Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live

JOTO LA ASUBUHI LA 93.7 EFM IJUMAA JULY 3, 2015


DIRA YA DUNIA YA IDHAA YA KIWASHILI YA BBC, LONDON

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LANG'ARA MAONYESHO YA 39 YA SABASABA

$
0
0
Afisa Mwandamizi wa Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Salvatory Hinju akitoa maelezo namna Shirika la Nyumba linavyofanya kazi zake kwa Wateja waliofika kwenye banda la maonyesho la Shirika hilo lililopo ndani ya viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Shirika la Nyumba la Taifa Tuntufye Mwambusi akizungumza na mmoja wa wateja wa Shirika la Nyumba alipofika kwenye banda la maonyesho la Shirika hilo lililopo ndani ya viwanja vya Maonyesho vya Sabasaba (Mwalimu Nyerere) katika maonyesho ya 39 ya biashara ya kimataifa.
 Mteja akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Aika Swai, anayewasikiliza ni Afisa Mauzo Mwandamizi wa NHC, Julieth Buberwa.
 Afisa Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa, Aika Swai akitoa maelekezo kwa wateja kuhusiana na ujenzi na mauzo ya nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa kwenye Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 39 yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba.

mkutano wa hadhara

NHC yanyang’anya mashine za kufyatulia matofari baada ya Halmashauri za Mikoa kushindwa kutumia fursa hiyo

$
0
0
NHC imeendelea kuwakagua vijana waliopewa msaada wa mashine za kufyatulia matofali yatakayowezesha wananchi kujijengea nyumba za gharama nafuu katika Halmashauri zote za Mikoa ya Katavi, Mbeya na kukamilika Mkoani Iringa. 

Kwa ujumla, vijana wana ari ya kutosha ingawa wana changamoto zinazohitaji msukumo wa Halmashauri zao, hasa za masoko ya matofali yao pamoja na mtaji wa kuwawezesha kuendelea na uzalishaji wa benki ya matofali ya kuuzia wananchi. 

Katika ziara ya NHC Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya hizo wameomba NHC isiwanyang’anye mashine na wameahidi kuwapa vijana mikopo na kuwasaidia malighafi za kuwawezesha kutengezea matofali hayo ikiwemo mchanga, sementi na udongo maalum kwa kazi hiyo. 

Hata hivyo, Mikoa ya Rukwa na Katavi muitikio wa vijana na Halmashauri hizo ukiacha Halmashauri ya Mlele ambayo inafanya vizuri, umekuwa hafifu sana na Shirika limelazimika kuzinyang’anya Halmashauri hizo mashine na kuzitaka kuomba upya kama bado wana azma ya kutumia mashine hizo kujiletea maendeleo ya kuwa na nyumba bora na kukuza ajira kwa vijana wao. Fuatilia yaliyojiri katika uhakiki huo katika picha.
New Picture (1)  
Kikundi cha ‘Mshikamano’ katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kikimsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC BW. Muungano Saguya akiwaelezea namna ya kukuza ujuzi na kutumia Halmashauri zao kuongeza ufanisi wa kazi alipowatembelea nakusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili. Vijana hao wameshapewe eneo la muda la kuendesheea shughuli zao na wameanza kutengeneza tofali kwa ajili ya kuwauzia wanmanchi.
New Picture (2)
Hii ndiyo hali iliyojitokeza Mkoani Katavi katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda pale NHC ilipolazimika kuzitwaa mashine ilizotoa msaada kwa vijana ili waweze kujiajiri. Kikundi hiki cha Mpanda Hotel ni mojawapo ya vikundi vilivyonyang’anywa mashine Mkoani Katavi na Rukwa kwa Halmashauri sita za Mikoa hiyo ukiacha Mlele inayofanya vizuri, kushindwa kuzitumia mashine hizo ipasavyo. Halmashauri hizo zimetakiwa kuomba upya mashine hizo na kuunda vikundi imara baada ya kubainika kuwa vikundi vya awali vilundwa kisiiasa.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TANGAZO LA VIWANJA NA MASHAMBA KWA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA (DIASPORA)

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaandaa mahitaji ya ardhi kwa ajili ya watanzania waishiao nje ya Tanzania.  
Nchini Uingereza, Ubalozi unaratibu zoezi hilo kwa watanzania waishio Uingereza na Ireland. 

Tunaomba maombi hayo yaainishe Mkoa na Wilaya hitajika, aina ya matumizi ya ardhi hiyo kama ni Makazi, Biashara au Kilimo.

Maombi yawasilishwe kwa Viongozi wa Jumuiya za Watanzania katika miji/ maeneo wanayoishi, ambao watayaleta ubalozini kwa hatua zaidi. Au muombaji wanaweza kujaza fomu ya maombi kupitia tovuti ya Ubalozi kwa anuani ifuatayo: - http://tanzania-online.gov.uk/?page_id=309

Kwa maelezo zaidi piga simu namba: +44 207 569 1482 au tuma Barua pepe (Email): balozi@tanzania-online.gov.uk

*IMETOLEWA NA UBALOZI WA TANZANIA, UINGEREZA*

BUNGENI LEO KUPITIA SIMU TV

$
0
0
SIMUtv: Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh.Silima akijibu swali juu ya hali ya ugaidi hapa nchini licha ya kifo cha kiongozi wa kundi la kigaidi Osama bin Ladden    https://youtu.be/9bir_jqGd8Y
SIMUtv: Tamko la serikali juu ya wakulima waliotumia sera za kilimo nchini Mkatika kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mazao ya kilimo.   http://youtu.be/CVv08Qx_0cQ
SIMUtv: Serikali imeombwa kuwashirikisha wadau mbalimbali toka sekta binafsi kuwekeza katika usafiri visiwani ili kurahisisha huduma za kijamii.    https://youtu.be/170Gd80Uy68
SIMUtv: Serikali imeombwa kushirikiana na sekta binafsi ili kuwapa huduma muhimu watu wenye albinism katika mapambano dhidi ya ukatili. http://youtu.be/gf32gpKkfl8
SIMUtv: Beki wa argentina awataka wachezaji wenzake kuwa watulivu katika maandalizi ya mchezo wa fainali kuwania kombe la Kopa Amerika.     http://youtu.be/3niVouCnCYE
SIMUtv: TFF imekingia kifua uamuzi wake wa kumrudisha Mguto kwenye uchaguzi wa Coastal union baada ya kutokuwa na  Cheti cha kidato cha nne      http://youtu.be/5mJiaZkSpyQ
SIMUtv: Uhalali wa muwekezaji katika shamba la mkonge la Kumburu lililopo Mkoani Tanga wazua tafran Bungeni.   http://youtu.be/RsjGjwTrj5Q
SIMUtv: Mnyika azidi kuvuruga Bunge, amtaka Spika kusitisha shughuli za bunge ili kujadili maswala ya  tume huru ya uchaguzi.    https://youtu.be/KABWtwCBjbs
SIMUtv: Hivi ndiyo vioja vilivyotolewa ba wabunge leo bungeni vilivyosababisha Bunge kuhairishwa kwa mara nyingine tena.     http://youtu.be/eepqgqu80mg

FINLAND NA TANZANIA KUSHIRIKIANA KIBIASHARA

$
0
0
 Mkurugenzi wa biashara ya ndani mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania (TANTRADE), Edwin Rutagarutwa akizungunza  katika semina ya kibiashara iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam  leo. Kuhusiana na  wigo wa biashara hapa nchini na nchi ya Finlan.
 Mwenyekiti wa mkutano na Ushirikishaji  wa ubalozi wa Finland,Siv Ahlberg katika akizungunza  katika semina ya kibiashara iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam  jana, kuhusiana na historia ya Finland pamoja na njia za kibuiashara za nchi yao.
 Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link, Abdulmalik Mollel akiuliza swali kuhusiana na utoaji elimu kwa wananchi kuhusiana na masual;a ya kibiashara kati ya wafinland waliopo hapa nchini na Watanzania.
Mkurugenzi mkuu mtendaji wa kampuni ya 3disius International , Afrodisius Sabuni akichangia  maada katika kuhusiana na kinga ya mjasisliamali wa kitanzania kwenye kutoa taarifa za kibenki kwa wawekezaji wa kigeni iko na imara kwa kiasi gani na inaulinzi wa kutosha katika jamii, katika semina ya kibiashara iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam  jana. 
Baadhi ya wadau wa biashara waliohudhuria katika mkutano unaoshirikisha wadau wa biashara wa hapa nchini na wafinland.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Jaji Mkuu aongoza sherehe za kuwakubali na kuwasajili Mawakili wapya jijini Dar leo

$
0
0
Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa katika meza kuu pamoja na Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Tanzania katika Sherehe za kuwakubali na kuwasajili Mawakili wapya, mapema leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Jaji Mkuu wa TanzaniaMhe. Mohamed Chande Othman,  (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani (walioketi), Mhe. Shaaban Ali Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (wa tatu kulia) na baadhi ya Mawakili wapya (waliosimama) waliopishwa mapema leo.
Pichani ni baadhi ya Mawakili wapya walioapishwa leo na Mhe. Jaji Mkuu, Mhe. Jaji Mkuu leo ameapisha jumla ya Mawakili 412 na kuongeza idadi ya jumla ya Mawakili 4874. (Picha na Mary Gwera, Mahakama)

KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA RUKWA AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA SIKU SITA YA WALIMU WAKUU NA WARATIBU ELIMU KATA

$
0
0
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Erasmus Rugarabamu akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku sita ya Walimu Wakuu Shule za Msingi na Waratibu Elimu Kata juu ya muongozo wa uendeshaji wa shule (School Management Tool Kit) pamoja na usimamizi wa ufundishaji wa kusoma, kuandika na kuhesabu leo tarehe 03 Julai 2015. Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu yanafanyika Mkoani Rukwa katika Chuo cha Ualimu Sumbawanga ambapo jumla ya washirikia 200 kutoka Halmashauri mbili za Manispaa ya Sumbawanga na Sumbawanga Vijijini wameshiriki kwenye awamu hii ya kwanza ya mafunzo. Mafunzo haya ni sehemu ya mpango wa BRN wenye lengo la kuinua ubora wa elimu nchini.
 Ndugu Nicholaus Moshi ambae ni Mratibu wa Programu ya Mafunzo ya Waalimu Kazini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza katika Semina hiyo. Ndugu Moshi ni mmoja ya wawezeshaji wakuu katika Mafunzo hayo.
 Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Maalim Seif afutari pamoja na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Rais wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu Ust. Ali Abdallah, alipowasili chuoni hapo kwa ajili ya kufutari na wanafunzi wa chuo hicho.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na wanafunzi wa Chuo kikuu cha Zanzibar Tunguu, baada ya kufutari na wanafunzi hao.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akijumuika na viongozi wa Mkoa wa Kusini Unguja, masheikh na wanafunzi wa ZU katika futari. Kutoka kulia ni Naibu Kadhi Mkuu Sheikh Othman Ngwali, Rais wa serikali ya wanafunzi (ZU) ust. Ali Abdalla na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt. Idrisaa Muslih Hijja.

Wanne wajishindia mamilioni ya Bayport

$
0
0
Wateja walioshinda katika bahati nasibu yetu na maeneo watokayo kwenye mabano ni pamoja na Simion Ngassa (Iringa), Sisco Haule, (Kigoma), Said M Mkinda (Dar es Salaam) na Phelis Nziku ambapo wote kila mmoja watakabidhiwa kiasi hicho cha pesa kutoka Bayport Financial Services. Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo aliipongeza Bayport Financial Services kwa kuendelea kubuni mambo yanayoweza kuwapatia mwanga wateja na Watanzania kwa ujumla.

“Hii ni bahati nasibu nzuri na rahisi kuchezwa na kila mtu, maana haina vigezo zaidi ya mtu kuingia kwenye droo kama atakuwa amekopa tu, iwe kwenye mtandao wao au kufika katika tawi la ofisi yao yaliyoenea sehemu mbalimbali za Tanzania Bara,” alisema Ngolo, huku akiwataka Watanzania kuendelea kunufaika na huduma mbalimbali za Bayport. Huduma zinazotolewa na Bayport ni pamoja na mikopo ya fedha, mikopo ya bidhaa mbalimbali kama vile vifaa vya ujenzi, bodaboda, injini ya boti, pembejeo za kilimo, zikiwa ni miongoni mwa huduma zinazorahisisha maisha kwa Watanzania wote.
Zoezi la kuchezesha droo hiyo ya Kopa na Bayport likiendelea. Washindi wanne walijishindia Sh Milioni 1,000,000 kila mmoja.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo kushoto, akizungumza jambo kwenye heka heka ya droo ya kutafutwa washindi wanne wa shindano la Kopa na Bayport linaloendeshwa na Taasisi hiyo. Aliyefungwa kitambaa usoni ni Meneja wa Bayport Financial Services, Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala. Kulia ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Jehud Ngolo. Washindi hao wanne kila mmoja amejishindia Sh Milioni 1,000,000 baada ya kukopa kwenye taasisi hiyo ya kifedha nchini.

Airtel yatangaza ofa kabambe - Nunua Airtel HOME Wi-Fi na upate nyingine ya BURE

$
0
0
Ofisa uhusiano na Matukio wa Airtel, Bi Dangio Kaniki akionyesha kifaa cha HOME Wi-Fi wakati wa kutangaza ofa kabambe ya Sabasaba itakayo wawezesha watanzania kupata kifaa cha bure cha ziada pindi watapokinunua katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba. Pichani, Afisa Masoko wa Airtel ,Ndevonaeli Eliakimu.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza ofa kabambe katika viwanja vya Sabasaba itakayomwezesha mteja kununua kifaa cha HOME Wi-Fi, chenye uwezo wa kuunganisha zaidi ya vifaa 32 kupata huduma ya internet kwa kutumia kifurushi kimoja kwa gharama nafuu zaidi na kuunganishwa kwenye kifurushi cha internet cha 40GB Bure.

Ofa hiyo itamwezesha mteja kununua HOME Wi-Fi, kwa shilingi 195,000/- na kujipatia Home Wi-Fi ya bure pamoja na kifurushi cha internet cha 40GB cha bure . Ofa hii inapatikana kwenye banda la Airtel katika viwanja vya maonyesho ya Sabasaba kwa muda wa kipindi hiki cha maonyesho.

Akiongea wakati wa kutangaza ofa hii Ofisa uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki alisema " Tumeona ni vyema kuwazawadia wateja wetu kwa kuwapatia ofa hii ya kifaa kitakachowawezesha kuunganishwa kwenye huduma ya internet kwani mahitaji ya huduma ya internet yanazidi kuongezeka kwa kasi. Airtel HOME WiFi inaweza kuunganisha vifaa zaidi ya 32 kwenye huduma ya intenet ya kasi bila kuhitaji simcard yoyote ya ziada".

"Sambamba na hilo, Airtel HOME Wi-Fi vilevile itaunganisha hadi simu 4 za mkononi zilizoko kokote nchini kwenye akaunti moja na kuwapatia internet ya kasi ya 3.75G. Kwa sasa wanafamilia na watumiaji wa intenet Tanzania hawana haja ya kununua vifurushi vya intaneti kwa kila simu , kompyuta, Television au vifaa vyovyote vinavyoweza kuunganishwa na internet na badala yake watakachotakiwa kufanya ni kununua kifurushi kwenye kifaa hiki cha HOME Wi-Fi na kuwawezesha wote waliounganishwa na kifaa hicho kupata huduma ya intaneti popote walipo Tanzania na watatumia kifurushi kimoja walichonunua"

"Natoa wito kwa wateja wetu na watanzania kutembelea Banda letu na kujipatia Home Wi-Fi na kuungalisha kweny internet wakati wote". Aliongeza Kaniki

NEC NA VIONGOZI WA VYAMA VYASIASA ,WAJADILI MAADILI YA UCHAGUZI WA RAIS,WABUNGE NA MADIWANI

$
0
0
Na Avila kakingo, Globu ya jamii.
TUME ya uchaguzi NEC  wakishirikiana na viongozi wa vyama  vya siasa wakutana kujadili  maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ikiwa tunaelekea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika  Oktoba mwaka huu.

 Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji  Mstaafu Damiani Lubuva, Kwenye ufunguzi wa mkutano wa tume na viongozi wa vyama vya siasa kuhusu maadili ya uchaguzi leo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji  Mstaafu Damiani Lubuva amesema kuwa kupiga kura ni haki ya msingi na ya kikatiba kwa kira raia wa Tanzania hivyo uchaguzi unatakiwa uwe wa haki, uhuru, uaminifu na wakuaminika.

Lubuva amesema kuwa  maadili yanayojadiliwa yahahusu zaidi  vyama vya siasa, wagombea wote, serikali pamoja na tume ya uchaguzi pia  kila chama na wagombea wanatakiwa kuheshimu na kutekeleza sheria za uchaguzi,kanuni na maadili na sheria nyingine za nchi katika kipindi cha kampeni kuanzia siku moja baada ya uteuzi hadi siku ya uchaguzi Oktoba mwaka huu.

Pia ametoa wito  kwa wanasiasa wote kuwaelimisha wafuasiwao kuondoka vituoni nara  baada ya kupiga kura ili kuepusha msongamano wa vitendo vingine vinavyoweza kuchochea kuvunjika kwa amani.

Kwa upande wa jeshi la polisi wametoa wito kwa wagombea wote watakao wania nafasi mbalimbali wafanye kampeni zake kipindi wakati kuna mwanga na si usiku ili kuepuka matatizo mbalimbali yatakayojitokeza.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji  Mstaafu Damiani Lubuva akizungumza wakati wa mkuato wa kujadili maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
  Baadhi ya viongozi wa vyombo vya siasa wakifuatilia kwa umakini katika mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Katibu Mkuu wa chama cha Tanzania Labour Part(TLP), Nancy Mrikalia akichangia maada katika mkutano wa kujadili maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani katika mkutano uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
 
  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

KATIBU MKUU KIONGOZI ,BALOZI OMBENI SEFUE ATEMBELEA MAONESHO YA 39 VIWANJA VYA M.J.NYERERE JIJINI DAR

$
0
0
 Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Fedha alipotembelea katika banda hilo katika maonesho ya 39 yanayofyanyika katika Viwanja Vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) leo jijini Dar es Salaam,Kushoto ni Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha,Ingiahedi Mduma.

Katibu Mkuu wa Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue  akisalimiana Afisa Habari wa Shirika la Taifa la  Bima( NIC),Mwanaidi Shemheta alipotembelea banda hilo katika maonesho ya 39 katika Viwanja vya Mwalim Nyerere (Sabasaba) leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi akisaini Kitabu cha wageni katika banda la Shirika la Taifa la Bima (NIC) alipotembelea Maonesho ya 39 yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Saba saba) leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akipata maelekezo katika Mfuko wa Pensheni wa PSPF alipotembelea maonesho ya 39 yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere (Saba saba) jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akipata maelezo kutoka Afisa Masoko Mwandamizi wa GEPF,Violeth Nyakunga  alipotembelea maonesho ya 39 yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar esalaam leo. 
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akipata maelekezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi wa ajira ,Masoko na Utafiti  wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA)Julius Mjelwa  alipotembelea katika maonesho ya 39 yanayofanyika katika viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akipata maelekezo kutoka kwa  Mwalimu wa Umeme   wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA),Majollo Mwigowe, alipotembelea katika maonesho ya 39 yanayofanyika katika viwanja vya Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam. (picha zote na Chalila Kibuda wa Globu ya Jami).

WAZIRI MKUU,MIZENGO PINDA AKUTANA NA WAJASIRIMALI WA ASALI KATIKA VIWANJA VYA M.J NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,akipata maelekezo ya asali alipotembelea banda la asali katika maonesho ya 39 yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Wajasiriamali wa bidhaa ya asali  ndani ya maonesho ya 39 yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

CHADEMA YAANDAA KONGAMANO LA WAZEE, KUFANYIKA KESHO HOTELI YA BLUE PEARL UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Hashim Juma Issa (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana, kuhusu kongamano litakalo wakutanisha wazee wote bila kujali itikadi za vyama vyao litakalo jadili mustakabali wa taifa kuelekea uchaguzi mkuu litakalofanyika  kesho ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl Ubungo jijini Dar es Salaam.
 Makamu  Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Suzan Lymo, akizungumza katika mkutano huo.
 Baadhi ya wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.
 Baadhi ya wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano huo.


Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeandaa 
kongamano la wazee ambalo litafanyika Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam kesho.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo mchana 
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la chama hicho, Hashim Juma Issa alisema kongamano hilo litawahusisha wazee wote nchini bila ya kujali itikadi za vyama vyao.

Alisema dhima kubwa ya kuanzisha kongamano hilo ni kuwapa elimu wazee bila kujali itikadi zao za kisiasa  hasa katika kipindi hiki cha  kuelekea uchaguzi mkuu. 

"Wazee wengi wamekuwa hawafahamu nini majukumu yao kama wazee lakini kongamano hili litakuwa ndiyo chanzo kikubwa cha 
kuwafahamisha wazee majukumu yao hasa katika wakati huu wa 
kuelekea uchaguzi," alisema Issa.

Alisema kila mtu anafahamu  binadamu huwa anapitia hatua muhimu za maisha nazo ni utoto,ujana na utu uzima hivyo hamna budi wazee hawa kuelewa lengo kuu katika katika uchaguzi mkuu huo kuwa katika mstari ulinyooka. 

"Kumekuwa na tabia ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwatumia wazee kwa ujanja tena hasa wakiwa na matatizo na kuwabagua wa vyama vingine lakini sisi katika kongamano hili hatutobagua mzee wa chama chochote katika kongamano hili kwani wazee wote ni hazina,"alisema

"Hakuna asiyefahamu kuwa kwa sasa nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu ambao uchaguzi huu utakuwa ni mkubwa na wa aina yake hivyo kwa kuwaita wazee hawa itakuwa ni muendelezo wa kupata hekima zao kama wazee"alisema.

Issa alisema katika uchaguzi mku wazee wana jukumu kubwa la 
kuhakikisha kushiriki kikamilfu katika zoezi zima la kujiandikisha na kupiga kura ipasavyo.Alisema hatua hiyo haina budi kuwasahawisi watoto na watu wakubwa na wajukuu kushiriki kwa ukamailifu katika tukio hili kwani kila mtu anahitaji mabadiliko katika nchi.

Hata hivyo Issa alisema wazee pia wana jukumu kubwa la kutatua 
migogoro ,kushawisi na kusimamia maadili lengo likiwa ni uthubutu wa kukemea viongozi wanaopata madaraka kwa njia ya rushwa na ufisadi.

Alisema wanahitaji wazee watakaosimama kidete na kupaza sauti zao katika kukemea maovu na watenda maovu bila kuona haya.

Alisema katika kongamano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Wilbroad Slaa huku mada mbalimbali zitatolewa na Mabere Marando pamoja na viongozi wa dini ili kuwapa elimu wazee kutokana na maadili ya nchi kumomonyoka kwa kiasi kikubwa.

NEC YATOA MWALIKO WA WAANGALIZI WA NDANI WA UCHAGUZI MKUU .

$
0
0

 Na Jovina Bujulu.

Taasisi na Asasi mbalimbali zimetakiwa kutuma maombi kwenye ya  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kusimamia uchaguzi mkuu utatarajia kufanyika mwezi oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume hiyo leo jijini Dar es salaam, imezitaka taasisi na asasi zenye nia ya kuwa waangalizi wa Uchaguzi Mkuu ujao kuwasilisha maombi yao katika ofisi ya NEC kuanzia  Julai 5 hadi Oktoba 6 mwaka huu.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa waombaji wanatakiwa kuwalisha maombi yao yakiwa na anuani kamili ikiwemo ya makazi ya taasisi na asasi husika , mahali inapofanyia kazi, shughuli zake na sehemu ambayo taasisi inataka kuendeshea shughuli za uangalizi.

Mambo mengine yanayohitajika katika maombi hayo ni idadi ya wafanyakazi wa taasisi husika na taarifa zao binafsi na pia taasisi iambatanishe vivuli vya nakala cheti za usajili na Katiba ya Taasisi husika.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa Mamlaka ya kusajili waangalizi wa ndani kwa mujibu wa sehemu ya IV na V ya kanuni ya uchaguzi wa Rais , Wabunge na Madiwani.

Uchaguzi Mkuu wa kuwamchagua  Rais , Wabunge na Madiwani  unatarajiwa kufanyika nchini kote Oktoba 25 mwaka huu.

SIMBA SPORT CLUB YAZINDUA HUDUMA MPYA YA SIMBA NEWS

$
0
0
Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva (katikati) Akizungumza katika Uzinduzi Huo Akiwa na   Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani Kajula (Kushoto) Pamoja na Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile Solutions, Bi Lulu Ramole.
Simba Sports Club kwa kushirikiana na Kampuni ya Tigo Tanzania zimezindua huduma ya ujumbe mfupi ijulikanayo kama ‘SIMBA NEWS’, ambayo lengo lake nikuwapatia wateja wa Tigo taarifa zinazoihusu klabu ya Simba popote walipo nchini.
Huduma hii mpya inajulikana kama ‘SIMBA NEWS’. Njia hii ni rahisi na yenye ufanisi yenye kuifanya dunia ijulikane kwa wateja wake.

 “Pamoja na kasi yaukuaji wa Tehama, Tigo inaelewa umuhimu wakutoa taarifa kwa wateja wake, ndiyo maana leo, tunajisikia fahari kuzindua huduma hii iliyotengenezwa vizuri ya SIMBA NEWS nawashirika wetu wa klabu ya SIMBA, EAG Group LTD pamoja na Premier Mobile Solutions (PMS), ilikuendelea kuwapa wateja wetu taarifa zinazohusu masuala ya sasa huku wakifurahia habari mpya zinazohusu klabu,”alisema meneja wa mawasiliano ya kibiashara Jacqueline Nnunduma.
Lengo letu si tu kuwapatia wateja wetu taarifa kiurahisi zaidi, lakini pia kuwapatia taarifa hizo kwa wakati na zenye uhakika kutoka vyanzo vya michezo vyenye kuaminika,” aliongeza Nnunduma.
Akizungumza kwa niaba ya Klabu ya Simba,Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva alisema, “Tunaamini ubunifu huu bila shaka utawawezesha mashabiki wote wa Simba na wa soka kwa ujumla ambao pia ni wateja wa Tigo kupata habari mbalimbali za klabu ya Simba kupitia simu zao za mkononi”.
Tunawahimiza mashabiki wetu kujiunga na huduma hii kupitia Tigo ili waweze kupata nakufurahia habari mbalimbali kutoka klabu ya Simba. Aliendelea Aveva.
Akiongea katika tukio hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa shughuli za kibiashara na masoko katika klabu ya Simba, alisema “Tunatarajia kuendelea kuwapatia mashabiki wa Simba huduma za kisasa kwa kutumia teknolojia zisizokuwa na usumbufu wa aina yeyote kupitia wadau wanaoaminika ndani ya Tanzania”
Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa Premier Mobile Solutions, Bi Lulu Ramole alisema kuwa huduma hii imetengenezwa ili kuwawezesha wateja kupata habari za papo kwa papo naaliongeza kuwa huduma ipo katika mfumo wa vifurushi vya Combo / BUNDLE PACK ambapo wateja wa Tigo watakuwa wakilipia mara moja kwa siku na kupokea kiwango cha chini cha habari nne (04) na habari mpya za kila siku zina zohusu klabu ya Simba.
Huduma pia itamruhusu mteja aliyejiunga kujitoa kwenye huduma hii wakati wowote akitaka bila vikwazo vyovyote na pia kwenye huduma hii kutakuwepo na neon kuu “MSAADA”kwa ajili ya kusaidia juu ya maswali mbalimbali ya nayo ulizwa mara kwa mara na wateja wakati wakifurahia huduma.
Ili kujiunga na huduma hizi unatakiwa kutuma neon kuu SIMBA kwenda 15460. Utakapo jiunga tu mteja atapokea habari kutokana na neon analolituma kila siku na atatozwa kiasi cha shilingi za kitanzania 150 kwa siku. Na ili kujitoa kwenye huduma mteja atahitaji kutuma neno ONDOA SIMBA kwenda 15,460.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA JENGO JIPYA LA OFISI YA TTCL, PEMBA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya TTCL, wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Julai 3,2015 Wilayani Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo jipya la Ofisi ya TTCL, Wilayani Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba, leo.
 Baadhi ya wawakilishi wa makampuni na Mashirika waliohudhuria hafla hiyo, wakimsikiliza Makamu wa Rais.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kuhusu ramani ya Jengo hilo la TTCL, kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi ya 'Quality Buildin Contractors Ltd', Khamis Ally Shaibu,  wakati wa hafla fupi ya uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Jengo jipya la Ofisi ya TTCL,  iliyofanyika leo Wilayani Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba. Kulia kwa Makamu ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa.
Viewing all 110021 articles
Browse latest View live


Latest Images