Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 901 | 902 | (Page 903) | 904 | 905 | .... | 3285 | newer

  0 0


   Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao maalum cha kamati kuu ya CCM katika ukumbi wa White House mjini Dodoma leo jioni.
  Kikao hicho pamoja na Mambo mengine kitachagua wagombea watano ambao majina yao yatapelekwa katika Halmashauri kuu katika mchakato wa kumpata mgombea atakaye peperusha bendera ya CCM kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Zanzibar ambaye pia ni Rais wa SMZ Dkt.Ali Mohamed Shein,Kulia ni Makamu Mwenyekiti Bara Ndugu Philip Mangula na Watatu kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
  Rais Mstaafu awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa,wakiongea kabla ya kuanza kwa kikao

   Baadhi ya wajumbe wa kikao maalum cha Kamati kuu ya CCM kutoka kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, Makamu mwenyekiti Bara Mstaafu Ndugu Pius Msekwa, Rais Mstaafu Zanzibar Ndugu Amani Abeid Karume, Mawaziri Mkuu wastaafu Cleopa David Msuya na Salim Ahmed Salim. Picha na Freddy Maro
  0 0

  Waandishi wa Vyombo mbali mbali vya habari nchini Tanzania walioweka kambi kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma kwa ajili ya kutoa taarifa za vikao mbali mbali vinavyopendelea ili kumpata mgombea Urais wa Mwaka 2015 kupitia chama hicho.

  0 0


  0 0

  Na Pius Yalula-MAELEZO
  Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa 12 wa watumishi wa umma wa nchi za Afrika ambazo ni wanachama Jumuiya ya Madola utakaonza Jumatatu ijayo jijini Dar es salaam. 
   Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimimwa  Jakaya Mrisho Kikwete na kufungwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es salaam. 
   Amesema kuwa Mkutano huo unatarajia utakaonza tarehe 13 na kumalizika tarehe 15 unatarajiwa kujumuisha nchi 18 za Afrika ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Madola . Bwana Mkwizu amezitaja nchi hizo ni Botswana,Namibia,Cameroon,Ghana,Kenya,Lesotho,Malawi,Mauritius,Msumbiji,Namibia,Nigeria,Rwanda,Sychelles,Sierra Leone, Afrika Kusini,Swaziland,Tanzania,Uganda,Uganda na Zambia. 
  Ameongeza kuwa wakati wa mkutano huo washiriki watapata fursa ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoukabili utumishi wa umma wa nchi husika na kubadilishana uzoefu ili kuimarisha utendaji na ufanisi katika utumishi wa umma. 
   Aidha Kaimu Katibu Mkuu huyo amesema kuwa wageni hao watapata fursa ya kutembelea mji wa kihistoria wa Bagamoyo,ili kuwapa fursa ya kujifunza hazina kubwa ya kihistoria katika mji huo. 
   Hivyo ametoa wito kwa wananchi wote kuonyesha moyo wa ukarimu kwa wageni katika kipindi chote cha mkutano ili kuendeleza jina zuri la Tanzania.
  Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Umma Bwana Hab Mkwizu (katikati) akizungumza na wanahabari jana (leo) jijini Dar es salaam , juu ya Mkutano wa 12 wa Wakuu wa Utumishi wa Umma wa Nchi za Afrika wanachama wa Jumuiya ya Madola utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 13 hadi 15 mwezi huu. Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasilano Serikalini Florence Temba (kushoto) Mkurugenzi wa Idara ya Rasilimali watu wa Utumishi Bibi Roxana Kijazi. Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam

  0 0

  UNICEF Tanzania has been supporting colleagues to share their experiences in supporting the Burundi refugees through writing blogs. Please visit our blog site to read: http://blogs.unicef.org/2015/07/10/in-tanzania-protecting-refugees-from-cholera/

  0 0

  First Secretary from the Embassy of the People’s Republic of China, XU Jingchun (r) handing over a checque amounted to USD 10,000 to Newala district for the construction of a ward at Kitangari hospital in Newala district in Mtwara.

  0 0  0 0

  WABONGO HOUSTON TX WHITE PARTY NI NEXT SATURDAY JULY 18th  9:00PM @PURE LOUNGE (Downtown Houston). NUNUA TICKET YAKO SASA HAPA... http://allwhitehouston.eventbrite.com/?s=40265011 . VIP BOOTH FOR 8 PPL $400 ( 2 Bottles, Snacks & Entry). 
  Regular tickets are $20 cover if buy online & $25 at the door (Include Cover, snacks & 1st drink) TELL, SHARE & TAG A FRIEND. 18th JULY ". Hosted by Zey Misstanga ‪#‎MoFlavaAllWhiteUSATour‬ " KARIBUNI WOTE!!

  0 0

  Tarehe 1 hadi 7 Julai 2015 kulikuwako maonyesho ya kibiashara yaliyofanyika mji wa Ndola. Kama ilivyo ada kwa Watanzania, walishiriki maonesho hayo na kutia fora kwa bidhaa zao mbalimbali. Kikundi cha Wajasiriamali kinachojulikana HOT kutoka Dar es Salaam kilishiriki kama kinvyoonekana kwenye picha mbali mbali wakiwa wamepiga picha na Balozi wetu wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace J. Mujuma. Balozi alikwenda Ndola kuwaunga mkono.
  Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace J. Mujuma akiangalia bidhaa za Kitanzania kwenye maonesho hayo
  Balozi wetu wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace J. Mujuma akiwa na mmoja wa kinamama wajasiriamali
  Balozi wetu wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace J. Mujuma akifurahia bidhaa za vikapu kutoka nyumbani
  Balozi wetu wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace J. Mujuma akikagua mabazee na khanga
  Balozi wetu wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace J. Mujuma akiendelea kutembelea wajasiriamali hao
  Balozi wetu wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace J. Mujuma akipozi na mjasiriamali
  Balozi wetu wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace J. Mujuma akiwa na mjasiriamali wa bidhaa za kusindikwa.

  0 0


  0 0

  Waandishi wa Vyombo mbali mbali vya habari nchini Tanzania na nje walioweka kambi kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma kwa ajili ya kutoa taarifa za vikao mbali mbali vinavyopendelea ili kumpata mgombea Urais wa Mwaka 2015 kupitia chama hicho.
  UPDATES:  Kikao cha  Kamati Kuu ya CCM   kimemalizika hapa Dodoma na Nape Nnauye akiongea na wanahabari hivi punde amesema kikao kimaeenda vyema kabisa na kumalizika vizuri - ila majina hatoyataja sasa. Hadi kesho saa nne asubuhi.... 
  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete(wa pili kushoto) akiongoza kikao cha Kamati Kuu Maalum cha CCM mjini Dodoma, Kikao hicho kitachuja majina ya wagombea na kupata majina matano(5) .
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa taarifa fupi ya wajumbe waliohudhuria kikao cha Kamati Kuu Maalum ambapo wajumbe 28 walihudhuria kati ya 32.
  Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakipitia baadhi ya makabrasha wakati wa kikao cha Kamati Kuu Maalum (Picha na Adam Mzee)

  Vijana wa CCM wakipakia mikoba yenye makabrasha ya mkutano maalum wa CCM Taifa 2015 unaotarajiwa kuanza baadaye leo  katika ukumbi mpya wa Dodoma Convention Centre mjini Dodoma  uliozinduliwa juzi.

  0 0

  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari usiku huu nje ya ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma, mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichokaa kupitisha majina matano ya wagombea Urais yatakayopelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM kujadiliawa hapo saa nne asubuhi. Nape hakutaja majina ya wagomea hao waliopita kwenye tano bora, kwa kuseka atataja asuhuhi. 
  Muda mfupi baada ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari, walitoka wajumbe watatu wa Kamati Kuu ambao ni Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mh. Sophia Simba na Mh. Adam Kimbisa ambao walizungumza na waandishi wa habari juu ya walichokizungumza kwenye kikao hicho, ambapo wao walisema wamegomea makubaliano ya majina yaliyopitishwa kwenye kikao hicho kwa madai kwamba Kikao kikekiuka tararibu za uchujaji wa majina hayo. kwani yalijadiliwa majina machache tu na kupitishwa kwenda tano bora, lakini nao hawakuyataja majina hayo.

  0 0

   Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari asubuhi hii nje ya Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma, akithibitisha taarifa iliyokuwa ikizagaa mitandaoni ya Wagombea Urais walioingia katika hatua ya tano bora, ambao aliwataja kuwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mh. Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. January Makamba pamoja na Balozi Amina Salum Ali. Majina hayo yanapelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kujadiliwa na kupatikana matatu yatakayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu na kupatikana moja ambaye ndie atakuwa Mgombea Urais.
  Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa nje ya Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma leo.

  0 0

    Wananchi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa katika harakati za kutafuta mahitaji kuelekea sikukuu ya kuhitimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
   Mzigo ukishushwa tayari kwa kuuzwa.
  Msongamano wa magari  katikati ya kariakoo jijini Dar es Salaam.
  Hapa ni hatari zaidi kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam maeneo ya mtaa wa Congo.

  Msongamano wa magari Mtaa wa Sokoni Kariakoo jijini Dar es Salaam.
  Picha zote na Avila Kakingo na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii


  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  JAMII imetakiwa kutambua mahitaji ya watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea  katika kubaini  changamoto zao katika maisha wanayoishi na kuweza kuguswa kutoa msaada.
  Hayo ameyasema leo Mhasibu Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Idara za Serikali na Mabalozi,Wema Mbaga wakati akitoa msaada wa kituo Khilati Kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam,amesema kuwa wanatambua umhimu wa kutoa msaada kwa makundi maalumu wakiwemo watoto wanaolelewa katika vituo.
  Amesema kuwa watoto wanachangamoto nyingi katika ukuaji wao ikichangiwa na kuondokewa na wazazi wao hivyo wanahitaji faraja kutoka kwa jamii katika kuweza kufikia ndoto zao.
  Wema amesema watu wengine wanawajibu kuwakumbuka watoto katika katika kipindi hiki cha kuelekea Siku Kuu ya Idd El-Fitri kuwaza kupata mahitaji yao.
  Vitu walivyotoa ni Magodoro ,Daftari,Kalamu ,vyenye thamani y ash.milioni 1.5 ambapo ni sehemu ya mchango wao.
  Mkurugenzi wa Kituo hicho ,Khadija Hussein  amesema kutuo kinachangamoto ya eneo kwani eneo waliopo watoto wanalipia kodi pamoja na matatizo ya chakula.
  Amesema watu wenye uwezo watembelee kituo hicho na kuona mahitaji yao ili waweze kusaidia katika kulea watoto hao ambao wako 65.
  Mhasibu Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Idara za Serikali na Mabalozi,Wema Mmbaga akitoa akikabidhi msaada kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto Yatima cha  Khayrat  Kilichopo ,Kigogo,Khadija Hussein katika hafla iliyofanyika kituo hicho ,jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto Yatima cha  Khayrat,Khadija Hussein akizungumza na waandishi wa habari juu ya msaada walioupata katika hafla iliyofanyika kituo hicho ,jijini Dar es Salaam.
   Mhasibu Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Idara za Serikali na Mabalozi,Wema Mmbaga akizungumza na waandishi wa habari juu ya msaada walioutoa katika kituo cha kulele watoto yatima cha Khayrat, katika hafla iliyofanyika kituo hicho ,jijini Dar es Salaam.  
  Sehemu ya watoto katika kituo cha Khayrat wakiwa na daftari zilizotolewa na NSSF Mkoa wa Idara za Serikali na Mabalozi katika hafla iliyofanyika kituo hicho ,jijini Dar es Salaam. 
  (Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii)

  0 0

   Watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam wakiwa wamekaa katika kituo hicho mara baada ya Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA),kuwatembelea na kufuturu pamoja nao katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
  Wanachama wa  Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) wakichukua Futari kwaajili ya kuwagawia watoto wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam jana.
  Mfanyakazi wa Wanachama wa Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA),akiwawekea Futari kwaajili ya kufutari pamoja na watoto wa kituo cha watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo vingunguti jijini Dar es Salaam jana.
   Watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini wakifutari pamoja na wanachama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) walipo futuru pamoja na watoto hao katika kituo cha Mwana jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Kituo cha watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam, Mohamed Wage akiwashukuru wanachama wa Chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA),walipoamua kutembelea kituo cha mwana.
  Mwakilishi wa chama Cha Wanawake wanasheria Tanzania (TAWLA) akimkabidhi vitu mbalimbali Mkurugenzi wa Kituo cha watoto yatima wa kituo cha Mwana kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam, Mohamed Wage, Mara baada ya Kufutari pamoja na watoto hao.
  Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.


  0 0

   Kazi zikiendele katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo jijini Dar es Salaam ikiwa na matengenezo ya fremu mbalimbali.
  Nondo zikiwa katwa kwaajili ya kutengeneza fremu katika mtaa wa Congo ,Kariakoo jijini Dar es Salaam.
  (Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)

  0 0

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, unaoendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, Mjini Dodoma. 

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

   

  ENDELEA KUFATILIA GLOBU YA JAMII KWA UPDATES KUTOKA DODOMA.

  0 0

   Sehemu ya Wafuasi wa Mmoja wa Wagombea Urais ambao hawakuingiakatika hatua ya tano bora ya ya kuwania nafasi hiyo kupitia CCM, wakiimba kwa pamoja wimbo wa kuwa na imani na Mgombea wao, nje ya Makao Makuu ya Chama hicho, Mjini Dodoma mchana huu. Pamoja na kwamba Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa unaendelea kwenye Ukumbi wa White House, huku nje hali iko namna hii na ulinzi umekuwa ni mkali sana katika eneo lote la Makao Makuu ya CCM.
  Askari Polisi akimzuia Mbwa wake asimzuru mmoja wa vijana waliopo nje ya Makao Makuu ya CCM.
   Askari Polisi wakiendelea na doria nje ya eneo la Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma leo hii.


  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akimuongoza Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum na wadau wa mfuko huo kupakua futari iliyoandaliwa na PPF Kanda ya Temeke kwa wadau wake, Dar es Salaam
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza na wadau wa mfuko huo baada ya kupata futari iliyoandaliwa na PPF Kanda ya Temeke, Dar es Salaam juzi. Wengine kutoka kulia kwake) ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, Mwakilishi wa Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sadi Msati na Msaidizi wa Sheikh Ahad Musa, Athumani Mkambaku.

   Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akitoa shukrani zake baada ya futari hiyo
   Sheikh Alhadi, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Erio.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, alhad Mussa Salum zawadi iliyotolewa na mfuko huo Kanda ya Temeke kwake baada ya kupata futari iliyoandaliwa na PPF Kanda ya Temeke, Dar es Salaam

  Wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF na wafanyakazi wa Mfuko huo, wakipakua futari iliyoandaliwa na PPF Kanda ya Temeke kwao, Dar es Salaam 

older | 1 | .... | 901 | 902 | (Page 903) | 904 | 905 | .... | 3285 | newer