Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 899 | 900 | (Page 901) | 902 | 903 | .... | 3286 | newer

  0 0


  0 0

  Yassini A Kapuya Business Consultant, Author na mmliki wa  TBX Entrepreneurs Magazine Kuzindua kitabu chake cha Tatu.. Ni jinsi gani ya kuwa bingwa katika mauzo.  Ameandika kutokana na ujuzi ulio mpatia tuzo za mauzo bora  nyingi tu Marekani. 

  0 0

  SHIRIKA LA MAJI SAFI NA MAJITAKA DAR-ES-SALAAM (DAWASCO),  LINAWATANGAZIA  WAKAZI WA JIJI LA DAR-ES-SALAAM NA MJI WA BAGAMOYO MKOANI PWANI  KUWA, UTARATIBU WA KUPATA BILI KWA MTEJA UMEBADILIKA KUTOKA “SPOT BILL” KWENDA “SPOT SMS” KUANZIA  JULAI 2015.

  UTARATIBU HUU UNAMAANISHA KUWA MTEJA ATAKUWA AKIPATIWA BILL YAKE YA MATUMIZI YA MAJI KILA MWEZI KUPITIA SIMU YAKE YA MKONONI, NA UTALENGA WATEJA WA MAJUMBANI TU NA HAUTAHUSISHA KAMPUNI NA TAASISI ZA SERIKALI.

  FAIDA ZA UTARATIBU HUU NI PAMOJA NA :
  1.KUBORESHA HUDUMA KWA MTEJA NA KUONGEZA MAWASILIANO YA MOJA KWA MOJA KATI YA SHIRIKA NA MTEJA
  2.MAENDELEO YA TECKNOLOJIA YANAKOPELEKEA UMUHIMU WA HUDUMA HII
  3.KUONGEZA WIGO WA ULIPAJI KWA MTEJA
  4.KUPUNGUZA GHARAMA ZA UTARATIBU WA AWALI

  NAMNA MTEJA ANAWEZA KUJISAJILI KUPATA HUDUMA HII KUPITIA NJIA ZIFUATAZO

  1.TOVUTI YA SHIRIKA www.dawasco.com
  2.KUMPA MSOMA MITA WA DAWASCO TAARIFA ZAKO
  3.KUFIKA OFISI YOYOTE YA DAWASCO ILIYO KARIBU NAWE

  EWE MTEJA, TOA NAMBA YAKO YA SIMU ILIYO SAHIHI ILI KUPATA BILI YAKO KILA MWEZI NA KUEPUKA USUMBUFU WA KUKATIWA HUDUMA HII .
  KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA HUDUMA KWA WATEJA NAMBA 022- 2194800 AU 0658-198889       

  IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
  DAWASCO-MAKAO MAKUU
  “DAWASCO MBELE KWA MBELE”

  0 0


  0 0


  Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. 
  Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ?
  Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu
  HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME
  Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo :
  Hatua  ya  kwanza, ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na  kuwa  mgumu  kama  msumari.
  Na  hatua  ya  pili  ni  lazima, uume  wake  uendelee  kusimama  kwa  muda  mrefu  wakati  wa  tendo  la  ndoa.  Hatua  zote  mbili  zinapo  kamilika, ndipo  tunapo  pata  kitu  kinaitwa  STRONGER  AND  LONGER  ERECTION.


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akibonyeza kitufe cha kengere kuashiria ufunguzi rasmi wa Ukumbi mpya na wakisasa wa mikutano wa CCM unaofahamika kwa jina la Dodoma Convention Centre, uliopo njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, mjini Dodoma leo Julai 9, 2015.Kulia kwake ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara, Mzee Phillip Mangula (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing wakifunua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Ukumbi mpya na wakisasa wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, uliopo njia ya kuelekea Chuo Kikuu cha UDOM, mjini Dodoma leo Julai 9, 2015.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Kikwete, akimkabidhi mfano wa ufunguo wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana, baada ya kuufungua rasmi ukumbi huo leo Julai 9, 2015 mjini Dodoma.
  Picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali baada ya uzinduzi huo.


  0 0
 • 07/09/15--05:37: AIRTEL FURSA YATUA MWANZA
 •  Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea na vijana
  wa Mwanza wakati wa uzinduzi  wa warsha maalum kwa vijana  ya'Airtel
  Fursa'  kutoka Airtel Tanzania yenye lengo la kuwawezesha Vijana
  wajasiliamali nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji
  Mwanza.
   Baadhi ya vijana wa mwanza wakifuatilia kwa makini mafunzo yalikuwa
  yakiendeshwa na Airtel Fursa yenye lengo la kuwawezesha vijana kupata
  mafunzo kwenye usimamizi wa fedha, upatikanaji wa mikopo, kufungua
  akaunti ya benki na mambo muhimu katika kuendesha biashara. Warsha
  hiyo ilifanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji Mwanza.
   Meya Stanslaus Mabula akiongea na vijana Mwanza wakati wa uzinduzi  wa
  warsha maalum kwa vijana  ya'Airtel Fursa'  kutoka Airtel Tanzania
  yenye lengo la kuwawezesha Vijana wajasiliamali nchini iliyofanyika
  katika ukumbi wa Halmashauri ya jiji Mwanza.
   Mtaalamu wa maswala ya kijamii na ujasiliamali bw, Fidelis Madaha
  akifundisha mada ya Masoko katika warsha ya Airtel fursa iliyofanyika
  katika ukumbi wa halmashauri ya jiji jana. Airtel inaendesha warsha
  hizo kwa lengo la kuwawezesha vijana kupata mafunzo kwenye usimamizi
  wa fedha, upatikanaji wa mikopo, kufungua akaunti ya benki na mambo
  muhimu katika kuendesha biashara.

  0 0

  Jamii yashauriwa kujenga utamaduni wa kusaidia watu wenye shida mbalimbali hasa wazee, watu wenye ulemavu na watoto yatima ili waweze kujisikia wanaishi sawa na watu wengine.

  Wito huo umetolewa na Meneja wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani Allen Nyumbo wakati alipokuwa akikabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa niaba ya Taasisi yao ya Vodacom Foundation kwa wazee kutoka kaya 65 za kijiji cha Mnimbila katika jimbo la Mtama jana.

  Nyumbo alisema kuwa matatizo ya wazee, walemavu, na watoto yatima yanahitaji kutatuliwa na watu wenye moyo wa huruma ambao wanaguswa na shida za makundi hayo,hivyo ni vyema kila Mtanzania na mashirika mbalimbali yakaona umuhimu wa kusaidia makundi hayo ambayo yanajiona na kuisi yametengwa.

  Alisema Vodacoma Foundation imeona umuhimu wa kusaidia chakula, mchele, sukari, unga wa mahindi, mafuta ya kula natende katika kaya hizi zilizopo Lindi, Kigoma, Rufiji, pamoja na Dar es salam baada ya kusukumwa na kuona umuhimu wa makundi hayo katika jamii.

  Akizungumza kwania ya wakazi wa kijiji hicho Sophia Nyamanzi alisema msaada huo umewafikia katika wakati mzuri kutokana na kupanda kwa bei ya vyakula hali ambayo inawafanya kushindwa kumudu hata kufuturu kwa msimu huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

  Nyamanzi alisema kuwa mahitaji yao ni makubwa lakini msaada hao umepunguza kiasi cha shida zao walizokuwa wanazikabili kwa wakati huu ila wanaomba watu wengine wanaokuguswa na familia kama zao kuiga mfano wa Vodacom Foundation ili waweze kuwasaidia.
  Meneja wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani Lindi, Allen Nyumbo(watatu toka kushoto) akimkabidhi Mzee Selemani Musa Mkazi wa Lindi kapu lenye vyakula mbalimbali kama msaada kwa ajili ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake Pamoja na Vodacom.
  Sophia Nyamazi kazi wa kijiji cha Mnimbila Lindi Mkoa wa Pwani(kulkia)pamoja na wenzake wakipokea kapu lenye vyakula mbalimbali toka kwa baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani ikiwa ni kama msaada kwa ajili ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake Pamoja na Vodacom.
  Mkazi wa Lindi Mkoa wa Pwani Aisha Saleh(wane toka kushoto)akipokea kapu lenye vyakula mbalimbali toka kwa baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani ikiwa ni kama msaada kwa ajili ya Mwezi mtukufu wa Ramadhani msaada huo ulitolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kupitia kampeni yake Pamoja na Vodacom.

  0 0

  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (kulia) pamoja na Rais wa Cambridge Development Initiative (CDI), Bw. Ravi Solanki wakitia saini makubaliano ya kuimarisha elimu ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini jana jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni Afisa Mwandamizi wa uwekezaji, NEEC, Bw. Oswald Karadisi (kulia) na Mkurugenzi Ujasiriamali wa CDI, Bi. Georgia Ware.
  Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa (kulia) akipongezana na Rais wa Cambridge Development Initiative (CDI), Bw. Ravi Solanki (kushoto) baada ya kutia saini makubaliano ya kuimarisha elimu ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini jana jijini Dar es Salaam. katikati ni Mkurugenzi wa Ujasiriamali wa CDI, Bi. Georgia Ware.

  Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

  Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limefikia makubaliano na Cambridge Development Initiative (CDI) ili kuimarisha mafunzo ya maswala ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini.

  CDI ni mpango ulioasisiwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini uingereza ambapo wanafunzi wenye vipaji toka chuo hicho na vyuo vikuu hapa nchini wanakutana, kubadilishana uzoefu ili kutatua changamoto mbalimbali.

  Mkataba wa makubaliano hayo umetiwa saini na Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng’i Issa wakati Rais wa mpango huo, Bw. Ravi Solanki aliwakilisha wenzake.

  Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam baada ya kutia saini mkataba huo, Bi. Beng’i alisema elimu na maarifa ya ujasiriamali ni muhimu sana kwa sasa ambapo changamoto ya ajira ni kubwa dunia nzima, Tanzania ikiwa mojawapo.

  “Mzingatie sana maarifa mnayopata hapa…yatawasaidia katika maisha yenu,” aliwaasa wanafunzi hao.


  0 0

  Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Wallace Karia ametuma salama za pongezi kwa uongozi mpya wa klabu ya Coastal Union uliochaguliwa mwishoni mwa wiki.

  Katika salamu zake kwa Mwenyekiti mpya wa klabu hiyo Dr. Twaha, Karia amesema anawapa pongezi wa kuchaguliwa na kupewa heshima hiyo na wanachama wa Coastal Union katika kuitumikia klabu yao.

  “Kikubwa wanachopaswa kufanya kwa sasa ni kuodokana na makundi ya aina yoyote, na kuifanya Coastal Union kuwa kitu kimoja na kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom” alisema Karia.

  Aidha Karia amesema, TFF itashirkiana na uongozi mpya katika utendaji wa kazi na kuleta maendeleo katika mpira miguu nchini.

  Klabu ya Coastal Union yenye makazi yake jijini Tanga ilifanya uchaguzi wake mwishoni mwa wiki na kuwapata viongozi wake wapya, akiwemo mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

   Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa (kushoto) akimkabidhi mfano wa ufunguo wa gari mshindi wa Promosheni ya 'Tuma Pesa na Simbanking Shinda Passo’, Peter Fundi katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkabidhi mfano wa funguo mshindi wa Promosheni ya ‘Tuma Pesa na Simbanking Shinda Passo’, Peter Fundi. Kushoto ni Meneja wa benki hiyo Tawi la Mzumbe, Jane Maganga.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya  Makamu wa Rais Anjelina Madete(katikati)  akifungua mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya zebaki uliofanyika jana kwenye hoteli ya peacock  jijini Dares Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka ofisi hiyo, Joseph Kihaule na  kushotoni Mwakilishi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti(UNITAR), Carlos Maren.
   Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Joseph Kihaule (kushoto)akisisitiza jambo wakati akiongoza mkutano wa Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya Zebeki uliofanyika jana kwenye hoteli ya peacock  jijini Dares Salaam, kulia ni Mwakilishi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti(UNITAR), Carlos Maren.
  Issaria Mangalili akitoa mada juu ya mikataba mbalimbali inayohusu kemikali mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya Zebeki uliofanyika jana kwenye hoteli ya peacock  jijini Dares Salaam.
   Mhandisi Peter Nyangombe (wa pili kushoto) akitoa mada juu ya Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya Zebeki uliofanyika jana kwenye hoteli ya peacock  jijini Dares Salaam.
   wadau wa mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya Zebeki uliofanyika jana wakijadiliana  jambo  kwenye hoteli ya peacock  jijini Dares Salaam.
   Picha ya pamoja kati ya Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya  Makamu wa Rais Anjelina Madete(wa pili kushoto)  mara baada ya kufungua mkutano wa  Mkataba wa  Minamata kuhusu  madini ya Zebeki uliofanyika jana kwenye hoteli ya peacock  jijini Dares Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira kutoka ofisi hiyo, Joseph Kihaule na  (wa pili kulia) ni  Mwakilishi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mafunzo na Utafiti(UNITAR), Carlos Maren. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa mazingira kutoka ofisi hiyo, Rogathe Kisanga.
  Picha na Magreth Kinabo – Maelezo

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe, amesema upatikanaji wa gesi ni nyenzo muhimu ya uendelezaji wa viwanda vya kati ili kutengeneza ajira na kuharakisha maendeleo ya nchi.

  Mhe. Membe alipongeza uamuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuichagua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tatu za Afrika itakapohamishia baadhi ya viwanda vyake, akazitaka taasisi za uwekezaji na uendelezaji wa viwanda kuweka mikakati madhubuti ya kutumia fursa hiyo kikamilifu.

  Mhe. Waziri alisema hayo leo wakati wa mhadhara wa aliyekuwa Mchumi Mkuu na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Prof. Justin Yifu Lin, kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar Es Salaam, uliohudhuriwa na wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na wadau wengine.

  Alisema uendelezaji wa viwanda lazima utiliwe mkazo katika mpango wa Tanzania kuingia uchumi wa kati 2025. "Tuache kukimbilia viwanda vikubwa vinavyohitaji mitaji mikubwa, ambayo hatuna.Tuchague viwanda vya kati vitakavyoajiri watu wengi kwa uwekezaji wa wastani."

  Mhe. Membe alisema uendelezaji wa viwanda usambae nchi nzima ili kuvutia vijana kuishi vijijini badala ya kukimbilia mijini. "Sasa hivi nchi yetu ina viwanda takriban 3,000 lakini zaidi ya theluthi mbili viko Dar Es Salaam. Lazima umeme upelekwe vijijini kuleta uwiano wa maendeleo ya viwanda," alisisitiza.

  Katika mhadhara wake, Prof. Lin alisema nchi nyingi zinazoendelea zilifanya maamuzi yasiyo sahihi kuhusu viwanda. "Nchi nyingi zilifuata kile kinachoitwa Muafaka wa Washington na kuanzisha viwanda vikubwa kwa maelekezo ya nchi tajiri, ambavyo viliwashinda kuendesha kwa kuwa vilihitaji uwekezaji mkubwa sana."

  Alisema nchi za Asia zilizoendelea kwa haraka ni zile zilizoamua kuzingatia mazingira halisi na kwenda hatua kwa hatua katika kuanzisha viwanda. "Hii iliimarisha uchumi wao na kuukuza."

  Prof. Lin alisema serikali zina wajibu wa kusimamia uendelezaji wa viwanda kwa kuweka sera sahihi, kuhimiza uwekezaji kwenye uzalishaji wa bidhaa zenye masoko ya uhakika na kusaidia sekta binafsi ishiriki kikamilifu.

  Akiongelea Tanzania, Mchumi huyo wa Kichina alisema ingawa gharama za ajira ziko chini, gharama za uendeshaji ziko juu, hivyo hazivutii uwekezaji. Alisema moja ya sababu kubwa za Shilingi ya Tanzania kushuka thamani ni uuzaji mdogo wa bidhaa nchi za nje.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb.), akiongea kwenye muhadhara kabla ya Mtoa mada mkuu Prof. Justin Yifu Lin hajaongea katika muadhara uliokuwa unazungumzia umuhimu wa viwanda nchini ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje
  Makamu wa Rais wa zamani wa Benki ya Dunia, Prof. Justin Yifu Lin akitoa mada yake juu ya uwanzishaji wa viwanda nchini Tanzania katika muadhara ulioandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0


  0 0

  Mwenyekiti wa Kampeni iliyolenga kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia wanahabari wanaougua magonjwa sugu yakiwepo ya saratani, (MEDIA CAR WASH FOR CANCER) , Benjamin Thompson akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kiasi cha fedha kilichopatikana katika harambee ya jijini Dar es Salaam ambapo kiasi cha shilingi Milioni 31 zilipatikan ikiwa ni ahadi na taslimu. Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa MAELEZO, Zamaradi Kawawa. Harambee nyingine kama hiyo inataraji kufanyika Jijini Mwanza mwezi Agosti mwaka huu.
  Mwenyekiti wa Kampeni iliyolenga kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia wanahabari wanaougua magonjwa sugu yakiwepo ya saratani, (MEDIA CAR WASH FOR CANCER) , Benjamin Thompson akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kiasi cha fedha kilichopatikana katika harambee ya jijini Dar es Salaam leo, ambapo kiasi cha shilingi Milioni 31 zilipatikan ikiwa ni ahadi na taslimu. Pamoja nao ni Wajumbe wa Kamati hiyo Mkurugenzi Msaidizi wa MAELEZO, Zamaradi Kawawa (kulia) na Judicate Shoo.Harambee nyingine kama hiyo inataraji kufanyika Jijini Mwanza mwezi Agosti mwaka huu.
  Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa katika mkutano huo hii leo. Kutoka kushoto ni Mroki Mroki, Leah Samike, Judicate Shoo, Mwenyekiti Benjamin Thomson, Zamaradi Kawawa, Angela Michael Msangi, Grace Nakson na Somoe Ng'itu. Harambee nyingine kama hiyo inataraji kufanyika Jijini Mwanza mwezi Agosti mwaka huu.

  0 0

  A special edition of BBC World Service’s global radio programme, BBC Africa Debate, will be coming from the British Museum in London. Presented by the BBC’s Alex Jakana and Zeinab Badawi and recorded in front of an invited audience, it will ask if Africa has outgrown development aid.

  Ten years ago the British Museum hosted the launch of the UK-government-led ‘Commission for Africa’. This was the time of a popular global movement to Make Poverty History in Africa, a revival of Live Aid concerts, and promises from the leaders of the world’s most developed nations to increase aid to Africa. The Commission for Africa encouraged partnership between Africa and the developed world, rather than a relationship of dependency. BBC Africa Debate will explore if this is now happening and asks if the continent is now in a position to be an agent of its own progress.

  The BBC debate coincides with the UN Financing for Development conference in Addis Ababa, Ethiopia, and comes just weeks after Kenya's President Uhuru Kenyatta urged fellow African leaders to stop receiving foreign aid. The panel will be:

  Andrew Mitchell - Secretary of State for International Development, 2010-12;

  Oby Ezekwisili - Co-founder of Transparency International, former World Bank Vice President for Africa and former Education Minister of Nigeria;

  Tutu Agyare - Managing Director of Nubuku Investments;

  Giles Bolton - author of "Aid and other dirty business", previously worked for DFID and now Responsible Sourcing Director at Tesco.

  Audiences can join the debate via social media, with conversations on Twitter (#bbcafricadebate) and on Facebook and Google+ (search for BBC Africa).

  BBC Africa Debate will be pre-recorded on Monday 13 July and broadcast at 19.00GMT (20.00 British Summer Time) on Tuesday 14 July. It will also be available as a podcast on the BBC World Service website.

  This edition of BBC Africa Debate is made with support from the Royal African Society.

  0 0

   Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. 
  IDARA ya Uhamiaji katika awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete imeingiza zaidi ya Sh.bilioni 474 kwa kipindi cha miaka 10 ambayo imetokana na maboresho mbalimbali katika idara hiyo.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamishina wa Fedha na Utawala,Piniel Mgonja amesema kuwa katika awamu ya nne uhamiaji imeweza kufanya kazi ya kisasa kutokana na mifumo pamoja na ujenzi wa Chuocha kuendeleza maafisa wa idara hiyo.

  Amesema katika utoaji wa hati ya kusafiria kwa mwezi wanatoa hati 5000 tofauti na miaka 10 iliyopita ambapo walikuwa wakitoa hati 2500 ambayo ilikuwa ikitokana na kuchukua muda mrefu wa kuchapa kuliko ivyo sasa zinachapwa kwa kompyuta.

  Mgonja amesema katika suala la uhamiaji bado changamoto kutokana na kuwa na uwazi katika mipaka ambapo walifanya uparesheni kuwakamata zaidi ya watu 74 000 kati ya hao watu zaidi 66000 waliondolewa nchini.
  Amesema wamezidi kuimarisha katika udhibiti wa njia za mipaka ili nchi isiweze kugubikwa na wahamiaji haramu.

  Amesema katika kipindi kijacho hati kusafiria kwa nchi za Afrika Mashariki itakuwa moja ya kimataifa ili kuondoa usumbufu kwa wateja wao kutafuta mara kwa mara kwa hati ya kusafiria kwa Afrika Mashariki
  Kamishina wa Fedha na Utawala wa Idara ya Uhamiaji, Piniel Mgonja akizungumza na waandishi habari juu ya mafanikio ya idara ya uhamiaji katika awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete iliyofanyika leo Makao Makuu ya Idara hiyo Kurasini jijini Dar es Salaam.
   Makamishina wa Idara ya Uhamiaji wa kwanza kushoto  kutoka mwanzo ,Msemaji wa Idara ya Uhamiaji,Naibu Kamishina wa Idara ya Uhamiaji ,Abbas Irovya ,Naibu Kamishina Mussa Lyamba,Mratibu Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji ,Petro Malima ,Mhasibu Mkuu Karunde ,pamoja na Mkaguzi wa Idara hiyo, Kyando wakimsikiliza Kamishina wa Fedha na Utawala ,Piniel Mgonja katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji Kurasini,jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya watenadaji wa ngazi za juu wa Idara ya Uhamiaji  pamoja na waandishi wakimsikiliza Kamishina wa Fedha na Utawala wa Idara ya Uhamiaji,Piniel Mgonja katika mkutano  uliofanyika jijini Dar es Salaam.Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

  0 0

  TX4A9780Mama wa mitindo hapa Tanzania maarufu kwa jina la Asya Idarous Khamsin na Titty wanakuletea futari ya pamoja ndani ya Terrace Lounge, Msasani City Mall,siku ya Jumapili 12, July 2015 kwaanzia mida ya saa kumi na mbili kamili hadi saa mbili usiku. Jipatie kadi yako kwa shilingo 25,000/= tu! kwani 15000/= ni special kwaajili ya Dinner yako, inayobaki ni sadaka itakayo tumika kununulia Khanga zitakazo pelekwa Hospitalini kwa wagonjwa wanawake siku ya IDD. Hivyo kwa moyo wa kujitolea nyote mnakaribishwa kushiriki katika zoezi hili, pia kwa mawasiliano zaidi piga namba o784263363 au 0754273472.Futari

  0 0

   Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mohamed Ally Mohamed (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati akifungua semina hiyo Dar es Salaam leo asubuhi. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Maafa na Dharura, Dk.Elias Kwesi.
   Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Maafa na Dharura, Dk.Elias Kwesi (kulia), akizungumza katika semina hiyo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Mohamed Ally Mohamed kufungua semina hiyo. 

   Ofisa Mradi wa Usalama Barabarani wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Marry Kessy (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa mada kwenye semina hiyo.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

older | 1 | .... | 899 | 900 | (Page 901) | 902 | 903 | .... | 3286 | newer