Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

KUMBUKUMBU

$
0
0

Marehemu AZIZ SHEWEEN

NI MWAKA MMOJA SASA TANGU ULIPOTUTOKA GHAFLA, NA KUTUACHIA HUZUNI KUU.

MWONGOZO NA MATENDO YAKO YATAENDELEA KUWA DIRA KWETU DAIMA.

UNAKUMBUKWA SANA NA MKEO NA WATOTO WAKO NA NDUGU NA JAMAA.
 
            Innalilah Wainnailayhi Rajuun

VODACOM GROWN AND SEXY PARTY YABAMBA VILIVYO NDANI YA UKUMBI WA MLIMANI CITY USIKU WA KUAMKIA LEO

$
0
0
 
Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano na Udhamini Kutoka kampuni ya Simu za Mikononi ya Vodacom,Kelvin Twisa akiwa katika Zuria jekundu Wakati wa Sherehe ya kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013 ijulikanayo kama Vodacom Grown and Sexy Party iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo
Baadhi ya Wahudhuriaji wa Party ya Vodacom Grown and Sexy Party Wakiwa kwenye Zuria jekundu la Vodacom Grown and Sexy Party iliyofanyika Usiku wa Mwaka Mpya Ndani ya Ukumbi wa Mlimani City 
 Wadau 
Warembo wakiwa ndani ya Ukumbi wa Mlimani city huku wakipata vinywaji baridi wakati walipohudhuria Sherehe ya Kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha Mwaka 2013 ijulikanayo Kama Vodacom Grown and Sexy Party iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo

Mh. Lowassa azindua VIKOBA kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasili kwenye kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli tayari kwa hafla fupi ya uzinduzi wa vikoba katika kijiji hicho.Katikati ni Mkewe Mama Regina Lowassa aliefatana nae kwenye hafla hiyo ya Uzinduzi wa Vikoba.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli walipowasili tayari kwa hafla fupi ya uzinduzi wa Vikoba katika kijiji hicho.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akitoa hotuba yake kwa wananchi wa kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli wakati wa hafla ya uzinduzi wa VIKOBA kijijini hapo.Mh. Lowassa katika hotuba yake,amesema kuwa ushirika wa VIKOBA ni sawa na mshipa wa damu kwa sera ya maisha bora kwa kila Mtanzania,pia alisema kuwa kutokana na kutambua hivyo ushirika wa Vikoba utaanzishwa katika wilaya nzima ya Monduli.Miasha bora kwa kila Mtanzania ni sera aliyoingia nayo madarakani Rais Jakaya Kikwete.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Monduli,Bi Judith (kulia) akikabidhi kwa Mhe. Edward Lowassa hati maalumu ya uzinduzi wa Vikoba ili ikabidhiwe kwa Wananchi Mswakini Monduli.
Baadhi ya wanachama wa Vikoba wa kijiji cha Mswakini Wilayani Monduli.

Rais kikwete na SALAMU ZA MWAKA MPYA 2013 & UZINDUZI WA AWALI WA MATOKEO YA SENSA

$
0
0
Rais Kikwete akihutubia salamu za Mwaka Mpya 2013

 SALAMU ZA MWAKA MPYA.


HOTUBA YA RAIS YA UZINDUZI WA MATOKEO YA SENSA 2012


TAARIFA YA MVUA KUBWA, UPEPO MKALI NA MAWIMBI MAKUBWA KWA MAENEO YA PWANI

DAR LIVE NA SHAMRA ZA MWAKA MPYA, UZINDUZI ALBAMU YA ‘DOMO LA UDAKU’

$
0
0

Umati ukirindima kwa burudani baada ya kutangaziwa kuwa mwaka mpya 2013 umeingia.
Kundi la Kings Modern Taarab likikonga nyoyo za mashabiki kabla ya kuwapisha T Moto.
Kundi la T Moto likizindua albam yake ya ‘Domo la Udaku’.
Mkurugenzi wa T Moto, Amini Salmini (kushoto) na muimbaji wa kundi hilo, Jokha Kassim (aliyevalia shela kama bi harusi) wakiingia jukwaani kimadaha.Jokha akikamua.
Wacheza kiduku nao wakimrusha roho ‘bi harusi’ kwa pembeni.
 ‘Bi. Harusi’ akiondolewa jukwaani baada ya kumaliza kufanya makamuzi.
Muimbaji mpya wa T Moto aliyetokea Kings Modern Taarab, Ustaadh Issa Ally, akikamua.
---
UMATI mkubwa wa wasaka burudani ulifurika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live huko Mbagala katika kusherehekea mwaka mpya ambapo pia kundi la taarabu la T Moto lilizindua albam ya ‘Domo la Udaku’
(PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY/ GPL)

RAIS KIKWETE AKARIBISHA MWAKA MPYA KIJIJINI KWAKE MSOGA

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakichangayika na wanakijiji wenzao wa kijijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani,kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za utamaduni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakichangayika na wanakijiji wenzao wa kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za utamaduni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kaka yake Mzee Selemani Kikwete kwa wanakijiji wenzake wa kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za utamaduni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa heri na wanakijiji wenzao wa kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, wakati wa kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za kienyeji.
Wanakiji wa Msoga wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani wakiangalia fashifashi wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya kijijini hapo. PICHA NA IKULU.

salamu za mwaka mpya toka serengeti freight forwarders

$
0
0
WAZEE WA KAZI wanawatakia wadau wote heri ya mwaka mpya kwa furaha na bashasha, ujumbe ukiwa MWAKA MPYA na MAMBO MAPYA. 
Pia watch this space!!!

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD
WAZEE WA KAZI
  TUNAWATAKIA WOTE HERI  MWAKA MPYA 2013

RATIBA YA MELI MPYA JANUARY 2013
 
FROM TILBURY 15/01/2013
FROM SHEERNESS 18/01/2013
BOOKINGS ZOTE SASA ZINAFANYIKA ONLINE
PLEASE VISIT OUR IMPROVED WEBSITE

VEHICLE INSPECTION FOR KENYA AND UGANDA NOW CAN BE DONE IN OUR OFFICES
JUST DROP YOUR  CAR IN OUR OFFICE AND WE WILL INSPECT IT AND DELIVER IT TO THE PORT FOR YOU
MITUMBA £65 KWA BALLE LA 45KGS AGIZA SASA 
kama unataka kuagiza kitu au kufanya booking yoyote ingia kwenye website yetu au tupigie kwenye namba zifuatazo;

CHRIS LUKOSI +44 07903828119  & 07404279633 
SIMON LOUIS (MOHSIN) +44 07950689243
HASSAN (RICHARD) +44 07405159255
HQ -  UNIT 92 THAMES INDUSTRIAL PARK, PRINCESS MARGARET ROAD, EAST TILBURY, RM18 8RHRH
Tell (+44) 01375 855917  Fax (+44) 01708202477



mbasha scotland tour 2013

$
0
0
Flora Mbasha and husband after  their tour Scotland, they will be ministering this Sunday 6th January, 2013 at Vision Gospel Ministry International, Hackney Wick, 68 Wallis Road, E9 5HL, London. The service starts at 11.00 till 15.00. You are all welcome to praise our Lord together and admission is free.

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA BONDIA DOTO KIPENGA

$
0
0
Waumini wa dini ya Kislam wakiomba dua mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Doto Kipenga (aliewahi kuwa Bondia Miaka ya nyuma) kabla ya mazishi yake.
Bondia wa timu ya Taifa Selemani Kidunda mbele akiwa amebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Doto Kipenga aliyekuwa bondia wakati wa uhai wake kwa ajili ya maziko yaliyofanyika katika makabuli ya Kigogo Mburahati leo.
Bondia wa ngumi za kulipwa Japhert Kaseba akiwaongoza wenzie kulibeba jeneza lenye mwili wa marehemu Doto Kipenga aliyekuwa bondia wakati wa uhai wake kwa ajili ya maziko yaliyofanyika katika makabuli ya Kigogo Mburahati leo.

MH. ADAD RAJAB AWAONGOZA WATANZANIA WAISHIO NCHINI ZIMBABWE KUSHEREHEKEA MWAKA MPYA 2013

$
0
0
BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZIMBABWE,MH. ADAD RAJAB (KULIA) AKIGONGANISHA GLASS ZA VINYWAJI NA WATANZANIA WAISHIO NCHINI ZIMBABWE KUASHIRIA SHEREHE YA MWAKA MPYA WA 2013 ZILIZOFANYIKA NCHINI HUMO JANA NA KUHUDHURIWA NA WATANZANIA PAMOJA NA MAOFISA MBALIMBALI WA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ZIMBABWE.
WATANZANIA MBALIMBALI WAKIWA KATIKA SHEREHE HIYO.
WADAU WA EDMARK-TANZANIA WALISHIRIKI SHEREHE ZA MWAKA MPYA NA KUWASILISHA MADA KUHUSU CHAKULA LISHE NCHINI ZIMBABWE.
WATANZANIA WAKIJUMUIKA PAMOJA KUSHEHEREKEA MWAKA 2013. ALIYEKETI KATIKATI NI BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZIMBABWE,MH. ADADI RAJABU, UPANDE WA KULIA KWAKE NI MWENYEKITI WA WATANZANIA WANAOISHI HAPO ZIMBABWE BW. APATAE FATACKY WAKISHIRIKIANA NA WATANZANIA WENGINE KUUKARIBISHA MWAKA MPYA.

MNUSO WA MKESHA WA MWAKA MPYA DMV WAFANA SANA

$
0
0

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Maajar akiongozana na mumewe Bwn Shariff Maajar (kati) wakisindikizwa na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Idd Sandaly (shoto) wakati walipokua wakiingia kwenye ukumbi wa Oxford uliopo Lanham, Maryland kwenye sherehe ya kuuaga mwaka 2012 na kuukaribisha 2013 iliyotayarishwa na Jumuiya DMVwakishirikiana na Ubalozi, pamoja na kuushukuru uongozi wa DMV, Mhe. Balozi aliwaaga rasmi wanajumuiya ya DMV kwamba muda wake umeisha na atarejea nyumbani kuendelea na kazi zake binafsi, Mhe. Balozi pia  aliwashukuru WanaDMV kwa ushirikiano waliompa yeye na mumewe ikiwemo familia yake kwa muda wote aliokaa hapa na kuomba waendelee na moyo huo kwa Balozi mpya atakaekuja kuchukua nafasi yake.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Maajar katika picha ya pamoja na mumewe Bwn. Shariff Maajar.
Mhe. Balozi akiongea jambo na Rais wa Jumuiya ya DMV, Bwn. Idd Sandaly.
Afisa Ubalozi Dr. Mkama katika picha ya pamoja na makamu wa Rais Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Raymond Abraham
Bwn. Shariff Maajar akiongea jambo na Dr. Hamza Mwamoyo (kulia) ambaye ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya udhamini Jumuiya DMV.
Meza kuu katika picha ya pamoja.
Rais wa jumuiya DMV Bwn. Idd Sandaly
Mhe. Balozi naMumwe katika picha ya pamoja na uongozi wa Jumuiya DMV wakati wa kukabidhi vyeti kwa wanajumuiya wanaojitolea katika kuchangia maendeleo ya Jumuiya katika sekta mbalimbali waliotukukiwa vyeti watu binafsi yakiwemo makampuni ni Asha Nyang'anyi, Didi Vava na Fadhili Londa, makampuni ni Metro Tires na Three Angeles Helth Care.

MDAU TAJI LIUNDI NDANI YA MKASI WA SALAMA PALE PALE AMAYA BEUTY

WANAFUNZI WA SHAHADA YA KWANZA YA SOSHOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) WAPOKEA MWAKA KWA UPANDAJI WA MITI MKOANI DODOMA

$
0
0
 Baadhi ya wanafunzi wa shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakisikiliza kwa makini wakati wakipewa elimu ya mazingira wakati walipoenda kupanda miti katika Shule zilizopo Mjini Dodoma
 Mmoja wa Wanafunzi wa shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Dorry Michael akipanda mti katika Shule ya Sekondari ya Itenga iliyopo Nkuhungu Mjini Dodoma
 Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakiwa wanapanda Miti katika Shule ya Sekondari ya Itenga iliyopo Nkuhungu,Wilaya ya Dodoma Mjini Mkoani Dodoma
 Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakipanda miti katika Shule ya Sekondari ya Itenga iliyopo Nkuhungu wilaya ya Dodoma Mjini Mkoani Dodoma
Baadhi ya wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakiwa katika Picha ya Pamoja na mratibu wa elimu wilaya ya Dodoma Mjini mara baada ya Kumaliza zoezi la upandaji wa Miti katika Shule ya Sekondari Itega iliyopo Nkuhungu, Wilaya ya Dodoma Mjini, Mkoani Dodoma.Picha Na Dorry Michael Wa Lukaza Blog UDOM

Filosofa Forum Imevutia Wengi

$
0
0
Discussion forum mpya – Filosofa Forum ni jukwaa jipya la malumbano ya hoja. Tangu kuanzishwa rasmi siku chache zilizopita kumekuwa na mlolongo wa wapenda hoja kujiunga na kuchangia hoja mbalimbali.

Malengo ya timu inayoendesha jukwaa hili ni kuhakikisha inampa kila mtu nafasi ya kutoa mawazo, kuuliza maswali, kuchangia hoja, n.k, bila kujali jinsia, maumbile, uwezo, cheo, kabila, itikadi au dini. Jukwaa hili limeundwa kwa kuzingatia maadili ya mtanzania. Maneno ya matusi yananaswa (detected automatically). Ni rahisi kujiunga au kuchangia hoja. Huhitaji ujuzi wa kompyuta wa hali ya juu sana kutumia. Karibu ujiunge uelimike na kuelimisha wengine. 
www.filosofaforum.com

Ngoma azipendazo ankal - Kizazi kipya

$
0
0
Introducing Karate: J.Kassam Ft Juma Jazz

ngoma azipendazo ankal - enzi hizo

$
0
0
Mwaka 1974 Carl Douglas alipiga bao na ngoma yake ya Kung fu Fighting

umbea wa nathan mpangala

Prof Mbele katika YouTube na Tangazo la Kitabu

$
0
0
Siku ya kwanza ya Mwaka Mpya, nimetua YouTube na kuweka tangazo la kitabu changu kimojawapo, Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. Binti yangu Zawadi ndiye aliyerekodi ujumbe wangu, akaiweka video YouTube. Nimejfunza kutoka kwake. 
MBELE

BREAKING NYUZZZZZ:........: MSANII SAJUKI HATUNAYE TENA

$
0
0
Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii asubuhi hii na kuthibitishwa kutoka katika vyanzo vyetu vya habari, inaeleza kuwa Msanii aliyekuwa akisumbuliwa kiafya kwa muda mrefu,afahamikae kwa jina la Sadick Juma Kilowoko Maarufu kwa Jina la Kisanii SAJUKI Amefariki Dunia mapema leo asubuhi.

Marehemu Sajuki,  ambaye hivi karibuni Serikali ilijitolea kubeba jukumu la kugharamia matibabu yake na hatimaye hivi karibuni kulazwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili,amefariki Dunia mapema leo majira ya saa moja. 

 Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi-Ameni. 

 Wadau tutazidi kutaarifiana kwa habari nyingine kuhusiana na msiba huu kwa kadiri zitakavyokuwa zikipatikana.
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images