Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 898 | 899 | (Page 900) | 901 | 902 | .... | 3285 | newer

  0 0

  JUMLA ya watu milioni 11,248,194 wameandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura zoezi ambalo linaendelea kwa sasa hapa nchini likiwa limeingia mkoani Pwani. 
  Hayo yalisemwa leo kwenye Kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Damian Lubuva alipokuwa anampa taarifa Rais Dk Jakaya Kikwete mara baada ya kujiandikisha. 
  Bw. Lubuva alisema kuwa malengo ni kuandikisha watu milioni 21 hadi 23 kote nchini mara zoezi hilo litakapokamilika kati ya Julai mwishoni au Agosti mwanzoni kama hakutatokea matatizo. 
  “Hadi sasa ni mikoa 11 inaendelea na zoezi ambayo ni Mwanza Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro Morogoro na jana ulianza mkoa wa Pwani,” alisema Lubuva. 
  Aidha alisema kuwa changamoto zilizojitokeza ni za kawaida hasa kutokana na mfumo huu kuwa ni mpya kwani kila jambo jipya lina changamoto zake. 
  “Mfumo huu ni mpya hivyo lazima kuwe na changamoto za hapa na pale lakini zoezi linakwenda vizuri na tunaamini kuwa tutafanikiwa kama tulivyopanga,” alisema Lubuva. 
  Mkoa wa Pwani una jumla ya vituo 1,752 na mashine za BVR 932 ambapo kata ya Msoga kuna jumla ya vituo 17 zoezi hilo kwa mkoa wa Pwani lilianza jana na litamalizika Julai 20.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektoniki(Biometric Voters Register( BVR) katika kijiji cha Msoga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo leo.Kulia akiangalia kwa makini ni mwandikishaji msaidizi Bi.Happyness Thomas Misana na katikati ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi Tume ya Taifa Uchaguzi Bi.Mariam Rajabu.Kushoto aliyesimama akishuhudia ni Mbunge wa Chalinze Ridhwani Kikwete.
   Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Uchaguzi Taifa ya Uchaguzi Bwana Sanif Khalfan akichukua lama za vidole vya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kijijini kwake Msoga wilaya ya Bagamoyo leo .
   Bwana SANIF Khalfan ambaye ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi akimpiga picha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kupiga kura kwa kutkumia teknolojia mpya ya BVR kijijini Kwake Msoga leo.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitambulisho chake wakati wa zoezi la kujiandikisha kijijni kwake Msoga leo.
   Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya Rais Kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
  Rais Kikwete akimshukuru Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva baada ya kukabidhiwa  kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya  kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo. Picha na Freddy Maro.

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akishuka katika pikipiki (Boda Boda) akitoka kukagua ujenzi wa zahanati kijiji cha Nyamihuu leo.
  Mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa akikabidhi saruji mifuko 60 kwa mwenyekiti wa kijiji cha Nyamihuu Bw Richard Mbembe  kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake.
  Wazee kijiji cha Nyamihuu wakimchangia pesa za fomu Mgimwa kulia.

  Na matukiodaimaBlog
  WAZEE  wa kijiji cha Nyamihuu kata ya Nzihi wamempongeza mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa kwa kumchangia Tsh 100,000 ya kuchukulia fomu tena ya ubunge baada ya kuwatumikia  vizuri kwa muda wa mwaka mmoja wa ubunge wake .

  Wakitoa pongezi hizo leo wakati wa ziara ya mbunge huyo kumalizia ahadi Yake ya Bati 60 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho ,walisema kuwa wamevutiwa na chapakazi wake alioonyesha katika kipindi chake kifupi cha mwaka mmoja.

  Akizungumza kwa niaba ya wazee hao na wananchi wa Kijiji cha Nyamihuu Bi shekela Mvela  alisema wamelazimika kuchangishana kila mmoja kiasi cha Tsh 10,000 na kufikisha kiasi hicho cha Tsh 100,000 kama ahsante Yao kwa mbunge huyo.

  Hata hivyo walisema imani kubwa ambayo wao wameionyesha kwa mbunge huyo ni wazi ni imani ya wananchi wote wa jimbo hilo ambao wamepata kushuhudia Kazi nzuri iliyofanya na mbunge huyo kijana kwa muda mfupi zaidi ukilinganisha na wabunge waliotangulia ambao walikuwa wakiahidi pasipo kutimiza

  Kwa upande wake diwani wa kata ya Nzihi Steven Mhapa mbali ya kumpongeza mbunge huyo kwa utekelezaji wa ahadi zake bado alisema CCM itaendelea kushinda katika jimbo hilo kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani uliofanyika.

  Kwa upande wake mbunge Mgimwa ambae alipokelewa kwa maandamano ya Boda Boda katika kijiji hicho cha Nyamihuu alisema amefarijika zaidi kwa upendo mkubwa ulioonyeshwa na wananchi hao wa Nyamihuu pia mchango wao wa fedha ya kuchukulia fomu

  Alisema kuwa wapo ambao wanaeneza uvumi kuwa hatagombea tena ubunge jambo ambalo si kweli isipo kuwa baada ya bunge kuvunjwa atachukua fomu tena ya ubunge ili kupata kipindi chake cha miaka mitano ya kuwaletea maendeleo wananchi hao wa jimbo la Kalenga .

  mbunge Mgimwa alitaja ahadi mbali mbali zilizokuwa zimebaki kata ya Nzihi na kuzitekeleza leo kuwa katika  kijiji cha kipera amekabidhi Tsh 500,000 kwa kikundi cha Umoja PTC, Kwaya ya mtakatifu Thomas Nzihi amekabidhi Tsh milioni 1, kanisa la TAG nzihi Bati 44 ,kijiji cha Nyamihuu mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji na Kidamali Tsh milioni 1.2 kwa ajili ya ujenzi wa ghala la kijiji.

  Alisema dhamila Yake ni kutimiza ahadi zake zote ndani ya siku mbili hizi ili anapogombea tena ubunge asiwe na kiporo cha ahadi.

  0 0

  Mwanamuziki wa Dance hapa  nchini ambaye anafanya shughuli zake nchini Uingereza, Said Tumba  akizungumza na  Globu ya Jamii na kuwaasa wasanii wa muziki hapa nchini  kutumia vyombo vya asili na si kutumia  vionjo vya kompyuta mara baada ya kufika hapa nchini katika hoteli ya Don Suite iliyoko Ilala, Bungoni jijini Dar es Salaam.
   
   Mwanamuziki wa Dance nchini Kongo, Fiston Lusambo (Filsa Papa) akizungumza na Globu ya Jamii juu ya ujio wao hapa nchini katika hoteli ya Don Suite iliyopo Ilala, Bungoni jijini Dar es Salaam.
   Mmoja wa Wanamuziki kutoka Kinshasa nchini Kongo, Nzaya Nzayad akizungumza na Globu ya Jamii juu ya ujio wao hapa nchini. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika hotel ya Don Suite iliyoko Ilala,Bungoni jijini Dar es Salaam  amesema amekuja jijini Dar es Salaam kutokana na mashabiki wa muziki wa hapa nchini. 
  (Picha na Bakari Issa)

  0 0

   MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiongozana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, (kulia), akiwapungia wana CCM waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Julai 8, 2015. 

  Mwenyekiti huyo wa CCM amewasili na kuanza kazi mara moja ya kuongoza kikao cha kamati ya maadili ili kupokea taarifa za watia nia wa CCM, kabla ya kuanza kuwajadili na kupunguza majina kutoka 39 hadi matano, kazi itakayofanywa na Kamati Kuu ya chama hicho inayotarajiwa kukutana Alhamisi Julai 9, 2015 majira ya usiku. 

  Baada ya zoezi hilo la Kamati Kuu, majina hayo matano yatapelekwa kwenye Halmashauti Kuu ya CCM, nayo itakaa na kuyapunguza tena na kufikia majina matatu ambayo nayo yatapelekwa mbele hya wajumbe zaidi ya 2000 wa Mkutano Mkuu wa chama hicho hapo Julai 12 na kuchaguz jina moja ambalo ndilo litapitishwa nan kuwa mgombea wa CCM wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015
  MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiongozana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, (kulia), akiwapungia wana CCM waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Julai 8, 2015. 
   Rais Kikwete, akisalimiana na viongozi wa juu wa chama hicho, makamu mwenyekiti (Bara), Philip Mangula, Katibu Mkuu, Abdulrahmani Kinana, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye

  0 0

   Daktari Bingwa wa Watoto na magonjwa ya figo, Jacquline Shoo akitoa maelezo kwa madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga katika kikao cha kuhitimisha (Exit Meeting) la huduma za madaktari Bingwa hapa nchini.
   Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, akishuukuru Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili katika kikao cha kuhitimisha zoezi.
  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ushauri kutoka NHIF Dokta Frank Lekey, akizungumza na timu ya madaktari Bingwa na madaktari wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, kikao cha kuhitimisha zoezi hilo.
   

   
  Zoezi la huduma za madaktari bingwa liliodhaminiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili limehitimishwa mwishoni mwa wiki katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
   
  Katika zoezi hilo la siku tano jumla ya wagonjwa 740 wamepata huduma na wagonjwa 24 wamefanyiwa upasuaji.
   
  Akizungumza katika mkutano wa madaktari na timu ya uendeshaji ya hospitali hiyo kabla ya kuhitimisha zoezi hilo Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Ushauri kutoka NHIF Dokta Frank Lekey amewashukuru madaktari Bingwa kwa uzalendo wao na kuitolea kufanya kazi katika mazingira magumu.
   
  Aidha amewahimiza madaktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana katika kutoa huduma kwa wagonjwa na kuhakikisha kuwa dawa zote muhimu zinapatikana wakati wote.
   
  Naye Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dokta Mfaume Salamu, kwa niaba ya uongozi wa Hospitali hiyo ameushukuru Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwapeleka madaktari bingwa katika hospitali hiyo na kuwapa uzoefu madaktari wake. Amesema ujuzi waliopata katika kipindi hicho cha siku tano utawasidia kuendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa watakaokuja kupata huduma katika hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Shinyanga.
   
  Zoezi hilo sasa linahamia katika mkoa wa Simiyu kuanzia tarehe 06 hadi 10 Julai, mwaka huu.

  0 0

  Baadhi ya wateja wakiwa katika banda la wajasiriamali walionufaika na huduma za kibenki na  DCB katika meonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
   Afisa Mauzo wa Benki ya DCB,Tatu Shija( katikati) akiwa na wajasiriamali walionufaika na huduma za kibenki na  DCB wakinyesha bidhaa zao  katika meonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
   Afisa Mauzo wa Benki ya DCB, Rashid Ngwali (amenyosha mkono) akitoa maelezo kwa wananchi waliopita katika banda la DCB  katika meonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
   Wakala wa Benki ya DCB Jirani,Silima Nassoro akitoa maelezo kwa wateja waliopita katika banda la DCB  katika meonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja vya Mwalimu Nyerere. (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii)

  0 0

   Mshambuliaji wa Yanga, Kpah Sherman akichuana na beki wa KMKM ya Zanzibar, Musa Said katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga imeshinda 1-0. (Picha na Francis Dande)
   Mshambuliaji wa Yanga, Kpah Sherman akichuana na beki wa KMKM ya Zanzibar, Musa Said.
   Mshambuliaji wa Yanga, Geofrey Mwashiuya akjimtoka beki wa KMKM, Kassim Abdulkadir.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  MENEJA Mkuu wa kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini, Acacia, Asa Mwaipopo, (katikati), akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandihi wa habari makao makuu ya kampouni hiyo barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, leo Julai 8, 2015. Kampuni ya Acacia, inayomiliki migodi ya kuchimba dhahabu ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara, imetangaza udhamini wa miaka miwili itakayotoa kwa klabnu ya soka ya Stand United ya mkoani Shinyanga. Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu iko mkoani humo. Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United ya Shinyanga, Amani Vincent, na kushoto ni Meneja wa kampuni ya Acacia, anayeshughulikia mahusiano ya kijamii, Stephene Kisakye
  Mwenyekiti wa Klabu ya Stand United ya Shinyanga, Amani Vincent akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Julai 8, 2015 kuhusu kuingia mkataba wa udhamini wa klabu hiyo na kampuni ya uchimbaji madini, Acacia.Udhamini huo utakuwa wa miaka miwili, kwa mujibu wa Meneja Mkuu anayeshughulikia uendelezaji wa kampuni hiyo, Asa Mwaipopo.(katikati). Kushoto ni Meneja anayeshughulikia mahusiano ya kijamii wa kampuni ya Acacia, Stephen Kisakye.


  0 0
 • 07/08/15--11:56: IN LOVING MEMORY


 • The Late, Dr.Philbert O.Katalyeba
  ****** 
  Our darling dad, 
  Always so good,
  unselfish and kind,
  None on this earth your equal we will find,
  Honorable and true in all your ways,
  Loving and faithful to the end of your days,
  Honest and liberal,
  ever upright, 
  Just in your judgment, 
  always right.

  Loved by your relatives, 
  friends and all whom you knew One in a million, 
  that husband was you! (5years have passed, 
  our hearts still sore)  As time has passed, 
  our hearts still sore As time rolls on, 
  we miss you more 

  A loving HUSBAND and DAD,  tender and kind What beautiful memories you left behind Still alive after 5years The love for you in the heart of  your darling wife Astridah, children, grand children, relative and friends keeps burning May heavens grant your soul eternal rest.

  0 0

  MWANASIASA mkongwe nchini Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutofanya dhihaka ya kumpendekeza kada yoyote kuwa mgombea wake wa urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, kwani kwa kufanya hivyo kitaanguka.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo Jumatano Julai 8, 2015, Kingunge ambaye ameshawahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini na ndani ya chama hicho alisema “ninatishwa na watu wanaotumia nguvu nyingi kwelikweli kupambana wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama, badala ya kuelekeza nguvu hizo kupambana na wapinzani wetu, hii ni hatari.’, alionya

  Amesema, CCM ni lazima ifuate katiba yake ili wajumbe wanaotarajiwa kutoa maamuzi watoe maamuzi sahihi na sio kupindisha katiba kwa kuanzisha utaratibu ambao sio utamaduni wa kidemokrasia.

  “kuna kiongozi mmoja anasema, kada yeyote wa chama hicho aliyeomba kuteuliwa kuwania urais, endapo jina lake litakatwa hatakuwa na nafasi ya kukata rufaa, hii haijawahi kutokea na wala haipo kwenye katiba yetu.’ Amesema Mzee Kingunge.
  "CCM lazima imteue mtu anayekubalika ndani na nje ya chama ili chama kiweze kushinda, kinyume na hapo, hii ni njama ya kukifanya kishindwe kwenye uchaguzi".

  Hivi karibuni Katibu wa Halmashauri Kuu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, aliwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa hakutakuwa na nafasi ya kada wa chama hicho atakayeenguliwa kwenye mchujo kuweza kukata rufaa, kwani hakuna kanuni inayoelekeza kufanya hivyo.
  Hata hivyo Kingunge amepinga kauli hiyo na kusema, inakwenda kinyume cha katiba ya CCM ambayo inaweka bayana kuwa maamuzi ya vikao vya chini yanaweza kukataliwa na vikao vya juu ikiwa ni pamoja na mwanachama ambaye anaona hakutendewa haki kuwa na nafasi ya kupinga uamuzi wa vikao vya chini.

  0 0

  SHIRIKA la Global Peace Foundation limewataka Watanzania kudumisha amani iliyopo ili nchi yetu isije ikakumbwa na machafuko kama nchi za jirani.

  Akizungumza leo jijini  Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Global Peace Foundation na Mshauri wa Amani Afrika , Arnold Kashembe alisema Shirika hilo limeandaa mkutano wa kujadili mkakati wa kudumisha amani utakao jumuisha nchi za Afrika Mashariki (EAC).

  "Shirika la GPF limeandaa mkutano wa kujadili mkakati wa kudumisha amani utakao jumuisha nchi za Afrika Mashariki (EAC) ambao utafanyika Zanzibar kuanzia Julai 21- 24," alisema Kashembe.

  Kashembe alisema mkutano huo wa kipekee utawakutanisha maraisi wastaafu nane akiwemo Keneth Kaunda na Amani Karume, viongozi wa dini, wafanyabiashara na viongozi wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki na nchi jirani.

  Aidha Global Peace Leadership Conference (GPLC) 2015 itatoa mafunzo na nyenzo ili kuhimiza ushirikiano katika ukanda wa Afrika Mashariki na kujaribu kupunguza tofauti na matatizo yanayowakumba.

  Mada nyingine ni kuwapongeza vijana 400 kutoka Afrika Mashariki wanaotarajiwa kushiriki kuongeza nguvu katika mbinu za ujasiriamali na kuwa mfano wa wanafunzi wa wengine huko watokapo.

  Kujenga mikakati imara ya kudumisha ukaribu na kusaidiana mbinu za kupambana na umaskini, tatizo la ajira, HIV, Malaria na kuwezesha na kuzindua misheni Maendeleo ya Afrika kama lengo kuu na kiini cha mabadiliko kupitia Amani, Uongozi bora, na Uimara wa maendeleo kiuchumi.
   Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation (GPF), Arnold Kashembe (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kongamano kubwa la vijana  litakalofanyika Zanzibar kwa kipindi cha mwezi mzima kuanzia Julai 12 mwaka huu. Kongamano hilo litahudhuriwa na marais wastafu na viongozi maarufu. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa GPF nchini, Martha Nghambi na Mratibu wa kongamano hilo, Antu Mandosa
   Mwakilishi Mkazi wa GPF nchini, Martha Nghambi  (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Balozi wa Amani, Risasi Mwaulanga na  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation (GPF), Arnold Kashembe.
   Balozi wa Amani, Risasi Mwaulanga  akizungumza katika mkutano huo.
   Mratibu wa kongamano hilo, Antu Mandosa akizungumza kuhusu kongamano hilo.

  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum Futuma Mikidadi na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Utumishi ya Bunge, Kitolina Kippa kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Julai 8, 2015.
  Waziri Mkuu,Mizego Pinda akizungumza na Mbunge wa Songwe, Philipo Mulugo (wapili kulia) na wabunge wa Viti Maalum (kutoka kushoto) Vicky Kamata, Fatuma Mikidadi, Mariamu Kisanji na Dkt Mary Mwanjelwa kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Julai 8, 2015.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Hassan Hamad, OMKR

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo ameitembelea na kuifariji familia ya Bw. Saleh Juma Saleh yenye watoto sita wenye ulemavu.

  Akizungumza na familia hiyo nyumbani kwao Kinyasini Mkarafuuni Wilaya ya Wete Pemba, katika mfululizo wa ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, Maalim Seif ameitaka kuwa na subra na upendo kwa watoto hao wakielewa kuwa huo ni mtihani kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

  Amemuagiza Mkuu Mkuu wa Wilaya ya Wete kukutana na familia hiyo, ili kuandaa mipango itakayoweza kuwasaidia katika kuendesha maisha yao na shughuli zao za kila siku.

  Baba mzazi wa watoto hao Bw. Saleh Juma Saleh amesema watoto wake wanashindwa kusoma kutokana na kukosa nyenzo kwa vile wote sita hawawezi kutembea.

  Amesema watoto hao wakiwemo wanne wa kike na wawili wa kiume wanasikia vizuri, wanazungumza na wanafahamu wanachoambiwa, ingawaje baadhi ya wakati wanapoteza uelewa kutokana na hali ya ulemavu wao.

  Amefahamisha kuwa iwapo watapatiwa nyenzo wataweza kwenda skuli na kusoma kama wenzao wengine, na kuiomba serikali na wasamaria wema kuwapatia misaada inayostahiki, ili nao waweze kwenda skuli.
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa pamoja na familia ya Bw. Saleh Juma Saleh (mwenye mtoto), yenye watoto sita wenye ulemavu wa aina tofauti, huko nyumbani kwao Kinyasini Mkarafuuni Wilaya ya Wete.(Picha na OMKR)

  0 0

   Mtoa mada Awadh Ali Said, akitoa mada kuhusu muungano na umuhimu wa kuzingatia misingi ya amani katika mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ambao ulifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo.
   Mtoa mada Dk. Humphrey Polepole akitoa mada kuhusu kuzingatia misingi ya amani na umoja wa taifa letu kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akitoa majumuisho ya jumla juu ya dhima ya mdahalo huo, ambapo aliwataka watanzania kuendelea kupiga vita rushwa na kusisitiza kutowachagua watoa rushwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  TIMU BORA YA WATANZANIA WAISHIO UGHAIBUNI FC KILIMANJARO YA STOCKHOLM IMEFANIKIWA KUNYAKUA KOMBE LA NATIONAL CUP, LILILOMALIZIKA  JUMAPILI JULAI 5, 2015 BAADA YA KUSHINDA MECHI ZAKE ZOTE NANE KATIKA VIWANJA VYA KÄRRTOP IP JIJINI STOCKHOLM.
   Kikosi cha Kilimanjaro kikipasha kabla ya mechi kuanza.
   Wapinzani wa Fc Kilimanjaro ktk semi final.
  Makapteni wasaidizi wa Fc Kilimanjaro Jamil Jabeer na Ahmed Daddy wakiwa pamoja na mchezaji veteran Andrew  Dudley.
    Kapteni msaidizi Jamil Jabeer akipozi na kombe pamoja na mmoja wa walezi wa team Naaman Jasson.
  Kikosi cha Fc Kilimanjaro pamoja na baadhi ya washabiki wakifurahia ushindi.

  0 0

   ‎ ‎Deborah Charles kutoka Kinondoni Moscow akipokea kitita chake  Kutoka kwa mkuu wa vipindi Dickson Ponela wa EFM leo baada ya kushinda shindano hilo linaloendelea kila kona ya jiji la Dar es salaam
  Mshindi wa Sakasaka na 97.3 EFM ‎Deborah Charles  akafurahia  kitita chake

  0 0


  0 0
 • 07/08/15--13:45: ze komiki na nathan mpangala
 • 0 0

  Posted: 08 Jul 2015 11:54 AM PDT
  Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Alli Hassan Mwinyi, akikagua maonyesho ya kazi zinazofanywa na manispaa ya Kinondoni.
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni , Yusuph Mwenda akimkabidhi jezi ya timu ya soka ya Kinondoni Municipal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi kama ishara ya kuwa mlezi wa timu hiyo
  Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Alli Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti na na nishani ya utumishi uliotukuka Mstahiki Meya wa Manispaa ya kinondoni, Yusuph Mwenda wakati wa sherehe zabkufunga baraza la manispaa hiyo
  Rais Mstaafu wa awamu ya pili , Alhaji Ally Hassan Mwinyi, akimkabidhi cheti cha utumishi uliotukuka katika baraza la madiwani Mkurugunezi wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Mussa Natty, wakati wa hafla ya kuvunja baraza la madiwani la Manispaa ya Kinondoni

  Na Mwandishi wetu
  Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeliahirisha rasmi Baraza la Madiwani ambapo mgeni rasmi katika kuahirisha Baraza hilo alikuwa mheshimiwa Rais mstaafu wa Tanzania Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi.
  Shughuli hizo zilianza kwa kikao cha baraza cha kawaida cha kupokea taarifa ya utekelezaji ambapo baada ya hapo aliwasili mgeni rasmi Mheshimiwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na kufuatiwa na tukio la kupita katika mabanda maalum yaliyoandaliwa yakionyesha shughuli za kila idara na kupata maelezo ya shughuli zinazofanywa na idara hizo pasitisha moja na mafanikio mbalimbali katika idara hizo.Baada ya mgeni rasmi kupita katika mabanda hayo na kupata maelezo ndi[po kilianza kikao rasmi cha baraza cha kusitisha rasmi baraza hilo ambapo lilianza kwa ufunguzi wa sala na kisha utambulisho uliofanywa na Mstahiki Meya Yusuphu Mwenda kabla ya wawakilishi mbalimbali wa vyama vya siasa kutoa neno.

  Akiongea mkurugenzi wa jiji alilipongeza baraza la Madiwani na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondonikwa kazi nzito waliyoifanya ambayo Tanzania nzima wanaikubali ikiwepo ukusanyaji mzuri wa mapato na kumalizia kuwa Manispaa hii ni mfano mzuri wa kuigwa na Mstahiki Meya ni Meya wamfano kwa Tanzania nzima.Akiongea katika kikao hicho mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni alilishukuru Baraza la madiwani kwa ushirikiano wao katika kutekeleza shughuli za maendeleo kwa Manispaa hii ambapo ni mengi sana yaliyotekelezwa na mengine kutokana na muda bado hayakuweza kutekelezeka,lakini ameahidi kuyatimiza yale ambayo wameyabariki yafanyike likiwepo la kujengwa kwa mtambo wa kuchakata taka huko mabwepande ambapo tayari na mkataba umeshasainiwa wa kuanza kujengwa kwa mtambo huo kwa msaada wa Humburg city.
  Mgeni rasmi alitoa medani na vyeti kwa madiwani na kwa baadhi ya watendaji akiwepo Mkurugenzi.Katika kuitambulisha timu ya KMC-FC ambayo ni timu ya Manispaa ya Kinondoni mgeni rasmi alikabidhiwa jezi ya timu hiyo yenye jina lake Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ,hali kadhalika madiwani pia walipewa jezi hizo kila mmoja zenye majina ya kila mmoja na mkurugenzi aliwaomba kuitangaza timu hiyo na kuisaidia kwa hali na mali .
  Akiongea katika hafla hiyo Mstahiki Meya aliwashukuru wakazi wa kinondoni kwa ushirikano.kuhusiana na suala la maendeleo Meya alisema kumekuwa na ushiriki mpana wa wananchi katika maendeleo na pia uboreshwaji wa fedha za matumizi ya umma kwa kujenga mashule,barabara,mahospitali ambapo aliiongelea pia hospitali ya Mabwepande ambayo itakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi,akiongelea upande wa mapato alisema pato limeongezeka sana kutoka bil.11 kutoka kipindi cha nyuma hadi kufikia bil.35 hivi sasa.Akiongelea suala la vibali vya ujenzi kwa sasa vimekuwa vikitolewa na kupunguza msongamano na nia ni kuhakikisha vibali vya ujenzi vinapatikana ndani ya wiki moja,kuhusu usafi.

  0 0

  Waziri katika Ofisi ya Rais Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya ametaka wabunge wote wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhudhuria bungeni kesho ambapo Rais Jakaya Mrisho Kikwete atapoingia bungeni kulihutubia na kulivunja bunge. 
   Prof. Mwandosya amesema jambo la Rais kulihutubia bunge ni suala muhimu sana hivyo si vyema mbunge ama kundi fulani la wabunge kuwepo nje ya bunge wakati Rais atakapokuwa analihutubia bunge.  
  Kauli hiyo ya Prof. Mwandosya ameitoa leo Bungeni, ikiwa siku chache tu kupita tangu Mkuu wa kambi ya Upinzani bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katika ya Wananchi (KAWA) Mhe. Freeman Mbowe kusema wabunge wa umoja huo hawatarejea tena bungeni.

older | 1 | .... | 898 | 899 | (Page 900) | 901 | 902 | .... | 3285 | newer