Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

Bei za Mafuta zashuka tena

$
0
0
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei kikomo cha bidhaa za mafuta kinachoonyesha kuwa petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeshuka kuanzia leo. 

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu imesema bei hizo zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la Desemba 5, mwaka jana.

 “Katika toleo hili, bei za rejareja kwa petroli, dizeli na mafuta ya taa, zimepungua kwa viwango vifuatavyo: petroli Sh126 kwa lita sawa na asilimia 5.96; dizeli Sh32 kwa lita sawa na asilimia 1.60 na mafuta ya taa Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.50,” imeeleza taarifa hiyo. 

Kwa punguzo hilo, bei ya rejareja ya petroli katika jiji la Dar es Salaam itauzwa kwa Sh1,993, dizeli Sh1,967 na mafuta ya taa Sh1,973. 

Arusha petroli ni Sh2,077, dizeli Sh2,051 na mafuta ya taa Sh2,057. Katika jiji la Mbeya petroli itauzwa kwa Sh2,099, dizeli Sh2,074 na mafuta ya taa Sh2,079 na jijini Mwanza, petroli itauzwa kwa Sh2,142, dizeli Sh2,117 na mafuta ya taa Sh2,122. 

Taarifa imefafanua kuwa mbali na kupungua bei hiyo katika uuzaji wa rejareja, bei pia imepungua kwa katika uuzaji wa jumla ikilinganishwa na matoleo mawili yaliyopita. “Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimepungua kama ifuatavyo: petroli kwa Sh126.10 kwa lita sawa na asilimia 6.17; dizeli kwa Sh32.48 kwa lita sawa na asilimia 1.69 na mafuta ya taa kwa Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.6,” alisema. 

Mkurugenzi huyo amesema katika taarifa hiyo kuwa mabadiliko hayo ya bei, yametokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuimarika kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.

 Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli, zitaendelea kupangwa na soko. “Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. 

Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya uamuzi stahiki kuhusu ununuzi wa bidhaa za mafuta,” alisema Masebu.

 Hata hivyo, Masebu alisema pamoja na mpango huo wa Ewura kuweka bei ya kikomo, kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa hizo kwa bei ya ushindani, ilimradi ziwe chini ya bei hiyo kikomo. 

Alivitaka vituo vya mafuta kuchapisha bei hizo mpya katika mabango yanayoonekana bayana na kuonyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. 

“Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika,” alisema. 

Masebu aliwashauri wanunuzi kuchukua stakabadhi ya malipo inayoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita ili itumike baadaye kama kidhibiti endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko ya kikomo au yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

salamu za mwaka mpya toka kwa babu kaju

$
0
0

Heri ya mwaka mpya 2013 watanzania wenzangu ,tunauanza mwa huu mpya kwa msimamo mmoja  wa kukuza maendeleo ya michezo na sanaa nchini kwetu  Tanzania,
 
Watanzania tuna uwezo mwingi wa kufanya mambo makubwa katika medani za kimataifa, kama vile muziki ,michezo na mambo mbalimbali, ila hatuna ushirikiano ,vilevile pia kudharauliana kwingi, kitu anchofanya mzawa watu hukibeza na kikidharau badala ya kukisapoti. Hivi nani anajua kama kuna Mtanzania toka Zanzibar alikuja Marekani akiwa na umri wa miaka 15 anaitwa FRED MERCRYhttps://www.youtube.com/watch?v=xdCrZfTkG1c&feature=youtube_gdata_player,mwanamuziki ambaye nyimbo zake mpaka leo hii zinatumika katika michezo mikubwa kama vile Baskett ,football  hockey na mingeneyo hapa nchini Marekani katika utangulizi kabla ya mchezo kuanza
 
Sio huyo tu tuna watu mbali mbali toka nchini ambao wameonyesha vipaji nje ya nchi kama akina Filbert Bayi ,John Bura, Nyambui katika mbio Rashid Matumla ngumi, mpira Peter Tino ,Dilunga , MOGELLA   Pondamalli  na wengineo walitufikisha katika fainali za kombe la Afrika miaka ya 80 mwingine mwanzilishi wa Bongo flavaDandu muziki wake unapigwa nje mpaka leo.Sasa kwanini tuishie hapo wakati uwezo tunao, ila ni sababu hatuna ushirikiano.Hatuthamini vitu vya nyumbani tumeupa nafasi utamaduni wa kigeni badala wa nyumbani.
 
Mfano mzuri  mimi ni mwafrika wa kwanza ambaye nguo zangu zinavaliwa Dunia nzima  , lakini watanzania wenzangu badala ya kuniunga mkono ndio kwanza wanabeza na kudharau nguo,  gani hizo kisa Kajumulo katengeneza. Sasa sio wakati wa kuilaumu serikali  eti haitusaidii badala ya kujilaumu wenyewe kwa roho zetu za ubinafsi.
 
Tunasema serikali imetutelekeza vijana, huku tukitaka wazee wote wang'atuke kwenye uongozi je? ni kweli unafikiri tutafika kwa mtindo huu wa vijana kuinga tamaduni za kigeni si tutashia Tanzania kuwa Taifa la kigeni. hivi inakuwaje wasanii vijana wa nyumbani tunashindwa hata kuuzaata hata nakala 200 tu za CD nje ya nchi Wakati huo tunatumia pesa za kigeni kununulia vifaa hivyo vya muziki wakati vinatupotezea hela haviingizi  kutoka nje.
 
Ushauri wangu nikiwa kama mdau mkubwa wa michezo na sanaa nchini kwetu Tanzania, nchi yetu haiwezi kuendelea kimichezo na utamaduni bila ya kuwa na ushirikiano mkubwa baina yetu.Huwezi kumuona Mwingereza kavaa jezi ya Simba ama Yanga au kuona Mwamerika anasikiiza muziki wa Diamond lakini nyumbani kila kijana anatamani awe mwamerika .je vijana mna haki ya kulalamika  serikali umewatupa?
 
Siongei hivi kama mwanasiasa ila nina uchungu na maendeleo ya nchi yangu  .Nipo huku ugenini  kwa ajili ya maslahi ya nchi yangu,sijaiba wala kufanya biashara haramu, ninachotaka ni kuonyesha kwamba kumbe kuna watanzania ambao wanaweza kufanya biashara nje ya nchi na wakakubalika.
 
Hizo ni salamu zangu kwa mwaka huu 2013 tupige harambee ya michezo na sanaa ili mataifa mengine yatujue ,mpaka sasa nimeshauza zaidi ya milioni 20 nguo za kajumulo lakini ni watanzania wachache  wanaunga mkono  je Addidas, Nike , Puma na  Kappa wasingesaidia nchi zao kimichezo  wangefika wapi ?
 
HIVYO NAOMBA USHIRIKIANO... 
HERI YA MWAKA MPYA
ALEX KAJUMULO

THOMAS MASHALI KUFANYA PAMBANO WA KUFUNGUA MWAKA 2013

$
0
0

Bondi wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali anatarajiwa kupanda ulingoni Januari 12 katika ukumbi wa Friends Corner Manzese Jijini Dar es Salaam kutetea Ubingwa wa Afika  Mashariki.

Akiongea na waandishi wa habari Mratibu wa pambano hilo Aisha mbegu alisema mashali atapambana kuzipiga na Mkenya Bernard Mackoliech mpambano utakaokuwa wa raundi 10.

Alisema maandalizi yamekamilika ikiwa pia na kutumiwa tiketi kwa bondia huyo mkenya ambaye anatarajiwa kuwasili januari nane kwa ajili ya kupima uzito na kupanda ulingoni.

“tunataraji mpambano utakuwa mkali wa kukata na shoka ukizingatia mashali ameweka kambi kwa muda mrefu nje ya mkoa lakini pia Mackoliech ni bondia mahiri ambaye anasaka rekodi ya kwenda kucheza nje ya nchi”,alisema Aisha.

Alisema nafasi iko wazi kwa watu wanaotaka kudhamini ili kuhakikisha mpambano huo unafanikiwa ukizingatia ndio mpambano wa kwanza kwa mwaka 2013 na pia mashali anavutia mashabiki wengi.

Kwa upande wake rais wa TPBO amesema mapambano ya utangulizi yanatarajiwa kuwa manne na mabondi tayari wamesaini mikataba na watatangazwa hivi karibuni.

Bondia Thomas Mashali anatetea ubingwa huo wa Afrika mashariki na kati ambao aliupata baada ya kumpiga Mganda Medi Sebyala Jijini Dar es salaam mpambano uliohudhuriwa na mashabiki lukuki.

Customers applaud Stanbic win

$
0
0
Stanbic Bank Head of Finance, Lydia Kokugonza (left) receives the Best Presented Financial Statement award for the year 2011 from Pan African Federation of Accountants Chief Executive officer Vickson Ncube (right) at an awards ceremony organized by the National Board of Accountants and Auditors in Arusha recently. The Bank won the first prize in the Banking Sector category.


By our reporter 

Stanbic bank customers have applauded the bank’s recent win of the best presented financial statements award from the National Board of Accountants and Auditors (NBAA) in Arusha.

Speaking in Dar es Salaam Ms. Mary Kimiti said, “I have been banking with Stanbic for the past 7 years and have been seeing marked improvements to their services, I am sure this win is a reflection of overall efforts to serve the Tanzanian market better.”

A veteran banker who preferred anonymity explained what it means to have well presented financial statements. “To have a quality financial statement means that it is presented to be understandable, consistent, relevant and reliable. And this is exemplified in the format, terms used, reliability of making economic decisions from it as well as being free from error.”

Stanbic Bank took the lead for commercial bank entities followed by CRDB Bank and Standard Chartered Bank. In the financial institutions category, the Tanzania Investment Bank (TIB) took the lead followed by the Dar es Salaam Community Bank (DCB).

According to NBAA, the evaluation exercise was done in accordance with international financial reporting standards.

The Chief Executive Officer of the Pan African Federation of Accounts (PAFA), Vickson Nkube handed over the prize to the Stanbic Head of Finance Ms. Lydia Kokugonza in a colorful ceremony at the Kibo Palace hotel in Arusha.

A total of 53 entities submitted their financial reports for the NBAA awards.

The win in Tanzania comes in the wake of another award presented to the Standard Bank Group which trades as Stanbic bank in Tanzania. Late November the Standard Bank Group was awarded the prestigious Global Finance award for 2013 Best Foreign Exchange Provider in Africa. According to information on the bank’s website, the Standard Bank Group was also named the Best Foreign Exchange Provider in four African countries: South Africa, Nigeria,Botswana and Zambia.

SJ Kok, Standard Bank Group's Head of Global Markets Sales in Africa, says the awards recognizes Standard Bank's position as Africa's leader in the provision of foreign exchange services. He says Africa continues to be central to the Standard Bank Group's growth strategy.

Standard Bank Group is playing a leading role in local market development on the continent. Standard Bank has a strong Africa presence with a footprint in 18 African countries and an ability to provide foreign exchange pricing in 40 of the 54 Africa countries.

"Our on the ground presence combines effectively with strong economic research to deliver a high quality foreign exchange offering to our clients. In addition, our local currency risk appetite and trading capability enable Standard Bank to provide solutions that differentiate our offering from competitors on the continent."

"As a bank, we are passionate about building out our African franchise across client segments and geographies, so the growth that we are seeing in our customer business is encouraging" says Mr Kok.

With Africa's rich mineral endowment and growing middle class having captured the attention of investors globally, the increased investment from offshore and burgeoning economic activity on the ground makes the development of local markets inevitable. Standard Bank Group is exceptionally well positioned to continue leading the way in African market development.

ROMA MKATOLIKI AWAPAGAWISHA WAKAZI WA JIJI KATIKA TAMASHA LA VODACOM-COCO BEACH

$
0
0
Msanii mahiri wa Muziki wa kizazi kipya" Roma Mkatoliki"akiwapagawisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam,waliofika kwenye ufukwe wa bahari ya Hindi coco beach,katika Tamasha la kuukaribisha mwaka mpya liliandaliwa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya wateja wake kwa msimu huu wa sikukuu.
Msanii chipukizi (underground)wa muziki wa kizazi kipya"Z-Thinker "wa Mabibo jijini Dar es Salaam akitoa mistari yake kabla ya Msanii"Roma Mkatoliki" kupanda jukwani na kuwapagawisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam,waliofika kwenye ufukwe wa bahari ya Hindi coco beach,katika Tamasha la kuukaribisha mwaka mpya liliandaliwa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya wateja wake kwa msimu huu wa sikukuu.
Msanii chipukizi(underground)wa muziki wa kizazi kipya"More Dreamer"wa manzese jijini Dar es Salaam akitoa mistari yake kabla ya Msanii"Roma Mkatoliki" kupanda jukwani na kuwapagawisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam,waliofika kwenye ufukwe wa bahari ya Hindi coco beach,katika Tamasha la kuukaribisha mwaka mpya liliandaliwa na Vodacom Tanzania kwa ajili ya wateja wake kwa msimu huu wa sikukuu.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AZINDUA KITABU CHENYE HISTORIA YA KABILA LA WAPIMBWE

$
0
0
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akionyesha kitabu chenye historia ya kabila la Wapimbwe linalotoka Mkoa wa Katavi (kushoto kwa Waziri Mkuu) ni mmoja wa watunzi wa kitabu hicho,Bwana Peter Mgawe mhadhiri wa Chuo cha Ustawi wa Jamii.anaye fuatia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi,Bwana Mselemu Abdallah na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Dkt. Rajabu Rutengwe.sherehe hizo zilifanyika katika mkesha wa kukaribisha mwaka mpya mkoani Katavi.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akimtunuku Tuzo ya Heshima,bibi Teresia Zakaria kutokana na kushiriki shindano la maisha plasi 2012 alishika nafasi ya kwanza na kuweza kutangaza mkoa wa Katavi.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akimtunuku RPC wa Mkoa wa Katavi,ACP Dhahiri Kidavashari Tuzo ya heshima ya mkoa wa Katavi ya mwaka 2012 kutokana na uhamasishaji wa jamii kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu yaani Polisi Jamii.kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi,Dkt. Rajabu Rutengwe na kulia kwa Waziri Mkuu ni Mbunge wa Mpanda,Mh. Saidi Arifi.sherehe hiyo ilifanyika usiku wa mkesha wa kukaribisha mwaka mpya mkoani Katavi.Picha na Chris Mfinanga.

MAMBO YALIVYOKUWA SIKU YA MWAKA MPYA DAR LIVE

$
0
0
 
USIKU wa kuadhimisha kuanza kwa Mwaka Mpya wa 2013 ulishuhudia burudani ya kukata na shoka katika Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ulioko Mbagala, ambapo wasanii kadhaa wa muziki wa kizazi kipya walitoa burudani ya kufa mtu. Wasanii ambao waliwafanya mashabiki wasitulie katika viti vyao ni wakongwe Profesa J, Inspekta, Juma Nature, pamoja na wasanii wanaokuja juu katika fani hiyo ambao ni Linex na Stamina, huku bendi ya African Star ‘Twanga Pepeta’ wakiwapindisha migongo mashabiki.Pichani ni Juma Nature akiwapagawisha mashabiki.
Mkongwe Profesa J akiwapelekesha puta mashabiki.
Linex akiwapagawisha mashabiki.

salamu za rambirambi kufuatia kifo cha msanii Juma Kilowoko Maarufu kama SAJUKI

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amewatumia salamu za rambirambi, ndugu, jamaa na wasanii wote nchini kufuatia kifo cha msanii Juma Kilowoko (SAJUKI)kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Taarifa iliyotolewa leo, jijini Dar es salaam ,Wizara ya Habari, Vijana na Utamauni na Michezo imepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za kifo cha msanii huyo na kuongeza kuwa kifo hicho ni pigo katika tasnia ya filamu hapa nchini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Kifo chake ni pengo kubwa kwa Serikali, wadau wa tasnia ya filamu na michezo ya kuigiza nchini kwa ujumla.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha SAJUKI sina maneno ya kuelezea masikitiko na huzuni nilinayo , kwani kifo chake ni pigo katika tasnia ya filamu za michezo ya kuigiza” alisema Dkt Mukangara.

Dkt. Mukungara amewataka ndugu, jamii na wasanii wote kuwa wavumilivu na watumilivu wakati wote wa msiba na kumuombea marehemu makao mema kwa Mwenyezi Mungu.

Juma Kilowoko (SAJUKI)ni mzaliwa wa mkoa wa Ruvuma. Sajuki alianza kujihusisha na masuala ya maigizo alipojiunga na kikundi cha Kaole na baadaye filamu. Filamu alizocheza ni pamoja na Revenge ya Kampuni ya RJ .

Mwaka 2008 aliamua kuanza kutengeneza kazi zake mwenyewe ambapo filamu yake ya kwanza iitwayo Two Brothers kwa kushirikiana na Shija Deogratious ilitoka. Sajuki baadaye aliamua kuanzisha kampuni yake iitwayo WAJEY Production Company ambapo alitengeneza filamu nyingi zikiwemo Mboni Yangu, Round, Briefcase , Kijacho, Kozopata, Mchanga na Keni, 077( Zero Seven Seven).nk.

Sajuki alifanikiwa kucheza michezo ya kuigiza na filamu na wasanii wengi wenye majina hapa nchini. Sajuki amebobea katika Uigizaji, Utayarishaji na Uongozaji wa filamu.

Sajuki alianza kuugua mwaka 2010 na hali ilizidi kudhoofu mwaka 2011,ambapo alikwenda kutibiwa nchini India. Wadau wengi wa tasnia ya filamu walifanikiwa kutoa michango mbalimbali iliyomwezesha Sajuki kupata matibabu yake. Alirudi na kuonekana kapata nafuu kidogo jambo ambalo lilileta matumaini na furaha kwa watanzania; aliporejea tu aliweza kutoa filamu iitwayo Kivuli huku filamu nyingine ikiwa katika hatua ya utengenezaji.

Aidha hali yake ilibadilika jambo lililolazimu alazwe katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili hadi umauti ulipomkuta usiku wa kuamkia tarehe 02/01/2013.

Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amen.

Imetolewa na: 
Mkurugenzi 
Idara ya Habari(MAELEZO). 
Dar es Salaam. 
2 Januari 2013

maendeleo ya msiba wa Sajuki nyumbani kwao tabata bima leo

$
0
0
Baadhi ya Wasanii wa Filamu nchini wakiwa kwenye msiba wa Msanii mwenzano,Marehemu Sadick Juma Kilowoko ama Sajuki aliefariki Dunia mapema leo asubuhi,kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.taratibu za Mazishi ya Sajuki zinakwenda vizuri na Mwenyezi Mungu akijaalia Siku ya Ijumaa,Marehemu Sajuki  atasikwa kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar,Majira ya Saa tano asubuhi kwa mujibu wa mtoa taarifa.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi an Teknolojia Mh. January Makamba (mwenye fulana ya njano) akisikiliza maelezo ya juu ya maendelea ya Msiba wa Msanii Sadick Juma Kilowoko a.k.a Sajuki aliefariki dunia leo kwenye Hospital ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa.Taarifa hiyo ilikuwa ikitolewa na Rais wa Shirikisho la Wasanii wa Filamu Tanzania (TAFF),Saimon Mwakifwamba
Wasanii wa kila wa tasnia mbali mbali hapa nchini wakiwa msibani hapo.
Waombolezaji wenginwa wakiwa wamekaa kwenye mtaro
Mazungumzo ya hapa na pale.
Rais wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (TAFF),Saimon Mwakifwamba (kushoto) akizungumza na baadhi ya waombolezaji wengine msibani hapo.
Waombolezaji wa msiba wa Sajuki wakiwa Nyumbani kwa Marehemu.
Kisomo kikiendelea.

taka hizi zimeshindikana kuondolewa??

$
0
0
Leo katika pita pita za kamera man wa Globu ya Jamii maeneo mbali mbali ya jijini Dar,Leo alipita mitaa ya Tabata na kukutana na lundo la taka kando kando ya Barabara ya Mandela Road.hali hii imekaaje wadau??

Kisomo cha Kumuombea Marehemu SAJUKI nyumbani kwao Tabata jijini Dar leo

Rais Atuma Salam za Rambi Rambi kufuatia Kifo cha Sajuki

SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI WA MUUNGANO WA TANZANIA

ATCL resumes Kigoma flights

$
0
0

AIR Tanzania Company Limited (ACTL) Acting Chief Executive Officer, Captain Milton Lazaro, speaks to journalists (not in picture) about the airline’s plans to resume Dar es Salaam- Kigoma daily flights on Thursday, 10th January this year after the services were suspended awaiting renovation of the Kigoma Airport. ATCL will deploy its Bombardier Dash 8-300 plane with a capacity of carrying 50 passengers to fly the route. Photo by correspondent.

=======    ======  ========
ATCL resumes Kigoma flights

By Correspondent

AIR Tanzania Company Limited (ACTL) resumes Dar es Salaam- Kigoma daily flights on Thursday, 10th January this year after the services were suspended awaiting renovation of the Kigoma Airport.

Speaking to reporters in Dar es Salaam yesterday, the ATCL Acting Chief Executive Officer, Captain Milton Lazaro said the company will deploy its Bombardier Dash 8-300 plane with a capacity of carrying 50 passengers to fly the route after the company’s engineers certified to have completed major check-C repair it was undergoing.

“We are now set to resume our Dar es Salaam- Kigoma flights on Thursday 10th January this year and we are also working on implementing our aggressive expansion plans which will see us flying to other destinations which we have not covered at the moment,” he said. Captain Lazaro mentioned that ATCL will soon fly to Tabora and Mpanda once renovation of those airport facilities are completed, hence giving their customers in various destinations a better most preferred airline service.

“ATCL’s strategic plan to commence flights to Songwe Airport in Mbeya is in a better stage. We expect to start flying passengers to that destination on 20th of January this year as we were still waiting completion of renovation of the airport,” he said.

According to him, after the launch of Mbeya route, the company will go ahead to start flights to Arusha via Zanzibar by the end of this month, which will be accompanied by flights to Mtwara. “I want to assure our esteem customers that our services are still the best and we offer a very competitive fare to the destinations we fly.

The completion of this Check-C repair which has been carried out by our local engineers is a great step we have made in the aviation industry in Tanzania as we have proved that we can now offer such services to other airlines with no such capacity. We have already entered into agreement with some airlines who are seeking such services and we are ready to offer,” he said. He said the fact that the company’s engineers has successfully completed that kind of repair, ATCL will not only save money being used to send planes abroad for repairs, but also has helped the company to build its engineering capacity.

Captain Lazaro said ATCL has plans to add three more planes before the end of this year, mentioning that they will go for Bombardier Dash 8 which are much bigger and with modern advanced technology.   

Salaam za mwaka mpya za Rais Jakaya Kikwete kwa wananchi


Safari ya Mwisho ya Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) kutokea Nyumbani kwenda mazikoni

$
0
0
 Waombolezaji wa Msiba wa Msanii wa Filamu hapa nchini,Marehemu  Sadick Juma Kilowoko wakibeba jeneza lenye mwili wake tayari kwa taratibu za kwenda Mazikoni,wakitokea Nyumbani kwa Marehemu Tabata Bima.Sasa hivi mwili wa Marehemu upo katika Msikiti wa Sheahk Adhir,Kariakoo kwa ibada ya Kusalia Mwili na baada ya Swala ya Ijumaa,Mwili utazikwa kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mwili ukipakiwa kwenye gari.
Dua ikisomwa kabla ya kuondoka na Mwili wa Marehemu kwenda mazikoni.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba akimpokea Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe alipokuwa akiwasili msibani hapo.
Waombolezaji wakiwa Msibani mapema asubuhi hii.
Pamoja na kwamba kulikuwa na Mvua kubwa lakini hakuna alitaka kuondoka msibani hapo mpaka pale mwili ulipoondoka kuelekea Msikitini kwa Kusalia na baadae kwenye Mazishi.
Mwili ukiondoka nyumbani.

Rais Kikwete aongoza Mazishi wa Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) Makaburi ya Kisutu jijini Dar leo

$
0
0
 Jeneza lililobeba Mwili wa Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) likiwasili kwenye Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam mchana huu tayari kwa Mazishi yaliyoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) wakati wa Mazishi yake yaliyofanyika mchana huu kwenye Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam.

Picha zaidi pamoja na Video ya Mazishi haya,zitawajia baadae kidogo.

SHAMRA SHAMRA ZA MIAKA 49 YA MAPINDUZI ZANZIBAR

$
0
0
Wafanyakazi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar wakifanya usafi katika maeneo ya Ofisi yao Rahaleo mjini Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za kuazimisha miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar ambapo kilele cha sherehe hizo ni January 12. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

TAARIFA YA KUAHIRISHA SAFARI ZA TRENI ZA ABIRIA KWENDA BARA

$
0
0
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawataarifu abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa kutokana na kuharibika njia ya reli eneo la Stesheni ya Mikese jana usiku, safari ya treni ya abiria ya kutoka Dar es Salaam kwenda Bara iliyopangwa kuondoka leo Ijumaa Januari 04, 2013 saa 8:30 mchana haitakuwepo.

Taarifa ya siku ya kuondoka itatangazwa baadae kulingana na ushauri wa Jopo la Wataalamu wa TRL waliopelekwa kusimamia ukarabati wa eneo hilo .
Tafadhali atakayesoma taarifa hii amuarifu mwenzake.
Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

IMETOLEWA NA AFISI YA UHUSIANO KWA
NIABA YA MKURUGENZI MTENDAJI –TRL
MHANDISI KIPALLO AMAN KISAMFU
DAR ES SALAAM , JANUARI 04, 2013

STARS KUJIPIMA KWA ETHIOPIA JANUARI 11

$
0
0

Timu ya Taifa (Taifa Stars) itacheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya Ethiopia. Mechi hiyo itachezwa Januari 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Stars chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen inatarajia kuingia kambini jijini Dar es Salaam keshokutwa (Januari 6 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo. Mechi hiyo itakuwa kipimo cha mwisho kwa Ethiopia kabla ya kwenda Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazoanza Januari 19 mwaka huu.

Ethiopia iko kundi C pamoja na mabingwa watetezi Zambia, Nigeria na Burkina Faso. Ethiopia itacheza mechi yake ya kwanza Januari 21 mwaka huu dhidi ya Zambia.

Katika mechi yake ya mwisho, Taifa Stars iliifunga Zambia bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Desemba 22 mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Ethiopia ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo dhidi ya Morocco kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014. Mechi hiyo itachezwa Machi mwaka huu.

Wachezaji wanaotakiwa kambini ni Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).

Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Wakati benchi la Ufundi lina Kim, Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live


Latest Images