Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 890 | 891 | (Page 892) | 893 | 894 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Na Dotto Mwaibale 
  KAMPUNI ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ambayo ni wasambazaji wa bia ya Windhoek inaidai Tume ya Ushindani (FCC), sh.tirioni 1 kwa kukiuka uhalali wa mkataba wa Mabibo na kudai unapingana na ushindani. 
  Katika hatua nyingine kampuni hiyo imeiomba Mahakama ya Rufaa kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa uamuzi uliochukuliwa na Baraza la Ushindani (FCT) mwezi Aprili 2015 kuhusu haki ya Mabibo ya kuagiza na kusambaza bia za Windhoek kipekee katika soko la Tanzania. 
  Hayo yalibainishwa na Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, James Rugemalira wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. 
  Alisema mwezi Aprili 2015, FCT ilitoa uamuzi ambao ni sawa na kutangaza kuwa mkataba kati ya Mabibo Beer Wines and Spirits na Namibia Breweries Limited uliosajiriwa kwa matakwa ya Sheria ya Alama za Biashara na Huduma wa kipee wa Mabibo haukuwa halali kisheria. 
  "Si FCC wala FCT yenye mamlaka yakutengua uamuzi halali wa Mahakama kutafsiri sheria na katiba ya Tanzania. Katika kufungua shauri lake katika Mahakama ya Rufaa tarehe 24 Juni 2015, Mabibo imeiomba Mahakama kuthibitisha kwamba mwenendo wa Mabibo ni sahihi kwa mujibu wa Sheria ya Ushindani ya mwaka 2003, kama Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ilivyoamua mwaka 2010 na kuwa FCC na FCT walifanya kinyume cha mamlaka zao za kisheria na kikatiba na kujipa uwezo wa kutengua maamuzi ya Mahakama za Tanzania" alisema Rugemalira. 
  Aliongeza kuwa mbali na kuzidisha na kupanua mamlaka yao maamuzi ya FCC na FCT pia yanapuuza ukweli wa msingi. 
  Wakati Windhoek ni bidhaa maalumu inayofahamika kimataifa, ambapo mauzo yake nchini ni kiasi cha asilimia 0.05 tu ya soko la jumla nchini na sio kampuni inayotawala soko la bia Tanzania. 
  Alisema Mabibo inataka fidia hiyo kutoka FCC na washirika wake kwa sababu amri isiyo halali ya FCC imeruhusu muendelezo wa uagizaji wa bia ya Windhoek na wasambazaji wasioruhusiwa hivyo kuharibu biashara ya Mabibo na mkondo wa uadilifu wa bidhaa ya Windhoek katika soko la bia Tanzania.
   Bia za Windhoek zinavyoonekana.
   Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Bw. James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu kupinga uamuzi wa tume ya ushindani (FCC)  na kuidai fidia hiyo ya sh. tirioni moja kutoka na hasara wanayoipata kwa kuruhusu bia ya Windhoek kuingia katika soko la Tanzania ki holela.
   Mwenyekiti wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd,  Mama Benedicta James Rugemalira (katikati), akizungumza katika mkutano huo na kusema bia halali iliyopo kwenye soko ni ile yenye namba MB 66 na inayosambazwa na kampuni hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Mabibo, Anic Kashasha na Wakili, Stephano Kamala.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Mahusiano ya Kampuni ya Mabibo, Bw. Anic Kashasha (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Wakili wa Kampuni hiyo, Respicious Didace na Mwenyekiti wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta James Rugemalira.
   Wakili Stephano Kamala (kulia), akizungumza katika 
  mkutano huo. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Mama Benedicta James Rugemalira

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali pamoja na Mashirika ya Kimataifa kabla ya kuzindua kikosi kazi cha kupambana  na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Kikosi kazi hicho kimeundwa kwa kushirikisha Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam
   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali pamoja na Mashirika ya Kimataifa kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto-meza kuu), kuzindua kikosi kazi cha kupambana  na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Katika hotuba yake IGP Mangu aliomba ushirikiano na wananchi katika kupambana na uharibifu  wa mazingira nchini. Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.  Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.
   Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la Utunzaji wa Mazingira (ICCF) la nchini Marekani, Dk Kaush Arha akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali nchini pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia meza kuu), kuzindua kikosi kazi cha kupambana na uhalifu wa kimazingira kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu nchini. Uuzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo.  Wapili kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu
   Viongozi mbalimbali wa Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na Wakuu wa Mashirika mbalimbali ya Kimataifa wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (hayupo pichani) wakati alipokuwa akizindua Kikosi Kazi kitakachokabiliana na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachopambana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari mara baada ya kuzindua Kikosi Kazi kitakachokabiliana na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachopambana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Kikosi kazi hicho kimeundwa kwa kushirikisha Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


  0 0


  0 0

   Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya (PBZ) na wageni walikwa wakiingia kwenye ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort kwa kupata futari iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa wana Famili wa Benki hiyo na wateja wao.

   Mkurugenzi Masoko PBZ Seif Suleiman akiwaongoza wageni walikwa kupata futari iliyoandaliwa na Benki hiyo. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

   Walikwa na wafanyakazi wa PBZ wakijipakuli futari.

   Walikwa na wafanyakazi wa PBZ wakijipakuli futari.
   Mkurugenzi Huduma za Kibenki Said M. Said akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya PBZ Juma Amour (hayupo pichani) azungumze na walikwa.

   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya watu wa Zanzibar PBZ Juma Amour akizungumza na wanafamilia wa Benki hiyo na wageni walikwa waliofika kupata futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki yao kwenye ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo, Zanzibar.  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete

  0 0

  Tanzania’s number one online marketplace, Kaymu, is set to feature at the SabaSaba trade festival this coming week. Kaymu will participate for 5 days in the event which is usually centered on the public holiday of 7thJuly.

  With its everlasting partnership with Tigo under its Digital lifestyle strategy, Tigo has once again taken Kaymu under its wing. Tigo will be hosting Kaymu in its pavilion where customers will get the opportunity to come and learn about the essence of e-commerce and online shopping. People will get the opportunity to demonstrate first-hand how to shop and sell online, attendees will also get to Download the mobile application and register to the Kaymu family.  Additionally, there will also get a chance to win many prizes if they are lucky, the prizes will consist of Tshirts, Kaymu shopping vouchers, Tigo airtime credits and so forth.


  Erfaan Mojgani, Kaymu Tanzania’s country manager, told us via call from the Saba Saba grounds in Kurasini, “The Saba Saba event has always been a great meeting point for both buyers and sellers, just like Kaymu is and so we are very excited to be a part of it. It is also a great opportunity for Kaymu to carry out some of its key functions which include first hand customer service and education towards the public. We are looking forward to having a good season at the Saba Saba 2015 and we hope people are looking forward to spotting Kaymu around.”


  0 0

  Afisa MtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula  Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu Wakiwa wameshika Mfano wa Kadi ya Club Hiyo waliyoizindua.
  Klabu ya Simba leo hii imeandika historia kwa kuzindua Kadi Mpya za Wanachama ambazo zinamwezesha  kila Mwanachama wa  Simba  kupata  bima  ya maisha  hadi  Tsh 250,000 ikiwa atafiwa  na  mwenza au mtoto au yeye  mwenyewe  kupitia  bima  ya  maisha   iitwayo Simba Pamoja. Pia Simba  leo hii imezindua  Kadi za watoto yaani Simba Cubs. 
  Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva Akimkabidhi Mtoto  Iqram Ally Kadi ya Simba Cubs waliyoizindua leo wanaoshuhudia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group Imani Kajula (kulia) Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange "Kaburu".
  Akizungumza wakati wa uzinduzi Rais wa Simba Evans Aveva alisema ‘’Simba inaendeleza falsafa yetu ya utendajii  kifanya kazi ‘’maneno machache vitendo vingi’’, baada ya kuboresha upatikanaji wa taarifa kupitia mtandao kwa kuzindua tovuti yenye taarifa na huduma mbalimbali ndani yake, leo tumewaita  hapa  kuandika historia mpya kwa wana Simba na hususani wale wanaota ka kuwa wanachama wa Simba’’.
  Aliongeza  kusema ‘’ Simba inapenda kuwajulisha kuwa sasa mpenzi wa Simba anayetaka kuwa mwanachama anaweza kuomba kupata kadi ya wanachama kupitia tovuti ya Simba yaani www.Simbasports.co.tz . Napenda mtambue hii ni historia katika  ukanda huu kuweza kutumia  teknojia kufikia wanachama, Sisi  ni wakisa  sana  tunaona  mbele!.
  AfisaMtendajiMkuuwa EAG Group Imani Kajula (Kulia) Akielezea Jambo  Akiwa Ameambatana na Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (katikati) Wakati wa Uzinduzi wa Kadi Hiyo ya Simba Sport  Club Pamoja na Makamu wa Rais wa Club ya Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu
  Kwa  upande wake Afisa Mtendaji  Mkuu  wa EAG Group ambao ni washauri watekelezaji wa mikakati  ya masoko na  biashara Imani  Kajula  alisema
  ‘’ Uanzishwaji  wa  Kadi  ya  Simba Cubs itawawezesha watoto sio tukutambuliwa  kuwamemba  wa  Simba, bali  pia  kupata  punguzo   kubwa au kuingia  bure  kwenye  matukio  yanayo  andaliwa  na  Simba Sports Club. Pia  maduka  mbalimbali  yatatoa  punguzo  kwa  watoto  wenye  Simba Cub Card.
  Wote  mna  jua fika  kuwa  mapenzi   hujengwa, Simb  aina lenga kujenga msingi  imara  wa kuendeleza  wanachama  na  wapenzi wake’’.

  0 0


  0 0


   In response to a rising groundswell of requests and recognizing the role and place ZIFF has in developing the film and creative industries in Tanzania and east Africa ZIFF has today announced the ZIFF East African Music Video Awards Competition. The Awards are managed in collaboration with Push Mobile Media Limited.

  The Award aims to highlight the link between film and music as well as support the growing music video production industry in the region.

  Music Video Production houses are requested to nominate 3 of their 2014/2015 videos and submit them for competition.  The videos can be submitted through the ZIFF email: videos@ziff.or.tz

  Send the link that can be downloaded, Vimeo, YouTube or as MP4, MPEG, MOV file.

  The Videos will be shown on the ZIFF Channel on SIMU.TV

  JUDGING CRITERIA

  ·         Video must be on original work not based on copyrighted work

  ·         Music composition

  ·         Visual composition

  ·         Production values (quality and professional merit)

  ·         Must be a music based video not product promotion

  ·         Collaborations are accepted

  Winner will be determined by a public vote after the top 10 videos have been selected.


  The Deadline for submitting videos is 10th July, 2015


  0 0

  Na Monica Mutoni
  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) wameandaa mafunzo ya hali ya hewa kwa kutumia modeli ya PRECIS (Providing Regional Climates for Impact Studies) kuanzia tarehe 29 Juni hadi 03 Julai 2015. 
  Warsha/ mafunzo haya yameandaliwa na TMA chini ya mwamvuli wa mradi wa GFCS unaotekelezwa kwa upande wa Afrika katika nchi za Tanzania na Malawi.  
  Washiriki wa mafunzo hayo kutoka TMA na Kurugenzi ya Hali ya Hewa ya Malawi wanategemea kujifunza matumizi ya modeli ya PRECIS kutoka kwa mtaalamu kutoka Ofisi ya Hali ya Hewa ya Uingereza ambayo imekuwa ikitumia modeli hiyo katika utekelezaji wa huduma za hali ya hewa. 
   Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa wa utoaji huduma za hali ya hewa pamoja na kuweza kutoa taarifa sahihi za muda mrefu zenye kuweza kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya hali ya hewa na tabia nchi. 
  Alisema Dkt.Kijazi PRECIS ni mfumo unaweza kutoa taarifa za hali ya hewa za muda mrefu (Klimatolojia) kwa eneo husika.
   Mkufunzi wa warsha kutoka Ofisi ya Hali ya Hewa Uingereza bw. David Hein akiendesha mafunzo kwa wanawarsha. 

   Baadhi ya wanawarsha kutoka Malawi na Tanzania wakati wa warsha ya kisayansi kuhusu huduma za hali ya hewa kupitia modeli ya ‘PRECIS’.
   Dkt. Agnes Kijazi akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa warsha ya kisayansi kuhusu huduma za hali ya hewa kupitia modeli ya ‘PRECIS’.

   Wanawarsha kutoka Malawi na Tanzania wakati wa warsha ya kisayansi kuhusu huduma za hali ya hewa kupitia modeli ya ‘PRECIS’.

  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Dkt. Agnes Kijazi katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo.


  0 0   Meneja Mahusiano wa Kampuni ya simu ya Airtel, Jackson Mmbando (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ushirikiano wa Airtel na Finca kutoa huduma za kifedha. Kutoka kulia ni , Vivian Temi na Meneja wa Huduma ya Airtel Money, Stephen Kimea.
   Meneja wa Huduma ya Airtel Money, Stephen Kimea (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu huduma hiyo. Kulia ni Msimamizi Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya Finca Microfinance, Vivian Temi, Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Sarah Daffa na Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando.

   Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Dar es Salaam, Sarah Daffa akizungumza katika mkutano huo. 

   Maofisa wa Airtel na Finca wakionesha bango wakati wa uzinduzi wa mpango huo.

  Na Dotto Mwaibale
  KAMPUNI ya simu za mkononi Airtel Tanzania imesaini makubaliano na benji ya Finca Microfinance kwaajili ya kuwezesha wateja kuzifikia pesa zao kirahisi kwa kupitia simu zao za mkononi.
  Huduma hiyo mpya itawawezesha wateja wa Airtel kutuma pesa kutoka kwenye akaunti za benki kwenda kwenye akaunti zao za Airtel Money na kutoa kwenye simu kwenda benki.
  Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema huduma hiyo inalenga kuwawezesha wateza wao kufanya miamala yao mbalimbali ya kifedha wakati wowote kwa usalam azaidi.
  Alisema kwa kutambua finca sasa ni taasisi ya kibenki wameona ni vyema kuungana na kuweza kutoa huduma za kuhamisha pesha kwa usalama na kwa ghalama nafuu kupitia simu za mkononi kwa wateja wao nchi nzima.
  "Airtel itaendelea kuboresha huduma zake ili kuweza kufikia mahitaji ya wateja wake kwa kushirikiana na mashirika na taasisi mbalimbali katika kuboresha huduma zao kwa wateja," alisema.
  Naye Meneja wa Kanda wa Finca Microfinance Benki, Sarah Daffa alisema huduma hiyo itawasaidia katika kuongeza ufanisi kwenye huduma zao.
  "Tunawashukulu Airtel kwa kuungana nasi kupitia huduma za Airtel Money, tunaimani ushirikiano utatuwezesha kuongeza idadi ya wateja wetu tu bali utasaidia kuongeza idadi ya miamala inayofanyika kwa urahisi na salama," alisema.
  "Wateja wetu sasa wataweza kufanya miamala ya pesa wakati wowote mahali popote mara nyingi zaidi ikiwa tu watasajiliwa kweye huduma hiyo na akaunti yake ya benki ikiwa hai," alisema.

  0 0

  Mradi wa nyumba unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi inayoitwa Dege Eco-Village umeshiriki Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa Jijini Dar es Salaam ya Saba Saba.
  Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Bw. Azhar Malik wa Dege eco-Village alisema  kwa sasa ujenzi unaendelea na karibu aina ya nyumba apartment 3000 zishakamilika.
  Aliongezea kusema kwamba kupitia mradi huu waTanzania watanufaika kwa kupata ajira na pia kuwa na huduma kama hospitali, shule, maduka eneo la Kigamboni.
  Mradi huu unajengwa kwenye eneo takriban eka 300 na kampuni hiyo imewekeza zaidi ya dola milioni 350. 
  Kwa ujumla nyumba aina ya villa ziko 300 na apartment ziko 7400. Mradi huu utakamilika mwaka 2018. Apartment zitakamilika mwaka 2017 na villa mwaka 2018.
  Ndani ya mji huu wa Dege Eco-Village wakaazi  wake hawatahitaji kwenda popote kwasababu kila kitu kitakuwepo kama shule za watoto, kituo cha polisi, hospitali, supermarket, na kadhalika. 
  Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Amref Health Africa has announced the appointment of Dr Githinji Gitahi as its new Chief Executive Officer. Dr Gitahi joined the organisation on June 1, 2015, and will be based at the global headquarters in Nairobi.

  Making the announcement, the chair of Amref Health Africa’s International Board of Directors, Mr Omari Issa, said that Dr Gitahi was selected through an extensive, competitive international search and after a rigorous process of assessment, interviews and review of reports from referees. 

  “Having served in the health, for-profit and non-profit sectors, Dr Gitahi brings the skills and expertise necessary to navigate Amref Health Africa through its next phase of growth and development as we seek to innovative solutions to health challenges on the African continent,” said Mr Issa. 

  Until his appointment at Amref Health Africa, Dr Gitahi was the Vice President and Regional Director for Africa, Smile Train International, where he successfully established partnerships for long-term sustainability with various African governments.  Prior to that he worked with the Nation Media Group, where he was the Managing Director for Monitor Publications in Uganda as well as General Manager for Marketing and Circulation in East Africa. He also held progressively senior positions at GlaxoSmithKline, Avenue Group and the insurance industry.

  Dr Gitahi has a Bachelor in Medicine and Surgery and a Masters in Business Administration, majoring in Marketing. He takes over from Dr Lennie Kyomuhangi-Igbodipe, who has been serving as Interim CEO since the retirement of Dr Teguest Guerma, who headed the organisation between 2011 and 2014.

  “On behalf of all of us at Amref Health Africa, I would like to express our deep appreciation to Dr Kyomuhangi-Igbodipe. She has demonstrated great commitment and held the organisation together since she was appointed Interim CEO in November 2014. An announcement on her new role will be made in due course,” said Mr Issa.


  0 0  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amepokea kwa mshtuko na majonzi taarifa ya kifo cha Chifu wa Waluguru, Chifu Kingalu Mwanabanzi (pichani, enzi za uhai wake) ambacho kimetokea asubuhi ya leo, Jumatano, Julai Mosi, 2015 Kitengo cha Moyo cha Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
  Katika salamu zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mheshimiwa Dkt. Rajabu Lutengwe, Rais Kikwete amesema kuwa amepokea taarifa cha kifo cha Chifu Kingalu kwa mshtuko na majonzi.

   ”Nimeshtushwa na taarifa za kifo cha Chifu Kingalu ambaye nimejulishwa kuwa kilitokea asubuhi ya leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Kwa hakika, kifo hiki kimeifanya jamii yetu kupoteza kiongozi aliyeendesha shughuli zake kwa busara kubwa,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

  “Binafsi nilimjua Chifu Kingalu katika maisha yake. Alikuwa kiongozi mwenye busara na aliyetetea mila na tamaduni za watu wake. Alikuwa kiongozi mpenda watu na aliyejali sana maslahi na matakwa ya wafuasi wake. Nakutumia wewe Mkuu wa Mkoa wa Morogoro salamu zangu za rambirambi nikikupa pole kwa kuondokewa na mmoja wa viongozi wa kijamii katika eneo lako.” 

  “Aidha, kupitia kwako nawatumia wananchi wote wa Mkoa wa Morogoro na wanajamii wa Kiluguru kwa kuondokewa na kiongozi wa tamaduni na mila zao. Vile vile, nakuomba unifikishie pole zangu nyingi kwa wanafamilia ambao wamepoteza mhimili wao. Naungana nao katika msiba huu ambao pia ni msiba wangu. Naungana nao pia kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Chifu Kingalu Mwanabanzi. Amina.”

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu – Dar es Salaam.
  1 Julai,2015


  0 0


  0 0  0 0

  Kijana Abel Machanga mwenye umri wa miaka 24 amelazwa Hospital ya Taifa Muhimbili Wodi ya Sewahaji,chumba namba 19,Kitanda namba 28 kwa tatizo la uvimbe kwenye ubongo ambalo limesababisha macho yake kutoka nje.

  Familia inaomba msaada wa wasamaria wema ili kugharamia matibabu ya Abel kutokana kuwa gharama za matibabu ni kubwa kuliko uwezo wa familia.


  Kwa yeyote atakayetakayeguswa na taarifa hii, anakaribishwa kumtembelea Abel Hospitalini ili kukutana naye na kusikia kilio chake Kwa mlio mbali, tunaomba misaada yenu kupitia kwa  kaka wa Abel  Bw.Christopher Machanga kwa namba


  Tigo                      0655 54 56 67

  Airtell                  0784 54 56 67

  Voda                    0755 54 56 67


  SHIME WATANZANIA TUJITOE KWA MOYO KUOKOA MAISHA YA MWENZETU NA KUPUNGUZIA MATESO MAKALI ANAYOKABILIANA NAYO KWA SASA.  TUNATANGULIZA SHUKRANI.

  0 0

  Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Major General G.S Milanzi kulia akiongea na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Helmas Mwansoko kushoto kabla ya Prof. Mwansoko kutoa Mhadhara juu ya Utamaduni unavyochangia katika usalama na ulinzi wa Nchi kwa Viongozi wa Ulinzi na usalama wa ndani na nje ya nchi pamoja na Taasisi za umma.Mhadhara huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Helmas Mwansoko akitoa mada kwa Viongozi wa Ulinzi na usalama wa ndani na nje ya nchi pamoja na Taasisi za umma juu ya Utamaduni unavyochangia katika usalama na ulinzi wa Nchi .Mhadhara huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Helmas Mwansoko akitoa mada kwa Viongozi wa Ulinzi na usalama wa ndani na nje ya nchi pamoja na Taasisi za umma juu ya Utamaduni unavyochangia katika usalama na ulinzi wa Nchi .Mhadhara huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo. Picha na Benjamin Sawe.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Tathmini ya Athari ya Mazingira kutoka Baraza la Taifa la kuhifadhi Mazingira (NEMC), Eng. Ignance Mchallo akielezea kuhusu Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 kwa mafundi sanifu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA.
  Mafundi Sanifu wakifanya tathmini na ukaguzi wa mazingira katika karakana ya TEMESA mjini Morogoro wakati wakiwa katika mafunzo ya tathmini, usimamizi na ukaguzi wa mazingira.
  Ofisa Manunuzi wa Wizara ya Ujenzi, Bw. Shukuru Sikunjema akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Eng. Melania Sangeu baada ya kuhitimu mafunzo ya tathmini, usimamizi na ukaguzi wa mazingira yaliyofanyika mkoani Morogoro.


older | 1 | .... | 890 | 891 | (Page 892) | 893 | 894 | .... | 3285 | newer