Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

Baraza la maulamaa la BAKWATA lamteua Sheikh Abubakhari Zubeir kuwa kaimu Mufti Mkuu


DIRA YA DUNIA YA IDHAA YA KISAHILI YA BBC, LONDON

Chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania wasitisha kukununua stika za TRA na kupeleka filamu zao Bodi ya filamu kwaajili ya kufanyiwa ukaguzi

0
0
 Mwenyekiti wa kikosi kazi kutoka chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania,Bw Moses Mwanyilu akionyesha baadhi ya filamu ambazo zinauzwa nchini bila kupata kibali kutoka bodi ya filamu Tanzania na kutokuwa na stika za ushuru za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakielezea changamoto zao kuhusiana na filamu za kitanzania kulazimishwa kukaguliwa na bodi ya filamu na kuwekwa stika za TRA ilhali filamu za nje hazifanyiwi hivyo na kupelekea filamu za kitanzania kutokuwa na ushindani sokoni.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kuandika kile kinachozungumzwa 
Mjumbe wa chama cha wasambazaji wa filamu Tanzania, Bw Saleh Abdallah akizungumzia kauli moja waliyokubaliana kama wasambazaji kuwa Kuanzia tarehe 1 Julai 2015 wao kama watayarishaji na wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania wamesitisha swala la kupeleka filamu zao bodi ya filamu kwaajili ya kukaguliwa wala kununua stika za TRA mpaka pale mamlaka husika zitakapokaa chini na kujadiliana kuhusu swala hili
Chama cha wasambazaji wa kazi za filamu Tanzania leo wamekutana na waandishi wa habari kuelezea nia yao ya kusitisha kupeleka filamu zao bodi ya filamu Tanzania kwaajili ya kukaguliwa huku wakielezea sababu kuwa Bodi ya filamu imekua ikikagua filamu za Tanzania tu huku zile za nje zikiwa hazikaguliwi na kupelekea kuwaumiza wao katika soko la filamu 
Vilevile wamesitisha zoezi la kununua stika za TRA kutokana na sababu kuwa kazi nyingi za nje hazina stika na pia maafisa wa TRA wakipita kukagua filamu wanachukua za Tanzania tu ambazo hazina stika huku wakiziacha zile zinazotoka nje na zile zinaharamiwa huku sheria ya filamu ya mwaka 2012 ikisema kuwa filamu zote ziwe za nje au za ndani zinatakiwa kukaguliwa na kupewa daraja.


Kutokana na sababu ambazo chama cha wasambazaji wamezieleza kuwa Pamoja na kuwaandikia barua Mamalaka ya Mapato Tanzania na Bodi ya Filamu kuhusiana na swala hilo hawakuweza kupatiwa majibu ya barua yao na ndipo walipoamua kusitisha kununua stika na kupeleka filamu zao bodi kwaajili ya kukaguliwa mpaka watakapokaa meza moja huku wakiendelea kupeleka filamu sokoni.

MKWASA KUINOA STARS, NOOIJ AWAAGA WATANZANIA

0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania - TFF, Jamal Malinzi leo ameagana rasmi na aliyekua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, mholanzi Mart Nooij.

Akiongea na waandishi wa habari leo katika hoteli ya Tansoma, Malinzi amesema wameamua kuagana nae mbele ya vyombo ya habari kama iliyofanyika pia wakati wa utambulisho wake wakati wa kuanza kazi.

“Mpira wa miguu unachangamoto nyingi, watanzania tunasafari ndefu katika mafanikio ndio maana  TFF imeanza kuwekeza katika soka la vijana, sababu ndio msingi wa kuwa na timu bora ya Taifa” alisema Malinzi.

Duniani kote chimbuko la timu bora ni soka la vijana na watoto, tukiwa na vijana wengi walioanza kucheza mpira katika umri mdogo wanapofikia umri wa kuchezea timu ya Taifa tutakua na kikosi bora.

Nchi za wenzetu inapofikia kocha kuita wachezaji wa timu ya Taifa anakuwa na wigo mpana, kwetu sisi wachezaji wanocheza soka nje ya nchi wanahesabika, hivyo ni lazima tuanze kuwekeza kwenye soka la vijana

TFF ilishaanza mkakati huo ndio maana kuna timu za U13, U15 ambazo zitakua zikiingia kambini na kucheza michezo ya kirafiki ndani ya nje kwa lengo la kupata uzoefu kabla ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za vijana mwaka 2016.

Kikosi cha U15 kinatarajiwa kufanya ziara mwezi Disemba mwaka huu katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini, kisha mwakani mwezi April 2016 kitaenda Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya kucheza michezo ya kirafiki.

Naye Mart Nooij aliyekua kocha wa Taifa Stars, akiongea na waaandishi wa habari alisema anawashukuru watanzania wote, serikali, wadau wa mpira wa miguu nchini na TFF kwa sapoti waliyompatia wakati akiwa kocha mkuu wa timu ya Taifa.

Nooij alisema alifurahia maisha yake akiwa Tanzania kwa kipindi chote alichokua akifundisha timu ya Taifa, lakini kwa sababu imefikia mwisho wa ajira yake hana jinsi anaondoka, lakini ataendelea kuikumbuka Tanzania na watanzania wote kila siku kwa ukarimu wao.

Wakati huo huo Rais wa TFF. Jamal Malinzi amemtangaza Charles Mkwasa kuwa kocha mpya wa Taifa Stars akisaidiwa na kocha Hemed Morocco, Mkwasa  ambaye ni kocha wa Yanga na Morocco kocha wa Mafunzo watafanya kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ambayo timu ya taifa itakua na michezo ya kuwania kufuzu kwa CHAN na AFCON.

Malinzi amesema uteuzi wa makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa timu ya Taifa kuwa na leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana kutoka mashiriksho mengine duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo makocha  hao wazawa wamekizi.

Kocha Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi  (zikiwemo posho) alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa mpira wa miguu na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao wazawa” aliongeza Malinzi”

Aidha Kamati ya utendaji ya TFF Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu wa timu ya Taifa, lengo la uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati ya kamati ya Utendaji na timu ya Taifa.

Airtel yazindua ofa ya LUKU

0
0
Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirika la umeme la (TANESCO) imezindua ofa kabambe itakayowazawadia wateja wake nchi nzima Unit za bure za Luku pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money

Ofa hii mpya ina lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma ya umeme na pia kuwazawadia wateja wa Airtel wanaonunua unit za LUKU kupitia huduma ya Airtel Money

Akiongea kuhusu ofa hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackosn Mmbandoalisema” Wateja wetu watazawadia unit LUKU za ziada Bure mara tu watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money. Tunaamini ofa hii inaendana na mahitaji na mwendendo wa maisha ya watanzania. Kwa sasa manunuzi ya umeme kupitia njia nyingine si tu yanaleta changamoto za kusafiri umbali mrefu na kupoteza muda mwingi kupata huduma bali husababisha watu kukaa foleni ndefu kusubiri kununua umeme. leo Airtel tunatoa ofa hii kwa wateja wetu na kuwawezesha kununua LUKU kwa urahisi wakiwa majumbani mwao pamoja na kunawazawadia kwa kuwapatia unit za Luku za ziada za bure”.

Aliongeza kwa kusema “ Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu zinazokithi na kutatua mahitaji ya wateja wetu , tukiwa na mawakala wa Airtel Money zaidi ya 45,000 nchini , wateja wetu wanafaidika na huduma ya mikopo, huduma za kuhamisha pesa, kutoa na kuweka pesa na nyingine nyingi.

Huduma ya Airtel Timiza inayotoa mikopo isiyo na dhamana kupitia simu za mkononi ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kutoa huduma za kisasa zenye ubunifu kwa watanzania.” aliongeza Mmbando
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando (katikati) akiongea na waandishi wa Habari leo katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salaam wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe itakayowazawadia wateja wa Airtel nchini kupata Unit za bure za LUKU pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money, kushoto ni Afisa uhusiano na matukio wa Airtel na (Kulia) Steven Kimea Meneja wa Airtel Money.
Meneja wa Airtel Money Steven Kimea (Kulia) akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ofa kabambe itakayowazawadia wateja wa Airtel nchini kujipatia nyongeza ya Unit za bure za LUKU pindi watakaponunua LUKU kupitia huduma ya Airtel Money, anayefwata kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando.Hafla ya uzinduzi huo imefanyika leo katika ofisi ya Airtel jijini Dar es Salaam.

Maalim Seif akutana na balozi wa Ufaransa nchini Tanzania

0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na balozi wa Ufaransa nchini Tanzania bibi Malika Berak, alipofika ofisini kwake Migombani kwa mazungumzo. Kulia ni ofisa wa ubalozi Philippe Boncour.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisisitiza jambo wakati akizungumza na balozi wa Ufaransa nchini Tanzania bibi Malika Berak, ofisini kwake Migombani.

ACACIA KUKUSANYA DOLA 200,000 KWA AJILI YA UFADHILI WA ELIMU KWA WATOTO MASKINI, NI KUPITIA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

0
0
 KAMPUNI ya ACACIA inayojishughulisha na uchimbaji na utafutaji madini, imezindua kampeni ya kukusanya fedha kupitia kupanda mlima Kilimanjaro, leo Jumatatu Juni 22, 2015, ambapo fedha hizo zitakwenda kusaidia sekta ya elimu kwenye maeneo yanayozunguka migodi mitatu inayomilikiwa na kampouni hiyo ya North Mara, Bulyanhulu na Buzwagi.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza kwa safari ya kupanda mlima Kilimanjaro kwenye lango la Machame,iliyo shirikisha watu 21, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Brad Gordon, alisema, kampuni yake ilianzisha mpango ujulkikanao kama “CAN EDUCATE”, ikimaanisha tunaweza kujieleimisha, imeamua kukusanya fedha kupitia kupanda mlima Kilimanjaro, ili kusaidia elimu na kampuni inimekuwa ikifanya hivyo kila mwaka.

“Lengo ni kukusanya dola za Kimarekani 200,000, zitakazosaidia jamii inayokaa kuzunguka maeneo ya migodi inayomilikiwa na kampuni hiyo” alisema Meneja Mkuu wa Uendelezaji wa Kmapuni, Asa Mwaipopo.

Na kuongeza kuwa kuna watoto wengi wanashindwa kendelea na elimu ya sekondari na ile ya chuo kikuu, sio kwa sababu za uwezo mdogo wa kimasomo, bali ni ukosefu wa fedha za kuendelea na elimu. 

Acacia imeamua kushiriki katika kuwasaidia watoto hawa ili watimize ndoto zao. Alimaliza Mwaipopo. 

Pichani, Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya ACACIA, Brad Gordon, (Wapili kushoto), akiongoza timu ya watu 21 wakiwemo wafanyakazi, marafiki na familia za wafanyakazi wa kampuni hiyo ,kupanda Mlima Kilimanjaro kwenye lango la Machame mkoani Kilimajaro Jumatatu Juni 22, 2015, kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia sekta ya elimu nchini.(Habarin na K-VIS MEDIA, picha na Dixon Busagaga)

 Kundi la watu 21, wakiwemo, wafanyakazi wa Acacia na familia zao pamoja na marafiki wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza safari yao ya kupanda Mlima Kilimanjaro Juni 22, 2015
 Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Acacia, Brad Gordon, (katikati), akiwa na Meneja Mkuu wa Uendelezaji wa kampuni hiyo, Asa Mwaipopo, (kushoto), akizungumza muda mfupi kabla ya kuongoza timu ya wapanda mlima Kilimanjaro kwa nia ya kukjsuanya fedha hizo
Brad, (kushoto), akijadiliana jambo na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Necta Pendaeli Foya (katikati)

SOS WAADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA KWA MWANZILISHI WA VIJIJI VYA WATOTO DUNIANI

0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
Watoto wametakiwa kujaliwa kwa kila namna ili kuwaanda kuwa taifa bora kutokana na misingi ambayo imewekwa kwa watoto hao.


Akizungumza na leo katika maadhimisho ya kuezi  kuzaliwa kwa mwanzilishi Vijiji vya Watoto SOS,Herman Gmeiner,Mkurugenzi wa Kijiji cha SOS,Anglolwisye Mwollo-ntalima,amesema  kuwa kila juni 23 kila mwaka wanaadhimisho kuzaliwa kwa Gmeiner.

Mwollo-ntalima amesema kuwa kutokana na mwanzilishi huyo kwa sasa Rais wa SOS ni mtu aliyetokana na SOS na kizazi hicho kinaendelea kuwepo.



Amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni Nijali mimi ambayo dunia nzima imeadhimisha siku hiyo kwa kumkumbukA Mwanzilishi wa SOS.


Katika maadhimisho  ya SOS ,Kampuni ya Kontena ya Maersk Line imetoa msaada wa komputa katika kijiji cha watoto ili waweze kutumia kutokana na ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano.


Mkurugenzi wa Maersk Line,Morten Juul amesema anatambua kazi inayofanywa na SOS  katika kuwatunza watoto kwa unagalifu.
Mkurugenzi wa kijiji cha watoto cha SOS hapa nchini, Angolwisye Mwollo-Ntallima akicheza na watoto katika siku ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa  SOS duniani,ambayo hufanyika kila Juni 23 kila mwaka, iliyofanyika katika kijiji cha SOS- Ubungo jijini Dar es Salaam leo.  
Mwalimu mkuu wa watoto wadogo wa kituo cha  SOS ,Agnes Mlema akizungumza leo katika siku ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa  SOS duniani,ambayo hufanyika kila Juni 23 kila mwaka, iliyofanyika katika kijiji cha SOS- Ubungo jijini Dar es Salaam leo.  
Baadhi ya watoto wakicheza ngoma leo katika kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS Ubungo jijinio Dar es Salaam.
Nkurugenzi mkuu wa Maersk Line, Morten Juul  akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa kituo cha SOS pamoja na viongozi wa kituo hicho baada ya kutoa msaada wa kompyuta katika kituo hicho leo jijini Dar es  Salaam.(Picha na Chalila Kibuda Globu ya jamii)

Wabunge Waipigia kura bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016

0
0
Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya akihitimisha Hoja ya Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Fedha, Bungeni Mjini Dodoma Juni 23, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akipiga kura ya ndio wakati bunge lilipokuwa likipitisha bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Bungeni mjini Dodoma leo. Kulia ni Mbunge wa Mbunge wa Viti Maalum, Mh. Diana Chilolo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mh. Mussa Azan Zungu wakati wa kupiga kura bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Bungeni mjini Dodoma leo. 
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Mizengo Pinda akiteta na Mbunge wa Mpanda Kati, Mh. Said Arfi, Bungeni mjini Dodoma Juni 23, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akijadiliana jambo na Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe wakati wa kupiga kura bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Bungeni mjini Dodoma leo. Kulia ni Mbunge wa Mbunge wa Viti Maalum, Mh. Diana Chilolo.
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Asiye na Wizara Maalum, Profesa Mark Mwandosya na Mbunge wa Kigoma Mjini,Mh. Peter Serukamba kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 23, 2015.
Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda na wabunge wa Viti Maalum, Mh. Anna Abdallah (kushoto) na Mh. Al Shymaa Kwegyir wakitoka kwenye kumbi wa Bunge mjini Dodoma Juni 23, 2015.

DKT. MAGUFULI ARUDISHA FOMU ZA UDHAMINI KUGOMBEA URAIS MJINI DODOMA

OWM YAPATA KOMBE KATIKA MAONYESHO YA UTUMISHI WA UMMA

0
0
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi Kombe la ushindi Mchumi Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji Bw. Girson Ntimba baada ya Ofisi hiyo kuibuka mshindi wa kwanza katika Uratibu na Usimamizi Bora wa masuala ya Ukimwi wakati wa kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma tarehe 23 Juni, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifurahia kombe la Ushindi baada ya kuibuka mshindi bora katika masuala ya menejimenti ya Ukimwi wakati wa kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma tarehe 23 Juni, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Chikawe: Niliamua kugombea urais miaka mitano iliyopita

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe (pichani), ambaye ni mmoja wa wanachama wa CCM waliochukua fomu za kugombea kiti cha urais, amesisitiza kuwa uamuzi wa kugombea nafasi hiyo aliufikia miaka mitano iliyopita na kuwaomba wana-CCM kuwapuuza wale wanaosema hakupanga kuomba nafasi hiyo.

Waziri Chikawe, ambaye amekamilisha kazi ya kusaka wadhamini katika mikoa 15 ya Tanzania Bara na Zanzibar kama taratibu zinavyoelekeza, amesema uamuzi wake wa kugombea nafasi hiyo aliufanya baada ya tafakari ya kina.

“Nilishasema wiki kadhaa zilizopita nikiwa Nachingwea na leo ninarudia, nimetafakari kwa miaka mitano kabla ya kuamua kugombea nafasi ya urais mwaka huu ... ni uamuzi wangu. Kwa hiyo huo ni uzushi tu ambao unapaswa kupuuzwa,” amesema Chikawe leo (Jumanne, Juni 6, 2015) kwa njia ya simu kutoka Dodoma na kuongeza:

“Hao wanaotunga hizo taarifa za uzushi ndiyo wametumwa,” amesema Chikawe akiwa Dodoma kikazi baada ya kuombwa kutoa ufafanuzi wa taarifa zinazosambwazwa katika mitandao ya kijamii.

Ufafanuzi wa Waziri Chikawe unafuatia taarifa zinazosambazwa katika baadhi ya mitandao ya kijamii kuwa hakupanga kugombea nafasi hiyo na kuwa ameelekezwa kugombea nafasi hiyo na mmoja wa wagombea anayehofia jina lake kukatwa na vikao vya juu vya CCM.

“Mimi si mtu wa kulumbana mitandaoni na hata nafasi ninayoomba haihitaji mtu mwenye hulka hiyo (ya kulumbana). Ninawaomba wananchi na wana-CCM wenzangu wayapuuze maneno hayo kwa kuwa hayana hata chembe ya ukweli,” amesema Chikawe na kuwasihi wananchi na wana-CCM kuwa na uvumilivu wakati wakisubiri maamuzi ya vikao vya chama.

Pamoja na kuwa Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, Chikawe ni Mbunge wa Nachingwea. Alihitimu shahada ya sheria katika Chuo Kikuu cha dar es Salaam mwaka 1965 na kufanya kazi serikalini kwa miaka mingi kabla ya kuingia katika siasa za majukwaani na kushinda ubunge mwaka 2005 na kuchaguliwa tena mwaka 2010. Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (2007-2012).

NHIF YAZOA VIKOMBE VYA UBUNIFU KATIKA MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.

0
0
 Rais mstaafu Alhaj Ali Hasan Mwinyi akimkabidhi kikombe cha ushindi wa ubunifu katika maonesho ya wiki ya utumishi wa Umma, mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa mfuko wa taifa wa  bima ya afya,Ali Othman katika maonyesho ya wiki ya utumishi wa Umma yaliyofikia kilele leo  katika viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 Picha ya pamoja wakiwa na vikombe vya ushiindi vya ubunifu katika maonesho ya utumishi wa umma yaliyofikia kilele leo  katika viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

 wafanyakazi wa NHIF wakiwa na vyeti na vikombe vya ushindi wa ubunifu katika maonesho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyofikia kilele leo  katika viwanja vya mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII.

Introducing: Chris Kipaya Ft Nelly Cp - I Dont Want To Leave You

INTRODUCING: Chemical ft Soprano Musiq Sielewi Official Music Video 2015


Bayport Financial Services yamfuta machozi Latifa Said

0
0
Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, kushoto akimkabidhi hundi Latifa Juma yenye thamani ya Tsh 3,000,000, baada ya mzazi wake Juma Said, aliyekuwa Mchapa Vitabu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, jijini Dar es Salaam. Kulia ni mume wa Latifa, anayeitwa Bakari Msumi. Picha zote kwa Hisani ya Bayport Financial Services.

Na Mwandishi Wwetu, Dar es Salaam

TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, leo jioni imemkabidhi hundi ya Sh Milioni tatu (3,000,000), mjasiriamali Latifa Juma, ikiwa ni sehemu ya mafao yake baada ya mzazi wake Said Juma, kuwa mteja wa Bayport kwa kupitia huduma yake ya Bima ya Elimu kwa Uwapendao iliyoanzishwa mapema mwaka jana.


Makabidhiano hayo yalifanyika Makao Makuu ya Bayport Financial Services, Morocco, jijini Dar es Salaam, huku akisindikizwa na mumewe Bakari Msumi. Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, alisema kwamba marehemu Said Juma alikuwa mteja wao, huku akijiunga pia katika huduma ya bima, ambayo leo imemnufaisha mtoto wake.

Mratibu wa Bima ya Elimu kwa Uwapendao kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services, Ruth Bura, kushoto, akiwa kwenye makabidhiano ya hundi Latifa Juma yenye thamani ya Tsh 3,000,000, baada ya mzazi wake Juma Said, aliyekuwa Mchapa Vitabu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko, jijini Dar es Salaam. Kulia ni mume wa Latifa, anayeitwa Bakari Msumi. Picha zote kwa Hisani ya Bayport Financial Services.

GEPF YAWAKIVUTIO KATIKA MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA.

0
0
Wananchi wakipata maelekezo kutoka kwa mwakilishi wa mfuko wa GEPF,  katika monyesho ya utumishi wa umma yaliyokiwa yakifanyika katyika viwanja vya Mnazi moja jijini Dar es Salaam.

DANISH AMBASSADOR BIDS FAREWELL TO EAC SECRETARY GENERAL

0
0
The Danish Ambassador to the United Republic of Tanzania, and also accredited to the EAC bloc, H.E. Johnny Flento, today paid a Farewell visit to Amb. Dr. Richard Sezibera, the Secretary General of the East African Community.

Amb. Flento, who was accredited to the EAC on 8th March 2012, is moving to the Republic of Mozambique having spent four years in the United Republic of Tanzania. During his tenure as the EAC Ambassador, Amb. Flento had the honor of accompanying the former Danish Prime Minister, Hon. Helle Thorning Schmidt on a courtesy visit to EAC Secretariat on 8th March 2013.

Amb. Sezibera briefed his guest on the latest developments in the regional integration process including the launch of the Common Market for Eastern and Southern Africa (COMESA), East African Community (EAC) and Southern African Development Community (SADC) Tripartite Free Trade Area (TFTA) by the COMESA-EAC-SADC Heads of State and Government on 10 June, 2015 in Sharm El Sheikh, Egypt.

The Secretary General noted that the (TFTA) represented an integrated market of 26 countries with a combined population of 632 million people, or 57 percent of Africa's population. It also provides a total Gross Domestic Product (GDP) of USD$ 1.3 Trillion (2014), contributing to 58% of Africa's GDP.

He further added that the establishment of a the TFTA will bolster intra-regional trade by creating a wider market, increase investment flows, enhance competitiveness and encourage regional infrastructure development as well as pioneer the integration of the African continent.

The Danish Ambassador briefed the Secretary General on the developments taking place in his country and appreciated the great milestones being recorded in the East African regional integration initiatives. The Secretary General was accompanied by his Deputy in charge of Finance and Administration Mr. Liberat Mfumukeko and other senior officials, while Amb. Flento was accompanied by the Danish Advisor on EAC Integration, Ms Agatha Nderitu.
EAC Secretary General, Amb. Dr. Richard Sezibera engaged in talks with outgoing Danish Ambassador to the United Republic of Tanzania and to the EAC bloc, H.E. Johnny Flento at the EAC Headquarters in Arusha.
A group photo opportunity (l-r) EAC Principal Information and Public Relations Officer, Mr. Othieno Richard Owora; EAC Principal Resource Mobilization Officer, Dr. James Njagu; EAC Secretary General, Amb. Dr. Richard Sezibera; outgoing Danish Ambassador to the United Republic of Tanzania and to the EAC bloc, H.E. Johnny Flento; EAC Deputy Secretary General in charge of Finance and Administration, Mr. Liberat Mfumukeko; Danish Advisor on EAC Integration, Ms Agatha Nderitu and EAC Principal International Relations Officer, Mr. Joseph Birungi.

TAARIFA YA TBS KUHUSU WAAGIZAJI WA MAGARI TOKA NJE YA NCHI

TFDA WAFUNGA MONYESHO YA UTUMISHI WA UMMA KWA KUWA NA BANDA BORA

0
0
 Mneja wa mawasiliano wa Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) Gaudensia Simwanza akiwa na kikombe cha ushindi katika maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma leo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi wa TFDA wakiwa katika picha ya pamoja wakifurahia kikombe katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
wafanyakazi wa TFD wakiwa na vyeti pamoja na vikombe vyao vya ushikndi katika kilele cha maonyesho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja   jijini Dar es Salaam.PICHA NA EMMENUEL MASSAKA.
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images