Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 881 | 882 | (Page 883) | 884 | 885 | .... | 3270 | newer

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wa pili kushoto), akishiriki kupalilia katika shamba la dengu la mwanakijiji cha Manawa, Kata ya Misasi, Luhoyo Mwilima (Wa tano kulia), akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, leo.

  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana,Leo aliendelea na ziara yake katika jimbo la Misungwi linaloongozwa na Mh. Charles Kitwanga ambaye pia ni naibu Waziri wa Nishati na Madini akitembelea maeneo mbalimbali na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015, inayotekelezwa na serikali ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ili kuzipatia ufumbuzi.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikatiza katika kijiji cha Mahando,mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika Ofisi ya CCM tawi la Kijiji cha Mahando, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza leo.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimueleza jambo Mbunge wa Jimbo la Misungwi Dkt.Charles Kitwanga,walipokwenda kuwasalimia Mama Lishe na kuzisikiliza changamoto zao na namna ya kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine.
  Wananchi wa kijiji cha Nyang'homango wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana alipowahutubia katika kijiji hicho ,wilayani Misungwi mkoani Mwanza. 
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezo Nape Nnauye akiwahutubia na kuwasalimia wakazi wa kijiji cha Nyang'homango waliokusanyika kwa wingi ,ikiwemo pia kumsilikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana
  Mbunge wa jimbo la Misungwi Dkt.Charles Kitwanga akiwasalimia wananchi katika kijiji cha Nyang'homango,wilayani humo.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akisindikizwa kwa ngoma ya Sungusungu, alipokuwa akienda kuzindua Ofisi ya CCM na kuzungumza na wananchi katika Kijiji cha Mahando, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCm na Uhai wa Chama katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza leo.

  PICHA NA MICHUZI JR-MISUNGWI,MWANZA


  0 0


  0 0  0 0


  0 0


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassa Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman wakiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa wa nishani za Jamhuri ya Muungano daraja la kwanza, Utumishi wa muda mrefu na maadili mema daraja la kwanza na Utumishi wa muda mrefu na maadili mema daraja la pili na Ushupavu Jumanne Juni 23, 2015 katika ukumbi mpya wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam. 
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassa Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman wakiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa wa nishani za Jamhuri ya Muungano daraja la kwanza
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassa Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman wakiwa katika picha ya pamoja na watunukiwa wa nishaniya Utumishi wa muda mrefu na maadili mema daraja la kwanza

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassa Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman wakiwa katika picha ya pamoja na mtunukiwa wa Nishani ya Ushupavu Koplo Liberatus Tibaitirwa Ndyetabula wa Magereza (kushoto)
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassa Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Jaji Mkuu Mhe Mohamed Chande Othman wakiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya hafla hiyo. 
  Mtoto wa mtunukiwa nishani Florens Martin Turuka alipata bahati ya kutumia Ipad yake kupiga picha viongozi na watunukiwa nishani.

  0 0

  Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Geita (CCM) Mheshimiwa Donald Kevin Max (58)(picha) amefariki dunia. 
  Kufuatia taarifa iliyotolewa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (Mb) kwa Waheshimiwa Wabunge wote pamoja na umma kwa ujumla,  Mhe. Max amefariki dunia tarehe 23 Juni, 2015 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu. 
  Kwa mujibu wa taarifa hii, taarifa zaidi juu ya msiba huu zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia kadri zitakavyopatikana ikiwa ni pamoja na ratiba ya Mazishi. 
  “BWANA ametoa, BWANA ametwaa, 
  Jina la BWANA  lihimidiwe.” Amina.


  Imetolewa na:

  Ofisi ya Bunge,

  Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na

  Uhusiano wa Kimataifa,


  DODOMA


  0 0
 • 06/24/15--04:54: MKWASA AITA 26 TAIFA STARS
 • Kocha Mkwasa (kushoto) na msaidizi wake Hemed Morocco wakiongea na waandishi wa habari.
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 104
  TAREHE 24 JUNI 2015

  Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine leo amemtambuisha kocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Charles Boniface Mkwasa mbele ya waandishi wa habari.

  Akiongea na waandishi wa habari, Mwesigwa amewaomba wadau wa mpira wa miguu nchini kuwapa sapoti makocha hao wazawa wanaoanza kazi kesho kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda julai 4, 2015 jijini Kampala.

  Mara baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari, Mkwasa amesema anashukuru kwa TFF kumpatia nafasi hiyo ya kuingoza Taifa Stars na msaidizi wake Hemed Morocco, na kuomba watanzania kuwapa sapoti.

  Mkwasa amesema cha kwanza atakachokifanya na msaidizi wake Morocco ni kurudisha imani ya watanzania juu ya timu yao ya Taifa, kisha watajitahidi kadri ya uwezo wao kuhakikisha kuwa timu inafanya vizuri katika michezo inayowakabili.

  Aidha Mkwasa ametangaza kikosi cha wachezaji 26 watakaoingia kambini kesho alhamisi katika hoteli ya Tansoma tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda.

  Wachezaji walioitwa ni makipa: Mudathir Khamis (KMKM), Mwadini Ally (Azam), Ally Mustafa “Barthez” (Yanga).

  Walinzi: Shomari Kapombe (Azam), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Mohamed Hussein “Tshabalala” (Simba), Haji Mwinyi (KMKM), Nadir Haroub “Cannavaro” (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Aggrey Morris (Azam).

  Viungo: Jonas Mkude (Simba), Abdi Banda (Simba), Salum Telela (Yanga), Frank Domayo (Azam).

  Viungo wa pembeni: Saimon Msuva (Yanga), Said Ndemla (Simba), Deus Kaseke (Mbeya City), Ramadhan Singano “Messi” (Simba).

  Washambuliaji: John Bocco (Azam), Atupele Green (Kagera Sugar), Rashid Mandawa (Kagera Sugar) na Ame Ally (Mtibwa Sugar).

  Wachezaji Juma Abdul (Yanga), Mudathir Yahya (Azam) na Samwel Kamuntu (JKT Ruvu) wameitwa kama wachezaji wa akiba katika kikosi cha timu ya Taifa kinachoingia kambini kesho.

  Katika hatua nyingine Mkwasa ametangaza benchi la ufundi la Taifa Stars, kocha msaidizi Hemed Morocco, kocha wa magolikipa Peter Manyika, Mshauri wa timu Abdallah Kibadeni, mtunza vifaa Hussein Swedi Gaga huku mratibu wa timu akiwa ni Alhaj Ahemd Mgoyi.

  Kamati ya tiba ya TFF itapendekeza majina ya daktari wa timu na mchua misuli watakaoungana na kambi ya Taifa Stars.


  IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

  Vyuo vilivyofutiwa usajili ni pamoja na Dar es Salaam College of Clinical Medicine cha jijini Dar es Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali, Ndatele School of Medical Laboratory Sciences cha Dar-es-Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali na Institute for Information Technology  cha jijini  Dar es Salaam pia chenye namba za usajili REG/EOS/014


  Taassi/vyuo vilivyoshushwa hadhi  baada ya kushindwa kutiza mashart ni pamoja na Sura Technologies – Dar es Salaam,  Institute of Management and Information Technology – Dar es Salaam, Techno Brain - Dar es Salaam, Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi – Mbeya, Mbozi School of Nursing – Mbeya, KCMC AMO Ophthalmology School – Moshi, KCMC AMO Anaesthesia School – Moshi, Advanced Pediatrics Nursing KCMC – Moshi.

  Vingine ni, AMO Training Centre Tanga – Tanga, CATC – Songea, CATC – Sumbawanga, COTC Maswa – Shinyanga, COTC – Musoma, Dental Therapists Training Centre – Tanga, Ngudu School of Environmental Health Sciences – Kwimba na KCMC AMO General School – Moshi.

  Kuhusu NACTE
  Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura ya 129, kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma zinazotolewa na taasisi na vyuo vva elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za kuendesha mafunzo ili tuzo zinazotolewa na taasisi na vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.
  Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam(hawapo pichani)wakati wa kutangaza ubora wa elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo.Baraza hilo limevifuta usajili vyuo  vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mitaala wa baraza hilo Twilumba Mponzi na Msaidizi wa katibu Mtendaji Alex Nkondola.
   Wakurugenzi wa Manejimenti ya NACTE wakiwa kwenye mkutano pamoja na waandishi wa habari uliohusu kutangaza ubora wa Elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo lilitangaza kuvifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
   Mwandishi wa habari kutoka kituo cha EAT, Noah Laltaila akimuuliza swali Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf Rutayuga kwenye mkutano  uliohusu kutangaza ubora wa Elimu ya ufundi inayotolewa na baraza hilo lilitangaza kuvifutia usajili vyuo  vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.


  0 0

   Baadhi ya warembo watakawo wania taji la Kilimanjaro Ambassador litakalofanyika Julai 24 katika ukumbi wa Kili Home Resort mkoa wa Moshi wakiwakipewa maelekezezo na mwalimu  Omary Bokilo leo katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya warembo watakawo wania taji la Kilimanjaro Ambassador litakalofanyika Julai 24 katika ukumbi wa Kili Home Resort mkoa wa Moshi wakiwa katika picha ya pamoja leo katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.
   Katibu mtendaji wa Rick Plan co.Ltd, Sebu Panya akizungumza  kuhusiana na mashindano ya   wania taji la Kilimanjaro Ambassador litakalofanyika Julai 24 katika katika ukumbi wa Kili Home Resort mkoa wa Moshi leo
   katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Rick Plan co.Ltd, Jaquline Chuwa na Mkuu wa itifaki  wa Rick Plan co.Ltd, Angeris Faber.

  Mkurugenzi wa Rick Plan co.Ltd, Jaquline Chuwa akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari leo  kuhusiana na mashindano ya   wania taji la Kilimanjaro Ambassador litakalofanyika Julai 24 katika katika ukumbi wa Kili Home Resort mkoa wa Moshikushoto ni
  Mkuu wa itifaki  wa Rick Plan co.Ltd, Angeris Faber. PICHA NA EMMENUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

  0 0

  Kutafuta liziki ni kwa kila mtu ila tofauti ni kwa namna gani jamaa kama alivyokutwa na kamera yetu leo katika eneo la Kinondoni B jijini dar es salaam.
  Mjasiliamali akimuuzia mteja wake mara baada ya kuegesha gari lake pembeni kama alivyonaswa na kamera yetu leo katika eneo la kariakoo jijini Dar es Salaam leo. 
  PICHA NA EMMENUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Hilan Mansoor wakati wa mapokezi kwenye kijiji cha Mwamaya kata ya Hungumalwa wilaya ya kwimba mkoani Mwanza.
   Walinzi wa Jadi wa kisukuma maarufu kwa jina la Sungusungu wakimpokea Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mavazi ya jadi ya walinzi wa Kisukuma maarufu kama Sungusungu.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia kikundi cha ngoma za utamaduni Idibuili wakati alipotembelea kijiji cha Hungumalwa kuona na kushiriki ujenzi wa Zahanati.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi ya Chadema kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilula Hamala Materemki, kata ya ilula wilani Kwimba aliyejiuzulu na kuamua kujiunga na CCM.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Diwani ya kata ya Hungumalwa Shija Marando wakati wa kuona na kushiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Hungumalwa.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa kijiji cha Hungumalwa wakati wa kuona maendeleo ya ujenzi wa zahanati ya kijiji.Wengine pichani ni Mbunge wa jimbo la Kwimba Mhe. Shanif Hilan Mansoor na Diwani wa Kata ya Hungumalwa Shija Marando.

  KWA PICHA ZIDI BOFYA HAPA.

  0 0

   BOTI ya Kilimanjaro V ikishushwa katika Meli ya Thorco Clairvaux ikitokea Nchini Australia , boti hiyo ilishushwa nje kidogo ya Bandari ya Malindi Mjini Zanzibar na tayari imeshazinduliwa rasmi kuanza safari zake. 
  Picha na Haroub Hussein.

   BOTI ya Kilimanjaro V ikitua katika maji ya bahari ya Hindi leo
  BOTI ya Kilimanjaro V ikielekea gatini Malindi, Zanzibar, tayari kwa uzinduzi.

  0 0

   Askari wa kaampuni ya G1 Security wakimrekebisha mtuhumiwa wizi ambaye jina lake halikupatikana  mara moja ambaye alikuwa katika harakati za kutaka kufanya uharifu  katika Jengo la PAM RESIDENCE jijini  Dar es salaam.
   Mtuhumiwa wa uharifu katika jengo la PAM RESIDENCE jijini Dar es Salaam.
  Mtuhumiwa wa wizi  ambaye jina lake halikupatikana mara moja akihojiwa na Askari wa kaampuni ya G1 Security juu ya jiwe alilokuwa nalo kwenya mfuko  picha na EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA. 

  0 0

  Mh. January Makamba na mkewe, Ramona(kulia) mara baada ya kushuka kwenye Ndege leo hii Jumatano asubuhi juni 24, 2015. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.
  Mh. January Makamba akisalimiana na Katibu wa Vijana Mkoa wa Kagera
  Mh. January Makamba akisalimiana na Wanafunzi wa Sekondari waliokuwa Uwanjani hapo ambao bila Shaka walikuwa wanasoma masomo ya Ndege inavyoruka na kutua na mengineyo kiujumla leo jumatano juni 24, 2015. Picha na Faustine Ruta, Bukoba
  January Akizungumza na wakazi wa Bukoba waliojitokeza kumsikiliza katika katika Ofisi za CCM Mkoa wa Kagera leo


  KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  VIONGOZI wa dini wakiwemo Maaskofu na Wachungaji wa Makanisa mbalimbali hapa nchini wamebariki uzinduzi wa albamu tatu za mwimbaji mahiri wa muziki wa Injili hapa nchini Bonny Mwaitege, unaotarajia kufanyika Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama sababu za viongozi hao wa dini kutoa baraka kwa albamu hizo ni kutokana na umahiri wa muimbaji huyo.
  Msama alisema amepokea baraka hizo kutoka kwa viongozi hao wa dini kwa sababu uzinduzi huo unashirikisha albamu tatu kwa pamoja, jambo ambalo linaonesha ni ukomavu na umahiri katika kufanikisha neno la Mungu ipasavyo.
  “Uzinduzi wa Bonny Mwaitege utakuwa ni wa aina yake kwa sababu viongozi wa dini mbalimbali wametia baraka kwa maneno matakatifu ambayo yatafanikisha ufikishwaji wa neno la Mungu kwa jamii ipasavyo,” alisema Msama.
  Msama alisema baraka hizo za viongozi wa dini zinakwenda sambamba na maombi ya kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu hapa nchini ambao utahusu urais, Wabunge na Madiwani.
  “Viongozi wa dini ndio wanafanikisha tunu ya amani tuliyonayo, hivyo wameongeza chachu ya maombi ya amani hiyo tuliyoachiwa na baba wa Taifa, Mwalim Julius Kambarage Nyerere,” alisema Msama.
  Aidha Msama alisema hivi sasa wanaendelea na maandalizi ya kurekodi albamu hizo jijini Mwanza ili kupata ladha nzuri ya nyimbo hizo za kumuimbia na kumtukuza Mungu.
  “Waandaaji wanaendelea na kazi yao ya kufanikisha kurekodi albamu hizo ambazo zitakuwa na ubora wa aina yake kwa sababu umahiri wa watendaji wake ambao ni wa kampuni yake ya Video Productions. Msama alitoa wito kwa mashabiki wa muziki wa Injili kujiandaa kupata kazi bora ya muimbaji huyo ambaye anashika anga la muziki huo Afrika Mashariki na Kati.

  0 0


   Since the launch of its Android and Blackberry apps in September 2014, and the recent launch of its iOS app in May 2015, Kaymu has been pushing to improve and promote its mobile phone applications.  
  Kaymu is offering unbelievable price discounts on so many products via the mobile app, in the celebration of this Saba Saba season. Products ranging from kitchen ware to television sets can be grabbed at unbelievable prices.


   Kaymu Tanzania’s Country Manager Erfaan Mojgani explains, “Most things can be done from a mobile phone these days and the number of people with internet access on their mobile phones is ever growing. 
  "This is why we dedicated so much time and effort to making sure mobile phone users can shop on Kaymu via our mobile application. It is very easy and convenient. You can shop anywhere, from home to your office. 
  "With this Saba Saba season in place, we expect to see more people downloading the application from their mobile stores and taking advantage of the many discounts we’re offering.”

  Be sure to look out for Kaymu social media posts on Twitter, Facebook and Instagram because this season there are lots of exciting prizes to be won. 
  Kaymu is giving away many gift vouchers this season, one could earn themselves vouchers ranging from a free delivery on a Kaymu order (This means that there will be no need for the winner to pay for the delivery fees that they usually pay on Kaymu orders) to a 20% off cart voucher (This means that the customer could use this voucher to get 20% off a Kaymu order).  
  If this isn’t enough, there are also many weekly super deals and special discounts that apply to mobile app purchases. Download the app today and enjoy your online shopping experience.

  The Kaymu mobile app for Android can be downloaded for free here-http://bit.ly/1TNdICg
  The Kaymu mobile app for Blackberry can be downloaded for free here-http://blck.by/1J52OBR

  The Kaymu mobile app for iOS can be downloaded for free here -https://appsto.re/tz/bk0C6.i

  0 0

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na wasanii wa tasnia ya filamu mkoa wa Morogoro jana, wakati alipokuwa mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo wanaCCM zaidi ya 950 walimdhamini.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa tasnia ya filamu mkoa wa Morogoro jana, wakati alipokuwa mkoani humo kwa ajili ya kutafuta wadhamini ili aweze kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo wanaCCM zaidi ya 950 walimdhamini. Picha na John Badi

  0 0

  Airtel Tanzania imetoa Tsh Milioni 20 kwa Jumuiya ya Waislamu kupitia Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa lengo la kufuturisha vituo kumi vya kulelea watoto yatima nchini. 
  Akikabidhi hundi kwa Naibu katibu Mkuu wa Bakwata Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Hawa Bayumi alisema vituo vitakavyopata msaada huo ni pamoja na Kigogo Fresh orphanage cha Ilala, IHSANI orphanage cha Temeke, Almadina center kinondoni.
  Pia kwa Arusha ni Kiboa Islamic orphanage, Nusuru yatima orphanage Bukoba, Nuru orphanage Mbeya, Zam zam orphanage Dodoma, Maua Daftari Foundation Zanzibar, Chuno orphanage center Mtwara na Makorora Yatima center cha Tanga ambapo kila kimoja kitapatiwa vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni2. 
  “Airtel Tanzania kama inavyofanya miaka mingine leo pia inaungana na ndugu na jamaa zetu waislamu kuadhimisha mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kwa kuwakumbuka watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kupitia hivi vituo ili nao waweze kushiriki mfungo wa Ramadhan.” alisema. 
  Aliongeza kuwa Airtel imekuwa ikitoa misaada kama hii kwa makundi mbalimbali katika jamii kila mwaka na kusisitiza kuwa baadhi ya wafanyakazi wa Airtel watajumuika na watoto hawa katika mwezi huu ili na wao pia wajiskie kama sehemu ya jamii. 
  “Tunapenda kutoa rai kwa mashirika mengine pia yawakumbuke hawa watoto na kuwasaidia ili wajisikie kama sehemu ya jamii,” alisema. 
  Akipokea hundi hiyo, Naibu katibu Mkuu wa Bakwata, Sheikh Mohamed Khamis Said aliishukuru Airtel Tanzania kwa msaada huo na kusisitiza kuwa utasaidia kwa kiasi kikubwa na kuhakikisha watoto wanaolelewa katika vituo hivi wanapata mahitaji muhimu hasa katika mwezi huu wa Ramadhan. 
  “Tunashukuru mno kwa niaba ya vituo hivi na tunatoa wito kwa mashirika mengine pia yajitokeze na kutuunga mkono ili tuweze kufikia yatima wengi zaidi na kuwapa faraja katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan” alisema.
   Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akiongea na waandishiwa wa habari katika hafla ya makabidhiano ya hundi kwa Bakwata, kwa vituo mbalimbali vya watoto yatima hapa nchini vyenye thamani ya sh. Milioni 20 , Kulia ni Sheikh Mohamed Khamis Said mwakilishi wa Bakwata.
  Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akikabidhi hundi yenye dhamani ya sh.milioni 20 ya msaada wa vyakula kwa BAKWATA kwa vituo mbalimbali vya watoto yatima hapa nchini, akipokea (Kulia) Sheikh Mohamed Khamis Said mwakilishi wa Bakwata.

  0 0

   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akihitimisha ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Wilaya ya Magharibi "A" na "B".
   Wananchi wakimsalimia Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad wakati akihitimisha ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Wilaya ya Magharibi "A" na "B".
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimfariji kijana mgonjwa wakato akihitimisha ziara yake ya kutembelea wagonjwa katika Wilaya ya Magharibi "A" na "B".
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa na Sheikh Habibu Ali Kombo wakiitia dua baada ya kumjuilia hali. (Picha na Salmin Said, OMKR)

older | 1 | .... | 881 | 882 | (Page 883) | 884 | 885 | .... | 3270 | newer