Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 884 | 885 | (Page 886) | 887 | 888 | .... | 3278 | newer

  0 0

   A team of 21 Acacia staff, friends and family led by Chief Executive Officer, Brad Gordon, are embarking on the journey of a lifetime to reach Uhuru Peak; the summit of Mount Kilimanjaro, to raise funds for education.


  Through its CanEducate, a charity that provides educational sponsorships to impoverished and at-risk children in developing countries including Tanzania, the company targets to raise $200,000.


  As it costs $75 a year to send a student to school in Tanzania, the targeted donation has the potential to help 2000 students in communities surrounding Acacia mine sites of Buzwagi, Bulyanhulu and North Mara, who fail to attend schools due to income constraints.


  Elaborating further, Brad said for less than a month, donations were going on so well hoping to attain the target, and that the company was set to match individual donations by a dollar for a dollar.


  “I am sure that the final figure is going to have an incredible and positive impact on the lives of children in Tanzania. If you haven’t done so yet, there is still time to give. We need those crucial dollars to get us to our target and to give the team 200,000 reasons to make it to the top,” he added.


  The CanEducate initiative started in 2010 covering 158 students at Bulyanhulu and by the end of 2014 the programme had grown to cover 1,800 students across Bulyanhulu, Buzwagi and North Mara and has delivered some of the best performers in various schools in the National Form 4 examinations.


  Mount Kilimanjaro, in Tanzania, is the highest freestanding mountain in the World and Uhuru Peak, at 5,895m is the highest point in Africa. Uhuru means freedom and Acacias believes education brings freedom through choice, which is why CanEducate is the perfect recipient of funds raised through the climb.


  Notes to the editor

  Acacia is the leading gold producer in Tanzania with three producing mines, all located in northwest Tanzania, together with several exploration projects at various stages of development, including exploration land holdings in the highly prospective greenstone belts in Western Kenya and Western Burkina Faso.


  Acacia Mining plc is a UK public company with its headquarters in London. We are listed on the Main Market of the London Stock Exchange under the symbol ACA and have a secondary listing on the Dar es Salaam Stock Exchange in Tanzania.If you wish to support this noble course.

  By Dixon Busagaga ,Michuzi blog representative Northern zone.

  0 0

    Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa PSPF mkoani Manyara Bw. Said Ismail akitoa mada kwa wanafunzi wa chuo cha Afya Huydom, mkoani Manyara. Moja ya jukumu la PSPF ni kutoa elimu juu ya PSPF na sekta nzima ya hifadhi ya jamii, PSPF inaendelea kutoa semina kwa vyuo mbalimbali nchini.
  Wanafunzi wa chuo cha Afya Huydom, mkoani Manyara.
  Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa PSPF mkoani Manyara Bw. Said Ismail, wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa chuo cha Afya Huydom, mkoani Manyara.

  0 0

   Ndege zikipita na kuchora rangi za bendera za Msumbiji jana wakati wa maadhimisho ya miaka 40 ya Uhuru wa msumbiji jana.
   Askari wa Msumbiji wakishuka na mwavuli wakati wa sherehe za uhuru(picha na Freddy Maro).
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Wa Malawi Profesa Peter Mutharika wakitoka katika uwanja wa michezo wa Machava jijini Maputo Msumbiji baada ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 40 ya uhuru wa Msumbiji jana.

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhandisi Angelina Madete (wanne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Warsha ya kupitia Ripoti ya Takwimu za Kemikali zinazokaa muda mrefu katika Mazingira. Warsha hiyo ya siku moja imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa National Institute for Medical Research, jijini Dar es Salaam na imehusisha wadau kutoka sekta mbalimbali.
  Sehemu ya Washiriki wa Warsha ya kupitia Ripoti ya Takwimu za Kemikali zinazokaa muda mrefu katika Mazingira wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi Mhandisi Angelina Madete (hayupo pichani) katika hafla ya ufunguzi iliyofanyika katika Ukumbi wa Medical Reseach.
  Washiriki wakiwa katika vikundi wakipitia na kurekebisha Ripoti hiyo.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani Bw. Benjamin Thompson Kasenyenda akitoa wito kwa watanzania wote wenye mapenzi mema kujitokeza kwa wingi kushiriki katika harambee hiyo itakayofanyika katika viwanja vya Leaders club,siku ya Jumamosi Julai 4,2015 wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene.Kulia ni wajumbe wa Kamati hiyo Bi. Mwanamkasi Jumbe na Angela Msangi.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwahamasisha waandishi wa habari kuimarisha mshikamano katika Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaosumbuliwa na magonjwa sugu ikiwemo kansa.Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Grace Nakson.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa ambaye ni mjumbe wa kamati ya kuratibu Harambee ya kuwachangia wanahabari wanasumbuliwa na magonjwa sugu ikiwemo kansa akiwahamasisha wanahabari wote nchini kuungana katika harambee hiyo kwa kuihamasisha jamaii kushiriki katika tukio hilo muhimu. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani Bw. Benjamin Thompson.
  Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa kuhamasisha kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani.
  Mjumbe wa Kamati ya Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani Bi. Angela Msangi akiwahamasisha wanahabari kujitokeza kwa wingi katika harambee hiyo na pia kutumia taaluma yao kuihamasisha jamii kujitolea katika kufanikisha lengo la harambee hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Mwanamkasi Jumbe. PICHA NA FRANK MVUNGI-MAELEZO

  0 0
 • 06/26/15--02:55: TAARIFA YA MSIBA
 • Familia ya marehemu Dr. Albert Chagula wa Chang’ombe maduka mawili inawatangazia kuondokewa na mama yetu mpendwa Mwl. Magdalena Chagula kilichotokea ghafla usiku wa juzi tarehe 24.06.2015. Msiba uko nyumbani kwetu Chang’ombe Maduka mawili mtaa wa Majimaji. 

  Maziko yanatarajiwa kufanyika kesho Jumamosi tarehe 27.06.2015 majira ya saa tisa alasiri katika makaburi ya Kinondoni, kabla ya mazishi kutakuwa na misa ikifuatiwa na shughuli ya kuaga mwili wa marehemu zitakazoanza majira ya saa tatu asubuhi hapo kesho. 

   BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) leo limefungua kozi ya makocha wa mpira wa miguu kwa watoto na vijana kwa nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha vijana wengi wanapata nafasi ya kufundishwa mpira na kuucheza mpira kuanzia katika umri mdogo.

  Akifungua kozi hiyo, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema ili nchi/Taifa lifanikiwe katika soka ni lazima kuwekeza katika mpira wa watoto na vijana ambao makocha hao ni sehemu ya uwekezaji huo.
  “Tumekua na mashindano ya Taifa U-13, kikosi cha timu ya Taifa ya U-15 ambayo inashirikisha vijana wadogo, vijana hao wanapaswa kupata malezi na mafunzo yenu waalimu ili wafikiapo kuchezea timu za Taifa wawe wamekua kwenye msingi bora wa kuujua mpira wa miguu” alisema Mwesigwa.

  Naye mkufunzi wa FIFA wa kozi hiyo ya makocha kutoka nchini Ujerumani, Eric Muller amesema hata ujerumani imefanikiwa baada ya kuwekeza katika soka la vijana, mwaka 2000 kwenye fainali za Euro nchi yao ilishika nafasi ya mwisho katika msimamo kundi lao kwa kupata poniti moja, lakini uwekezaji walioufanya kwenye soka la watoto na vijana umewapelekea kutwaa Ubingwa wa Dunia mwaka 2014.
  Washiriki wa kozi hiyo ni makocha wa timu za vijana za mikoa yoye Tanzania, ambao watashirki na timu zao za mikoa katika michuano ya Copa Coca Cola mwaka huu.

  Kozi hiyo ya makocha wa timu za watoto/vijana inayoendeshwa na wakufunzi wa FIFA, Ulric Mathews kutoka shelisheli na Eric Muller kutoka nchini Ujerumani itamalizika jumatatu tarehe 29 Juni, 2015.


  0 0

   Msimamizi wa masuala ya ushiriki wa watanzania wa wizara ya nishati na madini Neema Apson akizungumzia jinsi wizara ya nishati na madini inavyoshiriki katika kuhakikisha taarifa zinawafikia wananchi kwa usahihi kuhusiana na mafuta na gesi katika ukumbi wa mikutano wa British Cancil jijinin Dar es Salaam leo. pia wizara hiyo itaunda kitengo maalumu kwaajili ya kusimamia masuala ya gesi na mafuta na kuwajulisha wananchi kushiriki vyema katika nishati zitolewazo hapa nchini.
   Mkuu wa Biashara wa British Concil Hugh Penrhyn Jones akizungumza katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa British Cancil jijinin Dar es Salaam leo.
   Mratibu wa kitengo cha uwajibikaji wa makampuni na mazingira-kituo cha sheria na haki za binadamu,Wakili Flaviana Charsles akiuliza swali katika mkutano wa kujadili masuala ya mafuta na gesi pamoja na changamoto zake kwa jamii katika mkutano uliofanyika ukumbi wa mikutano wa British Cancil jijinin Dar es Salaam leo.
   Baadhi ya wadau wa maendeleo ya mafuta na gesi wakimsikiliza mtoa maada katika ukumbi wa mikutano wa British Cancil jijinin Dar es Salaam leo.(Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)

  0 0

   Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akifungua mkutano wa wanahisa wa benki hiyo katika Hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam.
   Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambwa akizungumza wakati wa mkutano wa wanahisa uliofanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya maofisa wa benki hiyo pamoja na wanahisa wakimsikiliza Dk.
  Dk. Charles Kimei.

  0 0

  SAM_3390
  SAM_3402Askofu Solomon Mwagisa ambaye ni katibu wa mkutano wa Amani na Upendo utakaofanyika leo jijini Arusha katika viwanja vya reli kwanzia saa 8 mchana hadi saa 12 jioni akielezea namna walivyojiandaa na mkutano huo,kushoto ni Askofu Mkuu wa makanisa ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini kati Solomon Massangwa(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
  SAM_3404Askofu Mkuu wa makanisa ya KKKT-Dayosisi ya Kaskazini kati Solomon Massangwa akizungumza na wanahabari jana jijini hapa kuhusu mkutano huo mkubwa wa Amani na Upendo ambapo alisema kuwa ni muhimu kwa kila mtu kuhakikisha Amani inakuwepo huku akisisitiza kuwa bila Amani hakuna kitu chochote kinachoweza kufanyika pasipo Amani
  SAM_3407Paul Malisa mwakilishi wa Askofu mkuu Josephat Lebulu wa kanisa Katoliki Arusha ,Paroko wa Parokia ya mtakatifu Theresia Arusha mjini akizungumza na wanahabari juu ya mkutano huo ambapo alisema kazi walionayo ni kuhakikisha wanapigia debe Amani hasa katika kipindi hichi kuelekea uchaguzi mkuu
  SAM_3401Eng.Tunzo Muzava ambaye ni mratibu wa mkutano huo akizungumza na vyombo vya habari jana alisema kuwa Muhubiri mkubwa wa kimataifa kutoka Marekani Will Graham anatarajiwa kuhubiri katika mkutano huo huku kwaya zaidi ya 200 kutumbuiza,Mkutano huo unashirikisha makanisa yote ya Arusha

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanja cha Ndege cha Guang Dong cha nchini China, Bw. Wen Wenxing (kushoto), akimpatia zawadi Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire, leo asubuhi baada ya ugeni huo kukutana na uongozi wa Wizara ya Uchukuzi leo asubuhi.
   Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanja cha Guang Dong cha nchini China, Bw. Wen Wenxing wakati ujumbe huo ulipokutana na uongozi wa Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi.
  Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Uchukuzi Tanzania, Bw. Gabriel Migire (kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa uongozi wa Wizara na ujumbe kutoka Kiwanja cha ndege cha Guang Dong kutoka nchini China, wakati ulipotembelea Wizara ya Uchukuzi, leo asubuhi. Ujumbe umeonyesha nia kuwekeza katika Viwanja vya Ndege vya Tanzania.
  (Habari Picha Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)     

  0 0

   Na Bakari  Issa Madjeshi,Globu ya jamii.
  Filamu ya Kiswahili ijulikanayo kama  Hamu ya Mafanikio ilizinduliwa rasmi  jana na Benki ya DCB katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
  Filamu hiyo imeandaliwa na DCB Commercial Benki kwa kushirikiana na Kampuni ya ConsNet,yenye lengo la kuelimisha na kuhamasisha  wateja, wadau na umma kwa ujumla juu ya umuhimu na faida za kufanya shughuli za kibenki na DCB ambazo zinabadili maisha ya wateja kwa kiasi kikubwa.
  Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Commercial Bank, Samwel Dyamo amesema moja ya changamoto zilizopo katika sekta ya benki ni jamii kukosa elimu ya kutosha juu ya huduma za Kibenki,hivyo mbali na kujitangaza, DCB imeamua kutoa elimu ya kibenki  kupitia Filamu hiyo.
  Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB, Balozi Paul Rupia amewashukuru waandaaji wa Filamu hiyo,ikiwa  Bodi ya Filamu nchini pamoja na wasanii wote walioshiriki kuigiza filamu hiyo  kwa kazi nzuri waliyoifanya.
  Pia ametoa wito kwa wasambazaji wa Filamu hiyo kuifanya  kazi  yao kimakini ili kutimiza malengo na madhumuni ya kuandaa Filamu hiyo.
  Washiriki katika Filamu hiyo ni pamoja na Tito Zimbwe,Rose Ndauka,Jackline Pentezel,Abdul Mhema,Hidaya Njaidi, Gojak na Wasanii wengine wengi. Baada ya kuzinduliwa Filamu hiyo itaonyeshwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo City Centre,Magomeni,Arnautoglu,Mnazi Mmoja,Tabata,Ukonga,Chanika,Mabibo na Kariakoo kwa nyakati tofauti kuanzia Julai mwaka huu.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Commercial Bank, Samwel Dyamo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Filamu ya Hamu ya Mafanikio 'Desire to Succeed' iliyozindulia katika ukumbi wa  Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB, Balozi Paul Rupia akizungumza katika hafla  ya uzinduzi wa Filamu hiyo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana ambapo alitoa wito kwa wasambazaji wa Filamu hiyo kuifanya  kazi  yao kwaumakini ili kutimiza malengo na madhumuni ya kuandaa Filamu hiyo.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB, Balozi Paul Rupia (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Commercial Bank, Samwel Dyamo (kulia) kwa pamoja wakionyesha DVD za Filamu hiyo.
  Baadhi ya  washiriki na wadau waliohudhuria uzinduzi wa Filamu hiyo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam,Juni 25,2015.PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

  0 0

   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na Umoja wa Madereva  Tanzania (TADWU)juu ya usajili waliopata ambao utafanya waweze kuingia mkataba wa waajiri wao na kuweza kujiunga katika mfuko wa bima ya Afya  uliofanyika katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam, Kushoto  ni Mwenyekiti wa Umoja huo,Clement Masanja, kulia ni  Katibu Mkuu  wa chama hicho Abdallah Lubala.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ,Paul Makonda akikabidhi Katiba ya Umoja wa Madereva  Tanzania (TADWU) kwa Katibu Mkuu wa Umoja huo Abdallah Lubala katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya madereva wakifurahia kupata umoja huo utakaoweka wazi juu ya ajira ya kazi zao katika katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ,Paul Makonda akiagana na madereva katika Hoteli ya Rombo jijini Dar es Salaam.( PICHA NA EMMANUEL MASSAKA.)

  0 0

   Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto), akigana na wafanyakazi wa kampuni ya Uhuru Publications Ltd (UPL), inayochapicha magazeti ya Uhuru na Mzalendo waliofika kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya mazungumzo naye na baadae kuapata muafaka kufuatia mgogoro uliokuwa ukifukuta katika kampuni hiyo.
   Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wa pili kushoto), akifurahia jambo na wafanyakazi wa kampuni ya Uhuru Publications Ltd (UPL), inayochapicha magazeti ya Uhuru na Mzalendo waliofika kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya mazungumzo naye na baadae kupata muafaka kufuatia mgogoro uliokuwa ukifukuta katika kampuni hiyo.
  Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (mwenye miwani nyuma), akifurahia jambo na wafanyakazi wa kampuni ya Uhuru Publications Ltd (UPL), inayochapicha magazeti ya Uhuru na Mzalendo waliofika kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya mazungumzo naye na baadae kupata muafaka kufuatia mgogoro uliokuwa ukifukuta katika kampuni hiyo.
  Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (wa pili kushoto), akiagana na Kaimu Mhariri Mtendaji wa kampuni ya Uhuru Publications Ltd (UPL), inayochapicha magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Ramadhan Mkomwa baada ya kikao na wafanyakazi wa kampuni hiyo, waliofika kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya mazungumzo naye na baadae kupata muafaka kufuatia mgogoro uliokuwa ukifukuta katika kampuni hiyo.
  John Badi

  0 0

  Mwanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Fedha mwaka 11, Khalfan Kikwete (kulia) ambaye alishinda medali ya dhahabu pamoja na mwenzake Seif Yahya Mhata wakizungumza na waandishi wa habari. Mwanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Fedha mwaka 11, Khalfan Kikwete (kulia) ambaye alishinda medali ya dhahabu pamoja na mwenzake Seif Yahya Mhata wakizungumza na waandishi wa habari.Mwanafunzi Veronica Samuel Ndomba akielezea (kulia) katika picha na abendera ya nchi yake mara baada ya ushindi katika mashindano ya Genius Olympiad hivi karibuni. Mwanafunzi Veronica Samuel Ndomba akielezea (kulia) katika picha na bendera ya nchi yake mara baada ya ushindi katika mashindano ya Genius Olympiad hivi karibuni.Picha ya Mwanafunzi Prince Mwemezi Muzamil Katunzi aliyoipiga na kushinda katika mashindano ya Genius Olympiad. Picha ya Mwanafunzi Prince Mwemezi Muzamil Katunzi aliyoipiga na kushinda katika mashindano ya Genius Olympiad.Wanafunzi wa Shule za Feza Tanzania walioshinda mashindano ya taaluma kimataifa ya 'Genius Olympiad' katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wao.Wanafunzi wa Shule za Feza Tanzania walioshinda mashindano ya taaluma kimataifa ya 'Genius Olympiad' katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wao.

  Mwanafunzi Yahya Mhata ambaye kwa pamoja wamebuni mfumo huo, ameuelezea kuwa ni mzuri na rafiki wa mazingira huku ukiweza kuhifadhi kumbukumbu za mawasiliano kwa uhakika tofauti na ule wa kadi za makaratasi ambao wengi hupoteza kadi hizo na kujikuta wakipoteza mawasiliano muhimu. 

   Wanafunzi wengine wa Shule za Fedha ambao ni Prince Mwemezi Muzamil Katunzi, Goodluck Komba, Sajjad El-Amin na Veronica Samuel Ndomba ambao kila mmoja ameshinda medali za fedha katika makundi ya ushindani tofauti chini ya usimamizi wa mwalimu Metin Er wa Masomo ya Biashara, Fedha International School walieleza kunufaika na mashindano kitaaluma na upeo. 

   Mwanafunzi Mwemezi Muzamil Katunzi, ambaye aliwasilisha picha yenye ujumbe wa mazingira na kushinda alisema picha hiyo aliipiga eneo la viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam ikielezea namna binadamu wanaathiri mazingira kwa kuchoma moto hovyo na kuleta matatizo mengine duniani. Kwa upande wao wanafunzi Goodluck Komba na Sajjad El-Amin waliwasilisha andiko la mradi wa kutengeneza mkaa kwa kutumia makaratasi taka ambao ulishika nafasi ya tatu katika mashindano ya Genius Olympiad yaliyofanyika jijini New York. 

  Mwanafunzi Komba alisema mradi wao ni rafiki wa mazingira na ukitumika utaokoa sehemu kubwa ya uharibifu wa mazingira. Kwa upande wake msichana pekee aliyeshinda katika mashindano hayo, Veronica Samuel Ndomba alisema andiko lake lilishinda kwenye kipengele cha 'Mazingira Yetu' na aliandika kuonesha namna elimu ya mazingira inaweza kutolewa na kulinda uharibifu mkubwa wa mazingira unaofanywa katika shughuli mbalimbali za binadamu.

   Naye msimamizi wa wanafunzi hao, mwalimu Metin Er alisema kundi hilo la wanafunzi mbali na kujijenga kimaarifa kwa wanafunzi hao wameiletea sifa Tanzania kwani kwani mashindano hayo ya kitaaluma yalishirikisha nchi mbalimbali zikiwemo USA, Romania, Nigeria, Tunisia, Holland, Turkmenistan, Kazakhstan and Russia. Shule za Fedha International School zimekuwa zikifanya vizuri kitaaluma kitaifa na kimataifa jambo linaloendeleza umaarufu wa shule hizo kila uchao. *Imeandaliwa na www.thehabari.com


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu kushoto wakionyesha magwanda yaliokabidhiwa kwao aiyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wilaya ya Magu,Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi kutoka CHADEMA.Zaidi ya wananchama 53 kutoka vyama vya upinzani walijiunga na CCM wakiwemo Chadema 28 na ACT 12 na wengine kutoka vyama vingine.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea magwanda ya aliyekuwa  Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Wilayani Magu  Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi, kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Miraji Mtaturu.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi zilizokuwa  za wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo na vyama vingine mara baada ya wanachama hao kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kituo cha mabasi cha Kisesa wilayani Magu mkoani Mwanza.

  Katibu Mkuu huyo amempokea aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA) Wilayani Magu  Bi. Juliana Kachilu ambaye amejiunga na Chama cha Mapinduzi , Kinana yuko katika ziara ya kikazi  ya mkoa Mwanza akimalizia mkoa wa mwisho wa Tanzania baada ya kuzunguka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani akipita katika majimbo yote, wilaya zote hapa nchini  na nusu ya Kata na vijiji kwa muda wa miaka miwili akikagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015.

  Kinana amesikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzipatia ufumbuzi huku akihimiza uhai wa CCM ambapo pia  katika ziara hiyo amekuwa akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Nape Nnauye . 
  Baadhi ya Kadi za wafuasi wa vyama mbalimbali walizoamua kuachia ngazi na kuhamia chama CCM.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu  Kinana akiwahutubia wakazi wa mji wa Kisesa mapema jioni ya leo alipokuwa akimaliza ziara yake ndani ya jimbo la Magu.


   Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ndugu Magesa Mulongo akizungumza na wananchi kuhusu kuiagiza mamlaka ya Mapato TRA na kikosi cha Usalama Barabarani kuenda katika wilaya kwa ajili ya kutoa huduma za utoaji wa leseni za uendeshaji vyombo vya moto na kukusanya kodi mbalimbali za vyombo vya moto ili kupunguza urasimu wa huduma hiyo ambazo zimekuwa zikipatikana kwenye miji mikuu ya mikoa peke yake.

  PICHA NA MICHUZI JR-MAGU-MWANZA

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  A prominent entertainment monthly magazine The Vibe which published by ABC Bros  was re launched and now will be distributed free to the readers. This will make it Tanzania’s number 1 FREE entertainment Youth Magazine
  The magazine Editor in Chief Allan Rwechungura said that since the magazine was launched,it has achieved the objectives and now is  leading entertainment magazine in Tanzania. “On behalf of Vibe Magazine team, I deeply appreciate your support and its great to know that we can count on you ”.Rwechungura said from this month the Vibe Magazine will be distributed  for free to its readers and advertisers, which means the increase number of readership and more exposures for advertisers,  “We promise to bring more news on entertainment, sports as well as other issue relevant to entrepreneurship skills targeting to empower and educate Tanzanians youths,hope our readers will enjoy more”
  He said the magazine will be distributed in prime locations in the country,in saloons/barbershops, in colleges and universities as well as remote areas to enable many readers to get entertainment news,and also will be available online.

  0 0


  0 0


  0 0

  KATIKAkuhakikisha kuwa msikilizaji wa Efm kupitia kipindi chake cha Joto la Asubuhi anapata taarifa za kutosha na zilizosheheni masuala mbalimbali ya Kijamii, kuanzia Juni 29, Jumatatu, kitakuwa na habari kutoka mikoa mbalimbali nchini katika kipengele cha kona zote.

  Msimamizi Mkuu wa Kipindi hicho Dennis Ssebo ameitonya Blog ya Jamii kuwa tofauti na utaratibu wa kuripoti matukio uliozoeleka Joto la asubuhi litakuwa likizimulika na kuzichambua habari hizo zilizoandikwa na wabobezi wa mambo katika tasnia ya habari kuanzia saa kumi na mbili hadi saa kumi na mbili na nusu asubuhi.

  Joto la asubuhi ni kipindi cha asubuhi ambacho kinaruka hewani kupitia 93.7 EFM kila siku Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa kumi na mbili hadi saa tatu kamili asubuhi chini ya watangazaji wake mahili Dennis Ssebo na Adella Tillya.

older | 1 | .... | 884 | 885 | (Page 886) | 887 | 888 | .... | 3278 | newer