Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 882 | 883 | (Page 884) | 885 | 886 | .... | 3278 | newer

  0 0

  Refarii wa mchezo wa masumbwi nchini Ally Bakari Champion  akiwa na mke wake Aisha Chilumba  baada ya kuowa hivi karibuni maeneo ya Vingunguti Dar es salaam

  Ally Bakari Champion akiozeshwa

  Refarii wa mchezo wa masumbwi nchni kushoto akiwa na mke wake Aisha Chilumba  baada ya kuowa hivi karibuni maeneo ya Vingunguti Dar es salaam

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, akiwaonesha waandishi wa habari (hawako pichani) moja kati ya tiketi 20 zilizotolewa na Benki hiyo kwa Chama cha Mchezo wa Pete Tanzania (CHANETA) ili kufanikisha safari ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Queens) kwenda nchini Botswana kwa ajili ya kushiriki michuano ya mabingwa wa Afrika benki hiyo imetoa zaidi ya milioni arobaini ili kufanikisha safari hiyo, Pamoja nae katika picha ni Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Kibira, na nahodha wa timu hiyo Sophia Komba.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja (Katikati) Pamoja na Mwenyekiti wa CHANETA. Anna Kibira, Nahodha wa Taifa Queens, Sophia Komba, ( kushoto) Baraka Enock, Meneja Uendeshaji Covenant Bank, na Allen Allex wa Wizara ya Michezo kwa pamoja wakiwa wameshika tiketi za ndege zilizotolewa na Benki hiyo kwa timu ya Taifa ya mpira wa Pete (Taifa Queens) ili kufanikisha safari ya kwenda nchini Botswana kwa ajili ya kushiriki michuano ya Mabingwa wa Afrika Benki hiyo imetoa zaidi ya Milioni Arobaini.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, akikabidhi tiketi za ndege kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Pete Tanzania (Taifa Queens) wakati wa Hafla ya kutangaza udhamini wa benki hiyo ili kufanikisha safari ya kwenda nchini Botswana kwa ajili ya kushiriki michuano ya Mabingwa wa Afrika Benki hiyo imetoa zaidi ya Milioni Arobaini.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, akimkabishi tiketi ya ndege, nahodha wa Taifa Queens, Sophia Komba wakati wa hafla ya kutangaza udhamini wa benki hiyo ili kufanikisha safari ya timu ya Taifa (Taifa Queens) kwenda nchini Botswana kwa ajili ya kushiriki michuano ya Mabingwa wa Afrika Benki hiyo imetoa zaidi ya Milioni Arobaini.

  0 0

  MABINGWA wa Ligi kuu soka Tanzania bara mwaka 1988,Coastal Union,Wagosi wa Kaya imeingia mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja ambaye ni raia wa Uganda kuifundisha timu ya Coastal Union katika msimu ujao wa Ligi kuu soka Tanzania Bara itakayoanza Mwezi Agosti mwaka huu . Utiliaji wa saini wa Kocha huyo ulifanyika leo  mjiniTanga  na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa timu ya Coastal Union akiwemo Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Albert Peter na Katibu Mkuu wa timu hiyo,Kassim El Siagi. 
  Akizungumza baada ya kumalizika zoezi hilo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa kutokana na umahiri aliokuwa nao kocha huyo wanaimani kubwa ataipa mafanikio timu hiyo hasa katika harakati za kuhakikisha inafanya vizuri ligi kuu msimu ujao. 
  Amesema kuwa uwezo wa Kocha huyo utaleta matumaini makubwa ya mafanikio hasa ukizingatia ni kocha mwenye uwezo mzuri wa kufundisha na kuzipa mafanikio timu hivyo tunaamini kuja wake kwetu itakuwa chachu katika maendeleo. 
  Mayanja ambaye aliwahi kuzifundisha timu za soka Kiyuvu FC ya Rwanda,Timu ya Mamlaka ya Mapato nchini Uganda (URA),Vipers FC ya Bunamwaya na KCC ya Uganda amesema kutua kwenye timu hiyo kumpa faraja kubwa hivyo atahakikisha anatoa mchango wake kwenye kuipa mafanikio. Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuhakikisha timu hiyo inang’ara katika michuano ya Ligi kuu msimu ujao ikiwemo kubadili aina ya mchezo wa timu hiyo ili iweze kupata mafanikio kwa kuweka umoja baina ya wachezaji mashabiki, wanachama na wapenzi. 
  Amesistiza pia umuhimu wa mshikamano baina ya wapenzi,wanachama na viongozi ili kuiwezesha timu hiyo kuchukua Ubingwa wa Ligi kuu msimu ujao kwani dhamira yake ni kutaka kuona timu hiyo inang’ara kwenye medani za kitaifa na kimataifa.
   Kocha Mkuu mpya wa timu ya Coastal Union,Jackson Mayanja kushoto akisaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu hiyo kulia ni Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi,Picha kwa Hisani ya Coastal Union.
  Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi akipokea mkataba wa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo,Jackson Mayanja mara baada ya kuusaini leo ambapo amesaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha timu hiyo,katika Halfa iliyofanyika mjini hapa,Picha kwa Hisani ya Coastal Union.

  0 0

  Na Hassan Silayo-MAELEZO 
  Mawakala wa Forodha nchini wameaswa kujisajili katika mfumo wa uondoshaji mizigo wa Himaya moja ya Forodha ya Afrika Mashariki (Single Custom Territory) utakao anza kutumika hivi Karibuni. 
  Hayo yamesemwa na Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi wakati mkutano na Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) Bw. Kabisi alisema kuwa mawakala wa forodha nchini hawana budi kufanya hivyo ili kuwezesha uondoshwaji wa mizigo kwa haraka zaidi pindi mfumo huo utakapoanza kutumika. 
  “Sasa tunaelekea katika matumizi ya Himaya moja ya Forodha ya Afrika Mashariki yaani Single Custom Territory ili kuwa na uwezo wa kupata huduma kwa kutumia mfumo huo pindi matumizi yatakapoanza mapema ili kuondoa usumbufu utakaoweza kutokea”,alisema Bw. Kabisi 
  Bw. Kabisi aliongeza kuwa mpaka sasa ni makampuni mawili (2) ya mawakala waliojisajili mpaka sasa, na kwamba  mawakala wa forodha hawana budi kuendelea kuwa waamifu ili waendelee kuongoza katika makusanyo ya fedha kwa mwaka ujao ambapo kwa mwaka huu wamechangia kwa asilimia 40 ya mapato ya serikali. 
  Naye Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) Bw. Stephen Ngatunga alisema kuwa wataendelea kushirikiana na Mamlaka la Mapato Tanzania (TRA) katika kuhakikisha wanaifanya idara ya forodha inafanya vizuri katika makusanyo ya fedha. 
  Pia Bw. Ngatunga aliitaka serikali kuendelea kushughulikia changamoto mabalimbali zinazoikabili idara hiyo ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu na kuendelea kuongoza katika makusanyo ya mapato ya serikali.
  Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi akiongea na viongozi wa Chama cha Mawakala wa Forodha na kuwataka mawakala wa Tanzania kujisajili katika mfumo wa uondoshaji wa Himaya moja ya Forodha(SINGLE CUSTUM TERRITORY) ili kuwezesha uondoshwa     wa mizigo kwa haraka zaidi pindi mfumo huo utakapoanza kutumika kwani mifumo huo na watanzania tayari zinawasiliana mpaka sasa, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kushoto ni Naibu Kamishna wa Forodha Dkt. Patrick Mugoya

  Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) Bw. Stephen Ngatunga akiongea  na viongozi wa Chama cha Mawakala wa Forodha na wawakilishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo aliipongeza serikali kupitia Mamlaka hiyo katika kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri kwa mawakala wa forodha na kuiasa kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali katika sekta hiyo ili kuiwezesha serikali kupata mapato kwa maendeleo ya Taifa, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kulia ni Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi.

   Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) wakimsikiliza Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam

   1-    Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) wakichangia wakati wa mkutano uliokutanisha Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
  Mwanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) akichangia wakati wa mkutano uliokutanisha Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). 
  PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

  0 0

  Shirika la Jambo Bukoba limepata Mwaliko kuhudhura Kongamano la Michezo Nchini Ujerumani lenye Malengo ya Kuinua Wanawake kupitia Kwenye Michezo(Soccer). Wakiwa Ughaibuni Ujerumani Watajifunza haki za Wanawake Kiujumla ili wawe Mabalozi kwa wenzao hapa Hapa Nyumbani. Kongamano hilo la Michezo linaloitwa Discover Football litashirikisha Nchi 100 na Tanzania itawakilishwa na Shirika hilo la Jambo Bukoba lenye Maskani yake Mkoa wa Kagera. Safari hiyo itaanza kesho juni 25, 2015. Picha na Faustine Ruta, Bukoba

  Jambo Bukoba ni Shirika lisilokuwa la Serikali linalofanya kazi mkoani Kagera kwa kushirikiana na serikali ya Mkoa. 
  Mwanzilishi wa Jambo Bukoba ni Bw. Clemence Mlokozi ambaye asili yake ni Mkoani Kagera katika Wilaya ya Missenyi Kijiji Ishozi na anaishi nchini Ujerumani. 
  Jambo Bukoba ilianzishwa Mkoani Kagera kwa kusaidia watoto hasa wanafunzi wa shule za msingi kuanzia miaka 5 hadi 19 kujenga afya zao kimichezo ili kujikinga na Maabukizi ya UKIMWI, kuweka haki sawa katika elimu kupitia michezo kwa wasichana na wavulana. 
  Shirika hili chini ya mwanzilishi wake Bw. Mulokozi tangu kuanzishwa kwake mkoani Kagera limekuwa likiwafunza watoto katika shule za msingi kila wilaya michezo midogo midogo ya kujenga ushirikiano wa pamoja hasa watoto wa kike kujiamini na kushirikiana zaidi na wenzao wa kiume.

  Kongamano hilo litafanyika katika Mji wa Berlin, Germany kuanzia tarehe 27 juni - 06 julai, 2015 na wawakilishi hao watakaa huko juma moja/ siku saba. Msafara huo Unaongozwa na Gonzaga Stephen ambaye ni Meneja wa Mradi huo wa Jambo Bukoba akisaidiana na msaidizi wake Bi. Imani Paul. Pia watandamana na Walimu mmoja mmoja kwa kila Shule za Msingi baadhi kutoka Kila Wilaya saba.
  Walimu hao ni Peace Saleand kutoka Biharamulo- Rubondo Shule ya Msingi. Grace Wamara kutoka Shule ya Msingi Tumaini ambayo Ipo Bukoba Mjini. Alistidia Bijura kutoka Shule ya msingi Kaisho - Kyerwa.

  Elizabeth John kutoka Rulenge Shule msingi - Ngara
  Abela Ndeyokobora Kutoka Shule ya Msingi Kayanga - Karagwe
  Jeni Mulokozi Kutoka kashekya Shule ya Msingi - Misenyi
  William Magosa kutoka Karalo Shule ya Msingi -Karagwe

  Kushoto ni Ni Meneja wa Mradi wa Jambo Bukoba Gonzaga Stephen akiwa na Walimu ambao wataiwakilisha Tanzania kupitia Shirika hilo la Jambo Bukoba Huko Berlin Ujerumani hivi karibuni kwenye Viwanja vya Gymkana Bukoba Mjini.
  Washiriki ambao wataiwakilisha Tanzania kwenye Kongamano/Tamasha hilo la Michezo la Discover Football, Picha na Faustine Ruta, Bukoba

  0 0

  Na Mwashungi Tahir na 
  Rahma Khamis-Maelezo Zanzibar 
  Chama cha Mapinduzi CCM kimelaani kitendo kilichofanywa na Wajumbe wa Baraza la wawakilishi kupitia chama cha Wananchi (CUF) kutoka ndani ya kikao halali cha Baraza la Wawakilishi wakati wa mjadala wa kupitisha Mswaada wa sheria wa matumizi ya fedha za serikali kwa mwaka 2015/2016 ukiwa bado unaendelea. 
   Akizungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake Kisiwandui Naibu Katibu mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai amesema kitendo kilichofanywa na Wawakilishi hao hakikuwafurahisha kwani kinaashiria uvunjifu wa amani ulipo nchini.
   Amefahamisha kuwa katika hali hiyo isiyo ya kawaida Wajumbe kutoka CUF waliamua kutoka nje ya Baraza baada ya Juma Duni Haji kuwasilisha hoja binafsi iliyodai “CUF hairidhishwi na Zoezi la uandikishaji la daftari la kudumu la wapiga kura linaloendeshwa Wilaya ya Magharibi kwa kugubikwa na udanganyifu wa kuandikisha watu wasio na sifa. 
   Hata hivyo Vuai amedai kuwa Madai ya CUF hayana msingi wowote na kwamba Lengo lao ni kuwazuia watu Unguja wasipate fursa ya kuandikishwa ipasavyo kwenye Daftari hilo ili kujiandalia mazingira ya Ushindi. 
   Aidha Vuai ametoa wito kwa WanaCCM kujitokeza kwa wingi katika Vituo vya Uandikishaji ili waweze kutimiza haki yao ya kidemokrasia. Ameviomba Vyombo vuya Dola viweke ulinzi wa kutosha ili wananchi wote wapate haki yao ya kuandikishwa katika Daftari bila wasiwasi wowote. 
   Vuai amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuweza kusimamia Maendeleo ya haraka ya Zanzibar jambo ambalo limewezesha ukuaji wa uchumi na huduma mbali mbali za kijamii. 
   Amesema mafanikio mengine ya kupongezwa Dkt Shein ni pamoja na kusimamia Amani na utulivu katika Visiwa vya Unguja na Pemba jambo ambalo limewezesha wazanzibar wote kushiriki katika shughuli zao za kisiasa,kiuchumi na kijamii.
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizungumza na Waandishi wa Habari katika Afisi kuu CCM Kisiwandui ambapo amelaani hatua ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha CUF kugomea Vikao vinavyoendelea vya Baraza la Wawakilishi hapo Jana.Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakichukuwa maeelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika Afisi kuu CCM Kisiwandui. Vuali amelaani hatua ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Chama cha CUF kugomea Vikao vinavyoendelea vya Baraza la Wawakilishi hapo Jana. picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar

  0 0

  Sehemu ya Umati wa wakazi wa wilaya ya Kwimba na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika katika mkutano wa hadhara,Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo, wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la Kwimba jioni ya leo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu,Ndugu Kinana alikemea tabia ya wapinzania kuwahadaa vijana nchini kuwa wakiingia madarakani wataweza kuwatekelezea kila kitu,aidha aliwataka vijana wa kitanzania kuacha kabisa kuhadaika na baadhi ya Wanasiasa ambao wamekuwa wakiwapotosha na kuamini kila kitu kitapatikana bila kufanya kazi na kujituma.

    Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani Kwimba, ambapo aliitaka jamii wakiwemo mabalozi wa mashina kuimarisha ulinzi kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO), ili kuepusha mauaji dhidi yao.
  Wananchi wilaya ya Kwimba wakiwa wamekusanyika katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo, wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la Kwimba jioni ya leo.
   Mbunge wa Jimbo la Kwimba,Mh., Shanif Mansoor akiwahutubia Wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mpira wa Ngudu, wilayani humo, wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo,wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake ndani ya jimbo hilo la Kwimba jioni ya leo. 
   Aliyekuwa Mwenyekiti wa  CHADEMA katika Kijiji cha Ilula kata ya Ilula wilayani Kwimba,ndugu AmaraMateremki  akizungumza baada ya kuamua kukihama chama hicho na kuijunga na CCM wakati wa mkutano huo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akionesha baadhi ya kadi za wafuasi wa chama cha CHADEMA kuhamia CCM.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akikabidhi msaada wa baiskeli kwa watu wenye ulemavu Mjini Ngudu. Msaada huo umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoor pichani shoto.
  Mmoja wa viongozi kutoka kikundi cha akina mama kiitwacha UAMSHO akimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana mara baada ya kukabidhiwa vyerehani vilivyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor .  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wanaCCM na Wananchi wa Jiji la Arusha waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Msikiti Mkubwa uliopo mbele ya Ofisi za CCM Mkoa wa Arusha, leo Juni 24, 2015. Jumla ya WanaCCM 120, 335 wa jiji la Arusha wamemdhamini Mh. Lowassa.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za WanaCCM wa Mkoa wa Arusha waliomdhamini ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Anaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini, Ferouz Bano, ambapo WanaCCM wapatao 120, 335 wamemdhamini Mh. Lowassa.

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Jiji la Arusha waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa ulipo mbele ya Ofisi za CCM Mkoa huo, leo Juni 24, 2015, wakati alipofika kwa ajili ya kupata udhamini utakaomuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
  Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akimpa pole Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya CCM, Mathias Manga, aliyejeruhiwa kwa risasi jana usiku na watu wasiofahamika, wakati alipomwita jukwaani kuwasalimia WanaCCM wa Arusha.
  Baadhi ya Wazee wa Kabila la Kimasai wakimbariki Mh. Lowassa katika Safari yake ya Matumaini.


  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry Ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Sheikh Suleiman Lolila  Ikulu jijini Dar es salaam leo.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza  Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry Ikulu jijini Dar es salaam leo.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya kumbukumbu  na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeiry na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Sheikh Suleiman Lolila Ikulu jijini Dar es salaam leo.

  0 0


  Na Bashir YAkub
  Sura  ya  29  Sheria  ya ndoa  imeeleza  mambo  mengi . Baadhi  yanajulikana  na  baadhi  hayajulikani.  Wakati  mwingine  hata  baadhi  ya yanayojulikana   haijulikani  kama  yameruhusiwa  na  sheria  au  yanafanyika  kimazoea.  Na  hapa  ndipo  inapoibukia  migogoro mingi  ambayo  tunayoshuhudia  mahakamani  na  hata nje  ya  mahakama. Aidha  sheria  hii  imebeba  mambo  mengi  ya  talaka, matunzo  ya  watoto  na  mwanamke, jinai  za  unyanyasaji  wa  kijinsia, ndoa  haramu  na  halali  na mengine  mengi  kuhusu  familia  na  ndoa. Mengi  kati  ya haya  yameishaelezwa  kwa  anayetaka  kuyajua  basi   atembelee SHERIA  YAKUB  BLOG  atafute atapata  humo.


   Leo  ni  muhimu  kuzungumzia  jambo  jingine  muhimu   ambalo  nalo  limekuwa  likitatiza   na kuleta  shida  kwa  wanandoa. Ni  kuhusu   ruhusa  ya kuoa  na  kuoa  mke  zaidi  ya  mmoja. Ndoa  zipo  aina  nyingi  na  upo  uhuru  wa  mtu kufunga  ndoa  kutokana  na  maamuzi   yake  na  mwenza  wake  wanavyoamua.  
  Yumkini   unapoamua  kufunga  ndoa  ya  aina  fulani  yakupasa  pia  uwe  umejua  matokeo, athari  za  ndoa  hiyo. Kila  aina  ya ndoa utakayofunga   ujue  wazi  kuwa  itaambatana  na   haki  fulani  , wajibu  fulani  na  mipaka  fulani.  Hakuna  ndoa utakayoifunga  iwe moja  kwa  moja bila  mipaka  .  Na  hili  hasa  ndilo  linalojadiliwa  na  makala  haya.

  0 0


  Zimekusanywa na 
  Samuel Kamugisha


  CHANNEL 10
  *Baraza la Taifa la elimu ya ufundi NACTE lafuta usajili wa vyuo 3 na 16 kushushwa hadhi katika jitihada za kulinda ubora wa elimu nchini. http://youtu.be/2HosRmHz7lU

  *Jaji Augustino Ramadhani apata wadhamini mkoani Kilimanjaro huku akisema endapo atachaguliwa atashirikiana na wagombea wenziwe. http://youtu.be/qU7V9hQfIlI
   *Kada wa CCM Edward Lowassa asema hababaishwi na kashfa,vitisho na matusi anavyokumbana navyo kwani ana nia ya dhati ya kuongoza taifa. http://youtu.be/E3B2b4y_uiQ 
   *Chama cha Mapinduzi Zanzibar kimesema kitendo cha wajumbe na mawaziri wa CUF kususia kikao cha Bajeti ni kinyume cha Katiba. http://youtu.be/2UiljpCNCho    
   *Jaji mkuu Othman Chande azindua majarida ya sheria yanayo husu maamuzi ama hukumu za mahakama kuu ikiwa ni mara ya kwanza nchini. http://youtu.be/pvJ_xL6GZD4
   *Kituo cha sheria na haki za binadamu kimezindua taarifa ya haki za binadamu na biashara 2014 huku ikionyesha ukiukwaji mkubwa wa haki. http://youtu.be/VtNbOW6H3tM  
   *Wananchi wilayani Misungwi waiomba serikali msaada wa chakula kufuatia njaa katika wilaya hiyo baada ya mvua kusomba chakula chao. http://youtu.be/gYD1YcRD6uA 
   STAR TV NEWS
  *Raisi Kikwete ataka Tanzania kutondokana na utegemezi huku akitaka raisi ajaye kuwekeza mageuzi makubwa ya sayansi na teknolojia.  http://youtu.be/zRVrFA5SunQ 
   *Dr. Mwele Malecela awataka wanawake nchini kutumia fursa ya uchaguzi mkuu ujao kuhakikisha wanawania uongozi ili kuwa miongoni mwa vyombo vya maamuzi nchini. http://youtu.be/XJBQMYwTJRM  
   *Ajali ya moto yatokea katika msikiti wa Masjid Omar jijini Dar es salaam huku sheikh wa msikiti huo akiwataka waumini wake kuwa watulivu. http://youtu.be/qlm9AeNgQGA 
   *Njia mpya ya utalii yabuniwa nchini itakayo wafanya watembelee vituo mbalimbali ya asili nchini.http://youtu.be/m41j6KgBbmU    
   AZAM TV NEWS
   *Madaktari wasema mavazi aina ya skin Jeans yanaharibu misuli na mishipa ya damu hivyo kuleta madhara kiafya.http://youtu.be/72C-dyJvjLI   
   *Vijana washauriwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha BVR ili kupata fursa ya kuchagua viongozi wanao wahitaji .http://youtu.be/bHPSBbD9ozU  
  *Wazee wasiojiweza na walemavu mkoani Mwanza wanakabiliwa na hali ngumu ya kimaisha baada ya Mzabuni kusitisha utoaji huduma kwa wazee hao kwa kinachodaiwa kuwa deni kubwa. http://youtu.be/12_tDsCctXw     
  TBC NEWS
  *Watu 6 wakiwemo raia 3 wa Kenya watiwa mbaroni mkoani Mara kwa kosa la kujaribu kuvuruga zoezi la uandikishaji wapiga kura BVR. http://youtu.be/uGcO0gnyNVo       
  *Jeshi la polisi Mkoani Manyara linawashikilia watu 3 kwa tuhuma za kujiandikisha mara mbili katika daftari la wapiga kura.http://youtu.be/G9BOu7RITL0
   *Chama cha Mapinduzi kimeishauri serikali kurejesha mswada wa habari kwa wadau wa habari kabla ya kuupeleka bungeni ili kuweze kupatika muafaka. http://youtu.be/PGkhpqD-dxg   
   *Kamati kuu ya CCM inatarajiwa kukutana mwishoni mwa wiki hii mjini Dodoma chini ya mwenyekiti wake Dr.Jakaya Mrisho Kikwete. http://youtu.be/Skg38Hrx0r4   


  0 0


  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa wito wa kutunza mali asili na mazingira kwa sababu ni urithi kwa vizazi vijavyo. 
  Aliongea hayo alipokuwa akifungua mkutano wa Wadau unaohusiana na Azimio la Gaborone jijini Dar es Salaam. 
  Aliongeza kuwa idadi ya watu duniani inazidi kuongezeka hivyo basi ni jukumu la kila mmoja kuacha kukata miti hovyo, kuacha kuchoma misitu na vitu vyote vinavyosababisha uharibifu wa mazingira kwa sababu upo uhusiano wa karibu sana kati ya umaskini na uharibifu wa mazingira. 
  'Uharibifu wa mazingira huongoza kusababisha umaskini' alisema Bi Samia. Aidha alisisitiza kuwa matokeo yataonekana iwapo maazimio yaliyopendekezwa katika Azimio la Gaborone yatatiliwa maanani. 
  Mkutano huo wa Wadau wa Azimio la Gaborone umeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Serikali ya Botswana. 
  Wadau mbalimbali wa mambo ya mazingira kutoka Wizara na Taasisi za Serikali wamehudhuria Mkutano huo.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akifungua Mkutano wa Wadau unaohusiana na Azimio la Gaborone juu ya utunzaji Mazingira jijini Dar es Salaam.
  Mtoa mada katika Mkutano huo Bwana Carlos Manuel Rodriguez akiwasilisha mada yake 
  Sehemu ya Wadau wa Mkuatano huo wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais-Muungano, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano huo.
  Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais-Muungano, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wadau waliohudhuria Mkutano huo.

  0 0

  Good Afternoon!
  Greetings from DAR!!

  What's your take on what's going on in Tanzania? What do you think is of importance but is not being discussed? Do you feel there's a story in Tanzania to tell that isn't being told? What's your personal views?
  TRUE Africa, the new media platform, will be the place to find out what Africans are thinking, at home and abroad. And we're looking for journalists who can give their take on what's going to be the next big thing in: 
  business, politics, youth culture, music, art, film, fashion, tech, sport, lifestyle, emerging new generation and news
  We want creative contributors who can get under a story's skin and have an eye for the details others have missed. If you're original, free-thinking, with your ear to the ground, and want to tell the world your version of what's happening in Africa, whether on film, in photos or in words, please get in touch. 
  We'd like to hear about who you are 
  and what you feel needs to be said! 
  The founder of TRACE magazine and TRACE TV is about to embark on a new venture: TRUE Africa a multimedia platform with all of the next thinking on culture, sports, lifestyle, politics, art and business in Africa. See here for the official project description: http://true212.com/insights/digital-africa/2015/06/calling-writers-photographers-filmmakers-creatives/.
  The team are looking for brilliant, 
  creative minds to contribute to the platform.

  Best Regards,
  Nesia 

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
  WATANZANIA walioko Ughaibuni wanatakiwa kuelezwa vitu ambavyo vitawafanya watanzania nchini kutambua umuhimu wa watu katika masuala mbalimbali ikiwemo uchumi.
  Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari  Maelezo  jijini , Dar es Salaam, Mratibu wa Watu Waishio Ughaibuni (Diaspora),Maggid  Mjengwa amesema kutokana na kutambua uwepo watu milioni mbili wako  nje nchi ambao wanatakiwa kushirikishwa katika masuala mbalilmbali yanayoendelea nchini.
  Mjengwa amesema kutokana na kuona hilo amebuni kipindi cha Diaspora katika kituo cha TBC kwa ajili ya kuelimisha watanzania juu watu wanaoishi  nje  ya nchi  juu ya faida kwa watu hao.
  Amesema katika kipindi hicho kitatoa mwanga kwa watu wa ughaibuni na watanzania nchini juu kushirikiana katika masuala mbalimbali.
  Kwa upande wa Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa,Rosemary Jairo amesema kuwa ubunifu wa mjengwa wa kipindi cha Diaspora kitasaidia kuelimisha watanzania juu maana wakishajua itakuwa ni rahisi kupata uraia pacha.
  Amesema watanzania wengi hawajui faida ya kuwa na watu nje ya nchi katika masuala ya uchumi wanawezaje kuchangia kuleta maendeleo.
  Jairo amesema kuna watanzania  wanafanya kazi ughaibuni wanafanya vizuri hali ambayo wanaweza kufanya katika nchi yao.
  Mratibu wa Kipindi cha Diaspora,Maggid Mjengwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya kipindi cha Diaspora kitachoanza kuruka katika kituo cha TBC 1 hivi karibuni katika ukumbi wa idara ya Habari Maelezo,Kushoto ni Mkurugenzi wa Diaspora Intiative,Emmanuel Mwachullah,Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Rosemary Jairo.
  Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Rosemary Jairo akizungumza na waandishi wa habari juu ya watu wanaoishi Ughaibuni katika ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es Salaam,kushoto ni Mratibu wa Kipindi cha Diaspora,Maggid Mjengwa picha na Chalila Kibuda)

  0 0

   Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati akifungua Kongamano la nne la Kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam Jumatano.

   Rais Kikwete akipata maelezo  ya tasisi ya SEMA inayojishughulisha na utumiaji wa teknolojia ya kisaa katika kupatikana kwa maji safi na salama vijijini wakati akitembelea mabanda ya maonesho katika  Kongamano la nne la Kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam Jumatano.
   Vitabu vya kiada katika banda la Oxford University Press
    Rais Kikwete akipata maelezo toka kwa kijana Godfrey Magila ambaye amebuni king'amuzi cha kutumika kwa simu za mikononi kupata TV zote nchini kwa gharama nafuu na popote ulipo nchini.
   Rais Kikwete akipata maelezo  toka kwa Profesa Nerey Mvungi juu ya teknolojia mpya ya kupunguza ajali barabarani wakati akitembelea mabanda ya maonesho katika  Kongamano la nne la Kimataifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam Jumatano.  0 0

   Wanawake nao katika harakati za kuweka mazingira ya kupendeza katika mabanda ya maonyesho ya sabasaba leo jijini Dar es Salaam.
   Mafundi wakitoa mizigo kwaajili maonyesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam leo.
  Mwonekano wa nje katika viwanja vya sabasaba ambapo maonyesho hayo yatafanyika katika viwanja hivyo.

  HABARI NA PICHA NA EMMANUEL 
  MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

  ZIKIWA  zimebaki siku 4 kabla ya kufuguliwa kwa maonesho ya Saba Saba hapa nchini, Makampuni 1500 toka ndani ya nchi na  mengine 400 toka nje ya nchi yanatarajiwa kushiriki maonyesho  hayo.
  Akizungumza na Globu ya jamii leo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Masoko ya Nje  wa Tan Trade, Bi.   Anna Florence Bulondo amesema katika maonyesho hayo, Banda la maonyesho  la Wizara ya Elimu litakuwepo katika maonyesho hayo kwa mara ya kwanza.
  Pia amesema nchi 25 toka sehemu mbalimbali  duniani  zinatarajiwa kushiriki maonyesho hayo.
  Aidha amevitaja viingilio katika maonyesho hayo kuwa ni shilingi 3000 kwa watu wa wazima  hiyo ikiwa Julai  1-6 huku akieleza kuwa siku ya kilele Julai 7 kiingilio kitakuwa shilingi 4000 kwa watu wazima na watoto wakiingia katika maonyesho hayo kwa shilingi 1000  mpaka mwisho wa maonyesho. Picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Kitambi  ni  ile  hali  ya  tumbo  kuwa kubwa  na  kuchomoza  kwa  mbele  na  wakati mwingine  kufikia  hatua  ya  kunin’ginia.
  JINSI  KITAMBI  KINAVYO  PATIKANA
  Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati  ya bilioni 50  hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili wa binadamu.
   Kwa wanawake  seli hizo  zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye  nyonga, kiunoni na kwenye makalio.

  Kwa upande  wa  wanaume seli  hizo zinapatikana  sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio pia.
  Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili:
  i.                    Njia  ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi
  ii.                  Na  njia  ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k

  0 0

  IDADI kubwa ya waimbaji  wa nyimbo za Injili Tanzania wameonesha nia ya kumsindikiza mwenzao, Bonny Mwaitege anayetarajia kuzindua albamu yake Agosti 2 mwaka huu.

  Uzinduzi huo unaotarajia kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam ambao utashirikisha albamu tatu za muimbaji huyo zinazoendelea kurekodiwa jijini Mwanza.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama hivi sasa utaratibu wa kurekodi albamu hizo unaendelea jijini Mwanza. Msama aliyezungumza na Mwandishi wa gazeti hili jijini Mwanza alisema amepokea maombi ya waimbaji mbalimbali hapa nchini ambao wanahitaji kuwa pamoja na mwenzao huyo.

  Msama alisema kwa kuwa bado wanaendelea na hatua za mwisho za kufanikisha kazi hizo, wanajipanga kushirikisha idadi kubwa ya waimbaji watakaomsindikiza mwezao. Aidha Msama alisema sambamba na waimbaji hao kutaka kupanda jukwaani siku hiyo, pia mashabiki wa muziki huo hapa nchini wanahitaji uzinduzi wa albamu hiyo ushirikishe pia waimbaji raia wa Afrika ya Kusini.

  0 0

   Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi  Ombeni Sefue (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi     (kulia) juu ya shughuli mbalimbali za PSPF, wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais (Utumishi) Bw. Habib Mkwizu  (kushoto) na Bw. Joseph Lyimo, ambaye ni Afisa wa PSPF. Mheshimiwa Sefue alitembelea banda la PSPF katika maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi juu ya shughuli mbalimbali za PSPF,  kulia ni Michael Tarimo, Afisa wa PSPF. Mheshimiwa Sefue alitembelea band la PSPF katika maonesho hya wiki ya Utumishi wa Umma yaliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
   Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi akitoa maelezo kwa mmoja wa wanachama wa PSPF waiotembelea banda la PSPF katika maonesho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyamalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF Bw. Abdul Njaidi akitoa maelezo kwa wanachama wa PSPF waiotembelea banda la PSPF katika maonesho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyamalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
   

older | 1 | .... | 882 | 883 | (Page 884) | 885 | 886 | .... | 3278 | newer