Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live

MATUKIO YA BUNGE LEO KUPITIA SIMU TV

$
0
0
TBC.
Baada ya malumbano Bungeni Leo yaliyopelekea kuahirishwa kwa Bunge, haya ni baadhi ya matukio yaliyotekea Bungeni.
SIMUtv: Hivi ndivyo timbwili lilivyozuka bungeni leo hadi kupelekea kuahirishwa kwa kikao cha bunge.Tazama hapa.    http://youtu.be/zFRWtB0lbKo
SIMUtv:  Naibu Waziri Tamisemi Mhe Majaliwa akijibu swali Bungeni Juu ya maegesho  ya magari katika miji mbalimbali nchini.   http://youtu.be/CTJ9oznbgEE
SIMUtv:  Mbunge aibana serikali juu ya upotevu wa fedha za umma kama inavyoainisha na ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali. http://youtu.be/4856G_lVqRc
SIMUtv:  Changamoto za ukusanyaji wa mapato ya maegesho ya magari katika jiji la Dar Es Salaam waibua maswali Bungeni.      http://youtu.be/a4AGzh0geJw
SIMUtv:  Kibano alichokitoa Mhe  Mnyika dhidi ya serikali juu  ya ubadhilifu unajitokeza katika manispaa za Jiji la Dar Es Salaam.       http://youtu.be/f3Kwx9Tlsbg
SIMUtv:  Serikali kukomesha tabia ya ulipaji wa mishahara kwa  watumishi  hewa serikalini kwa kuimarisha mawasiliano katika ngazi zote za serikali.    http://youtu.be/4QcL9RIqA44
SIMUtv:  Misingi Imara ya utawala bora inakipasa Chama kiwe na Uwazi kwa jamii, Ungana na Zitto Kabwe akizungumzia misingi ya Utawala Bora.     http://youtu.be/1de_hY9xMmY
SIMUtv:  Mjadala wa vitambulisho vya taifa wafufuliwa upya Bungeni na haya ndio majibu yaliotolewa na naibu waziri wa mambo ya ndani  Mh Pereira Silima.  https://youtu.be/X_4tip1nik0
SIMUtv:  Naibu waziri wa Mawasiliano,Sayansi na  Teknolojia Mh January  Makamba akijibu swali juu ya makampuni ya simu yaliowekeza katika halmashauri ya vunjo   http://youtu.be/rMsnWXzBljw
SIMUtv:  Serikali yawaasa wananchi kusimamia na kuhakikisha wanapata mapato zaidi kutokana na uwekezaji wa minara ya simu katika ardhi yao.    http://youtu.be/bOGkvRDl8H4
SIMUtv:  Hivi ndivyo kambi rasmi ya upinzani  Bungeni walivyowasha moto bungeni na kusababisha spika kuhairisha Bunge.    http://youtu.be/QRUni90WHh8
SIMUtv:  Hivi ndivyo timbwili lilivyozuka bungeni leo hadi kupelekea kuahirishwa kwa kikao cha bunge.Tazama hapa.    http://youtu.be/zFRWtB0lbKo
Madai ya Mbunge wa Ubungo Mhe. Mnyika juu ya ukiukwaji wa kanuni za bunge yaleta mzozo Mkali na kupelekea bunge kuahirishwa.    https://youtu.be/HO6GH8fs4K4

APPRECIATION

$
0
0
The family of the late Judge(Rtd) Anthony Bahati of Oysterbay - Dar es-salaam would like to express our heartfelt thanks to relatives, friends, neighbours, and well wishers who joined us throughout the difficult period of nursing and later bereavement of our beloved father who passed away on the 28th May,2015 at Muhimbili National Hospital (MNH) and was peaceful laid at Kinondoni grave yard on the 2nd June,2015.

The family sincerely valued your spiritual, moral and material support extended to us during our difficult moments. It is our sincere wish to mention all who participated in all errands in one way or another but the list is too long, for those who are not mentioned here, we humbly valued your participation and contribution hence kindly accept our appreciation. Specifically, the family would like to mention the following;

The State House, the First Lady Mama Salma Kikwete,Hon. Mizengo Pinda, the Prime Minister, the Principal Judge, Judges and staff of the High the Court, retired judges, Chairman of the Law Reform Commission, Regional Commissioner of Dar-es salaam, Coast,Morogoro and Arusha, Regional Administrative Secretaries of Dar-es salaam and Coast Region, Chief Court Administrator, doctors and nurses at Muhimbili National Hospital, Tanganyika Law Society, Regional Commissioner-Dar-es salaam, Saint Peter’s Church Parish priest, Don Bosco choir-from Tabata Kimanga, UDSM class of 1968 Faculty of Law,Jumuiya ya Moyo Mt. wa Yesu-Oysterbay, National Social Security Fund(NSSF),ADEM,SWISSPORT,LRCT and Judge (rtd) Stephen Ihema.

We also extend our appreciations to all MZIWA members.
There will be a requiem mass on Saturday 4th July, 2015 at 11:00 am at St. Peters Church-Oysterbay.

Thereafter we cordially invite you to join us for lunch at Oysterbay- Mzinga way No. 14 from 12.45pm.

“ A tree is known by its fruit; a man by his deeds.’’
‘ 'A good deed is never lost; he who sows courtesy reaps friendship and who plants kindness gathers love’’. Saint Basil.

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YANG’ARA KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA YA SABASABA

$
0
0
Mmoja wa wakina mama kutoka Kikundi cha Wachimbaji Madini Wanawake Tanzania, (Tanzania Women Mining Association) Shamsha Diwani (katikati) akitoa maoni yake mara baada ya kutembelea banda la Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Vito na Almasi Nchini ( TANSORT) kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtaalam kutoka Kitengo cha Uthamini wa Madini ya Vito na Almasi Nchini ( TANSORT) Dorcus Moshi (katikati) akiwaelimisha watoto waliotembelea banda hilo aina za madini yanayopatikana nchini Tanzania.
Baadhi ya wananchi wakiangalia aina za madini ya mawe katika banda la Wakala wa Jiolojia Nchini (GST), kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Banda la Wizara ya Nishati na Madini kama linavyoonekana pichani kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

STARS YAWAFUATA THE CRANES

$
0
0
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager inaondoka nchini leo jioni kuelekea Kampala - Uganda kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya The Cranes siku ya jumamosi.

Kikosi cha Taifa Stars kinaondoka kikiwa na wachezaji 20, bechi la ufundi 7, pamoja na viongozi kwa shirika la ndege la Rwanda (Rwada Airi) ambapo wanatarajiwa kuwasili uwanja wa Entebe majira ya saa 3 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

Mchezo wa jumamosi ni wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika nchini Rwanda, huku mechi hiyo ikichezwa saa 10 jioni katika uwanja wa Nakivubo.

Kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema vijana wake wamefanya mazoezi vizuri katika kipindi chote cha maandalizi, na sasa wako tayari kwa mchezo huo, mipango ikiwa ni kupata ushindi siku ya jumamosi.

Aidha Mkwasa amesema watawakosa wachezaji wawili, Abdi Banda na Mohamed Hussein (Tshabalala) waliopata majeruhi jana wakati wa mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Boko Vatereani, na kusema nafasi zao zitazibwa na wachezaji waliopo kambini.

Wachezaji wanaosafiri ni: Ally Mustafa, Mudathir Khamis, Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mngwali, Michael Aidani, Hassan Isihaka, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Salum Telela, Said Ndemla, Saimon Msuva, Deus Kaseke, Ramadhan Singano, Atupele Green, Rashid Mandawa, John Bocco na Ame Ally.

TFF YATUMA SALAM ZA RAMBI RAMBI KWA MWAKALEBELA, MWAMBUSI
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine ametuma salamu za rambi rambi kwa famili aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela kufuatia kufiwa na baba yake mzazi jana mjini Irinnga na mazishi yakitarajiwa kufanyika kesho mjini Iringa.

Aidha TFF imetuma salam za rambi rambi kwa kocha mkuu wa timu ya Mbeya City, Juma Mwambusi kufutia kufiwa na mama yake mzazi mjini Mbeya.

TFF pia imetuma salam za rambi rambi kwa familia ya mtangazi maarufu wa wa michezo nchini Ezekiel Malongo  aliyefariki dunia jana.

Katika salam zake kwa familia ya Mwakalebela, Mwambusi na Malongo, Mwesigwa amesema wanawapa sana pole wafiwa kwa kuondokewa na wapendwa wao na kusema kwa niaba ya TFF, familia ya mpira na watanzania wote wapo nao pamoja katika kipindi hichi cha maombolezo.


IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Mtandao wa Vodacom kutatua tatizo la Mawasiliano chini ya ardhi Afrika ya Kusini

$
0
0
Tatizo la kupata mawasiliano ya simu kwenye vituo vya usafiri vilivyojengwa chini ya ardhi nchini Afrika Kusini limekuwa ni tatizo sugu kwa muda mrefu.

Kituo maarufu cha Gautrain ambacho kimekuwa kikitumiwa na wasafiri wengi wakiwemo wanafunzi,wafanyakazi na watalii kwa muda mrefu tangia kifunguliwe mwaka 2010 kimekuwa kikikabiliwa na tatizo la mtandao ambao ulisababisha wasafiri wanaokitumia kituo hicho kushindwa kuwasiliana kwa njia ya simu na barua pepe. 

Kampuni ya Vodacom imejitosa kumaliza tatizo hilo kwa wateja wake ambapo kwa kushirikiana na Idara inayosimamia usafiri wa reli na barabara,uongozi wa kituo cha Gautrain,makampuni ya Bombela na Strategic kwa pamoja makampuni hayo yanafanya mchakato wa kumaliza tatizo la mawasiliano katika kituo hicho.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Ukuzaji Teknolojia wa kampuni ya Vodacom Afrika ya kusini Andries Delport anasema “Siku zote nilikuwa nakerwa na kukosekana mtandao wa mawasiliano ya simu na internet kwenye vituo vya treni vlivyopo ardhini hali ambayo imekuwa ikiwasababishia usambufu abiria.Tunajivunia kuwa mtandao wetu mkubwa nchini Afrika ya Kusini tumeamua kumaliza tatizo hili kwa wateja wetu”.

Tatizo  hili litamalizika kutokana na vifaa bora vya mawasiliano vilivyofungwa na Vodacom  katika vituo vitatu vya treni za ardhini,vifaa hivyo vya kisasa ambavyo ni pamoja na antenna za kurusha mawasiliano zimeunganishwa na mkongo wa mawasiliano uliopo eneo la Rosebank na hatua hii pia itawezesha upatikanaji wa huduma za internet kwa urahisi.

“Utekelezaji huu ni wa awamu ya kwanza tukimaliza hatua hii tutajenga mtandao wa mawasiliano chini ya ardhi  njia yote inayopita treni na kuhakikisha mawasiliano yanakuwa mazuri muda wote,tuko katika mazungumzo ya awali na wadau tutakaoshirikiana nao kutekeelza mradi huu wa kuboresha mawasiliano kwenye miundo mbinu ya usafri iliyojengwa chini ya ardhi”.Alisema Delport.

NMB yatia fora Saba Saba

$
0
0
Mabanda ya Benki ya NMB katika maonyesho ya saba saba mwaka huu yametia fora kwa kuwa kivutio kikubwa kwa watu wengi kutembelea na kujipatia huduma mbali mbali ikiwemo huduma ya wateja kujaza fomu maalum za kubadirisha kadi zao za ATM kuwa za MasterCard, kuweka na kutoa fedha kupitia gari maalumu pamoja na huduma za NMB Wakala.

Ndani ya viwanja vya saba saba, banda la NMB lipo mtaa wa Mabalozi mkabala na banda la Sido, pia kuna gari maalumu lenye ATM moja na madisisha mawili ya wahudumu (Tellers) wanaofanya huduma zote za kibenki.

Pia kuna mabanda madogo madogo 10, matano ya NMB Wakala ambapo wateja wanaweza kutoa na kuweka fedha zao na mabanda matano yanayotoa huduma za NMB Chap Chap Instant Account ambapo watu wengi wamekuwa wakifurika kwaajili ya kufungua akaunti za NMB.

Pia huduma za mikopo ya fedha na mikopo ya poikipiki za miguu miwili na miguu mitatu kwaajili ya watanzania wanaotaka kufanya biashara ya usafirishaji wa abiria kupitia vyombo hivyo.

Watanzania wote mnakaribishwa kupata huduma bora na ufafanuzi wa bidhaa mbalimbali zinazotolewa na benki ya NMB.
Mkurugenzi wa NMB – Ineke Bussemaker akipata maelezo mafupi kutoa kwa Meneja Masoko wa NMB nje ya banda la NMB lililopo kwenye viwanja vya saba saba leo. Bi Ineke alitembelea maonyesho ya saba saba kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa NMB.
Gari la NMB benki la kisasa kabisa kuliko magari yote ya namna hii katika viwanja vya saba saba. Katika gari hili kuna huduma zote za kibenki kama tawi na NMB linalotembea na huduma za ATM ndani yake.
Wateja wakisaini mikataba baada ya kutimiza mashart ya kukopa pikipiki za miguu miwili aina ya Bajaj.
Wateja wakipata huduma za kibenki katika viwanja vya saba saba. NMB Karibu yako.

TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA KUANZA UANDIKISHAJI BVR DAR ES SALAAM NA PWANI

$
0
0
Na Mwandishi-Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la wapiga kura kwa teknolojia ya Biometric Voters Registration (BVR) lililoahirishwa katika jiji la Dar es salaam na mkoa wa Pwani hivi karibuni sasa litafanyika kuanzia  Julai 7-20 kwa mkoa wa Pwani na Julai 16- 25 kwa jiji la Dar es salaam. 

Uboreshaji wa Daftari hilo kwa jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani uliahirishwa kutokana na kuchelewa kwa vifaa vya uboreshaji kutoka mikoani ambavyo vilipelekwa ili kuongeza ufanisi kutokana na maeneo hayo kuwa na idadi kubwa ya watu wenye sifa ya kuandikishwa kuwa Wapiga Kura.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Julius Mallaba amewataka wananchi wote wa mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya uandikishaji vitakavyokuwa kwenye Vijiji, Vitongoji na Mitaa ili kujiandikisha  waweze kupiga kura na kuchagua viongozi wanaowataka katika Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba Mwaka huu.

Amewataja watakaohusika na zoezi hili kuwa ni watu wote waliotimiza umri wa Miaka 18 na kuendelea na wale watakaotimiza Miaka 18 ifikapo mwezi Oktoba Mwaka huu.

Wengine ni waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura. Aidha Mallaba amewataja wengine wenye sifa ya kujiandikisha kuwa ni wale wote wenye sifa za kujiandikisha lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye Daftari hilo.

Amesema wale wote wenye Kadi za kupigia Kura za zamani wanatakiwa kwenda na Kadi zao ili kurahisisha uchukuaji wa taarifa zao na kadi hizo zitarudishwa NEC na watapata vitambulisho vipya.  Wananchi wanatakiwa kujiandikisha katika Vituo vilivyopo ndani ya Kata zao ili kuweza kupata fursa ya kumchagua Diwani, Mbunge na Rais.

Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wananchi wa mikoa hiyo kuhakikisha wanajiandikisha kwani bila kufanya hivyo hawataweza kupiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu. Vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kila siku kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa ifikapo saa 12:00 jioni. 

POLISI ARUSHA KUWAFANYIA USAILI ASKARI WATARAJIWA

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Liberatus Sabas

Na Woinde Shizza,Arusha

Jeshi la Polisi Mkoani hapa linatarajia kuwafanyia usaili vijana wa Mkoa huu waliomaliza kidato cha nne mwaka 2014 ambao wamechaguliwa kupitia tovuti ya Tamisemi ambayo ni www.pmoralg.go.tz. Wanaotarajia kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Liberatus Sabas aliyasema hayo ofisini kwake leo asubuhi ambapo alisema zoezi hilo litafanyika kwa muda wa siku mbili mfululizo yaani kuanzia tarehe 06.07.2015 na tarehe 07.07.2015 katika ofisi za Makao Makuu ya Polisi za Mkoa huu.

Aidha alisema zoezi hilo litaanza kuanzia saa 02:00 Asubuhi hadi saa 10:00 Jioni huku tayari majina ya vijana waliochaguliwa na maelezo yake yameshabandikwa katika ofisi za Mkuu wa Mkoa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Mkuu wa wilaya ya Arusha na Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa wilaya ya Arusha Mjini huku wilaya za Longido, Arumeru, Monduli, Karatu na Ngorongoro majina yao yatabandikwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri husika za wilaya hizo.

Waombaji watatakiwa wawe na vyeti vyote vya masomo (Academic Certificate(s)/Result Slip(s) & Leaving Certificate(s) na nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (original Birth Certificate) huku Hati ya Kiapo cha kuzaliwa haitakubaliwa pia atatakiwa kuwa na namba za simu ambayo itasaidia kumjulisha endapo atachaguliwa.

Aidha Kamanda Sabas alisema kwamba kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili huku atatakiwa kuwa na kalamu ya wino kwa ajili ya usaili wa kuandika bila kusahau kuzingatia tarehe na muda kuanza usaili.

Kamanda alimalizia kwa kusema kwamba, Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye ili mradi awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili.

Zantel yasaidia Chama Cha Maalbino Tanzania kutoa elimu kwa umma.

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose akikabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Bwana Ernest Kimaya. 
 Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya ushirikiano na kampuni ya Zantel leo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose na Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Bi Progress Chisenga,
   Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Pratap Ghose (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya ushirikiano wao na chama cha Maalbino Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel, Bi Progress Chisenga, na Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya

 Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imekisaidia Chama cha Maalbino Tanzania katika mpango wake wa kusambaza elimu juu ya ulemavu wa ngozi kwa jamii pamoja na msaada wa jumla ya shilingi milioni 5 ambao unalenga kusaidia uendeshaji wa shughuli zake hapa nchini.

Zantel kwa kushirikiana na Chama Cha Maalbino kitajikita kutoa elimu hii kwa kusambaza ujumbe mfupi kwa wateja wake pamoja na kutumia vipindi vyake inavyodhamini ili kupeleka ujumbe kwa jamii kiujumla.

Pamoja na hiyo pia, Zantel inajipanga kutumia mikutano ya wafanyakazi pamoja na matamasha ili kuhakikisha ujumbe kuhusu ulemavu wa ngozi unawafikia watu wengi zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel, Pratap Ghose alisema mchango huo katika kuwawezesha Chama cha Maalbino ni sehemu ya huduma za kampuni yake kwa jamii.

“Tatizo kubwa ni ukosefu wa elimu miongoni mwa wanajamii, na kwa hakika hatua kubwa imepigwa katika kupambana na tatizo hili tayari, na sisi kama Zantel tunaamini kwa kutumia uwezo wetu kama kampuni ya simu tunaweza kushiriki kulimaliza tatizo hili la mauaji ya ndugu zetu’ alisema Pratap.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, Tanzania ina jumla ya watu wenye ulemavu wa ngozi 5,200 na wengi wao wanaishi kanda ya ziwa, na toka mwaka 2009 jumla ya kesi 155 zinazohusu walemavu wa ngozi zimeripotiwa kwa vyombo vya sheria kwa mujibu wa taasisi ya Under the Same Sun.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino Tanzania, Ernest Kimaya, ameipongeza kampuni ya Zantel kwa mchango wao akisema utasaidia sana katika juhudi zao za kupigania haki za walemavu wa ngozi nchini.

‘Watu wenye ulemavu wa ngozi ni kama binadamu wengine wa kawaida, hivyo tunaiomba jamii isiwatenge ndugu zetu hawa’ alisema Kimaya.

Bwana Kimaya pia aliomba wadau wengine wajitokeze kuwawezesha walemavu wa ngozi waweze kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo.

“Jamii yetu ya walemavu wa ngozi ina matatizo mbalimbali, hivyo tunazidi kuwaomba watu binafsi, serikali pamoja na makampuni mbalimbali wazidi kujitokeza kusaidia kundi hili la jamii’ alisisitiza Kimaya.

Chama cha Maalbino Tanzania kilianzishwa mwaka 1978 kikiwa na lengo la kulinda na kuwezesha watu wenye ulemavu wa ngozi nchini na kinahudumia zaidi ya wanachama 1,200.

BENKI YA CRDB YASAIDIA KAMATI YA AMANI YA DINI

$
0
0
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa  akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hundi ya Shilingi milioni 12 kwa ajili maandalizi ya Futari iliyoandaliwa na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Madhehebu ya Dini. Kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum.  
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum wakionyesha hundi ya shilingi milioni 12 kwa ajili ya maandalizi ya futari iliyoandaliwa na Kamati ya Amani ya viongozi wa Madhehebu ya dini itakayofanyika Ijumaa Julai 3 kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

BONANZA MASAUNI CUP LILIVYOFANA ZANZIBAR

$
0
0
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Abdalla Bulembo wa kwanza kushoto Mbunge wa Kikwajuni Mhe Hamad Masauni na Kada wa CCM Abass Bahari wakijiandaa kuelekea kukagua timu hizo wakati wa Bonaza hilo linaloendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja usiku kwa micxhezo miwi kila siku.
                                                      Kizazaa golini kwa timu ya Rahaleo
Mchezaji wa timu ya Muembeladu akimpita mchezaji wa timu ya Rahaleo akiwa chini, wakati wa mchezo wao wa Bonaza Kombe la Masauni timu hizo zimetoka sare ya 2--2
Golikipa wa timu ya Rahaleo Saleh Machupa akiokoa mpira golini kwake wakati wa mchezo wao Bonaza Kombe la Masauni inayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Zanzibar Bonaza hilo limedhaminiwa na Mbunge wa Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni ili kuinua vipaji vya Vijana katika mchezo wa Soka Zanzibar.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WAZIRI WA UJENZI AKAGUA MIRADI YA NYUMBA ZA TBA KWA AJILI YA WATUMISHI WA UMMA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (wakwanza kulia) akipiga makofi mara baada ya kufungua nyumba za makazi ya Watumishi wa Umma zilizoko Mbezi Beach (E-NMC) jijini Dar es Salaam. Wa tatu kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe akifatiwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Arch. Elius Mwakalinga.
Nyumba ya Makazi ya Watumishi wa Umma ilioko Mbezi Beach (E-NMC) jijini Dar es Salaam kama linavyoonekana.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Mussa Iyombe akitoka kufanya ukaguzi wa jengo la Makazi ya Watumishi Sida Flats Kinondoni jijini Dar es Salaam.

MATUMIZI MABAYA YA ARDHI TISHIO KWA UHIFADHI

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu 

 Na Woinde Shizza,Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amesema kuwa matumizi mabaya ya ardhi yasiyozingatia mpango bora wa matumizi ya ardhi yamekua tishio kwa maeneo uhifadhi hivyo kupelekea uvamizi wa maeneo hayo na kutumiwa kwa shughuli za ufugaji na kilimo kinyume cha utaratibu.

Nyalandu amesema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa kati ya Wizara na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) uliofanyika jijini hapa,amesema kuwa ili kuwa na uhifadhi endelevu utakaorithiwa na vizazi vijavyo mpango wa matumizi bora ya ardhi hauna budi kuzingatiwa.

Waziri huyo amesema kuwa ujenzi wa miji katika maeneo ya uhifadhi ikiwemo Hoteli na kumbi za starehe unaathiri shughuli za uhifadhi hivyo amewataka wadau wa utalii kugawanya uwekekezaji kwa kuwekeza nje ya hifadhi.

“Mtu anayefikiria kujenga miji ndani ya hifadhi anakua hajapiga hesabu vizuri lazima tutawanye uwekezaji hoteli zijengwe nje ya hifadhi” Alisema Nyalandu.

Alisema kuwa kwa sasa Tanzania ina jumla ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) 21 ambazo ni kilometa za mraba 36237.7 na jumuiya nyingine 17 ziko katika hatua mbalimbali za uanzishwaji,amezitaka jumuiya hizo kuhakikisha kuwa zinawashirikisha wananchi katika kuhifadhi na kunufaika kwa mujibu wa sera ya wanayama pori ya mwaka 1998.

Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza watalii nchini Wilbard Chambulo alisema kuwa ili uhifadhi uweze kufanikiwa lazima wanakijiji wawe na hati miliki za maliasili ili waweze kuzitunza vyema. Chambulo anaeleza kuwa ushirikishwaji wa wananchi katika uhifadhi ni nguzo muhimu sana kwa uhifadhi itakayosaidia kuwa na utalii endelevu kwa vizazi na vizazi.

Upendo Nkone kumsindikiza Bonny Mwaitege

$
0
0
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili Tanzania, Upendo Nkone amekuwa wa kwanza kujitokeza kusindikiza uzinduzi wa mwenzake Bonny Mwaitege, utakaofanyika Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,  Alex Msama Nkone amekuwa wa kwanza na ameonesha nia ya kumsindikiza Mwaitege kwa sababu ya ubora wa uzinduzi huo. “Uzinduzi wa Mwaitege utakuwa ni wa aina yake kwa sababu maandalizi yake kwa yamefanywa kwa ustadi mkubwa  hasa hatua za mwisho za rekodi ya albamu hizo inayomaliziwa  jijini Mwanza na baadaye Nairobi,” alisema Msama.

Msama alisema Mwaitege anatarajia kuzindua albamu  tatu  ambazo zitashika anga la muziki huo hapa nchini kwa sababu ya ubora. Msama alisema sambamba na muimbaji huyo, mikoa mbalimbali imeonesha nia ya kutaka uzinduzi wa albamu hizo.

Aidha Msama alitoa wito kwa mashabiki wa muziki wa Injili Tanzania kujiandaa kupata neno la Mungu kupitia muimbaji huyo.  Bonny Mwaitege anatamba na nyimbo mbalimbali kama Mama ni Mama, Mke mwema, Wakusamehe, fungua moyo wako na njoo uombewe na Yesu yupo.
 

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR YAKABIDHIWA MAGARI YA MSAADA TOKA UINGEREZA

$
0
0
Na Makame Mshenga- 
Maelezo Zanzibar
Shirika la Shistosomiasis Control Initiative (SCI) la Uingereza limetoa Msaada wa Magari mawili aina ya Toyota Double Cabin kwa Wizara ya Afya Zanzibar kupitia kitengo chake cha Maradhi yasiyopewa umuhimu (NTD).

 Akikabidhi msaada huo leo Mwakilishi wa Shirika hilo Dkt. Khalfan Abdallah Mohamed amesema lengo la Msaada huo ni kuiwezesha Zanzibar kupiga hatua katika mapambano yake na Maradhi hayo ambayo yanawaandama watu wengi.
 Maradhi hayo ni pamoja na Matende, Minyoo,Kichocho ambayo ni vigumu kupata Misaada ya matibabu kutoka kwa Wafadhili wa jumuiya za kimataifa.

“Ni rahisi sana kuomba Msaada wa Maradhi kama UKIMWI kwa vile yanapewa kipaumbela na Wafadhili lakini maradhi mengine kama Minyoo au Matende ni vigumu sana kumshawishi mfadhili akasaidia” alisema Mwakilishi huyo wa SCI. 

Amesema Gari hizo ni kwa ajili ya kazi za kitengo cha Maradhi yasiyopewa umuhimu na kwamba zitatumika zaidi katika zoezi la ulishaji Dawa.
 Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amelishukuru Shirika la SCI kwa mashirikiano ya muda mrefu na Wizara ya Afya kupitia kitengo cha NTD kinachoendesha zoezi la ulishaji Dawa Mashuleni na katika jamii kwa ujumla.

Aidha ametowa wito kwa Mashirika mengine ya maendeleo kuunga mkono jitihada za Wizara ya Afya Zanzibar katika kupambana na Maradhi mbalimbali ambayo yanadhoofisha afya za Wazanzibari kupitia Vitengo mbalimbali.
 Waziri Mahmoud amezipokea gari kwa niaba ya Waizara ya Afya na kuliahidi Shirika la SCI kuzitunza ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa. Gari hizo mbili zitagawiwa ambapo Unguja itabakia moja na Pemba kupelekwa moja ili kusaidia mapambano ya Maradhi yasiyopewa umuhimu.

Imetolewa na Maelezo Zanzibar

DC MAVUNDE AZINDUA MASHINDANO YA MPIRA WA MIGUU MPWAPWA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Adv. Anthon Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mpira wa Miguu kuwania Kombe la DC na kushirikisha timu 24 kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo jana.
Timu za Mpwapwa Academy na Kota FC zikizubiri kukaguliwa na mgeni rasmi. Katika mchezo huo wa ufunguzi Kota FC wqalishinda goli 3-2.
DC akikaribishwa kusalimiana na wachezaji.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Zanzibar akabidhi vifaa mbalimbali kwa Skuli ya Rahaleo

$
0
0
Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Vifaa kwa Wananchi wa Jimbo lake iliofanyika katika Skuli ya Msingi Rahaleo Zanzibar.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Zainab Omar, akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Rahaleo na wanafunzi wa skuli hiyo katika hafla ya kukabidhi vifaa vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe. Nassor Salim Jazira.
Waziri wa Uwezeshaji Ustawi wa Jamii Vijana Wanawake na Watoto Mhe Zainab Omar akimkabidhi Seti ya Komputer Mwanafunzi wa Chuo cha Ualimu Rahaleo,kwa ajili ya matumizi ya Chuo hicho vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mhe Nassor Salim Jazira, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Skuli ya Rahaleo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TAIFA STARS YAAPA KUFANYA KWELI KATIKA MCHEZO WA MARUDIANO DHIDI YA UGANDA'CRANES'

Employers responsible for developing talent in Africa - DHL's VP of Human Resources

$
0
0
Lebo Tseladimitlwa, VP of Human Resources
at DHL Express Sub Saharan Africa.
While many global companies are expanding, or seeking to expand in Africa, the availability and retention of talent is proving to be one of the main challenges facing growth and expansion on the continent. 
According to Lebo Tseladimitlwa, VP of Human Resources at DHL Express Sub Saharan Africa, talent is perceived to be one of the major challenges facing business leaders in the region, with 83%1 of African CEOs admitting that they are especially worried about availability of key skills on the continent.  

Tseladimitlwa says that in addition to this statistic, the PWC Africa Business Agenda1 report also reveals that most CEOs expect to increase and maintain staff headcount in the next year. “In Africa’s competitive labour environment, these statistics highlight that attracting and developing the right skills is crucial.”


Tseladimitlwa adds that it is therefore important to adopt leadership styles which will support and nurture the skills and talent needed for growth. “Essentially, talent will no longer be the main concern when it comes to employees’ skill-sets, but rather the leader’s ability and responsibility to teach and develop these skills.”  To read more CLICK HERE

Rais Kikwete na Waziri Mkuu wa Ethiopia wazindua kiwanda cha Kudhibiti Malaria Pwani

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua rasmi kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza Malaria kilichopo eneo la viwanda TAMCO kibaha,Mkoani Pwani leo.Kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia wakiangalia uzalishaji wa viuadudu vya mbu wanaoeneza Malaria kilichopo eneo la viwanda TAMCO kibaha,Mkoani Pwani leo muda mfupi baada ya uzinduzi rasmi leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn muda mfupi kabla uzinduzi wa kiwanda cha kudhibiti malaria Mkoani Pwani leo. Picha na Freddy Maro.
Kusoma hotuba ya Rais Kikwete BOFYA HAPA
Viewing all 110186 articles
Browse latest View live




Latest Images