Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110181 articles
Browse latest View live

WAKUU WA TAASISI ZA MAGEREZA KUTOKA NCHI ZA AFRIKA WATEMBELEA KIWANDA CHA VIATU CHA GEREZA KUU KARANGA MOSHI, MKOANI KILIMANJARO

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Botswana, Silas Motlalekgosi akisalimiana na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wa Mkoani Kilimanjaro alipotembelea Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga Moshi leo Juni 25, 2015 akiwa na Viongozi Wakuu wa Taasisi za Urekebishaji/ Magereza kutoka Nchi za Swaziland, Uganda, Kenya, Zambia.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Swaziland, Isaya Ntshangase akisaini kitabu cha Wageni alipowasili katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga, Moshi ambapo Viongozi hao wa Magereza kutoka Nchi za Afrika wapo ziara ya kikazi nchini Tanzania.
 Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile akitoa utambulisho kwa Ujumbe wa Viongozi wa Magereza kutoka Nchi za Afrika ambao wapo Nchini kwa ziara ya kikazi. Viongozi hao wametembelea Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga, Moshi.
 Wafungwa wa Gereza Kuu Karanga Moshi wakiwa wanashona viatu aina ya Buti ambavyo hutumiwa na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama hapa nchini kama wanavyoonekana katika picha wakishona sehemu ya juu ya viatu hivyo. Wafungwa hao wa Gereza Kuu Karanga wananufaika na Stadi ya Ushonaji viatu katika Kiwanda hicho kwa kujipatia ujuzi wa Ushonaji.
Muonekano wa viatu aina ya Buti vinavyotengenezwa katika Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga Moshi, viatu hivyo hutumiwa na Maafisa na Askari wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikiwa tayari vimekwishatengenezwa kama vinavyoonekana katika picha.
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

SSRA iliposhiriki maonuesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

$
0
0
Mkurugenzi wa Matekelezo na Uandikishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Lightness Mauki (kulia) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipotembelea Banda la SSRA wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Matekelezo na Uandikishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Lightness Mauki akikabidhi zawadi kutoka SSRA kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue baada ya kutembelea banda la SSRA.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Mussa Assad akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Kushoto ni Mkurugenzi wa Matekelezo na Uandikisha akifuatiwa na Afisa Utafiti na Sera Bw.Simon Aikambe.
Maafisa wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) wakisikiliza maswali na maoni mbalimbali kutoka kwa wananchi waliotembelea Banda la SSRA katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Rais Kikwete ahudhuria Sherehe za Miaka 40 za Uhuru wa Msumbiji

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiukagua gwaride la heshima muda mfupi baada ya kuwasili jijini Maputo Msumbiji kuhudhuria sherehe za miaka 40 ya uhuru wa Msumbiji zilizofanyika katika uwanja wa Michezo wa Machava jijini Maputo.
Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi amkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete katika uwanja wa Michezo wa Michezo wa Machava jijini Maputo Msumbiji kuhudhuria sherehe za miaka 40 za Uhuru wa Msumbiji.Msumbiji ilipata uhuru wake tarehe25 June mwaka 1975 kutoka kwa mkoloni Mreno.(picha na Freddy Maro).

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA JIMBO LA SUMVE MKOANI MWANZA LEO.

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi za Chadema kutoka kwa vijana 20 waliojiunga na CCM na wanachama wapya zaidi ya 1520 walipewa kadi zao za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Sumve. Katika ziara yake kwenye jimbo la Sumve Katibu Mkuu wa CCM amepokea kadi 48 kutoka Chadema ikiwa 28 zilizorudishwa katika kijiji cha Goloma kata ya Mwadu.
 kadi za Chadema kutoka kwa vijana 20 waliojiunga na CCM na wanachama wapya zaidi ya 1520 walipewa kadi zao za CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Sumve.
 Wananchi wa Kata ya malya wakionyesha Bango kubwa lenye ujumbe kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana lenye madai ya kudhulumiwa viwanja ambavyo tangia walipie miaka mitatu sasa hawajapata viwanja,Katibu Mkuu wa CCM alikuwa njiani kuelekea Nyambiti ndipo wananchi hao walimsimamisha barabarani na kutoa kero zao.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungunza na wakazi wa kata ya Malya ambao wanadai viwanja vyao walivyovilipia miaka mitatu iliyopita,lakini mpaka sasa wananchi hao hajakabidhiwa,Ndugu Kinana ameipa muda wa miezi miwili  na ushehe kuwa ifikapo septemba 1,2015 ,Halmashauri ya wilaya ya Sumve ihakikishe imelitatua tatizo hilo na wananchi kupewa viwanja vyao. Katibu Mkuu wa CCM alikuwa njiani kuelekea Nyambiti ndipo wananchi hao walimsimamisha barabarani na kutoa kero zao. 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Sumve,Mh Richard Ndassa,mara baada ya kuzindua  huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa kijiji cha Mwabilanda  wilayani Kwimba.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia sehemu ya kunyweshea maji mifugo katika kijiji cha Kishilili, ambapo Ng'ombe zaidi ya 800 hupata huduma ya maji safi na salama katika mradi ambao pia husaidia kaya 102 kupata maji safi na salama katika kisima kinachotumia mfumo wa jua (solar power).


MAKALA YA SHERIA: MIRATHI ZA WATOTO WADOGO NA WASIO NA AKILI TIMAMU HUSIMAMIWA NA NANI KISHERIA?

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.

Suala  la  mirathi  popote  linapotokea   hutokea  iwapo  kuna  mtu  amekufa  na   ameacha  mali  . Mtu  akishakufa  akaacha  mali  hata  kama  hakuna  ndugu wa kurithi  suala  la  mirathi  lazima  liibuke.  Huibuka kwakuwa  lazima  zile  mali  ziende  pahali  iwe  kwa  mtu  au  kwa  mamlaka. Hata  hivyo  suala  la  mirathi  huibua  hisia  zaidi  hasa  panapokwa  hamna  wosia.  Marehemu  asipoacha wosia  lakini  akaacha   mali  mambo  huwa  sio  mepesi  sana labda  iwe vinginevyo.

  Ifahamike  kuwa mirathi  huhusisha   mambo  mengi. Lakini  pia huhusisha  sheria  nyingi.  Sheria  za kiislam huhusika, sheria  za  kimila  huhusika   na  pia  sheria  za  nchi  ambayo  ni  sura  ya  352. 

1.USIMAMIZI  WA  MIRATHI  KAMA  KUNA  WOSIA.

Kama  marehemu  ameacha  wosia    basi  ni  vema  kuangalia  wosia  huo  umemtaja  nani awe  msimazi wa  mirathi. Hili  ni muhimu  watu  walijue  hata  wale  walioandika  wosia  tayari au  wanaotarajia  kuandika  wosia.  Wengi  wamekuwa  wakiandika  wosia  na  kugawa  mali  lakini  wakisahau  kuteua  na  kumtaja  msimamizi  wa  mirathi  wakiamini  kuwa  kila  mtu  atakapochukua  chake   mambo  yataishia  hapo. 

Laa  hasha  mambo  si  mepesi  kiasi  hicho.  Kwa  hiyo  yafaa  kuangalia  nani  ametajwa  kama  msimamizi  wa  mirathi  katika  wosia    na  huyu  ndiye  atakuwa  msimamizi  wa  mirathi. Ikiwa  wosia  upo  lakini  haukumtaja  msimamizi  wa  mirathi  basi  taratibu  za  kimahakama  nitakazoeleza  hapa  chini  zitafuata.

2.  KUMTHIBITISHA  MSIMAMIZI  WA  MIRATHI  MAHAKAMANI.

Ikiwa  wosia   umemtaja  msimamizi  wa mirathi  basi  hilo  tu  halitoshi. Sheria  inataka  msimamizi  wa  mirathi  athibitishwe  pia na  mahakama. Hii  ni  kwasababu   mahakama  hutoa  hati  maalum   kwa  aliyethibitishwa kuwa  msimamizi  wa  mirathi  ambayo  hutum ika  sehemu  zote  za  kisheria  kwa  mfano  kuchukua  hela  za  marehemu  benki, kuchukua  hisa za  marehemu, kuuza  na  kununua  mali  za  marehemu,kubadilisha  vitu  kama  hati na kila  kitu  ambacho  huhusisha  taratibu  maalum  za  kisheria. Kwakweli  isingewezekana  kutumia wosia  kwa kuuonesha  kila ofisi  unayoingia  katika kufanya  michakato  hii yote.  Na  hapa ndio  mahitaji  ya  kuthibitishwa  na  mahakama  na  kupata  hati maalum ambayo  ni  kama  utambulisho  yalipotokea. 

Waziri Dkt Asha-Rose Migiro atua nyumbani Mwanga kupokea wadhamini

$
0
0
 Waziri wa Sheria na Katika Dkt. Asha-Rose Migiro akipokea majina ya wadhamin toka kwa katibu wa CCM Mwanga Bi Mwanaidi
 Dkt. Migiro  akiwa na list yake ya wadhamini Mwanga Kilimanjaro
Dkt. Migiro akiwa na kaka zake kwenye kaburi la baba yake Cheif Shaaban Mndorwe Mtengeti Sangiwa II na babu zake waliotangulia.

MKOA WA DAR ES SALAAM WAMDHAMINI BERNARD MEMBE

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akionyesha fomu zilizojazwa na wanaCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam zaidi ya 1,500 kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Shesha (kulia) katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni Juni 25.2015. Kushoto ni mkewe Mama Dorcas Membe. 
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mkoani Dar es Salaam Juni 25.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo wanaCCM zaidi ya 1,500 walimdhamini.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiagana na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mkoani Dar es Salaam Juni 25.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo wanaCCM 1,500 walimdhamini.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiagana na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mkoani Dar es Salaam Juni 25.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo wanaCCM 1,500 walimdhamini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiagana na umati wa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliofurika katika ukumbi wa Vijana Kinondoni mkoani Dar es Salaam Juni 25.2015, kwa ajili ya kumdhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya chama hicho, ambapo wanaCCM 1,500 walimdhamini. Picha zote na John Badi

MCHAKA MCHAKA WA LOWASSA WATINGA MANYARA LEO, APATA UDHAMINI WA WANACCM 42, 405

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Edward Lowassa akizungumza wakati akiwashukuru wanaCCM wa Mkoa wa Manyara, waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Lowassa amepata wadhamini 42, 405 , Mjini Babati Mkoani Manyara leo, Juni 25, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Edward Lowassa akipokea fomu ya udhamini kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Babati Mjini, Daniel Ole Porokwa, leo Juni 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 42, 405 wa Mkoa wa Manyara.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akimsalimia Kijana Jacob Jeremiah ambaye ni mlemavu wa miguu, alipokutana nae nje ya Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Manyara, iliopo Mjini Babari leo Juni 25, 2015, wakati akiwa katika ziara ya kusaka wadhamini  watakaomuwezesha kutapa ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.


News alert: bei mpya za usajili makampuni na majina ya biashara Brela kuanzia Tarehe 1 Julai.

MBUNGE WA GEITA MAREHEMU DONALD MAX KUZIKWA JUMAMOSI MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
MAREHEMU DONALD MAX

RATIBA YA KUAGA RASMI NA MAZISHI YA MAREHEMU DONALD MAX, SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 27 JUNI, 2015 KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE NA MAKABURI YA KINONDONI. 
BOFYA HAPA

Joto La Asubuhi la 97.3 EFM kesho Ijumaa

DONDOO ZA HABARI KUTOKA VITUO MBALIMBALI VYA TV LEO KUPITIA SIMU TV

$
0
0

Zimekusanywa na Samwel Kamugisha


Ch10 News
Simutv:Kada wa CCM January Mkamba awasihi wagombea wenza wa uraisi kupitia chama chake kuacha kuchafuana kwani wao wote ni wamoja. http://youtu.be/xIXTuhLqDVw  
Simutv:Wafanyakazi wa tume ya utumishi wa umma watakiwa kuwa wabunifu zaidi ili kukabiliana na changamoto ufinyu wa bajeti badala ya kuwa walalamikaji. http://youtu.be/Qa7f6Ns-VAQ
Simutv:Katibu mkuu wa CCM Abdulahman Kinana awataka watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kwimba kutenda haki kwa wananchi pindi watakapo anza ugawaji viwanja kwa ajili ya upanuzi wa mipango miji. http://youtu.be/R4-LJoUp6mo     
Simutv:Wajumbe wa Baraza la wawakilishi wanadaiwa kumzuia makamo wa kwanza wa raisi wa Zanzibar Maalim Seif kuhudhuria shughuli ya kuvunja baraza la wawakilishi. http://youtu.be/25W3sFRszQk  
Simutv:Halmashuri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam yaanza zoezi la kuvunja uzio wa majengo yanayojengwa baada ya wamiliki kushindwa kulipia ushuru kwa manispaa hiyo. http://youtu.be/UzC4VLHziwU
 Azam tv news
Simutv:Kada wa CCM Prof.Muhongo arudisha fomu Dodoma baada ya kusaka wadhamini huku akikana kupokea fedha za Escrow mbele ya waandishi. http://youtu.be/hyUCdiGfgUI
Simutv:Makamo wa pili wa Raisi wa Burundi akimbia nchi yake na kuelekea Ubelgiji huku akikemea hatua ya Raisi Nkurunzinza kugombea uraisi muhula wa tatu. http://youtu.be/yHbb92fsN9A     
Simutv:Sintofahamu juu ya ujenzi wa maghorofa mkoani Mbeya kufuatia hofu ya tetemeko la ardhi yaanza kupotea baada ya ujenzi huo kushika kasi mkoani humo. http://youtu.be/688yzVQY078    
Simutv:Sintofahamu yaikumba UKAWA kufuatia kutoafikiana juu ya kugawana majimbo 13 kwa ajili ya ujaguzi ujao baina ya washirika wa muungano huo. https://youtu.be/ckN1sOYd4Ro
Simutv:Jeshi la polisi nchini linamshikilia mtu mmoja kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya alizokuwa akisafirisha kwenda nchini Ghana. http://youtu.be/XLfLeoFayUs
 STAR TV NEWS
Simutv:Mbunge wa Kigoma Kaskazini David Kafurila aomba mwongozo wa Spika juu ya sakata la ununuaji mabehewa feki.http://youtu.be/Qck1aj8FGpg
Simutv:Kiongozi wa kundi la waasi la ADF aamuriwa na mahakama kurejeshwa nchini Uganda akafunguliwe mashitaka huku mwenyewe akikata rufaa dhidi ya hukumu hiyo. http://youtu.be/CMFlKQaGyjE   
Simutv:Halmashauri kuu ya CCM Shinyanga vijini pamoja na madiwani wapinga agizo la waziri mkuu la kumrudisha kazini aliyekuwa mwenyekiti wa halimashauri hiyo baada ya kukataliwa na madiwani kwa tuhuma mbalimbali.http://youtu.be/KVyUk65rpOE 
Simutv:Wizara ya ardhi inaendelea na mikakati ya kuwafikisha mahakamani wamiliki wa ardhi milioni 3 nchini kwa makosa ya kukwepa kulipa kodi ya pango la ardhi. http://youtu.be/OZpVcNknt7k
Simutv:Watuhumiwa 3 wa mauaji ya kukata watu makoromeo huko Kagera wanusurika kifo baada ya wananchi kuzingira kituo cha polisi wakitaka kuwaua. http://youtu.be/1DAi08ExyQs 
 TBC NEWS
Simutv:Serikali yahaidi kuzifanyia marekebisho baadhi ya sheria za masuala ya fedha,kodi,ushuru na tozo kwa lengo la kuboresha ukusanyaji mapato. http://youtu.be/fS3wG2_zWL8   
Simutv:Wakazi wa wilaya ya Tanga waipongeza serikali kwa kuboresha huduma za uandikishaji BVR licha ya kuwepo na changamoto kadhaa katika uandikishaji. http://youtu.be/ybNqFEJjUuo
Simutv:Kikao cha sekritarieti ya CCM chini ya uongozi wa katibu mkuu wa chama hicho Abdulahman Kinana kinatarajiwa kukutana kesho mjini Dodoma. http://youtu.be/8hRQK0Llq-Y
Simutv:CCM yatoa wito kwa mabalozi wa nyumba 10 kuhakikisha wanashirikiana na serikali na wadau mbalimbali ili kudhibiti mauaji ya Albino. http://youtu.be/DHMCFnI7xAo  
Simutv:Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa raisi wa Zanzibar awaagiza wananchi kuzingatia na kufuata sheria katika kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura. http://youtu.be/3LUhgmkTdDs

JK AHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 40 ZA UHURU WA MSUMBIJI

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiukagua gwaride la heshima muda mfupi baada ya kuwasili jijini Maputo Msumbiji kuhudhuria sherehe za miaka 40 ya uhuru wa Msumbiji zilizofanyika katika uwanja wa Michezo wa Machava jijini Maputo.

Rais wa Msumbiji Felipe Jacinto Nyusi amkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete katika uwanja wa Michezo wa Michezo wa Machava jijini Maputo Msumbiji kuhudhuria sherehe za miaka 40 za Uhuru wa Msumbiji.Msumbiji ilipata uhuru wake tarehe25 June mwaka 1975 kutoka kwa mkoloni Mreno. Picha na Freddy Maro.

mpiganaji Edson Kamukara afariki dunia

$
0
0

Mhariri  wa Mwana Halisi Online, Edson Kamukara (pichani), amefariki Dunia kwa ajali ya moto nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam leo hii majira ya saa moja kasorobo jioni, baada ya kulipukiwa na jiko la gesi, habari zilizotufikia sasa hivi zinasema kuwa Polisi wameuchukua mwili wa marehemu na kwenda kuhifadhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa kifo chake.


Ofisa Uhusiano wa NMB, Viccent Mnyanyika akimkabidhi zawadi marehemu Edson Kamukara wakati wa uhai wake kwenye wa utoaji wa tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) zilizofanyika Aprili 24 mwaka huu.

Globu ya Jamii inaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wafanyakazi wenzake, marafiki na majirani katika msiba huu. Mola na aiweke mahala pema Roho ya Marehemu,
AMINA

MAKALA YA SHERIA: MIRATHI ZA WATOTO WADOGO NA WASIO NA AKILI TIMAMU HUSIMAMIWA NA NANI KISHERIA ?

$
0
0
Suala  la  mirathi  popote  linapotokea   hutokea  iwapo  kuna  mtu  amekufa  na   ameacha  mali  . Mtu  akishakufa  akaacha  mali  hata  kama  hakuna  ndugu wa kurithi  suala  la  mirathi  lazima  liibuke.  
Huibuka kwakuwa  lazima  zile  mali  ziende  pahali  iwe  kwa  mtu  au  kwa  mamlaka. 

Hata  hivyo  suala  la  mirathi  huibua  hisia  zaidi  hasa  panapokwa  hamna  wosia.  Marehemu  asipoacha wosia  lakini  akaacha   mali  mambo  huwa  sio  mepesi  sana labda  iwe vinginevyo.  Ifahamike  kuwa mirathi  huhusisha   mambo  mengi. Lakini  pia huhusisha  sheria  nyingi.  Sheria  za kiislam huhusika, sheria  za  kimila  huhusika   na  pia  sheria  za  nchi  ambayo  ni  sura  ya  352.

DIRA YA DUNIA YA IDHAA YA KISWAHILI YA BBC, LONDON

APPRECIATION

$
0
0
   The late Juliana Bankolwa Mashiba 
1st July 1934 - 04th May 2015 

The family of Martin Mashiba of Kisesa –Mwanza would like to express our deepest appreciation for the outpouring of sympathy and comfort we received during our loss. Thank you to all those who visited, called, sent prayers, cards, memorials, flowers, or helped in any way. 

Our heartfelt thanks for the condolence and sympathy you have extended towards us goes to the President of the United Republic of Tanzania H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, and the First Lady mama Salma Kikwete, the management and members staff of the State house – Dar es Salaam, the office of the Director General of Tanzania Intelligence and Security Services, staff and the management of Tanzania Revenue Authority, St. John’s University of Tanzania, DED Bahi District, UCSAF, Umoja wa Wake wa Viongozi,   Polycarp Cardinal Pengo, Mwanza Regional Commissioner, The Archbishop Diocese of Mwanza, Vicar General, all clergy, Bujora Parish Choir, Bugando, Kawekamo, Nyakahoja, Paradiso A.I.C. Nyakato and Wanamoyo Safi wa Bikira Maria-Bukumbi choir, Mwashita MlimwaDodoma, 
We also extend our appreciations to all Kisesa Village Members (Wananzengo), all relatives and friends. 

It is our sincere wish to mention all who participated in one way or another but the list is too long, for those who are not mentioned here we apologise and request that they also accept our appreciation and that we are really thankful to you and appreciate your support and love in this time of loss. 

There will be a requiem mass on Saturday 27th June, 2015, at 11:00AM at Martin Mashiba’s Residence Kisesa-Mwanza. 

“He will wipe every tear from their eyes. There will be no more death’ or mourning or crying or pain, for the old order of things has passed away.” Revelation 21:4 

THANK YOU   

SOLUTION BLOCKS YAANDAA MIKUTANO ILI KUKUTANISHA NGO’S,TAASISI ZA KIRAIA NA TAASISI ZA SERIKALI KWA KILA MWENZI.

$
0
0
 Na Avila kakingo,Globu ya jamii.
KAMPUNI ya Solution BLOCKS ikishirikiana na kampuni ya Anglo Gold Ashanti waandaa mkutano wa  Alhamisi ya kila mwezi ili kushirikisha taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali kuzungumzia kuchangia katika maendeleo katika  jamii.

Hayo yamesemwa na Makamo wa Rais wa Sustainability Aglo Gold Ashanti, Simon Shayo katika ufunguzi wa mkutano ambao umejulikana kwa jina la THURSDAY TALK  uliofanyika katika hoteli ya Colosseum  jijini Dar es Salaam jana.

  Nae Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Solution Blocks (Facilitator), amesema kuwa Makampuni na taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali lazima ziwajibike na kuelemisha jamii pia na kutoa fursa kwa wadau wa maendeleo hapa nchini ili kushiriki vyema katika kuleta maendeleo.

Pia ametoa wito kwa makampuni, NGO, taasisi za Serikali pamoja na Asasi za kiraia kuwajibika kushiriki vyema katika  kuleta maendeleo ya elimu,Afya,mazingira, maji pamoja na utawala bora katika taasisi hizo.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Solution Blocks, Msomisi Mbenna akizungumza katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam jana.
 Makamu wa Raisi-Sustainability Anglo Gold Ashanti-Mgodi wa Geita,, Simon Shayo akizungumza na wadau waliohudhuria katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam jana kuhusiana na mgodi wa dhahabu wa Geita jinsi unavyofanya kazi zake na kulinda afya za wananchi wa maeneo hayo ili wasidhurike na uchimbaji wa madini hayo.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Anglo Gold Ashanti -Mgodi wa Geita, Tenga .M. Tenga akizungumza katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam jana ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks.
Baadhi ya wadau waliohudhuria katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam jana kampuni ya Solution Blocks.
 Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

WANANCHI WA KATA YA MALYA WILAYANI YA KWIMBA WAZUNGUMZIA DHULMA YA ARDHI

HATIMAYE DOGO JEMBE ACHUKUA FOMU YA URAIS

Viewing all 110181 articles
Browse latest View live




Latest Images