Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 886 | 887 | (Page 888) | 889 | 890 | .... | 3286 | newer

  0 0  Kwa mara nyingine tena Yule msanii machachari ambaye anainukia kwa kasi katika muziki wa bongofleva  Boniface( a.k.a handsome boy a.k.a asali ya Morogoro   a.k.a bon-to-face)  kwa mara nyingine tena ameachia wimbo na video yake mpya iitwayo  “Nikitaka”
  Audio ya wimbo huo umefanyika katika studio  za Authentic Record jijini Dar es salaam chini ya Producer mwenye kiwango za hali ya juu Mr. Allan Mapigo
  Video ya wimbo huu imefanywa kampuni mpya kabisa shine studioz, ni moja ya kazi safi kabisa chini ya Director matata kabisa  Ivan
  Boniface ni miongoni mwa wasanii  wenye sauti nzuri na  kujituma kwenye muziki, takribani ameshatoa nyimbo kadhaa siku za nyuma ambazo zimefanya vizuri sana nje ya nchi, 
  Aidha,  kwa sasa Boniface ameweka wazi kuwa hana meneja au msimamizi wa shughuli zake za muziki, kwahiyo milango ipo wazi kwa yeyote ambaye yupo tayari kufanya nae kazi za  muziki kwa ujumla.

  Wimbo                   :         Nikitaka
  Msanii                             :         Boniface (Bon-To-Face)
  Studio                   :         Authentic Records
  Producer                :         Allan Mapigo

  Mawasiliano::
  Simu            :         +255 716 542640
  Facebook     :         bonyface.mateza@yahoo.com
  Instagram    ;         bon-2-faceBONIFACE - NIKITAKA (Offial Video music)

  0 0


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika  Jumamosi  kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
  Mama Salma  Kikwete akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika  Jumamosi  kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, marehemu Donald Kelvin Max, wakati wa shughuli za kuaga mwili zilizofanyika leo Juni 27, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.


   Rais Jakaya Kikwete, mkewe Mama Salma, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Geita, marehemu Donald Kelvin Max.
  Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiifariji familia ya marehemu
   Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Max, wakati wa  shughuli za kuaga mwili. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA  0 0

  Contact: +2550719786099
  Uza,Nunua- Smart Phone,Tablets,Smart Watches, Head Phones, memory cards, tablets na kifaa kingine Kwenye SMART GULIO

  0 0

   Mke wa Thobias Mwanakatwe, Levina Michael Genda, 
  enzi za uhai wake.
  Mwanahabari Thobias Mwanakatwe, \
  akiwa na mke wake enzi za uhai wake.

  Dotto Mwaibale

  MWANAHABARI wa Kampuni ya The Guardian na Nipashe, Thobias Mwanakatwe, amepoteza mke wake baada ya kugongwa na gari eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana usiku majira ya saa 2:30.
  Akizungumza na mtandao wa www.habari za jamii.com. Mwanakatwe amesema kifo cha ghafla cha mke wake ni pigo kubwa kwake na familia zote mbili.
  Mwanakatwe amesema shughuli za kuuaga mwili wa marehemu zitafanyika kesho kuanzia saa tano na baada ya hapo watausafirisha kwenda kijiji cha Endala Karatu mkoani Arusha kwa mazishi yatakayofanyika kesho kutwa.
  Kama kuna yeyote atakaye penda kumtolea chochote mwenzetu Mwanakatwe ili kimsaidie kwa msiba huo anaweza kuwasiliana naye kwa namba hizi za simu-0762-183666, 0655-183666 na 0787184666. 
  Bwana alitoa na 
  bwana ametwaa jina 
  lake lihimidiwe
  AMINA.


  0 0

  WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake, haviwezi kutishwa na mtu yeyote katika kutekeleza maamuzi yoyote kutokana na kuwa na historia ya kuwa na msimamo usioyumba na uongozi thabiti. Membe ambaye ni miongoni mwa wana CCM waliotangaza nia ya kuwania urais kupitia chama hicho, amesema yeye binafsi hatokuwa na kinyongo kwa maamuzi yoyote yatakayochukuliwa na chama hicho hata ikiwa yatakuwa maamuzi machungu kwake. 
  Akizungumza na wanachama wa CCM wa mkoa wa Kigoma waliofika kumdhamini juzi Jumamosi, Membe amesema Watanzania wakatae vitisho na ulaghai kutoka kwa mtu yeyote katika maandalizi ya uchaguzi Mkuu wa mwaka huu. 
  “Watanzania tukatae aina yoyote ya vitisho wala ulaghai katika uchaguzi wetu. Sisi na wengine katika makundi yetu tutakaa kusubitri maamuzi sahihi ya chama chetu, ambacho hakikufanya makosa miaka yote ya nyuma…
  "Tutaheshimu maamuzi yatakayotoka Dodoma siku ile hata yangekuwa machungu kama pilipili. Na ole wao ama ole wake mtu yeyote atakayejitia kuletaleta bughudha pale eti kwa kisingizio kwamba eti chama hakikuchukua hatua sahihi, mtachukua hatua sahihi maana muna uzoefu wa kufanya hivyo. 
  “Nataka kuwambia Dodoma wajumbe wa Mkutano Mkuu ni watu makini sana na wewe (akimuelekeza kiongozi wa CCM Kigoma), mwaka 2012 tulipochagua wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, wajumbe walimuangalia mtu usoni na kumuuliza maswali, mtu anaposema Fulani asichaguliwe, unamuuliza kwanini asichaguliwe (sauti ikasikika ikisema “tulipambana sana”) walisema Fulani mchagueni na Fulani usimchague, wajumbe walihoji kama wewe unakuja na hela mifuko miwili, mmoja unasema mchague huyu na mwingine usimchague Fulani, lakini mulihoji kwanini na kusema huyu si mwenzetu. 
  “Ndugu zangu Watanzania kataeni upuuzi wa aina hiyo, angalieni vigezo mukiangalia familia zenu kwamba na kuhoji kama nikimpa huyu kesho nitakuwa salama!” Alisema Membe huku akishangiliwa na wana CCM waliokuwapo 
  Alisema ni wajibu wana CCM kumpa kiongozi ambaye wakiangalia watakuwa na imani kwamba nchi na familia zao zitakuwa salama na heshima na amani ya nchi itakuwa katika mikono salama na si vinginevyo. Akizungumzia kuhusu maendeleo ya Kigoma alikomalizia mkoa wa 31, Membe alisema ataimarisha miundombinu ya reli na barabara na kuwasaidia kupata mwekezaji atakeyefanikisha mpango huo. Alisema kampuni moja ya Kichina imeonyesha nia ya kuboresha huduma ya reli ikiwa ni pamoja na kujenga reli ya kisasa kati ya Dar es Salaam na Kigoma ambayo itawezesha safari ya siku moja. 
  Membe ambaye amekuwa akiahidi kusimamia uchumi wa viwanda unaotegemea kilimo, alisema viongozi waliotangulia akiwamo maraisi Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na sasa Jakaya Kikwete, wameweka misingi imara katika maenndeleo, na hivyo itakuwa ni rahisi kwake kuendeleza walipoishia. 
  Jana alipokua Sumbawanga na Mpanda, alimsifia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye alisema ni mmoja wa watangaza nia mwenye sifa za kuwa kiongozi wa nchi kutokana na historia yake ya uadilifu ndani na nje ya serikali na kwamba ingekuwa si mwanasiasa huyo angekwisha kujiona mteule ndani ya CCM.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofika mjini Kigoma jana, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofika mjini Kigoma jana, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.
  umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofika mjini Kigoma jana, wakimsikilza Waziri Membe aliyewatembelea kwa ajili ya kuomba udhamini wao  ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Maghufuli alipokuwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  Makutopora kwa mujibu wa sheria

  0 0

   Meneja Mradi wa Sports Development Aid (SDA) Bw. Mohamed Chigogolo akielezea jambo wakati wa hafla ya kuwaaga watoto wanaoenda kushiriki michuano ya Kombe la Helsinki nchini Finland, hafla hiyo imefanyika jana katika ukumbi wa Ubalozi wa Finland jijini Dar es Salaam.Katikati ni Afisa Michezo Mwandamizi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, na Michezo Bw. Nicholaus Bulamile na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Boniface Wambura.

   Balozi wa Finland nchini Bibi. Sinikka Antila akipeana mkono wa mmoja wa wachezaji wa timu ya Vito FC ya wilayani Kilwa mkoa wa Lindi wakati wakiagwa kwa ajili ya kuelekea nchini Finland jana jijini Dar es Salaam. Timu hiyo inaelekea nchini humo kushiriki mashindano ya Kombe la Helsinki ambayo yanahusisha jumla ya timu za watoto walio na umri chini ya miaka 12.Mshindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 05 Julai 2015 na kushirikisha zaidi ya timu 1000. 
   Balozi wa Finland nchini Tanzania Bibi. Sinikka Antila akipngea  na wachezaji wa Timu ya VITO FC kutoka Kilwa mkoani Lindi, ambayo ilikuwa inaagwa kabla ya kuelekea nchini Finland kwa ajili ya kushiriki michuano ya Kombe la Helsinki itakayoanza kutimua vumbi tarehe 05 Julai jijini Helsinki Finland. Timu hiyo imepata ushiriki huo kupitia Asasi ya kirai ya Sports Development Aid (SDA) ikiwa na lengo la kutumia michezo kama nyenzo ya kuhamasisha jamii kuwapeleka watoto wao wakapate elimu.

   Balozi wa Finland nchini Bibi. Sinikka Antila akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Vito FC ya Kilwa mkoani Lindi wakati wa hafla ya kuwaga kwa ajili ya kuelekea nchini Finland jana jijini Dar es Salaam. Timu hiyo inaelekea nchini humo kushiriki mashindano ya Kombe la Helsinki ambayo yanahusisha jumla ya timu za watoto walio na umri chini ya miaka 12.Mshindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 05 Julai 2015 na kushirikisha zaidi ya timu 1000.

  Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Boniface Wambura akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Vito FC ya Kilwa mkoani Lindi wakati wa hafla ya kuwaga kwa ajili ya kuelekea nchini Finland jana jijini Dar es Salaam. Timu hiyo inaelekea nchini humo kushiriki mashindano ya Kombe la Helsinki ambayo yanahusisha jumla ya timu za watoto walio na umri chini ya miaka 12.Mshindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 05 Julai 2015 na kushirikisha zaidi ya timu 1000.


  Picha na Frank Shija, WHVUM


  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya miezi 26 katika mikoa 31 nchini, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. 

  Mkutano huo umefanyika kwenye viwanja vya Furahisha, Kirumba jijini Mwanza jioni ya leo. Ndugu Kinana ambaye katika ziara hiyo ameambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, tayari wamesafiri umbali wa Km 193,537, kwa kufika katika Wilaya 163, majimbo 239, nusu ya vijiji na kata 1938 za Tanzania. Pia msafara wake ulitumia jumla ya saa 84 kuzunguka mikoa yote hiyo, na kusafiri kwa mitumbwi katika visiwa 16. Amehutubia jumla ya mikutano ya ndani/hadhara 1918 na kujikusanyia wanachama wapya 284300 ambapo kutoka upinzani 38984.
  Aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya Chadema, katika uchaguzi mkuu uliopita, Twalib Ngika, akikabidhi Kadi ya Chadema kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  baada ya kutangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu huyo uliofanyika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo.
   Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza leo, ambapo amewataka viongozi wa chama na Serikali kutoka maofisini kwenda kwa wananchi kuzitafutia ufumbuzi kero zao.


  Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akifafanua jambo mbele ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake,alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya miezi 26 katika mikoa 31 nchini, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. 

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiagana na wananchi mara baada ya kumaliza kuwahutubia kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jioni ya leo,Kinana aliwahutubia wananchi na kuahidi kuwa bunge lijalo kwa upande wa CCM, litakuwa na mabadiliko makubwa kwa kuwapa nguvu wabunge kuihoji serikali kuhusu utendaji wake.
  Ndugu Kinana akiwapungia mkono wananchi alipokuwa wakiwasili kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza, ambapo aliwahutubia wananchi na kuahidi kuwa bunge lijalo kwa upande wa CCM, litakuwa na mabadiliko makubwa kwa kuwapa nguvu wabunge kuihoji serikali kuhusu utendaji wake.
  Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mkutano wa CCM kwenye Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza leo.  0 0

   Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF - LINDI Ndg: Ramadhani Mtumwa akikabidhi Msaada wa Mifuko ya Sementi 300 kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, iliyopokelewa na Mkuu wa wilaya ya Lindi Ndg Yahaya E. Nawanda
   Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg Yahaya E. Nawanda (Kulia) akikabidhi Msaada wa Mifuko ya Sementi 300 kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Ndg Seleman Ngaweje aliyo ipokea toka kwa Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF-LINDI kwa ajili ya Umaliziaji wa Ujenzi wa Maabara katika wilaya ya Lindi Vijijini. Kaimu Mkurugenzi huyo ameshukuru mfuko huo kwani msaada huo utaweza kusaidia Umaliziaji wa Ujenzi wa Maabara katika sehemu zilizobaki katika wilaya hiyo.
   Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF - LINDI Ndg: Ramadhani Mtumwa akitoa maelezo juu ya Msaada wa Mifuko 300 ya Sementi iliyotolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa Mkoa wa Lindi ilikumalizia ujenzi wa Maabara, Meneja huyo amesema wameweza kutoa msaada huo kwani wameguswa na suala hilo na pia kutimiza ahadi waliyompatia Mbunge wa Viti maalum kupitia CCM, Mama Lulida. Zoezi hilo la Makabidhiano Yamefanyika  katika Ofisi za PSPF-LINDI 
  Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF - LINDI Ndg: Ramadhani Mtumwa akiwa katika Picha ya Pamoja na Mkuu wa wilaya ya Lindi Ndg Yahaya E. Nawanda (mwenye suti ya kijivu) pamoja na Kaimu mkurugenzi wa wilaya ya Lindi Vijijini Ngd Selemani Gaweje, wakati wa Makabidhiano ya Mifuko 300 ya Sementi kwa ajili ya Ujenzi wa Maabara makabidhiano yaliyofanywa  katika Ofisi za PSPF-LINDI

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwapungua mkono WanaCCM wa Mji wa Kibaha Mjini wakati alipofika kwenye Ofisi za CCM kukabidhiwa orodha ya majina ya WanaCCM waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Jumla ya WanaCCM 78, 500 wamdhamini Mh. Lowassa, Mkoani Pwani.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

  Katibu wa CCM Wilaya ya Temeke, Abdallah Mdimu akikabidhi fomu yenye orodha ya majina ya Wadhamini kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa leo Juni 28, 2015. Jumla ya WanaCCM 78, 500 wa Mkoa wa Pwani Wamemdhamini Mh. Lowassa ili apate ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
  Askofu mstaafu wa Kanisa kuu la KKKT Dayosisi ya Dodoma, Peter Lukumbusho Mwamasika akimuombea Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, wakati alipofika kwenye Ofisi ya CCM Wilaya ya Kibaha Mjini kukabidhiwa orodha ya majina ya WanaCCM waliomdhamini kugombea Urais wa Tanzania, leo Juni 28, 2015.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwaralimia Watoto, Aisha (12) na Sikuzani (4) waliomfata kumsalimia.


  0 0

  By Ayoub Mzee, London
  Meet Angela Benedicto Mnagoza, a girl from a humble background  in  Tanzania, a former child domestic worker, who has  achieved  so  much  to  warrant  an  Award  from  her  majesty  Queen  Elizabeth II  in London.
  Last year a search was launched to find exceptional young people to receive the first ever Queen’s Young Leaders Awards. Hundreds of applications flooded in from incredible young people all dedicated to making lasting change in their community and beyond.
  The award, started by the Queen Elizabeth Golden Jubilee Trust, recognises the contributions of 18-29 year olds from 35 Commonwealth countries. As part of their prize, winners were able able to meet the Queen and Prime Minister David Cameron and take part in a 2 day leadership course in Cambridge. 
  They were also  given a mentor for a year and able to take a distance learning course to help them to develop their leadership skills.

  The award, which is also in partnership with Comic Relief and the Royal Common Wealth Society, had thousands of applications this year and will run for a period of 4 years.

   “This programme will celebrate the achievements of these extraordinary individuals and help develop their skills, thus creating a lasting legacy – benefiting the whole of the Commonwealth – to honour the long and successful reign of HM Queen Elizabeth II.”

  In  the case  of  Angela Benedicto Mnagoza, thanks  for  the  support  from  Anti-Slavery and the local NGO Kivulini in  Tanzania.

  Applications to become a 2016 Queen’s Young Leader will open on 22nd June.
  HE QUEEN’S YOUNG LEADERS GRANTS SCHEME
  Grants will be available to eligible organisations in selected countries across the Commonwealth that are working with young people to transform their lives. Projects will be supported that are led by or focused on young people and provide opportunities for them to learn new skills, secure employment, create enterprises or have a say in decisions affecting their future. Each project will place young people at the heart of their communities, working with them to help solve the issues that affect their lives.

  The Grants will be available to organisations working with young people in UK, Zambia, Sierra Leone, Bangladesh, Jamaica and Solomon Islands.

  WHO IS ELIGIBLE?

  You are eligible if your organisation:
  *Is registered in one of the six eligible countries, or is registered in a Commonwealth country and will work through a named partner who is registered in one of the six eligible countries
  *Has independently audited accounts within the last two years
  *Has managed grants of equal size before
  Is not a Company limited by shares or a Public Limited Company
  *Has governance structures that involve, or are made up of, young people and beneficiaries of youth-focused projects
  Has demonstrable experience of working with young people
  Can demonstrate where young people have played a clear role in the planning of projects and activities
  Has a child protection policy.

  0 0

  Na Makame Mshenga-
  Maelezo Zanzibar 
  Wakulima wa zao la Karafuu wametakiwa kuacha tabia ya kuchukua Miche mingi ya Zao hilo ambayo wanashindwa kuishughulikia ipasavyo, kwani kwa kufanya hivyo ni kurudisha Juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuliimarisha zao hilo kwani Miche hiyo inagharimu kiasi kikubwa cha Pesa za kuitunza. 
   Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Mwanahija Almas alipokuwa akizungumza na Wakulima wa Zao la Karafuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Ukumbi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Mkokotoni. 
   Amesema inashangaza kuona baadhi ya Wakulima huchukua miche ambayo hawawezi kuihudumia vyema kwa vile tu hutolewa bure na Serikali, jambo ambalo hupelekea Miche hiyo Kufa.
  “Tumesikia hapa katika Mijadala kuwa kuna baadhi ya Wakulima huchukua mpaka Miche 400 wakati hawana uwezo wa kuihudumia matokeo yake yote huangamia bila kuleta faida” Alisema Mkurugenzi Mwanahija. 
   Amewataka Wakulima hao kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa na Serikali ili kuhakikisha ubora wa zao la Karafuu za Zanzibar unabakia ili kukidhi vigezo vya sifa vya Kimataifa. 
   Amesema lengo la Serikali katika kilimo cha zao la Karafuu ni kuona linaendelea kuwa tegemeo katika kuingiza fedha za kigeni na kusaidia kukuza Uchumi hivyo linahitaji kulindwa na kila Mwananchi kwa kuongeza uzalishaji na kulinda ubora wake. 
   Kwa upande wao Wakulima waliiomba Serikali kuendeleza ushirikiano na Wakulima hao ikiwa ni pamoja na kuongeza Bei ya zao hilo pale Soko la Kimataifa litakapoimarika. 
   Awali akitoa Mada Mkurugenzi wa Jumuiya ya Wakulima wa Karafuu Zanzibar (ZACPO) Abuubakar Mohammed Ali alielezea umuhimu wa Jumuiya hiyo kuwa ni kuwa na Sauti ya Pamoja ya Wakulima katika kupigania Maslahi yao. Sambamba na hilo Mohammed alisema malengo yao ni kuhakikisha kila Mkulima anamiliki Kitalu chake cha kuzalisha miche badala ya kuitegemea Miche inayotolewa na Serikali. 
   Akifunga Mkutano huo wa Wakulima wa Karafuu Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Juma Kassim Tindwa amesisitiza haja ya kuwepo Uadilifu baina ya Wakulima na Shirika la ZSTC ili kila upande unufaike. 
   Amewataka Wakulima hao kuhakikisha wanapeleka zao hilo katika Vituo halali vya Kuuzia ZSTC ili kuepuka aina yoyote ya Magendo.
   Zao la Karafuu ni zao tegemezi katika uchumi wa Zanzibar ambalo pia huipatia Zanzibar Fedha za kigeni baada ya kuuzwa katika Soko la Dunia.
  Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Mhe. Juma Kassim Tindwa akifungua Mkutano wa Wakulima wa zao la Karafuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofanyika Chuo cha Amali Mkokotoni. 
   Baadhi ya wakulima wa zao la karafuu wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Chuo cha Amali Mkokotoni.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya wakulima wa Karafuu (ZACPO) akifafanua kitu mara baada ya kulizwa swali na wakulima wa Karafuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Mkutano wa wakulima wa zao hilo.
   Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Mwanahija Almas Ali akizungumza na wakulima wa zao la Karafuu katika Mkutano na wadau wa zao hilo huko Chuo cha Amali Mkokotoni. 

   Mkurugenzi Fedha (ZSTC) Ismail Omar Bai akitoa tathmini ya manunuzi ya Karafuu kwa upande wa Pemba kwa niaba ya Afisa Mzamini ZSTC Pemba katika Mkutano wa wazalishaji wa zao la karafu wa Mkoa Kaskazini Unguja. Picha na Makame Mshenga- Maelezo Zanzibar.


  0 0


  0 0

  TIMU ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15, jioni ya leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kombaini ya vijana chini ya umri wa 17 ya mkoa wa Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini hapa.

  Katika mchezo huo uliohudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi dakika 45 za kwanza zilimalizika U15 wakiwa mbele kwa bao 1-0.

  Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji Timoth Maziku dakika ya 17 kwa guu la kulia akimalizia krosi ya Nahodha Issa Abdi.

  Baada ya bao hilo, Mbeya Kombaini walitulia na kuanza kusukuma mashambulizi langoni mwa timu ya taifa, hali ambayo ilifanya timu hizo zishambuliane kwa zamu huku pia vijana wakionyesha uwezo wa kuridhisha.

  Dakika ya 72, Albinius Haule almanusra aisawazishie bao Mbeya kama si shuti lake zuri la kitaalamu alilopiga kutoka umbali wa mita 25 kugonga mwamba wa juu na kutoka nje.

  Nahodha Issa Abdi aliifungia timu ya taifa bao la pili dakika ya 82 kwa shuti la mpira wa adhabu baada ya Timoth Maziku kuangushwa nje kidogo ya boksi na Richard Paul.

  Emmanuel Ntindi wa Mbeya alijifunga dakika ya 87 katika harakati za kuokoa krosi ya Asad Ally dhidi ya Maziku.

  Mchezo ulikuwa mzuri, vijana walionyesha ufundi wa hali ya juu na Mbeya pamoja na kufungwa, walicheza vizuri na kilichowakwamisha kupata japo bao moja ni uhodari wa kipa Kelvin Deogratius wa U15 ya taifa.

  Timu hizo zinatarajiwa kurudiana kesho jioni kwenye Uwanja Sokoine na mapema Jumanne U15 watarejea Dar es Salaam na vijana kuvunja kambi hadi watakapokusanyika tena mwishoni mwa mwezi ujao kwa safari ya Zanzibar kwa michezo mingine ya kujipima.

  Vijana hao walio chini ya kocha Bakari Shime wanaandaliwa kwa ajili ya kucheza mechi za kufuzu Fainali za Vijana Afrika chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2017 na kila wiki ya mwisho wa mwezi watakuwa wakikutana kwa mazoezi na michezo ya kujipima nguvu.

  Kikosi cha Mbeya Kombaini kilikuwa; Edward Mwakyusa, Josephat Frank, Seif Gabriel, Emmanuel Ntindi, Richard Paul/Hassam Abdallah dk87, Goodluck Ezeria, Amiri Nyeo, Castro Issa, Albinius Haule, Biya Stephen na Daniel Samson/Castro Moses dk73.

  Tanzania U15; Kelvin Deogratius, Kibwana Ally, Faraji John, Maulid Salum, Ally Hussein, Athumani Maulid/Rashid Kilomtola dk75, Robert Philipo/Morris Michael ‘Chuji’ dk86, Asad Ally, Timoth Joseph, Issa Abdi na Juma Zubeiry/Juma Juma dk61.  

  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0


  SIMUTV: Watoto yatima wawili  wakazi wa manispaa ya Ilemela mjini Mwanza  wafanikiwa kupata hati ya nyumba yao ya urithi  baada ya shririka lisilo la kiserikali KIVULINI kushirikiana na uongozi wa mtaa kuingilia kati sakata hilo. http://youtu.be/3PB-kjC4sNI

  SIMUTV: Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba awataka wananchi kijiandikisha katika daftari la wapiga kura wakita akihutubia mkutano wa hadhara mkoani Mwanza. http://youtu.be/1VWsaj6DNHM
  SIMUTV: Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Christopher Kongoye Awaomba Viongozi wa Dini Kuwahamasisha waumini kudumisha amani Kuelekea Uchaguzi Mkuu. http://youtu.be/3FcJp3aF_Vg
  SIMUTV: Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi 100 duniani zilizo mstari wa mbele kutetea haki za watoto wakiwemo wanaoishi katika hali ngumu, bado ina safari ndefu baada ya kubaini mapungufu ya kutetea haki za watoto hao kikamilifu.http://youtu.be/thlrtrEy8QY


  0 0

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea Mhe. Mathias Chikawe, akizungumza na wanamichezo kabla ya kuanza fainali ya Kombe la Chikawe katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya Black Fire kutoka Kata ya Marambo na Timu ya Motisha kutoka Kata ya Kilimanihewa zilipambana na Timu ya Black Fire iliibuka mshindi kwa magoli 3 kwa 1. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Mhe Pololeti Mgema.

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea akimsalimia mchezaji wa Timu ya Black Fire, Faraji Mohamed wakati alipokuwa anaikagua timu hiyo kabla ya fainali ya Kombe la Chikawe ambayo yalifanyika katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya Black Fire kutoka Kata ya Marambo iliibuka kidedea baada ya kuinyuka Timu ya Motisha, Kata ya Kilimani magoli 3 kwa 1. Nyuma ya Waziri Chikawe ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.

   Kapteni wa Timu ya Black Fire, Ally Njaidi (kulia) akipokea fedha taslimu Shilingi 500,000 pamoja na Kikombe cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema, baada ya kumalizika fainali ya Kombe la Mbunge wa Jimbo hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Timu hiyo iliirarua timu ya Motisha mabao 3 kwa 1 katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salimu Mwalimu, naye alihudhuria fainali ya mashindano hayo ambayo yalianzishwa na Mbunge Chikawe jimboni humo kwa kushirikisha timu 178 katika jimbo hilo.

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe  (aliyevaa kofia) akiwa na wachezaji wa timu ya Motisha kutoka Kata ya Kilimanihewa. Kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.

   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe  (aliyevaa kofia) akiwa na wachezaji wa timu ya Black Fire ambao ndio waliibuka washindi. Kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya biashara ya DCB Bw. Samwel Dyano akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo Balozi Paul Rupia hayupo pichana juzi jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya Desire to Succeed iliyodhaminiwa na benki hiyo kwa lengo la kuhamasisha jamii kutumia huduma za kibenki katika kuyafikia mafanikio yao.

   Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Balozi Paul Rupia akizungumza wakati wa  hafla ya uzinduzi wa filamu ya Desire to Succeed juzi jijini Dar es Salaam.Filamu hiyo imetengenezwa na ya Kampuni ya Consnet Group Ltd ya jijini Dar es Salaam kufuatia udhamini wa DCB Benki ikiwa ni njia ya kujitangaza.

   Mwakilishi wa Kampuni ya Consnet Group ambayo ndiyo waandaaji wa filamu ya Desire to Succeed Bw. Sanctus Mtisimbe (mwenye tai nyekundu) akiwatambulisha baadhi ya wasanii (wahusika) muhimu walioshiriki katika filamu hiyo juzi jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu hiyo iliyoambatana na futari chini ya udhamini wa Benki ya Biashara ya DCB.

   Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo akitambulishwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa filamu ya Desire to Succeed iliyodhaminiwa na benki hiyo kwa lengo la kuhamasisha jamii kutumia huduma za kibenki katika kuyafikia mafanikio yao.

   Baadhi ya wasanii waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa filamu ya Desire to Succeed wakijitambulisha juzi jijini Dar es Salaam.Filamu hiyo iliyodhaminiwa na benki ya Biashara ya DCB.

  Kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo, msanii Rose Ndauka, Tito Mrisho Zimbwe na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB Balozi Paul Rupia wakionyesha DVD ya filamu ya Desire to Succeed juzi jijini Dar es Salaam mara baada ya kuzinduliwa rasmi. Filamu hiyo imetengezwa na kampuni ya Consnet Group chini ya udhamini wa DCB Benki ikiwa ni njia ya kujitangaza kupitia ubunifu wa sanaa ya filamu.


  Picha na Frank Shija, WHVUM. Kwa habari kamili BOFYA HAPA


  0 0

   Mratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka, akifafanua juu ya Umuhimu wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe  nchini wakati Wataalam na waratibu maafa mkoani Shinyanga walipokuwa wakijifunza uendeshaji wa tathmini hiyo katika kijiji cha Uzogore mkoani humo
   Wataalam na waratibu maafa mkoani Shinyanga wakijifunza kwa vitendo uendeshaji wa Tathmini ya Hali ya Chakula na Lishe  nchini  katika kijiji cha Uzogore mkoani Shinyanga, mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu
   Mwanakijiji cha Uzogore, Mkoani Shinyanga, akitumia mawe kufafanua uwiano wa Hali ya Chakula na Lishe kijijini hapo wakati Wataalam na waratibu maafa mkoani humo wakijifunza kwa vitendo uendeshaji wa Tathmini ya Hali ya Chakula, mafunzo hayo yameratibiwa na Ofisi  ya Waziri Mkuu
  Mratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Theodosia Mbunda akipongezwa na wanakijiji cha Uzogore, Mkoani Shinyanga, mara baada ya kuwaeleza umuhimu wa Hali ya Chakula na Lishe kijijini hapo wakati Wataalam na waratibu maafa mkoani humo walipojifunza kwa vitendo uendeshaji wa Tathmini hiyo

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Bw. Keneth Kaseke, Kamishna wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani Ijumaa. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Suleiman Rashid na wa Pili Kulia ni Dkt Bwijo Bwijo wa UNDP.
  Rais Kikwete na meza ku wakipokea Maandamano kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.
  Maandamano kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.
  Mary Kibwana na Christa Komba Walimu wakongwe  na magwiji wa sanaa za maonesho wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakiongoza kikundi cha maigizo tumbuiza Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.
  Hassan  Salum, Msanii mahiri ambaye ni  mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) akiigiza kama 'Teja' 
  Wanafunzi wa mwaka wa tatu katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) wakiigiza  mbele ya Wananchi waliohudhuria kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani mjini Bagamoyo mkoa wa Pwani.older | 1 | .... | 886 | 887 | (Page 888) | 889 | 890 | .... | 3286 | newer