Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live

PROPERTY FOR SALE

0
0



A multistory brand new house registered in favor of Mr. Daniel Timothy Matiku, located along the road at Njiro 7 kilometers south of the City Centre of Arusha Tanzania is available for sale and has the following specifications:-

The ground floor has a total of seven (7) self contained rooms with suite toilet, bathroom unit, kitchenette and inbuilt wardrobes

The first floor has four (4) self contained rooms with kitchenette, cupboards and wardrobes, one (1) storeroom for any desired installations and Balcones in each room.

Basement floor with two rooms and one storeroom suitable for gym, storage and internet facilities.

A separate building block is available for managerial offices/facilities and parking bays.

Environmental consideration has been taken care of and there is a garden with trees for adequate shading and fresh air.

An 81meters deep borehole is available for reliable water supply. There is also an overhead water tank with 500 liters capacity provided for storage of water from mains for life support.

The house is fitted with bed, mattress and intercom system in each room.

The price tug of the property is USD 2 Million only, however it is negotiable on a give and take - win win basis. This property is flexibly suitable for a Hotel, Apartments, Rest House or Office block etc on owners’ discretion.

Attached are interior and exterior photos of the property. However Mr. Abel Norbert Jeketi Cell no. +255 752831393 who is the guard is available on site 24/7 for the conduct of any visitation. Therefore an inspection of the property can be arranged at any time of the day through the undersigned contact.

POTENTIALS OF THE PROPERTY

This property is located within the tourist circuit of Tanzania in the proximity of Ngorongoro Crater, Manyara, Tarangire and Kilimanjaro National Parks. A bypass road is envisaged to run from Arusha Airport near Kisongo suburb to Mererani which is a Tanzanite mining Centre in the vicinity of Mount Kilimanjaro and Kilimanjaro International Airport (KIA) which connects the City with the rest of the world.

Mr. DT Matiku, 
P.O Box 33984 
DAR ES SALAAM, 
Tanzania 
Cell +255754788238 
dmatiku@gmail.com

ANDROID WAJA NA APPLICATION YA KUPERUZI HABARI ZA TANZANIA

0
0

Apprux application inapenda kuwatangazia kupatikana kwa android application buree yenye uwezo wa kukusaidia kuperuzi kwenye vichwa vya habari vya baadhi ya blogs, website na magazeti ya Tanzania, pia inakupa uwezo wa kuona habari toka kwenye original source kwa urahisi zaidi
Application hii imetengenezwa kwa ajili ya watanzania na ni bure kabisa. 

Kwa wote wenye  phone yenye android 2.1 na kuendelea unaweza kutumia hii application kwenye simu yak bila shida.

Tunategemea itawasaidia, pia tunakaribisha maoni yenu kupitia email ya iannashin@gmail.com


Au kwenye simu yako ingia kwenye store halafu search peruzi

KIBONZO CHA KIJAST BIKOZZZ LEO

USIKU WA ZAWADI MWAKA MPYA NDANI YA DAR LIVE

VOTING FOR NEW SEVEN NATURAL WONDERS OF AFRICA ENDS ON DECEMBER 31, 2012

0
0
Tanzania Tourist Board (TTB) wishes to inform Tanzanians and the general public that the competition to vote for entries into the list of SEVEN NATURAL WONDERS OF AFRICA, conducted via the Website, http://sevennaturalwonders.org involving twelve (12) tourist attraction sites on the African continent will come to an end on December 31, 2012. Tanzania was the only blessed country with the most entries in the list: 

these are Mount Kilimanjaro, the Ngorongoro Crater, and the Serengeti National Park. Tanzania Tourist Board, would like to take this opportunity to sincerely thank all those who voted for Tanzania tourist attractions and requests all those who have not yet casted their votes to seize this opportunity and vote for the entry of all the Tanzania tourist attractions into the list of the NEW SEVEN NATURAL WONDERS OF AFRICA. 

 Issued by the Managing Director 
TANZANIA TOURIST BOARD

RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI WA KAMATI TENDAJI YA TASAF

KUMBUKUMBU YA MIAKA 3 TANGU KUFARIKI KWA SIMBA WA VITA (MZEE RASHID MFAUME KAWAWA)

0
0
Ni miaka mitatu sasa tangu mzee wetu mpendwa Rashid Mfaume Kawawa (Simba wa Vita) ulipotutoka. Bado tuna majonzi kila tunapokumbuka hasa kwa mambo mema uliyotufundisha. Mungu ailaze mahala pema  peponi roho yako amin.

 Innalilah wainnailayhi rajuun.

Jicho la Kitime na Muziki wa Tanzania


MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA AKABIDHI ZAWADI ZA MWAKA MPYA KWA KITUO CHA TUSHIKAMANE CHILDREN CARE TRUST FUND

0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akikabidhi Mbuzi kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Tushikamane Children Care Trust Fund Bw. Gratho Messy Mbele (wa kwanza kulia) na Mkuu wa Shule ya Tushikamane Bi. Euphrosine Mtundu, kama zawadi kwa watoto yatima wa kituo hicho ambapo panapo majaliwa hapo kesho atajumuika nao kupata chakula cha mchana. Anayeshuhudia tukio hilo ni Diwani wa Kata ya Tabata Hajati Mtumwa Mohamedi (wa pili kushoto)
Mstahiki Meya Jerry Silaa akikabidhi ndoo ya mafuta kwa kituo hicho chenye lengo la kuhudumia watoto yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi kwa kuwapa mahitaji muhimu kama vile elimu, afya, chakula, malazi, mahitaji ya shule, pamoja na huduma za kisaikolojia na ulinzi dhidi ya manyanyaso.
Viongozi wa kituo hicho wakimshukuru Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Meya wa Manispaa Mstahiki Jerry Silaa akibadilishana mawazo na baadhi ya viongozi wa kituo hicho mara baada ya kukabidhi zawadi za vyakula ikiwa ni mchango wake kwa vijana hao katika kusherehekea mwaka mpya 2012/2013.

Kila mwaka wakati wa sherehe za mwaka mpya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala yeye binafsi hutoa sadaka kwa wahitaji kwa kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha kumaliza mwaka salama.

Leo Mstahiki Meya Jerry Silaa ametoa chakula kwa kituo cha Watoto Yatima na watoto Yatima na watoto Waishio Katika Mazingira Hatarishi cha Tushikamane Children’s Care Trust Fund ambapo pamanapo majaliwa hapo kesho atakula chakula pamoja nao.

Asasi hiyo ya Tushikamane Children’s Care Trust Fund ilianzishwa mwaka 2001 na kupata usajili wa kudumu mwaka huo huo ili iweze kujiendesha kwa mujibu wa sheria za nchi.

AJALI MBAYA JIJIBI DAR LEO

0
0
Kaka Michuzi ajali hii mbaya imetokea lao Tarehe 31/12/2012 mida ya saa 10:20 jioni maeneo ya TOANGOMA.
.
Ajali ilihusisha gari aina ya Toyota Surf pamoja na Min-Canter ambapo zote zilikuwa zinatokea barabara inayounganisha Kongowe na Kigamboni..
.
Mwenye Toyota Surf ni mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi na inasemekana alikuwa amesimama akiwa amewasha indiketa ya kuingia kulia kuelekea nyumbani kwako ambapo nyuma yake tayari kulikuwa na magari matatu yakiwa yamesimama yakimruhusu na kumsubiri aingie kwake..
.
Baada ya kuona ameruhusiwa kwenye "Site Morror" ndipo alichukua uamuzi wa kuingia mara ndipo ilitokea Kenta hiyo iliyokuwa imebeba Kokoto ikiwa kwenye kasi ya ajabu na kuibamiza Toyota Surf hiyo kwenye mlango wa nyuma na hatimaye kuiburuza hadi kwenye mtaro kama inavyoonekana..
.
Mwanajeshi huyo aliyejulikana kwa jina moja tu ka Bw. KAMUNDE alikuwa na mkewe ndani ya Surf hiyo lakini kwa maajabu ya Mungu woote ji wazima wa afya na walikuwepo salama salmini kwenye eneo la tukio wakiwaeleza wananchi na askari polisi wa usalama barabarani namna ajali ilivyotokea..
.
Hata hivyo dereve wa Kenta hiyo aliingia mitini baada ya tukio hilo. Kunusurika kwa wote katika tukio hili ni mapenzi ya Mungu tu maana hali ya magari yote haitamaniki. .
.
Jamani tunawaimba Madereve wote na kuwasihi kuwa waangalifu hasa kipindi hichi cha mwisho wa mwaka. Jeshi la polisi ni vyema likajipanga vya kutosha kukabiliana na udereva zembe ambao unaweza kugharimu maisha ya watu pasi na sababu kama ilivyotaka kutokea katika tukio hili..
.
Habari na mdau Herman Edgar Berege, TOANGOMA.



RAIS KIKWETE APONGEZWA KWA MAFANIKIO YA SENSA YA WATU NA MAKAZI

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba leo Desemba 31, 2012 wakati wa kupiga picha baada ya kuzindua matokeo ya sensa ya watun na makazi katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

Salamu Za Mwaka Mpya Kutoka Mjengwablog

0
0

Ndugu zangu,

Imekuwa ni utamaduni wangu kutuma salamu za Mwaka Mpya kwa wanakijiji wa Mjengwablog, marafiki zangu kwenye FB na wengine walio ndani na nje ya mitandao ya kijamii.

Nimefanya hivyo tangu mwaka 2006 ilipoanzishwa Mjengwablog. Na mwaka huu naendeleza utamaduni huo. Nina mambo makubwa mawili kwenye salamu za mwaka huu, lakini, nitaanza salamu hizi kwa kukumbushua ahadi muhimu ya Mwana –TANU; kwamba;

” Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa manufaa ya wote”.

Ndugu zangu,

Siku kama ya leo miaka 30 iliyopita nilikuwa ndani ya garimoshi la Tazara nikielekea Dar kutokea kijijini kwetu Nyeregete.

Nikiwa Nyeregete kwenye likizo ndefu ya kusubiri matokeo ya Kidato cha Nne, zilinifikia taarifa kuwa nahitajika haraka Dar es salaam kwenda kufanya maandalizi ya kuanza Kidato cha Kwanza shule ya Sekondari Tambaza. Masomo yetu pale Tambaza yalianza Januari 13, 1983.

Siku kama ya leo miaka 30 iliyopita nilivuka kwa kuogelea korongo la Lihamile ili kuifikia Rujewa na hatimaye stesheni ya Tazara kule Ihanga. Korongo hilo lilijaa maji ya mvua ya masika yaliyokuwa yakipita kwa kasi.

Hakukuwa na daraja. Baadae likajengwa daraja la magogo wakati wa kipindi cha Ubunge wa Kanali Mstaafu, Edmund Mjengwa. Daraja hilo sasa limeoza. Halipitiki. Ahadi nyingi zimetolewa kulijenga upya. Zimebaki kuwa ahadi. Ni daraja muhimu kiuchumi na kijamii kwa watu wa Nyeregete na wengine wengi wenye kulitumia. Ni kero kubwa kwa wananchi wa Nyeregete.

Nimeongea na baadhi ya viongozi wa Nyeregete. Na nimewaambia, kuwa tushirikiane kuhakikisha, kuwa mwaka 2013 daraja hizo linajengwa hata kama ni kwa nguvu za wananchi. Tayari tumeshafanya utafiti na kuona inawezekana likajengwa kwa kiwango cha zege na chini ya shilingi milioni 20.

Hivyo basi, mwaka 2013 nitashirikiana na wananchi wa Nyeregete na wengine wote watakaokuwa tayari kusaidia kuhakikisha tunapitisha harambee ya kujenga daraja hilo. Miaka 30 baada ya mimi kuvuka Lihamile kwa kuogelea itakuwa ni aibu kubwa kuwaona tena wananchi wa Nyeregete na wengine wakivuka korongo hilo kwa kuogelea. Ni nini basi maana ya kwenda shule?

Ndugu zangu,

Maji ni kero kubwa kwa wananchi wengi wa Bonde la Usangu, Mbarali Mbeya.

Badala tu ya kuilalamikia na kuisubiri Serikali iwasaidie wananchi kutatua kero ya maji, mwaka 2013 nimeazimia nitashirikiana na wanakijiji wa vijiji vya Magwalisi na Lihamile wilayani Mbarali ili tuweze kuchangisha fedha za kuchimba visima vya pampu kimoja katika kila kijiji husika.

Nitashiriki kuchangisha sehemu ya fedha zinazohitajika kugharamia visima hivyo kwa kupanda Mlima Kilimanjaro, kitu ambacho nimependa nikifanye katika maisha yangu lakini sijapata bahati ya kufanya.

Ndugu zangu,

Hayo ni mawili makubwa niliyotaka kuyasema kupitia salamu za mwaka mpya wa 2013.

Ni matumaini yangu, Desemba 31, 2013 Mungu atanijalia uhai na kurudi tena hapa kutoa tena salamu za mwaka mpya huku hayo mawili yakiwa tayari yameshafanyiwa kazi kwa nguvu za pamoja, ikiwamo ushirikiano wenu. Nawatakia Heri na Fanaka Za Mwaka Mpya wa 2013.

Maggid Mjengwa,

Morogoro

0788 111 765

http://mjengwablog.com 

WACHEZAJI 22 WAITWA KAMBINI TAIFA STARS

0
0
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 22 watakaoingia kambini Januari 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco itakayochezwa Machi mwaka huu.

Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma saa 11.30 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza Januari 7 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).

Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

LIBENEKE LA KANDANDA NA Shukrani zake kwa GLOBU YA JAMII

0
0

Timu nzima ya Kandanda.co.tz inapenda kutoa Shukrani za Dhati kwa Michuzi Media Group, kwa kuwa blogu zenu zinaongoza kwa kutuletea watembeleaji katika tovuti yetu ya www.kandanda.co.tz kwa upande wa Tanzania.

Shukrani

BONANZA LA NNE LA VIKUNDI VYA MAZOEZI LAFANYIKA ZANZIBAR

0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk watatu kutoka kulia akiongoza Vikundi mbalimbali vya Mazoezi katika Bonanza la Nne kuelekea Uwanja wa Aman Mjini Zanzibar kulia yake ni Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui.
Vikundi mbalimbali vya Mazoezi vilivyo shiriki katika Bonanza la Nne la Vikundi vya Mazoezi vikielekea Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
Vikundi vya Mazoezivilivyo shiriki katika Bonanza la Nne la Vikundi vya Mazoezi vikiingia ndani ya Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na MichezoSaid Ali Mbarouk akipokea Vikundi mbalimbali vilivyo shiriki katika Bonanza la Nne la Vikundi vya Mazoezi Zanzibar.
Vikundi mbalimbali vya Mazoezi vilivyo shiriki katika Bonanza la Nne la Vikundi vya Mazoezi vikifanya Mazoezi ya Viungo ndani ya Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na MichezoSaid Ali Mbarouk akitoa Hotuba ya kuwapongeza Wanavikundi na kuwapa hongera ya Mwaka mpya baada ya kushiriki katika Bonanza la Nne la Vikundi vya Mazoezi Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na MichezoSaid Ali Mbarouk akitoa Zawadi kwa Vikundi mbalimbali vilivyo shiriki katika Bonanza la Nne la Vikundi vya Mazoezi Hapo Uwanja wa Amani Zanzibar. PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

Article 13

Karate: J.Kassam Ft Juma Jazz

Rais Kikwete alipozindua Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi jijini Dar

0
0

 Bango linaloonyesha Idadi ya watu wote Watanzania, baada ya kuhesabiwa katika zoezi la kuhesabu Sensa lililoanza mwezi Agosti mwaka huu na kufikia tamati hii leo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, alipotangaza rasmi matokeo ya Senza ya watu na makazi na kutaja idadi kamili, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na wananchi wakati akisoma hotuba yake ya kutangaza rasmi uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi, leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Rais Jakaya, alisema kuwa katika Sensa ya mwaka huu, watanzania wameongezeka kwa asilimia kubwa ukilinganisha na Sensa iliyofanyika kwa mara ya kwanza nchini ya mwaka 1967, ambapo Watanzania wote walikuwa ni Milioni 12, 313, 054, na Tanzania Bara walikuwa ni milioni 11, 958,654 na Visiwani Zanzibar, walikuwa ni 354, 400, ambapo baada ya mwaka huo, Sensa kama hiyo ilifanyika tena mwaka 1978, 1988,2002 na hii ya mwaka huu 2012, ambapo imetoa idadi ya Watanzania wote kuwa ni jumla ya Milioni 44, 929,002. 
 Baadhi ya Madiwani na viongozi mbalimbali wa Serikali, waliohudhuria katika hafla hiyo leo.
 Kikundi cha Uhamasishaji cha Temeke, akikiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kilichokuwa kikiendelea na kazi yake ya uhamasishaji uwanjani hapo.
 Sehemu ya wananchi waliojitokeza kuhudhuria hafla hiyo.
 Bendi ya THT, kutoka (kulia) ni Marlow, Amin na Linah, wakitoa burudani jukwaani wakati wa hafla hiyo.
 Wananchi wakisebeneka kushangilia baada ya Rais Jakaya Kikwete, kutangaza rasmi matokeo hayo ya Sensa.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
 Picha ya pamoja kwa kumbukumbu.
Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba, wakati akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja, baada ya kuzidua rasmi matokeo ya Sensa ya watu na makazi.

Kocha Mpya wa Simba awasili jijini Dar tayari kwa kuinoa timu hiyo

0
0

  Katibu wa Simba, Evodius Mtawala akimwongoza kocha mpya wa klabu hiyo, mfaransa Patrick Liewing mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam akitokea Ufaransa 

Twanga Pepeta walivyoukaribisha Mwaka Mpya wa 2013

0
0

 Luiza Mbutu (kushoto) na mtangazaji wa TBC (katikati) na shabiki wa Twanga, kwa pamoja wakifungua shampeni kuashiria kuukaribisha mwaka mpya wa 2013, na kuuaga mwaka 2012 wakati wa onyesho maalum la bendi hiyo katika ukumbi wa Mango Garden kinondoni,jijini Dar usiku wa kuamkia mwaka huu.

 Mashabiki wa bendi ya Twanga, wakisebeneka, katika onyesho la bendi yao kwenye Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni wakati wa Sherehe ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013.
 Kalala  Junior, akiwachezesha mashabiki wake kwa kusugua kisigino jukwaani.
 Kalala Junior, akiwachezesha wanenguaji wake, na sebene la Twanga......
 Wanamuziki wa bendi ya Twanga, wakipozi kwa picha ya kumbukumbu baada ya kushangilia kuukaribisha mwaka mpya na kufungua shampeni.
Viewing all 109602 articles
Browse latest View live




Latest Images