao binafsi jambo ambalo halikubaliki”,alisema Dk.Mgetta. Alisema mbali na uhaba wa shuka na magodoro,hosptali hiyopia ina uhaba wa vitanda na hasa kwenye wodi ya wazazi, kitendo kinachochangia wajawazito wanne watumie kitanda kimoja.

“Natoa wito kwa wadau mbalimbali,waangalie uwezekano wa kuisaidia kwa hali na mali hospitali yetu hii na vituo mbalimbali,ili viweze kutoa huduma bora inayokidhi mahitaji ya wananchi”’alisema Dk.Mgetta. Kwa upande wake Meneja wa NHIF mkoa wa Singida, Agnes Chaki,alisema kuwa wametoa msaada huo wa mashuka hayo baada ya kuombwa na serikali ya wilaya ya Singida.

Alisema majukumu ya NHIF,ni pamoja na kuhakikisha vituo vya kutolea huduma za afya zinajitosheleza kwa kuwa na mahitaji yote muhimu kwa kutoa misaada na vile vile mikopo ya kununulia dawa,vifaa tiba na uboreshaji wa majengo.

“Nina imani kituo cho chote cha afya,zahanati na hospitali,kinapokuwa na vitanda,mashuka na mambo mengine muhimu kwa wagonjwa wanaolazwa,kitendo hicho kitakuwa kinawajengea mazingira mazuri ya kuendelea na matibabu bila usumbufu wo wote”,alifafanua meneja huyo.

Chaki alisema NHIF itaendelea kutoa misaada mbalimbali kadri uwezo utakavyoruhusu kwa lengo la kusaidiana na serikali katika kuboresha utoaji wa huduma za afya.

In Tanzania, protecting refugees from cholera

$
0
0
IMG_20150620_094935
Refugees at the Nyarugusu Camp receive the Oral Cholera Vaccine. (c) UNICEF Tanzania/2015/Thomas Lyimo.

Last week the Oral Cholera Vaccine, OCV, was administered at the Nyarugusu Refugee Camp, in Kigoma Region, Tanzania, to over 106,000 refugees from the Congo and – more recently – Burundi, out of an estimated camp population of 120,000 (children under the age of one were not vaccinated, hence the discrepancy in numbers). Medicins Sans Frontiers (MSF), who administered the vaccine, administered to Muslims observing Ramadan after sundown. We had been concerned whether the whole eligible community would receive the vaccine – and they did!

This is a significant event not only for the huge numbers of people who have been given the vaccine but also because it’s the first time the OCV has been administered in an emergency situation in Tanzania Mainland. Previously we simply relied on WASH (water, sanitation and hygiene) interventions, by sensitizing the people on good practices to help prevent diseases. However, given that refugees are still arriving from Burundi, this compromises our WASH interventions as facilities are no longer sufficient to meet the growing numbers. What makes OCV special is that it can help to fill this gap easily and quickly.

I’m a Health Specialist at UNICEF and as such my part in the OCV campaign has been to support the social mobilization task force – which is a key aspect of the campaign’s success. In the camp, in partnership with the Tanzanian Red Cross Society, we have trained 121 health information volunteers – community workers from the refugee community. They conduct household visits providing key messages not only on the OCV, but also cholera prevention through appropriate hand washing at critical times, and safe latrine use.


TANZANIA BOYS YANYAKUA KOMBE LA MIAKA 40 YA MSUMBIJI JIJINI MAPUTO

$
0
0
Timu ya vijana Watanzania, Tanzania Boys ilicheza ligi maalum ya kusherehekea miaka 40 ya Uhuru wa Mozambique na kufanikiwa kulichukua kombe hilo baada ya kufikisha pointi 7.Mchezo wa kwanza Tanzania Boys 4 na Laulane Sports 3, mechi ya pili Tanzania Boys 4 Raiva Mfalala 2 na mechi ya mwisho Tanzania Boys 5 na 25 de Setembro 5. Tanzania Boys walimkabidhi kikombe hicho Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Mhe. Shamim Nyanduga ofisini kwake.
 Timu ya vijana Watanzania, Tanzania Boys iliyocheza ligi maalum ya kusherehekea miaka 40 ya Uhuru wa Msumbiji
 Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Mhe. Shamim Nyanduga akikabidhiwa kikombe na Kiongozi wa Timu ya Tanzania Boys Salum Magimba.

Balozi Nyanduga akiwa na baadhi ya  wachezaji wa timu ya vijana Watanzania, Tanzania Boys iliyocheza ligi maalum ya kusherehekea miaka 40 ya Uhuru wa Msumbiji

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM MJINI DODOMA LEO, TANO BORA YA WAGOMBEA KUPATIKANA BAADA YA KIKAO HIKI

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) kinachoendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, Mjini Dodoma. Kikao hiki kinapitia majina yote 38 ya Watangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, ambapo majina matano yatapatikana baada ya kikao hiki.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM - Zanzibar, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara, Mzee Phillip Mangula (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, DODOMA.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiwa kwenye Kikao cha kupitia Wagombea wanaowania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia CCM, ambapo majina matano yatapatikana katika kikao hiki na kupelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM ili kupata majina matatu yatakayokwenda kupigiwa kura kwenye Mkutano Mkuu.
Baadhi ya Wapigapicha za Habari wakichukua taswira ya Wazee wa Kamati ya Ushauri wa Chama.
Wazee wa Kamati ya Ushauri ya CCM ikiongozwa na Rais Mstaafu awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Mzee Pius Msekwa, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mh. Aman Abeid Karume, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Cleopa Msuya pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim.

KAMANDA MPINGA AFUNGUA NUSU FAINALI MASHINDANO YA SOKA YA BODABODA (MPINGA CUP)

$
0
0
 Kamanda wa Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga akiwasalimia kwa kuonesha vidole baada ya kuzikagua timu za Foma na Mtongani katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya mpira wa miguu ya timu za Bodaboda ya Mpinga Cup, Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam leo.Lengo la mashindano hayo yaliyoshirikisha timu 108 ni kutoa elimu ya usalama barabarani kwa Bodaboda. Kushoto kwake ni Msimamizi wa mashindano hayo, Mrakibu Msaidizi wa Polisi,Mbunja Matibu. (PICHA NA RICHARD  MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Mchezaji wa timu Foma (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa timu ya Mtongani.
Ni heka heka katika lango la timu ya Foma.

MADAKTARI BINGWA WA MOYO WAFANYA ZIARA MKOA WA SIMIYU.

$
0
0


 Madaktari  bingwa kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakimfanyia  upasuaji  mgonjwa  katika hosptali ya Wilaya ya Bariadi mkoani  Simiyu Zowezi  hilo lina endelea katika  hosptali ya Wilaya ya Bariadi hadi sasa zaidi ya watu 480
Bingwa wa magonjwa ya moyo Dokta Tatizo Wane akimpima mgonjwa kwa kutumia mashine ya kisasa inayojulikana kama ECHOCARDIOGRAM Machine Zowezi  hilo lina endelea katika  hosptali ya Wilaya ya Bariadi hadi sasa zaidi ya watu 480.
 Wakazi wa mji wa Bariadi na maeneo  ya  jirani wakisubiri huduma za matibabu za madaktari  bingwa kaitka hosptali ya Wilaya ya Bariadi mkoani  Simiyu. 
Viewing all 110171 articles
Browse latest View live




Latest Images