Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 887 | 888 | (Page 889) | 890 | 891 | .... | 3284 | newer

  0 0

   Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa  na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini CGP John Casmir Minja  katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam Jumamosi, kuhudhuria Siku ya MAgereza na  kufunga mafunzo ya uofisa wa Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Jeshi hilo. Maafisa 104 wa kozi hiyo walihitimu mafunzo hayo na kuvishwa vyeo hivyo. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe.
   Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride liloandaliwa kwa ajili yake na wahitimu wa Mafunzo ya Uongozi wa Ngazi za Juu wa Jeshi la Magereza kabla ya kuyafunga mafunzo ya Cheo cha Mrakibu Msaidizi yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam. Rais Kikwete aliyafunga mafunzo hayo ambayo yalienda sambamba na Siku ya Magereza ambapo alikagua bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na jeshi hilo nchini.
   Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete akimvisha mhitimu Amina Lidenge, Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Magereza kwa niaba ya wenzake 104 waliomaliza mafunzo hayo katika Chuo cha Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam.
  Gwaride la Wahitimu wa mafunzo ya uofisa wa Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Jeshi hilo.
   Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Chikawe  na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini CGP John Casmir Minja wakiwa na Makamishna Jenerali wastaafu. Kutoka Kulia ni Augustine Nanyaro, Nicas Banzi, CGP John Minja, Rais Kikwete, Alhaj Jumanne Mangara, Simon Mwanguku, na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mathias Mathias Chikawe.

  0 0


  0 0

  IMG_4628
  Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida, akitoa maelezo ya kongamano kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kulifungua kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma ambalo liliandaliwa na taasisi yake.
  IMG_4729
  Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha, Ngosha Magonya akisoma hotuba ya ufunguzi wa kongamano hilo kwa niaba ya mgeni rasmi Katibu Mkuu wa wizara hiyo katika hoteli ya St. Gasper mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
  IMG_4678
  Mtaalamu wa masuala ya uchumi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo akitoa salamu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) wakati wa kongamano hilo la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.

  Afisa Mwandamizi wa uhamasishaji na uwekezaji kutoka kituo cha uwekezaji nchini (TIC), Lilian Mwamdanga akishiriki kuchangia maoni wakati kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA


  0 0

  DSC_0598
  Muonekano wa nje wa Banda la Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania lililopo ndani ya Karume Hall wanaoshiriki katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya sabasaba yaliyoanza kurindima jana kwenye katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

  Modewji blog team, Sabasaba
  Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania wapo katika maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyoanza kurindima mapema jana.

  UN Tanzania ambao wapo katika banda la Karume ndani ya mabanda hayo ya Sabasaba, kutoa elimu inayolenga kuionyesha jamii mafanikio, changamoto na fursa zilizopo katika Umoja wa Mataifa ambapo mwaka huu unafikisha miaka 70 tangu shirika hilo lianzishwe.

  “Huu ni mwaka muhimu sana kwani safari ya Umoja wa Mataifa ilianza mwaka 1945, hadi kufikia sasa kuwa umefikia wapi, tupo wapi na tunaelekea wapi katika kushughulikia changamoto za kidunia ikiwemo Amani na usalama, changamoto za maendeleo, changamoto za mabadiliko ya tabia nchi, na changamoto zingine”, alieleza Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama.

  Aidha, alibainisha kuwa, UN ambayo imeweza kufikisha miaka 15 ya malengo ya Milenia yaliyokubaliwa na nchi wanachama wa Umoja huo mwaka 2000, yanafikia kilele hapo Desemba 30, mwaka huu hivyo wakuu hao wanchi watakutana tena mwezi Septemba mwaka huu, kupanga malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) ambayo yatakapokubalika yataanza kutumika mwakani.


  0 0

  JAMII imeombwa kutoa msaada wa hali na mali kwa BI GRACE KAIZA mkazi wa Igoma jijini Mwanza ambaye ameomba mukatwa mguu wake kutokana na Saratani ( Kansa) katika mguu huo.

  Akizungumza na *JEMBE Habari* Bi. Grace Kaiza amesema amekuwa akisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda mrefu jambo lililomuathiri kwa kiasi kikubwa kiafya na hata kiuchumi.


  Akielezea namna tatizo hilo lilivyompata amesema lilianza kama uvimbe katika mguu wake kisha kufanyiwa upasuaji mara kadhaa lakini haikusaidia na ndipo alipobainika kuwa na ugonjwa huo.

  Kwa yeyote atakayeguswa na taarifa hii anaweza kuwasiliana na BI GRACE kwa ajili ya kumsaidia kupitia namba za simu 0768 264 182 

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la 
  Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi Mteule wa 
  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Kenya Mhe,John Michael Haule 
  alipofika Kujitambulisha Ikulu Mjini Zanzibar leo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
  Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Balozi Mteule wa
  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Kenya Mhe,John Michael Haule
  alipofika Kujitambulisha Ikulu Mjini Zanzibar leo.
    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
  Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Balozi Mteule wa Jamhuri 
  ya Muungano wa Tanzania Nchini Kenya Mhe,John Michael Haule baada ya 
  mazungumzo yao alipofika Kujitambulisha Ikulu Mjini Zanzibar
  leo,[Picha na Ikulu.]

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea akizungumza na wanamichezo (hawapo pichani) kabla ya kuanza fainali ya Kombe la Chikawe katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya Black Fire kutoka Kata ya Marambo na Timu ya Motisha kutoka Kata ya Kilimanihewa zilipambana na Timu ya Black Fire iliibuka mshindi kwa magoli 3 kwa 1. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
   Kapteni wa Timu ya Black Fire, Ally Njaidi (kulia) akipokea fedha taslimu Shilingi 500,000 pamoja na Kikombe cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema, baada ya kumalizika fainali ya Kombe la Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Timu hiyo iliirarua timu ya Motisha mabao 3 kwa 1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini NachingweaKushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salimu Mwalimu, naye alihudhuria fainali ya mashindano hayo ambayo yalianzishwa na Mbunge Chikawe jimboni humo kwa kushirikisha timu 178 katika jimbo hilo.
   Kapteni wa Timu ya Motisha,  Saidi Chakupewa (kulia) akipokea zawadi ya ushindi wa pili, kikombe na fedha taslimu Shilingi 200,000 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema, baada ya kumalizika fainali ya Kombe la Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Timu hiyo ilifungwa na Timu ya Black Fire mabao 3 kwa 1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini NachingweaKushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salimu Mwalimu, naye alihudhuria fainali ya mashindano hayo ambayo yalianzishwa na Mbunge Chikawe jimboni humo kwa kushirikisha timu 178 katika jimbo hilo.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe  (aliyevaa kofia) akiwa na wachezaji wa timu ya Black Fire ambao ndio waliibuka washindi. Kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe  (aliyevaa kofia) akiwa na wachezaji wa timu ya Motisha kutoka Kata ya Kilimanihewa. Kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.


  0 0


  ·        Wasanii kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia kunufaika na huduma hii.

  Abu Dhabi – Kampuni ya Clouds Media International leo imetangaza kuzindua huduma mpya ya kutafuta na kuwaunganisha wasanii kwenye nafasi za kutoa burudani kwenye matamasha na matukio mbalimbali.

  Kazi hiyo ya kuunganisha na kuwatafutia wasanii nafasi ya kutoa burudani itakuwa chini ya Status Bookings ambayo ni kampuni dada ya Clouds Media Group.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Clouds Media, Joseph Kusaga, uzinduzi wa huduma hii ni muendelezo wa kawaida wa kukua kwa kampuni yake.

  "Kwa kipindi cha miaka 15 iliyopita tumekuwa tukifanya kazi ya kuwatafuta na kuwapa nafasi ya kutoa burudani wasanii wakubwa kama Jay-Z, T.I., Ludacris, Rick Ross, T-Pain, Shaggy, Wayne Wonder, Fat Joe, Chaka Khan, Ja Rule pamoja na wasanii wakubwa wa Afrika kama P-Square, Iyanya, Diamond Platnumz, Davido, Waje, Vanessa Mdee, 2Face, Ali Kiba, Victoria Kimani, Avril na Patoranking kwa ajili ya tamasha letu la Fiesta, kwahiyo sasa ni wakati muafaka kutumia mahusiano mazuri tuliyonayo na wasanii pamoja na mameneja wao ili tuanzishe huduma hii kwenye maeneo ya masoko tunayoyahudumia," alisema Kusaga.

  Tamasha la Fiesta linaloandaliwa na Primetime Promotions ni moja ya tamasha kubwa zaidi Afrika na sasa linaingia mwaka wa 15 likiwa na wahudhuriaji zaidi ya 400,000 kwa mwaka.

  Huduma hii ya kutafuta na kuwaunganisha wasanii itakuwa inasimamiwa kutoka makao makuu ya Status Communications yaliyoko Abu Dhabi huku yakipata ushirikiano kutoka ofisi za Status zilizoko Dar es Salaam, Tanzania pamoja na Nairobi, Kenya.

  Huduma hii itawapa nafasi waandaji wa shughuli za burudani pamoja na makampuni mbalimbali kuwasiliana na kupata wasanii mbalimbali kutoka chanzo kinachoaminika.

  Afsa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni ya Status anasema huu ni wakati muafaka wa kuingia kwenye huduma ya kuunganisha na kuwatafuta wasanii nafasi ya kuburudisha.  


  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimkabidhi zawadi ya Ngao ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo wizarani humo. Zawadi hiyo ya kushtukiza iliandaliwa na viongozi hao wa Idara baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wao katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Lilian Mapfa. Picha zote  na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimkabidhi zawadi ya ua Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo wizarani humo. Zawadi hizo za kushtukiza ziliandaliwa na viongozi hao baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wao katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto), akimshukuru Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Lilian Mapfa, pamoja na Wakuu wa Idara wengine baada ya kupewa zawadi za kushtukiza na wakuu hao baada ya Katibu Mkuu huyo hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia), akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa wizara hiyo, Martina Nguluma pamoja na Wakuu wa Idara wengine baada ya kupewa zawadi za kushtukiza na watendaji hao baada ya Katibu Mkuu huyo hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wanne kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi (watatu kulia), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lilian Mapfa (katikati), Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Haji Janabi (wanne kulia), Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi, Manyama Mapesi (watatu kushoto), Mkurugenzi wa Huduma za Sheria, Marlin Komba (kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Jane Massawe (wapili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu, Edwin Makene (wapili kulia) na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Christina Mwangosi. Wakuu wa Idara wa wizara hiyo walimpa zawadi ya kushtukiza Katibu Mkuu wao baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I).


  0 0


   
  STATE HOUSE ZANZIBAR
  OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
  PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                                                                           29.06.2015

  RAIS  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Kenya na Tanzania ni nchi zenye uhusiano wa muda mrefu hivyo kuna kila sababu za kuendelea kuimarisha na kuitekeleza Sera ya Demokrasia ya Uchumi  kwa manufaa ya pande mbili hizo.

  Dk. Shein aliyasema hayo leo, huko Ikulu mjini Zanzibar wakati alipofanya mazungumzo na Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya Mhe. John Michael Haule, ambaye alifika Ikulu kwa ajili ya kuaga na kupata baraka za Rais.

  Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi Haule  kuwa kwa vile Kenya na Tanzania zimo katika mchakato wa kutekeleza Sera ya Demokrasia ya Uchumi ana matumani makubwa kuwa mafanikio makubwa ya kiuchumi yataendela kupatikana baina nchi mbili hizo.

  Dk. Shein alisema kuwa mashirikiano katika nyanja mbali mbali za maendeleo hasa ikizingatiwa nchi mbili hizo zimo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki yamekuwa yakiimarika siku hadi siku.

  Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa nchi mbili hizo zimekuwa na historia ya kusaidiana pale nchi moja wapo inapopata matatizo, hivyo ana imani kubwa na Balozi Haule kuwa ataendeleza uhusiano na ushirikiano huo kati ya nchi mbili hizo kutokana na utendaji wake wa kazi.

  Kwa upande wa Zanzibar, Dk. Shein alimueleza Balozi Haule kuwa kumekuwa na uhusiano wa kidugu na kihistoria kati ya nchi hiyo na Zanzibar hasa ikizingatiwa uhusiano kati ya Zanzibar na Mombasa katika nyakati za ukoloni hatua ambayo imepelekea kuimarika kwa uhusiano huo hadi hii leo na kuweza kuwepo kwa Ubalozi Mdogo huko mjini Mombasa.

  Dk. Shein alisema kuwa hivi sasa Kenya na Zanzibar kumekuwa na uhusiano na ushirikiano mzuri wa kibiashara hasa katika zao la karafuu, ambapo wafanyabiashara wa nchi hiyo wamekuwa wakinunua karafuu kupitia Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC).

  Alisema kuwa hatua hiyo imeweza kuondosha tatizo lililokuwepo hapo siku za nyuma ambapo biashara hiyo ilikuwa ikifanywa kimagendo  na baadhi ya watu kati ya Kenya na Zanzibar na kuikosesha Zanzibar kuimarisha pato lake la uchumi.

  Pamoja na hayo, Dk. Shein alitumia fursa hiyo kumueleza Balozi Haule haja ya kulitangaza soko la Utalii nchini Kenya kwani nchi hiyo nayo imeweza kupata mafanikio katika sekta hiyo.

  Nae Balozi Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya Mhe. John Michael Haule alimuahidi Dk. Shein kuwa katika utekelezaji wa Kazi zake nchini humo atazidi kujenga uhusiano na kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Kenya.

  Balozi Haule alieleza kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini humo utaimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati katika kuhakikisha Sera ya Demokrasia ya Uchumi kati ya pande mbili hizo inaimarishwa.

  Katika mazungumzo yake Balozi huyo, alisisitiza haja ya kuimarisha ulinzi katika maeneo ya Utalii hapa nchini sambamba na kuimarishwa kwa usafiri kati ya Kenya na Tanzania ikiwemo Zanzibar ili kutoa usafiri wa uhakika kwa wageni wanaotembelea vivutio vya kitalii vilivyopo katika maeneo hayo.

  Aidha, Balozi huyo aliahidi kuendeleza uhusiano na ushirikiano katika nyanja ya uwekezaji na biashara hasa ikizingatiwa kuwa katika nchi za Afrika ya Mashariki nchi ya Kenya inaongoza kwa wawekezaji na wafanyabiashara wake kuekeza hapa Tanzania.

  Pamoja na hayo,  mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha mambo mbali mbali ya kimaendeleo yakiwemo ya kiuchumi kati ya Kenya na Tanzania.

  Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
  Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
   E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

  0 0


  0 0

  WAKAZI wa Mkoa wa Kigoma, wameiomba Kampuni ya Msama Promotions kuwapelekea uzinduzi wa albamu tatu za mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili nchini Boniface Mwaitege.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amepokea maombi mengi kwa wakazi wa mkoa huo wakihitaji uzinduzi huo ufanyike mkoani kwao.

  “Nimepokea maombi ya wakazi wa Kigoma wakihitaji uzinduzi wa muimbaji nguli, Bonny Mwaitege ambaye anatarajia kuzindua albamu tatu,” alisema Msama.

  Msama alisema mbali ya Kigoma mikoa mingine imeonesha nia ya kutaka uzinduzi huo ufanyike mikoani kwao. Alisema  wakazi wa Kigoma wanatamani kumuona akifanya onyesho mkoani humo kwa kuwa ni moja ya waimbaji ambao wamekuwa wakiwashuhudia wakifanya makubwa jukwaani.

  Aidha Msama alisema kuwa kujitokeza kwa baadhi ya wananchi wa mikoa mbali hiyo kuomba, inampa moyo kuona watu wamemgeukia Mungu na kutaka kupata neno kutoka kwa waimbaji wa muziki wa injili ambako alisistiza kuwa  yuko pamoja nao na atajitahidi.

  Mwimbaji huyu machachari ambaye anatamba na nyimbo mbalimbali kama Mama ni mama, Mke mwema, Wakusamehe, fungua moyo wako na njoo uombewe na Yesu yupo anatarajia kuzindua albamu hizo tatu Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Msama alisema kuwa Kamati ya Maandalizi itaketi na kujadili kwa sababu ni mikoa mingi iliyoomba kupelekewa uzinduzi huo hivyo ni jambo la kujipanga kuona namna itakavyoweza kufanya na kuwafikia katika mikoa yao.

  0 0

  WAJASIRIAMALI wanawake nchini wametakiwa kuwa na moyo wa uthubutu ili kupiga hatua ya maisha na kiuchumi badala ya kuwa waoga.

  Mwito huo umetolewa na Mratibu wa Kongamano la Jumuia ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, Julieti Mjale wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden Dar es Salaam jana.

  "Uthubutu katika jambo lolote ni muhimu kwani unamfanya muhusika kupiga hatua ya maendeleo" alisema Mjale

  Alisema wajasiriamali waliowengi wamekuwa na mipango mizuri ya kubuni biashara fulani lakini wanakuwa na hofu ya kupoteza fedha zao na hiyo inatokana na kushindwa kuthubutu au kuchukua maamuzi magumu ya kuanza kufanya biashara waliyoikusudia.

  Akijitolea mfano yeye alisema alithubutu kwa kuanza kufanya biashara za chini lakini leo hii ana nyumba za kupangisha na kufikia hatua ya kufanya biashara za kwenda nje ya nchi na kuandaa makongamana ya namna hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya biashara.

  Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Haika Lawere alisema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wajasiriamali wanawake ili kupeana uzoefu wa biashara na kujua changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kupanua wigo wa shughuli zao na kutafuta masoko mapya ya bidhaa zao.

  Katibu wa Jumuia hiyo, Hilda Ngaja, alisema changamoto kubwa waliyonayo wajasiriamali wanawake ni kutokuwa na uelewa mkubwa wa kufanyabiashara zao na kujikuta wakirudi nyuma kimaendeleo na ndio maana wamekuwa wakitumia fursa za semina na makongamano kwa ajili ya kuelimishana.
    Wadau mbalimbali wakitizama bidhaa mbalimbali katika Kongamano hilo.
   Mwenyekiti wa Tanzania Business Entrepreneurs for Women,  Haika Lawere akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Guarden Dar es Salaam.
   Wadau wa kongamano hilo wakiwa wamejipanga kisawasawa. Kutoka Kulia ni Getrude Kilyabusebu, Haika Lawere, Hilda Mgaja na  Julieth Mjale.
   Mwezeshaji wa Kongamano hilo, James Mwang'amba 
  akitoa mada.
   Muwezeshaji wa kongamano hilo, Chriss Rupia (kulia), akitoa maelezo juu ya namna ya kuanzisha Kampuni na hatua mbalimbali ambazo mtu anatakiwa azifuata wakati wa kufungua kampuni hasa binafsi.


  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Fikiri Juma, pindi alipowasili kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Morogoro, leo Juni 29, 2015 kwa ajili ya kukabidhiwa orodha ya majina ya WanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalageris. Mh. Lowassa amehitimisha zoezi hilo la kutafura Wadhamini, leo Juni 29, 2015 katika Mkoa wa Morogoro na amedhaminiwa na WanaCCM 104,038.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea orodha ya majina ya WanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015, kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Kulwa Mironge, leo Juni 29, 2015. Mh. Lowassa amehitimisha zoezi hilo la kutafura Wadhamini, leo Juni 29, 2015 katika Mkoa wa Morogoro na amedhaminiwa na WanaCCM 104,038.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akionyesha fomu yenye orodha ya majina ya wanaCCM waliomdhamini, kwa kadamnasi iliyokuwepo kwenye Uwanja wa CCM Mkoa wa Morogoro, leo Juni 29, 2015, baada ya kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Kulwa Mironge.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akizungumza machache na kutoa shukrani kwa WanaCCM waliomdhanini ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania, kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.  0 0
 • 06/29/15--12:26: HOJA YA HAJA TOKA KWA MDAU
 • Ankal pole na hongera kwa kazi nzuri ya kutupatia taarifa mbali mbali zinazo tuhusu watanzania, napenda kutumia nafasi hii kuomba serikali ya Mh Rais Kikwete iliyopewa dhamana na watanzania kuwaonea huruma watanzania kwakuwapunguzia mzigo mzito wa malipo ya kuingia kwenye maonesho ya SABASABA. 

  Nimeenda kwenye maonesho hayo lakini nilichoshuhudia jana nikwamba maonesho hayo yamewalenga wenye kipato cha juu tu na si watanzania wakawaida asilani, kwa sababu inashangaza sana kwa serikali kuwakabidhi kampuni ya Maxmalipo kukusanya viingilio tena kwa gharama ya juu sana, Usumbufu mwingine ambao kwakweli auvumiliki, ni kwamba hawa MaxMalipo wanatoza maegesho ya magari kw ash elfu 10, tena wanawafuata hata walio paki nje ya eneo la sabasaba, nakuwalazimisha watu walipia elfu 10 najiuliza hivi hawa wameingia mkataba wakufanya haya na nani asie na huruma na watanzania wenye kipato cha chini?

  Nimeshuhudia mzozo mkubwa pale eneo la Jeshini karibu na ATM ya NMB, mteja kaja kutoa pesa kisha wakamlazimisha alipe Tsh elfu 10 kwakuwa ameegesha gari pale, hivi serikali kweli imejiuza kwa hawa MaxMalipo kiasi hicho??? Kwanini mliokabidhiwa mamlaka mnatufanyia hivi walalahoi? Kwanini mnatufanya tushindwe kuingia sabasaba? Mtu huyu anaenda na gari lake tena apaki viwanja vya sabasaba, mnamlazimisha kulipa eflu kumi, kisha alipie elfu 4 getini, mnatutendea haki???? Isitoshe hao vijana wa MAXMALIPO wanakuli mbaya na kuonesha ubabe tena eneo la Jeshi, na nilimsikia mdada mmoja Mjeshi MP aliekuwa zamu mida ya saa nane nane mchana akimlazimisha mtu awalipe MaxMalipo Elfu 10 kwakuwa wanauwalali wakulipwa tozo ya kupaki pale jeshini, hii haikukaa sawa hata kidogo.

  Nashauri, Serilika ya Mkoa wa Dar es Salaam, Wizara husika, Jeshi la Wananchi na Mh Rais na CCM chama kilicho iweka serikali Madarakani  kuingilia kati suala hili haraka iwezekanavyo, ili kuiepusha serikali kupata sifa mbaya mbele ya wananchi, haiwezekani kukawa na taratibu zisizofaa zinazo wakwaza wananchi wakipato cha chini kuingia kwenye maonesho ya SABASABA, kwanini serikali isidhibiti mapato pale mlangoni au kwenye maegesho kuliko kuingia ubia na mnadu anaeongeza garama zisizo na sababu kwa sisi walalahoi.

  Nimatumaini yangu kuwa Serikali hii sikivu ilationa hili na kuwashauri kwa busara walio fanya maamuzi haya ya kumkandamiza mtanzania mwenye shahuku alieituza mwaka mzima ya kwenda Sabasaba kuachana maramoja na msimamo waho huo, maana huko ni nikuendelea kuitengenezea uhasama serikali na wananchi wake hasa tunapoelekea Uchaguzi mkuu.

  Ni mimi Mdau wa maonesho ya SABASABA.

  0 0

  Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa vya hospitali kwaajili ya zahanati ya chuo kikuu cha Dodoma vyenye thamani ya Shilingi milioni 20.

  Vifaa hivyo vilivyotolewa kwa Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dodoma – Prof Shaaban Mlacha ni pamoja na - Jokofu kwaajili ya benki ya Damu, Meza ya upasuaji (Operating Table), Taa maalumu za kwenye chumba cha upasuaji (Overhead Operating Lamp) vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 20.

  Msaada huo ulipokelewa vyema na uongozi wa chuo kikuu cha Dodoma kusifu juhudi za benki ya NMB katika kuchangia maendeleo nchini.
  Afisa Mkuu wa Idara ya Wateja wa Jumla na Serikali wa NMB – Richard Makungwa akikabidhi taa maalumu za chumba cha upasuaji kwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma – Prof Shaaban Mlacha kwaajili ya zahanati ya chuo kikuu cha Dodoma. Pamoja na taa hizo, NMB pia ilikabidhi Jokofu la kutunzia damu ( Blood Bank), meza ya upasuaji ( Operating table) vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 20. NMB ilikabidhi vifaa hivyo ikiwa ni mchango wake kwa jumuia ya chuo kikuu cha Dodoma ili kuinua kiwango cha huduma zinazotolewa na zahanati hiyo.
  Afisa Mkuu wa Idara ya Wateja wa Jumla na Serikali wa NMB – Richard Makungwa akikabidhi meza ya upasuaji (Operating table) kwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof Shaaban Mlacha kwaajili ya zahanati ya chuo kikuu cha Dodoma. Pamoja na taa hizo, NMB pia ilikabidhi Jokofu la kutunzia damu ( Blood Bank), meza ya upasuaji ( Operating table) vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 20. NMB ilikabidhi vifaa hivyo ikiwa ni mchango wake kwa jumuia ya chuo kikuu cha Dodoma ili kuinua kiwango cha huduma zinazotolewa katika zahanati hiyo.
  Wafanyakazi wa NMB kanda ya Kati wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya vifaa vya hospitali vilivyotolewa na NMB kwaajili ya zahanati ya chuo kikuu cha Dodoma. Katika kuhakikisha huduma za zahanati ya chuo kikuu cha Dodoma zinaboreshwa, NMB ilimkabidhi Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma – Prof Shaban Mlancha taa maalumu za kufanyia upasuaji (overhead lamp) Jokofu la kutunzia damu ( Blood Bank), meza ya upasuaji ( Operating table) vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 20.


  0 0

  Mkuu wa Idara ya Kiswahili ya Radio Deutsche WELLE Bi. Andrea Schmidt akimshukuru Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya baada kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Jumuiya ya Ulaya ofisini kwake Bonn.

  0 0

   Mhariri wa Gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu (kushoto), na waombolezaji wengine wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mke wa mwanahabari wa Kampuni ya The Guardian, Thobias Mwanakatwe, Levina Genda wakati wakilipekeka kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda Karatu mkoani Manyara kwa mazishi yatakayofanyika kesho.
  Mwanahabari wa Kampuni ya The Guardin Ltd, Thobias Mwanakatwe akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa mke wake, Levina Genda wakati wa ibada ya kumuaga iliyofanyika Hospatali ya Amana Dar es Salaam leo a. Mke wa Mwanakatwe alifariki kwa kugongwa na gari maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mwishoni mwa wiki.
   Waombolezaji wakiwa kwenye ibada ya kumuaga Levina Genda, iliyofanyika Hospitali ya Amana Ilala Dar es Salaam leo asubuhi.


  0 0

  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya mmiliki wa shule ya Mtakatifu Zion iliyopo  maeneo ya Ununio, Mbezi Beach wilaya ya kipolisi Kawe mkoa wa kipolisi wa Kinondoni aliyejulikana kwa jina la ANNA D/O MIZINGI, Miaka 48, Mfanyabiashara, Mkazi wa Boko.

  Mnamo tarehe 02/02/2015 majira ya saa za mchana mtoa taarifa alifika kituo cha Polisi na kueleza kwamba marehemu ANNA D/O MIZINGI aliondoka tangu tarehe 26/12/2014 majira ya saa 1:00hrs akiwa na mmoja wa watuhumiwa wakitumia gari dogo aina ya Toyota Verosa ambayo namba zake hazikufahamika mara moja iliyokuwa inamilikiwa na marehemu na tangu wakati huo hakuwa ameonekana tena.

  Kutokana na taarifa hizo Jeshi la Polisi lilifungua jalada la uchunguzi na kuanza uchunguzi mara moja. Wakati uchunguzi ukiendelea zilipatikana taarifa zilizosaidia kukamatwa kwa watuhumiwa hao huko Uchira Miwaleni, Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

  Watuhumiwa walipokamatwa na kuhojiwa mtuhumiwa mmoja kati ya hao watatu amekiri na kutoa maelezo kuwa siku ya tukio aliondoka na marehemu kuelekea katika shule ya Mt. Zion. Kwamba walipofika shuleni hapo walivamiwa na watu wapatao wanne na kuanza kupigwa lakini yeye alifanikiwa kutoroka na kujificha katika uzio wa shule hiyo. Amesema akiwa katika uzio huo aliwaona watu hao wakiendelea kumpiga marehemu ANNA D/O MIZINGI na kisha kumtupa katika shimo la choo. Baada ya kitendo hicho watu waliotenda uhalifu huo waliondoka na gari la marehemu na kutokomea kusikojulikana. 

  Tarehe 22/06/2015 mabaki ya mwili wa marehemu ANNA D/O MIZINGI yalipatikana eneo la Ununio baada ya Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Zima moto kubomoa shimo la choo cha shule hiyo.

  Watuhumiwa waliokamatwa ni hawa wafuatao:
  1.DANIEL S/O RANADHANI MKILINDI @ ABDALLA @ DULLA, Miaka 25, Mganga wa kienyeji, Mkazi wa Uchira Moshi – Kilimanjaro.

  2.SAID S/O RASHID OMARY @ SAID NTIMIZI au DUVII, Miaka 34, Mfanyabiashara, Mkazi wa Mbweni JKT.

  3.ERICK S/O MZIRAY, Miaka 40, Mfanyabiashara, Mkazi wa Kurasini.

  Watuhumiwa hawa wanaendelea kuhojiwa ili kupata undani wa tukio hili ikiwa ni pamoja na kuwatafuta na kuwakamata watuhumiwa wengine wanaohusiana na tukio hili. 
  Mara baada ya uchunguzi kukamilika jalada la shauri hili litapelekwa kwa mwanasheria wa serikali kwa hatua zake za kisheria.

  S. H. KOVA
  KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
  DAR ES SALAAM


  0 0


older | 1 | .... | 887 | 888 | (Page 889) | 890 | 891 | .... | 3284 | newer