Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 888 | 889 | (Page 890) | 891 | 892 | .... | 3286 | newer

  0 0


   Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabani (kulia) akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (katikati), kwa waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani humo jana, wakati waumini hao walipomwita kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi. Kushoto ni Diwani wa Kwadelo, Alhaj Omary Kariati.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza na waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma jana, wakati waumini hao, walipomwita kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumza na waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma jana, wakati waumini hao
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiagana na  waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma jana, wakati waumini hao walipomwita kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi. Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabani. 
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (wa pili kushoto) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu Shabani (kushoto), wakishiriki katika chakula cha usiku kilichoandaliwa na waumini wa Msikiti wa Gaddafi mkoani Dodoma jana, wakati walipomwita kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi. 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akiagana na viongozi wa dini ya kiislam mkoa wa Dodoma jana,  wakati waumini wa Msikiti wa Gaddafi, walipomwita kwa ajili ya kumshukuru kutokana na jitihada zake katika kuwezesha ujenzi wa msikiti huo uliojengwa kwa ufadhili wa aliyekuwa Kiongozi wa Libya, marehemu Muammar Gaddafi. Picha na John Badi

  0 0
  0 0

  Wabongo in ‪#‎HOUSTON‬ This one is for you. ‪#‎AllWhitePartyUSATour‬ /‪#‎OldSkoolParty‬ #HOUSTON TX. Hosted by the One & Only Zey MisstangaOn JULY 18th 2015 (Possible EID EL FITR NIGHT). Check Details at "MoFLAVA ALL WHITE PARTY HOUSTON TX SAT JULY 18TH" @Pure 505 Main St. Downtown Houston. 

  To buy V.I.P/SECTION/BOOTH or REGULAR Advance Tickets (In Reduced Price) go HERE http://houstonwhite.eventbrite.com/?s=40265011. You have Seen Other Cities Tour Turn Up! Now Lets See what Yall got Over them. MFUNGO MWEMA NA KARIBUNI WOTE HOUSTON TX ON THE 18TH JULY.

  0 0


  0 0


  0 0

   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya juu ya Daraja la Kariakoo katika eneo la Ruvu Chini katika barabara ya Bagamoyo-Msata
   Sehemu ya Daraja la Kariakoo katika eneo la Ruvu chini katika mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Bagamoyo-Msata ukiendelea kujengwa.


   Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akikagua sehemu ya chini ya daraja la Kariakoo.

   Mkandarasi wa Barabara ya Bagamoyo-Msata kushoto  akitoa maelezo ya Mradi wa Madaraja katika eneo la Ruvu Chini Mkoani Pwani huku Waziri wa Ujenzi Dkt. Magufuli akimsilikiza kwa makini.

  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akishuka ngazi mara baada ya kufanya ukaguzi wa Daraja la Kariakoo  katika barabara ya Bagamoyo-Msata mkoani Pwani.
  Picha kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano  Serikalini-Wizara ya Ujenzi


  0 0  0 0  0 0

  Balozi wa Japani nchini, Masaharu Yoshida( katikati) akikata utepe kuzindua gari la maalumu litakalotumika na kikosi cha usalama barabarani katika shughuli za uelimishaji, (kushoto) ni Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani, Naibu kamishina wa Polisi(DCP) Mohamed Mpinga ( kulia )ni Msaidizi wa balozi, Bw Kazioshi. 

  0 0

   MKUU wa wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Glorious Luoga, (Katikati), akinyanyua juu mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 800, baada ya kukabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampouni ya Acacia, Brad Gordon, (kushoto), katika hafla fupi iliyofanyika kwenye lango la kushukia kutyoka kilele cha  Mlima Kilimanjaro, Mweka, Juni 28, 2015.
    Fedha hizo ambazo ni kwa ajili ya kusaidia sekta ya eli kwa watoto kutoka familia duni, zimetokana na wafanyakazi wa Acacia na familia zao pamoja na marafiki, kupanda Mlima Kilimanjaro kwa nia ya kuchangisha fedha chini ya mpango wa kampuni hiyo wa "CanEducate".

  0 0

   Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Angela Kairuki ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa ‘Viongozi Wanawake Vijana Wanaochipukia’ uliondaliwa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Mfuko wa Wanawake Tanzania mapema leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulilenga kuzungumzia suala la wanawake na uongozi, na namna ya kutatua changamoto wanazozipata katika kufanikisha ndoto zao za kiuongozi katika sekta mbali mbali nchini.

   Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI Institute Prof. Joseph Semboja akitoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa ‘Viongozi Wanawake Vijana Wanaochipukia’ uliondaliwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Mfuko wa Wanawake Tanzania mapema leo jijini Dar es Salaam.
   Mbunge wa Viti Maalum ambaye pia ni Rais wa VICOBA Mh. Devota Likokola akichangia katika mjadala uliohusu wanawake na changamoto zao wanazozipitia katika kufanikiwa kutimiza ndoto zao, na namna ambavyo wanaweza kupita changamoto hizo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania Bi. Mary Rusimbi (kushoto) akichangia akiendesha mjadala wakati wa mkutano wa ‘Viongozi Wanawake Vijana Wanaochipukia’ uliondaliwa na taasisi hiyo kwa kushirikiana na Mfuko wa Wanawake Tanzania mapema leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano wa ‘Viongozi Wanawake Vijana Wanaochipukia’ katika picha ya pamoja. Walioketi kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Anna Maembe, Mhadhiri wa wa MUHAS Dk. Ave-Maria Semakafu, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Mh. Eusebia Munuo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania Bi. Mary Rusimbi na Mbunge wa Viti Maalum ambaye pia ni Rais wa VICOBA Mh. Devota Likokola.

  0 0

   Mgeni rasmi katika mchezo wa robo fainali ya Netiboli kati ya Mtwara dhidi ya Mwanza Bibi Odilio Mushi ambaye pia ni Afisa Elimu Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI akitoa nasaha kwa wanamichezo hao mara baada ya kuzikagua timu zao  katika viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Butimba, Mwanza.
   Waamuzi wa mchezo wa riadha wanaoshiriki katika mashindano ya UMITASHUMTA wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufanyika kwa fainali ya mbio za mita 400 yanayoendelea katika viwanja vya Chuo cha Ualimu cha Butimba, Mwanza.
  -------------------------------------------------
  Matokeo ya mpira wa miguu kwa wavulana yanaonyesha kuwa Ruvuma na Katavi  zilitoka sare ya 1-1, Tanga walifungwa na Rukwa  2-1, huku Kilimanjaro ilitoka sare ya 1-1 na Tabora. Pia Shinyanga iliifunga pwani 1-0, Kigoma iliifunga Iringa mabao 2-0 huku Mbeya ikaibamiza Manyara 4-0.

  Matokeo ya mpira wa wavu kwa wavulana yanaonyesha kuwaMtwara ilishinda Mara kwa seti 2-0, Mwanza ikaichapa Shinyanga seti 2-0, Manyara ikaishinda Tabora seti 2-0, na Ruvuma ikaichabanga Kilimanjaro seti 2-0.

  Kwa upande wa wasichana Tanga ikaifunga Shinyanga seti 2-0, Mtwara iliichabanga Manyara seti 2-0, Kigoma iliifunga Singida seti 2-0 na Katavi iliilaza Simiyu seti 2-0.

  Katika mpira wa mikono kwa wavulana Rukwa iliichapa Manyara mabao 15-10, Dar es salaam iliichapa na Tabora mabao 31-11, Singida ilifungwa na Mwanza mabao 20-5, ma Morogoro iliifunga Kigoma  mabao 15-8.

  Katika mchezo wa mpira wa mikono wasichana, Geita iliichapa Tabora mabao 24-6, Pwani iliifunga Iringa mabao 7-5, huku timu za Mbeya na Lindi zilitoka sare mabao 11-11m na Tanga iliichabanga Manyara mabao 11-2.

  Kwa upande wa mpira wa Netiboli, Arusha iliifungaSimiyu mabao 29-13,  Katavi ilifungwa na Morogoro mabao 36-18, Mbeya iliichakaza Manyara mabao 31-16, Dodoma iliifunga Singida mabao 21-12 na Lindi iliilaza Kigoma mabao 38-36.

  Matokeo ya mpira wa kengele kwa wavulana yanaonyesha Mtwara iliifunga Mbeya mabao 11-3, Kilimanjaro iliifunga Singida mabao 8-5, Dodoma ilifungwa na Kagera mabao 9-11 na Manyara iliifunga Tabora mabao 5-2.


  Kwa upande wa mpira wa kengele wasichana Kilimanjaro iliifunga Singida mabao 10-3 na Kagera iliilaza Tabora mabao 9-4.  0 0  0 0

   Jana tarehe 29 Juni 2015, Mamlaka ya Bandari Tanzania imefungua rasmi Ofisi nchini Zambia. Ofisi hizo zimefunguliwa katika Jiji la Lusaka. 
   Dhumuni kubwa la Mamlaka ya Bandari kufungua ofisi hii Lusaka ni kutokana na kuwepo malalamiko kwa upande wa Zambia ambaye ni mteja wake mkubwa ya kuwepo ukiritimba wa utoaji wa mizigo yao bandarini Dar es salaam. 
  Hivyo Mamlaka ikaona ni vema kuja kufungua ofisi jijini  Lusaka ili kutatua tatizo hilo. 
   Sherehe za ufunguzi wa ofisi hii ulihudhuriwa na Mhe Dkt. Charles Tizeba Naibu Waziri wa Uchukuzi na viongozi waandamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania. 
  Ofisi za Mamlaka ya Bandari zipo katika Jengo la Ubalozi wa Tanzania Lusaka Zambia. Ofisi hii imefunguliwa rasmi na Waziri wa Uchukuzi wa Zambia Mhe Yamfwa Dingle Mukanga.
   KAIMU MKURUGENZI MKUU WA TPA  BW A. MASSAWE AKITOA HOTUBA WAKATI WA UFUNGUZI

   VIONGOZI WAANDAMIZI WAKIMSILIKIZA MHE. BALOZI AKITOA HOTUBA

   MHE GRACE J. MUJUMA BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA AKITOA HOTUBA WAKATI WA SHEREHE ZA UFUNGUZI


   MHE BALOZI NA MHE NAIBU WAZIRI WAKIKAGUA OFISI YA TPA NCHINI ZAMBIA KABLA YA UFUNGUZI

  BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA MHE. BALOZI GRACE J. MUJUMA AKIWA NA MHE. NAIBU WAZIRI CHARLES TIZEBA UBALOZINI. MHE. TIZEBA ALIKWENDA KUMSALIMIA MHE. BALOZI OFISINI KWAKE.


  0 0

  Msomaji wa Maoni hayo Mhe. Mohamed Habib J. Mnyaa (Mb) K.n.y Msemaji Mkuu-Kambi Rasmi ya Upinzani, Wizara ya Fedha 29.06.2015.

  0 0

  Msomaji wa Maoni hayo Mhe. David Ernest Silinde (Mb) K.n.y Waziri Kivuli- Wizara ya Fedha 29.06.2015

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipunga mkono kwa umati wa watu wakazi wa Mji wa Dumila, Mkoani Morogoro, waliomsimamisha ili awasalimie wakati alipokuwa safarini kuelekea Mkoano Dodoma, leo Juni 30, 2015. Mh. Lowassa anatarajia kurudisha fomu ya kuomba ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania, kesho Julai 1, 2015.PICHA NA OTHMAN MICHUZI.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wanaCCM wa Mji wa Dumila, Mkoani Morogoro, waliomsimamisha wakati alipokuwa safarini kuelekea Mkoano Dodoma, leo Juni 30, 2015.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Ofisini kwake, Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya TBEA, Zhong Yanmin, wakati alipofika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 30, 2015 kwa mazungumzo 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya TBEA, Zhong Yanmin, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya TBEA, uliofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 30 2015 kwa ajili ya mazungumzo
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kampuni  ya TBEA, Zhon Yanmin (kulia) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Juni 30, 2015. Kushoto ni Mkarimani wa Makamu Mwenyekiti huyo
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na Ujumbe wa Kampuni ya TBEA, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwake Ikulu  jijini Dar es Salaam, leo Juni 30, 2015. Picha na OMR

  0 0

  Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kuondoka nchini siku ya alhamis kuelekea nchini Uganda kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaofanyika siku ya jumamosi nchini humo.

  Mchezo huo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN 2017 zitakazofanyika nchini Rwanda utachezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Nakivubo jijini Kampala kuanzia majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

  Kocha mkuu wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa amesema kikosi chake kinaendelea vizuri na maandalizi ya mchezo huo utakaochezwa mwishoni mwa juma nchini Uganda.

  “Wachezaji wote waliopo kambini wanaendelea na mazoezi, vijana wanajituma mazoezin, morali ni ya hali ya juu naamini tutafanya vizuri katika mchezo wetu wa siku ya jumamosi” alisem Mkwasa.

  Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya alhamisi jioni kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda (Rwanda Air) ikiwa na kikosi cha wachezaji 20, benchi la ufundi pamoja na viongozi.

  Aidha Mkwasa amesema ataongea na waandishi wa habari siku ya alhamis asubuhi saa 5 kamili - Karume juu ya maandalizi ya kikosi chake kuelekea kwenye mchezo wa marudiano na kuweka wazi kikosi kitakachosafiri kuelekea nchini Uganda.

  Stars imeweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo na inafanya mazoezi katika uwanja wa Boko Veterani kila siku jioni kuanzia majira ya saa 10 jioni.


  0 0

   Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhavi fomu za kuwania Uteuzi wa CCM wa kugombea urais kwenye Ofisi Kuu ya CCM mjini DOdoma leo
  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizunguza na waandishi wa habari  baada ya kurejesha fomu za kuwania Uteuzi wa CCM wa kugombea urais kwenye Ofisi Kuu ya CCM mjini Dodoma leo Juni 30, 2015.Wapili kulia ni mkewe Tunu na kulia ni mjukuu, michele (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

older | 1 | .... | 888 | 889 | (Page 890) | 891 | 892 | .... | 3286 | newer